Search the region
22511 stories
JKT Tanzania yajipanga kuchukua alama kwa Mnyama.
JKT TANZANIA vs SIMBA SC: “Kesho tutakuwa na wakati mzuri uwanjani...” Kocha wa JKT Tanzania, Ahmad Ally amesema kikosi chake kimejiandaa vizuri kiakili na kisaikolojia kuelekea mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Simba SC. Ahmad amesema Simba SC ni timu kubwa, si tu ndani ya Tanzania bali pia katika soka la Afrika, hivyo mchezo huo utakuwa fursa nyingine kwa kikosi chake kujifunza na kupima uwezo wake. Kwa upande wake mchezaji wa timu hiyo, Jafar Maneno amesema wachezaji wamejiandaa kupambana kwa nguvu zote ili kupata alama tatu, na iwapo hilo halitawezekana basi watahakikisha wanaondoka na angalau alama moja. #NBCPremierLeague #LigiKuuYaNBC #NBCPLUpdates #ImenogaZaidi #JKTTanzania #SimbaSC #JKTTanzaniaSimbaSC
2026-11-20T12:00:56+00:00Anfield awaits as Liverpool v Manchester United blockbuster
Few rivalries in world football command the attention, passion and intensity of Liverpool against Manchester United. When these two giants meet, history is never far…
RecentlyNew vehicle dealers surpass 2025 sales in 10 months
Read the full report from the original source.
RecentlyVIJANA WAASWA KULINDA AMANI TANZANIA IKIJIANDAA KWA AFCON 2027
Rais Samia Suluhu Hassan amewataka vijana kulinda amani na usalama wa Tanzania wakati nchi ikijiandaa kupokea wageni wa kimataifa kwa ajili ya shughuli mbalimbali zitakazofanyika nchini. Rais Samia ametoa wito huo leo, Novemba 20, aliposalimia wananchi wa Bomang’ombe, wilayani Hai, akiwa njiani kuelekea mjini Moshi. Amesema idadi ya watalii wanaoingia nchini na mikutano ya kimataifa inayofanyika Tanzania ni kielelezo cha nchi kuendelea kuwa salama. “Ombi langu kwenu ni amani na utulivu kwa nchi yetu,” amesema Rais Dkt. Samia. Ametaja michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) ya mwaka 2027, na mashindano ya urembo wa dunia mwaka 2027 kuwa miongoni mwa matukio yatakayoleta wageni wengi nchini. Katika hatua nyingine, Rais Dkt. Samia amesema Serikali imetenga tena fedha za kujenga soko la kimataifa wilayani Hai. “Ninataka niwahakikishie, tunakwenda kujenga soko la kimataifa ndani ya wilaya hii,” amesema Rais Dkt. Samia, na kuongeza kuwa soko hilo litawapa wakulima sehemu ya uhakika ya kuuza mazao yao. Rais Dkt. Samia yupo mjini Moshi, katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi, unaofanyika katika Shule ya Polisi mjini humo. Vilevile, ameahidi kurejea mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya ziara rasmi ya kikazi, ambapo atatembelea miradi ya maendeleo na kuzungumza na wananchi wa mkoa huo.
Fri, 20 Nov 2026 12:01:59 +0000Comprendre les tensions entre la Guinée et le Burkina Faso
La Guinée a décidé de suspendre la diffusion de la chaîne publique burkinabè, la RTB, sur toute l'étendue du territoire. Mais, comment en est-on arrivé à cette situation ?
RecentlyZanzibar conducts eye health camp in partnership with Denmark’s Louis Nielsen
ZANZIBAR: THE Zanzibar Ministry of Health, through its Eye Health Services Coordination Unit, in collaboration with Denmark-based Louis Nielsen, has…
RecentlySAROTOGA YAGONGANA NA YUTONG CHALINZE, WATU WATATU WAJERUHIWA
Na Mwamvua Mwinyi, Pwani WATU watatu wamejeruhiwa katika ajali ya magari mawili kugongana iliyotokea eneo la Chamkweza, njia panda ya mnadani, Tarafa ya Chalinze, Wilaya ya Bagamoyo, mkoani Pwani. Ajali hiyo imetokea Novemba 20, 2026, majira ya saa 7:50 asubuhi, ikihusisha basi la Sarotoga lililokuwa likitokea Morogoro kuelekea Dar es Salaam na gari aina ya Yutong lenye namba za usajili T.453DCX, lililokuwa likitokea Kigoma kuelekea Dar es Salaam. Kaimu Kamanda wa Polisi, Kamishna Msaidizi wa Polisi Kennedy Mgani alieleza kuwa gari aina ya Yutong lilikuwa likiendeshwa na Ailly, mwenye umri wa miaka 47, mkazi wa Kigoma, huku basi la Sarotoga likiwa limeendeshwa na John Kisingi, mwenye umri wa miaka 34, aliyekuwa akitokea Dar es Salaam kuelekea Arusha. Mgani alifafanua, katika ajali hiyo, watu watatu waliokuwa kwenye basi la Sarotoga wamejeruhiwa, akiwemo Mrina Mtambuka, mwenye umri wa miaka 33, mkazi wa Kibaha, Mkoa wa Pwani; Haruna Yusuf, mwenye umri wa miaka 47, mkazi wa Kigoma; pamoja na Hamada Shabani, mwenye umri wa miaka 35, mkazi wa Kigoma ambaye ni kondakta wa basi la Sarotoga. Majeruhi wote wamepelekwa katika Kituo cha Afya Chalinze kwa matibabu zaidi. Chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa basi la Kampuni ya Sarotoga kuyapita magari mengine bila kuwa na tahadhari kwa watumiaji wengine wa barabara, ambaye alikimbia baada ya kusababisha ajali. Mgani alisisitiza kwamba, dereva huyo anapaswa kujisalimisha katika kituo cha polisi ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake, huku akiwataka madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani, kuepuka vitendo vya uzembe na kuacha kuyapita magari mengine pasipo kuchukua tahadhari.
Fri, 20 Nov 2026 11:58:21 +0000Kujenga kijijini ni wajibu au shinikizo
Soma zaidi...
RecentlyWatanzania wanne wang’ara tuzo za wanawake katika sayansi Afrika
Soma hapa...
RecentlyOPINION: When Silence Denies Justice: Fixing NSSF’s Survivor Claims Process
Read the full report from the original source.
RecentlyKindiki: We remain committed to an independent judiciary
Kindiki said the administration had demonstrated its commitment through increased budgetary allocations since taking office in 2022
RecentlyTanzania develops action plan to fast-track implementation of IHR 2005 goals
ARUSHA: TANZANIA has developed an action plan aimed at strengthening the implementation of the International Health Regulations (IHR 2005), with…
RecentlyRAIS SAMIA KUFUNGUA MKUTANO MKUU WA TUME ZA UCHAGUZI ECF-SADC
Na Mwandishi Wetu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 28 wa Mwaka wa Tume za Uchaguzi za Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (ECF-SADC) utakaofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 23 Novemba, 2026 hadi 24 Novemba, 2026. Akizungumza jijini Dar es Salaam, leo tarehe 20 Novemba, 2026, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Ndg. Ramadhani Kailima amesema mkutano huo wa siku mbili utahudhuriwa na Wenyeviti wa Tume za Uchaguzi 15, Makamishna, Watendaji Wakuu wa Tume za Uchaguzi za ECF-SADC na maafisa waandamizi kutoka katika Nchi wanachama. Amesema katika mkutano huo mada mbalimbali zenye lengo la kuboresha utendaji wa Tume za Uchaguzi na kuweka mikakati ya kuendana na mabadiliko ya teknolojia kwenye uendeshaji wa shughuli mbalimbali za uchaguzi, zitawasilishwa na kujadiliwa. Ndg. Kailima ameongeza kuwa tukio la ufunguzi wa mkutano huo litatangazwa Mubashara kupitia vyombo mbalimbali vya habari na kurasa za mitandao ya kijamii na amewakaribisha wananchi kufuatilia mkutano huo. Amezitaja tume wanachama wa ECF-SAC zitakazoshiriki mkutano huo kuwa ni Tume ya Uchaguzi ya Angola (CNE), Tume Huru ya Uchaguzi ya Botswana (IEC), Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) (CENI), Tume ya Uchaguzi na Mipaka ya Eswatini (EBC), Tume Huru ya Uchaguzi ya Lesotho (IEC), Tume ya Uchaguzi ya Malawi (MEC) na Ofisi ya Tume ya Uchaguzi ya Mauritius (ECO). Tume nyingine ni Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Msumbiji (CNE), Tume ya Uchaguzi ya Namibia (ECN), Tume Huru ya Uchaguzi ya Afrika Kusini (IEC), Tume ya Uchaguzi ya Seychelles (ECS), mwenyeji wa mkutano huo Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania (INEC), Tume ya Uchaguzi ya Zambia (ECZ), Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC); na Tume ya Uchaguzi ya Zimbabwe (ZEC). “Umoja huu umeendelea kuziwezesha Tume za uchaguzi kupata fursa ya kuimarisha uwezo wa kusimamia na kuratibu uendeshaji wa uchaguzi kwa njia ya kujadiliana na kubadilishana uzoefu kwenye masuala yanayolenga kuboresha, uratibu na usimamizi wa chaguzi”, amesema Ndg. Kailima na kuongeza kuwa: “Kupitia Mkutano Mkuu wa Mwaka wa 28 wa ECF SADC tunatarajia Nchi yetu itapata faida mbalimbali ikiwa ni pamoja na kudumisha na kukuza mahusiano ya kikanda na kimataifa, kutangaza vivutio vya utalii, Tume zetu za uchaguzi, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar zitapata fursa ya kujifunza na kubadilishana uzoefu na Tume zingine za Uchaguzi.” Kaulimbiu ya mkutano huo ni “Management of elections and social media - exploring the role of EMBs in the SADC Region’’, yaani, “Usimamizi wa uchaguzi na mitandao ya kijamii – kubaini wajibu wa Tume za Uchaguzi katika Ukanda wa SADC”.” Ameongeza kuwa maandalizi yote muhimu kuelekea Mkutano Mkuu wa 28 wa Mwaka wa ECF – SADC yamekamilika, hivyo Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi inatoa wito kwa umma wa Watanzania kujiandaa kuwapokea wageni kutoka nchi wanachama wa ECF-SADC wanaoshiriki mkutano huo wa kihistoria. ECF-SADC ni jukwaa lililoanzishwa tarehe 27 Julai, 1998 ambalo wanachama wake ni Tume za Uchaguzi za nchi za kusini mwa Afrika. Makao makuu ya Jukwaa hili yapo Mjini Gaborone, Botswana.
Fri, 20 Nov 2026 11:50:56 +0000IST seeks Tanzania’s facilitation in forming new NCPS to address a regulatory vacuum
MWANZA: THE Institution of Surveyors of Tanzania (IST) has requested the Government through the Ministry of Lands, Housing and Human…
RecentlyFurious NRM EC Chairperson Tanga Odoi Turns Guns on Judge Over Tororo Municipality MP Shyam Tanna’s Election Petition Victory
Read the full report from the original source.
RecentlyKsh800,000 cancer treatment benefit remains unchanged, SHA clarifies
SHA CEO Dr Mercy Mwangangi says the recent changes affect how cancer treatment is approved and priced, but do not reduce the approved benefit.
RecentlyIndiGo Air launches its maiden Mumbai-Dar direct flight
Read the full report from the original source.
RecentlyZAIDI YA WANANCHI 4,500 WAFANYIWA UCHUNGUZI WA MAGONJWA YA MOYO MOROGORO KUSINI MASHARIKI
Na Farida Mangube Morogoro Jumla ya wananchi 4,563 wamefanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo na magonjwa mengine yasiyoambukiza kupitia Kambi Maalum ya Afya iliyofanyika katika Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki, mkoani Morogoro. Kambi hiyo iliyoanza Novemba 10 na kufungwa rasmi leo, Novemba 20, 2026, ilifanyika katika tarafa za Ngerengere, Mikese na Mkuyuni kwa lengo la kusogeza huduma za kibingwa za afya karibu na wananchi. Akizungumza wakati wa kufunga kambi hiyo, Waziri wa Afya, Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa, alimpongeza Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki, Mheshimiwa Hamiss Taletale, kwa juhudi zake za kuhakikisha wananchi wanapata huduma za uchunguzi na matibabu ya kibingwa karibu na maeneo wanayoishi. Aidha, Waziri Mchengerwa aliwaagiza Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha hospitali zote nchini zinakuwa na upatikanaji wa dawa kwa kiwango cha asilimia 90 hadi 98 ili kuwawezesha wananchi kupata dawa wanazohitaji kwa uhakika. Pia, alimtaka Mbunge Taletale kuendelea na juhudi za kuwasaidia wananchi wake kwa kujitolea kusogeza huduma za afya karibu nao. Akitoa taarifa ya utekelezaji wa kambi hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Dkt. Tatizo Waane, alisema kambi hiyo imefanikiwa kwa kiasi kikubwa na kuthibitisha umuhimu wa kuwafikishia wananchi huduma za uchunguzi na matibabu mapema. Alisema kati ya wananchi 4,563 waliofanyiwa uchunguzi, watoto 533 walichunguzwa magonjwa ya moyo. Aidha, katika uchunguzi wa shinikizo la damu, watu 3,148, sawa na asilimia 69 ya waliopimwa, walibainika kuwa na kiwango cha juu cha shinikizo la damu. Dkt. Waane alisema takwimu hizo zinaonesha ukubwa wa changamoto ya shinikizo la damu katika jamii na kusisitiza umuhimu wa kuimarisha elimu ya afya, uchunguzi wa mara kwa mara pamoja na matibabu kwa watu wenye changamoto hiyo. Katika huduma nyingine, wananchi 536 walifanyiwa kipimo cha Echocardiography (ECHO) kwa ajili ya kuangalia muundo na utendaji kazi wa moyo, huku watu 651 wakifanyiwa kipimo cha Electrocardiography (ECG) kwa ajili ya kuchunguza mfumo wa umeme wa moyo. Vilevile, wananchi 483 walipata huduma za uchunguzi wa afya ya meno. Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo hilo, Hamiss Taletale, alisema wagonjwa 61 walipewa rufaa kwenda hospitali za mkoa, huku wagonjwa wengine 30 wakipewa rufaa kwenda Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya matibabu zaidi. Taletale, maarufu kama Babu Tale, alisema hadi sasa ametumia zaidi ya shilingi milioni 100 kugharamia matibabu ya wagonjwa waliopewa rufaa kwenda kwenye vituo vingine vya afya, fedha ambazo ni tofauti na gharama za kuendesha kambi hiyo. Alisisitiza kuwa ataendelea kuwahudumia na kuwasaidia wananchi wa jimbo lake bila kujali tofauti zao za kidini, kisiasa wala kikabila. Hata hivyo, alimuomba Waziri Mchengerwa kusaidia kutoa msukumo katika ujenzi wa barabara ya Bigwa–Kisaki ili iweze kujengwa kwa kiwango cha lami, akieleza kuwa itakuwa na manufaa makubwa kwa wananchi wa maeneo hayo.
Fri, 20 Nov 2026 11:47:44 +0000Ukraine updates: Russian attack 'one of largest,' Zelenskyy says
Read the full report from the original source.
RecentlyTanga Odoi Turns Guns on Judge Over Shyam Tanna’s Election Petition Victory
Read the full report from the original source.
RecentlyPage 100 of 1126 · 22511 stories