Search the region
22509 stories
Tanzania yafungua milango kwa uwekezaji wa madini ya kimkakati, yalenga kujenga viwanda badals ya kuuza malighafi
Read the full report from the original source.
RecentlyTRAMEPRO YATOA WITO WA KULINDA UADILIFU WA TAARIFA KWA AJILI YA UMOJA, AMANI NA MAENDELEO
Dar es Salaam, Septemba 28, 2026 — Shirika la Dawa Asilia na Ulinzi wa Mazingira Tanzania (TRAMEPRO) limetoa wito kwa wananchi, viongozi, waandishi wa habari na watumiaji wa mitandao ya kijamii kuhakikisha wanahakiki taarifa kabla ya kuzisambaza, likisisitiza kuwa taarifa sahihi ni msingi wa kujenga umoja, amani na maendeleo ya Taifa. Wito huo umetolewa leo, Septemba 28, 2026, wakati dunia ikiadhimisha Siku ya Kimataifa ya Upatikanaji wa Taarifa (International Day for Universal Access to Information). TRAMEPRO imesema maadhimisho hayo yanapaswa kuwa fursa ya kutafakari umuhimu wa wananchi kupata taarifa sahihi, za kuaminika, kwa wakati na zinazoweza kufikiwa, sambamba na wajibu wa kila mmoja kuzihakiki na kuzitumia kwa uadilifu. TRAMEPRO imesema maendeleo ya teknolojia za kidijitali, mitandao ya kijamii na zana za akili bandia yameongeza kasi ya uzalishaji na usambazaji wa taarifa, hivyo kuna umuhimu wa kujenga utamaduni wa kuhakiki taarifa kabla ya kuzisambaza. Kwa mujibu wa shirika hilo, taarifa sahihi zina nafasi muhimu katika kujenga uelewa, kuimarisha uwajibikaji, kulinda afya ya jamii, kuhifadhi mazingira na kuimarisha umoja, amani na mshikamano wa Taifa. Kaulimbiu ya maadhimisho ya mwaka huu inalenga “Kulinda Uadilifu wa Taarifa katika Enzi ya Kidijitali: Nafasi ya Upatikanaji wa Taarifa katika Kukabiliana na Mkanganyiko wa Taarifa.” Wito kwa Waandishi wa Habari TRAMEPRO imewasihi waandishi wa habari kuendelea kuzingatia weledi, maadili na ukweli katika utekelezaji wa majukumu yao, huku wakifanya uhakiki wa taarifa kabla ya kuzichapisha. Shirika hilo limesema vyombo vya habari vina nafasi muhimu katika kujenga uelewa wa jamii na kutoa taarifa zinazoweza kusaidia kuimarisha umoja, amani na mshikamano. Aidha, limewataka viongozi na taasisi za umma kutoa taarifa kwa wananchi kwa uwazi, usahihi, kwa wakati na kwa lugha inayoeleweka. Shirika hilo pia limeonya kuhusu taarifa zisizo sahihi zinazohusu afya, dawa na tiba, likisisitiza kuwa taarifa hizo zinaweza kuwa na madhara kwa afya na maisha ya wananchi. Changamoto nyingine zilizotajwa ni pamoja na upatikanaji usio sawa wa teknolojia, gharama za intaneti, ujuzi mdogo wa kidijitali na changamoto ya kutambua maudhui yaliyotengenezwa au kubadilishwa kwa kutumia teknolojia za akili bandia. TRAMEPRO imewataka wananchi na watumiaji wa mitandao ya kijamii kuwa na utamaduni wa kuhakiki taarifa kabla ya kuzisambaza, ili kuzuia taarifa zisizo sahihi kuwa chanzo cha hofu, migawanyiko au madhara kwa jamii. Shirika hilo pia limewataka wataalamu wa tiba asili kuzingatia usalama, ushahidi, maadili na uwajibikaji wanapotoa taarifa kuhusu dawa na tiba asili, na kuepuka madai ya kitabibu ambayo hayawezi kuthibitishwa. TRAMEPRO imesema Tanzania yenye umoja na amani inahitaji utamaduni wa mawasiliano unaoheshimu ukweli na utu wa kila mwananchi. “Taarifa sahihi hujenga uaminifu. Uaminifu hujenga uelewa. huimarisha Umoja na Amani. Kwa mujibu wa shirika hilo, taarifa sahihi zinaweza kusaidia kuelimisha jamii kuhusu afya, kumsaidia mkulima, kumlinda mtumiaji wa dawa, kuhamasisha uhifadhi wa mazingira na kumwezesha mwananchi kushiriki katika maendeleo ya Taifa. Siku ya Kimataifa ya Upatikanaji wa Taarifa huadhimishwa kila mwaka tarehe 28 Septemba, ikiwa na lengo la kuhamasisha upatikanaji wa taarifa, uwazi, uwajibikaji na mazingira yanayomwezesha mwananchi kupata taarifa muhimu kwa maisha na maendeleo yake. Taarifa hii imetolewa na Boniventura Mwalongo, Katibu Mkuu wa Shirika la Dawa Asilia na Ulinzi wa Mazingira Tanzania (TRAMEPRO).
Mon, 28 Sep 2026 15:48:31 +0000How Nigeria’s overlapping data rules affect fintechs and banks
Read the full report from the original source.
Recently6.4 million older Kenyans by 2045: Are systems ready? Experts says Kenya needed to prepare its systems for longer lives while ensuring older persons remain healthy
Experts says Kenya needed to prepare its systems for longer lives while ensuring older persons remain healthy
RecentlyHatma ya Dira 2050 iko mabegani mwa vijana wenye ujuzi
Read the full report from the original source.
RecentlyInjinia Samamba atoa maelekezo kwa wamiliki wa migodi, maafisa kujiandaa na mvua za El nino
Read the full report from the original source.
RecentlyDPP accuses Karugu brothers of threatening complainant, skipping court mention
Read the full report from the original source.
RecentlyWWF-Kenya, Forestry State Department partner to Drive 15 billion trees initiative
Read the full report from the original source.
RecentlyMotorists Rejoicing as Katonga–Lwera–Kalandazi Road Reconstruction Nears Completion
When floods struck in May 2023, the collapse of the Katonga Bridge and severe damage to the Lwera and Kalandazi swamp sections of the Kampala–Masaka highway plunged Uganda into a…
Recently“Don’t wait for Ministers to come to your areas and start reacting,” Hajji Kakande cautions RDCs
The Secretary in the Office of the President, Hajji Yunus Kakande, has urged Resident District Commissioners (RDCs) and other public servants to take a proactive approach to monitoring government programmes,…
RecentlyMAKAMU WA RAIS AAGIZA MILANGO IFUNGULIWE KWA VIJANA 10,000
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi ametoa wiki mbili kwa Wizara ya Mipango na Uwekezaji, Fedha na Kilimo kuandaa mpango wa mafunzo kwa Vitendo ambao utaanza kuchukua walau vijana 10,000 kupata uzoefu katika Taasisi, Mashirika ya Umma na Sekta binafsi ili kuandaa vijana watakaokuwa na uzoefu wa kujiajiri na kuajiriwa kama sehemu muhimu ya kutekeleza nguzo ya pili ya Dira ya Taifa 2050 na kusaidia maendeleo ya Nchi. Makamu wa Rais ametoa maelekezo hayo wakati alipomwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan, kwenye ufunguzi wa Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Mashirika ya Umma, kinachofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC). Amewataka Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Mashirika ya Umma kubadili namna taasisi hizo zinavyofanya kazi na kuwa injini ya mageuzi ya uchumi kuelekea Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, huku akielekeza kuanzishwa kwa mkakati huo utakaowapatia angalau wahitimu 10,000 nafasi za mafunzo kwa vitendo na kuwapatia fedha za kujikimu katika mashirika ya umma na wengine wasiopungua 20,000 katika sekta binafsi. " Kila mwaka kwa takribani vijana 62,570 wanahitimu elimu ya juu na hii ni takwimu ya mwaka Jana 2025 toka TCU, idadi hiyo haihusishi wale wanaomaliza VETA na Vyuo vya Kati. Ukiangalia TAESA takwimu zao zinaonesha vijana 3,200 pekee walikuwa wamepitia programu za mafunzo internship, idadi hii ni ndogo sana kwa kulinganishwa na wahitimu 62,570 kutoka vyuo mbalimbali nchini. Mlitazame hili kama uwekezaji wa kimkakati katika nguvu kazi ya Taifa kwa kubana matumizi ya kawaida, na hapa mtakuwa mmetekeza kwa Vitendo nguzo ya pili ya Dira 2050" alisisitiza Mhe. Ndejembi, amesema dhamana ya Watendaji, Wakuu wa Mashirika na Wenyeviti wa Bodi ni kubwa, na hivyo wanatakiwa kutekeleza majukumu yao kwa ustadi na umakini mkubwa na kwa wakati sahihi katika kujenga uchumi, kuibua fursa mpya na kuinua maisha ya watanzania. "Mashirika ya Umma yana nafasi ya kipekee katika kufikia malengo ya Dira 2050 kutokana na dhamana yake ya kusimamia mali za umma, kuendesha miundombinu ya kimkakati, kutoa huduma muhimu za nishati, usafirishaji, mawasiliano, fedha, afya, maji, na nyingine zinazobeba uchumi wetu. Kutokana na hilo, lazima tuyaangalie mashirika hayo kama injini ya mageuzi makubwa ya kiuchumi tunayoyalenga katika Dira 2050.” alisisitiza Ndejembi. Sambamba na ajira na ujuzi kwa vijana, Makamu wa Rais amezitaka Taasisi na Mashirika ya Umma ukiangalia namna ya kupunguza matumizi yasiyo na tija na utegemezi kwa Serikali, huku zikibuni vyanzo endelevu vya mapato na kuhakikisha kila shilingi ya umma inaleta thamani inayostahili. Ili kuhakikisha maelekezo hayo yanatafsiriwa kuwa matokeo, Ndejembi ameitaka Ofisi ya Msajili wa Hazina kuimarisha mfumo wa tathmini ya utendaji wa mashirika ya umma, na kutambua kwenye tuzo za mwaka ujao Taasisi zitakazotekeleza agizo la kuchukua vijana na kuwapa mafunzo. Amehitimisha kwa kuzitaka Taasisi na Mashirika kujiandaa mapema kukabiliana na athari za mvua za El Niño ili kulinda miundombinu na uwekezaji wa umma na kuhakikisha huduma muhimu kwa wananchi haziathiriki. Kikao hicho cha C-CEOs Forum 2026 kimewakutanisha jijini Arusha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi, Mashirika ya Umma na Wakala za Serikali, pamoja na Mawaziri, Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge, Makatibu Wakuu na viongozi wengine wa Serikali. Kikao hicho cha siku tatu kimeandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa lengo la kutoa mwelekeo wa kimkakati kuhusu mustakabali wa Mashirika ya Umma, kutathmini yalipotoka na kujadili hatua zinazopaswa kuchukuliwa ili kuongeza mchango wake katika uchumi na maendeleo ya Taifa, hususan wakati Tanzania imeanza utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Mon, 28 Sep 2026 15:30:55 +0000Case lodged to compel FKF, Sports Ministry to pay Harambee Stars debts immediately
Latest · Harambee Stars
RecentlyNGORONGORO YAIVUNJA MIAMBA C-CEOs FORUM ARUSHA.
Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) ni miongoni mwa taasisi kumi za Serikali nchini zilizooongoza katika ufanisi wa mapato, matumizi bora ya fedha za umma kwa tija na umahiri katika rejesho la mtaji kwa mashirika ambayo ni ya kibiashara. Akielezea kuhusiana na taasisi hizo kumi zilizotajwa vinara katika kundi hilo Msajili wa Hazina Bw. Nehemia Mchechu amesema mashirika yaliyofanya vizuri katika kundi hilo yameonesha umahiri mkubwa katika kudhibiti matumizi, kuongeza mapato na kusimamia vema rejesho Serikalini sambamba na utoaji huduma kidijitali kwenye utoaji wa huduma kwa wateja. Kikao hicho kilichofunguliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi kimehudhuriwa pia na Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi NCAA Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali Venance Mabeyo Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka hiyo Abdul-Razaq Badru ,Ngorongoro imeonesha ushiriki wake kwa kutangaza vivutio vya utalii mubashara kupitia luninga kubwa iliyopo nje ya ukumbi wa mikutano AICC jijini Arusha. Katika kipindi cha miaka ya hivi Karibuni NCAA imejipambanua katika kujitangaza kimkakati pamoja na kuibua vivutio vya mazao mapya ya utalii katika kampeni inayojulikana kama Ngorongoro Beyond the Crater. Katika ufunguzi wa kikao hicho Mheshimiwa makamu wa Rais aliwataka viongozi wa mashirika ya umma na binafsi kuja na mpango mkakati wa kutoa mafunzo kwa vitendo na kujitolea (intenship) kwa vijana 10,000 kila mwaka.\
Mon, 28 Sep 2026 15:22:54 +0000NEWZ ALERT : BRELA YATOA NOTISI YA MWISHO YA KUFUTA KAMPUNI 5277
Mon, 28 Sep 2026 15:20:19 +0000Sicily: Mount Etna ash disrupts Catania flights again
Read the full report from the original source.
RecentlyRDCs told: Don’t wait for ministers to expose problems in your districts
Read the full report from the original source.
RecentlySpaceX launches supersized Starship into orbit
Read the full report from the original source.
RecentlyBuilding African-language AI is easier than finding the data
Read the full report from the original source.
RecentlyBabu: MP record makes me fit for Nairobi governor Babu has outlined his record in Embakasi East and proposals to address city challenges
Babu has outlined his record in Embakasi East and proposals to address city challenges
RecentlyKAM Vice Chair Mary-Ann Musangi Calls for Private Sector to Drive AfCFTA at Unstoppable Africa 2026 Forum In New York
Latest · Kenya
RecentlyPage 1002 of 1126 · 22509 stories