Unganishwa

Search the region

22511 stories

Uncategorized · Issa Michuzi

DKT. MWIGULU AKUTANA NA BALOZI WA SWEDEN, WAJADILI KUIMARISHA USHIRIKIANO

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Ingrid Johansson, katika Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu, Magogoni, jijini Dar es Salaam, leo Novemba 20, 2026. Mazungumzo hayo yamejikita katika kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na kupanua ushirikiano kati ya Tanzania na Sweden katika maeneo mbalimbali yenye maslahi ya pamoja.

Fri, 20 Nov 2026 11:44:44 +0000
Uncategorized · The Citizen

Tanzania Labour federation split deepens as suspended deputy disputes election date

Read the full report from the original source.

Recently
Sports · Azam TV Videos

Simba SC yaweka wazi dhamira ya kuendeleza Unbeaten.

JKT TANZANIA vs SIMBA SC: “Ili kuendeleza rekodi ya kutofungwa, lazima uwe na mtazamo wa ushindi...” Kocha wa Simba SC, Steve Barker amesema ana imani na kikosi chake kuelekea mchezo wa kesho Novemba 21, 2026 dhidi ya JKT Tanzania, kutokana na maandalizi waliyoyafanya wakati wa mapumziko ya ligi. Barker amesema mapumziko hayo yamekuwa muhimu kwa kikosi chake kupata nafasi ya kujipanga upya na kurekebisha maeneo yenye mapungufu hasa baada ya matokeo yasiyoridhisha katika michezo miwili iliyopita ya ligi. Kwa upande wa mchezaji wa Simba SC, Charles Semfuko amesema mchezo huo ni kama fainali kwao kutokana na umuhimu wa alama tatu wanazozihitaji, hivyo wamejiandaa kupambana kuhakikisha wanapata ushindi. #NBCPremierLeague #LigiKuuYaNBC #NBCPLUpdates #ImenogaZaidi #JKTTanzania #SimbaSC #JKTTanzaniaSimbaSC

2026-11-20T11:18:36+00:00
Uncategorized · DW Rwanda

EU and UK hold a rare summit in bid to 'rebuild ties'

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Chimpreports

Muhoozi Appoints Maj Gen Richard Otto to Special Operations Office

Read the full report from the original source.

Recently
Business · HabariLeo

Teknolojia kurahisisha biashara AFCON 2027

Read the full report from the original source.

Recently
Sports · Azam TV Videos

VIWANJANI | Yanga SC kibaruani mbele ya Polisi Tanzania uwanja wa Ushirika Moshi.

Mchambuzi wa soka, Juma Abdul amesema mchezo huo utakuwa mgumu kwa Yanga SC kutokana na aina ya mpinzani wanayetarajia kukutana naye pamoja na hali ya uwanja, hususani eneo la kuchezea ambalo linaweza kuwa changamoto kwa timu hiyo.

2026-11-20T11:12:06+00:00
Uncategorized · The Star Kenya

Why Sifuna-Babu fallout should worry the Opposition

The disagreement centres on an alleged power-sharing arrangement between the two politicians over the leadership of the political outfit

Recently
Uncategorized · KBC

Man sentenced to 30 years for raping 80-year-old woman in Kiambu

Read the full report from the original source.

Recently
Business · Issa Michuzi

CHINA YATAKA KUONGEZA UWEZO WA USAFIRISHAJI TAZARA HADI KUFIKIA TANI MILIONI 2.4 ZA MIZIGO

NA MWANDISHI WETU CHINA imesema mradi wa ufufuaji wa Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) unatarajiwa kuongeza uwezo wa usafirishaji wa mizigo kutoka tani 200,000 za sasa hadi tani milioni 2.4. Imeelezwa mradi huo unatarajiwa kupunguza muda wa usafirishaji kwa karibu theluthi mbili, hatua inayolenga kuimarisha usafirishaji na kukuza shughuli za kiuchumi katika ukanda huo. Akizungumza katika uzinduzi wa ziara ya waandishi wa habari wa China na Tanzania ya kutembelea reli ya TAZARA, Balozi wa China nchini Tanzania, Chen Mingjian, alisema mradi huo ni sehemu ya juhudi za kuimarisha ushirikiano wa Tanzania, Zambia na China. Alisema ziara hiyo yenye kaulimbiu “Kuhuisha Mustakabali, Kushirikiana Katika Ustawi” imeandaliwa katika kuadhimisha miaka 50 tangu reli hiyo ianze rasmi kutoa huduma, imekuwa alama ya urafiki na mshikamano kati ya nchi hizo China, huku ikichangia ukombozi, uhuru na maendeleo ya nchi za Afrika. Chen alisema mradi huo hautaishia katika kuboresha usafiri pekee, bali pia utaimarisha mawasiliano ya kikanda, kupunguza gharama za usafirishaji kwa nchi zisizo na bandari na kukuza maendeleo ya kilimo cha kisasa, miundombinu pamoja na maeneo ya viwanda. Aidha alisema hatua hiyo inalenga kuboresha maisha ya wananchi wanaoishi katika maeneo yanayopitiwa na reli hiyo na kuifanya TAZARA kuwa kitovu kipya cha ukuaji wa uchumi. Pia Chen alizitaka taasisi za habari za China na Tanzania kutumia ziara hiyo kuandika na kuonesha maendeleo ya mradi, historia ya reli hiyo na mabadiliko ya maisha ya wananchi wanaoishi kandokando ya reli. Alisema vyombo vya habari vina nafasi muhimu ya kujenga uelewa na kuimarisha urafiki kati ya wananchi wa nchi hizo kupitia taarifa zinazotokana na ushuhuda na uchunguzi wa moja kwa moja. "China itaendelea kushirikiana na Tanzania na Zambia kuendeleza roho ya TAZARA, kutekeleza mradi wa ufufuaji wa reli hiyo na kujenga Ukanda wa Ustawi kwa lengo la kukuza mshikamano, ushirikiano na maendeleo ya pamoja kati ya China na Afrika", alisema. Naye, Naibu Mkurugenzi wa Wizara ya Uchukuzi Benjamin Adam Mbimbi alisema hiyo ufufuaji wa reli hiyo unalenga kuongeza uwezo wake wa kusafirisha mizigo ili kuimarisha biashara ya kikanda na kukuza maendeleo ya kiuchumi. Alisema mradi huo unatekelezwa kwa ushirikiano wa Serikali za Tanzania na Zambia na Kampuni ya Uhandisi na Ujenzi wa China (CCECC). Mbimbi alisema mradi huo utahusisha ukarabati wa miundombinu ya reli, mifumo ya mawasiliano na uashiriaji na upatikanaji wa vichwa vya treni na mabehewa, kwa lengo la kuifanya TAZARA kuwa reli ya kisasa, yenye ufanisi, uhakika na uwezo wa kujiendesha kibiashara. Alisema ufufuaji huo utaimarisha ushindani wa Bandari ya Dar es Salaam, kupunguza gharama za usafirishaji na kuunganisha masoko ya Zambia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na nchi nyingine za Kusini na Kati mwa Afrika. "Serikali itaimarisha pia miundombinu ya bandari, vituo vya makasha na uratibu kati ya TAZARA, Shirika la Reli Tanzania (TRC), Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na wadau wengine wa usafirishaji. Aidha, Mbimbi aliitaka sekta ya habari Tanzania na China kutumia ziara hiyo kuelimisha umma kwa kutoa taarifa sahihi na zenye uwiano kuhusu maendeleo ya mradi huo, akisisitiza kuwa ufufuaji wa TAZARA ni uwekezaji wa kimkakati utakaosaidia biashara, ajira, ushirikiano wa kikanda na ustawi wa wananchi. Naye, Hamisi Shimye ambaye ni Mratibu wa Taasisi ya Habari Development, alisema ufufuaji na uboreshaji wa Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) unatarajiwa kuwa kichocheo muhimu cha mageuzi ya kiuchumi barani Afrika kwa kuongeza ufanisi wa usafirishaji, kukuza biashara ya kikanda na kuvutia uwekezaji katika sekta ya viwanda. Alisema mradi huo una fursa kubwa ya kuimarisha nafasi ya Tanzania kama kitovu cha biashara na usafirishaji katika Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika. Alisema TAZARA haipaswi kuangaliwa kama miundombinu ya kusafirisha mizigo pekee, bali kama nyenzo ya kimkakati ya kuunganisha uchumi wa nchi mbalimbali na kufungua fursa mpya za maendeleo. Alisema makubaliano ya ufufuaji wa reli hiyo yaliyohitimishwa Septemba 29, 2025, kati ya Tanzania, Zambia na China, yanahusisha uwekezaji unaokadiriwa kufikia dola za Marekani bilioni 1.4 chini ya mkataba wa uendeshaji wa miaka 31. Kwa mujibu wa Hamis, mradi huo unahusisha ukarabati wa takribani kilomita 1,860 za reli, ununuzi wa vichwa vipya 34 vya treni, mabehewa 760 ya mizigo na mabehewa 16 ya abiria, pamoja na kuboresha mifumo ya mawasiliano na uendeshaji. Alisema kukamilika kwa mpango huo kutakuwa na umuhimu mkubwa katika kupunguza gharama za usafirishaji, kuongeza uwezo wa Bandari ya Dar es Salaam kuhudumia mizigo ya nchi jirani na kuimarisha biashara baina ya nchi za Afrika. Alisisitiza kuwa fursa zinazotokana na TAZARA zinapaswa kutumika kukuza viwanda vya ndani, hususan vya kuchakata madini na mazao ya kilimo, badala ya kuendelea kusafirisha malighafi kwenda nje bila kuongeza thamani yake. "Maendeleo ya reli hiyo yanapaswa kuambatana na uwekezaji katika maeneo ya viwanda, maghala, vituo vya biashara na huduma nyingine za kiuchumi zitakazozalisha ajira kwa vijana." Alisema Aidha, alieleza kuwa ushirikiano kati ya China na Afrika unapaswa kwenda zaidi ya ujenzi wa miundombinu na kujikita katika uhamishaji wa teknolojia, mafunzo ya kitaalamu, ubunifu na kujenga uwezo wa Waafrika kusimamia na kuendeleza miradi mikubwa ya kimkakati. Alisema mafanikio ya TAZARA hayapaswi kupimwa kwa idadi ya treni zitakazonunuliwa au kilomita za reli zitakazokarabatiwa pekee, bali pia kwa ajira zitakazozalishwa, viwanda vitakavyoanzishwa, gharama za usafirishaji zitakazopungua na mchango wake katika kuboresha maisha ya wananchi. Hivyo, alisema Tanzania na Zambia zinapaswa kuitumia reli hiyo kama daraja la kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kukuza ustawi wa wananchi wa nchi hizo na Afrika kwa ujumla.

Fri, 20 Nov 2026 11:05:52 +0000
Uncategorized · BBC Rwanda

Amerika: Yangiwe gufungurwa by'agateganyo nyuma y'imyaka 32 yishe abana be babiri

Mu iburanisha, Susan Smith yavuze ko yicuza cyane ibyo yakoze kandi ko iyo aza kugira amahirwe yari guhindura ibyabaye.

Recently
Uncategorized · Isango Star

INGINGO Z'INGENZI Z'IMPAMVU YO GUSABA GUHINDUZA AMAZINA

Fri, 20 Nov 2026 13:00:36 +0200
Business · Issa Michuzi

Benki ya Exim Yaimarisha Ushirikiano na Sekta ya Madini Kupitia TMIC 2026

Jitihada za Tanzania kuongeza manufaa ya kiuchumi yatokanayo na rasilimali za madini zinafungua fursa mbalimbali katika mnyororo mzima wa thamani wa sekta hiyo, kuanzia uchimbaji na uchakataji hadi uzalishaji viwandani na huduma saidizi. Hata hivyo, ili kutumia fursa hizo kikamilifu, kunahitajika uwekezaji, upatikanaji wa mitaji na ushirikiano imara utakaowezesha rasilimali za madini kuchochea maendeleo ya viwanda na ukuaji endelevu wa uchumi. Katika kuunga mkono juhudi hizo, Benki ya Exim Tanzania imeshiriki katika Mkutano wa Saba wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini Tanzania (Tanzania Mining and Investment Conference – TMIC 2026), ikiwa miongoni mwa wadhamini wa mkutano huo. Kupitia ushiriki wake, Benki inaendeleza ushirikiano na wadau mbalimbali katika kukuza uwekezaji na kuongeza thamani ya madini nchini. Mkutano huo wa siku tatu, ulifanyika kuanzia Novemba 19 hadi 21 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam, unawakutanisha viongozi wa Serikali, wawekezaji, kampuni za uchimbaji madini na taasisi za fedha kujadili fursa za uwekezaji, mahitaji ya kifedha, teknolojia na ushirikiano unaoweza kuharakisha maendeleo ya sekta ya madini nchini. Kaulimbiu ya mkutano wa mwaka huu, ‘Madini Yaliyoongezwa Thamani: Chachu ya Ukuaji wa Viwanda na Uchumi,’ Kauli mbiu hii inaakisi azma ya Tanzania ya kupanua shughuli za uchakataji wa madini nchini, kuimarisha viwanda vinavyotumia madini kama malighafi na kuongeza manufaa ya kiuchumi yatokanayo na rasilimali hizo. Ajenda ya mkutano pia inasisitiza umuhimu wa upatikanaji wa mitaji na ubia wa kimkakati katika kufanikisha azma hiyo. Ushiriki wa Benki ya Exim Tanzania katika mkutano huo unaakisi dhamira yake pana ya kusaidia biashara na uwekezaji katika mnyororo mzima wa thamani wa madini. Benki inatambua kuwa ukuaji wa sekta hiyo hauishii kwenye uchimbaji pekee, bali unahusisha pia uchakataji wa madini, usambazaji wa vifaa na mitambo, ukandarasi, usafirishaji na biashara nyingine zinazotoa huduma kwa sekta hiyo. Dhamira hiyo inadhihirishwa pia na hatua za Benki kuimarisha uwepo wake mkoani Geita, mojawapo ya maeneo muhimu ya uchimbaji madini nchini. Mwezi Mei 2026, Exim Bank ilifungua tawi jipya mkoani humo ili kusogeza huduma zake za kifedha karibu na wachimbaji madini, wafanyabiashara, wajasiriamali na wadau wengine wa shughuli za kiuchumi katika eneo hilo. Kupitia huduma ya Ufadhili wa Miradi (Project Finance), Benki ya Exim Tanzania hutoa ufadhili kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mikubwa katika sekta mbalimbali. Uwezo wake katika eneo hili unatokana na uelewa wa kina wa mazingira ya biashara nchini na mifumo ya udhibiti, pamoja na uhusiano imara ambao Benki imejenga na taasisi za fedha za maendeleo. Mbali na ufadhili wa miradi, Benki ya Exim hutoa huduma mbalimbali za kibenki kwa biashara, zikiwemo mikopo ya mtaji wa uendeshaji, mikopo ya muda mfupi na mikopo ya muda maalumu, ufadhili wa pamoja wa mikopo, huduma ya punguzo la ankara, huduma za fedha za biashara, huduma za kibenki za kidijitali na usimamizi wa fedha. Huduma hizi zimekusudiwa kusaidia biashara zinazohusika katika mnyororo wa thamani wa madini kusimamia mtiririko wa fedha, kugharamia shughuli za uendeshaji na kutekeleza mipango ya kukuza na kupanua biashara zao. Katika siku ya ufunguzi wa mkutano huo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Tanzania, Jaffari Matundu, aliongoza ujumbe wa viongozi waandamizi na wataalamu kutoka vitengo mbalimbali vya Benki, ushriki wao ni kielelezo cha dhamira ya Benki ya kuimarisha ushirikiano na wadau wa sekta hiyo, kujadiliana nao na kubaini fursa zinazoweza kuchochea uwekezaji katika sekta ya madini. Akizungumzia ushiriki wa benki ya Exim Tanzania katika mkutano huo, Matundu alisema: “Fursa katika sekta ya madini nchini haziishii kwenye shughuli za uchimbaji pekee, bali zinajumuisha pia biashara zinazohusika katika mnyororo mzima wa thamani, kuanzia uchakataji na usambazaji wa vifaa hadi usafirishaji na huduma nyingine za ndani. Benki yetu inalenga kujenga ushirikiano imara na kutoa suluhisho za kifedha zinazokidhi mahitaji ya biashara. Kwa kufanya hivyo, tunaziwezesha biashara kukua, tunachochea maendeleo ya viwanda na kusaidia Tanzania kupata manufaa makubwa zaidi ya kiuchumi kutokana na rasilimali zake za madini”. Kupitia udhamini na ushiriki wake katika mkutano wa TMIC 2026, Exim Bank imeonyesha kuendelea kuunga mkono azma ya Tanzania ya kukuza uwekezaji na kuongeza manufaa yatokanayo na rasilimali zake, huku ikichangia ukuaji wa muda mrefu na endelevu wa sekta ya madini nchini. Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Tanzania, Jaffari Matundu (wa pili kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine wa Benki hiyo, wakati wa Mkutano wa Saba wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini Tanzania (TMIC 2026), unaofanyika jijini Dar es Salaam. Benki ya Exim Tanzania ni miongoni mwa wadhamini wa mkutano huo, unaotumia jukwaa lake kuimarisha ushirikiano na wadau wa sekta ya madini na kuonesha namna huduma za kifedha za Benki zinavyoweza kusaidia biashara katika mnyororo wa thamani wa madini. Wengine katika picha ni Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki hiyo, Shani Kinswaga (wa pili kulia), pamoja na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano, Stanley Kafu (kulia)

Fri, 20 Nov 2026 08:00:00 +0000
Uncategorized · The Standard

Inside deadly world of landlord tenant feuds

Cases abound of landlords going to extreme lengths to force tenants to pay, including sealing doors, removing roofs, disconnecting water and electricity, and even hiring goons to intimidate occupants

Fri, 20 Nov 2026 13:25:00 +0300
Uncategorized · BBC Afrique

Un expert médico-légal affirme que son analyse des photos de l'autopsie d'Epstein suggère que le financier a été assassiné en prison

Le professeur Michael Freeman a déclaré à la BBC qu'il estimait que les blessures du délinquant sexuel condamné étaient compatibles avec un homicide.

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

PS Omollo: 114,000 adults receive national IDs in Nyanza

PS Raymond Omollo credits youth initiative with helping identify first-time applicants, following the removal of ID fees

Recently
Uncategorized · Burundi Forum

Burundi : La Russie offre 1 102 tonnes de vivres à 40 000 victimes des aléas climatiques

À Bujumbura, la Russie renforce son soutien alimentaire aux populations vulnérables du Burundi. Mukaza, Bujumbura (BDIAGNEWS), 17/11/2026 – L’ambassadeur russe Tchernenko Sergueï a remis au Programme alimentaire mondial (PAM) 1 102 tonnes de vivres, d’une valeur de deux millions de dollars, destinées...

Fri, 20 Nov 2026 10:43:39 +0000
Uncategorized · SoftPower News

Gen Muhoozi Appoints Maj Gen Richard Otto to Special Operations Office

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · DW Rwanda

Ukraine updates: Kyiv targeted by missile strikes, bridges hit

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · DW Rwanda

Have we missed our chance to stop climate change?

Read the full report from the original source.

Recently

Page 101 of 1126 · 22511 stories