Unganishwa

Search the region

22499 stories

Uncategorized · The Ankole Times

‘I Am Going To Hang Eddie Mutwe And All NUP Terrorists’ Muhoozi Kainerugaba Confirms

Read the full report from the original source.

Recently
National · The Observer Uganda

Minister Balaam closes Yalelo fish shop in Busia

Local Government minister Balaam Barugahara has ordered the immediate closure of Yalelo Fish shop in Busia town following complaints from local fish traders over its…

Recently
Uncategorized · Issa Michuzi

TONE LA MAJI LA KWANZA KILWA LAFUNGULIWA,WAZEE WAOMBA DUA KWA RAIS SAMIA

Mradi mkubwa wa Maji wa Miji 28 unaotekelezwa katika Kijiji cha Mavuji kilwa Masoko umekamilika na wananchi wameanza kupata huduma ya maji na kuondokana na changamoto ya magonjwa kama kipindupindu ulokua unawakumba mara kwa mara kutokana na adha ya maji. Baada ya kufunguliwa kwa tone la kwanza la Mradi huu mkubwa wa kihistoria, Wananchi wameupokea mradi huu kwa furaha na shangwe huku wazee wakimuombea Dua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan. Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso (Mb) ametembelea mradi huo nakujionea utekelezaji wake uku akisema maunganisho mapya ya huduma ya maji kwa wananchi wa Mavuji ni siku Saba tu. Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mavuji, kilwa Masoko , Lindi baada ya kukagua mradi mkubwa wa Maji wa Miji 28, amesisitiza kwa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa mazingira Kilwa Masoko (KIMUWASA) na Mamlaka zote za maji nchini huduma ya kuunganishiwa maji majumbani isizidi siku Saba. Mradi huu mkubwa wa Maji wa Miji 28 Kilwa umegharimu kiasi cha Fedha Shilingi Bilioni 44 za kitanzania na umefikia asilimia 94.3 ya utekelezaji wake na tayari umeanza kutoa huduma kwa wakazi wa Kijiji cha Mavuji huku ukitegemewa kuwanufaisha wakazi zaidi ya 59,983 ambapo lita milioni 5 .5 za maji zitazalishwa kwa siku kutoka kwenye chanzo cha Mto Mavuji.

Sat, 26 Sep 2026 19:05:47 +0000
Uncategorized · Citizen Digital

Murkomen defends Samburu security operation, orders caution to prevent collateral damage

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

Ndindi Nyoro demands investor protection, full disclosure of Lamu refinery shareholders

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

University of Eldoret probes lecturer over pro-Ruto remarks, threats to students

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Ankole Times

NUP Is Full Of Terrorists!! Muhoozi Says NUP Members, Including Eddie Mutwe Will Be Hanged

Read the full report from the original source.

Recently
National · Issa Michuzi

KIHONGOSI: RAIS SAMIA NI RAIS MWENYE UWEZO MKUBWA BARANI AFRIKA

NA MWANDISHI WETU, TANGA KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Kihongosi, amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ni kiongozi mwenye uwezo mkubwa ndani ya Bara la Afrika, mvumilivu na mchapakazi. Kihongosi ameyasema hayo wakati akihutubia mamia ya wananchi wa Tanga katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Lamore, ikiwa ni hitimisho la ziara yake mkoani humo ya kukagua uhai wa Chama pamoja na utekelezaji wa Ilani ya CCM ya 2025–2030. Amesema Rais Samia ameithibitishia dunia kuwa wanawake wanaweza kuongoza nchi kwa ufanisi na kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ndani ya muda mfupi. “Rais Samia ni kiongozi mwenye uwezo mkubwa, si Tanzania pekee bali pia ndani ya Bara la Afrika. Ni mvumilivu, mchapakazi, mwenye hofu ya Mungu, anayesikiliza na kutatua kero za wananchi,” amesema Kihongosi. Amesema utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini, ikiwemo mkoani Tanga, ni miongoni mwa ushahidi wa juhudi za Serikali katika kuendeleza maendeleo ya Taifa. Ametaja baadhi ya miradi hiyo kuwa ni ujenzi wa Bandari ya Tanga, ukarabati na upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Tanga pamoja na ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR). Aidha, Kihongosi amewataka wananchi kuendelea kumuunga mkono Rais Samia katika jitihada za kuwatumikia Watanzania na kuhakikisha Taifa linaendelea kupata maendeleo endelevu.

Sat, 26 Sep 2026 18:43:55 +0000
National · Issa Michuzi

DIWANI KATA YA BUKANDWE WILAYANI MBOGWE ALIA SHULE KUTELEKEZWA,KUCHAKAA

Na George Maziku, Mbogwe DIWANI Kata ya Bukandwe, iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Mbogwe, mkoani Geita Paulo Raphael Sahani amewalaumu wazazi katika shule ya msingi Kanegere, iliyopo kijiji cha Kanegere wilayani humo, kwa kuitelekeza shule hiyo na kusababisha uchakavu mkubwa. Diwani huyo ametoa lawama hizo jana Alhamisi, Septemba 24, katika sherehe za mahafari ya 22 ya wanafunzi waliohitima darasa la saba mwaka huu, ambapo diwani huyo alikuwa mgeni rasmi. Alisema kuwa wazazi na wananchi wa kijiji cha Kanegere wameacha kujitolea kuchangia maendeleo ya shule yao, badala yake jukumu hilo wamewaachia wawekezaji wa sekta ya madini waliopo kijijini hapo, ambao hatahivyo diwani huyo alidai hawasomeshi watoto wao katika shule hiyo. "Sisi viongozi, walimu, kamati ya shule na wazazi wa shule hii kwa ujumla wetu tumefeli kabisa kuihudumia shule yetu. Tumeitelekeza kabisa na kuifanya ichakae na kukosa hadhi ya kuitwa shule inayotegewa kutoa elimu bora kwa watoto wetu. Tumewaachia wawekezaji jukumu la kuhudumia shule yetu lakini wao hawana watoto wanaosoma hapa", alisema diwani Sahani. "Lazima tubadilike, tuanze kuchangia shule yetu sasa. Wazazi wa watoto wanaohitimu darasa la saba wachangie angalau mfuko mmoja wa saruji kwa ajili ya maendeleo ya shule hii, haiwezekani mtoto akae hapa miaka saba halafu aondoke hivi hivi bila kuchangia chochote, na katika kipindi hicho inawezekana ameharibu miundombinu ya shule kama milango, madirisha au ameharibu bati kwa kutupa mawe kwenye paa, hii siyo sawa hata kidogo", alifafanua Sahani. Sahani alisema kuwa kuanzia mwakani kutakuwa na mabadiliko makubwa ambapo kila mzazi wa mtoto anaehitimu darasa la saba katika shule hiyo atatakiwa kuchangia angalau mfuko mmoja wa sementi kwa ajili ya ukarabati na umaliziaji wa majengo ya shule ya Kanegere. "Tuanze mwakani kwasababu tutakuwa na wahitimu wengi, kwa maana wanafunzi waliopo leo darasa la sita na la tano watahitimu pamoja. Tunaweza kuwa na wahitimu kati ya 300 mpaka 400, hivyo tunaweza kupata mifuko 300 mpaka 400 ya saruji na kuweza kumalizia baadhi ya majengo yetu na kufanyia ukarabati mengine", alisisitiza diwani huyo. Wakati huo huo diwani huyo amewatolea wito watu wote waliosoma shule ya msingi Kanegere kuikumbuka shule hiyo kwa kuchangia maendeleo yake. Diwani huyo ambaye pia alihitimu darasa la saba katika shule hiyo mwaka 2004, aliahidi kuwatafuta na kuwaunganisha watu wote waliohitimu shuleni hapo kati ya mwaka 2004 mpaka 2010 ili waweze kuchangia ujenzi na ukarabati wa shule yao kama shukrani kwa mafanikio yao ya leo. "Napenda kutangaza kupitia mahafari haya kwamba katika mahafari ya mwaka ujao, wahitimu wote wa shule hii wa kuanzia mwaka 2004 mpaka 2010 ndio watakuwa wageni rasmi na mimi ndiye mwenyekiti wa kamati ya maandalizi hayo, nitawatafuta kila mahali walipo na kuwashawishi wachangie yao", alibainisha diwani huyo. Aliongeza, "Lazima tufanye kazi mchana na usiku ili kurejesha haraka hadbi ya shule yetu, inatubidi turudishe shukrani zetu kwenye shule iliyotusomesha. Inakuwaje tutoe fungu la kumi kanisani halafu tushindwe kuchangia shuleni", alihoji diwani huyo. Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi waliohitimu darasa la saba shuleni hapo mwaka huu walielezea furaha yao pamoja na matumaini yao ya baadaye. "Najisikia vizuri na nina furaha sana kufikia hatua hii. Malengo yangu ni kuendelea na masomo ya sekondari na chuo ili niweze kutimiza ndoto zangu za kuwa rubani wa ndege", alisema Janeth Emmanuel (14) mmoja wa wahitimu wa mwaka huu. Nae mhitimu mwingine Gaudencia William (13) alisema kuwa ana imani kubwa kwamba atafaulu mtihani wake wa darasa la saba na kuendelea na masomo ya sekondari na hatimaye kutimiza lengo lake la kuwa daktari wa binadamu. "Mimi nataka kuwa daktari wa kutibu watu, naamini nitafaulu kwenda sekondari na nikifikaa huko nitasoma masomo ya sayansi kwasababu nayapenda na ninayaweza", alijigamba Gaudencia.

Sat, 26 Sep 2026 18:36:51 +0000
National · Issa Michuzi

SERIKALI KUFANYA MAREKEBISHO YA SHERIA YA NDOA KUKOMESHA NDOA ZA UTOTONI

Na Janeth Raphael - MichuziTv Serikali imesema ipo katika mashauriano ya kufanya marekebisho ya baadhi ya vifungu vya Sheria ya Ndoa kwa lengo la kukabiliana na tatizo la ndoa za utotoni na kuhakikisha watoto wa kike wanapata fursa ya kuendelea na elimu bila vikwazo. Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Juma Zuberi Homera, amesema hatua hiyo inalenga kuweka mazingira yatakayowawezesha mabinti kuendelea na masomo kuanzia ngazi ya awali hadi kidato cha sita, huku wakilindwa dhidi ya ndoa za utotoni na ukatili wa kijinsia. Dkt. Homera ameyasema hayo jijini Dodoma wakati wa programu ya “Sema na Waziri”, ambapo alieleza kuwa Serikali inaendelea na mashauriano kuhusu mabadiliko ya sheria hiyo ili kushughulikia changamoto zinazowakabili watoto wa kike. Amesema Serikali inatambua umuhimu wa elimu katika kumwezesha mtoto wa kike kujenga maisha yake na kufikia ndoto zake, akisisitiza kuwa uwekezaji katika elimu na mitaji ni miongoni mwa nguzo muhimu za kuwawezesha wasichana kujikwamua kiuchumi. Katika hatua nyingine, Dkt. Homera amepongeza juhudi zinazofanywa na Plan International Tanzania katika kutetea na kulinda haki za watoto wa kike, akiahidi kuwa Wizara itaendelea kushirikiana na taasisi hiyo katika kukabiliana na ukatili wa kijinsia na kuwawezesha mabinti walio katika mazingira magumu. Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Plan International Tanzania, Jane Sembuche, amesema takwimu zinaonesha kuwa asilimia 29.1 ya wanawake wenye umri wa miaka 20 hadi 24 waliolewa kabla ya kufikisha miaka 18, hali ambayo imekuwa na athari katika fursa zao za elimu na maendeleo ya kiuchumi. Sembuche ameitaka Serikali kuharakisha mchakato wa marekebisho ya Sheria ya Ndoa ili kuweka miaka 18 kuwa umri wa chini wa ndoa kwa wote, akieleza kuwa hatua hiyo itasaidia kulinda haki za watoto na kuchangia utekelezaji wa malengo ya Dira ya Tanzania 2050.

Sat, 26 Sep 2026 18:31:27 +0000
Uncategorized · Citizen Digital

Opposition leaders accuse Ruto government of abductions, torture

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

'Ata ukiongeza kura Uganda, wewe ni one term!' Kalonzo slams Ruto over Murkomen’s border mobilisation

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · UN News Burundi

Cuba warns against ‘law of the jungle’ as Foreign Minister denounces US pressure

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · UBC

President Museveni hails Pastor Kayanja’s work, backs African integration

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Observer Uganda

Ebola: UAE lifts travel restrictions on Ugandan nationals

The United Arab Emirates (UAE) has lifted travel and entry restrictions imposed on Ugandan nationals following the Ebola outbreak in Uganda. The decision was announced…

Recently
Uncategorized · Issa Michuzi

Pelican Payday Yaja Meridianbet Na Safari Ya Mabonanza

MASHABIKI wa michezo na burudani ya kasino wana sababu nyingine ya kuongeza burudani zao, baada ya Pelican Payday kuwasili kwenye jukwaa la kasino mtandaoni la Meridianbet . Mchezo huu mpya kutoka Pragmatic Play umeingia na upepo mpya, ukiwaalika wachezaji kuanza safari ya kusisimua iliyojaa burudani na fursa za kupata ushindi. Wakati pelican anapaa angani akitafuta mawindo yake, safari ya Pelican Payday nayo inaanza kwa mchezaji kucheza na kusubiri kile kitakachojitokeza. Kinachofanya ujio huu kuwa wa kuvutia zaidi ni kwamba wachezaji wanaweza kuanza kuufurahia mchezo huu kabla haujachukua safari yake rasmi. Hii ni nafasi ya kujitumbukiza katika ulimwengu wa Pelican Payday, kuzoea mchezo na kufurahia kila mzunguko huku msisimko ukipanda. Kila mzunguko unaweza kuleta msisimko mpya, hivyo safari hii si ya kukaa pembeni, bali ni ya kuingia uwanjani na kuona kile ambacho mchezo umeandaa. Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi. Kupitia kasino mtandaoni ya Meridianbet, Pelican Payday inaleta ladha mpya kwa wapenzi wa michezo ya kasino wanaotafuta burudani tofauti. Pragmatic Play, ambayo imekuwa ikileta michezo mbalimbali yenye mvuto kwa wachezaji, safari hii imekuja na Pelican Payday ikiwa na mazingira yanayolenga kuifanya kila raundi kuwa sehemu ya burudani. Hivyo, unapofungua mchezo huu, ni muda wa kuanza safari mpya ambayo kila mzunguko unakuwa na simulizi yake. Lakini safari ya Pelican Payday haiishii hapo tu. Kiini chake ni kufurahia mchezo huku ukifuatilia uwezekano wa kupata ushindi unaoweza kuongeza msisimko zaidi. Kila raundi ina nafasi yake katika safari hii, na kadiri raundi zinavyozunguka, ndivyo hamu ya kuona kitakachotokea inavyoongezeka. Kwa wachezaji wanaopenda burudani, msisimko na matarajio ya ushindi, Pelican Payday sasa imefungua lango lake ndani ya kasino ya Meridianbet . Sasa ni wakati wa kupaa na Pelican Payday. Ingia Meridianbet kasino , tafuta mchezo wa Pelican Payday kutoka Pragmatic Play na anza kuonja burudani ya mchezo huu mpya kabla safari yake rasmi haijachukua kasi.

Sat, 26 Sep 2026 06:00:00 +0000
Uncategorized · UBC

Spotting AI writing: how reliable are the detectors?

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · UBC

Pope celebrates giant Paris mass, flies to Lourdes

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · UBC

Guinea opposition figure, former PM Sidya Toure, dies in Paris

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · UBC

UAE eases Ebola-related entry restrictions on Ugandans

Read the full report from the original source.

Recently

Page 1030 of 1125 · 22499 stories