Search the region
22499 stories
MAFUNZO YA UONGOZI NI MUHIMU KUKIIMARISHA CCM - ABDI
Na MWANDISHI WETU, Zanzibar NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Abdi Mahamoud Abdi, amesema mafunzo ya uongozi ni muhimu katika kuwawezesha viongozi na wanachama wa chama hicho kuwa wazalendo, pamoja na kuzingatia na kutekeleza sera, kanuni na taratibu za CCM. Abdi ameyasema hayo leo, Septemba 26, 2026, wakati wa hafla ya ufunguzi wa mafunzo ya Itikadi, Uenezi na kuongeza wanachama wapya wa CCM kwa awamu ya pili, yaliyofanyika Tunguu, Mkoa wa Kusini Unguja. Amesema CCM imekuwa na utaratibu wa kutoa mafunzo ya uongozi kwa wanachama wake kwa lengo la kuwaongezea uelewa na uwezo wa kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia misingi na taratibu za chama. Amesema elimu inayotolewa kwa viongozi na wanachama kupitia mafunzo hayo itasaidia kukiimarisha CCM na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za chama, pamoja na kuchangia juhudi za kuleta maendeleo kwa ujumla. Aidha, Abdi amewataka washiriki kutumia fursa hiyo kujifunza, kubadilishana uzoefu na kuongeza uelewa kuhusu Itikadi, Uenezi na misingi ya CCM ili elimu watakayoipata iweze kutumika ipasavyo katika utekelezaji wa majukumu yao. Amesisitiza kuwa uelewa mzuri wa misingi na taratibu za chama ni muhimu kwa viongozi na wanachama katika kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kwa kuzingatia malengo ya CCM.
Sat, 26 Sep 2026 15:45:47 +0000Trump rejects Iran proposal to reopen Strait of Hormuz
Read the full report from the original source.
RecentlyHEMED ASISITIZA MAKADA KUFAHAMU ITIKADI NA HISTORIA YA CCM
Na MWANDISHI WETU, Zanzibar MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla, amewataka makada wa chama hicho kuwa na uelewa mpana wa Itikadi, misingi na historia ya CCM ili waweze kutoa ufafanuzi sahihi kwa wananchi. Hemed ameyasema hayo leo, Septemba 26, 2026, wakati akifungua mafunzo ya Itikadi, Uenezi na kuongeza wanachama wapya wa CCM kwa awamu ya pili, yaliyofanyika katika Chuo cha Mafunzo ya Uongozi Dambwe, Tunguu, Zanzibar. Amesema sera za CCM zinalenga kuleta maendeleo na kuimarisha uchumi wa nchi, hivyo ni muhimu kwa makada kuwa na uelewa wa kutosha kuhusu sera, misingi na historia ya chama hicho. Amewataka washiriki wa mafunzo hayo kuhakikisha wanatumia fursa hiyo kujifunza na kupata tija, ikiwemo kubadilishana uzoefu na kushirikiana katika kutafuta suluhisho la changamoto mbalimbali zinazokikabili chama. Aidha, Hemed amesema CCM inapotoa ahadi kwa wananchi, inaendelea kuzitekeleza kwa vitendo, akieleza kuwa hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za kuimarisha umoja na mshikamano miongoni mwa viongozi na wanachama wa chama. Katika hatua nyingine, amewataka makada hao kujifunza kwa kina historia ya CCM na kuwa na uelewa wa pamoja kuhusu misingi na Itikadi ya chama ili waweze kueleza na kutetea kwa usahihi misimamo na sera zake wanapowahudumia wananchi. Zaidi ya makada na wanachama 380 wa CCM kutoka mikoa mbalimbali ya Unguja, Pemba na Tanzania Bara wanashiriki mafunzo hayo yanayolenga kuongeza uelewa kuhusu Itikadi na Uenezi, pamoja na kuimarisha uhai wa Chama Cha Mapinduzi.
Sat, 26 Sep 2026 09:00:00 +0000Trump rejects Iran proposal to reopen Strait of Hormuz
Read the full report from the original source.
RecentlyPrime Minister Nsengiyumva meets Rwandans living around New York City
Read the full report from the original source.
RecentlyNigeria fight back as Gambia, Rwanda and Guinea-Bissau make winning starts to AFCON 2027 qualifiers
Read the full report from the original source.
RecentlyRwanda Foreign Minister exchanged with AU Commission Deputy Chairperson
Read the full report from the original source.
RecentlyTOP NEWS: Here Are The Six Crucial Road Projects Set to Begin Soon by Works Ministry
Kampala: The Ministry of Works and Transport has ignited fresh optimism across Uganda as it begins the technical review of six major national road projects, a decisive step toward design…
RecentlyRuto: No retreat in mission to transform Kenya “I am a man on a mission to transform our great country."
“I am a man on a mission to transform our great country."
RecentlyKISUTU WAKOLEZA MOTO KAMPENI YA USAFI
Na MWANDISHI WETU - DAR ES SALAAM WAKAZI wa Kata ya Kisutu, Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam, wameendelea kuhamasisha kampeni ya usafi kwa kuanzisha shughuli za usafi katika maeneo mbalimbali ya kata hiyo. Kampeni hiyo imezinduliwa leo na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mtendeni, Kata ya Kisutu, Mustaquim Daruga, na imeandaliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), Shina Namba 8, Tawi la Mtendeni, chini ya Mwenyekiti wake, Al Hajj Mahmood Amirali Walrji. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Daruga amesema wananchi wa Kisutu hawataki uchafu na kwamba usafi umefanywa kuwa sehemu ya maisha yao ya kila siku. Amesema hatua hiyo ni sehemu ya kuitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, wa kuhakikisha Jiji la Dar es Salaam linakuwa safi. “Mkuu wa Wilaya ya Ilala amesema mtu atakayejihusisha na uchafu atatozwa faini ya Sh300,000 hadi Sh milioni moja au kifungo cha jela. Adhabu hii si kwa ajili ya watu wasafi. Hii ni kwa wachafu. Sisi Kisutu ni wasafi, haitatuhusu. Wachafu wafungwe na wapigwe faini,” amesema Daruga. Daruga ameipongeza CCM Shina Namba 8 kwa kuanzisha kampeni hiyo katika ngazi ya shina, akisema hatua hiyo inapaswa kuwa mfano kwa mashina mengine katika kuhamasisha usafi wa mazingira. Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Kisutu, Tousif Bhojani, amesema tayari kata hiyo imezindua kampeni ya usafi katika ngazi ya kata, hivyo hatua iliyochukuliwa na Shina Namba 8 ni mwendelezo wa kuhakikisha maeneo yote ya Kisutu yanakuwa safi. “Sisi Kata ya Kisutu kila siku tutaendelea na usafi. Nawaomba wananchi wa Kisutu wazingatie usafi. Hii iwe mfano kwa mashina mengine. Tuonyeshe kwa vitendo kuitikia wito wa Rais wetu wa kuhakikisha jiji letu linakuwa safi,” amesema Bhojani. Naye Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kisutu, Multazar Daruga, amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kusisitiza umuhimu wa Jiji la Dar es Salaam kuwa safi, akisema Kisutu itaendelea kutekeleza maelekezo hayo. “Hii kampeni ya usafi Kisutu tunaisisitiza, lakini kata zingine nazo ziendelee. Tutaanza ngazi ya kata, Mkoa wa Dar es Salaam na hatimaye nchi nzima itakuwa safi,” amesema Multazar. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM Shina Namba 8, Tawi la Mtendeni, Al Hajj Mahmood Amirali Walrji, amewashukuru wananchi, wadau na taasisi mbalimbali kwa kujitokeza kushiriki kampeni hiyo. Amesema Shina Namba 8 linatambua na kuheshimu tamko la Mwenyekiti wa CCM, ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, la kuhakikisha Jiji la Dar es Salaam linakuwa safi. Ameahidi kuwa shina hilo litaendelea kushiriki kikamilifu katika shughuli za usafi na kuhamasisha wananchi kuhakikisha Kata nzima ya Kisutu inakuwa safi, kuanzia ngazi ya shina.
Sat, 26 Sep 2026 15:29:11 +0000"L'un des grands mystères non résolus de la science" : ce que l'anesthésie générale révèle sur notre cerveau
Le mécanisme d'action des anesthésiques généraux reste encore mal compris, mais ces substances fournissent des indices précieux sur la nature de la conscience.
RecentlyHarry says it is 'great' to be back in Britain after six years in US He says his children are “happy in school” and the family returned to the UK for "lots of reasons".
He says his children are “happy in school” and the family returned to the UK for "lots of reasons".
RecentlyUN Special Representative for Central Africa commends China’s cooperation with Rwanda
Read the full report from the original source.
RecentlyKihongosi afunika mkutano CCM Tanga
Read the full report from the original source.
RecentlyGermany's FM Wadephul meets Lavrov on UNGA sidelines
Read the full report from the original source.
RecentlyLe Rwanda et Djibouti souhaitent élever leur partenariat vers de nouveaux sommets
Read the full report from the original source.
RecentlyLes habitants de Gasabo invités à voter et à lutter contre l’abus de drogues
Read the full report from the original source.
RecentlyPeople with hearing disability demand sign language services in public institutions
Read the full report from the original source.
RecentlyWalimu names UNATU leaders among defaulters on UGX 11 billion teachers’ loans
KAMPALA — Walimu Cooperative Union has rejected claims by the Uganda National Teachers' Union (UNATU) that it mismanaged a government fund meant for teachers. Union officials said the UGX 11 billion...
RecentlyThe Takeaway: UN General Assembly debate Day 4
Read the full report from the original source.
RecentlyPage 1032 of 1125 · 22499 stories