Unganishwa

Search the region

22477 stories

Uncategorized · Capital FM

Netanyahu defends Israeli military action as delegates walk out before UN speech

Latest · News

Recently
Uncategorized · Issa Michuzi

INADES YAZITAKA NGO's KUWA NA VYANZO MBALIMBALI VYA MAPATO.

Mkurugenzi wa Shirika la INADES Formation Tanzania, Jacqueline Nicodemus, amesema mashirika yasiyo ya kiserikali yanapaswa kuweka mikakati ya kuwa na vyanzo mbalimbali vya mapato ili kuhakikisha yanaendelea kutekeleza shughuli zake bila kutegemea zaidi fedha kutoka kwa wafadhili. Akizungumza leo Septemba 24, 2026, jijini Dodoma kwenye Jukwaa la Mwaka la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Mkoa wa Dodoma, amesema ushiriki wao katika jukwaa hilo ulianza katika ngazi za wilaya, ambapo walishiriki katika majukwaa yaliyofanyika katika wilaya tano kabla ya kufikia ngazi ya mkoa. Amesema ajenda kubwa iliyojadiliwa ni uendelevu wa mashirika yasiyo ya kiserikali, hususan changamoto ya kuwa na vyanzo vya kutosha vya mapato ili kupunguza utegemezi wa fedha kutoka kwa wafadhili. Aidha, amesema mashirika yanaweza kutumia fursa zilizopo kuendeleza bidhaa na huduma mbalimbali zinazoweza kuzalisha mapato, hatua ambayo itasaidia kupanua wigo wa mapato na kuimarisha utekelezaji wa shughuli zao. Kwa upande mwingine, amesema kupitia majukwaa hayo, wadau wameweza kujadili na kuweka mikakati ya kuhakikisha mashirika yanapata fursa zaidi za mapato na kuwa na uwezo wa kujiendesha kwa uendelevu. Ameongeza kuwa mjadala huo utaendelea katika ngazi ya kitaifa mwezi Oktoba, ambapo mashirika yasiyo ya kiserikali kutoka maeneo mbalimbali Nchini yataendelea kutoa mchango kuhusu namna ya kujenga uendelevu wa sekta hiyo nchini Tanzania. Naye Rajab A. Rajab, ambaye ni mjumbe wa Baraza la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali NACONGO, kutoka Wilaya ya Kondoa, ameeleza kuwa INADES Formation Tanzania imeendelea kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo, ikiwemo mazingira, kilimo, ufugaji, elimu na uwezeshaji wananchi kiuchumi. Amesema kupitia shughuli za mazingira, shirika hilo limefanikiwa kupanda zaidi ya miti 80,000 katika mkoa wa Dodoma, huku likiendelea kuwafikia wakulima na wafugaji kwa kutoa elimu na kuwawezesha kushiriki katika shughuli za maendeleo. Aidha, amesema katika maeneo ambayo shirika halifiki moja kwa moja, hutumia njia mbalimbali kuwafikishia wananchi elimu na taarifa muhimu, ikiwemo tafiti na machapisho yanayowasaidia wakulima kupata uelewa kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo. Ameeleza pia kuwa matokeo ya shughuli za shirika yanaonesha kuwa zaidi ya vikundi saba vinaendelea kutekeleza shughuli za maendeleo ya kiuchumi na kijamii vijijini, huku vikifikia zaidi ya watu 150,000. Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Khatibu Kazungu, amezitaka mashirika yasiyo ya kiserikali kuzingatia masharti ya sheria, kushiriki mikutano na vikao vya wadau, kuwasilisha kwa wakati taarifa za robo mwaka na mwaka pamoja na kulipa ada kwa wakati. Kazungu pia amesisitiza mashirika hayo kulinda maslahi ya nchi, kuheshimu mila, desturi, utamaduni na maadili, kuhakikisha wanufaika wanashirikishwa katika utekelezaji wa miradi na kuzingatia mipango na vipaumbele vya Serikali, hususan Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2050. Kwa upande wake, Patrick Mafuru, akizungumza kwa niaba ya Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Makundi Maalumu, amesisitiza mashirika kufanya kazi kwa ushirikiano na kuzingatia sheria, taratibu na kanuni zinazowaongoza, akieleza kuwa lengo kuu linapaswa kuwa kuisaidia Serikali kufikisha huduma kwa jamii katika maeneo ambayo bado haijafika.

Fri, 25 Sep 2026 07:10:11 +0000
Uncategorized · Citizen Digital

'My home away from home': Gachagua takes Wamunyoro spirit to Dallas as he meets Kenyans

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

Protest survivor shot three times appeals for Ksh.500K medical support

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Daily News

Stakeholders call for sustained blue economy gains

TANGA: STAKEHOLDERS in the blue economy sector have called for concerted efforts to sustain gains made under the Regenerative Seascapes…

Recently
Uncategorized · Issa Michuzi

TANZANIA YATOA WITO KWA DUNIA KUFANYA KWA VITENDO AHADI YA KUKABILI ATHARI ZA KUPANDA KWA KINA CHA BAHARI

Tanzania imetoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa kuongeza kasi ya upatikanaji wa fedha za mabadiliko ya tabianchi, teknolojia na mifumo madhubuti ya tahadhari za mapema ili kuzisaidia nchi zinazoendelea kukabiliana na athari zinazoongezeka za kupanda kwa kina cha bahari. Akihutubia Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu kupanda kwa kina cha Bahari mjini New York, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius John Ndejembi, amesema tatizo hilo si tishio la siku zijazo tena, bali tayari linaathiri maisha ya watu, uchumi na mifumo ya ikolojia duniani. Kwa Tanzania, athari hizo ni kubwa kutokana na ukanda wake wa pwani ya Bahari ya Hindi, Zanzibar na visiwa vingine ambavyo vinategemewa na mamilioni ya watu kupitia uvuvi, utalii na biashara. Mmomonyoko wa fukwe, kuingia kwa maji ya chumvi katika vyanzo vya maji baridi na mafuriko vinatajwa kuwa miongoni mwa vitisho kwa wananchi, miundombinu na mafanikio ya maendeleo ya nchi. Makamu wa Rais ameeleza kuwa, Tanzania tayari inachukua hatua kwa kuimarisha ulinzi wa pwani, kurejesha mikoko na mifumo ya ikolojia, kuimarisha usalama wa maji na kuendeleza mikakati ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi inayoongozwa na jamii. Hata hivyo, Makamu wa Rais amesisitiza kuwa juhudi za nchi moja moja hazitoshi, akitaka fedha za tabianchi kuwa za kutosha, za uhakika na zinazopatikana kwa urahisi zaidi kwa nchi zinazoendelea na jamii za pwani zilizo katika mazingira hatarishi. Mkutano huo wa Septemba 24, 2026, umezikutanisha nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, Viongozi, Wataalamu na Wadau wengine kuweka msimamo wa pamoja na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa dhidi ya tishio la kupanda kwa kina cha bahari. Mkutano huo unafanyika ikiwa ni mwendelezo wa Mkutano wa Ngazi ya Juu wa mwaka 2024 uliolifanya suala hilo kuwa ajenda muhimu ya kimataifa. Miongoni mwa maeneo ya msingi yanayopewa uzito ni ulinzi wa maisha na shughuli za kiuchumi katika maeneo ya pwani, mifumo ya tahadhari za mapema, takwimu za tabianchi, miundombinu himilivu, teknolojia, suluhisho zinazotegemea mazingira asilia pamoja na kuongeza uwezo wa nchi zilizo hatarini kukabiliana na athari zisizoepukika. Mkutano huo unatarajiwa kufikia Azimio la pamoja lenye mwelekeo wa utekelezaji, likilenga kuimarisha hatua za kimataifa, ustahimilivu na uwezo wa kukabiliana na kupanda kwa kina cha bahari. Tanzania imeunga mkono kupitishwa kwa Azimio hilo kwa makubaliano ya pamoja, huku ikisisitiza umuhimu wa dunia kuhamisha mjadala kutoka katika ahadi kwenda kwenye utekelezaji wenye matokeo. Kwa Tanzania, utekelezaji wa dhamira hizo unaweza kufungua fursa zaidi za ushirikiano wa kimataifa katika rasilimali za tabianchi, teknolojia, mifumo ya tahadhari za mapema na ujenzi wa miundombinu himilivu, hatua zenye umuhimu mkubwa katika kulinda jamii za pwani hususani Zanzibar, sekta ya utalii, uvuvi na shughuli nyingine za uchumi wa buluu. Akihitimisha ujumbe wake, Makamu wa Rais ametoa mwito wenye msisitizo kwa jumuiya ya kimataifa: “Bahari inatuunganisha. Hivyo basi, kupanda kwa kina cha maji yake kunapaswa pia kutuunganisha katika kuchukua hatua za pamoja.” Makamu wa Rais yuko New York nchini Marekani, akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwenye Mkutano wa 81 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Fri, 25 Sep 2026 07:03:59 +0000
Uncategorized · KBC

Schools in Taita Taveta to benefit from mobile library initiative

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Daily News

Bulyanhulu safety efforts win praise

SHINYANGA: THE Parliamentary Standing Committee on Welfare and Social Development has commended Barrick Bulyanhulu Gold Mine for complying with workplace…

Recently
Uncategorized · Daily News

EAC farmers push for faster climate finance

EAST AFRICA: FARMERS in East Africa have called on East African Community (EAC) Partner States to ensure climate finance reaches…

Recently
Uncategorized · Issa Michuzi

TUME YATANGAZA RATIBA YA UCHAGUZI MDOGO WA UBUNGE CHAMWINO NA UDIWANI KATA 11

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza Novemba 04, 2026 kuwa siku ya uchaguzi mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Chamwino, Mkoa wa Dodoma, pamoja na Madiwani katika kata 11 za Tanzania Bara. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ramadhani Kailima, imesema uchaguzi huo unafanyika kufuatia kuwepo kwa nafasi wazi za uongozi katika maeneo ya uchaguzi. “Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ilipokea taarifa kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu kuwepo kwa nafasi wazi ya Ubunge katika Jimbo la Chamwino, Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, Mkoa wa Dodoma,” ilisema taarifa hiyo. Nafasi hiyo imetokea baada ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumteua aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Deogratius John Ndejembi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Uteuzi wake ulifanyika tarehe 26 Agosti, 2026 na kuthibitishwa na Bunge tarehe 28 Agosti, 2026. Aidha, Kailima kupitia taarifa hiyo amesema Tume kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 57(1) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Sura ya 343 ilipokea taarifa kutoka kwa Waziri mwenye dhamana juu ya uwepo wa nafasi wazi za madiwani 11 kwa Tanzania bara. “Tumepokea taarifa kutoka kwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa kuhusu uwepo wa nafasi wazi za madiwani 11 kwa Tanzania Bara. Nafasi hizo wazi zilitokana na vifo vya madiwani nane (08) kwa nyakati tofauti na madiwani watatu (03) kujiuzulu,”taarifa ilisema. Tume imesema kuwa fomu za uteuzi kwa wagombea wa Ubunge Chamwino na Udiwani katika kata 11 zitatolewa kuanzia tarehe 7 hadi 13 Oktoba 2026, huku zoezi la uteuzi wa wagombea likifanyika tarehe 13 Oktoba 2026. Baada ya uteuzi, kampeni za uchaguzi zitaanza tarehe 14 Oktoba 2026 na kuendelea hadi 3 Novemba 2026. Kailima amesema Uchaguzi mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Chamwino na Madiwani katika kata 11 za Tanzania Bara utafanyika siku ya Jumatano tarehe 04 Novemba, 2026. Kailima amezitaja Kata 11 zitakazofanya uchaguzi Uchaguzi wa Madiwani kuwa ni Nonde – Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Lugenge – Halmashauri ya Mji Njombe, Bargish – Halmashauri ya Mji Mbulu, Makole – Halmashauri ya Wilaya ya Muheza, Mwera – Halmashauri ya Wilaya ya Pangani na Oldonyosambu – Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro. Kata zingine ni pamoja na Igalula – Halmashauri ya Wilaya ya Uyui, Shelui – Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Mvumi – Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa, Nyarero – Halmashauri ya Wilaya ya Tarime na Ilolangulu – Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe. Tume imevikumbusha vyama vya siasa, wagombea na wadau wote wa uchaguzi kuzingatia Katiba, sheria, kanuni, maadili ya uchaguzi, taratibu, miongozo na maelekezo ya Tume katika kipindi chote cha utekelezaji wa ratiba hiyo.

Fri, 25 Sep 2026 07:01:49 +0000
Uncategorized · Daily News

Dear haven of peace, must Mama always blow the whistle?

DAR ES SALAAM: HER Excellency Mama recently called a spade a spade, then understandably wondered why that same spade was…

Recently
Uncategorized · Issa Michuzi

TAEC YAIMARISHA USALAMA WA MIONZI MIPAKANI KUPITIA MAFUNZO MAALUM YA VIFAA

TUME ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) imeendelea kuimarisha usalama wa mionzi na nyuklia katika mipaka ya nchi kwa kuwajengea uwezo wataalamu wake kuhusu uendeshaji, matengenezo na utunzaji wa vifaa vinavyotumika kugundua mionzi katika maeneo mbalimbali ya kuingia na kutoka nchini. Hatua hiyo inalenga kuhakikisha vifaa vilivyowekwa katika maeneo ya kimkakati mipakani vinafanya kazi kwa ufanisi na vinaendelea kuwa katika hali nzuri wakati wote, ili kusaidia kubaini uwepo wa vifaa vya mionzi au nyuklia vinavyoweza kuingizwa au kusafirishwa nchini bila kufuata taratibu zinazotakiwa. Akizungumza jijini Mwanza wakati wa mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Teknolojia na Huduma za Ufundi wa TAEC, Dkt. Remigius Kawala, amesema Tume imeendelea kuwekeza katika vifaa na miundombinu ya kisasa ili kuongeza uwezo wake wa kutoa huduma za kitaalamu kwa usahihi na kwa viwango vinavyokubalika. Amesema katika mwaka huu wa fedha, TAEC imenunua vifaa mbalimbali vya maabara vyenye thamani ya takribani Sh bilioni 3, ikiwa ni sehemu ya uwekezaji unaolenga kuimarisha uwezo wa Tume katika kufanya vipimo, uchunguzi na tafiti mbalimbali zinazohusiana na matumizi salama ya teknolojia ya nyuklia. Kwa mujibu wa Dkt. Kawala, wataalamu wamekutana kwa siku mbili katika Kanda ya Ziwa kujitathmini kuhusu namna huduma za maabara zinavyotolewa, hali na ubora wa vifaa vinavyotumika pamoja na kuweka mikakati ya kuhakikisha vipimo vinavyofanyika vinakuwa sahihi na vya kuaminika. “Tumekutana wataalamu Kanda ya Ziwa kwa lengo la kuweka mikakati ya utoaji wa huduma za maabara kwa usahihi bila kuwa na mashaka. Hivi ni vipimo ambavyo vinapaswa kuendana na viwango vinavyotambulika duniani,” amesema Dkt. Kawala. Ameeleza kuwa TAEC ina takribani maabara tano katika maeneo mbalimbali nchini, ikiwemo Zanzibar, huku pia ikitoa huduma katika maeneo mbalimbali ya mipakani. Kutokana na ukubwa wa majukumu hayo, uwekezaji katika vifaa vya kisasa na kuwajengea uwezo wataalamu ni muhimu katika kuhakikisha huduma zinazotolewa zinakuwa na ubora unaotakiwa. Katika mafunzo hayo, wataalamu wamejengewa uwezo wa kuendesha kwa usahihi vifaa vya kugundua mionzi vilivyowekwa mipakani, kufanya ukaguzi na matengenezo ya kawaida pamoja na kuvihifadhi na kuvitunza ili viweze kufanya kazi kwa ufanisi kwa muda mrefu. Mafunzo hayo pia yameweka mkazo katika namna ya kutambua na kuchukua hatua pale vifaa vinapotoa tahadhari ya uwepo wa mionzi, sambamba na kuzingatia taratibu za kujikinga na mionzi wakati wa utekelezaji wa majukumu yao. Vifaa hivyo vina umuhimu mkubwa katika mfumo wa usalama wa nchi kwa kuwa vinasaidia kugundua na kuzuia usafirishaji usioidhinishwa wa vifaa vya mionzi na nyuklia kupitia mipaka na maeneo mengine ya kimkakati ya kuingia na kutoka nchini. Dkt. Kawala amesema uwekezaji unaoendelea kufanywa na Serikali unalenga kuhakikisha TAEC inakuwa na uwezo wa kufanya vipimo, uchunguzi na tafiti mbalimbali kwa kutumia vifaa vya kisasa, huku matumizi ya teknolojia ya nyuklia yakifanyika kwa kuzingatia viwango vinavyotakiwa vya usalama. Ameongeza kuwa teknolojia ya nyuklia haipaswi kuonekana kama eneo linalohusu kundi fulani la wataalamu pekee, kwa kuwa matumizi yake yana mchango katika maisha ya wananchi kupitia sekta mbalimbali zikiwemo afya, kilimo, viwanda, mazingira na utafiti. Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa TAEC, Bw. Peter Ngamilo, amesema pamoja na uwekezaji unaofanywa katika vifaa na kuwajengea uwezo wataalamu, Tume itaendelea kutoa elimu kwa umma ili wananchi waelewe umuhimu wa matumizi salama ya mionzi na teknolojia ya nyuklia katika maendeleo ya Taifa. “Ni muhimu wananchi waelewe kuwa teknolojia ya nyuklia ina matumizi mengi yenye manufaa katika maisha yetu. Jukumu letu ni kuhakikisha matumizi hayo yanafanyika kwa usalama, lakini pia wananchi wanapata taarifa sahihi kuhusu kazi zinazofanywa na TAEC katika kuwalinda wao na mazingira dhidi ya madhara yanayoweza kutokana na matumizi yasiyo salama ya mionzi,” amesema Ngamilo. Amesema uwepo wa vifaa vya kugundua mionzi katika maeneo ya mipakani ni sehemu muhimu ya mfumo wa ulinzi na usalama, kwa kuwa unasaidia kuhakikisha vifaa vya mionzi vinavyoingia au kutoka nchini vinatambuliwa na kushughulikiwa kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa. Aidha, Serikali imeendelea kuweka mazingira yanayowezesha taasisi za umma na sekta binafsi kushirikiana katika matumizi ya teknolojia ya nyuklia kwa madhumuni ya amani na maendeleo, ili manufaa ya teknolojia hiyo yaweze kuwafikia wananchi wengi zaidi. Katika hatua nyingine, Dkt. Kawala amesema TAEC ipo katika hatua za mwisho za kupata ithibati zinazohitajika kwa ajili ya maabara yake kubwa na ya kisasa iliyopo jijini Arusha. Kukamilika kwa hatua hiyo kutaongeza uwezo wa maabara hiyo kutoa huduma za vipimo na uchunguzi kwa kuzingatia viwango vinavyotambulika. Maabara hiyo inatarajiwa kuongeza uwezo wa Tanzania kufanya vipimo na tafiti za kitaalamu nchini na hivyo kuimarisha upatikanaji wa huduma zinazohusiana na teknolojia ya nyuklia pamoja na kupunguza utegemezi wa baadhi ya huduma kutoka nje ya nchi. TAEC imeendelea kuimarisha uwezo wa Taifa katika usalama wa mionzi na nyuklia kupitia uwekezaji katika vifaa na miundombinu, mafunzo kwa wataalamu, usimamizi wa matumizi salama ya mionzi pamoja na ushirikiano na taasisi mbalimbali za ndani na nje ya nchi. Hatua hizo zinalenga kuhakikisha teknolojia ya nyuklia na mionzi inaendelea kutumika kwa usalama na kwa madhumuni ya amani, huku afya ya wananchi, wafanyakazi na mazingira ikilindwa.

Fri, 25 Sep 2026 06:53:20 +0000
Uncategorized · Iwacu

Engrais : le recensement des agriculteurs ne rassure pas les bénéficiaires

En l’espace d’une semaine, chaque colline devra avoir recensé les besoins individuels en engrais, a annoncé le président Évariste Ndayishimiye le 17 septembre 2026 à Gitega. Face aux difficultés d’approvisionnement et aux soupçons de détournement, des experts préconisent la dépolitisation du secteur et le retrait des autorités de la distribution des fertilisants. Par Jules Bercy Igiraneza et Félix Haburiyakira

Fri, 25 Sep 2026 06:53:33 +0000
Uncategorized · Citizen Digital

Kindiki in Nyeri to inspect projects, warns contractor over stalled Ksh. 1.2B Kiawara Market

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · KBC

EACC wins bid to recover Ksh426.8M assets from former Kilifi land registrar

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Chanzo

The Boy by the Radio: Zitto Kabwe at Fifty

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Chanzo

Lissu Says Treason Case Rests on Police Inference as Final Submission Continues

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · SoftPower News

Ghanaian Businessman Basil Anthony Expands Modern Floors & Walls into East Africa

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Nile Post

Qcil, Medicines Patent Pool Sign Licence to Expand Access to Influenza Treatment

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Daily News

What kind of football nation does Tanzania want to become

DAR ES SALAAM: AS the country heightens preparations to host the 2027 Africa Cup of Nations finals, there is a…

Recently

Page 1059 of 1124 · 22477 stories