Search the region
22461 stories
Taifa Stars’ AFCON 2027 campaign gets 500m/- boost as NBC hands over new bus
DAR ES SALAAM: A national football team cannot prepare effectively for major international competitions if basic logistical needs remain unresolved.…
RecentlyONU : ce que des dirigeants africains ont dit à la tribune
Read the full report from the original source.
RecentlyTobacco Bill: Businesses push back against new licences Stakeholders say the proposed rules could raise business costs and fuel illicit trade.
Stakeholders say the proposed rules could raise business costs and fuel illicit trade.
RecentlyUNGA81: Rwanda highlighted the importance of investing in skills and digital infrastructure
Read the full report from the original source.
RecentlySenate Vice President welcomes the new Clerk of the Senate
Read the full report from the original source.
RecentlyUganda, Denmark explore Cooperation on Firefighting and Emergency response
Read the full report from the original source.
RecentlyPreps for maternal health marathon pick up tempo
The race for a healthier Uganda will take on a deeper meaning on October 4 when the Independence Marathon brings together runners, fitness enthusiasts and corporate partners in a drive to help save mothers’ lives. Last S
Recently"Je ne savais pas que mon partenaire me violait pendant mon sommeil."
Adelle Overton était en couple avec Steven Uden depuis 13 ans lorsqu'elle a découvert qu'il la violait.
RecentlyMatovu was not intended target, says ‘girlfriend’
Afrigo Band icon Moses Matovu may not have been the intended target in the fatal attack that followed a confrontation involving his alleged girlfriend and…
RecentlyWinnie Odinga to youth: Question leaders, think independently Winnie says even admired leaders should remain open to scrutiny, reflecting on her late father Raila Odinga’s legacy
Winnie says even admired leaders should remain open to scrutiny, reflecting on her late father Raila Odinga’s legacy
RecentlyBMH YAWEKA BAYANA WAJIBU, HAKI 10 ZA MGONJWA KATIKA HUDUMA ZA AFYA
Na Janeth Raphael - MichuziTv Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) Dodoma imewataka wagonjwa kuwa sehemu ya mchakato wa matibabu kwa kufahamu haki zao na kushiriki kikamilifu katika maamuzi yanayohusu afya zao, ikiwa ni pamoja na kupewa taarifa sahihi, kuheshimiwa na kupata huduma salama kwa wakati. Akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Usalama wa Mgonjwa yaliyofanyika hospitalini hapo leo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa BMH, Dk. Abdalah Baja, amesema mgonjwa ana haki ya kupata huduma bora na salama kulingana na mahitaji yake, kushirikishwa katika maamuzi ya matibabu, kupata maoni ya pili ya kitabibu na kuhakikishiwa faragha wakati wa kupatiwa huduma. Dkte. Baja amesema haki nyingine ni kuheshimiwa utu wa mgonjwa, kulindwa kwa usiri wa taarifa zake za kiafya, kupewa nafasi ya kueleza changamoto zake na kusikilizwa, kuhudumiwa kwa wakati pamoja na kupata taarifa zilizo wazi kuhusu gharama, huduma anazohitaji na maendeleo ya matibabu yake. Dk. Baja alisisitiza kuwa utoaji wa taarifa sahihi humwezesha mgonjwa kuelewa huduma anayopewa na kushiriki ipasavyo katika maamuzi ya matibabu. Pia Dkt. Baja, amesema usalama wa mgonjwa unaweza kuathiriwa na changamoto mbalimbali, ikiwamo baadhi ya wagonjwa kuchelewa kufika hospitalini katika muda waliopangiwa, kutomuona daktari au kutofanyiwa vipimo walivyoelekezwa, pamoja na changamoto za miundombinu. Amesema hali hizo zinaweza kuongeza hatari ya madhara kwa mgonjwa, ikiwamo matumizi yasiyo sahihi ya dawa. Kwa upande wake, Daktari bingwa wa Upasuaji toka BMH Kakorongo Mugisha amesema BMH inaendelea kuimarisha usalama wa wagonjwa kwa kuwajengea uwezo wataalamu wa afya na kuhakikisha huduma zinatolewa kwa kuzingatia taratibu za kitaalamu. Alisema pia wagonjwa wana haki ya kuamua iwapo wanataka wanafunzi washiriki wakati wa huduma zao, huku hospitali ikiendelea kutoa mafunzo ya vitendo kwa wanafunzi kwa kuzingatia ridhaa ya mgonjwa na usalama wake. Aidha, alisema muda wa kupata majibu ya vipimo hutegemea aina ya kipimo, ambapo baadhi ya vipimo vya kawaida vinaweza kutoa majibu ndani ya saa tatu, huku vipimo kama CT Scan na MRI vikitarajiwa kutoa majibu ndani ya saa 24 kulingana na taratibu za huduma. Nao Baadhi ya wagonjwa waliopatiwa huduma BMH wameeleza kuridhishwa na huduma wanazopata, huku wakitoa mapendekezo ya maboresho. Omary Namganda, mkazi wa Kigoma Mjini, aliwapongeza wataalamu wa afya kwa huduma wanazowapatia wagonjwa, wakati Jasery Zacharia wa Kahama, Shinyanga, alisema amepata huduma na ufuatiliaji katika matibabu ya tatizo la figo lililohusisha mawe. Kwa upande wake, Sospiter Chibanila aliitaka hospitali kuendelea kuboresha kasi ya upatikanaji wa majibu ya vipimo vinavyohitaji muda mrefu ili kuwawezesha wagonjwa kupata huduma kwa wakati.
Thu, 24 Sep 2026 14:48:19 +0000RAIS SAMIA AONGOZA DHAMIRA YA AFRIKA KUTOKOMEZA VIFO VYA MAMA NA MTOTO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amepongezwa kwa uongozi wake mahiri katika kusukuma mbele ajenda ya Afrika ya kutokomeza vifo vinavyoweza kuzuilika vya mama na mtoto, huku bara hilo likikabiliwa na karibu asilimia 70 ya vifo vya akina mama duniani na takribani theluthi mbili ya vifo vya watoto walio chini ya miaka mitano. Akiwa Kinara wa Umoja wa Afrika katika Afya ya Mama na Mtoto, Rais Samia anaongoza ajenda ya “Malengo Matatu ya Sifuri” (Three Zeros) inayolenga kufikia sifuri ya kujifungulia nyumbani, sifuri ya vifo vinavyoweza kuzuilika vya mama na mtoto mchanga, pamoja na sifuri ya watoto wasiopata chanjo. Ajenda hiyo imepewa msukumo katika Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Wakuu wa Nchi kuhusu Afya ya Mama, Mtoto Mchanga na Mtoto, iliofanyika pembezoni mwa Mkutano wa 81 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA81), ukiwakutanisha Wakuu wa Nchi na Serikali, viongozi wa taasisi za Umoja wa Afrika, mashirika ya kimataifa ya afya na washirika wa maendeleo. Akiwasilisha ujumbe wa Rais Samia katika mkutano huo, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, amesema ukubwa wa changamoto unahitaji Afrika kutoka kwenye ahadi na kuelekea katika hatua madhubuti zinazoweza kupimwa kwa maisha ya wanawake na watoto yanayookolewa. Amesema, pamoja na hatua ambazo Bara la Afrika limepiga, Afrika bado inachangia karibu asilimia 70 ya vifo vya akina mama duniani na takribani theluthi mbili ya vifo vya watoto walio chini ya miaka mitano, huku sehemu kubwa ya vifo hivyo ikiwa inaweza kuzuilika. Makamu wa Rais amesema msukumo wa Rais Samia unalenga kuimarisha mifumo ya afya ya nchi za Afrika, kuongeza ufadhili wa ndani, kuboresha huduma za dharura na mifumo ya rufaa, kuongeza upatikanaji wa wahudumu wa afya wenye ujuzi na kuhakikisha takwimu zinatumika kufuatilia matokeo na kubaini maeneo yanayohitaji hatua zaidi. Akielezea uzoefu wa Tanzania, Makamu wa Rais amesema uwekezaji katika huduma za afya ya msingi na za dharura kwa mama na mtoto mchanga, pamoja na kuimarishwa kwa mifumo ya rufaa ikiwemo M-Mama, unaonesha namna uongozi wa kisiasa, teknolojia na utoaji wa huduma kwa wananchi vinavyoweza kuunganishwa katika kuokoa maisha. Hatua hizo zimekwenda sambamba na kuongezeka kwa wanawake wanaojifungulia katika vituo vya afya kutoka asilimia 51 mwaka 2015 hadi asilimia 81 mwaka 2022, mafanikio yanayoonesha uwezekano wa kubadili mwenendo wa vifo vya mama na mtoto pale uwekezaji unapounganishwa na utekelezaji katika ngazi ya jamii. Makamu wa Rais alisema ajenda anayoiongoza Rais Samia pia inatoa uzito kwa suala la Afrika kujitegemea katika afya, akisisitiza kuwa mafanikio hayapaswi kupimwa pekee kwa uwezo wa bara kugharamia, kuzalisha au kununua mahitaji yake, bali pia kwa uwezo wa kuhakikisha huduma muhimu zinamfikia kila mama na mtoto kwa wakati na mahali wanapozihitaji. Katika kufanikisha hilo, nchi za Afrika zimehimizwa kuimarisha uwajibikaji wa kisiasa, kuongeza uwekezaji wa ndani katika huduma zinazookoa maisha na kuhakikisha rasilimali zinafika hadi katika ngazi ya utoaji huduma. “Dhamira ni kuhakikisha hakuna mama anayepoteza maisha kwa kukosa usafiri, damu, mhudumu mwenye ujuzi au huduma ya dharura; hakuna mtoto mchanga anayefariki kwa kukosa huduma inayoweza kuokoa maisha yake, na hakuna mtoto anayebaki bila chanjo kwa sababu mfumo wa afya haukuweza kuifikia familia yake,” amesema Mhe. Ndejembi. Makamu wa Rais amesema kulinda uhai wa mama na mtoto si suala la afya pekee, bali ni uwekezaji katika rasilimali watu, uchumi na mustakabali wa Afrika, pamoja na kuwa sehemu muhimu ya utekelezaji wa Ajenda 2063 ya Bara la Afrika. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Africa CDC, Dkt. Jean Kaseya, alipongeza uongozi wa Rais Samia na kueleza dhamira ya Taasisi hiyo kuendelea kumuunga mkono katika jukumu lake la Kinara wa Umoja wa Afrika katika Afya ya Mama na Mtoto, huku akitaja hatua zilizopigwa na Tanzania kama mfano wa mafanikio yanayoweza kupatikana barani Afrika. Takwimu za Africa CDC zinaonesha kuwa Tanzania imepunguza uwiano wa vifo vya uzazi kwa takribani asilimia 80, kutoka vifo 556 kwa kila vizazi hai 100,000 mwaka 2016 hadi 104 mwaka 2022, hatua inayohusishwa na kuimarishwa kwa huduma za dharura za uzazi na watoto wachanga, mifumo ya rufaa, ongezeko la wahudumu wa afya pamoja na ufuatiliaji wa vifo vya mama na watoto. Dkt. Kaseya alisema Africa CDC itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kusukuma mbele ajenda hiyo, akisisitiza umuhimu wa uongozi wa kisiasa, uwekezaji na mifumo imara ya afya katika kulinda uhai na ustawi wa mama na mtoto barani Afrika. Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani Dkt. Adhanom Ghebreyesus amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuandaa mkutano huo na kuwa kinara wa Umoja wa Mataifa wa Afya ya Mama na Mtoto. Amesema katika kipindi cha miaka sita pekee, Tanzania imepunguza kiwango cha vifo vya kina mama kwa asilimia 81. Amesema kwa kuzindua mpango mkakati huo wa sifuri tatu (Three Zeros), Tanzania inaongoza kwa mfano na inapaswa kuungwa mkono. Amesema Shirika la Afya Duniani limejidhatiti kusaidia kila nchi mwanachama kulingana na mazingira yake na kufikia malengo yake kwa kuimarisha viwango vya huduma za kitabibu vinavyotumiwa na wahudumu walio mstari wa mbele kuokoa maisha ya kina mama na watoto wachanga. Kupitia nafasi yake kama Kinara wa Umoja wa Afrika katika Afya ya Mama na Mtoto, Rais Samia anasukuma dhamira ya kulifanya bara hilo kufikia hatua ambayo vifo vinavyoweza kuzuilika havitachukuliwa tena kuwa jambo lisiloepukika, huku kaulimbiu ya “Jiongeze, Tuwavushe Salama” ikibeba wito wa Afrika kwenda hatua ya ziada kwa ajili ya kila mama, mtoto mchanga, mtoto na kijana balehe. Mkutano huo, umehudhuriwa na Viongozi kutoka nchi mbalimbali za Afrika, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani, Dkt. Adhanom Ghebreyesus, Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Afrika cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (Africa CDC) Dkt. Jean Kaseya, Mwenza wa Rais wa Benin Bi. Nathalie Vilette Wadagni, Wadau wa Maendeleo wakiwemo, Gates Foundation, Global Fund, Gavi, UNFPA, Unicef, Suzan Thompson Buffett Foundation, Beginning Fund pamoja na Viongozi kutoka Umoja wa Afrika (AU).
Thu, 24 Sep 2026 14:52:24 +0000Mvurya says Sh15.27 billion disbursed through Youth Enterprise Development Fund
Read the full report from the original source.
RecentlyAfrica seeks funding to eradicate livestock disease with $33 return on every dollar
Latest · Africa
RecentlyRégion Sud/Rumonge : Plusieurs faits perturbent la sécurité
Plus d’une vingtaine de chèvres volées depuis le début du mois de septembre, des feux de brousse signalés dans certaines localités de la commune Rumonge, des abandons scolaires ainsi que le phénomène El nino ont retenu l’attention des participants à une réunion de sécurité tenue le 16 septembre 2026 par l’administrateur communal. Des recommandations ont été formulées pour relever ces défis qui hantent la sécurité, l’environnement et l’éducation.
Thu, 24 Sep 2026 14:42:48 +0000Korir out to reclaim Chicago title as Kenya Marathon Dinner Welcomes Elite Runners to Illinois
Latest · Athletics
RecentlyRégion Centre/Gitega Le calvaire des vendeurs de certaines boissons très alcoolisées n’en finit pas
Saisies, destructions, faillites, réautorisation surprise avant une nouvelle interdiction brutale, ... Tel est le vécu quotidien des vendeurs de boissons locales de Gitega. Entre manque de garanties des licences officielles et pertes financières, beaucoup font désormais le choix radical de tourner le dos au made in Burundi.
Thu, 24 Sep 2026 14:37:30 +0000Africa’s $30 smartphone goal is becoming harder to achieve
Read the full report from the original source.
RecentlyKILOSA YAANZA MAANDALIZI YA KUKABILIANA NA EL NINO
-DC SHAKA APIGA MARUFUKU MAFUNZO, AAGIZA FEDHA ZINUNUE VIFAA VYA DHARURA Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Mhe. Shaka Hamdu Shaka ameongoza Kikao Maalum cha Kamati ya Maafa ya Wilaya kilichojumuisha Kamati ya Ulinzi na Usalama na wadau mbalimbali kujadili maandalizi ya kukabiliana na mvua kubwa za El Nino zinazotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu kwa mujibu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA). Akifungua kikao hicho, Mhe. Shaka amesema Wilaya ya Kilosa imejifunza kutokana na athari za mafuriko ya miaka ya nyuma na safari hii maandalizi yote yatajikita kwenye vitendo, sio kwenye makaratasi. Amefafanua kuwa uamuzi huo ni utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyeagiza mikoa na wilaya zote kuchukua tahadhari mapema na kuhakikisha taarifa za TMA hazibaki kwenye makaratasi bali zinafuatwa na hatua za vitendo. Akizungumza kwa msisitizo, DC Shaka alisema:"Wilaya ya Kilosa tumeamua fedha zote zilizotengwa kwa ajili ya maafa zitanunua vifaa vya dharura vinavyoonekana. Sitaki kusikia mafunzo, semina na warsha. Wananchi wa Kilosa wanajua mafuriko ni nini. Wanachohitaji ni boti la kuwaokoa, blanketi la kujifunika na dawa wakiumwa." "Nimesikia kuna fedha zimetengwa kwa ajili ya mafunzo ya maafa. Sitaki kusikia mafunzo. Sitaki kabisa. Nani hapa Kilosa hajui mafuriko? Mtoto wa miaka 10 wa Kimamba anajua mafuriko kuliko mtaalamu. Fedha zozote za maafa zisiguse mafunzo." "Mafuriko yakija kesho, hutamwambia mama aliyekwama na watoto wawili juu ya paa - 'Mama subiri nikupe brochure ya mafunzo'. Hapana. Utamwambia - 'Mama panda boti, hiki hapa blanketi, huu hapa mchele'." Kwa upande wao, wadau mbalimbali walioshiriki kikao hicho wamepongeza utaratibu wa Wilaya ya Kilosa wa kushirikisha makundi yote na kueleza kuwa mipango iliyopangwa itatekelezeka na kuhakikisha usalama wa wananchi katika kipindi hiki cha tahadhari. Kikao kimeazimia kuanzishwa kwa Stoo ya Dharura ya Wilaya na kuhamishwa kwa wananchi wanaoishi maeneo hatarishi.
Thu, 24 Sep 2026 14:33:49 +0000UNGA81: Rwanda’s Prime Minister met UN boss António Guterres
Read the full report from the original source.
RecentlyPage 1069 of 1124 · 22461 stories