Search the region
22416 stories
Hospitality Challenge puts Young Professionals to the Test
Read the full report from the original source.
RecentlyQuestions swirl over opaque Sh26 billion maize import tender
A Sh26 billion deal to import 540,000 metric tonnes from Zambia has thrust a little-known private company into the centre of the countrys food security crisis
Thu, 24 Sep 2026 00:00:00 +0300Nile Breweries Launches National Road Safety Campaign
Read the full report from the original source.
RecentlySpeke Resort Munyonyo in Independence Day bonanza
KAMPALA — Speke Resort Munyonyo has unveiled a special Freedom Getaway package aimed at travellers seeking a lakeside staycation over Uganda's Independence Day holiday on 9 October 2026. The five-star property,...
RecentlyWhat Ruto will address at UNGA
According to the UN schedule, Ruto will speak in the general debate on Wednesday afternoon, New York time (Wednesday night EAT).
Wed, 23 Sep 2026 23:11:53 +0300CONRAD AHABWE | PML Daily Senior Correspondent
LAGOS, NIGERIA — An international law expert has rejected the argument that Britain's present government cannot be held responsible for wrongs committed under colonial rule, saying a change of leadership does...
RecentlyLaw expert challenges UK’s refusal to pay reparations over colonial ecocide
LAGOS, NIGERIA — An international law expert has rejected the argument that Britain's present government cannot be held responsible for wrongs committed under colonial rule, saying a change of leadership does...
RecentlyUFUATILIAJI NA TATHMINI KISISUBIRIE MWISHO WA MWAKA KUTAMBUA MALENGO HAYAJAFIKIWA
Na Vero Ignatus – Michuzi TV, Arusha Kongamano la Tano la Taifa la Ufuatiliaji, Tathmini na Kujifunza linalofanyika jijini Arusha kuanzia Septemba 22 hadi 26, 2026, limeendelea kupata mafanikio makubwa baada ya kuweka rekodi ya kukusanya jumla ya washiriki 1,664 kutoka ndani na nje ya nchi Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo Hoteli ya Ngurdoto Wilayani Arumeru mkoani Arusha,Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Daniel Sillo akimuwakilisha Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba, amezitaka taasisi za umma kutumia mfumo wa ufuatiliaji na tathmini kama kifaa cha kutoa tahadhari ya awali badala ya kusubiri hadi mwisho wa mwaka. "Ufuatiliaji na tathmini ni chombo muhimu cha usimamizi katika taasisi. Msisubiri mwisho wa mwaka ndipo mtambue kwamba shabaha hazijafikiwa," amesema Mhe. Sillo. Amesema viongozi na watendaji wa Serikali wanapaswa kusoma na kujadili taarifa hizo kwenye vikao vya menejimenti ili kuchukua hatua za haraka pale changamoto zinapobainika,Pia aliongeza kuwa changamoto kubwa kwa sasa si uzalishaji wa takwimu, bali ni kuhakikisha matokeo ya tafiti hizo yanatumika ipasavyo kuboresha sera, utendaji na huduma kwa wananchi. Mhe. Sillo alibainisha kuwa utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 unahitaji ushirikiano wa wadau wote na mfumo imara wa tathmini,alisisitiza kuwa mafanikio ya Dira hiyo hayatapimwa kwa idadi ya mikakati au shughuli zilizopangwa pekee, bali kwa matokeo yanayoonekana katika maisha ya wananchi, ikiwemo: Ubora wa elimu na huduma za afya,Upatikanaji wa ajira na miundombinu Huduma za msingi na hifadhi ya mazingira,Ushiriki wa vijana na wanawake katika maendeleo Aidha, alieleza kuwa kaulimbiu ya kongamano hilo linalosisitiza kutoka kwenye ushahidi kwenda kwenye utekelezaji halisi lazima itafsiriwe kwa vitendo ili kusaidia kufanya maamuzi sahihi. Akitoa salamu za Wizara, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Wenye Ulemavu), Dkt. Jimmy Yonazi, alieleza safari ya ukuaji wa kongamano hili tangu kuanzishwa kwake 2022 Dkt. Yonazi alibainisha kuwa utekelezaji wa maazimio 13 yaliyopitishwa katika kongamano lililopita la Mwanza umeleta mafanikio makubwa. Ameainisha mafanikio hayo ni pamoja na Kuanzishwa kwa vitengo vya M&E: Vitengo vya ufuatiliaji na tathmini vimeundwa katika wizara zote, sekretarieti za mikoa yote 26, na halmashauri 104.ambapo zaidi ya watumishi wa umma 800 wamepatiwa mafunzo ya ufuatiliaji na tathmini kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu ikishirikiana na taasisi wadau. Kongamano la mwaka huu lenye kaulimbiu “Kutoka Ushahidi Kwenda Vitendo: Kuimarisha Tathmini ya Umma kwa Maendeleo Endelevu” linafanyika wakati muafaka ambapo Tanzania inaanza utekelezaji wa Dira ya 2050 pamoja na Mpango wa Nne wa Maendeleo wa Miaka Mitano ulioanza Julai 2026.
Wed, 23 Sep 2026 20:30:47 +0000UPPC Attains ISO 9001:2015 Certification, Sets Sights on International Market
Read the full report from the original source.
RecentlyPolice officer shot dead in daytime ambush by bandits in Isiolo
Read the full report from the original source.
RecentlyWAKAGUZI WA NDANI WATAKIWA KUONGEZA THAMANI, UADILIFU NA UWAJIBIKAJI
Na Vero Ignatus – Michuzi TV, Arusha WAKAGUZI wa ndani wanapaswa kuwa wataalamu wanaosaidia taasisi kuelewa vihatarishi, kutambua fursa za maboresho, kuimarisha udhibiti wa utendaji na kuongeza thamani, huku uaminifu, ukweli, ubora, uwajibikaji na matumizi sahihi ya rasilimali vikiwa rasilimali muhimu katika taasisi za umma na binafsi. Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Ikulu) Zanzibar, Dkt. Saada Mkuya, wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 19 wa Mwaka wa Ukaguzi wa Ndani pamoja na Jukwaa la 13 la Utawala Bora jijini Arusha. Akimwakilisha Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, alisema ukaguzi wa ndani unapaswa kuwa sehemu muhimu ya kufanya maamuzi na kuboresha utendaji badala ya taarifa zake kusomwa wakati wa vikao pekee. Dkt. Mkuya alisema ni vyema kutambua kwamba rasilimali za umma zinatumika kwa ufanisi, tija na kuzingatia thamani ya fedha. Aliongeza kuwa jukumu la wakaguzi halipaswi kuishia katika kuthibitisha taratibu, kanuni na mifumo iliyowekwa tu, bali wanapaswa kujiuliza kama ukaguzi na mifumo hiyo ya utawala inazalisha thamani inayokusudiwa. Kwa mujibu wa Dkt. Mkuya, kaulimbiu ya mkutano huo inayosisitiza kwenda “Beyond Assurance” inalenga kuwakumbusha wakaguzi wa ndani kwamba wajibu wao hauishii katika kutoa uhakikisho pekee, bali wanapaswa pia kutoa maarifa, ushauri na mtazamo wa kitaalamu unaosaidia taasisi kuboresha utendaji na kufikia malengo yake. We wewe ndiye mwenye dhamana ya UKAGUZI wa ndani na kuangalia namna ambayo matumizi ya fedha na uratibu bora,kushauri namna gani kuwe na matumizi bora ili taasisi iende mbele. Alisema Dkt. Mkuya Dkt. Mkuya aliongeza kuwa serikali inaendelea kuchukua hatua za kuimarisha kada ya ukaguzi wa ndani, ikiwemo kuandaa sheria mahususi ya ukaguzi wa ndani itakayoweka msingi wa kisheria na kitaasisi wa kulinda uhuru, mamlaka na uwajibikaji wa wakaguzi wa ndani pamoja na kamati za ukaguzi. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa mkutano huo, Benedicto Baragomwa, alisema mkutano huo unawakutanisha wakaguzi wa ndani, viongozi wa bodi, watendaji wa taasisi, wataalamu wa vihatarishi, sekta binafsi na wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi. Baragomwa alisema mazingira ya utendaji yameendelea kubadilika kutokana na maendeleo ya teknolojia, ongezeko la vihatarishi vya usalama wa mtandao, mabadiliko ya sheria na mahitaji ya wananchi; hivyo wakaguzi wa ndani wanapaswa kuwa na uwezo wa kutazama mbele na kutoa ushauri unaoendana na mabadiliko hayo. Akizungumza katika mkutano huo, Rais wa Taasisi ya Wakaguzi wa Ndani Tanzania (IIA Tanzania), Jonathan Ngoma, amezishukuru Wizara ya Fedha ya Muungano, Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, taasisi za serikali, sekta binafsi, wadau wa maendeleo na wadhamini kwa kushiriki katika maandalizi ya mkutano huo. Ngoma alisema mkutano huo unatoa fursa kwa wataalamu kubadilishana uzoefu, kujifunza mbinu mpya na kujadili namna ya kuimarisha utawala bora, usimamizi wa vihatarishi na uwajibikaji katika taasisi, pamoja na kuimarisha usimamizi wa fedha za umma na kuchangia utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya taifa.
Wed, 23 Sep 2026 20:27:37 +0000UNGA: Ruto to push for Africa investment, global reforms
Read the full report from the original source.
RecentlyCoffee, Cocoa Price Drop is Temporary – MAAIF
Read the full report from the original source.
RecentlyWATAALAMU WATAKIWA KUIJENGA SEKTA IMARA YA USAFIRI MAJINI
Na Oscar Assenga, TANGA KAIMU Katibu Tawala Mkoa wa Tanga, Emidius Kasunzu, amesema maendeleo ya sekta ya Usafiri majini yanahitaji kuwa na wataalamu, wabunifu, wajasiriamali na watafiti wenye uwezo wa kutambua changamoto na kuzigeuza kuwa fursa za maendeleo. Amesema Tanzania inapaswa kujiandaa kikamilifu kukabiliana na mabadiliko makubwa yanayoendelea katika sekta ya usafiri wa majini, ikiwemo matumizi ya nishati safi, teknolojia za kidijitali na mifumo ya kisasa ya uendeshaji wa bandari. Alitoa kauli hiyo jijini Tanga wakati akifungua warsha ya Siku ya Bahari Duniani 2026, iliyolenga kujadili namna ya kuimarisha utekelezaji wa viwango vya kimataifa na kitaifa vinavyosimamia sekta ya usafiri wa majini. Amesema miongoni mwa masuala yanayojadiliwa katika warsha hiyo ni kuimarisha usalama na ufanisi wa shughuli za usafiri wa majini, matumizi ya nishati safi na kupunguza uzalishaji wa hewa ukaa katika meli na bandari. Pia amesema warsha hiyo inalenga kujadili namna ya kuimarisha ustawi, usalama na hifadhi ya kijamii kwa mabaharia, kuwaandaa wataalamu kukabiliana na mabadiliko ya teknolojia yanayokua kwa kasi pamoja na kuboresha mafunzo na maendeleo ya rasilimali watu. Kwa mujibu wa Kasunzu, lengo ni kujenga sekta ya usafiri wa majini yenye ufanisi, usalama na endelevu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho. Amesisitiza kuwa mijadala inayofanyika katika warsha hiyo haipaswi kuishia katika kubainisha changamoto pekee, bali inapaswa kuzaa hatua mahususi zitakazowezesha utekelezaji wa suluhisho. “Warsha hii inapaswa kuwa na matokeo ya vitendo,” amesema. Kasunzu amesema sekta ya usafiri wa majini kwa sasa inapitia mabadiliko makubwa yanayochangiwa na matumizi ya nishati safi, maendeleo ya teknolojia za kidijitali, mifumo ya kisasa ya uendeshaji wa bandari pamoja na mahitaji mapya ya ujuzi kwa mabaharia. Amesema mabadiliko hayo, pamoja na kuleta changamoto, yanatoa fursa kubwa kwa Tanzania, hivyo nchi haiwezi kubaki mtazamaji wakati dunia ikiendelea kubadilika. “Tanzania haiwezi kubaki kuwa mtazamaji wa mabadiliko haya. Tunapaswa kujiandaa kuyatumia kwa manufaa ya Taifa letu na kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo,” amesema. Amesema maandalizi hayo yanapaswa kuzingatia mazingira ya Tanzania, uzoefu uliopo pamoja na mahitaji ya wananchi, huku rasilimali watu ikiwa msingi muhimu wa kufanikisha mabadiliko hayo. Kasunzu amesema teknolojia mpya zinahitaji wataalamu wenye ujuzi unaoendana na mahitaji ya sasa ya sekta, akieleza kuwa meli za kisasa zinahitaji mabaharia walioandaliwa kwa viwango vya kisasa. Ameongeza kuwa bandari za kisasa nazo zinahitaji wataalamu wenye uwezo wa kusimamia, kuendesha na kuboresha mifumo ya kiteknolojia ili kuongeza ufanisi wa shughuli za usafiri na biashara. Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Usalama na Mazingira kutoka Wizara ya Uchukuzi Zanzibar, Stella Katondo, amesema maadhimisho hayo pamoja na warsha yameandaliwa kwa lengo la kuhakikisha masuala ya ulinzi, usalama na uhifadhi wa mazingira katika sekta ya usafiri wa majini yanapewa kipaumbele. Katondo amesema ni muhimu kuhakikisha bahari, mito na vyanzo vingine vya maji vinatumika kwa namna ambayo haitawanufaisha watu wa kizazi cha sasa pekee, bali pia vinahifadhiwa kwa ajili ya vizazi vijavyo. Amesema Shirika la Kimataifa la Usafiri Majini (IMO) huweka miongozo mbalimbali ya usalama, ulinzi na uhifadhi wa mazingira ambayo Tanzania, kama mwanachama, inapaswa kuifuata na kuitekeleza. Amesema kaulimbiu ya maadhimisho ya mwaka huu inasisitiza umuhimu wa kutoka katika hatua ya kutunga sera na kuelekea katika utekelezaji wake kwa vitendo. Kwa mujibu wa Katondo, utekelezaji huo unahitaji wataalamu wenye weledi na uwezo wa kuhakikisha masuala ya ulinzi, usalama na uhifadhi wa mazingira yanazingatiwa ipasavyo katika shughuli za usafiri wa majini. Amesema kamati ya maandalizi imeandaa mada mbalimbali zinazolenga kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa ulinzi, usalama na uhifadhi wa mazingira. Katondo amesema makundi mbalimbali yamehusishwa katika shughuli hizo, wakiwemo wanafunzi ambao amewataka kuwa mabalozi wa kuhamasisha wenzao, vijana, walimu na wazazi kuhusu umuhimu wa kulinda mazingira na kuzingatia usalama katika shughuli za usafiri wa majini. Awali, Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Mamlaka ya Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (TASAC), Judith Kakongwe, aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, amesema warsha hiyo pia inatoa nafasi kwa Tanzania kutafakari utekelezaji wa mikataba ya kimataifa katika maeneo ya usalama, mazingira na mabaharia. Kakongwe amesema Tanzania imeridhia mikataba 25 kati ya mikataba 50 ya kimataifa inayosimamia sekta hiyo na kwamba inaendelea kupitia mikataba mingine ili kuhakikisha nchi haiwi nyuma katika utekelezaji wa viwango vinavyotumika kimataifa. Amesema mikataba ambayo Tanzania imeridhia imewezesha kutengenezwa kwa sheria na kanuni mbalimbali zinazosaidia kusimamia sekta hiyo. “Tunatoa elimu, tunatafakari na kufanya tathmini ya sheria tulizonazo, ikiwemo katika usajili wa meli, mabaharia, elimu zao na utekelezaji wa majukumu katika maeneo ya mazingira,” amesema. Kakongwe amesema TASAC ina sheria 64 zinazotekeleza mikataba ya kimataifa ambayo Tanzania imeridhia, hivyo tathmini inayofanyika inalenga kuhakikisha sheria hizo zinatekelezwa kwa ufanisi na matokeo yake yanaonekana kwa wananchi. Amesema moja ya hatua zinazochukuliwa ni kuhakikisha huduma za usafiri wa majini zinakuwa na uwezo wa kutoa msaada wa haraka pale ajali zinapotokea. Ametoa mfano wa hatua za kupeleka boti katika maeneo mbalimbali ya Maziwa Makuu kwa ajili ya kusaidia katika matukio ya dharura, akisema hatua hiyo inalenga kuhakikisha wananchi wanapata msaada kwa wakati na kupunguza madhara kwa maisha na mali. Kwa ujumla, warsha hiyo inalenga kujenga uelewa, kuibua suluhisho na kuweka mikakati ya kuhakikisha sekta ya usafiri wa majini nchini inaendana na mabadiliko ya teknolojia, viwango vya kimataifa pamoja na wajibu wa kulinda mazingira kwa ajili ya vizazi vijavyo.
Wed, 23 Sep 2026 20:22:14 +0000WHI YAWAELIMISHA WANANCHI KUHUSU FURSA ZA UMILIKI WA NYUMBA
Watumishi Housing Investments (WHI) inaendelea kuwafikia na kutoa elimu kwa wananchi mbalimbali wanaotembelea banda lake lililopo katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wakaguzi wa Ndani unaofanyika jijini Arusha kuanzia tarehe 21 hadi 25 Septemba, 2026. Kupitia banda hilo, wananchi wanapata fursa ya kuzungumza moja kwa moja na wataalamu wa WHI na kupata maelezo kuhusu huduma na fursa mbalimbali zinazotolewa na taasisi hiyo, ikiwemo fursa za kumiliki nyumba, uwekezaji kupitia Faida Fund na huduma ya e-Wekeza, pamoja na huduma za ujenzi na ushauri elekezi. Ushiriki wa WHI katika mkutano huo ni sehemu ya jitihada za taasisi hiyo za kuendelea kusogeza huduma na taarifa karibu na wananchi, sambamba na kuongeza uelewa kuhusu fursa za makazi na uwekezaji zinazopatikana kupitia WHI. Wananchi waliopo Arusha wanakaribishwa kutembelea banda la WHI katika AICC hadi tarehe 25 Septemba, 2026, ili kupata maelezo zaidi na kuzungumza moja kwa moja na wataalamu kuhusu huduma na fursa zinazotolewa na taasisi hiyo.
Wed, 23 Sep 2026 20:12:30 +0000Museveni Warns Busoga: Small Land Cannot Sustain Poverty Farming, Embrace High-Income Enterprises
Read the full report from the original source.
RecentlyRABIA ACHANGIA SH MILIONI 12 KWA WAHANGA WA MOTO MACHINGA COMPLEX DODOMA
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Idara ya Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), Rabia Abdalla Hamid (MCC), ametoa mchango wa Sh milioni 12 kwa wahanga wa moto ulioteketeza vibanda vya wafanyabiashara katika Soko la Machinga Complex, Jijini Dodoma. Mchango huo umetolewa leo, Septemba 23, 2026, wakati Rabia akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Dodoma, ambapo amepokelewa katika Ofisi za CCM Mkoa wa Dodoma, kufanya kikao na Kamati ya Siasa pamoja na kutembelea vikundi mbalimbali vya wajasiriamali. Katika ziara hiyo, Rabia pia amekutana na makundi mbalimbali ya kijamii, yakiwemo viongozi wa dini, wazee, machifu, wakulima, wafugaji, wafanyabiashara, mafundi gereji, mafundi ujenzi, wanamichezo, wanafunzi wa vyuo, walimu, machinga, Mawinga, Mama Lishe, Baba Lishe, watu wenye mahitaji maalum, wajane na wagane. Makundi mengine aliyokutana nayo ni vyama vya ushirika, maafisa usafirishaji pamoja na vikundi mbalimbali vya ujasiriamali. Akizungumza na wananchi, Rabia amesikiliza changamoto zinazowakabili na kutoa maelekezo ya utatuzi wa baadhi ya kero hizo papo hapo, huku akisisitiza umuhimu wa wananchi kutumia fursa zilizopo katika maeneo mbalimbali ya kiuchumi kwa ajili ya kujiletea maendeleo. Amesema CCM itaendelea kushirikiana na wananchi katika kusikiliza na kutafuta ufumbuzi wa changamoto zao, pamoja na kuhamasisha shughuli za uzalishaji na ujasiriamali kwa ustawi wa Watanzania. Aidha, Rabia amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ana dhamira njema ya kuijenga Tanzania kwa maslahi ya Watanzania wote.
Wed, 23 Sep 2026 20:04:43 +0000Burundi : Ndayishimiye évoque la menace du Rwanda et l’accueil de migrants transférés par les USA
À New York, le Président Ndayishimiye Évariste affirme que les tensions avec Kigali demeurent et privilégie néanmoins le dialogue. Il s’est également expliqué sur l’accueil au Burundi de migrants transférés depuis les États-Unis. New York, 23/09/2026 (BDIAGNEWS) – En marge de la...
Wed, 23 Sep 2026 20:00:32 +0000Minister Warns Rabies Is a ‘Death Sentence’ as Uganda Targets 2030 Eradication
Read the full report from the original source.
RecentlyUganda Calls for Sustained Follow-Up on Financing for Development and Sevilla Commitments
Read the full report from the original source.
RecentlyPage 1085 of 1121 · 22416 stories