Search the region
22405 stories
TFS YATOA MADAWATI 50, YAOKOA WANAFUNZI 150 KUKAA CHINI KILOSA
Farida Mangube, Kilosa Morogoro Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Kanda ya Mashariki, kupitia Ofisi ya Mhifadhi Misitu Wilaya ya Kilosa, imekabidhi madawati 50 yenye thamani ya Sh milioni 12 kwa Shule ya Msingi Mazinyungu, ikiwa ni sehemu ya mpango wa taasisi hiyo kurejesha kwa jamii. Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo kwa niaba ya Kamanda wa TFS Kanda ya Mashariki, SACC Nethew Ntilicha, Mhifadhi Misitu wa TFS Wilaya za Kinondoni na Ubungo Dotto Ndumbikwa amesema msaada huo ni sehemu ya utaratibu wa TFS kurudisha kwa jamii huku akiwataka wakazi wa Kilosa kuendelea kutunza misitu kwa kuwa faida zinazotokana na uhifadhi wake ndizo zinazowezesha shughuli za kijamii kama utoaji wa msaada huo. Ndumbikwa amesema TFS inaendelea kushirikiana na wadau katika kulinda na kuhifadhi rasilimali za misitu, huku akisisitiza kuwa jamii ina nafasi kubwa katika kuhakikisha misitu inalindwa kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho. Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Shaka Hamdu Shaka, ameishukuru TFS kwa msaada huo akisema umefika wakati muafaka kutokana na ongezeko la idadi ya watoto wanaojiunga na shule. Amesema serikali haiwezi kufanya kila kitu bila ushirikiano wa wadau, hivyo akaitaka TFS kuendelea kuifikia shule nyingine zenye mahitaji pia amesisitiza umuhimu wa jamii kupanda na kutunza miti, akisema Kilosa haitakiwi kuwa jangwa, huku akibainisha kuwa walimu wana nafasi muhimu kuwafundisha watoto umuhimu wa uhifadhi ili ujumbe huo usambae katika jamii. Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mazinyungu Kajika Gallani amesema msaada huo umepunguza changamoto ya upungufu wa madawati na kuwawezesha wanafunzi 150 waliokuwa wakikaa chini kupata sehemu za kukaa hata hivyo amesema shule hiyo bado ina upungufu wa madawati 50 na kuomba wadau wengine kuiga mfano wa TFS. Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi Kaka Mkuu wa shule hiyo, Marco Ng’ondya, mwanafunzi wa Darasa la Sita, ameishukuru TFS kwa msaada huo akisema awali baadhi ya wanafunzi walilazimika kukaa chini, hali iliyowafanya kupata changamoto katika kuandika, kuchafua sare na kushindwa kumfuatilia mwalimu kwa umakini. Aliahidi kuwa wanafunzi wataitumia fursa hiyo kusoma kwa bidii na kufanya vizuri katika masomo, huku akiomba wadau wengine kuendelea kusaidia shule hiyo kukamilisha mahitaji yaliyopo.
Wed, 23 Sep 2026 15:51:11 +0000Ces Africains exploités dans les centres d'arnaques en Asie
Read the full report from the original source.
RecentlyVers l’exemption de visa pour des titulaires de passeports diplomatiques et de service
Read the full report from the original source.
RecentlyHuit abris ingénieux pour la faune sauvage à travers le monde
D'un abri pour chauves-souris dans la campagne britannique à un refuge multispécifique dans les Catskills, voici huit havres de paix pour la faune sauvage conçus avec ingéniosité.
RecentlyLa sécurité du marché moderne de Bugenyuzi sera renforcée
Read the full report from the original source.
RecentlyGermany news: Call to scrap once-a-day gas price rises
Read the full report from the original source.
RecentlyAline Ishimwe turned a dream into a tourism destination business
When Aline Ishimwe looks at her journey in hospitality, she does not only see the growth of a tourism business. She sees a process of
RecentlyMulwa family to take plea in Dr Victoria Mutiso murder case next week
News · Quick read
RecentlyTwo pilots eject and parachute out of RAF plane before crash North Wales Police says the pilots of the RAF T2 Hawk aircraft are being treated for minor injuries.
North Wales Police says the pilots of the RAF T2 Hawk aircraft are being treated for minor injuries.
RecentlyTanzania co-chairs Transport Ministers’ Forum to advance technological ties with China
BEIJING: TANZANIA has been appointed Co-Chair of the Transport Ministers’ Forum being held in Beijing, China, with Minister for Transport…
RecentlyDeux instruments de laboratoire octroyés par la commune Cibitoke à l’hôpital de Murwi
Read the full report from the original source.
RecentlyBuilding a new beginning: refugee students shaping their future through education
Read the full report from the original source.
RecentlyIs your building on govt’s demolition list
For owners of old buildings along Kampala’s major streets, an “X” painted on the property could soon carry an unsettling message: the government believes the…
RecentlyL’ADB sensibilise les investisseurs aux opportunités offertes par la ZLECAF
Read the full report from the original source.
RecentlyFrom Fatherhood to Face Ink: Chameleone’s Son Abba Marcus Turns Heads With New Tattoos
Jose Chameleone’s son Abba Marcus has once again set tongues wagging after showing off a fresh batch of facial tattoos, adding yet another chapter to his increasingly unconventional style. The…
RecentlyTodwong urges youth to embrace issue-based politics
The National Resistance Movement (NRM) Secretary General, Rt. Hon. Richard Todwong, has urged young political leaders to embrace issue-based politics and reject partisan hostility, saying Uganda’s development challenges
RecentlyNestor Basemera, PhD: Uganda’s Urbanization Crisis: Turning Chaos into Engines of Growth
Cities are home to 45 per cent of the global population (UN, 2025). By 2060, half of the world’s population is projected to live in cities (ibid). In Uganda, this…
RecentlyUnpaid allowances, work permit issues: McCarthy lifts lid on Harambee Stars woes ahead of AFCON qualifier
Fresh turmoil surrounds Harambee Stars' preparations for Saturdays 2027 AFCON qualifier against Eritrea after head coach Benni McCarthy revealed a series of problems surrounding the team
Wed, 23 Sep 2026 17:24:22 +0300Rwanda Forces in Mozambique joins Palma community in clean-up activity
Read the full report from the original source.
RecentlyLa Croix-Rouge de Muramvya clôture l’encadrement de plus de 600 jeunes volontaires en vacances
Read the full report from the original source.
RecentlyPage 1091 of 1121 · 22405 stories