Search the region
22397 stories
CHANZO MGOGORO MIGODI YA INK,MAYOMBA CHATAJWA
Na George Maziku, Mbogwe CHANZO cha mgogoro baina ya mgodi wa INK na Mayombya Gold Mine iliyopo kata ya Lugunga, wilayani Mbogwe, mkoa wa Geita, kimewekwa hadharani. Mgogoro huo umesababisha Serikali kuifunga migodi hiyo kwa muda mwisho wa wiki iliyopita ili kupisha uchunguzi, unadaiwa kuchochewa na kampuni ya Dwasi Simon Company Limited, inayomiliki duara namba F1 iliyopo ndani ya leseni ya Mayombya Gold Mine. Akitoa ufafanuzi kuhusu mgogoro huo, Meneja Mkuu wa mgodi wa Mayombya Gold Mine Majuto Manyilizu alisema uongozi wa mgodi wake hauwatambui wachimbaji wa kigeni kutoka China, bali unamtambua na umeingia mkataba na mwekezaji mtanzania aitwaye Dwasi Simon Company Limited anaemiliki duara namba F1. “Kwenye leseni yangu sina wachimbaji wachina, siwatambui wala sijaingia mkataba na wachina,nimeingia mkataba na mwekezaji anayeitwa Dwasi Simon Company Limited ambaye anamiliki duara namba F1, huyu ndiye ninamtambua kama mwekezaji kwenye leseni yangu”, alifafanua Manyilizu. Hata hivyo, Manyilizu alikiri kufahamu uwepo wa raia hao wa kigeni kutoka China, wanaofanya kazi ya uchimbaji kwenye kitalu kinachomilikiwa na Dwasi Simon Company Limited. Kwa muda mrefu sasa kumekuwepo mgogoro baina ya migodi hiyo miwili inayohusu kuingiliana kwa mipaka pamoja na matumizi ya milipuko mikubwa inaayodaiwa kufanywa na mgodi wa Mayombya ambayo inaathiri shughuli za uchimbaji katika mgodi wa INK. Mgogoro huo ulichukua sura mpya Ijumaa, wiki iliyopita, baada ya uamuzi wa Tume ya Madini nchini kusitisha shughuli za uchimbaji katika migodi yote miwili ili kupisha uchunguzi utakaofanywa na wataalamu wa tume hiyo. Kiini cha mgogoro huo kinadaiwa kuwa ni vitendo vya wachimbaji wa kichina kuendesha shughuli za uchimbaji bila kuzingatia kwanza mipaka baina ya mgodi wa Mayombya na mgodi jirani wa INK, ambapo inadaiwa wamevuka mpaka na kuingia eneo la leseni la mgodi wa INK. “Mojawapo ya changamoto zilizozalisha mgogoro huu ni shughuli za kichimbaji za daraja la kati zinazoendeshwa katika leseni ya jirani zetu kwa kutumia raia wa kigeni ambazo zinaambatana na milipuko mikubwa ambayo zimeleta athari kubwa katika maduara yanayomilikiwa na wachimbaji wadogo kwenye mgodi wetu… “Uchunguzi wa awali unaashiria hatari kubwa kama hatua za haraka hazitachukuliwa kunaweza kutokea ajali kubwa na kusababisha mauaji ya wachimbaji wengi”, alisisitiza Meneja Mkuu wa mgodi wa INK Farid Lugwisha. Kwa upande wake Mkurugenzi wa Dwasi Simon Company Limited , Dwasi Simon alipotafutwa ili kutoa ufafanuzi wa mgogoro huo hakuwa tayari kuzungumza kwa madai alikuwa msibani wilayani Bariadi, mkoani Simiyu, hivyo akimtaka mwandishi kusubiri hadi atakaporejea Mbogwe.
Wed, 23 Sep 2026 14:02:37 +0000Kindiki: Kenya Kwanza implementing manifesto ‘project by project’
Kenya · 3 hours ago
RecentlyKakuzi birdwatching tour ends in triumph as Japanese royalty sights rare migratory birds
Latest · Kenya
RecentlyDramatic eviction of woman aged 87 highlights Spain's housing shortage Maricarmen's father first rented the property in 1956 and she continued as the tenant after her parents died
Maricarmen's father first rented the property in 1956 and she continued as the tenant after her parents died
RecentlyREA pledges to complete distribution of power in all rural hamlets by 2030
DODOMA: THE Tanzanian government is committed to completing electricity distribution projects in all rural hamlets by 2030, a move expected…
RecentlyUN General Assembly: Syria's al-Sharaa kicks of Day 2
Read the full report from the original source.
RecentlyMurkomen warns new reservists over firearm misuse The CS warned that reservists who misuse their guns for personal gain will face prosecution.
The CS warned that reservists who misuse their guns for personal gain will face prosecution.
RecentlyMizigo yawaweka matatani madereva bajaji 72 Mwanza
Read the full report from the original source.
RecentlyMSD receives first shipment of Naltrexone for the treatment of alcohol addiction
DAR ES SALAAM: THE Medical Stores Department (MSD) has successfully imported the first shipment of Naltrexone, a medicine used in…
RecentlyGovernment Commits to End Persistent Power Outages by 2029
Read the full report from the original source.
RecentlyDKT. GWAJIMA: MALEZI DUNI YA WATOTO YANACHOCHEA TABIA HATARISHI
Na Janeth Raphael - MichuziTv Malezi ya mtoto katika hatua za awali za maisha yana nafasi kubwa katika kujenga tabia, mwenendo na mustakabali wake, huku ukosefu wa uangalizi na malezi bora ukitajwa kuwa miongoni mwa sababu zinazoweza kuwafanya watoto kukua katika mazingira hatarishi na kujihusisha na vitendo visivyofaa. Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, amesema hayo leo jijini Dodoma wakati akifungua Mkutano wa Nusu ya Mwaka wa Tathmini ya Utekelezaji wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto. Dkt. Gwajima amesema baadhi ya wazazi wanapopata watoto hawatoi malezi na mwelekeo unaostahili, hali ambayo huwa mbaya zaidi pale wazazi wanapotengana na watoto kuachwa bila uangalizi wa kutosha, hivyo kuwalazimu baadhi yao kujilea wenyewe katika mazingira ya mitaani. Amesema malezi ya mtoto yanapaswa kuanza kwa maandalizi na makubaliano ya wazazi kabla ya kupata watoto, huku akisisitiza kuwa jukumu la malezi halipaswi kuachwa kwa mzazi mmoja pekee, bali linahitaji ushirikiano wa familia na jamii nzima ili kuhakikisha mtoto anakua katika mazingira salama na yenye mwelekeo sahihi. Dkt. Gwajima, amesema uwekezaji katika maendeleo ya binadamu huanza tangu hatua za mwanzo kabisa za maisha, hivyo ni muhimu kuhakikisha watoto wanapata malezi, makuzi na huduma stahiki katika umri wao wa awali, ikiwa ni pamoja na kupitia familia, jamii na vituo vinavyotoa huduma za malezi ya watoto. Aidha, amewataka waandishi wa habari kutumia nafasi yao kuelimisha na kuhamasisha wazazi na wananchi kuhusu umuhimu wa malezi bora, akisisitiza kuwa mtoto anayejengewa misingi imara tangu utotoni anaandaliwa kuwa sehemu muhimu ya kizazi kinachojitambua na kuchangia katika maendeleo ya Taifa. Amesema, kama ilivyo kwa nyumba inayohitaji msingi imara ili iweze kudumu, ndivyo maisha ya mtoto yanavyohitaji msingi mzuri wa malezi tangu mwanzo.
Wed, 23 Sep 2026 13:38:05 +0000Government moves to accelerate completion of development project
The government is stepping up efforts to accelerate the completion of infrastructure projects across the country by clearing outstanding payments owed to contractors and ensuring adequate funding for ongoing works.…
RecentlyWhen the card isn’t there: why trust will define East Africa’s next phase of digital commerce
Latest · Opinion
RecentlyDKT. MWIGULU AHIMIZA USHIRIKIANO WA KIKANDA KUDHIBITI MAGONJWA YA MIFUGO
▪️︎ EU kuwekeza Euro milioni 50 kusaidia kutokomeza sotoka barani Afrika WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Tanzania itaendelea kushirikiana na FAO, Shirika la Afya ya Wanyama Duniani (WOAH), Umoja wa Afrika, jumuiya za kikanda, na wadu wengine katika kuimarisha uwekezaji na mifumo ya kudhibiti magonjwa ya mifugo kwa lengo la kuchangia kutokomeza Sotoka ifikapo mwaka 2040. “Tunataka kuona uwekezaji wenye nguvu zaidi, unaotabirika na endelevu. Umiliki wa kitaifa na ufadhili wa ndani lazima viwe msingi, vikisaidiwa na FAO, WOAH, Umoja wa Afrika, jumuiya za kikanda, taasisi za fedha za kimataifa, washirika wa maendeleo na sekta binafsi.” “Tunapaswa kuondoka katika hatua zilizotawanyika na kuelekea kwenye mifumo ya kudumu; kutoka mipango ya kitaifa pekee kwenda ushirikiano wa kikanda; na kutoka ahadi kwenda kwenye matokeo yanayoweza kupimika,” alisisitiza Waziri Mkuu. Alisema hayo jana, (Jumanne, Septemba 22, 2026) jijini Roma, Italia, wakati akishiriki mjadala wa ngazi ya juu kuhusu uwekezaji katika kutokomeza Sotoka na kudhibiti Ugonjwa wa Miguu na Midomo kwenye Mkutano wa Kimataifa ulioandaliwa na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) kuhusu utekelezaji wa Afya Moja katika mifumo ya chakula na kilimo. Alisema chanjo pekee haitoshi, bali Tanzania inahitaji maabara zinazofanya kazi, mifumo madhubuti ya ufuatiliaji, usambazaji wa chanjo wa uhakika, utambuzi wa mifugo, wataalamu wenye ujuzi na ushirikiano baina ya nchi na nchi hasa kwenye maeneo ya mipakani. Akizungumzia umuhimu wa ushirikiano wa kikanda, Dkt. Mwigulu alisema magonjwa ya mifugo hayaheshimu mipaka ya nchi, na kubainisha kuwa wakati nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zikijadili hatua za kuelekea shirikisho, wanyama tayari wameungana kwa kasi zaidi. “Wakati nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zikiendelea kujadili namba ya kuingia katika mfumo wa shirikisho, wanyama tayari wameungana haraka kuliko sisi,” alisema. Akifungua mlango wa kuchangia mada kwenye mjadala huo, Balozi wa Umoja wa Ulaya jijini Roma na Mwakilishi wa Kudumu wa Umoja huo katika Mashirika ya Umoja wa Mataifa ya Roma, Dkt. Martin Selmayr, alisema Umoja wa Ulaya unaandaa uwekezaji mpya wa Euro milioni 50 kwa ajili ya awamu ya pili ya mpango wa kutokomeza Sotoka barani Afrika. Balozi Selmayr alisema uwekezaji huo unalenga kuongeza nguvu katika juhudi za kutokomeza ugonjwa huo na kuwa kichocheo kwa nchi husika, taasisi za fedha za maendeleo, sekta binafsi na washirika wengine kuongeza uwekezaji katika programu za kitaifa za kutokomeza sotoka. “Umoja wa Ulaya unaamini kuwa uwekezaji huo haupaswi kuishia katika kampeni nyingine ya chanjo pekee, bali unapaswa kusaidia pia kuimarisha huduma za mifugo, uzalishaji na ubora wa chanjo, ushirikiano wa sekta binafsi pamoja na hatua za pamoja za kukabiliana na magonjwa yanayovuka mipaka,” alisisitiza. Naye, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa FAO, Godfrey Magwenzi, alisema afya ya wanyama ni uwekezaji wa kimkakati katika usalama wa chakula, maendeleo ya uchumi na ustahimilivu, akisisitiza umuhimu wa uwekezaji wa muda mrefu katika kutokomeza sotoka. Kwa upande wake, Waziri wa Mifugo na Uzalishaji wa Wanyama wa Chad, Prof. Abderrahim Awat Atteib, alisema juhudi za kutokomeza ugonjwa huo zinahitaji ufadhili endelevu na unaotabirika ili kuzuia ugonjwa huo kurejea katika maeneo ambayo tayari yamedhibitiwa. Naye, Dkt. Samuel Thevasagayam, Mkurugenzi wa Timu ya Mifugo wa Taasisi ya The Gates Foundation, alisema mafanikio ya kutokomeza sotoka yanahitaji umiliki wa Serikali, ushiriki wa wafugaji na sekta binafsi, pamoja na matumizi ya sayansi na ushahidi katika kupanga na kutekeleza hatua za kudhibiti ugonjwa huo.
Wed, 23 Sep 2026 13:37:07 +0000ONE Campaign launches advocacy academy for young Africans
Latest · Africa
RecentlyKenya universities struggle to attract foreign students University Statistics Report 2025 shows that Kenyan nationals accounted for 98.39 per cent of students.
University Statistics Report 2025 shows that Kenyan nationals accounted for 98.39 per cent of students.
RecentlyIPOA probing Dennis Osiemo's death at Narumoru Police Station
IPOA conveys condolences to the family of the deceased and assures them that the matter is receiving the attention it so deserves.
Wed, 23 Sep 2026 15:39:10 +0300Vyanda : des agriculteurs réclament leurs engrais déjà payés mais non livrés
Read the full report from the original source.
RecentlyLoyalty over form! McCarthy defends omission of in-form stars in favour of trusted “soldiers”
Latest · Harambee Stars
RecentlyTop 10 counties in factory modernisation grants Tharaka Nithi received Sh35 million, while Kirinyaga County received Sh28.7 million.
Tharaka Nithi received Sh35 million, while Kirinyaga County received Sh28.7 million.
RecentlyPage 1094 of 1120 · 22397 stories