Search the region
22347 stories
NYONGO AWATAKA WAFUGAJI KUACHA KUINGIZA MIFUGO MASHAMBANI
Na Mwamvua Mwinyi, Pwani MKUU wa Mkoa wa Pwani, Stanslaus Nyongo , amewaagiza wafugaji mkoani humo kuacha mara moja kuingiza na kulisha mifugo katika mashamba ya wakulima, akisisitiza kuwa Serikali haitavumilia uharibifu wa mazao unaosababishwa na mifugo. Nyongo alitoa agizo hilo Septemba 22, 2026, wakati wa ziara yake ya kikazi katika Halmashauri za Mji wa Rufiji na Kibiti, ambako alisikiliza kero za wananchi na kutoa maelekezo ya hatua za kuchukuliwa. Alisema Serikali haiwezi kuendelea kushuhudia mazao ya wakulima yakiharibiwa na mifugo, wakati maeneo yametengwa kwa ajili ya kilimo na ufugaji. “Hatukubali kuendelea kuona mazao ya wakulima yakiharibiwa wakati kila kundi limetengewa maeneo kwa ajili ya shughuli zake. Wafugaji waheshimu maeneo ya wakulima na waache mara moja kuingiza mifugo kwenye mashamba,” alisema. Aidha, alimtaka Mkuu wa Wilaya ya Rufiji kusimamia utekelezaji wa agizo hilo na kuhakikisha wafugaji watakaobainika kuingiza au kulisha mifugo katika mashamba ya wakulima wanachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria. Katika hatua nyingine, Nyongo aliipongeza Halmashauri ya Rufiji kwa kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato na kuvuka malengo yaliyowekwa, huku akizitaka Halmashauri za Rufiji na Kibiti kuimarisha usimamizi wa vyanzo vya mapato ili kuongeza uwezo wa Serikali za mitaa kutoa huduma bora kwa wananchi. Kuhusu utabiri wa mvua kubwa za msimu wa Vuli unaohusishwa na hali ya El Niño , Nyongo alizitaka halmashauri hizo kuimarisha maandalizi na kuchukua hatua za tahadhari mapema ili kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza. Aliwataka wananchi wanaoishi katika maeneo ya mabondeni na maeneo mengine hatarishi kuhama mapema na kuhamia maeneo salama, akisisitiza kuwa usalama wa maisha ya wananchi unapaswa kupewa kipaumbele. Pia, aliwataka Wakuu wa Wilaya za Rufiji na Kibiti kutambua na kuainisha maeneo salama yatakayotumika kuwaweka wananchi watakaoweza kuathiriwa na mvua hizo, pamoja na kuhakikisha huduma muhimu zinapatikana katika maeneo hayo. Ziara hiyo ni ya kwanza ya kikazi kwa Nyongo katika halmashauri hizo tangu alipoteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, ikiwa na lengo la kujitambulisha, kusikiliza kero za wananchi na kukagua utekelezaji wa shughuli za maendeleo.
Wed, 23 Sep 2026 06:28:24 +0000MUHIMBILI YAPOKEA MSAADA WA TZS. 23 MIL KUTOKA LIONS CLUB INTERNATIONAL
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), leo imepokea vifaa vya kutolea huduma za tiba aina ya Infusion Pumps vyenye thamani ya Shilingi milioni 23, vilivyotolewa na Lions Club International, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha ubora wa huduma za afya na kuongeza usalama wa wagonjwa wakati wa matibabu. Akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Mkurugenzi wa Tiba Shirikishi, Dkt. Mbonea Yonazi, ameishukuru Lions Club International kwa mchango huo muhimu, na kuongeza kuwa vifaa hivyo vitaenda kuongeza ufanisi wa matibabu na usalama wa wagonjwa. “ Vifaa hivi vitasaidia kuboresha utoaji wa huduma na kuhakikisha wagonjwa wanapata huduma sahihi kulingana na mahitaji yao, huu ni mchango mkubwa katika kuimarisha usalama wa mgonjwa na ubora wa huduma tunazozitoa,”amesema Dkt. Yonazi. MNH inaendelea kuwekeza katika matumizi ya teknolojia za kisasa katika huduma za afya, hatua inayochangia kuongeza ufanisi, usahihi na usalama wa huduma kwa wagonjwa.
Wed, 23 Sep 2026 07:40:58 +0000TANZANIA YAPIGA HATUA KUPUNGUZA VIFO VYA MAMA NA MTOTO, YAWANIA KITI BARAZA LA USALAMA UN
NEW YORK, Marekani TANZANIA imetangaza rasmi azma ya kuwania nafasi ya uanachama usio wa kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN) kwa kipindi cha mwaka 2029–2030, ikiahidi kupeleka sauti imara ya Afrika na kusukuma mbele diplomasia ya kuzuia migogoro, utatuzi wa migogoro kwa njia za amani na mageuzi ya operesheni za kulinda amani. Msimamo huo umetolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Mjadala wa Mkutano wa 81 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa unaofanyika jijini New York, Marekani. Mhe. Ndejembi amesema iwapo Tanzania itachaguliwa, itatoa kipaumbele kwa diplomasia ya kuzuia migogoro kabla haijageuka kuwa vita, utatuzi wa migogoro kwa njia za amani, kuimarisha nafasi ya wanawake katika ulinzi na ujenzi wa amani, kuongeza ushiriki wa vijana katika ajenda ya amani na usalama, pamoja na kusukuma mbele mageuzi ya operesheni za Umoja wa Mataifa za kulinda amani. Amesema azma hiyo imepata uungwaji mkono wa Umoja wa Afrika (AU), huku uchaguzi wa wajumbe wa Baraza la Usalama kwa kipindi hicho ukitarajiwa kufanyika Juni 2028. TANZANIA YASISITIZA MAGEUZI UN Katika hotuba hiyo, Tanzania imesisitiza umuhimu wa kuendelea kufanyika kwa mageuzi katika Umoja wa Mataifa ili kuimarisha misingi ya haki, usawa na uwakilishi wenye uwiano, badala ya mfumo wa kimataifa kuendelea kuakisi zaidi nguvu na ushawishi wa mataifa machache. Mhe. Ndejembi amesema mageuzi hayo ni muhimu zaidi katika kipindi ambacho dunia inakabiliwa na migogoro na vita, athari za mabadiliko ya tabianchi, milipuko ya magonjwa, kasi ya maendeleo ya Akili Mnemba (AI) na changamoto za usalama wa nishati. TANZANIA YAPUNGUZA VIFO VYA MAMA NA MTOTO Akizungumzia afya ya mama na mtoto, Mhe. Ndejembi amesema Tanzania imepiga hatua kubwa katika kupunguza vifo vya mama na mtoto, ikiwamo kuongeza kiwango cha uzazi unaofanyika katika vituo vya afya kutoka asilimia 51 mwaka 2015 hadi asilimia 81 mwaka 2022. Amesema uzoefu huo unaonesha kuwa uwekezaji katika miradi inayotekelezeka na inayoweka ustawi wa watu mbele unaweza kugeuza ahadi kuwa matokeo yanayoonekana na kupimika. Kwa msingi huo, amesema Rais Samia Suluhu Hassan alikubali kuwa kinara wa masuala ya Afya ya Mama na Mtoto kwa niaba ya Umoja wa Afrika. Mhe. Ndejembi amesema chini ya uongozi huo, Tanzania imefanikiwa kupunguza vifo vya akina mama kwa asilimia 80 ndani ya kipindi cha miaka saba, akisisitiza kuwa nchi hiyo inalenga kufikia malengo ya “Sifuri Tatu” (Three Zeros) . Malengo hayo ni kutokuwepo kwa vifo vya mama na mtoto vinavyoweza kuzuilika, kutokuwepo kwa uzazi unaofanyika majumbani na kutokuwepo kwa watoto ambao hawajapata chanjo. Amesema Afrika inaweza kufikia malengo hayo, lakini inahitaji uongozi thabiti wa kisiasa, rasilimali fedha za kutosha na ushirikiano imara zaidi kutoka kwa jumuiya ya kimataifa. TANZANIA YATAKA MAGEUZI YA MFUMO WA FEDHA DUNIANI Tanzania pia imesisitiza umuhimu wa nchi zinazoendelea kupewa sauti kubwa zaidi katika taasisi na mifumo ya kimataifa inayofanya maamuzi ya kifedha yanayoathiri uchumi na maendeleo yake ya muda mrefu. Mhe. Ndejembi amesema Tanzania imewasilisha Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 kama msingi wa kujenga uchumi jumuishi, shindani na unaoweza kustahimili misukosuko, kupitia uwekezaji katika watu, miundombinu yenye tija, teknolojia, ubunifu, wanawake na vijana. Amesema mageuzi katika mfumo wa fedha wa kimataifa ni muhimu ili nchi zinazoendelea ziweze kupata rasilimali zinazohitajika kuharakisha utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs). Ametaja umuhimu wa kuongeza mikopo yenye masharti nafuu, kuhamasisha uwekezaji wa sekta binafsi, kurahisisha upatikanaji wa fedha za maendeleo na tabianchi, pamoja na kuongeza ushiriki wa nchi zinazoendelea katika maamuzi ya kifedha duniani. TABIANCHI, NISHATI SAFI Katika eneo la mabadiliko ya tabianchi, Tanzania imeeleza wasiwasi kuhusu pengo lililopo kati ya kiwango cha uzalishaji wa gesi chafuzi duniani na fedha zinazotolewa kusaidia nchi zinazoathirika kukabiliana na madhara yake. Tanzania imesisitiza kuwa nchi zinazochangia kwa kiwango kikubwa uzalishaji wa gesi chafuzi zinapaswa kubeba wajibu mkubwa zaidi katika kugharamia hatua za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi. Katika mkakati wake wa mpito kuelekea nishati safi, Tanzania imetaja Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere lenye uwezo wa kuzalisha megawati 2,115, miradi ya nishati ya jua na upepo yenye jumla ya megawati 650, pamoja na mipango ya kuzalisha megawati 130 za nishati ya jotoardhi. Pia, Tanzania imeeleza uwekezaji katika reli ya umeme na lengo la kuongeza matumizi ya nishati safi ya kupikia hadi kufikia asilimia 80 ya kaya ifikapo mwaka 2034. TANZANIA YAPINGA VIKWAZO VYA UPANDE MMOJA Katika diplomasia ya kimataifa, Tanzania imepinga matumizi ya vikwazo vya upande mmoja vinavyowekwa na baadhi ya mataifa dhidi ya mataifa mengine, ikisema hatua hizo zinaweza kudhoofisha mamlaka ya nchi, kuathiri maendeleo na kupunguza uwezo wa wananchi kunufaika kikamilifu na haki zao. Tanzania imeeleza mshikamano wake na Cuba, Zimbabwe na mataifa mengine yanayokabiliwa na vikwazo hivyo, huku ikitoa wito wa kuchukuliwa hatua za makusudi kuelekea kuondolewa kwa vikwazo bila masharti. TANZANIA YATOA WITO WA AMANI GAZA Kuhusu hali ya Gaza na Mashariki ya Kati, Tanzania imesisitiza umuhimu wa kuwalinda raia, kuruhusu misaada ya kibinadamu kuwafikia wanaohitaji bila vikwazo na kurejesha diplomasia kuwa njia kuu ya kutafuta amani ya kudumu. Kwa ujumla, ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 81 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa umeunganisha ajenda ya maendeleo ya Taifa na hoja pana kuhusu nafasi ya Afrika katika mfumo wa kimataifa. Tanzania imesisitiza kuwa Umoja wa Mataifa haupaswi kuwa jukwaa linaloakisi pekee uwiano wa nguvu duniani, bali taasisi inayosimamia haki, mshikamano, usawa na maendeleo kwa mataifa yote. Msimamo huo unaweka bayana ajenda ambayo Tanzania inalenga kuibeba katika safari yake ya kuwania nafasi ya uanachama usio wa kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kipindi cha 2029–2030; kuimarisha sauti ya Afrika, kuzuia migogoro, kutetea suluhu za amani na kusukuma mageuzi ya mfumo wa kimataifa ili uwe na uwakilishi wenye uwiano zaidi.
Wed, 23 Sep 2026 07:41:37 +0000WATALAAMU WA USAFIRISHAJI WAKUTANA ARUSHA
-TEKNOLOJIA, UBUNIFU KUTUMIKA KUPUNGUZA GHARAMA ZA USAFIRISHAJI Na Ashura Mohamed – Arusha WATAALAMU wa usafirishaji, ununuzi na mnyororo wa ugavi kutoka ndani na nje ya Afrika wamekutana jijini Arusha kujadili namna teknolojia na ubunifu unavyoweza kutumika kupunguza gharama za usafirishaji na kuimarisha mchango wa sekta hiyo katika uchumi. Akizungumza wakati akimwakilisha Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, katika Mkutano wa Nane wa Afrika wa Usimamizi wa Uendeshaji na Mnyororo wa Ugavi (ACOSCM), Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile, amesema uboreshaji wa miundombinu ya usafirishaji ni muhimu katika kupunguza gharama za usafirishaji nchini. Amesema sekta ya usafirishaji ni mhimili muhimu wa uchumi kwa kuwa inaunganisha wazalishaji na masoko, kuwezesha biashara na kuchochea shughuli za kiuchumi. Kwa mujibu wa Kihenzile, sekta ya usafirishaji nchini ilizalisha dola za Marekani bilioni 2.7 mwaka 2025, sawa na asilimia 15.6 ya mauzo ya nje ya Tanzania, ikilinganishwa na dola bilioni 2.2 mwaka 2024. “Serikali yetu inaendelea kuboresha miundombinu ya usafirishaji nchini kwa sababu sekta hii ni muhimu kwa wakulima, wavuvi na wajasiriamali. Gharama za usafirishaji zinapopungua, mnufaika wa mwisho ni mwananchi, kwa kuwa gharama za kusafirisha bidhaa zake hupungua,” amesema Kihenzile. Aidha, amewataka washiriki wa mkutano huo kujikita katika kujadili suluhisho la changamoto zinazokabili sekta ya usafirishaji, ikiwamo namna vijana na makundi mengine yanavyoweza kushiriki na kunufaika na fursa zinazotokana na miradi mbalimbali ya miundombinu, ikiwamo Reli ya Kisasa (SGR). Kwa upande wake, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe anayeshughulikia Taaluma, Prof. Hawa Tundui, amesema mkutano huo umewakutanisha wataalamu takribani 200 kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika pamoja na mabara ya Ulaya na Asia. Amesema mjadala mkuu umejikita katika namna ya kutumia ubunifu na teknolojia katika masuala ya usafirishaji, ununuzi na mnyororo wa ugavi ili kupunguza gharama na kuongeza ufanisi. “Mada kubwa ni namna bora ya kutumia ubunifu na teknolojia katika masuala ya usafirishaji, ununuzi na ugavi. Tumewakutanisha wadau mbalimbali, wakiwemo watafiti na wataalamu kutoka Afrika, Ulaya na Asia, ili kuangalia namna ubunifu na teknolojia unavyoweza kuleta mchango katika serikali zetu na kusaidia kupunguza gharama za usafirishaji,” amesema Prof. Tundui. Amesema lengo la mkutano huo ni kufikia maazimio ya pamoja yatakayosaidia kuhakikisha sekta ya uchukuzi inakuwa na ufanisi na kuleta unafuu katika mnyororo mzima wa usafirishaji. Mkutano huo umeandaliwa na Chuo Kikuu cha Mzumbe kwa kushirikiana na Khune Foundation Tanzania.
Wed, 23 Sep 2026 08:43:15 +0000VERTO,VISA WZINDUA KADI MAALUM YA KIMATAIFA KWA BIASHARA ZA AFRIKA
Na Mwandishi Wetu KAMPUNI ya kimataifa ya teknolojia ya fedha, Verto kwa kushirikiana na Visa, imezindua kadi maalumu ya biashara inayojumuisha sarafu nyingi kuwezesha malipo ya kimataifa. Kadi hiyo inalenga kusaidia wafanyabiashara barani Afrika kupunguza gharama za ubadilishaji wa fedha za kigeni, kuboresha usimamizi wa matumizi ya fedha na kuongeza ufanisi wa shughuli zao katika masoko ya kimataifa. Kadi hiyo ya Verto inawawezesha wafanyabiashara kutumia fedha moja kwa moja kutoka kwenye akaunti zao bila kulazimika kuhamisha fedha kati ya akaunti ama kubadilisha fedha kabla ya kufanya malipo. Kupitia kadi hiyo wafanyabiashara wanaweza kuzifikia sarafu 11 moja kwa moja huku wakipata fursa ya kutumia zaidi ya sarafu nyingine 160 kupitia mtandao wa kimataifa wa malipo wa Visa.Aidha,huduma hiyo haitatoza nyongeza ya gharama za ubadilishaji wa fedha za kigeni katika sarafu kuu 10. Akizungumza kuhusu uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi Mwenza wa Verto, Ola Oyetayo, alisema huduma hiyo inalenga kukabiliana na pengo kubwa la miundombinu ya kifedha linalozikabili biashara za barani Afrika zinazofanyika kimataifa. “Biashara za Afrika zimekua na kuvuka mipaka kwa kasi kikubwa kuliko miundombinu ya kifedha inayozihudumia. Kwa sasa, changamoto si upatikanaji wa masoko, bali ni namna fedha zinavyohamishwa. “Kampuni nyingi bado zinapoteza fedha kutokana na gharama zisizo za lazima katika ubadilishaji wa fedha, ucheleweshaji wa malipo na taratibu za kibenki zilizogawanyika, ambazo huathiri moja kwa moja faida na ukuaji wa biashara. “Kadi ya Verto imeundwa kuwapa wafanyabiashara udhibiti mkubwa zaidi wa matumizi ya kimataifa, huku ikipunguza baadhi ya vikwazo ambavyo kwa muda mrefu vimeambatana na biashara za hizo kimataifa,” alisema. Kadi ya Verto inakubalika katika zaidi ya maduka na biashara milioni 150 duniani kote, popote ambapo kadi zote za Visa zinakubalika, ikiwemo kwa wafanyabiashara wanaohitaji mifumo ya malipo ya kadi za mkopo. Hali hiyo inaziwezesha biashara kupata fursa ya kufanya malipo kwa wafanyabiashara wa kimataifa kwa kutumia kadi moja iliyounganishwa na akaunti zao za Verto. Kadi hiyo pia inaruhusu biashara kugharamia miamala moja kwa moja kutoka kwenye pochi zao za sarafu za Verto, hatua inayosaidia kupunguza ubadilishaji wa fedha usio wa lazima na kuboresha ufuatiliaji pamoja na udhibiti wa matumizi ya fedha kimataifa. Jukwaa hilo linajumuisha pia mifumo ya kudhibiti matumizi, utoaji wa kadi papo hapo na usalama wa miamala ulioimarishwa. “Usimamizi wa sarafu nyingi haupaswi kuwa kikwazo cha ukuaji kwa biashara zinazolenga kupanua shughuli zao kimataifa,” alisema Shahebaz Khan, Makamu wa Rais Mwandamizi na Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Uhamishaji Fedha wa Visa. “Ushirikiano wetu na Verto unasaidia kurahisisha namna biashara zinavyowalipa wasambazaji, kusimamia gharama na kufanya miamala kimataifa huku zikipata usalama na ukubalifu mpana wa kimataifa wanaoutegemea kutoka Visa,” alisema. Wakati biashara za Afrika Mashariki zikizidi kupanua shughuli zao katika masoko mapya, uwezo wa kuhamisha na kusimamia fedha kwa ufanisi kuvuka mipaka unazidi kuwa suala la muhimu. Kuanzia kuwalipa wasambazaji wa kimataifa na kusimamia usajili wa huduma hadi kugharamia shughuli za uendeshaji katika masoko mbalimbali, biashara zinahitaji mifumo ya malipo inayoweza kwenda sambamba na shughuli zao zinazozidi kukua kimataifa. Uzinduzi huo ni sehemu ya mpango mpana wa Verto wa kupanua miundombinu yake ya usimamizi wa fedha na malipo ya kimataifa kwa lengo la kusaidia biashara katika masoko mapya zinapopanua shughuli zao kuvuka mipaka na kusaka fursa mpya kimataifa. Kuhusu Verto Verto ni kampuni ya kimataifa ya teknolojia ya fedha inayolenga biashara kwa biashara (B2B) ikiwezesha biashara za ukubwa wowote kupata huduma za malipo yanayovuka mipaka, ubadilishaji wa fedha za kigeni na huduma za kibenki zenye viwango vya biashara kubwa. Kupitia miundombinu ya kiteknolojia iliyoundwa mahsusi na mifumo ya malipo, biashara zinaweza kutuma na kupokea fedha papo hapo katika nchi zaidi ya 190 na kubadilisha fedha hizo katika sarafu 48. Kwa sasa, Verto inahudumia biashara zaidi ya 5,000 duniani kote, kuanzia kampuni ndogo na za kati hadi mashirika makubwa ya kimataifa. Biashara hizo hufanya miamala yenye kufikia zaidi ya dola za Marekani bilioni 25 kwa mwaka. Kuhusu Visa Visa ni kampuni inayoongoza duniani katika malipo ya kidijiti inayowezesha miamala kati ya watumiaji, wauzaji, taasisi za kifedha na mashirika ya serikali katika nchi zaidi ya 200.
Wed, 23 Sep 2026 09:18:23 +0000WAZIRI AKWILAPO AZINDUA MPANGO WA KKK ENEO LA SHAMBA LA MWAKINYUMBI KOROGWE
Na Munir Shemweta, WANMM KOROGWE WAZIRI wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo amezindua rasmi mpango wa kupanga, kupima na Kumilikisha Ardhi (KKK) katika eneo la Shamba la Mwakinyumbi lililopo Kata ya Hale, Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga huku akiwataka wananchi wanaoishi eneo hilo kushirikiana na wataalamu ili zoezi hilo likamilike ndani ya muda uliopangwa. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango huo katika uwanja wa Mwenge, Hale Korogwe leo Sept 21, 2026 mkoani Tanga Mhe. Dkt Akwilapo amesema, hatua hiyo inalenga kuwatambua wananchi wanaostahili, kupangiwa na kupimiwa ardhi hiyo, na hatimaye kuwamilikisha viwanja vilivyopimwa kwa mujibu wa taratibu za kisheria. Mpango wa uendelezaji wa ardhi katika eneo hilo unahusisha ekari 5000 zilizotengwa kwa ajili ya matumizi ya kilimo, makazi na huduma za jamii, miundombinu, ardhi ya akiba, ardhi ya uwekezaji na uchimbaji madini, hifadhi ya mlima na hifadhi ya vyanzo vya maji. Aidha ekari 4,220 zimetengwa kwa vijiji vya Mwanyumbi Station na Miembeni na kufanya jumla ya ekari 9220 kuwa katika mpango huo wa uendelezajI. Aidha, Dkt Akwilapo aliweka wazi kuwa, kabla ya kuanza kwa zoezi hilo la upangaji na upimaji, wananchi watapatiwa elimu kuhusu taratibu zitakazotumika, vigezo vya utambuzi, ukubwa wa maeneo watakayopangiwa pamoja na masuala mengine ya kisheria na kitaalamu. " Niwaombe wananchi wa Mwakinyumbi kushiriki kikamilifu katika hatua hiyo ili kupata ufafanuzi na kuelewa namna zoezi litakavyotekelezwa". Amesema Mbunge wa jimbo la Korogwe Vijijini Mhe. Timotheo Mzava amemuomba Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuhakikisha wananchi Mwakinyumbi katika kata ya Hale Korogwe wanapewa kipaumbele kwa kuwapatia viwanja kwa gharama nafuu. Aidha, ametaka pasiwe na utaratibu wa kuwaondoa wanachi walioingia katika shamba la Mwakinyumbi na kufanya maendelezo kwa kuwa tayari wamefanya uwekezaji mkubwa. " Pasiwe na utaratibu wa kuwaondoa wananchi wa Mwakinyumbi walifanya maendelezo na badala yake warasimishiwe maeneo yao kwa utaratibu ili waendelee kuishi". Amesema Mhe Mzava Mkuu wa wilaya ya Korogwe kwa upande wake amesema kila mtu ahakikishe anajaza fomu kulingana na maelekezo wasifanye magumashi ili kila mtu apate haki yake. Eneo la mradi lilikuwa likimilikiwa na Kampuni ya M/S Mwakinyumbi iliyopewa ardhi hiyo mwaka 1989 kwa ajili ya uwekezaji katika kilimo cha mkonge. Hata hivyo, kampuni hiyo ilishindwa kutekeleza masharti ya umilikishwaji, ikiwemo kuliendeleza eneo hilo, hali iliyosababisha milki hiyo kubatilishwa mwaka 2023 na ardhi kurejea serikalini. Katika hatua nyingine , Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo amewaonya wananchi dhidi ya kuendelea kuuza au kununua ardhi kiholela katika eneo la Shamba la Mwakinyumbi wakati zoezi la upangaji na upimaji likiendelea. Dkt Akwilapo amewataka wananchi wa eneo hilo kutoendeleza uvamizi wa ardhi au kufanya mauziano yasiyo rasmi, huku akianisha kuwa serikali tayari imeanza kuchukua hatua za kisheria dhidi ya baadhi ya watu wanaodaiwa kuuza ardhi kwa njia za ulaghai. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo akizungumza na wananchi wa Mwakinyumbi wilayani Korogwe wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Kupanga, Kupima na Kumilikisha Ardhi katika eneo la shamba la Mwakinyumbi lililopo kata ya Hale Sept 21, 2026 mkoani Tanga Sehemu ya wananchi wa eneo la Mwakinyumbi katika kata ya Hale wilayani Korogwe wakimsikiliza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo alipokwenda kuzindua mpango wa kupanga, kupima na kumilikisha ardhi katika eneo hilo Sept 21, 2026. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini Mhe. Timotheo Mzava wakati wa uzinduzi wa mpango wa Kupanga, Kupima na Kumilikisha ardhi katika eneo la shamba la Mwakinyumbi lililopo kata ya Hale Sept 21, 2026 mkoani Tanga. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo akifurahia jambo na Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini Mhe. Timotheo Mzava wakati wa uzinduzi wa mpango wa Kupanga, Kupima na Kumilikisha ardhi katika eneo la shamba la Mwakinyumbi lililopo kata ya Hale Sept 21, 2026 mkoani Tanga. Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo akipeana mikono na wananchi wa Mwakinyumbi waliofurahishwa na uamuzi wa serikali wa kupanga, kupima na kumilikisha ardhi eneo la shamba la Mwakinyumbi wakati wa uzinduzi wa mpango huo Sept 21, 2026 mkoani Tanga. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)
Wed, 23 Sep 2026 09:49:42 +0000Minerais : des milliers de tonnes exportées mais, où sont les recettes ?
Depuis bientôt une année, le gouvernement burundais multiplie les convois d’exportation de minerais. Lancée en octobre 2025, cette campagne a déjà permis l’exportation de plusieurs milliers de tonnes de minerais. Le dernier convoi, organisé le 7 septembre 2026, a transporté 516 tonnes. Si l’envoi de ces convois est largement médiatisé, le rapatriement des devises générées par ces exportations reste, lui, entouré d’un silence radio. La société civile dénonce une situation qui dépasse l'entendement
Sun, 20 Sep 2026 09:34:23 +0000Coupures du courant électrique, les médias privés en veille
Manque de carburant, coupures intempestives du courant électrique, … ces dernières semaines, les médias burundais surtout privés sont très affectés. Involontairement, ils sont obligés d’interrompre des émissions, des débats, … et passer des jours sans informer. Les conséquences sont fâcheuses.
Mon, 21 Sep 2026 08:48:46 +00001xBet et FC Barcelone féminin : l’équipe qui a fait de la victoire une tradition
Le 30 août, le FC Barcelone féminin a lancé une nouvelle saison de Liga F avec un objectif aussi simple à formuler que difficile à atteindre : décrocher un huitième titre de champion consécutif. Le club reste sur sept sacres d’affilée en Espagne, compte déjà quatre Ligues des champions féminines à son palmarès et vient […]
Mon, 21 Sep 2026 10:29:41 +0000Uhuru, 22 septembre : le vol des Hirondeaux face à l’orage tanzanien
Le verdict est tombé au terme d'une démonstration implacable. En infligeant à l'Éthiopie une correction sans appel, quatre buts à zéro, la Tanzanie a validé son billet et connaît déjà son adversaire en demi-finale de la CECAFA U20 . Ce sera le Burundi.
Mon, 21 Sep 2026 18:03:34 +0000Le championnat s’est écrit en lettres de feu
Il est des journées qui ne se comptent pas, elles se contemplent. La quatrième levée de la Primus Ligue fut de celles-là : fiévreuse, lyrique, impitoyable, où chaque stade fut un théâtre et chaque but une strophe.
Mon, 21 Sep 2026 18:08:00 +0000Journée 4 de la Primus Ligue Nationale A 2026-2027 : La hiérarchie s’ébauche, le vertige commence
Au terme de la quatrième journée, la Primus Ligue possède un maître, provisoire certes, mais éclatant. Vision FC . Quatre rencontres, trois victoires, un nul, aucune défaite. Dix points au compteur et une différence de buts de +6. Le leader ne s'est pas contenté de gagner, il a conquis. Sa démonstration face à Young Star, cinq buts à un, fut moins un match qu'une profession de foi.
Mon, 21 Sep 2026 18:12:09 +0000Entreprises publiques : Les gestionnaires défaillants dans le viseur du président de l’Assemblée nationale
Daniel Gélase Ndabirabe se dit préoccupé par la mauvaise gestion des entreprises publiques qui cause un manque à gagner à l’Etat. Pour Léonce Ngendakumana, ex-président de ladite institution, le député Ndabirabe ne devrait pas se lamenter mais plutôt exercer le contrôle de l’action gouvernementale et, le cas échéant, prendre des sanctions.
Tue, 22 Sep 2026 05:51:23 +0000Le sentiment anti-étrangers au Kenya bouleverse des vies
La fermeté affichée par les autorités de la première économie de l’EAC envers les étrangers exerçant de petits métiers a laissé un goût amer à ceux qui avaient choisi d’y construire une nouvelle vie. Pour plusieurs ressortissants burundais, les nouvelles mesures ont entraîné des pertes économiques et précipité leur retour au pays. La société civile burundaise tire la sonnette d’alarme.
Tue, 22 Sep 2026 09:04:43 +0000À des milliers de lieues du nid, une Hirondelle a chanté : Nduwarugira fait parler de lui
Le décor planté ce dimanche 20 septembre 2026 à l'Indomilk Arena de Tangerang, 32 degrés sous un ciel laiteux, une humidité à couper au couteau. Le PSS Sleman , le club d'adoption de Christophe Nduwarugira , s'enlisait. Deux buts encaissés face au Dewa United. Zéro point après trois journées. Une 17ème place sur 18, synonyme de lanterne rouge. Le navire prenait l'eau de toute part, et le spectre d'une saison en enfer se dessinait déjà.
Tue, 22 Sep 2026 16:51:20 +0000Du dégoût de la vie au suicide
Des cas de suicide sont légion et emportent annuellement des milliers de vies humaines à travers le monde. Le Burundi n’est pas épargné. Athanase Ngendakuriyo, psychoclinicien et expert en santé mentale, indique que de nombreuses causes sont à l’origine de la décision pour une personne de passer à un acte de suicide.
Wed, 23 Sep 2026 05:34:23 +0000Ndindi Nyoro begins nationwide political mobilisation ahead of 2027
Kiharu MP Ndindi Nyoro has said he will take his campaign for national transformation across Kenya as he positions himself for the 2027 presidential race.
Sun, 23 Aug 2026 17:22:30 +0300Relief for schools as government releases Sh18.5b capitation
Government releases Sh18.5b capitation, primary education to get Sh1.4b, Junior Schools Sh6.1b and Senior Schools Sh10.9b, Education CS Ogamba says.
Mon, 24 Aug 2026 16:54:03 +0300Gachagua to Duale: You don't own pastoralists
DCP Leader Rigathi Gachagua has accused Health Cabinet Secretary Aden Duale of allegedly doing nothing for pastoralist communities in the country.
Tue, 25 Aug 2026 17:51:24 +0300Ruto hands Sh2.6bn to Mau Forest evictees
Each beneficiary received Sh200,000 through M-Pesa to help them resettle.
Wed, 26 Aug 2026 18:28:11 +0300Page 1116 of 1118 · 22347 stories