Unganishwa

Search the region

22602 stories

National · Issa Michuzi

SERIKALI YAWEKA MKAKATI KUTOKOMEZA UKIMWI IFIKAPO MWAKA 2030

Na Said Mwishehe,Michuzi TV SERIKALI imesema dhamira yake ni kutokomeza UKIMWI kama tishio la afya ya umma ifikapo mwaka 2030, huku ikiwataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kuadhimisha Siku ya UKIMWI Duniani. Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Profesq Palamagamba Kabudi, amesema kilele cha maadhimisho kitafanyika Desemba 1, 2026 katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Convention Centre, Dodoma. Mgeni Rasmi atakuwa Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba. “Maadhimisho ya mwaka huu yataenda sambamba na jubilee ya miaka 25 ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), iliyoanzishwa mwaka 2001. Sherehe za kitaifa zitaanza Novemba 29 Dodoma, zikiwa na maonesho ya wadau, huduma za afya na elimu.” Amesema kuanzia Novemba 24 hadi Desemba 1, shughuli pia zitafanyika katika kanda saba za TACAIDS: Mashariki, Kati, Ziwa, Kusini, Nyanda za Juu Kusini, Magharibi na Kaskazini. Mawaziri na naibu mawaziri watashiriki, na mikoa yote itaadhimisha siku hiyo. Kauli mbiu ya mwaka huu ni "Huduma Bora za Afya ni Msingi wa Kutokomeza UKIMWI, Tuendelee Kuimarisha Upatikanaji". Pia amesema hadi Desemba 2025, asilimia 92.7 ya watu wanaoishi na VVU walikuwa wamepima na kujua hali zao, asilimia 99.5 ya wanaojua hali zao walikuwa wakipata ARV, na asilimia 98.2 ya walio kwenye dawa walikuwa wamefubaza VVU. “Kati ya mwaka 2010 na 2025, maambukizi mapya yalishuka kutoka watu 98,754 hadi 33,511, na vifo vitokanavyo na UKIMWI kutoka 55,833 hadi 25,995. Maambukizi ya mama kwenda kwa mtoto yalipungua kutoka asilimia 9.1 hadi 6.2,”amesema Prof.Kabudi. Akifafanua amesema vijana wa miaka 15 hadi 24 wanachangia asilimia 33.3 ya maambukizi mapya, na asilimia 77.7 yao ni vijana wa kike. Aliwataka vijana kujikinga na kujua hali zao. Amesema Serikali itaimarisha uwekezaji wa rasilimali za ndani na kushirikisha sekta binafsi, ili mabadiliko ya ufadhili wa kimataifa yasiathiri huduma za kinga, upimaji na matibabu. Pia ametoa rai kwa wananchi wasimnyanyapae mtu anayeishi na VVU. "Ushindi dhidi ya UKIMWI unawezekana ikiwa tutafanya kazi kwa pamoja," amesema.

Thu, 19 Nov 2026 17:24:27 +0000
Uncategorized · Radio Publique Africaine

Isare : des habitants de Gashingano réclament l’indemnisation de terres occupées par un camp militaire

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · KBC

Ruto: Opposition preparing to blame IEBC for 2027 election loss

The opposition is preparing to blame the Independent Electoral and Boundaries Commission (IEBC) for losing the 2027 General Election, President William Ruto has said. The President pointed out that they…

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

Four arrested over attack on Natembeya's aide

The attack happened on the night of November 16, 2026, at Orombe Farm in Trans Nzoia East Sub-County.

Recently
Business · Issa Michuzi

𝐌𝐀𝐊𝐀𝐌𝐔 𝐖𝐀 𝐑𝐀𝐈𝐒 𝐀𝐖𝐀𝐓𝐀𝐊𝐀 𝐖𝐀𝐂𝐇𝐈𝐌𝐁𝐀𝐉𝐈 𝐖𝐀 𝐌𝐀𝐃𝐈𝐍𝐈 𝐊𝐔𝐅𝐔𝐀𝐓𝐀 𝐌𝐀𝐒𝐇𝐀𝐑𝐓𝐈 𝐘𝐀 𝐋𝐄𝐒𝐄𝐍𝐈

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi ,amewaagiza wenye leseni za uchimbaji madini kuzifanyia kazi kwa mujibu wa masharti yake, akionya kuwa Serikali itachukua hatua iwapo masharti hayo hayatatekelezwa. Makamu wa Rais ametoa onyo hilo, wakati alipomwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa Madini na Uwekezaji Tanzania (TMIC 2026), unaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam. Katika hotuba yake, Makamu wa Rais amesema Serikali itaendelea kusimamia katazo la kusafirisha madini ghafi nje ya nchi. Amezitaka kampuni za ndani na nje kuwekeza katika viwanda vitakavyochakata madini hapa nchini hadi hatua ya bidhaa za mwisho. Amesema uwekezaji huo utapanua fursa za ajira, utatoa malighafi kwa viwanda na kuongeza mapato ya Taifa. Mkutano huo unawakutanisha zaidi ya wadau 1,700 kutoka ndani na nje ya nchi kujadili namna ya kuongeza uchakataji wa madini nchini ili kukuza viwanda, kuongeza ajira na mapato ya Taifa. Wizara ya Madini imeandaa mkutano huo kwa kushirikiana na Chemba ya Migodi Tanzania.Majadiliano yanahusu fursa za uwekezaji katika dhahabu, kinywe, nikeli, shaba, madini adimu na niobiamu, pamoja na namna ya kuongeza ushiriki wa wachimbaji wadogo na kampuni za Kitanzania katika mnyororo wa thamani wa madini.

Thu, 19 Nov 2026 17:19:33 +0000
Uncategorized · Daily News

Tanzania strikes gold in Barrick-Twiga partnership

DAR ES SALAAM: TANZANIA has struck gold in Barrick-Twiga mining partnership, the ongoing Tanzania Mining and Investment Conference held in…

Recently
Uncategorized · Daily News

Ebola, El Niño risks put Tanzania’s health preparedness in focus

DODOMA:THE government has been urged to strengthen environmental health services, particularly at border points, to protect the country against Ebola…

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

Khalwale to Opposition: Pick flagbearer based on popularity

Khalwale said the opposition was entering a critical stage in the process of identifying a single candidate to represent it in the next presidential election.

Recently
Uncategorized · The Standard

UDA threatens to boycott IEBC meetings over alleged harassment of delegates

The United Democratic Alliance (UDA) has threatened to boycott future consultative meetings convened by the Independent Electoral and Boundaries Commission (IEBC).

Thu, 19 Nov 2026 19:16:11 +0300
Uncategorized · KBC

Four arrested over attack on Natembeya’s aide

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

UN court: Myanmar committed genocide against Rohingya

The ruling marks a major legal victory for the Rohingya, thousands of whom fled a brutal military crackdown in 2017

Recently
Uncategorized · The Standard

IEBC warns court battles could derail 2027 election preparations

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

WATCH LIVE: IEBC Engagement Meeting with Political Party Leaders

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

8 Kenyan students to travel to China for Huawei tech programme

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Daily News

OTR briefs IMF on reforms, performance of public enterprises

DAR ES SALAAM: THE Office of the Treasury Registrar (OTR) has briefed an International Monetary Fund (IMF) delegation on reforms…

Recently
Uncategorized · Daily News

Govt steps up drive to ensure every household has a toilet

DODOMA: THE government has stepped up efforts to eliminate households without toilets, with new figures showing that only one per…

Recently
Uncategorized · Issa Michuzi

RAIS SAMIA AHIMIZA UZALISHAJI WA PAMOJA AFRIKA MASHARIKI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan,akivuta kitambaa pamoja na Mhe. Yoweri Kaguta Museveni, Rais wa Jamhuri ya Uganda, kama ishara ya uzinduzi Kiwanda cha Kuunganisha Magari cha Double Q Automotive Assembly Plant kilichopo Mpigi nchini Uganda, tarehe 19 Novemba, 2026. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan,pamoja na Mhe. Yoweri Kaguta Museveni, Rais wa Jamhuri ya Uganda, wakitembelea Kiwanda cha Double Q Automotive Assembly Plant kilichopo Mpigi nchini Uganda, tarehe 19 Novemba, 2026. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan,akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni, baada ya kuwasili katika eneo la Kiwanda cha Kuunganisha Magari cha Double Q Automotive Assembly Plant kilichopo Mpigi nchini Uganda, Novemba 19, 2026. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Mhe. Yoweri Kaguta Museveni, Rais wa Jamhuri ya Uganda, baada ya kuwasili katika eneo la Kiwanda cha Kuunganisha Magari cha Double Q Automotive Assembly Plant kilichopo Mpigi nchini Uganda, tarehe 19 Novemba, 2026. Mhe. Rais Dkt. Samia pamoja na Mwenyeji wake Mhe. Yoweri Kaguta Museveni, Rais wa Jamhuri ya Uganda, wazindua Kiwanda cha Kuunganisha Magari cha Double Q Automotive Assembly Plant, Mpigi nchini Uganda Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na Mhe. Yoweri Kaguta Museveni, Rais wa Jamhuri ya Uganda, wakitembelea Kiwanda cha Double Q Automotive Assembly Plant Mpigi nchini Uganda Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveni, Rais wa Jamhuri ya Uganda, akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa Kiwanda cha Kuunganisha Magari cha Double Q Automotive Assembly Plant kilichopo Mpigi nchini Uganda, tarehe 19 Novemba, 2026. Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa Kiwanda cha Kuunganisha Magari cha Double Q Automotive Assembly Plant kilichopo Mpigi nchini Uganda, tarehe 19 Novemba, 2026. Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye hafla ya uzinduzi wa Kiwanda cha Kuunganisha Magari cha Double Q Automotive Assembly Plant kilichopo Mpigi nchini Uganda, tarehe 19 Novemba, 202 Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiagana na mwenyeji wake Mhe. Yoweri Kaguta Museveni, Rais wa Jamhuri ya Uganda, baada ya kuhitimisha Ziara yake ya Kitaifa ya siku mbili, Kampala nchini Uganda, tarehe 19 Novemba, 2026. Matukio mbalimbali katika uzinduzi wa Kiwanda cha Kuunganisha Magari cha Double Q Automotive Assembly Plant kilichopo Mpigi nchini Uganda, tarehe 19 Novemba, 2026.

Thu, 19 Nov 2026 16:46:58 +0000
Uncategorized · Business Daily

Equity Group CEO on dividends, growth amid cyber threats and rising profits

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · UN News Burundi

COP31 deadlock persists as countries launch new ‘climate reality check’

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · SoftPower News

Musasizi Urges Accountants to Embrace AI and Strengthen Digital Skills

Read the full report from the original source.

Recently

Page 119 of 1131 · 22602 stories