Unganishwa

Search the region

22625 stories

Uncategorized · Issa Michuzi

MKUYU AFRICA YAZINDUA MILIKI YOUTH CLUB KUWEZESHA VIJANA KUMILIKI MALI

Kampuni ya MKUYU Africa imezindua jukwaa la Miliki Youth Club kwa lengo la kuwawezesha vijana kupata elimu ya uwekezaji, usimamizi wa fedha na umiliki wa mali, ili kuwajengea uwezo wa kujitegemea kiuchumi badala ya kutegemea ajira rasmi pekee. Jukwaa hilo limekusudiwa kuwakutanisha vijana kutoka vyuoni na maeneo mbalimbali ya kazi kwa ajili ya kubadilishana uzoefu, kujifunza fursa za kiuchumi na kujenga uelewa kuhusu namna ya kutumia rasilimali walizonazo kuanzisha shughuli za uzalishaji mali. Miongoni mwa mada zilizojadiliwa katika jukwaa hilo ni namna vijana wanavyoweza kumiliki mali zisizohamishika, kufanya uwekezaji wa muda mrefu na kujenga utajiri kupitia fursa mbalimbali za biashara na uwekezaji. Akizungumza katika jukwaa hilo, Mkurugenzi wa MKUYU Africa, Juneid Othman, aliwahimiza vijana kubadili mtazamo kuhusu mafanikio ya kiuchumi kwa kuanza kufikiria zaidi kuhusu umiliki wa mali na uwekezaji wa muda mrefu. Alisema vijana wanapaswa kuanza kujenga msingi wa kifedha mapema, hata wanapokuwa bado vyuoni au katika hatua za mwanzo za maisha yao ya kazi, badala ya kusubiri kupata ajira rasmi ndipo waanze kufikiria uwekezaji. Juneid alieleza kuwa safari yake ya ujasiriamali ilianza akiwa na umri wa miaka 19, wakati akisomea uhasibu, ambapo alianza biashara ya nishati ya jua kwa mtaji wa Sh milioni tatu. Alisema biashara hiyo ilikua na kupanuka hadi kufikia masoko ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Zambia, kabla ya baadaye kuingia katika sekta ya ujenzi na uwekezaji wa mali isiyohamishika. Kwa sasa, kupitia uwekezaji wake katika sekta hiyo, Juneid anamiliki mali isiyohamishika zenye thamani inayokadiriwa kufikia zaidi ya Dola za Marekani milioni 30, zikihusisha miradi zaidi ya 10 ya majengo jijini Dar es Salaam. Kwa upande wake, Dkt. Beatrice Ndung’u, mtaalamu wa biashara, chapa na masoko, alisema kuanzishwa kwa Miliki Youth Club kunalenga kuwapa vijana maarifa na ujuzi utakaowawezesha kufanya maamuzi sahihi ya kifedha na kutumia fursa zilizopo kujenga ustawi wao wa kiuchumi. Alisema jukwaa hilo litakuwa sehemu ya kuwajengea vijana uwezo katika masuala ya uwekezaji, usimamizi wa fedha na mbinu mbalimbali za kujenga utajiri kupitia umiliki wa mali. Uzinduzi wa Miliki Youth Club unakuja wakati vijana wengi wanakabiliwa na changamoto mbalimbali za kiuchumi, zikiwemo ukosefu wa ajira, kipato kisicho na uhakika na uelewa mdogo kuhusu matumizi bora ya rasilimali katika kujenga maisha endelevu ya kifedha. Kupitia jukwaa hilo, vijana wanatarajiwa kupata fursa ya kujifunza namna ya kupanga matumizi ya fedha, kuweka akiba, kufanya maamuzi sahihi ya kifedha na kutambua fursa za uwekezaji zinazoweza kuwasaidia kujenga mali na kuongeza kipato kwa muda mrefu. Aidha, jukwaa hilo linatarajiwa kuwa kiunganishi cha vijana na wataalamu wa biashara na uwekezaji, pamoja na kutoa nafasi ya kujenga mitandao ya kibiashara, kubadilishana uzoefu na kupata maarifa yatakayowasaidia kuanzisha na kukuza shughuli zao za kiuchumi. Mkurugenz wa mkuyu Juneid Othman (wa pili kulia)akiwa katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa MILIKI YOUTH CLUB jijini Dar es salaam Juneid akifurah na wadau wa MILIKI YOUTH CLUB

Thu, 19 Nov 2026 10:00:00 +0000
Uncategorized · Daily News

Here comes AFCON 2027 logo reflecting East African heritage, unity

DAR ES SALAAM: THE official logo for the 2027 Africa Cup of Nations (AFCON 2027) has been unveiled, featuring a…

Recently
Uncategorized · Daily News

Dr Samia, Museveni jointly launch the Double Q Automotive Plant in  Uganda

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Mwanaspoti

Namna mpira wa mikono unavyokua Zanzibar

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Mwanaspoti

Bado sijamuelewa Gamondi kwa Nado

MIGUEL Gamondi ametuchanganya sana katika mechi mbili zilizopita za Taifa Stars ambazo ilicheza dhidi ya Nigeria.

Recently
Uncategorized · Mwanaspoti

Tunamuachaje Samatta

Soma zaidi hapa

Recently
Sports · Mwanaspoti

Kibamba amenyooka wagombea Simba SC mjipange

KIOMONI Kibamba ametokea kupata mashabiki wengi hapa kijiweni kutokana na namna anavyotimiza majukumu yake kwa weledi.

Recently
Sports · Mwanaspoti

FA yamkomalia Infantino

Read the full report from the original source.

Recently
Sports · Mwanaspoti

Pochettino atua Old Trafford kwa kishindo

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Daily News

Africa records 71.4bn instant payment transactions worth 1.8tri US dollars

MAURITIUS: AFRICA has recorded 71.4 billion instant payment transactions valued at 1.8tri US dollars in 2025, nearly three times the…

Recently
Uncategorized · IWACU English News

Droits de l’enfant : L’exploitation des mineurs reste préoccupante au Burundi

Alors que le Burundi se joint au reste du monde pour célébrer, le 20 novembre, la Journée internationale des droits de l’enfant, ces droits restent bafoués dans plusieurs milieux. Les défenseurs des droits de l’enfant tirent la sonnette d’alarme et appellent le gouvernement à renforcer les mesures de protection.

Thu, 19 Nov 2026 13:11:09 +0000
Uncategorized · DW Rwanda

APEC summit: Trump, Xi, Putin talks end with 'peace declaration'

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

Dissecting Ruto's 2026 address vs 2022 manifesto

Four years after unveiling The Plan, Ruto cited progress in agriculture, housing, healthcare and jobs, but several specific targets remain unaccounted for.

Recently
Uncategorized · Daily News

IST calls on experts to adopt modern technology in resolving land disputes

MWANZA: THE Deputy Minister for Lands, Housing and Human Settlements Development, Mr Kaspar Mmuya, has urged land sector experts to…

Recently
Uncategorized · DW Rwanda

Myanmar committed genocide against Rohingya, top UN court rules

Read the full report from the original source.

Recently
Sports · Azam TV Videos

Simba TV | Maisha ya Nathaniel Chilambo nje ya soka, akiwa nyumbani anafanya nini?

Azam TV

2026-11-19T12:37:16+00:00
Sports · Azam TV Videos

ZILIZOBAMBA MITANDAONI | Ceasiaa Queens wawachokoza Simba Queens

Baada ya kunyakua alama moja mbele ya Simba Queens, Ceasiaa Queens hawapoi kwenye ukurasa wao.

2026-11-19T12:48:10+00:00
Uncategorized · Business Daily

Stanchart profit up 7pc to Sh10.5bn on lower costs

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Daily News

Dr Abbasi chairs preparatory meeting for WTA ceremony in Serengeti

DAR ES SALAAM: THE Permanent Secretary in the Ministry of Natural Resources and Tourism, Dr Hassan Abbasi, has chaired a…

Recently
Uncategorized · Rwanda News Agency

Maroc/ accélération du développement de l’industrie nationale de défense et de sécurité/ séance de travail présidée par Sa Majesté le Roi Mohammed VI

Read the full report from the original source.

Recently

Page 125 of 1132 · 22625 stories