Search the region
22629 stories
MAAFISA VIUNGO TAASISI ZA MUUNGANO WATAKIWA KUHUDUMIA WANANCHI KWA UKARIBU
Maafisa Viungo wa Taasisi za Muungano wametakiwa kuhudumia wananchi kwa karibu zaidi kupitia hatua itakayoimarisha Muungano wetu hivyo kupunguza malalamiko na changamoto zinazowakabili wananchi. Wito huo umetolewa na Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Maduhu Kazi wakati wa ufunguzi wa kikao na maafisa viungo wa taasisi za Muungano kilichofanyika jijini Dodoma leo Novemba 19, 2026. Akifungua kikao hicho kwa niaba ya Dkt. Maduhu, Mkurugenzi wa Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Juma Mohamed Salum alisema wananchi wana matarajio makubwa kutoka kwa Serikali zote mbili ili waweze kunufaika na matunda ya Muungano. Alisema kuwa kikao hicho kina lengo la kuwa na uelewa wa pamoja wa utekelezaji wa mambo ya Muungano na kuimarisha utekelezaji wa majukumu ya Taasisi za Muungano ikiwa ni pamoja na kuhakikisha taarifa za utekelezaji zinaandaliwa na kuwasilishwa kwa wakati. “Kama mnavyofahamu, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 nyongeza ya kwanza imeorodhesha maeneo 22 ya Muungano ambayo yanasimiwa na Taasisi za Muungano, hivyo Taasisi za Muungano ziana umuhimu mkubwa katika kuimarisha na kuendeleza Muungano kwa kuhakikisha ziantekeleza majukumu yake kwa weledi na kuhakikisha huduma zinatolewa pande zote mbili za Muungano,“ alisisitiza. Aidha, Dkt. Juma alieleza kuwa kikao hicho kimefanyika katika wakati muhimu ambapo Serikali inaendelea kusisitiza uwajibikaji, ufanisi na matokeo chanya katika utekelezaji wa majukumu ya kila Taasisi. Alisema Taasisi za Muungano zina wajibu mkubwa wa kutekeleza majukumu yaliyoainishwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Sheria zilizopo, hivyo alisisitiza ni jukumu la afisa kiungo wa taasisi kuhakikisha kuwa majukumu yanatekelezwa ili kuimarisha na kudumisha Muungano kwa kuzingatia misingi ya Muungano na maslahi mapana ya Taifa. Halikadhalika, Dkt. Juma alisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa karibu kati ya Ofisi ya Makamu wa Rais na Maafisa Viungo wa Taasisi zote za Muungano kwani ni nguzo muhimu katika kuhakikisha masuala ya Muungano yanashughulikiwa kwa wakati, weledi na kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo iliyopo. Hivyo, alisisitiza kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais itaendelea kutoa mwelekeo, uratibu na usimamizi unaohitajika ili Taasisi za Muungano ziweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.
Thu, 19 Nov 2026 11:57:39 +0000How dfcu Bank Is Enabling Customers Get More Value from Everyday Spending This Festive Season
Read the full report from the original source.
RecentlyCourt blocks publication of judges performances
Petitioner claims that publishing the figures in the proposed manner risked creating a misleading public impression about judges and judicial officers
RecentlyBenki ya Absa Tanzania yaongeza kiwango cha mikopo ya watumishi wa umma na kuongeza muda wa marejesho
Benki ya Absa Tanzania leo imetangaza maboresho ya huduma yake ya mikopo kwa watumishi wa umma, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuwapatia watumishi hao unafuu zaidi wa kifedha, urahisi wa kupata huduma na upatikanaji wa mikopo kwa haraka zaidi. Kupitia maboresho hayo, watumishi wa umma wanaokidhi vigezo sasa wataweza kupata mikopo ya hadi shilingi milioni 300, kutoka milioni 200 za awali, huku muda wa marejesho ukiongezwa kutoka miaka 10 hadi miaka 13. Aidha, Benki imeunganisha mfumo wake wa maombi ya mikopo na mfumo wa Serikali wa Employee Self-Service (ESS), hatua inayowawezesha watumishi wa umma kuwasilisha maombi ya mikopo kwa urahisi zaidi na, kwa kuzingatia vigezo na idhini ya mkopo, kupata fedha ndani ya dakika tano pekee. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo iliyoboreshwa, Mkurugenzi wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Ndabu Swere, alisema maboresho hayo yanaakisi dhamira ya Benki ya kukidhi mahitaji ya kifedha ya watumishi wa umma yanayoendelea kubadilika. “Tunatambua kuwa wateja wetu wana malengo mbalimbali ya kifedha, yakiwemo kuwekeza katika biashara, kujenga nyumba, kusaidia familia zao na kugharamia elimu ya watoto wao. Kwa kuongeza kiwango cha juu cha mkopo hadi shilingi milioni 300, kuongeza muda wa marejesho hadi miaka 13 na kurahisisha upatikanaji wa mikopo kupitia mfumo wa ESS, tunawapatia watumishi wa umma unyumbufu na urahisi zaidi wa kifedha ili waweze kutimiza mambo yenye umuhimu mkubwa katika maisha yao,” alisema Swere. Aliongeza kuwa kampeni hiyo imekuja wakati muafaka ambapo Watanzania wanajiandaa na mahitaji ya msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka pamoja na kuanza kwa mwaka mpya wa masomo. Hivyo, aliwahimiza wateja waliopo na wale wanaotarajia kujiunga na Absa kutumia fursa hiyo kunufaika na maboresho hayo ya mikopo. Kwa upande wake, Meneja wa Masoko na Mawasiliano wa Absa Bank Tanzania, Bw. Beda Biswalo, akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano ya Umma wa benki hiyo, alisema kampeni hiyo inaimarisha dhamira ya Benki ya kuwawezesha wateja wake kufikia malengo na matarajio yao. “Katika Absa, tunaamini kuwa nyuma ya kila lengo la kifedha kuna simulizi binafsi yenye thamani inayostahili kuungwa mkono. Iwe ni mzazi anayewekeza katika elimu ya watoto wake au mtumishi wa umma anayejitahidi kutimiza ndoto yake ya muda mrefu, tunathamini malengo hayo. Huduma hii mpya iliyoboreshwa inadhihirisha ahadi ya chapa yetu isemayo ‘Stori yako Ina Thamani’, sambamba na kuendeleza dhamira yetu ya ‘Kuiwezesha Afrika ya Kesho Pamoja, Hatua Moja baada ya Nyingine.’ Tumejizatiti kufanya huduma za kifedha zipatikane kwa urahisi zaidi ili kuwawezesha Watanzania wengi zaidi kubadili ndoto na matarajio yao kuwa uhalisia,” alisema Biswalo. Kupitia kampeni hiyo ya uhamasishaji, Absa Bank Tanzania inawahimiza watumishi wa umma kote nchini kuingia katika mfumo wa Serikali wa ESS, kuchagua Absa Bank Tanzania kama benki wanayoipendelea kwa ajili ya kupata mikopo na kuwasilisha maombi yao ya mkopo. Watumishi wa umma ambao bado hawajawa wateja wa Absa pia wamealikwa kutumia fursa hiyo, kufahamu zaidi huduma zinazotolewa na Benki hiyo na kujiunga nayo ili kunufaika na huduma hiyo iliyoboreshwa. Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Ndabu Swere (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa Uzinduzi wa Maboresha ya Mikopo ya Watumishi wa Umma. Kupitia maboresho hayo, viwango vya mikopo vimepanda kutoka shs milioni 200 hadi milioni 300 na mud awa marejesho umeongezeka kutoka miaka 10 hadi 13. Kulia ni Mkuu wa Mikakati na Bidhaa za Wateja Binafsi wa benki hiyo, Bw. Heristraton Genesis. Mkuu wa Mikakati na Bidhaa za Wateja Binafsi wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Heristraton Genesis (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa Uzinduzi wa Maboresha ya Mikopo ya Watumishi wa Umma. Kupitia maboresho hayo, viwango vya mikopo vimepanda kutoka shs milioni 200 hadi milioni 300 na mud awa marejesho umeongezeka kutoka miaka 10 hadi 13. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa benki hiyo, Bi. Ndabu Swere na wafanyakazi wengine wa Absa. Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Ndabu Swere (waliokaa wa pili kushoto) na Mkuu wa Mikakati na Bidhaa za Wateja Binafsi wa benki hiyo, Bw. Heristraton Genesis (Katikati) wakipiga picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo jijini leo baada ya Uzinduzi wa Maboresha ya Mikopo ya Watumishi wa Umma, jijini Dar es Salaam leo.
Thu, 19 Nov 2026 07:30:00 +0000WALEMAVU IRINGA WAIPONGEZA BoT KWA ELIMU YA FEDHA, WATAKA IFIKIE WENGI ZAIDI
Na Farida Mangube Walemavu mkoani Iringa wameipongeza Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa kuwafikia na kutoa elimu ya fedha, ikiwemo utunzaji sahihi wa fedha na namna ya kutambua alama za usalama zilizopo kwenye noti, huku wakitaka elimu hiyo iwafikie walemavu wengi zaidi, hususan wanaoishi maeneo ya vijijini. Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) Mkoa wa Iringa, Bw. Shabani Shomari, leo Alhamisi, Novemba 19, 2026, wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na BoT mkoani humo. Akizungumza katika mafunzo hayo, Bw. Shomari amesema elimu ya fedha ni muhimu kwa watu wenye ulemavu kwa kuwa inawawezesha kufanya maamuzi sahihi ya kifedha na kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi. “Tunaishukuru BoT kwa kutupatia nafasi hii ya kupata elimu ambayo walemavu wanastahili kuipata, hasa katika kipindi ambacho nchi inaelekea kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050. Hata hivyo, tunatamani elimu hii iwafikie walemavu wengi zaidi, hasa wale wanaoishi vijijini,” alisema Bw. Shomari. Awali, akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, Afisa Ustawi wa Jamii wa Mkoa huo, Bw. Ashery Mndalila, aliwataka washiriki kutumia elimu waliyoipata kuwa mabalozi wazuri katika jamii kwa kuhamasisha utunzaji bora wa fedha, matumizi sahihi ya mikopo na utambuzi wa alama za usalama kwenye noti. Kwa upande wake, Afisa wa Benki Kuu, Bw. Sadi Makomba, amesema BoT itaendelea kutoa elimu hiyo katika maeneo mbalimbali nchini ili kuhakikisha watu wenye ulemavu wanapata uelewa wa kutosha kuhusu masuala ya fedha na uchumi. Benki Kuu ya Tanzania inaendelea kutekeleza programu za elimu ya fedha na uchumi kwa makundi mbalimbali ya jamii, ikiwemo watu wenye ulemavu, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kufanikisha azma ya ujumuishi wa huduma za fedha kwa asilimia 100.
Thu, 19 Nov 2026 11:41:18 +0000ICJ: Myanmar committed genocide against Rohingya
Read the full report from the original source.
RecentlySEQUIP YAMPA ROSE NAFASI YA PILI YA ELIMU, NJOMBE HADI MOROGORO
NA FARIDA MANGUBE MOROGORO Serikali kupitia Mradi wa Kuimarisha Ubora wa Elimu ya Sekondari (SEQUIP) imemrejeshea matumaini ya elimu Rose Mlata (16), mkazi wa Njombe, aliyelazimika kufanya kazi za ndani baada ya kukosa msaada wa kuendelea na masomo. Kupitia elimu nje ya mfumo rasmi, Rose amehitimu kidato cha nne mwaka 2026 mkoani Morogoro na sasa ana ndoto ya kuwa mwanasheria. Safari ya elimu ya Rose ilikwama baada ya wazazi wake kutengana, hali iliyomkosesha msaada wa kujiunga na kidato cha kwanza. Wakati wenzake wakiendelea na masomo, yeye alielekea Morogoro kutafuta kazi za ndani ili kujikimu, huku matumaini ya kutimiza ndoto zake yakianza kufifia. Maisha yake yalichukua mwelekeo mpya alipopata kazi nyumbani kwa Stephano Nyonyo, Mwalimu Mkuu Mstaafu wa Shule ya Msingi Mwande, mkoani Morogoro. Baada ya kutambua hamu yake ya kusoma, Nyonyo alimsaidia kujiunga na Kituo cha Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Wamo mwaka 2022, ambako alipata fursa ya kuendelea na elimu kupitia Mradi wa SEQUIP. Nyonyo hakumtafutia nafasi ya masomo pekee, bali alimlea kama sehemu ya familia yake na kuhakikisha anapata mahitaji muhimu hadi alipohitimu kidato cha nne. Anamwelezea Rose kuwa mtoto mwenye bidii, upendo na nidhamu, sifa zilizoimarisha uhusiano wao na kumwezesha kuendelea na masomo katika mazingira yenye faraja. Akisimulia safari yake huku machozi yakimlengalenga, Rose anasema kurejea darasani kumemrudishia matumaini na kumjengea ujasiri wa kufikia malengo yake. Pamoja na maumivu ya changamoto za kifamilia, upendo alioupata na fursa ya elimu vimempa nguvu ya kuipigania ndoto yake ya kuwa mwanasheria na kusimamia haki. Simulizi ya Rose inaonesha namna Serikali kupitia Mradi wa SEQUIP, kwa kushirikiana na jamii, inavyowapa nafasi ya pili vijana waliokosa fursa ya kuendelea na masomo. Kwa Rose, kuhitimu kidato cha nne ni mwanzo mpya unaompeleka karibu zaidi na ndoto yake ya kuvaa joho la uwakili.
Thu, 19 Nov 2026 11:36:34 +0000Judiciary pilots AI tool to tackle case backlog
The rollout of Mahakama AI comes as Kenya's courts buckle under a staggering backlog of nearly 580,000 pending cases.
RecentlyTRA, Korean facility, exchange experiences on managing customs systems
DAEJEON, South Korea: TANZANIA Revenue Authority (TRA) Commissioner General Yusuph Juma Mwenda has visited the South Korean Customs Service facility…
RecentlyRuto Rejects Politics of Exclusion, Pledges Equal Development
Latest · Politics
RecentlyGovernment Plans 12 Regional Ambulance Dispatch Centres
Read the full report from the original source.
RecentlyCourt adjournments decline to 7% in 2025/26 financial year
State of the Judiciary and the Administration of Justice Report records 274,478 adjournments, with internal factors accounting for 53.4pc of delays.
RecentlyJustin Muturi joins election observers mission in The Gambia
Read the full report from the original source.
RecentlyThe Equitable Party founding member files petition opposing name change to Linda Mwananchi
Read the full report from the original source.
RecentlyMTRH project equips workers with skills for future opportunities
Read the full report from the original source.
RecentlyFishing nets, maize stalks linked to deaths of two hippos in Naivasha
KWS postmortems found that one hippo died from a digestive blockage caused by discarded nets, while the other suffered fatal stomach bloating
RecentlyBoT yaimarisha ujumuishi wa kifedha kwa walemavu
Read the full report from the original source.
RecentlyOpposition sets 4 irreducible minimums for IEBC
They want a clean and verifiable voter register, an end to presidential vote tallying at Bomas, electronic voting for Kenyans abroad and livestreaming of voting
RecentlyTanzania, Morocco agree to introduce Dar- Casablanca direct flights to bolster ties in aviation sector
MONTREAL: TANZANIA and Morocco have discussed ways of strengthening cooperation in the aviation sector, including plans to introduce direct flights…
Recently'Intambara' hagati ya RD Congo n'Urwanda: OIF mu mayira abiri
Kuba Urwanda na RD Congo vyompi bifise abakandida, ivyo gutora umunyamabanga mushasha wa OIF vyahindutse urugamba rwa dipolomasi muri iryo shirahamwe.
RecentlyPage 128 of 1132 · 22629 stories