Unganishwa

Search the region

22634 stories

Uncategorized · Rwanda News Agency

Rwanda Agriculture Minister received new IFAD Country Director

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · SoftPower News

Minister Santa Alum Visit Exposes Inactive Emyooga SACCOs, Extortion and Staffing gaps in Karamoja

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

KEBS seizes 54 bales of maize flour over licensing breach

The agency urged consumers to exercise caution when purchasing packaged products and verify that they have been certified by the regulator

Recently
Uncategorized · Daily News

Tanzania hailed for successful Military-Civilian Cooperation Week

DAR ES SALAAM: TANZANIA has been commended for successfully hosting the Sixth East African Community (EAC) Military-Civilian Cooperation Week, held…

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

Dozens missing after boat carrying 100 migrants sinks off Senegal

Initial reports said that one person had died, but some local media have reported that at least four bodies have been recovered. Dozens of people still missing

Recently
Uncategorized · Issa Michuzi

TIRA YATAKIWA KUDUMISHA VIWANGO VYA KIMATAIFA VYA UBORA WA HUDUMA

Na. Joseph Mahumi, WF, Dodoma Katibu Mkuu Wizara ya Fedha ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, ameitaka Mamlaka hiyo kuhakikisha kuwa upatikanaji wa Cheti cha Mfumo wa Usimamizi wa Ubora ISO 9001:2015 unakuwa chachu ya kuimarisha uwajibikaji, ufanisi na utoaji wa huduma bora kwa wananchi na wadau wa sekta ya bima nchini. Ametoa msisitizo huo wakati wa hafla ya makabidhiano ya Cheti cha Mfumo wa Usimamizi wa Ubora ISO 9001:2015 kwa TIRA, iliyofanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya Mamlaka hiyo, Bima House, Njedengwa jijini Dodoma, ambapo alisema kupata cheti hicho si mwisho wa safari ya ubora, bali ni mwanzo wa hatua nyingine ya kuimarisha utendaji wa taasisi hiyo kwa kuzingatia viwango vinavyotambulika kimataifa. Dkt. Mwamba alisema mafanikio hayo yanaonesha dhamira ya TIRA katika kuimarisha mifumo yake ya kiutendaji, kuzingatia taratibu na viwango vya ubora, pamoja na kuongeza uwezo wa taasisi katika kutekeleza majukumu yake ya kusimamia na kuendeleza sekta ya bima nchini. “Cheti hiki kisiwe pambo la ofisi au nyaraka ya kutunzwa kwenye mafaili pekee, bali kiwe kielelezo cha utamaduni wetu wa kazi na dhamira yetu ya kutoa huduma bora kila siku,” alisisitiza Dkt. Mwamba Aidha alieleza kuwa Mfumo wa Usimamizi wa Ubora (ISO 9001:2015) una umuhimu mkubwa katika kuimarisha michakato ya kazi, ufuatiliaji wa utekelezaji wa majukumu, utatuzi wa changamoto na matumizi ya maoni ya wadau kama nyenzo ya kuboresha huduma zinazotolewa na taasisi. Dkt. Mwamba alisema mafanikio ya TIRA katika kupata cheti hicho yanaendana na mwelekeo wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, inayosisitiza mageuzi ya kitaasisi na uimarishaji wa mifumo ya utoaji huduma ili kujenga taasisi imara, zenye ufanisi na zinazoweza kuchochea maendeleo endelevu ya Taifa. Akizungumzia mchango wa sekta ya bima katika uchumi wa Taifa, Dkt. Mwamba aliipongeza TIRA kwa juhudi za kusimamia sekta hiyo, kulinda maslahi ya watumiaji wa huduma za bima na kuendeleza mazingira bora ya ukuaji wa soko la bima nchini ambapo mwaka 2025 ilichangia asilimia 2.11 ya Pato la Taifa. “Natoa rai kwenu kuendelea kuzihimiza kampuni za bima nchini kuwekeza katika mifumo ya usimamizi wa ubora ili kuimarisha ushindani, kuongeza uaminifu wa wateja na kuhakikisha huduma zinazotolewa zinakidhi viwango vinavyotambulika kimataifa” alisema Dkt Mwamba. Alilipongeza Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa utaalamu, mwongozo na ushirikiano uliowezesha TIRA kufikia hatua hiyo, huku akilihimiza shirika hilo kuendelea kusaidia taasisi nyingine nchini kuimarisha mifumo yao ya usimamizi wa ubora. Kwa upande wake Kamishna wa Bima nchini ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) Dkt. Baghayo Saqware, alisema kuwa Mamlaka hiyo inalenga kuhakikisha kuwa ofisi zake zote nchini zinafikia viwango hivyo ifikapo mwaka 2028. Dkt. Saqware alisema kuwa katika kufikia azma hiyo, TIRA itaendelea kuimarisha maeneo mbalimbali ya utoaji huduma ikiwemo miundombinu na majengo ya ofisi, uwezo wa watumishi pamoja na michakato ya kiutendaji inayotumika katika kutoa huduma kwa wananchi na wadau wa sekta ya bima. “TIRA itaendelea kuboresha mazingira ya kazi na mifumo ya utoaji huduma ili kuhakikisha kuwa wadau wote, wakiwemo wananchi, Serikali, kampuni za bima, watumishi na watoa huduma, wanapata huduma zinazokidhi viwango vinavyotakiwa” alisema Dkt. Saqware. Naye, Mkurugenzi wa Usimamizi wa Ubora, wa Shirika la Ubora Tanzania -TBS, Mhandisi Abdallah Kileo, akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TBS, alisema kuwa kupata Cheti cha Mfumo wa Usimamizi wa Ubora ISO 9001:2015 kwa TIRA ni hatua muhimu inayoonesha dhamira ya Mamlaka hiyo katika kuimarisha mifumo ya usimamizi, kuongeza ufanisi na kuhakikisha huduma zinazotolewa kwa wananchi na wadau wa sekta ya bima zinakidhi viwango vinavyotambulika kimataifa. Alisema kuwa uthibitisho huo unahusisha ofisi tano za TIRA, zikiwemo Makao Makuu ya Dodoma, Ofisi ya Zanzibar, Ofisi ya Dar es Salaam pamoja na Ofisi za Kanda ya Mashariki na maeneo mengine yaliyohusika katika utekelezaji wa mfumo huo. “Mfumo huu wa ISO 9001:2015 unatoa mwongozo wa kuimarisha taratibu za usimamizi wa ubora, uwajibikaji na ufuatiliaji wa michakato ya kiutendaji, huku ukilenga kuhakikisha taasisi zinakidhi mahitaji ya wateja na kufanya maboresho endelevu ya huduma” alisema Mhandisi Kileo. Aliongeza kuwa umuhimu wa mfumo huo kwa TIRA unatokana na ukubwa wa majukumu yake, yakiwemo kutoa leseni kwa kampuni na wadau wa sekta ya bima, kusimamia ushindani wa haki, kulinda maslahi ya wateja, kudhibiti shughuli za bima na kusimamia biashara za bima zinazovuka mipaka ya nchi, ambazo zinahitaji mifumo madhubuti ya usimamizi na uzingatiaji wa viwango vya ndani na kimataifa. Alieleza kuwa TBS itaendelea kutoa huduma za upimaji, uthibitishaji na tathmini ya mifumo ya usimamizi wa ubora kwa taasisi za Serikali na sekta binafsi, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha ubora, ufanisi na ushindani wa huduma na bidhaa nchini. Katibu Mkuu Wizara ya Fedha ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, akizungumza jambo wakati wa hafla ya makabidhiano ya Cheti cha Mfumo wa Usimamizi wa Ubora ISO 9001:2015 iliyotolewa kwa TIRA, na Shirika la Ubora Tanzania -TBS, iliyofanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya Mamlaka hiyo, Bima House, Njedengwa jijini Dodoma, ambapo aliitaka Mamlaka hiyo kuhakikisha kuwa upatikanaji wa vyeti hivyo inakuwa chachu ya kuimarisha uwajibikaji, ufanisi na utoaji wa huduma bora kwa wananchi na wadau wa sekta ya bima nchini. Katibu Mkuu Wizara ya Fedha ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Dkt. Natu El-Maamry Mwamba (Katikati), akipokea Cheti cha Mfumo wa Usimamizi wa Ubora ISO 9001:2015 iliyotolewa kwa TIRA, na Shirika la Ubora Tanzania -TBS, wakati wa hafla ya makabidhiano ya Vyeti vya Ubora iliyofanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya Mamlaka hiyo, Bima House, Njedengwa jijini Dodoma. Anayemkabidhi cheti hicho ni Mkurugenzi wa Usimamizi wa Ubora, wa Shirika la Ubora Tanzania -TBS, Mhandisi Abdallah Kileo (kulia), na kushoto ni Kamishna wa Bima nchini ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) Dkt. Baghayo Saqware. Katibu Mkuu Wizara ya Fedha ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Dkt. Natu El-Maamry Mwamba (kulia), akikabidhiwa Tuzo ya kutambua mchango wake katika Tasnia ya Bima, kutoka kwa Kamishna wa Bima nchini ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) Dkt. Baghayo Saqware, wakati wa hafla ya makabidhiano ya Cheti cha Mfumo wa Usimamizi wa Ubora ISO 9001:2015 iliyotolewa kwa TIRA, na Shirika la Ubora Tanzania -TBS, iliyofanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya Mamlaka hiyo, Bima House, Njedengwa jijini Dodoma. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma )

Thu, 19 Nov 2026 09:03:43 +0000
Uncategorized · Issa Michuzi

KAMPENI YA UGAWAJI WA VYANDARUA RUVUMA YAZINDULIWA RASMI

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brigedia Jenerali Ahmed Abbas Ahmed amezindua rasmi kampeni ya usambazaji na ugawaji wa vyandarua bure kwa wananchi wa mkoa huo, ikiwa ni mkakati wa kufikia lengo la kutokomeza malaria nchini (Zero Malaria) ifikapo mwaka 2030. Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo, Brigedia Jenerali Ahmed amesema kiwango cha maambukizi ya malaria mkoani Ruvuma bado kiko juu ya wastani wa kitaifa, hali inayolazimu kuongeza kasi ya mapambano dhidi ya ugonjwa huo. Pamoja na mambo mengine, RC Ahmed amekemea tabia ya baadhi ya wananchi kutumia vyandarua kinyume na malengo, ikiwemo kuvitumia kuvulia samaki na kuzungushia bustani za mbogamboga. Pia, ametoa wito kwa wananchi wa maeneo ya mijini na vijijini kuzingatia usafi wa mazingira, kudhibiti mazalia ya mbu kwa kutumia viuatilifu vya kuua viluilui, pamoja na kuacha matumizi holela ya dawa bila kupima ili kujua ugonjwa halisi. Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma, Wakili Mary Makondo, amesema kulinda afya za wananchi ni msingi muhimu wa kuwa na nguvu kazi imara itakayochangia ukuaji wa pato la kaya na taifa kwa ujumla. Kwa upande wake, Mwakilishi wa Bohari ya Dawa (MSD), Mboyi Wishega, amesema vyandarua 901,336 vitasambazwa katika vituo 888 vya kutolea huduma kwenye halmashauri tano za mkoa huo ambazo ni Madaba, Namtumbo, Nyasa, Songea Vijijini na Tunduru. Kwa upande mwingine, Mwakilishi wa Wizara ya Afya, Peter Gitanya, amesisitiza umuhimu wa kudhibiti vyandarua hivyo visichepushwe kwenda nchi jirani ili malengo ya kitaifa ya kutokomeza malaria yaweze kutimia. Akitoa Takwimu za ugonjwa wa Malaria za mkoa wa Ruvuma, Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Louis Chomboko, amesema mkoa umefanikiwa kupunguza kiwango cha maambukizi ya malaria kutoka asilimia 26 mwaka 2007 hadi kufikia asilimia 8.3 sasa. Mkazi wa Manispaa ya Songea, Jacob Lwambano, ameishukuru serikali kwa kujali afya za wananchi na kuahidi kuwa watavitunza vyandarua hivyo na kuvitumia kwa lengo lililokusudiwa

Thu, 19 Nov 2026 09:05:09 +0000
Uncategorized · The Standard

Isiolo residents cautioned over floodwaters

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Capital FM

Cheptai elevated to Sydney Marathon champion after Jepchirchir stripped of title

Latest · Athletics

Recently
Uncategorized · Capital FM

Stanbic Bank profit climbs to Sh10.3bn on higher interest income

Corporate · Quick read

Recently
Uncategorized · Capital FM

Zverev to defend himself against fresh lawsuit

Tennis · 4 hours ago

Recently
Uncategorized · Capital FM

Jambojet turns to flight data, single-engine taxiing to cut fuel consumption

Corporate · 4 hours ago

Recently
Uncategorized · Capital FM

Peres Jepchirchir banned, stripped of marathon title over doping

Athletics · 4 hours ago

Recently
Uncategorized · Capital FM

Killer building collapses expose Kenya’s regulatory rot

Latest · News

Recently
Business · Issa Michuzi

TAKWIMU SAHIHI MSINGI WA MAENDELEO NA UWEKEZAJI ENDELEVU – MUNDE

Na. Josephine Majura na Farida Ramadhan, WF, Dodoma Serikali imetoa wito wa matumizi ya takwimu sahihi katika kuelekeza uwekezaji wa sekta ya maji, kilimo na miundombinu ili kuongeza uzalishaji, kukuza uchumi na kuboresha maisha ya wananchi. Wito huo umetolewa jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb) kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) katika hafla ya maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika. Mhe. Munde alisema kuwa takwimu ni nyenzo muhimu katika kubaini mahitaji ya wananchi, kupanga matumizi ya rasilimali na kuhakikisha uwekezaji unaleta matokeo yaliyokusudiwa. “Maji ni rasilimali yenye mchango mkubwa katika maendeleo ya uchumi, hususan katika uzalishaji wa chakula, kilimo, viwanda, afya na uhifadhi wa mazingira, hivyo ni muhimu kuwa na mifumo imara ya takwimu ili kusimamia rasilimali hiyo kwa ufanisi”,alisema Mhe. Munde. Alisema Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kuwekeza katika sekta ya maji kwa lengo la kuongeza upatikanaji wa huduma hiyo na kutekeleza azma ya kumtua mama ndoo kichwani, hatua inayolenga kuwawezesha wanawake na watoto kutumia muda wao katika shughuli za uzalishaji na masomo badala ya kutafuta maji. Mhe. Munde alisema kuwa kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Maji na Mamlaka za Maji kwa mwaka 2025/26, upatikanaji wa huduma ya maji umefikia wastani wa asilimia 85.2 vijijini na asilimia 92.5 mijini, ambapo Serikali imepanga kukamilisha takriban miradi 1,214 ya maji, ikiwemo miradi 992 vijijini, 196 mijini na Miradi 26 ya Usafi na Mazingira maeneo ya mijini katika mwaka wa fedha 2026/27. “Maji tuliyonayo hayapaswi kutazamwa kama hitaji la matumizi ya nyumbani pekee, bali pia kama rasilimali muhimu kwa uzalishaji wa chakula, maendeleo ya kiuchumi, uhifadhi wa mazingira na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi”, alisisitiza Mhe. Munde. Alisema Serikali imeendelea kutekeleza miradi ya ujenzi, ukarabati na upanuzi wa miundombinu ya umwagiliaji ili kupunguza utegemezi wa mvua, kuongeza uzalishaji wa chakula na kuimarisha kipato cha wakulima hatua iliyowezesha eneo linalomwagiliwa kuongezeka kutoka hekta 727,280.06 mwaka 2024/25 hadi hekta 983,466.60 mwaka 2025/26. Alibainisha kuwa uwekezaji huo ni muhimu katika kuongeza uzalishaji wa chakula, kuimarisha usalama wa chakula nchini na kuongeza kipato cha wakulima, huku takwimu zikisaidia kubaini maeneo yenye uhitaji mkubwa wa miundombinu hiyo. Mhe. Munde alisema kuwa mabadiliko ya tabianchi, yakiwemo ukame na mafuriko, yanaendelea kuwa changamoto katika upatikanaji wa maji na uzalishaji wa kilimo, hivyo kuna umuhimu wa kuimarisha mifumo ya takwimu ili kufanya maamuzi yanayozingatia hali halisi ya rasilimali zilizopo. Aidha, amezitaka Wizara, mamlaka za maji, mikoa na halmashauri kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) katika kuimarisha ubora, uratibu na upatikanaji wa takwimu kwa wakati, akisisitiza kuwa machapisho yaliyozinduliwa yanapaswa kutumika katika maamuzi na utekelezaji wa mipango ya maendeleo. Pia, amewahimiza wananchi kuendelea kutoa taarifa sahihi wakati wa sensa na tafiti mbalimbali ili kuiwezesha Serikali kupata takwimu zinazowakilisha mahitaji halisi ya wananchi. Awali akizungumzia takwimu katika Sekta ya Maji, Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri alisema matumizi ya taarifa sahihi na zinazopatikana kwa wakati ni muhimu katika kubaini maeneo yenye upungufu wa huduma na kuelekeza uwekezaji kulingana na mahitaji halisi ya wananchi. Alisema kwa mujibu wa takwimu za sekta ya maji, Tanzania ina jumla ya vijiji 12,333, ambapo vijiji 10,758 vimefikiwa na huduma ya maji safi na salama, huku vijiji 1,575 vikiwa bado havijafikiwa, kutokana na hali hiyo, Serikali imepanga kuanza kutekeleza miradi ya maji katika vijiji 400, hatua inayodhihirisha umuhimu wa takwimu katika kupanga vipaumbele na kugawa rasilimali. Mhandisi Mwajuma alisema pamoja na takwimu zinazoonesha kiwango cha upatikanaji wa huduma za maji, ni muhimu kuimarisha ukusanyaji na uchambuzi wa taarifa kuhusu hali ya vyanzo vya maji, mwenendo wa mvua, mtiririko wa mito, kiasi na ubora wa maji pamoja na utendaji wa miundombinu. Alieleza kuwa taarifa hizo zitasaidia kutambua mapema athari za ukame na mafuriko, kutabiri changamoto zinazoweza kujitokeza na kuwezesha uwekezaji katika miundombinu inayostahimili mabadiliko ya tabianchi. Kwa upande wake Mtakwimu Mkuu wa Serikali, kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS), Dkt. Amina Msengwa alisema inaendelea kuimarisha matumizi ya teknolojia za kisasa katika uzalishaji na uchambuzi wa takwimu ili kuongeza ufanisi wa maamuzi ya Serikali na sekta binafsi. Alisema kupitia Mpango Kabambe wa Pili wa Takwimu Tanzania (TSMP II), wataalamu 79 wamewezeshwa kitaaluma na taasisi 27 zimeunganishwa katika Mfumo Jumuishi wa Takwimu Tanzania (TISP), hatua inayolenga kurahisisha upatikanaji na matumizi ya taarifa kutoka vyanzo mbalimbali kwa ajili ya mipango ya maendeleo na uwekezaji. Aliongeza kuwa NBS pia imeanza kuweka kipaumbele katika kuanzisha Maabara ya Uchambuzi wa Data (Data Analytics Laboratory), itakayowezesha kuunganisha na kuchambua taarifa zinazotokana na sensa, tafiti, takwimu za kiutawala na vyanzo vipya kwa kutumia Akili Unde (AI) na teknolojia za kijiografia. “Maabara itawezesha kuunganisha na kuchambua data za sensa, tafiti, takwimu za kiutawala na vyanzo vipya, kwa kutumia akili unde, uchambuzi wa kijiografia na makadirio ya maeneo madogo. Itasaidia kutoa taarifa za kina kwa wakati, kupima mbinu mpya kabla ya matumizi rasmi na kutoa mafunzo ya vitendo kwa wataalamu na vijana” alibainisha Dkt. Msengwa. Aidha, Dkt. Msengwa amesema NBS inaendelea kukuza ushiriki wa vijana katika sekta ya takwimu kupitia programu za ubunifu na mashindano ya NBS Data Challenge, yaliyolenga kutumia teknolojia na uchambuzi wa data kutafuta suluhisho la changamoto mbalimbali za maendeleo. Katika maadhimisho hayo, Serikali imezindua machapisho manne ya takwimu yatakayosaidia kuboresha mipango ya maendeleo na uwekezaji nchini. Machapisho hayo ni Wasifu wa Kiuchumi na Kijamii wa Mikoa, Mkakati wa Taifa wa Kuendeleza Takwimu wa mwaka 2026/27 hadi 2036/37, Mwongozo wa Ukusanyaji wa Viashiriavya Takwimu za Maji, Vyoo na Usafi wa Mazingira wa mwaka 2025/26 na Ripoti yaKutathmini Upatikanaji Endelevu wa Huduma za Maji, Vyoo na Usafi wa Mazingira ya mwaka 2023. Siku ya Takwimu Afrika huadhimishwa kila mwaka Novemba 18 tangu mwaka 1990 kwa lengo la kuhamasisha matumizi ya takwimu katika maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kimazingira. Kwa mwaka 2026, maadhimisho hayo yanaongozwa nakaulimbiu isemayo: “Kuweka Mifumo Rasmi ya Takwimu za Maji na Usafi waMazingira kwa Maendeleo Endelevu yanayostahimili Mabadiliko ya Tabianchi Barani Afrika.” Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Handisi Mshamu Ali Munde (Mb) akimkabidhi Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri, nakala za Ripoti ya Kutathmini Upatikanaji Endelevu wa Huduma za Maji, Vyoo na Usafi wa Mazingira, katika hafla ya maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika iliyofanyika jijini Dodoma. Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Handisi Mshamu Ali Munde (Mb) akimkabidhi Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri, nakala za Ripoti ya Kutathmini Upatikanaji Endelevu wa Huduma za Maji, Vyoo na Usafi wa Mazingira, katika hafla ya maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika, iliyofanyika jijini Dodoma. Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Handisi Mshamu Ali Munde (Mb), akiwakabidhi washindi wa kwanza wa Mashindano ya NBS Data Challenge mfano wa hundi wenye thamani ya sh. Milioni 20, katika hafla ya maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika, iliyofanyika jijini Dodoma. Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Handisi Mshamu Ali Munde (Mb), akimkabidhi tuzo mwanafuzi aliefanya vizuri katika masomo ya takwimu kwenye ngazi ya Shahada ya Uzamili kutoka Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC), Bi. Ester Joseph, katika hafla ya maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika, iliyofanyika jijini Dodoma. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha, Dodoma)

Thu, 19 Nov 2026 08:55:13 +0000
Uncategorized · BBC Afrique

Un moment diplomatique remarquable pour Xi Jinping, le président chinois, mais il comporte des risques.

Cette rencontre comporte des défis car il y a des sujets que Xi ne semble pas vouloir aborder avec Poutine et Trump.

Recently
Uncategorized · The Observer Uganda

Oboth courts British support as Uganda braces for Afcon 2027

Speaker of Parliament Jacob Marksons Oboth has called on Britain to reciprocate Uganda’s longstanding support for English football by backing the country as it prepares…

Recently
Uncategorized · Daily News

Tanzania and Norway hold 4th political consultations to strengthen bilateral relations

OSLO: TANZANIA and Norway have reaffirmed their commitment to strengthening bilateral relations, expanding economic cooperation and enhancing collaboration on regional…

Recently
Uncategorized · DW Rwanda

APEC summit: Xi, Trump and Putin kick off trilateral talks

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

Sifuna swears on Bible while responding to Babu Owino

The Nairobi senator disputes Babu's account of an initial agreement on leadership positions in the Linda Mwananchi movement

Recently

Page 133 of 1132 · 22634 stories