Unganishwa

Search the region

22655 stories

National · Issa Michuzi

NYONGO AAGIZA MFUMO WA TAHADHARI ZA TABIANCHI ULETE MATOKEO CHANYA SHULENI

Na Mwamvua Mwinyi, Pwani WAKURUGENZI wa Halmashauri mkoani Pwani wameagizwa kuhakikisha Dashibodi ya Ramani ya Hatari za Tabianchi inayotumika katika sekta ya elimu inafanya kazi kikamilifu ili kutambua mapema vihatarishi vinavyoweza kuathiri shule na kuchukua hatua za kukabiliana navyo. Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Stanslaus Nyongo, katika uzinduzi wa dashibodi hiyo inayolenga kusaidia kubaini shule zilizo katika hatari ya kukumbwa na mafuriko na ukame, pamoja na kutoa tahadhari za haraka kupitia ujumbe mfupi wa simu (SMS). Nyongo amesisitiza kuwa uzinduzi wa mfumo huo haupaswi kuwa tukio la kawaida lisilo na matokeo, bali unapaswa kuambatana na matumizi endelevu yatakayosaidia kutatua changamoto zilizokusudiwa na kuhakikisha wanafunzi wanaendelea kupata elimu katika mazingira salama licha ya athari za mabadiliko ya tabianchi. Ameelekeza wakuu wa shule kutumia taarifa zinazopatikana kwenye mfumo kutambua vihatarishi katika maeneo yao na kuandaa mipango ya kukabiliana na majanga kulingana na mazingira ya shule husika. Aidha, maofisa elimu wa kata na wilaya wametakiwa kuimarisha usimamizi na ufuatiliaji wa matumizi yake ili taarifa hizo zijumuishwe katika mipango ya kuimarisha usalama wa shule. Pia, ameutaka mkoa na maofisa elimu kushirikiana na maofisa TEHAMA wa mkoa na halmashauri kutoa msaada wa kitaalamu na kutatua kwa haraka changamoto zinazoweza kujitokeza wakati wa matumizi ya mfumo huo. Kwa upande wake, Kiongozi wa Timu ya Programu ya Shule Bora, Virginia Briand, amesema kuboresha ubora wa elimu kunahitaji miundombinu himilivu, walimu wenye uwezo, mazingira salama ya kujifunzia na mifumo imara inayowezesha shule kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi. Amesema katika kipindi cha miaka sita ya utekelezaji wa programu hiyo, imefanikiwa kusaidia kuweka teknolojia za kupikia safi katika shule 22 za mikoa ya Pwani na Katavi, zikiwemo 12 za Pwani, pamoja na kukamilika kwa takribani madarasa 121 yanayozingatia ustahimilivu dhidi ya athari za tabianchi katika shule 80, zikiwemo shule 10 za Pwani. Ameongeza kuwa Programu ya Shule Bora inayofadhiliwa na Serikali ya Uingereza kupitia FCDO, inatekelezwa chini ya Serikali ya Tanzania kupitia Ofisi ya Rais-TAMISEMI na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, kwa msaada wa kitaalamu wa Cambridge Education. Naye mwakilishi wa Mkurugenzi wa TEHAMA wa Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI, Erick Lesilwa, amesema dashibodi hiyo ni nyenzo muhimu ya kuboresha utendaji na kuhakikisha kila mtoto anapata elimu katika mazingira salama.

Wed, 18 Nov 2026 19:28:14 +0000
Uncategorized · Daily News

Indusmach Tanzania 2026 opens with 30 exhibitors

DAR ES SALAAM: Industrial machinery manufacturers from India, China and Tanzania are showcasing equipment and technologies at the 26th Indusmach…

Recently
Uncategorized · KT Press

All Tanzanian, Congolese Airlines Banned From EU Skies

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Daily News

From TAZARA to orphanages, Huawei seeks to bridge Tanzania’s digital divide through inclusive technology initiatives

When technology becomes part of everyday learning, a child’s opportunities should not be determined by family circumstances or economic background.…

Recently
Uncategorized · UN News Burundi

COP31: The push to protect warming oceans reaches the negotiating table

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Yaga Burundi

OIF-Burundi : quelle profondeur diplomatique face à la rivalité RDC-Rwanda ?

En s’opposant publiquement à un troisième mandat de la Rwandaise Louise Mushikiwabo à la tête de l’Organisation internationale de la Francophonie (OIF), le Burundi a rompu avec la réserve diplomatique qui caractérisait jusque-là sa position sur la scene internationale. Cette […] L’article OIF-Burundi : quelle profondeur diplomatique face à la rivalité RDC-Rwanda ? est apparu en premier sur Yaga Burundi .

Wed, 18 Nov 2026 19:06:24 +0000
Uncategorized · UN News Burundi

Ukraine: Civilian casualties in 2026 already far exceed previous years’ tolls

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

Ruto: I’ve delivered, give me second term

President William Ruto has used his State of the Nation Address to defend his administration’s performance and make a case for another term

Recently
National · Issa Michuzi

PWANI YAPONGEZA UZINDUZI KITAMBULISHO KIPYA CHA TAIFA

Na Said Mwishehe,Michuzi Blog MKUU wa Mkoa wa Pwani, Stanlaus Nyongo, ameipongeza Serikali kwa maboresho ya huduma za usajili na utambuzi wa watu kupitia Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), akisema teknolojia mpya ya uzalishaji wa vitambulisho itaimarisha usalama, ubora na ufanisi wa huduma hizo. Amesema uzinduzi wa kitambulisho kipya cha taifa pamoja na teknolojia mpya ya uzalishaji wake ni hatua muhimu katika kuboresha mfumo wa utambulisho wa wananchi na kurahisisha upatikanaji wa huduma za NIDA. Nyongo aliyasema hayo leo Novemba 18,2026 wakati wa hafla ya uzinduzi wa kitambulisho kipya cha taifa na teknolojia mpya ya uzalishaji wa vitambulisho, iliyohudhuriwa na Waziri Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba, akiwa mgeni rasmi.Uzinduzi huo umefanyika Kibaha Pwani Amesema wakazi wa Mkoa wa Pwani wana furaha kubwa kuwa wenyeji wa tukio hilo la kitaifa, akibainisha kuwa wamepata fursa ya kuwa miongoni mwa wananchi wa kwanza kunufaika na huduma zilizoboreshwa za NIDA, zikiwemo huduma zinazolenga kupunguza foleni. Amefafanua maboresho hayo yatasaidia wananchi wengi zaidi kupata vitambulisho vya taifa kwa urahisi na kwa muda mfupi, hivyo kuondoa changamoto zinazoweza kujitokeza katika upatikanaji wa huduma hizo. Pia ameishukuru Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi pamoja na NIDA kwa kuuchagua Mkoa wa Pwani kuwa mwenyeji wa uzinduzi huo. Nyongo amesema mafanikio ya shughuli za usajili na utambuzi wa watu yanategemea ushirikiano wa karibu kati ya NIDA na Serikali za Mitaa, akisisitiza umuhimu wa viongozi wa wilaya, kata, vijiji, mitaa na vitongoji katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma hizo. Amesema viongozi hao wana nafasi muhimu kwa kuwa wako karibu na wananchi na wana uwezo wa kuratibu shughuli za usajili na kuwafikia wananchi katika maeneo yao. Ameongeza kuwa uongozi wa Mkoa wa Pwani utaendelea kushirikiana na NIDA kuhakikisha shughuli za usajili na utambuzi wa watu zinatekelezwa kwa ufanisi na kuwafikia wananchi wengi zaidi. Katika hatua nyingine, Nyongo amesema mkoa huo uko salama na wananchi wanaendelea na shughuli zao za kijamii na kiuchumi, licha ya baadhi ya maeneo kukumbwa na athari za mvua. Amesema Serikali ya mkoa inaendelea kufuatilia na kusimamia athari hizo ili kuhakikisha zinadhibitiwa na hazisababishi madhara zaidi kwa wananchi. Aidha, amemuomba Waziri Mkuu kufikisha salamu za upendo na shukrani kwa Rais Samia Suluhu Hassan, akisema wakazi wa Pwani wanamthamini, wanamuombea afya njema na kuendelea kuongoza nchi katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo.

Wed, 18 Nov 2026 19:02:06 +0000
National · Issa Michuzi

KOKA AMLILIA WAZIRI MKUU MAJI, BARABARA NJIA NANE KIBAHA

Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Kibaha MBUNGE wa Jimbo la Kibaha Mjini mkoani Pwani Silvester Koka, ameiomba Serikali kuharakisha utekelezaji wa miradi ya kimkakati ya maji na barabara katika Manispaa ya Kibaha, akieleza kuwa baadhi ya miradi hiyo imekuwa ikisuasua kwa muda mrefu na kusababisha usumbufu kwa wananchi. Amesema miongoni mwa miradi inayotia wasiwasi ni ujenzi wa tenki la maji la Pangani, ambao licha ya kusainiwa kwa mkataba takribani miaka mitatu iliyopita, umefikia asilimia 13 pekee ya utekelezaji. Akizungumza leo Novemba 18,2026 mbele ya Waziri Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba, Koka amesema mradi huo ni muhimu kwa wakazi wa Kata ya Pangani na maeneo jirani ambayo yamekuwa yakikabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama. Ametaja maeneo yanayohitaji huduma hiyo kuwa ni Mpapa, Pangani, Mdeja, Majimoto na Lulanzi, akisema wananchi wake wameendelea kuhangaika kutafuta maji licha ya mradi huo kuanza kutekelezwa Amesema hali hiyo inahitaji uingiliaji wa Serikali ili mkandarasi aharakishe kazi na kuhakikisha wananchi wananufaika na uwekezaji huo badala ya kuendelea kusubiri huduma muhimu. Katika hatua nyingine, mbunge huyo ameiomba Serikali kuongeza kasi ya upanuzi wa barabara ya Morogoro, akieleza kuwa eneo la Kibaha limekuwa likikabiliwa na msongamano mkubwa wa magari kutokana na shughuli za kiuchumi na usafiri kuelekea mikoa ya Magharibi. Ameongeza magari mengi yanayoingia na kutoka Dar es Salaam yanapita katika eneo hilo, huku sehemu kubwa ya msongamano ikijitokeza kati ya Kibaha na Chalinze, hali inayopoteza muda na kuongeza gharama za usafirishaji. Koka amesema barabara hiyo ni miongoni mwa miundombinu muhimu zaidi kiuchumi nchini, hivyo Serikali inapaswa kuipa kipaumbele katika utekelezaji wa miradi ya upanuzi. Pia ameeleza kusuasua kwa mradi wa barabara ya Chang’ombe–Mapinga yenye urefu wa takribani kilomita 25, akisema hadi sasa ni kilomita 10 pekee zilizojengwa. Ameongeza kuchelewa kukamilika kwa miradi ya aina hiyo kunachelewesha manufaa yaliyokusudiwa na kuongeza gharama za utekelezaji, hivyo akaiomba Serikali kuingilia kati ili kuhakikisha mradi huo unakamilika Kuhusu usafiri wa umma, Koka amesema wananchi wa Kibaha Mjini bado hawajanufaika na huduma ya mwendokasi licha ya miundombinu ya barabara kujengwa na kuwepo kwa mazingira ya kuanza kwa huduma hiyo. Ameiomba Serikali kuharakisha maandalizi na kuweka utaratibu utakaowezesha wananchi kuanza kutumia usafiri huo, akisema utasaidia kupunguza adha ya usafiri kati ya Kibaha na Dar es Salaam. “Barabara hizo zina umuhimu mkubwa katika kufungua fursa za biashara, uwekezaji na usafirishaji wa bidhaa, hasa kutokana na matarajio ya kuongezeka kwa shughuli za kiuchumi katika maeneo hayo.” Aidha, ameelezachangamoto ya daraja la Lunguki linalopita Mto Mpiji na kuunganisha Kata ya Pangani na maeneo ya Mkamba, Maringota pamoja na Wilaya ya Mkuranga. Amefafanua daraja hilo limekuwa likikumbwa na changamoto ya mabadiliko ya mkondo wa mto, hali inayosababisha wananchi kushindwa kuvuka kwa urahisi, huku watoto wakipata wakati mgumu kufika shuleni na wafugaji wakikabiliwa na changamoto ya kuvusha mifugo. Ameiomba Serikali kwa kushirikiana na Halmashauri ya Mkuranga kutafuta suluhisho la kudumu la ujenzi wa daraja hilo ili kurahisisha mawasiliano na shughuli za kiuchumi. Pamoja na changamoto hizo, Koka ameipongeza Serikali inayoongozwa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji katika maendeleo ya Manispaa ya Kibaha, akisema hatua mbalimbali zimeongeza kasi ya utoaji wa huduma za kijamii. Pia amesema Halmashauri imeendelea kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato ya ndani, ambapo katika robo ya pili ya mwaka wa fedha 2026/27 ilikuwa imekusanya takribani Shilingi milioni 18, sawa na asilimia 55.5 ya makadirio ya kipindi hicho. Ameongeza kuwa katika kipindi cha mwaka wa fedha 2026/27, takribani Shilingi milioni 600 zimetumika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya huduma za jamii. Katika sekta ya elimu, amesema Serikali imejenga shule mpya za msingi 12 na sekondari 10, huku ujenzi wa madarasa na maabara ukiendelea kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji. Ameongeza hatua hizo zimechangia kuongezeka kwa ufaulu, kiasi cha shule za sekondari za kata kuanza kushindana na shule binafsi katika matokeo ya mitihani. Kuhusu afya, amesema Halmashauri imeendelea kuboresha huduma kwa kujenga vituo vya afya na zahanati, huku upatikanaji wa dawa ukiongezeka ikilinganishwa na hali ya awali. Serikali pia imeendelea kuwekeza katika miundombinu ya barabara, maji na umeme, akitaja utekelezaji wa miradi ya maji yenye thamani ya Shilingi milioni 700.5 na ujenzi wa miundombinu mingine ya kusogeza huduma karibu na wananchi. Koka alihitimisha kwa kuiomba Serikali kuyafanyia kazi maombi yaliyowasilishwa, akisema kukamilika kwa miradi hiyo kutafungua fursa za uwekezaji, kuongeza shughuli za kiuchumi na kuboresha maisha ya wakazi wa Kibaha Mjini.

Wed, 18 Nov 2026 18:58:55 +0000
Uncategorized · Issa Michuzi

TUME YA TAIFA YA MIPANGO, UNFPA KUDUMISHA USHIRIKIANO KATIKA UTEKELEZAJI WA DIRA 2050

Na Mwandishi Wetu - Dar es Salaam. Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Mipango na Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango, Dkt. Tausi Kida amekutana na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA), Bw. Mark Bryan Schreiner, leo Novemba 18, 2026, jijini Dar es Salaam. Viongozi hao, wamefanya tathmini ya ushirikiano baina ya taasisi zao kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na maendeleo baina ya baina ya nchi. Katika mazungumzo hayo, Katibu Mkuu amemshukuru Bw. Schreiner kwa mchango wake katika kuimarisha ushirikiano wa Tanzania na UNFPA, hususan katika masuala ya idadi ya watu na mipango ya maendeleo. Dkt. Kida amesisitiza umuhimu wa kuzingatia mwenendo wa idadi ya watu, uwekezaji kwa vijana na maendeleo ya rasilimali watu katika utekelezaji wa Dira 2050 na Mpango wa Nne wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano. Aidha, amesisitiza kuwekeza kwa vijana, kuimarisha rasilimali watu na kukabiliana na changamoto za umaskini, mimba za utotoni na ukatili wa kijinsia ili Taifa liweze kunufaika na fursa za idadi kubwa ya vijana. Aidha, viongozi hao wamekubaliana kukamilisha mapitio ya Sera ya Taifa ya Idadi ya Watu na kuandaa programu mpya ya ushirikiano inayoakisi vipaumbele vya Dira 2050. Kwa upande wake, Bw. Schreiner amethibitisha dhamira ya UNFPA kuendeleza ushirikiano huo, ikiwemo kutoa msaada wa kitaalamu katika uchambuzi wa takwimu na mwenendo wa idadi ya watu.

Wed, 18 Nov 2026 18:55:09 +0000
Uncategorized · Citizen Digital

Pochettino arrives at Man Utd to start work

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · KBC

Waunifor–Flax road opens new economic frontiers for rural communities

Read the full report from the original source.

Recently
World · Daily News

The Diplomacy Beneath the Veto: Tanzania, Russia, and the Mechanics of Multilateral Leverage: Stratgic Non-Alignment and Executive Realism in Modern Geopolitics

Western foreign policy establishments are sleepwalking into a multipolar reality they refuse to name. While Washington and Brussels obsess over…

Recently
Uncategorized · Issa Michuzi

DKT. MWIGULU AZINDUA KITAMBULISHO CHA TAIFA KILICHOBORESHWA

▪️ Serikali yawekeza zaidi ya Sh. bilioni 30 katika kadi na mashine za uzalishaji ▪️ Asisitiza wananchi kupata vitambulisho bila usumbufu ▪️ Vitambulisho vya awali vinaendelea kutumika WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, amezindua kitambulisho cha Taifa kilichoboreshwa, toleo la mwaka 2026, akisisitiza kuwa uwekezaji huo unapaswa kurahisisha upatikanaji wa huduma na kupunguza usumbufu kwa wananchi. Katika hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya Stendi ya Zamani ya Mailimoja, Kibaha, mkoani Pwani, Waziri Mkuu pia amezindua teknolojia mpya ya uzalishaji wa vitambulisho, programu tumizi ya NIDA Wallet na magari 10 ya huduma za usajili. Amesema maboresho hayo yanafungua fursa ya kuunganisha huduma mbalimbali kupitia utambulisho mmoja, hivyo kupunguza ulazima wa wananchi kubeba vitambulisho vingi katika shughuli zao za kila siku. “Lengo la Serikali ni kuhakikisha uwekezaji huu unaleta matokeo yanayoonekana katika maisha ya kila siku ya Mtanzania,” amesema. Dkt. Mwigulu amesisitiza kuwa kila Mtanzania anayestahili kupata kitambulisho cha Taifa anapaswa kukipata kwa wakati, bila usumbufu wala urasimu. Amempongeza Rais Dkt. Samia kwa kuwezesha uwekezaji huo, akisema matumizi ya teknolojia yanapaswa kuboresha huduma, kuimarisha utawala bora na kupanua fursa za wananchi katika shughuli za kiuchumi. Akifafanua maboresho hayo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), James Kaji, amesema Serikali imewekeza zaidi ya shilingi bilioni 30 katika ununuzi wa kadi mpya na mashine tano za kisasa zenye uwezo wa pamoja wa kuzalisha vitambulisho 2,800 kwa saa. Amesema mashine hizo zinatumia teknolojia ya kuchora taarifa na picha kwa mionzi ya leza ndani ya tabaka za kadi, badala ya kuzichapisha kwa wino juu ya uso wake. Hatua hiyo inalenga kuongeza uimara wa kitambulisho na kupunguza uwezekano wa kughushi. Aidha, amesema nafasi za programu za kidijitali zinazoweza kuunganishwa kwenye kadi zimeongezwa kutoka nne hadi nane, ili kuwezesha matumizi mapana zaidi ya kitambulisho hicho katika huduma mbalimbali. Ameeleza kuwa uunganishaji wa huduma, zikiwemo bima ya afya, leseni za udereva na usafiri, utafanyika kwa hatua kulingana na utayari wa mifumo, makubaliano ya taasisi husika na matakwa ya kisheria. “Lengo si kuongeza teknolojia kwa ajili ya teknolojia, bali ni kumwezesha mwananchi kutumia utambulisho wake katika huduma mbalimbali kwa usalama na urahisi zaidi,” amesema Kaji. Kuhusu NIDA Wallet, amesema ni programu tumizi inayowezesha mwananchi kuwa na utambulisho wake wa kidijitali kwenye simu na kuutumia kuthibitisha taarifa zake wakati wa kupata huduma, kadiri mifumo ya taasisi husika itakavyounganishwa. Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, amesisitiza kuwa uzinduzi huo hauondoi uhalali wa vitambulisho vya awali, hivyo wananchi hawalazimiki kubadilisha vitambulisho visivyo na dosari. “Hauna sababu ya kwenda kubadilisha kitambulisho chako cha zamani kwenda kupata kipya kama hakuna sababu yoyote ya msingi,” amesema. Katambi pia amewahimiza wananchi kuchukua vitambulisho vilivyo tayari katika maeneo walikojisajili. Naye Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Paschal Inyasi Chinyele, amepongeza maboresho hayo, huku akisisitiza ulinzi wa taarifa binafsi za wananchi, ushirikiano baina ya NIDA na taasisi nyingine na uendelevu wa teknolojia inayotumika.

Wed, 18 Nov 2026 18:37:38 +0000
National · Issa Michuzi

DKT. MWIGULU: MSITWAE ARDHI ZA WANANCHI BILA FIDIA

▪️︎ Akemea matumizi mabaya ya mamlaka kuwatisha wamiliki wa maeneo ▪️︎ Ataka uwekezaji uwanufaishe pia wananchi wanaopisha miradi WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, amewataka maafisa wa ardhi kuzingatia sheria na kuhakikisha wananchi wanaopisha miradi ya maendeleo na uwekezaji wanalipwa fidia, akisisitiza kuwa matumizi ya maeneo hayo kwa manufaa ya umma hayapaswi kupuuza haki za wamiliki. Amesema katika maeneo mbalimbali amekutana na malalamiko ya wananchi ambao mashamba yao yametumika kujenga shule, vituo vya afya na kutekeleza miradi mingine, lakini hawajalipwa fidia licha ya huduma kuanza kutolewa. “Tuache kutumia vibaya sheria. Tuache kutumia vibaya mamlaka,” amesema. Dkt. Mwigulu ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi katika viwanja vya Stendi ya Zamani ya Mailimoja, Kibaha, mkoani Pwani, baada ya kuzindua kitambulisho cha Taifa kilichoboreshwa. Ameeleza kuwa Serikali inapohitaji ardhi kwa ajili ya miradi yenye maslahi mapana ya Taifa, wahusika wanapaswa kuzingatia masharti ya sheria na kulinda haki za wanaopisha maeneo hayo. Amesema kuwepo kwa shule au kituo cha afya kinachotoa huduma hakuondoi wajibu wa kuzingatia haki ya mwananchi aliyekuwa akimiliki eneo hilo, likiwemo shamba la urithi wa familia. Waziri Mkuu pia amekemea tabia ya baadhi ya maafisa kuwataka wananchi kurejesha hati zao kwa ahadi ya kupatiwa maeneo mengine, kisha maeneo hayo kuuzwa bila haki za wamiliki kuzingatiwa. Amesisitiza kuwa wananchi wanapaswa kuunga mkono uwekezaji kwa sababu unaongeza ajira, uzalishaji na mapato ya nchi. Hata hivyo, amesema manufaa hayo yanapaswa kuwafikia pia wananchi wanaopisha miradi. Dkt. Mwigulu amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kusimamia malipo ya fidia, akisema alipokuwa Waziri wa Fedha alishuhudia Serikali ikilipa madai ambayo baadhi yake yalikuwa yamedumu kwa miaka mingi. Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameeleza kuwa Serikali imetanguliza malipo ya miradi ambayo wakandarasi walikuwa wamesimamisha kazi, ikifuatiwa na malipo ya awali kwa miradi yenye mikataba, kabla ya kusaini mikataba mipya iliyokamilisha taratibu za manunuzi. Amewataka wakandarasi waliopokea fedha kurejea kazini na kuongeza kasi ya utekelezaji ili wananchi wapate huduma zilizokusudiwa. Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Dkt. Pius Stephen Chaya, amesema Serikali imeandaa utaratibu wa kulipa kwa awamu wananchi wanaodai fidia katika eneo maalumu la uwekezaji la Bagamoyo. Amesema hatua hiyo inafuatia maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha wananchi hao wanalipwa. Naye Waziri wa Maji, Juma Aweso, ameelekeza madai ya mkandarasi wa mradi wa maji Pangani ya shilingi milioni 700 yalipwe kabla ya mwezi huu kuisha ili kuharakisha utekelezaji. Pia, ameitaka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kuanza utaratibu wa kuwapatia wananchi wa Pangani maji bila kusubiri ujenzi wa tenki ukamilike.

Wed, 18 Nov 2026 18:39:49 +0000
Uncategorized · The Star Kenya

Duale: Over 33m Kenyans registered with SHA

Duale commended Nairobi County for training 923 health workers and 1,598 Community Health Promoters (CHPs) as part of the response

Recently
Uncategorized · DW Afrique

Quel rôle pour l'Afrique dans la COP31 ?

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · DW Rwanda

Israel launches new ground operation in Gaza

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Business Daily

Stanbic freezes Vodacom’s Sh9bn over Safaricom sale

Read the full report from the original source.

Recently

Page 144 of 1133 · 22655 stories