Search the region
22726 stories
TIRA YAWEKA MSISITIZO BIMA YA AFYA KWA WOTE, YATOA ONYO KWA SKIMU ZA BIMA
*Yasisitiza wananchi kujiunga na skimu zilizosajiliwa, yataka uwazi wa vifurushi na huduma Na Said Mwishehe,Michuzi Blog MAMLAKA ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) imewataka Watanzania kujiunga na skimu za bima ya afya zinazotambulika kisheria ili kujikinga na gharama za matibabu, huku ikizionya kampuni na skimu zinazotoa huduma hizo kuhakikisha wananchi wanapewa taarifa sahihi kuhusu vifurushi na stahiki zao. Mamlaka hiyo imesema utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote ni hatua muhimu katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma za matibabu wanapozihitaji bila kukabiliwa na vikwazo vya kifedha, lakini mafanikio yake yanategemea uwazi, uaminifu na usimamizi madhubuti wa watoa huduma. Akizungumza leo Novemba 16,2026 jijini Dar es Salaam katika kikao kilichoandaliwa na TIRA chini ya uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina Kamishna Mkuu wa TIRA, Dk. Baghayo Saqware, amesema mamlaka hiyo ina jukumu la kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote ya mwaka 2023, ikiwamo kuhakikisha skimu za umma na binafsi zinatoa huduma kwa kuzingatia sheria na kulinda haki za wanachama. Amesema wananchi wanapaswa kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) au kampuni binafsi za bima zilizosajiliwa na kusimamiwa na TIRA, akisisitiza kuwa bima ya afya ni kinga inayopaswa kununuliwa kabla ya mtu kuugua. “Bima ya afya ni utaratibu wa kununua kinga kabla ya ugonjwa ili uweze kupata matibabu unapougua. Huwezi kusubiri gari ipate ajali ndipo uanze kutafuta bima,” amesema. Dk. Saqware amesema wananchi wanaojiunga na NHIF au kampuni binafsi zilizosajiliwa wana haki ya kupata huduma kwa mujibu wa viwango vilivyowekwa, huku TIRA ikiendelea kusimamia watoa huduma ili kuhakikisha wanatimiza wajibu wao. Amezitaka kampuni na skimu za bima kuhakikisha kabla ya mwananchi kujiunga, anapewa maelezo yanayoeleweka kuhusu huduma zinazolipiwa, zile ambazo hazijumuishwi, masharti ya matumizi ya bima na utaratibu wa kupata matibabu. Pia ameonya dhidi ya matumizi ya matangazo na ahadi zinazoweza kuwapotosha wananchi na kuwafanya kujiunga na vifurushi bila kuelewa huduma wanazostahili kupata. Aidha amezitaja skimu hizo kuweka wazi orodha ya hospitali, vituo vya afya na zahanati zinazotambuliwa katika utoaji wa huduma ili wananchi waweze kujua wanakoweza kupata matibabu kupitia bima zao. “Ni muhimu malalamiko ya wanachama kupokelewa, kuchunguzwa na kutatuliwa kwa wakati katika ngazi za kampuni na skimu husika, huku wananchi wanaoshindwa kupata suluhisho wakipewa nafasi ya kuwasilisha malalamiko yao TIRA kwa hatua zaidi za kiudhibiti.” Amefafanua jukumu la mamlaka hiyo si kuwa idara ya madai ya kampuni za bima, bali kuhakikisha watoa huduma wanatimiza wajibu wao na kulinda haki za wananchi. Kuhusu sekta ya bima kukua kwa kasi amesema mchango wake katika Pato la Taifa umeongezeka kutoka asilimia 1.68 mwaka 2021 hadi asilimia 2.11 mwaka 2025, huku mamlaka hiyo ikilenga kufikisha mchango huo asilimia tano ifikapo mwaka 2050. Amefafanua ongezeko hilo linaashiria kuimarika kwa matumizi ya huduma za bima nchini, ambapo idadi ya watumiaji imeongezeka kutoka milioni 5.6 mwaka 2021 hadi milioni 26.8 mwaka 2025. “Mafanikio hayo yanaonyesha kuongezeka kwa uelewa wa wananchi kuhusu umuhimu wa bima katika kulinda mali, afya, biashara na uwekezaji dhidi ya vihatarishi mbalimbali. “Aidha ajira rasmi katika sekta hiyo zimeongezeka kutoka 3,777 mwaka 2021 hadi 15,568 mwaka 2025, huku matumizi ya huduma za bima kwa kila Mtanzania yakipanda kutoka Sh15,560 hadi Sh67,455 katika kipindi hicho.” Dkt. Saqware amesema ukubwa wa soko la bima nao umeongezeka, ambapo thamani ya ada za bima zilizokusanywa imepanda kutoka Sh bilioni 911 mwaka 2021 hadi Sh trilioni 2.55 mwaka 2025. Amesema mali za kampuni za bima zimeongezeka kutoka Sh bilioni 979 mwaka 2021 hadi Sh trilioni 2.2 mwaka 2025, huku thamani ya mali zilizowekewa kinga ya bima ikipanda kutoka Sh bilioni 367 hadi Sh trilioni 1.29. Ameongeza sekta hiyo imeendelea kuimarika katika ulipaji wa madai, ambapo takwimu za mamlaka zinaonyesha kuwa asilimia 95 ya madai hulipwa, huku changamoto zinazobaki zikihusishwa na masuala ya nyaraka na uchunguzi wa udanganyifu.
Mon, 16 Nov 2026 17:43:39 +0000MCHENGERWA: ATAKA UCHUNGUZI UFANYIKE HOSPITALI YA WILAYA YA MAFIA
Na John Mapepele, Mafia Waziri wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa amemtaka Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt. Grace Magembe kuunda Kamati ya uchunguzi ili kuchunguza utolewaji wa huduma katika Hospitali ya Wilaya ya Mafia ili kuboresha huduma katika hospitali hiyo. Mhe. Mchengerwa ametoa kauli hiyo leo Novemba 16, 2026 baada ya kufanya ziara ya kikazi na kukagua maeneo mbalimbali ya Hospitali hiyo ambapo hakuridhishwa na utendaji kazi. Ninamuelekeza Katibu Mkuu kuunda timu kuja kufanya uchunguzi na kubaini changamoto ili kuja na suluhisho la maboresho ya kudumu katika hospitali Amesema dhamira ya Serikali kwa sasa ni kuifanya hospitali hiyo kutoa huduma za afya kwa kiwango cha kisasa na kuachana na mazoea. amefafanua sababu za kuifanya Hospitali hiyo kutoa huduma kwa kiwango cha kisasa kuwa ni pamoja na sehemu ya kisiwa hicho kuwa na Hifadhi ya Bahari ambayo huleta wageni wengi kutoka sehemu mbalimbali duniani. "Sote tunajua eneo hili la mafia ni eneo la kimkakati katika nchi yetu lina Hifadhi ya Bahari ambayo inatembelewa na watalii wengi hivyo pindi wanapopata shida za kiafya lazima tuwe na hospitali inayoweza kutoa huduma ya uhakika tofauti na sasa". Ameongeza Mhe. Mchengerwa Aidha, ameitaja sababu nyingine kuwa kisiwa cha Mafia kipo pembeni mwa Tanzania bara na bado hakuna usafiri wa uhakika hivyo ni muhimu kuwa na huduma zilizoboreka. Ametoa wiki mbili kwa uongozi wa hospitali hiyo kufunga mashine za kisasa za X-ray ambazo imepelekwa kwenye zahanati ya Chole. "Naelekeza ile X-ray Mashine ya kisasa ambayo haijafungwa kwenye zahanati ya Chole sasa ije ifungwe hapa kwa kuwa hapa kuna uhitaji zaidi kuliko kule." amesisitiza Mhe. Waziri Mchengerwa. Katika ziara hiyo ambayo aliambatana na Mkurugenzi wa Idara Kinga Dkt. Hamad Nyembea alipata fursa ya kuongea na wagonjwa waliofika kutibiwa.
Mon, 16 Nov 2026 17:50:52 +0000WAFUGAJI KIBAHA WATAKIWA KUFUGA KISASA KUNASA SOKO LA NJE-MAGOGWA
Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha WAFUGAJI katika Manispaa ya Kibaha mkoani Pwani wametakiwa kuboresha ufugaji kwa kuzingatia kanuni za kisasa ili kukidhi vigezo vya masoko ya nje na ndani ya nchi, ikiwemo kupanda majani ya malisho, kutoa chanjo kwa mifugo na kutumia mfumo wa ufugaji wa ndani (zero grazing). Hatua hiyo inalenga kuongeza ubora na uzalishaji wa mifugo, kudhibiti magonjwa pamoja na kupunguza migogoro kati ya wakulima na wafugaji. Wito huo umetolewa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Kibaha, Moses Magogwa, Novemba 16, 2026, wakati akizindua awamu ya pili ya zoezi la chanjo na utambuzi wa mifugo kwa ruzuku, eneo la Mtakuja, Kata ya Pangani, kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Fadhil Nkurlu. Magogwa alisema wafugaji wamekuwa wakikosa fursa za soko la nje kutokana na kutofikia vigezo vinavyohitajika, huku akitaja uwepo wa viwanda vya kuchakata nyama vya Tan Choice na Union Meat kuwa fursa inayopaswa kutumiwa na wafugaji wa eneo hilo. Alisema viwanda hivyo vimekuwa vikikabiliana kutopata mifugo inayokidhi mahitaji yake, hivyo ni muhimu wafugaji kuboresha mbinu za ufugaji ili kuongeza uzalishaji na ubora wa mifugo inayozalishwa. Alieleza kuwa Serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imekuja na mpango wa chanjo na utambuzi wa mifugo kwa ruzuku ili kukabiliana na magonjwa mbalimbali, ikiwemo homa ya mapafu kwa ng'ombe, pamoja na kuweka alama za utambulisho zitakazosaidia kudhibiti wizi wa mifugo. Aidha, Magogwa aliwataka wataalamu wa mifugo kuendelea kutoa elimu kwa wafugaji kuhusu ufugaji wa kisasa, ikiwemo kuwatembelea katika shamba la mbegu za majani lililopo Vikuge, Kata ya Soga, ili kujifunza namna ya kupanda na kuzalisha malisho kwa ajili ya mifugo yao na hivyo kupunguza tabia ya kuhama hama kutafuta chakula. Kwa upande wake, mfugaji wa Mtaa wa Mtakuja, Twalibu Selemani, alisema mpango huo wa miaka mitano ni mkombozi kwao kwa kuwa utasaidia kukabiliana na changamoto ya vifo vya mifugo vinavyotokana na magonjwa pamoja na wizi unaochangiwa na kutokuwepo kwa alama za utambulisho. Naye Daktari wa Mifugo wa Manispaa ya Kibaha, Chiza Martin, alisema Serikali imetoa chanjo kwa ruzuku pamoja na kuweka miundombinu wezeshi kwa ajili ya kurahisisha utekelezaji wa zoezi hilo. Alisema kabla ya kuanza kwa mpango huo, wafugaji walikuwa wakichangia Sh 1,500 kwa chanjo ya ng'ombe, Sh 300 kwa mbuzi na kondoo, huku chanjo ya kuku ikitolewa bure. Alifafanua kuwa chanjo hizo zinalenga kukabiliana na magonjwa ya homa ya mapafu, sotoka na mdondo (kideli). Alisema Manispaa ya Kibaha ina jumla ya ng'ombe 85,000, mbuzi 65,000 na kuku 300,000, huku katika awamu hii Serikali ikiwa imeanza kutoa chanjo kwa ng'ombe 2,000, kuku 150,000 na mbuzi 1,500.
Mon, 16 Nov 2026 17:55:32 +0000Krismasi Yazidi Kunoga! Kwa Wateja wa Meridianbet
MERIDIANBET imekuja na zawadi nyingine ya burudani kwa wapenzi wa michezo ya kasino kupitia Xmas Guardians Megaways, mchezo maalumu kutoka Pragmatic Play unaobeba mvuto wa sikukuu za Krismasi. Mchezo huu unawaalika wateja kuingia katika ulimwengu wa kipekee uliojaa mandhari ya sikukuu, ubunifu na msisimko wa kila mzunguko. Kupitia mchezo huu, wachezaji wanapata nafasi ya kuungana na Walinzi wa Krismasi katika safari inayochanganya burudani na mazingira ya kuvutia. Muonekano wake maalumu unaendana na furaha ya msimu wa sikukuu, na kuufanya kuwa chaguo la kipekee kwa wanaopenda michezo yenye mandhari tofauti. Moja ya vitu vinavyoongeza mvuto wa mchezo huu ni mfumo wa Megaways unaobadilisha idadi ya alama zinazoweza kuonekana katika kila mzunguko. Mfumo huu unaifanya kila spin kuwa na muundo tofauti, huku ukiwapa wachezaji uzoefu wa kipekee wanapoendelea kufurahia mchezo. Katika kipindi hiki maalumu, Meridianbet imewaandalia wateja wake fursa ya kufurahia Xmas Guardians Megaways kupitia michezo ya kasino . Ni sehemu ya burudani inayowaletea wapenzi wa michezo ya kasino chaguo jipya linaloendana na msimu wa Krismasi. Jambo la kuzingatia ni kwamba mchezo huu utapatikana kwa wateja wa Meridianbet pekee ndani ya kipindi maalumu cha promosheni. Hii inawapa wateja wa jukwaa hilo nafasi ya kipekee ya kujaribu mchezo huu kutoka Pragmatic Play na kujionea burudani yake. Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi. Walinzi wa Krismasi wanakuita, je, uko tayari kuungana nao? Tembelea Meridianbet, ingia kwenye sehemu ya kasino na ujaribu Xmas Guardians Megaways . Usikose burudani hii maalumu, cheza ufurahie ushindi. Jiunge na meridianbet leo ufurahie mzuka wa krismasi.
Tue, 17 Nov 2026 04:30:00 +0000Ushindi Mkubwa Unakusubiri Siku ya Leo
LEO hii unaweza ukaondoka na pesa ukibashiri mechi zako za ushindi, Kule Ulaya na huku Afrika mechi za Kimataifa bado zipo. Ingia kwenye akaunti yako na usuke jamvi lako sasa. Pesa ipo kwenye mechi ya Denmark dhidi ya Norway ambapo kwenye msimamo wa Kundi wanapishana pointi 3 pekee, hii ni mechi ambayo kila timu inahitaji ushindi ili kuweza kujiweka kwenye nafasi ya pili. Denmark ametoka kushinda mechi yake iliyopita hivyo anaingia kwenye mchezo huu akiwa na ari ya nguvu kabisa, halikadhalika kwa Norway naye amtoka kutoa dozi kubwa. Odds kubwa zipo kwenye mechi hii. Suka jamvi hapa. Timu zote zina wachezaji wakubwa na ambao wanacheza ligi kubwa wakiwemo kina Haaland, Hojlund, Odergaard na wengine wengi. Piga pesa kwenye michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi. Mechi nyingine ya UEFA NATIONS ni hii inayowakutanisha kati ya Wales dhidi ya Ureno moja ya mechi ambayo itakuwa ikitazamwa sana kutoka na matokeo yao yaliyopita, ambapo timu hizi zote zimetoka kupoteza michezo yao iliyopita. Lakini kwa upande wa Ureno hali imekuwa mbaya zaidi baada ya kupokea kipigo kizito kabisa huku maneno yakiibuka kwamba kutokuwepo kwa Ronaldo pia imechangia hivyo timu hiyo chini ya kocha mkuu Jorge inabidi ijiangalie. Jisajili hapa. Vijana wa Bellamy, Wales wanahitaji matokeo mazuri katika mchezo huu ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kuepuka kushuka daraja, lakini wanakutana na Ureno yenye kikosi chenye uzoefu na ubora mkubwa. Wales imekuwa na wakati mgumu katika michezo ya hivi karibuni, ikipoteza mechi nne kati ya tano za Nations League. Hata hivyo, uwepo wa Harry Wilson, David Brooks na Brennan Johnson unaweza kuongeza makali katika safu yao ya ushambuliaji. Kwa upande wa Ureno, licha ya kupokea kichapo cha mabao 4-1 dhidi ya Denmark katika mchezo uliopita, wana wachezaji wenye uwezo wa kubadilisha matokeo kama Bruno Fernandes, João Félix na Gonçalo Ramos. Pia, Ureno itahitaji kujipanga upya katika safu ya ulinzi kutokana na kukosekana kwa Rúben Dias, huku Wales ikitafuta kutumia faida ya kucheza nyumbani kupata matokeo mazuri. Kule kwa wakali wa ubashiri Tanzania, Meridianbet wao wanampa nafasi kubwa ya kushinda Ureno. Je wewe beti yako unaiweka kwa nani siku ya leo?. Jisajili hapa. Lakini pia ile michuano ya kufuzu AFCON inaendelea kwa michezo mingi lakini sisi tutajikta na mchezo wa Tanzania dhidi ya Nigeria huku hii ikiwa ni mechi ya kisasi kwa wenyeji baada ya kupigika kwenye mechi ya kwanza walipokutana. Kwenye Kundi lao, Tanzania ambao ni moja ya wenyeji wa michuano hii 2027, wapo nafasi ya mwisho ambayo ni ya mwisho, huku Nigeria wao wakiwa nafasi ya 2 kwenye msimamo baada ya kujikusanyia pointi zao 6. Chini ya kocha mkuu Gamondi bado Stars haipewi nafasi ya kushinda mechi hii kutokana na ubora wa wachezaji ambao timu pinzani inayo, pia wengi wa wachezaji wao wanacheza kwenye ligi kubwa Duniani. Je hii ni mechi ya wenyeji kushinda?. Suka jamvi hapa.
Tue, 17 Nov 2026 06:00:00 +0000Kampuni Mpya ya Betting Yazinduliwa, GBT Yasisitiza Uwajibikaji Kwa Jamii.
Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT) imezitaka kampuni za michezo ya kubahatisha (betting) na kasino, kuzingatia kikamilifu sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia sekta hiyo ili kulinda maadili na ustawi wa vijana, sambamba na kuongeza mchango wao katika maendeleo ya kijamii kupitia sekta za elimu, afya na michezo. Wito huo umetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa GBT, James Mbalwe, wakati akiongoza hafla ya uzinduzi wa kampuni mpya ya michezo ya kubashiri ya BetSasa, iliyoambatana na uzinduzi wa kampeni maalumu ya kuwazawadia wateja zawadi mbalimbali, ikiwemo gari jipya aina ya Jetour. Akizungumza katika hafla hiyo, Mbalwe alisema ongezeko la kampuni zinazoendesha shughuli za michezo ya kubahatisha nchini linapaswa kwenda sambamba na manufaa ya kiuchumi na kijamii kwa taifa, yakiwemo mapato ya Serikali na mchango katika kuboresha huduma za kijamii. “Tunawakaribisha BetSasa katika soko la Tanzania. Tumeona wameanza vizuri kwa kuja na kampeni hii inayolenga kuwazawadia wateja wao zawadi mbalimbali, ikiwemo gari jipya la kisasa. Hata hivyo, tunatoa wito kwao na kampuni nyingine katika sekta hii kuongeza tija ya shughuli zao kwa kuhakikisha wanarejesha kwa jamii kupitia kusaidia sekta za afya, elimu, michezo na maeneo mengine muhimu ya maendeleo,” alisema Mbalwe. Aidha, aliwataka washiriki wa michezo ya kubahatisha, hususan vijana, kushiriki kwa uwajibikaji na kwa kiasi, huku wakitambua umuhimu wa kutenga muda na rasilimali zao kwa ajili ya kazi, shughuli za uzalishaji na majukumu mengine ya kijamii. Akizungumzia kampeni hiyo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa BetSasa, Jimmy Kenneth, alisema kampeni hiyo itadumu kwa kipindi cha mwaka mmoja na inajulikana kwa jina la “Kusanya Point, Usepe na Jetour”, ikiwa na lengo la kuwapa wateja fursa ya kushinda zawadi mbalimbali, kuanzia fedha taslimu kila wiki hadi gari jipya aina ya Jetour. “Promosheni hii imeandaliwa mahususi kwa ajili ya wadau na wateja wetu. Kupitia kampeni hii, tutakuwa tukiwazawadia washindi 50 fedha taslimu kila wiki, huku zawadi kubwa ikiwa ni gari jipya aina ya Jetour litakalotolewa kila baada ya miezi mitatu,” alisema. Aliongeza kuwa BetSasa imejipanga kuendesha shughuli zake kwa kuzingatia sheria, kanuni, masharti na miongozo ya mamlaka zinazosimamia sekta ya michezo ya kubahatisha nchini, sambamba na kutekeleza wajibu wake Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), James Mbalwe (wa kwanza kulia), akikagua gari jipya aina ya Jetour litakalotolewa kama zawadi kwa washindi wa kampeni ya BetSasa, kampuni mpya ya michezo ya kubashiri nchini. Kampeni hiyo inayojulikana kwa jina la “Kusanya Point, Usepe na Jetour” inawapa wateja fursa ya kushinda zawadi mbalimbali, zikiwemo fedha taslimu kwa washindi 50 kila wiki na gari jipya aina ya Jetour kila baada ya miezi mitatu. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi na Mmiliki wa BetSasa, Vakhtang Nikoleishvili (kushoto), pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Jimmy Kenneth (katikati) Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), James Mbalwe (kushoto), sambamba na Mkurugenzi na Mmiliki wa BetSasa, Vakhtang Nikoleishvili (katikati), pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Jimmy Kenneth (kulia) wakijipongeza wakati wakionyesha zawadi ya gari jipya aina ya Jetour litakalotolewa kama zawadi kwa washindi wa kampeni ya BetSasa, kampuni mpya ya michezo ya kubashiri nchini. Kampeni hiyo inayojulikana kwa jina la “Kusanya Point, Usepe na Jetour” inawapa wateja fursa ya kushinda zawadi mbalimbali, zikiwemo fedha taslimu kwa washindi 50 kila wiki na gari jipya aina ya Jetour kila baada ya miezi mitatu Akizungumzia kampeni hiyo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa BetSasa, Jimmy Kenneth (alieshika mic) alisema kampeni hiyo itadumu kwa kipindi cha mwaka mmoja na inajulikana kwa jina la “Kusanya Point, Usepe na Jetour”, ikiwa na lengo la kuwapa wateja fursa ya kushinda zawadi mbalimbali, kuanzia fedha taslimu kila wiki hadi gari jipya aina ya Jetour.
Tue, 17 Nov 2026 08:30:00 +0000WAZIRI MKUU AIPONGEZA WIZARA YA UCHUKUZI KWA UFANISI WA USHIRIKIANO NA SEKTA BINAFSI, AITAKA KUONGEZA KASI KUELEKEA DIRA 2050
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, ameipongeza Wizara ya Uchukuzi kwa hatua zilizopigwa katika kuendeleza miundombinu na huduma za uchukuzi kupitia ushirikiano na sekta binafsi, huku akisisitiza kuongezwa kwa kasi, ufanisi na uwajibikaji katika utekelezaji wa miradi kuelekea Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 Dkt. Nchemba ametoa pongezi hizo Novemba 16, 2026, wakati akifungua Mkutano wa 19 wa Tathmini ya Pamoja ya Sekta ya Uchukuzi (JTSR) jijini Mwanza, akieleza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi katika kuongeza uwekezaji na kuboresha utoaji wa huduma za uchukuzi Amesisitiza kuwa pamoja na hatua zilizofikiwa, sekta hiyo inapaswa kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi, kuimarisha matengenezo ya miundombinu na usalama, pamoja na kuweka mikakati ya kukabiliana na changamoto za upungufu wa fedha na ucheleweshaji wa miradi Akitoa salamu za Wizara, Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, amesema Serikali imeendelea kupiga hatua katika kuendeleza miundombinu ya reli, barabara, bandari na anga, sambamba na kuimarisha mifumo ya udhibiti na usimamizi wa sekta hiyo Amesema mkutano huo unaofanyika Novemba 16–18, 2026, wenye kaulimbiu ya “Kuharakisha Utoaji wa Huduma Jumuishi za Uchukuzi, Ufadhili Endelevu na Uwajibikaji wa Sekta kuelekea Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050” ni jukwaa muhimu la kutathmini mafanikio, kubaini changamoto na kuweka mikakati ya kuongeza ufanisi wa sekta Awali, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Abubakar Assenga, ameipongeza Serikali kwa uwekezaji katika miundombinu ya uchukuzi na kusisitiza umuhimu wa kuimarisha usimamizi wa miradi ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati na kuleta tija kwa wananchi na taifa. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba akionesha tuzo mara baada ya kukabidhiwa na Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 19 wa Tathmini ya Pamoja ya Sekta ya Uchukuzi (JTSR) jijini Mwanza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba akipokea tuzo kutoka kwa Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 19 wa Tathmini ya Pamoja ya Sekta ya Uchukuzi (JTSR) jijini Mwanza. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba akimkabidhi tuzo Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 19 wa Tathmini ya Pamoja ya Sekta ya Uchukuzi (JTSR) jijini Mwanza. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba akizungumza na wadau mbalimbali wa Usafirishaji wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 19 wa Tathmini ya Pamoja ya Sekta ya Uchukuzi (JTSR) jijini Mwanza. Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa akisoma hotuba pamoja na kumkaribisha mgeni rasmi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 19 wa Tathmini ya Pamoja ya Sekta ya Uchukuzi (JTSR) jijini Mwanza. Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Abubakar Assenga akitoa salamu za Kamati ya Bunge wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 19 wa Tathmini ya Pamoja ya Sekta ya Uchukuzi (JTSR) Mkutano ukiendelea Picha za pamoja
Tue, 17 Nov 2026 14:16:48 +0000TRA DODOMA YAANZA RASMI KAMPENI YA UKAGUZI WA BIDHAA NA KUTOA ELIMU KUHUSU STEMPU ZA KODI ZA KIELEKTRONIKI
Kaimu Meneja wa TRA Mkoa wa Dodoma, Aubrey Silayo,akizungumza na waaandishi wa habari leo Novemba 17,2026 jijini Dodoma kuhusu matumizi ya mfumo wa Stempu za kodi za Kielektroniki kwenye vinywaji na bidhaa nyingine. Na.Mwandishi Wetu – DODOMA MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Dodoma imeanza rasmi kampeni ya ukaguzi wa bidhaa na kutoa elimu kwa umma kuhusu stempu za kodi za kielektroniki katika wilaya zote za Mkoa wa Dodoma. Kampeni hiyo inalenga kuhakikisha bidhaa zinazouzwa sokoni zinatumia stempu halali za kielektroniki, kudhibiti matumizi ya stempu bandia na bidhaa zisizolipiwa ushuru, pamoja na kuongeza uelewa kwa wafanyabiashara na wananchi kuhusu umuhimu wa kuhakiki stempu kabla ya kununua au kutumia bidhaa. Akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 17, 2026 jijini Dodoma, Kaimu Meneja wa TRA Mkoa wa Dodoma, Aubrey Silayo, amesema zoezi hilo litahusisha ukaguzi wa uhalali wa stempu zinazobandikwa kwenye bidhaa mbalimbali, zikiwemo vinywaji, bia, pombe kali, sigara na mvinyo, pamoja na kutoa elimu kwa wafanyabiashara na wananchi kuhusu umuhimu wa kuhakiki stempu kabla ya kununua au kutumia bidhaa. Silayo amesema matumizi ya stempu za kodi za kielektroniki ni sehemu ya jitihada za Serikali kuimarisha usimamizi wa kodi, kudhibiti bidhaa zisizo halali na kuhakikisha wafanyabiashara wote wanatekeleza wajibu wao wa kulipa ushuru kwa mujibu wa sheria. “Mfumo wa stempu za kodi ulianza kutumika nchini mwaka 1998, kabla ya Serikali kupitia TRA kuanzisha mfumo wa kisasa wa stempu za kielektroniki mwaka 2018, ambao umechukua nafasi ya stempu za karatasi zilizokuwa katika mazingira rahisi ya kughushiwa,” amesema Bw. Silayo. Ameeleza kuwa mfumo huo wa kidijitali unawezesha kila bidhaa kuwa na namba maalumu ya utambulisho pamoja na alama za kiusalama, zinazosaidia kutambua uhalali wa bidhaa na kutoa nafasi kwa watumiaji kufanya uhakiki kabla ya kuzitumia. Silayo amesema hatua hiyo siyo tu inalenga kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali, bali pia inalinda afya za wananchi dhidi ya bidhaa bandia au ambazo hazijathibitishwa ubora na usalama wake na mamlaka husika. “Wananchi wanaweza kutumia simu janja kupakua programu ya HAKIKI STEMPU, ambayo inawawezesha kuhakiki bidhaa wanazokusudia kununua au kutumia kwa kuchunguza uhalali wa stempu iliyobandikwa kwenye bidhaa husika,” amesisitiza. Ameongeza kuwa endapo mtumiaji atabaini bidhaa yenye stempu isiyothibitishwa au inayotia shaka, anaweza kutoa taarifa kupitia mfumo huo kwa kueleza eneo alilonunua bidhaa, aina ya bidhaa na kuambatanisha picha pamoja na taarifa nyingine zitakazosaidia TRA kufanya ufuatiliaji. Katika hatua nyingine, Silayo amewatahadharisha wafanyabiashara, watengenezaji na waagizaji wa bidhaa kuhakikisha wanatumia stempu sahihi za kielektroniki kabla ya kuingiza bidhaa sokoni, akisisitiza kuwa matumizi ya stempu bandia ni kosa linaloweza kuchukuliwa hatua za kisheria. Amesema TRA imeimarisha uwezo wa kubaini stempu za kughushi kwa kutumia mifumo ya kiintelijensia pamoja na skana maalumu, hivyo wahusika wanaojihusisha na udanganyifu huo watabainika na kuwajibishwa kwa mujibu wa sheria. Kwa mujibu wa Silayo, adhabu kwa watakaobainika kutumia vibaya stempu za kielektroniki ni faini isiyopungua Sh milioni tano na isiyozidi Sh milioni 50, au kifungo kisichozidi miaka mitatu, au adhabu zote mbili kwa pamoja. Amesisitiza kuwa jukumu la kuhakikisha bidhaa zinazotumika ni halali halipaswi kuachwa kwa TRA pekee, bali linahitaji ushirikiano wa wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla, huku akiwataka kutoa ushirikiano kwa maafisa watakaotekeleza zoezi la ukaguzi katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo. Amesema matumizi sahihi ya stempu za kielektroniki yataimarisha ushindani wa haki katika biashara, kudhibiti ukwepaji wa kodi, kuongeza mapato ya Serikali na kulinda afya za wananchi. Hata hivyo, amewahimiza wananchi kujenga utamaduni wa kuhakiki stempu za kodi kabla ya kutumia bidhaa, akieleza kuwa hatua hiyo ni sehemu ya uwajibikaji wa kila mmoja katika kulinda uchumi wa nchi na usalama wa jamii. HAKIKI STEMPU, TUMIA BIDHAA HALALI, LINDA AFYA YAKO! Kaimu Meneja wa TRA Mkoa wa Dodoma, Aubrey Silayo,akizungumza na waaandishi wa habari leo Novemba 17,2026 jijini Dodoma kuhusu matumizi ya mfumo wa Stempu za kodi za Kielektroniki kwenye vinywaji na bidhaa nyingine.
Tue, 17 Nov 2026 14:19:27 +0000TANZANIA, IAEA NA EU KUIMARISHA USALAMA WA MIONZI KUPITIA MAFUNZO YA KIKANDA
NA MWANDISHI WETU - ARUSHA Serikali ya Tanzania imeendelea kuimarisha juhudi za kuhakikisha usalama wa mionzi kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomu (IAEA) na Umoja wa Ulaya (EU), kupitia mafunzo ya kikanda yanayolenga kuwajengea uwezo wataalamu katika uandaaji wa viwango maalum vya usalama wa mionzi kwa vifaa vinavyokusudiwa kutumika tena, kuchakatwa au kutupwa. Mafunzo hayo ya siku tano, yanayofanyika jijini Arusha kuanzia tarehe 16 hadi 20 Novemba 2026, yanalenga kuimarisha uwezo wa nchi katika kufanya tathmini ya viwango vya mionzi kwenye vifaa mbalimbali ili kuhakikisha kuwa matumizi yake hayaleti madhara kwa afya za binadamu na mazingira. Akifungua mafunzo hayo leo, Novemba 16, 2026, kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo, Mkurugenzi Msaidizi wa Sayansi na Teknolojia, Dkt. Harun Makandi, amesema mafunzo hayo ni muhimu katika kuimarisha uwezo wa kitaalamu na mifumo ya udhibiti wa usalama wa mionzi, hususan katika kipindi ambacho matumizi ya teknolojia ya nyuklia na vyanzo vya mionzi yanaendelea kuongezeka katika sekta mbalimbali. Dkt. Makandi ameeleza kuwa uandaaji wa viwango maalum vya kuondoa vifaa kwenye udhibiti wa mionzi (Specific Clearance Levels) ni hatua muhimu inayowezesha kufanya maamuzi ya kitaalamu kuhusu vifaa vinavyoweza kutumika tena, kuchakatwa au kutupwa bila kuhatarisha usalama wa wananchi, wafanyakazi na mazingira. Katika mafunzo hayo, washiriki watajifunza masuala mbalimbali yakiwemo misingi ya ulinzi dhidi ya mionzi, taratibu za kuandaa viwango maalum vya usalama, tathmini ya athari zinazoweza kutokana na mionzi pamoja na matumizi ya mbinu za kitaalamu katika kufanya maamuzi kuhusu usimamizi wa vifaa vyenye mionzi. Aidha, mafunzo hayo yanatoa fursa kwa wataalamu kutoka nchi mbalimbali kubadilishana uzoefu, kujadili changamoto na kuimarisha ushirikiano wa kikanda katika kuhakikisha kuwa viwango vya usalama wa mionzi vinazingatiwa kwa mujibu wa miongozo na viwango vya kimataifa. Mafunzo hayo yanahusisha wataalamu kutoka Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomu (IAEA), Umoja wa Ulaya (EU), Shirika la Nishati ya Nyuklia la Afrika Kusini (NECSA) pamoja na washiriki kutoka nchi mbalimbali, huku Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) ikiwa mwenyeji wa mafunzo hayo. Kupitia mafunzo hayo, Tanzania inaendelea kuimarisha nafasi yake katika usimamizi wa matumizi salama ya teknolojia ya nyuklia na mionzi kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi, sambamba na kulinda mazingira, wafanyakazi, wagonjwa na wananchi dhidi ya madhara ya mionzi.
Tue, 17 Nov 2026 14:20:37 +0000MWIGULU KUMWAKILISHA RAIS SAMIA UZINDUZI WA KITAMBULISHO CHA TAIFA NOV 18 PWANI
Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, anatarajiwa kumwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uzinduzi wa Kitambulisho cha Taifa Kilichoboreshwa, toleo la mwaka 2026, utakaofanyika Novemba 18, katika Viwanja vya Stendi ya zamani ya Maili Moja, Kibaha mkoani Pwani. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Stanslaus Nyongo, alisema Waziri Mkuu atakuwa mkoani humo Novemba 18 na 21 mwaka huu ambapo baada ya uzinduzi huo atafanya mkutano wa hadhara na wananchi wa Manispaa ya Kibaha. Nyongo amesema uzinduzi huo ni hatua muhimu katika kuboresha mfumo wa utambulisho wa Taifa, kuongeza ufanisi wa utambuzi wa watu, kuimarisha usalama wa taarifa za wananchi na kurahisisha upatikanaji wa huduma zinazohitaji utambulisho rasmi. Ameeleza sambamba na uzinduzi huo, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) itazindua huduma mpya ya Huduma Bila Foleni, inayolenga kupunguza muda wa wananchi kusubiri na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma. Amefafanua kuwa wananchi kutoka wilaya zote za Mkoa wa Pwani watapata huduma mbalimbali katika eneo la uzinduzi, zikiwemo usajili wa ambao hawajajisajili, uhakiki na marekebisho ya taarifa, ufuatiliaji wa maombi pamoja na utoaji wa vitambulisho vilivyokamilika kwa wenye namba za utambulisho wa Taifa ambao hawajavichukua. Vilevile, wananchi watapata elimu na ushauri kuhusu taratibu na huduma zinazotolewa na NIDA, huku akiwahimiza kujitokeza kwa wingi kutumia fursa hiyo na kushiriki mkutano wa hadhara utakaofanyika baada ya uzinduzi. Katika hatua nyingine, Nyongo amesema Novemba 21 mwaka huu, Waziri Mkuu atafanya ziara katika Halmashauri ya Chalinze, wilayani Bagamoyo, ambako atafanya mkutano wa hadhara katika Viwanja vya Polisi Chalinze.
Tue, 17 Nov 2026 14:23:26 +0000PSSSF YASHIRIKI MAONESHO YA MKUTANO MKUU WA 40 WA ALAT JIJINI MWANZA
Meya wa Jiji la Mwana na Mwenyekiti mpya ALAT Taifa, akipokea zawadi kutoka kwa Meneja PSSSF Kanda ya Ziwa Mashariki, CPA Rajabu Kinande alipotembelea huduma za PSSSF zinazoendelea kutolewa katika maonyesho yanayofanyika sambamba na Mkutano Mkuu wa 40 ALAT Bi. Glory Selene Chidumizi, Afisa Huduma Kwa Wateja wa PSSSF Makao Makuu, akimuhudumia mwanachama wa Mfuko Bi. Diana Zacharia Sonno, katika maonyesho yanayoendelea sambamba na mkutano mkuu wa ALAT Bi. Aziza Baruti Mkurugenzi Halmashauri ya Butiama, akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea huduma za PSSSF zinazoendelea kutolewa katika maonyesho yanayofanyika sambamba na Kikao kikuu cha ALAT jijini Mwanza. Mhe. Isack Joseph Copriano, Mbunge wa Monduli (wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa PSSSF mara baada ya kutembelea banda la PSSSF katika maonyesho yanayofanyika sambamba na kikao cha 40 cha Jumuiya ya Serikali za Mitaa (ALAT) Meneja wa kanda ya Ziwa Mashariki CPA. Rajabu Kinande wakiwa na Afisa wa PSSSF Bw.Nyanga M . Makani wakufatilia ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 40 wa ALAT uliofunguliwa leo na Mh. Mwigulu Nchemba jijini Mwanza Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) unashiriki katika maonesho yanayoambatana na Mkutano Mkuu wa 40 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), yanayofanyika jijini Mwanza. Mkutano huo umefunguliwa rasmi Novemba 16, 2026, na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, na unatarajiwa kuhitimishwa Novemba 20, 2026. Akizungumzia ushiriki wa Mfuko katika maonesho hayo, Meneja wa Kanda ya Ziwa Mashariki wa PSSSF, CPA Rajab Kinande, amesema mkutano huo ni fursa muhimu kwa Mfuko kukutana na wadau wake, hususan watumishi wa Serikali za Mitaa, ambao ni miongoni mwa wanachama wake. Amesema kupitia maonesho hayo, watumishi hao watapata fursa ya kufahamu majukumu ya Mfuko, huduma zinazotolewa pamoja na maboresho mbalimbali yaliyofanyika kwa lengo la kuongeza ufanisi na kuboresha utoaji wa huduma kwa wanachama na wastaafu na hatimaye kufikia lengo kama kauli mbiu isemavyo ‘tunalipa jana’ Aidha, amesema ushiriki wa PSSSF katika maonesho hayo ni sehemu ya jitihada za Mfuko za kusogeza huduma karibu na wanachama wake, kuwaelimisha kuhusu haki na stahiki zao pamoja na kuwajengea uelewa wa namna bora ya kutumia mifumo ya kidijitali inayowezesha upatikanaji wa huduma kwa urahisi na haraka.
Tue, 17 Nov 2026 14:27:26 +0000NDEJEMBI ASHIRIKI VIKAO VYA CCM MKOA WA DAR ES SALAAM
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Mlezi wa Chama hicho Mkoa wa Dar es Salaam, ameshiriki vikao vya Kamati ya Siasa na Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam. Vikao hivyo vilivyofanyika katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, vililenga kutathmini utekelezaji wa majukumu ya Chama hicho mkoani humo. Hii ni mara ya kwanza kwa Mhe. Ndejembi kushiriki vikao hivyo tangu alipoteuliwa na Kamati Kuu ya CCM kuwa mlezi wa mkoa huo. Awali, alipowasili, alipokelewa na viongozi na wanachama wa CCM, huku mapokezi hayo yakihusisha gwaride rasmi la vijana wa UVCCM na kuvikwa skafu maalumu iliyoashiria amani, umoja na uwajibikaji
Tue, 17 Nov 2026 14:55:42 +0000TRA YAENDELEA KUBORESHA MFUMO WA KODI KUVUTIA UWEKEZAJI
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imeeleza dhamira yake ya kuendelea kusimamia mfumo wa kodi unaovutia uwekezaji, kukuza biashara na kuwezesha ukuaji wa uchumi wa Taifa, kwa kuzingatia misingi ya haki, usawa na uwazi katika usimamizi wa kodi. Hayo yameelezwa leo, Novemba 17, 2026, na Kamishna Mkuu wa TRA, Yusuph Mwenda, katika mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini Korea Kusini, Noel Kaganda, yaliyolenga kuimarisha ushirikiano katika masuala ya kodi, biashara na uwekezaji. Akizungumza katika mazungumzo hayo, Balozi Kaganda ameipongeza TRA kwa mafanikio yaliyopatikana katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali, huku akitambua juhudi zinazofanywa na Mamlaka hiyo katika kuboresha mifumo ya kodi na kuongeza ufanisi wa ukusanyaji wa mapato. Aidha, amesisitiza umuhimu wa kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na Korea Kusini. Kwa upande wake, Mwenda amesema TRA inaendelea kuboresha mifumo na huduma zake kwa kutumia teknolojia, kurahisisha taratibu za kikodi na kutoa elimu kwa walipakodi ili kuhakikisha mazingira ya kodi yanawezesha biashara na uwekezaji, sambamba na kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali. Aidha, Mwenda amesisitiza utayari wa TRA kuendeleza ushirikiano na Korea Kusini katika maeneo yenye maslahi ya pamoja, ikiwemo kubadilishana uzoefu na kujifunza mifumo bora ya usimamizi wa kodi, hatua itakayochangia kuimarisha mazingira ya uwekezaji, kukuza biashara na kuongeza mchango wa sekta binafsi katika maendeleo ya uchumi wa Taifa.
Tue, 17 Nov 2026 15:28:12 +0000WMA YATOA ELIMU YA VIPIMO SAHIHI KWA MAAFISA USAFIRISHAJI DODOMA.
Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Dodoma umetoa elimu ya vipimo sahihi kwa maafisa usafirishaji ili kuwajengea uelewa wa umuhimu wa kuhakiki vipimo wanaponunua bidhaa mbalimbali kwa niaba ya wananchi, zikiwemo gesi ya kupikia, nyama, vyakula na nafaka, hatua inayolenga kulinda haki za walaji na kupunguza udanganyifu katika biashara. Akizungumza Novemba 17, 2026, wakati wa kutoa elimu hiyo Kaimu Meneja wa WMA Mkoa wa Dodoma, Edward Patrick, amesema maafisa usafirishaji ni wadau muhimu katika kufikisha elimu ya vipimo sahihi kwa jamii kutokana na nafasi yao ya kuunganisha wauzaji na walaji katika shughuli za kila siku, amesema wanapaswa kuhakikisha wanashuhudia upimaji wa bidhaa wanazonunua ili kujiridhisha kuwa kiasi wanachopokea kinalingana na kile walicholipia. Amesema changamoto ya upungufu wa bidhaa kama gesi na nyama inaweza kupungua iwapo maafisa hao watahakikisha wanapimiwa bidhaa wanaponunua badala ya kuamini maelezo ya wauzaji pekee, aidha amewataka kukagua mizani inayotumika kuhakikisha ina stika ya WMA inayoonesha kuwa imehakikiwa, imewekwa katika hali sahihi na iko tayari kutumika kabla ya upimaji kuanza. Patrick amesema WMA inaendelea kupanua wigo wa utoaji elimu kwa makundi mbalimbali ya jamii, ikiwemo wanafunzi kupitia klabu za vipimo shuleni na madiwani, ili kuwajengea wananchi uelewa wa haki zao na umuhimu wa kutumia vipimo sahihi, ameongeza kuwa Wakala unaendelea kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wanaokiuka sheria za vipimo, ikiwemo kuwafikisha mahakamani na kuwatoza faini, kwa lengo la kuhakikisha kila mmoja anazingatia matumizi ya vipimo sahihi kuelekea utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Maafisa Usafirishaji Mkoa wa Dodoma, Baraka Obadia Mbuye, amesema elimu hiyo imewajengea uelewa kuhusu wajibu wao katika kuhakikisha bidhaa wanazonunua kwa niaba ya wateja zinakuwa na vipimo sahihi, amewataka maafisa usafirishaji kuwa makini wanaponunua bidhaa, kushuhudia upimaji na kukagua alama za uhakiki wa WMA kwenye mizani na vifaa vya kupimia mafuta katika vituo vya mafuta ili kujiridhisha na usahihi wa vipimo. Naye Msemaji Mkuu wa Bodaboda na Bajaji Mkoa wa Dodoma, Simon Elias Mangula, ameishukuru WMA kwa kuwashirikisha katika elimu hiyo, akisema madereva wana nafasi muhimu ya kusaidia kulinda haki za wananchi kutokana na kushiriki mara kwa mara katika manunuzi ya bidhaa mbalimbali, hata hivyo, ameiomba WMA kuongeza ukaguzi katika masoko ya vijijini ambako wakulima wanakabiliwa na changamoto za vipimo wanapouza mazao yao, pamoja na kuimarisha ushirikiano na taasisi za bodaboda na bajaji katika kufikisha elimu hiyo kwa jamii. Amesisitiza kuwa ushirikiano kati ya Wakala wa Vipimo na maafisa usafirishaji ni muhimu katika kujenga jamii inayozingatia vipimo sahihi, huku akiwataka madereva wa bodaboda na bajaji kuwa waaminifu wanapotekeleza maagizo ya wateja, kuhakikisha bidhaa zinapimwa kwa usahihi na kuepuka vitendo vinavyoweza kusababisha hasara kwa wananchi, Utekelezaji wa elimu hiyo unatarajiwa kusaidia kuongeza uelewa wa walaji, kupunguza malalamiko na kuimarisha haki katika shughuli za manunuzi na biashara.
Tue, 17 Nov 2026 15:30:35 +0000SAMIA KALAMU AWARDS KUFANYIKA DESEMBA 5, WAANDISHI 64 WAFUZU
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Rolf Kibaje, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kukamilika kwa mchakato wa upigaji kura na waandishi 64 pamoja na vyombo vya habari 11 vilivyofuzu kuwania tuzo za Samia Kalamu Awards (SKA) 2026. Hafla ya kutangaza washindi inatarajiwa kufanyika Desemba 5, 2026, katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam. Na Karama Kenyunko Michuzi Tv RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya kutangaza washindi wa tuzo za uandishi wa habari za maendeleo za Samia Kalamu Awards (SKA) 2026, itakayofanyika Desemba 5 mwaka huu katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Katika tuzo hizo, waandishi wa habari 64 na vyombo vya habari 11 vimefuzu kuingia hatua ya mwisho ya kuwania tuzo hizo, baada ya kukamilika kwa mchakato wa tathmini na upigaji kura kwa umma. Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mhandisi Peter Mwasalyanda, Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano, Rolf Kibaje kuhusu kukamilika kwa mchakato huo, amesema jumla ya kazi 3,003 ziliwasilishwa kwa ajili ya kushindanishwa katika tuzo hizo. Amesema baada ya tathmini ya majaji, kazi 882 zilifuzu kuingia katika hatua ya upigaji kura kwa umma, ambapo jumla ya kura 317,399 zilipigwa "Waandishi waliofuzu wamepatikana kupitia mchakato wa upigaji kura kwa umma pamoja na tathmini ya majaji 19 waliobobea katika taaluma ya uandishi wa habari na mahusiano kwa umma...tathmini hiyo ilizingatia vigezo mbalimbali, vikiwemo ubora wa maudhui, uzingatiaji wa maadili ya taaluma, matumizi ya utafiti na takwimu, athari chanya kwa jamii na mchango katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2050. Tuzo hizo zinajumuisha tuzo za kisekta, tuzo za vyombo vya habari na tuzo maalum za kitaifa, huku zikitambua kazi za waandishi wa habari, maafisa habari na vyombo vya habari zilizochapishwa au kurushwa hewani ndani ya kipindi kilichoainishwa kwenye mwongozo wa tuzo. Mhandisi amesema washindani na mwitikio wa wananchi kupitia upigaji kura unaonesha umuhimu wa tuzo hizo katika kuhamasisha uandishi wa habari unaozingatia maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla. Aidha ameeleza kuwa, Orodha ya waandishi wa habari na vyombo vya habari vilivyofuzu kuingia hatua ya mwisho inapatikana kupitia tovuti ya www.samiawards.co.tz. na washiriki waliofuzu watapokea maelekezo kuhusu ushiriki wao katika hafla hiyo kutoka kwa kamati ya maandalizi. Samia Kalamu Awards ni tuzo maalum za kitaifa zilizoanzishwa mwaka 2024 kwa lengo la kutambua, kuenzi na kuhamasisha ubora, weledi na ubunifu katika uandishi wa habari na makala za maendeleo nchini. Tuzo hizo zinaratibiwa na TCRA kwa kushirikiana na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) na JAMU, kupitia kaulimbiu ya mwaka huu isemayo Kalamu kwa Maendeleo. Kaulimbiu hiyo inahimiza uzalishaji wa maudhui ya ndani yenye ubora yanayozingatia utafiti na takwimu, usahihi, weledi na maadili ya taaluma ya uandishi wa habari.
Tue, 17 Nov 2026 15:34:19 +0000RAIS SAMIA KUFUNGUA MKUTANO UWEKEZAJI MADINI,SERIKALI YAJIVUNIA
RAIS Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufungua Mkutano wa Saba wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini (TIMC), huku Serikali ikijivunia mafanikio ya sekta hiyo yanayooneshwa na kuongezeka kwa mchango wake katika Pato la Taifa, mapato na mauzo ya madini nje ya nchi. Mkutano huo utafanyika kuanzia Novemba 19 hadi 21, mwaka huu, katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam, ukiwa na washiriki 1,700 kutoka ndani na nje ya nchi ambao tayari wamethibitisha kushiriki. Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, amesema mafanikio yaliyopatikana katika sekta hiyo yametokana na juhudi za Serikali kuboresha usimamizi wa rasilimali za madini, kuongeza mapato, kuvutia uwekezaji na kuwawezesha wachimbaji wadogo. Amefafanua mkutano huo ni wa saba tangu kuanzishwa kwake mwaka 2019 na utatoa fursa ya kujadili mafanikio yaliyopatikana, changamoto zilizopo pamoja na fursa mpya za uwekezaji, hususan katika kuongeza thamani ya madini nchini. Amesema mkutano huo utafanyika chini ya kaulimbiu isemayo: “Madini Yaliyoongezwa Thamani, Chachu ya Ukuaji wa Viwanda na Uchumi.” Ameongeza kaulimbiu hiyo inalenga kuhamasisha uwekezaji katika uchakataji na uongezaji thamani wa madini ndani ya nchi ili sekta hiyo izalishe manufaa makubwa zaidi kwa uchumi na wananchi. Akielezea mafanikio ya sera ya ushirikishwaji wa Watanzania katika sekta ya madini, amesema ununuzi wa bidhaa na huduma kutoka kwa wazalishaji na watoa huduma wa ndani umeongezeka kutoka Sh.bilioni 884.09 mwaka 2010 hadi Sh.trilioni 5.2 mwaka 2025. Amesema ongezeko hilo linaonesha namna shughuli za uchimbaji madini zinavyoendelea kufungua fursa za kibiashara kwa kampuni za ndani na kuongeza ushiriki wa Watanzania katika mnyororo mzima wa thamani wa sekta hiyo. Katika hatua nyingine, amesema mchango wa sekta ya madini katika Pato la Taifa umeongezeka hadi kufikia asilimia 10.3 mwaka 2025, kutoka asilimia 7.8 mwaka 2024. Waziri Mavunde amesema ukuaji huo umechangiwa kwa kiasi kikubwa na kuongezeka kwa thamani ya madini yanayouzwa nje ya nchi, ambayo yalipanda kutoka Dola za Marekani bilioni 4.12 mwaka 2024 hadi bilioni 5.46 mwaka 2025. Kwa mujibu wa Waziri huyo, ongezeko hilo linaashiria kuimarika kwa nafasi ya sekta ya madini katika uchumi wa Taifa na uwezo wake wa kuchangia upatikanaji wa fedha za kigeni. Kuhusu mapato ya Serikali, amesema yameongezeka kutoka takribani Sh bilioni 526 katika mwaka wa fedha 2020/2021 hadi Sh trilioni 1.39 katika mwaka wa fedha 2025/2026. “Mafanikio hayo yanatokana na kuimarishwa kwa usimamizi wa shughuli za madini na mifumo ya ukusanyaji wa mapato, hatua iliyowezesha Serikali kunufaika zaidi na rasilimali hizo.” Akizungumzia ajira, Waziri Mavunde amesema hadi Aprili 2025, sekta hiyo ilikuwa imetoa ajira rasmi 10,874, ambapo asilimia 97.4 zilikuwa za Watanzania. Amesema takwimu hizo zinaonesha mchango wa sekta ya madini katika kupanua fursa za ajira kwa wananchi, kuongeza kipato na kukuza shughuli nyingine za kiuchumi zinazohusiana na uchimbaji na biashara ya madini. Hivyo amesema mkutano huo utakuwa jukwaa muhimu la kuwakutanisha wawekezaji, wadau wa sekta ya madini na Serikali kujadili namna ya kuongeza uwekezaji, kuimarisha ushiriki wa wazawa na kuhakikisha rasilimali za madini zinachangia zaidi katika maendeleo ya Taifa.
Tue, 17 Nov 2026 16:01:17 +0000SHULE YA SEKONDARI VUGA BAZO YANUFAIKA NA HOSTELI, VYOO 14 KUPITIA SHIRIKA LA BETTER WORLD CANADA
Wadau wa maendeleo waombwa kuongeza vitanda, nyumba za walimu na miundombinu mingine ili kuboresha mazingira ya kujifunzia na kuinua ufaulu wa wanafunzi. Na Mwandishi Wetu, Bumbuli SHULE ya Sekondari Vuga Bazo iliyopo Kata ya Soni, Halmashauri ya Bumbuli, Mkoa wa Tanga, imenufaika na ujenzi wa hosteli ya wavulana pamoja na matundu 14 ya vyoo, hatua inayotarajiwa kuondoa changamoto ya uhaba wa vyoo na umbali mrefu wa safari kwa wanafunzi. Mradi huo umefadhiliwa na Shirika la Better World Canada kwa kushirikiana na Shirika la Vuga Development Initiative kutekeleza mradi huo kwa kwa gharama ya shilingi Milioni 93. Akizungumza kuhusu manufaa ya mradi huo, Mkuu wa Shule ya Sekondari Vuga Bazo, Mathias Chambwite, alisema shule hiyo ilikuwa ikikabiliwa na changamoto kubwa ya uhaba wa matundu ya vyoo pamoja na kukosekana kwa hosteli kwa wanafunzi wanaotoka maeneo ya mbali. Alisema kabla ya msaada huo, shule ilikuwa na matundu 12 ya vyoo, hali iliyosababisha wanafunzi kusubiri kwa muda mrefu ili kupata nafasi ya kutumia vyoo kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi. Chambwite alisema kwa sasa shule imeongezewa matundu 14 na kufanya jumla ya matundu ya vyoo kufikia 26, ambayo yanakidhi mahitaji ya wanafunzi 390, wakiwemo wasichana 210 na wavulana 180. Alisema ujenzi huo umeondoa changamoto iliyokuwa ikiathiri mazingira ya kujifunzia na kwamba uwepo wa hosteli utawasaidia wanafunzi wanaotoka maeneo ya mbali kupata nafasi nzuri ya kulala, kupumzika na kujisomea. “Tunawashukuru sana wafadhili wa Better World Canada kwa kutusaidia kujenga hosteli na vyoo. Changamoto kubwa tuliyokuwa nayo ilikuwa miundombinu, lakini kupitia msaada huu tunaamini wanafunzi watapata mazingira mazuri ya kusoma na kufikia malengo yao,” alisema Chambwite. Alisema kwa upande wa Serikali, shule hiyo haina changamoto kubwa ya walimu, kwani ina walimu wa kutosha, walimu wa masomo ya sayansi pamoja na mtaalamu wa maabara. Hata hivyo, aliwaomba wadau wengine kuendelea kuisaidia shule hiyo, hasa kwa kuongeza vitanda vya hosteli, kujenga jengo la utawala na kuongeza nyumba za walimu ambazo bado hazitoshelezi mahitaji ya watumishi waliopo. Alisema shule hiyo ina idadi kubwa ya wanafunzi wa kike ambao wanahitaji mazingira bora ya kujifunzia ili waweze kutimiza ndoto zao, akibainisha kuwa jitihada za kuwawezesha wasichana kuendelea na masomo ni muhimu katika kukabiliana na changamoto zilizokuwa zikiwakwamisha hapo awali. Mratibu wa Shirika la Vuga Development Initiative, Rama Kaoneka aliwataka watu walisoma katika shule hiyo watambue nyumbani ni nyumbani hivyo ni vizuri wakumbuke na kurudisha fadhila zao ili wanafunzi waweze kusoma sehemu nzuri. Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Vuga, Jumaa Dhahabu, alisema wanamshukuru Mungu na wafadhili kwa kufanikisha ujenzi wa hosteli hiyo, akieleza kuwa awali wanafunzi walikuwa wakitembea umbali wa zaidi ya kilomita 18 kwenda na kurudi shuleni kila siku. Alisema hali hiyo ilikuwa ikiathiri maendeleo ya kitaaluma ya wanafunzi na kuchangia matokeo yasiyoridhisha, kutokana na uchovu waliokuwa wakipata wakati wa safari. “Tunawashukuru sana wafadhili kwa kuona changamoto iliyokuwa ikiikabili shule yetu. Tunaamini hosteli hii itabadilisha matokeo ya wanafunzi kwa sababu sasa watapata nafasi ya kukaa karibu na shule na kutumia muda mwingi kujisomea,” alisema Dhahabu. Aliwapongeza Shirika la Better World Canada pamoja na Kaoneka, Mkurugenzi wa Shirika la Vuga Development Initiative, kwa juhudi zake za kuunganisha jamii na wafadhili, huku akitoa wito kwa wadau wengine kujitokeza kusaidia ujenzi wa mabweni zaidi ili wanafunzi wengi waweze kupata huduma hiyo. Naye Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bumbuli, Magreth, aliishukuru Better World Canada kwa kuendelea kushirikiana na halmashauri katika sekta za elimu na afya, akizitaja kuwa ni maeneo muhimu yanayogusa maisha ya wananchi. Alisema pamoja na hosteli ya wavulana na matundu 14 ya vyoo, halmashauri inaomba wadau hao waendelee kusaidia miradi mingine ya maendeleo, ikiwemo ujenzi wa hosteli ya wasichana katika shule hiyo. Aidha, alisema halmashauri inahitaji shule nyingine ya sekondari yenye masomo ya sayansi kwa ngazi ya kidato cha tano na sita, ili kuwasaidia wanafunzi wanaofaulu kidato cha nne lakini wanashindwa kuendelea na masomo katika maeneo ya mbali kama Arusha, Kigoma na Dar es Salaam kutokana na changamoto za kifedha kwa wazazi. Alisema upatikanaji wa shule hiyo utasaidia wanafunzi wengi kuendelea na masomo ya sayansi, kufikia elimu ya juu na baadaye kuwa wataalamu watakaolisaidia eneo hilo. Pia aliomba msaada wa ujenzi wa jengo la utawala na upatikanaji wa vitanda ili hosteli hiyo iweze kuanza kupokea wanafunzi kuanzia Januari mwakani. Kwa upande wake, Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Lushoto ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bumbuli, Zepahia Sumaye, aliwashukuru wafadhili na Shirika la Vuga Development Initiative kwa juhudi za kuunganisha halmashauri na wadau wa maendeleo. Sumaye alisema mchango huo ni mkubwa katika kuboresha miundombinu ya elimu, akibainisha kuwa pamoja na juhudi zinazofanywa na Serikali katika ujenzi wa madarasa, vyoo na hosteli, bado kuna mahitaji mengine yanayohitaji ushirikiano wa wadau. Alisema hosteli hiyo itawasaidia wanafunzi kupata sehemu salama ya kulala, kupumzika na kujisomea, hivyo kuongeza uwezekano wa kufanya vizuri katika masomo yao. Aliwataka wananchi kutambua umuhimu wa maendeleo yanayoletwa na wadau na kuhakikisha wanatunza miundombinu inayojengwa kwa manufaa ya jamii. “Tunawaomba wanafunzi na wananchi wote kutunza majengo haya, hosteli na matundu ya vyoo 14 ili yaweze kudumu na kuwa na thamani. Wafadhili wanapokuja kuona matumizi mazuri ya miradi waliyoigharamia, wanapata moyo wa kuendelea kutusaidia,” alisema Sumaye. Pia alimshukuru Kaoneka kwa jitihada zake za kutafuta marafiki na mashirika ya maendeleo, akieleza kuwa ushirikiano huo umechangia kupatikana kwa miradi mbalimbali katika eneo la Bumbuli. Aidha, alimwomba Diwani wa Kata ya Vuga kuratibu harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ununuzi wa vitanda vya hosteli, huku akiahidi kuchangia katika zoezi hilo. Alisema ushirikiano kati ya Serikali, wananchi na wadau wa maendeleo ni muhimu katika kuhakikisha shule hiyo inapata miundombinu inayokidhi mahitaji ya wanafunzi na kuboresha kiwango cha elimu katika eneo hilo.
Tue, 17 Nov 2026 20:28:31 +0000MENEJA MKUU KARIAKOO: MATANGAZO YA BIASHARA MTANDAONI HAYAEPUKIKI KATIKA UFANISI WA BIASHARA
Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo CPA. Ashraph Abdulkarim amewashauri wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kariakoo kutangaza bidhaa zao mtandaoni jambo litakaloendelea kutavutia wateja wengi zaidi wa ndani na nje ya nchi. Ushauri huo umetolewa wakati wa mkutano baina ya uongozi wa shirika hilo na wafanyabiahara wa Soko soko hilo, mkutano ambao umelenga kusikiliza kero na changamoto za wafanyabiashara ili kuendelea kuboresha mazingira ya biashara katika soko hilo. Amebainisha kuwa shirika limeendelea na mipango mbalimbali ya kuvutia wateja kwa kutangaza huduma na bidhaa zinazopatikana sokoni hapo, jitihada ambazo zimekuwa na mafanikio chanya kwa kuongeza mzunguko wa watu wanakuja na kutoka sokoni hapo. Ameongeza kuwa kutokana na mabadiliko ya teknolojia nchni, ubunifu katika kuendesha biashara ni jambo lisiloepukika, kwakuwa mtu anaweza kufanya maamuzi ya bidhaa anayoitaka akiwa nyumbani au mahali popote na kuja kuichukua au kutuma mtu aifuate kwa niaba yake. Shirika la Masoko ya Kariakoo limekuwa na utaratibu wa kukutana na wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kariakoo kila baada ya miezi mitatu kwa lengo la kusikiliza changamoto zinazowakabili, kupokea mrejesho na kushirikisha shughuli mbalimbali zinazoendelea sokoni hapo ili kujenga uelewa wa pamoja miongoni mwao.
Tue, 17 Nov 2026 20:31:38 +0000DAUD YASSIN KUANZA ZIARA YA SIKU 11 KUIMARISHA CHAMA MKOANI IRINGA
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa, Comrade Daud Yassin, anatarajiwa kufanya ziara maalum katika wilaya zote nne za mkoa huo kuanzia Novemba 21 hadi Desemba 1, 2026, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha chama na kusogeza shughuli zake karibu na wanachama. Kwa mujibu wa ratiba iliyotangazwa na CCM Mkoa wa Iringa, ziara hiyo itaanza Novemba 21 katika Wilaya ya Iringa Mjini, kabla ya kuelekea Kilolo Novemba 23 na 24, kisha Mufindi Novemba 28 na 29, na kuhitimishwa katika Wilaya ya Iringa Vijijini Novemba 30 hadi Desemba 1, 2026. Ziara hiyo yenye kaulimbiu ya #KazinaUtuTunasongaMbele inalenga kuimarisha shughuli za chama katika maeneo mbalimbali ya mkoa, huku ikitoa fursa ya uongozi wa chama kufika katika wilaya zake zote nne kupitia ratiba hiyo maalum. Hatua hiyo inaweka msisitizo katika kuendeleza uhai wa chama, kuimarisha mshikamano na kuendeleza utekelezaji wa majukumu ya CCM katika Mkoa wa Iringa.
Tue, 17 Nov 2026 20:34:02 +0000IRINGA YAKARIBIA LENGO LA DUNIA LA 95-95-95, UELEWA WA UKIMWI WAFIKIA ASILIMIA 94.6
Mkoa wa Iringa umeendelea kupiga hatua katika mapambano dhidi ya Virusi vya UKIMWI (VVU), huku kiwango cha uelewa wa wananchi kuhusu ugonjwa huo kikiongezeka kutoka asilimia 86.5 hadi asilimia 94.6 ndani ya kipindi cha miaka mitano, hatua inayokaribia lengo la kitaifa la asilimia 95. Akizungumza wakati wa kukabidhi vitendea kazi vilivyobaki baada ya kukamilika kwa Mradi wa Afya Yangu Southern Project, Mkurugenzi wa mradi huo, Dkt. Denis Mzaga, amesema mafanikio mengine yaliyopatikana ni kuwafikia asilimia 98 ya watu waliobainika kuwa na maambukizi na kuwaanzishia matibabu, huku asilimia 98 ya wanaotumia dawa za kufubaza virusi wakifanikiwa kufikia kiwango cha udhibiti wa virusi mwilini. Amesema katika kipindi cha miaka mitano ya utekelezaji wa mradi huo, vituo 147 vya kutolea huduma na matunzo kwa watu wanaoishi na VVU (CTC) vimeendelea kutoa huduma, huku jumla ya wananchi 71,149 wakifikiwa na huduma za matibabu. Hata hivyo, Dkt. Mzaga amebainisha kuwepo kwa changamoto ya baadhi ya watu wanaogundulika kuwa na maambukizi mapya wakiwa katika hatua ya ugonjwa, hali inayohitaji kuimarishwa kwa elimu na tahadhari ili kuzuia maambukizi zaidi. Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Kheri James, amewataka waganga wakuu wa halmashauri kuendeleza kampeni za elimu na uhamasishaji kwa wananchi ili kudhibiti maambukizi mapya na kulinda mafanikio yaliyopatikana. Amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo, wakiwemo Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), imefanya juhudi kubwa kupunguza kasi ya maambukizi, hivyo wataalamu wa afya wanapaswa kuhakikisha hatua zilizofikiwa zinaendelezwa ili kufikia lengo la asilimia 95-95-95 ifikapo mwaka 2030. Aidha, amesisitiza kuwa vitendea kazi vilivyokabidhiwa vinapaswa kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuimarisha huduma za kinga, upimaji na matibabu ya VVU mkoani humo. Ameagiza waganga wakuu wa halmashauri kufuatilia kwa karibu watu wanaobainika kuwa na maambukizi ili kuhakikisha wanapata huduma stahiki na kuendelea na matibabu, huku akisisitiza umuhimu wa kupinga unyanyapaa dhidi ya watu wanaoishi na VVU.
Tue, 17 Nov 2026 20:40:58 +0000Page 175 of 1137 · 22726 stories