Unganishwa

Search the region

22735 stories

Uncategorized · The Standard

After 22 years of waiting, woman welcomes quadruplet boys

After 22 years of waiting to become a mother, a woman has welcomed quadruplet boys in a rare and joyful birth that has brought immense happiness to her family.

Tue, 17 Nov 2026 16:58:45 +0300
Uncategorized · The Standard

Why Ruto's State of the Nation must measure the state of the people

The true State of the Nation will always be measured by the lives of its people beginning with the five basics that govern our daily lives.

Wed, 18 Nov 2026 10:39:02 +0300
Uncategorized · The Star Kenya

Ruto appoints Odundo Machakos University chancellor

Odundo will serve as the university's Chancellor for the next five years, a position that places him at the helm of the institution's ceremonial and governance

Recently
Business · Issa Michuzi

TANZANIA KUNUFAIKA NA UZOEFU WA KENYA KATIKA UWEKEZAJI WA MIUNDOMBINU

Na Mwandishi WAZIRI wa Ujenzi Masanja Kungu Kadogosa, amesema Serikali ya Tanzania imejipanga kuimarisha utekelezaji wa miradi ya miundombinu kupitia mfumo wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (Public Private Partnership – PPP), kwa kujifunza uzoefu wa Kenya katika kuvutia uwekezaji na kusimamia miradi mikubwa ya maendeleo. Kadogosa ameyasema hayo jijini Nairobi, Kenya, wakati wa Kongamano la 16 la Bara la Afrika kuhusu Ushirikiano kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP), ambapo amesisitiza umuhimu wa nchi za Afrika kutumia mfumo huo kama njia mojawapo ya kuongeza uwezo wa kugharamia na kutekeleza miradi mikubwa ya miundombinu. Amesema Tanzania inaendelea kuandaa na kutekeleza mikakati ya kutumia mfumo wa PPP katika miradi mbalimbali, hivyo kujifunza uzoefu wa Kenya kutasaidia kubaini mifumo bora ya utekelezaji, namna ya kuvutia wawekezaji binafsi na kukabiliana na changamoto zinazoweza kujitokeza katika utekelezaji wa miradi hiyo. Aidha, amesema katika mazungumzo yaliyofanyika pembezoni mwa kongamano hilo, wamejadili fursa za uwekezaji katika sekta ya miundombinu nchini Tanzania, hususan miradi ya barabara ya Kibaha–Chalinze, Chalinze–Morogoro, Morogoro–Iringa na Igawa–Tunduma. Kadogosa ameeleza kuwa miongoni mwa mambo muhimu yaliyojadiliwa ni namna Kenya ilivyoanzisha Mfuko wa Taifa wa Miundombinu (Kenya National Infrastructure Fund), wenye mtaji unaokadiriwa kufikia dola za Marekani bilioni tatu, kwa lengo la kusaidia kugharamia miradi ya miundombinu na kupunguza vihatarishi vya uwekezaji vinavyoweza kuwafanya wawekezaji binafsi kusita kushiriki katika miradi ya PPP. Amesisitiza kuwa uzoefu huo ni muhimu kwa Tanzania katika kuimarisha mazingira ya uwekezaji, kuongeza ushiriki wa sekta binafsi na kuhakikisha miradi mikubwa ya miundombinu inapata vyanzo endelevu vya fedha kwa ajili ya utekelezaji wake. Kongamano hilo limewakutanisha wadau kutoka mataifa mbalimbali, yakiwemo Kenya, Uganda, Ufaransa, Tunisia, Ivory Coast na Senegal, kwa lengo la kubadilishana uzoefu na kujadili mikakati ya kuimarisha ushirikiano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi katika kufadhili na kutekeleza miradi ya maendeleo barani Afrika. Hatua hiyo inaendana na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 inayolenga kujenga uchumi shindani na jumuishi kupitia uwekezaji katika miundombinu ya kisasa, kuongeza ushiriki wa sekta binafsi na kuharakisha utekelezaji wa miradi ya kimkakati kwa maendeleo ya Taifa

Sat, 14 Nov 2026 10:33:14 +0000
Uncategorized · Issa Michuzi

WAHITIMU ATC WATAKIWA KUWA CHACHU UTEKELEZAJI DIRA 2050

Na Seif Mangwangi, Michuzi TV, Arusha WAHITIMU wa Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) wametakiwa kutafakari na kujiwekea mikakati ya namna ya kutumia ujuzi na maarifa waliyoyapata chuoni hapo katika kuchangia utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, inayolenga kuifanya Tanzania kuwa nchi yenye uchumi wa kipato cha juu na shindani. Wito huo umetolewa Novemba 12, 2026 na mkuu wa chuo cha ufundi Arusha (ATC), Profesa Mussa Chacha alipokuwa akitoa hotuba katika mahafali ya 18 ya chuo hicho yaliyofanyika chuoni hapo. Profesa Chacha amewataka wahitimu hao wa ngazi mbalimbali za uhandishi kwa viwango vya Stashahada na Shahada kutambua kuwa elimu na ujuzi walioupata ni nyenzo muhimu katika kujenga uchumi wa viwanda, kukuza teknolojia na kuongeza uzalishaji nchini. Amesema Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 inahitaji nguvu kazi yenye maarifa, ujuzi, ubunifu na uzoefu katika sekta mbalimbali, hivyo wahitimu wa elimu ya ufundi wana nafasi muhimu katika kufanikisha malengo hayo. “Mnatakiwa kutambua kuwa kuhitimu si mwisho wa kujifunza, bali ni mwanzo wa safari ya kutumia maarifa katika kutatua changamoto za kijamii na kiuchumi, lakini pia napenda kuishukuru Serikali yetu chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan , wadau wa maendeleo, wazazi, walezi na washirika wa chuo kwa mchango wao katika kuendeleza elimu ya ufundi nchini.l,” amesema. Kwa upande wake, Mgeni rasmi katika mahafali hayo Mkurugenzi wa Utafiti na Mafunzo wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Fredrick Salukile, Kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Prf.Carolyne Nombo amesema wahitimu hao wanatakiwa kuunganisha elimu ya ufundi na mahitaji halisi ya soko la ajira na maendeleo ya viwanda. Dkt. Salukile amesema maendeleo ya taifa hayaishii katika kujenga miundombinu pekee, bali yanahitaji pia wataalamu wenye uwezo wa kuendesha, kuhudumia na kutengeneza mifumo na vifaa mbalimbali, akisisitiza kuwa teknolojia, ubunifu na ujuzi ni msingi muhimu wa kujenga uchumi imara. Amesema Serikali inatambua umuhimu wa vijana wenye ujuzi katika sekta za uzalishaji na ndiyo maana imeendelea kuimarisha elimu ya ufundi, huku akizitaka kampuni, viwanda na taasisi mbalimbali kutoa nafasi kwa wahitimu ili wapate uzoefu wa kazi na kutumia maarifa yao katika mazingira halisi ya uzalishaji. Aidha Dkt Salukile, amesisitiza umuhimu wa kuendeleza kituo cha Uhandisi wa Vifaa Tiba (Biomedical Engineering) kwa ajili ya mafunzo, tafiti, ubunifu na matengenezo ya vifaa tiba, huku akieleza kuwa chuo hicho kufanya ushirikiano na vyuo na taasisi za kimataifa ikiwemo Cornell University, Clemson University na vyuo vikuu vya Korea Kusini ni fursa ya kuongeza uwezo wa wataalamu wa ndani. Mwenyekiti wa bodi ya chuo hicho Dkt. Noel Mbonde, amesema chuo hicho kinaendelea kuimarisha mafunzo yanayozingatia ujuzi wa vitendo, sayansi, teknolojia, nishati endelevu na ujasiriamali ili kuandaa wahitimu watakaokidhi mahitaji ya uchumi wa kisasa. Dkt. Mbonde amesema bodi inatambua mchango wa wadau wa maendeleo na taasisi za kimataifa katika kuimarisha uwezo wa chuo, akitaja ushirikiano na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) pamoja na UNESCO Global Skills Academy kuwa sehemu ya juhudi za kuboresha elimu ya ufundi. Amesema ushirikiano huo unapaswa kuzaa matokeo yanayoonekana katika viwanda, taasisi na maeneo mbalimbali ya uzalishaji badala ya kuishia katika maonesho na makubaliano, huku akisisitiza umuhimu wa kufanya tathmini ya mafanikio ya mafunzo na matumizi ya teknolojia zinazozalishwa. Aidha, ameeleza kuwa chuo kinaendelea na ujenzi wa kiwanda cha mafunzo na uzalishaji wa mashine, ambapo vifaa na mashine kutoka Austria vinatarajiwa kuwasili mwishoni mwa Novemba 2026 na kuanza kufungwa mara baada ya kufika ili kuwawezesha wanafunzi kupata mafunzo katika mazingira halisi ya viwanda. Amewapongeza wahitimu kwa kufikia hatua hiyo na kuwataka kuendelea kuongeza maarifa, kuwa wabunifu na kutumia ujuzi wao kujiajiri na kuajiriwa, huku akiwataka kuwa mabalozi wazuri wa chuo kwa kuonesha nidhamu, uadilifu na umahiri katika maeneo yao ya kazi. Katika mahafali hayo ya 18, jumla ya wahitimu 1337 wametajwa kuhitimu katika ngazi mbalimbali za mafunzo ya ufundi katika kozi za uhandisi wa mitambo, uzalishaji wa umeme, petroli na gesi, ujenzi wa barabara, majengo.

Sat, 14 Nov 2026 10:36:08 +0000
Uncategorized · The Standard

Political storm at Maa festival as Lenku accuses UDA of turning event into campaign platform

Lenku criticised what he called double standards by UDA leaders, who had initially urged participants to keep politics out of the event but were allegedly engaging in political mobilisation.

Sat, 14 Nov 2026 13:00:00 +0300
Business · Issa Michuzi

MASAUNI AZIPONGEZA NCMC NA CRDB, AITAKA BIASHARA YA KABONI KUWANUFAISHA WATANZANIA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhandisi Hamad Masauni, amepongeza Kituo cha Taifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni (NCMC) na Benki ya CRDB PLC kwa kuingia makubaliano ya ushirikiano yenye lengo la kuimarisha soko la biashara ya kaboni nchini na kuvutia uwekezaji katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Masauni ameyasema hayo wakati wa hafla ya utiaji saini wa Hati ya Makubaliano (MoU) kati ya NCMC na Benki ya CRDB iliyofanyika jijini Antalya, Uturuki. Amesema ushirikiano huo ni muhimu katika kuunganisha uwezo wa Serikali kupitia NCMC katika kusimamia na kuratibu biashara ya kaboni pamoja na utaalamu wa CRDB katika huduma za kifedha na uwekezaji. Ameeleza kuwa Tanzania kupitia Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050 imeitambua biashara ya kaboni kuwa sekta muhimu katika kuvutia uwekezaji wa kijani, kupata fedha za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuchochea maendeleo endelevu ya kiuchumi. Aidha, ameitaka CRDB kubuni mifumo bunifu ya kifedha ikiwemo mikopo ya vifaa, dhamana na nyenzo nyingine zitakazowezesha utekelezaji wa miradi ya kaboni na kuongeza upatikanaji wa mitaji kwa wawekezaji. Hata hivyo, Masauni amesisitiza kuwa upatikanaji wa fedha kwa ajili ya miradi ya kaboni haupaswi kuchukuliwa kama kibali cha utekelezaji, akieleza kuwa miradi yote lazima izingatie sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa na Serikali. Ameongeza kuwa biashara hiyo inapaswa kuzingatia haki za binadamu, kulinda jamii zinazozunguka maeneo ya miradi, kuhifadhi mazingira na kuhakikisha wananchi wanapata manufaa ya kiuchumi na kijamii, yakiwemo ajira na uhamishaji wa teknolojia. Amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kuimarisha mifumo ya kitaasisi na udhibiti wa biashara ya kaboni ili kuhakikisha uwazi, uwajibikaji na manufaa ya sekta hiyo yanawafikia Watanzania.

Sat, 14 Nov 2026 10:30:25 +0000
Uncategorized · DW Rwanda

India: Delhi surpasses Lahore as world's most polluted city

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Issa Michuzi

NDEJEMBI AAGIZA FIDIA KULIPWA, ATOA SIKU 60 KUKAMILISHA MRADI WA MAJI MADANGWA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, Novemba 14, 2026, ameanza ziara ya kikazi mkoani Lindi kwa kuzungumza na wananchi wa Madangwa, Jimbo la Mtama, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake katika mikoa ya Kusini. Madangwa ni kituo cha kwanza cha ziara yake mkoani Lindi baada ya kutoka mkoani Mtwara. Akiwasili katika eneo hilo, alipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Adam Malima, Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye, wabunge wa Mkoa wa Lindi pamoja na viongozi mbalimbali wa CCM na Serikali. Akiwa Madangwa, Makamu wa Rais ameiagiza Wizara ya Ujenzi kuanza kulipa fidia kwa wananchi waliopisha maeneo yao kwa ajili ya ujenzi wa barabara, ikiwezekana malipo hayo yafanyike kwa awamu. Aidha, Wizara ya Maji imeahidi kutoa Sh milioni 500 kwa ajili ya ukarabati wa mradi wa maji ili huduma hiyo irejeshwe na kupatikana kwa wananchi ndani ya miezi miwili. Katika hatua nyingine, Wizara ya Kilimo imeahidi kuhakikisha salfa ya unga kwa ajili ya zao la korosho inawafikia wakulima kabla ya Machi 2027. Makamu wa Rais alianza ziara ya siku saba katika mikoa ya Kusini Novemba 9, 2026, akitembelea mikoa ya Ruvuma, Mtwara na Lindi kwa ajili ya kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza pamoja na kutatua kero za wananchi.

Sat, 14 Nov 2026 10:18:58 +0000
Uncategorized · The Star Kenya

Ruto stuns in Maasai Shuka at Maa Festival

The President was received at the festival by several leaders and government officials who had gathered to participate in the celebrations.

Recently
Uncategorized · Azam TV Videos

VITA YA MKANDA: Ibrahim Class ameutetea mkanda wake dhidi ya Aran Depaen

MKANDA UMEBAKI TANZANIA: Mtanzania, Ibrahim Class ameutetea mkanda wake WBC International Chamion akishinda kwa pointi dhidi ya Aran Depaen kutoka Thailand. Burudani ilikuwa LIVE #AzamSports5HD ✍️ @katty_shirima Mhariri | @rajjmsangi #VitasaNight #UsikuWaVitasa #VitaYaMkanda #Ngumi #IbrahimClass #AranDipaen

2026-11-14T09:51:20+00:00
Uncategorized · Capital FM

Trump, Putin and Xi plan historic joint meeting in China next week, White House says

Latest · News

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

Maa cultural fete disrupted as rival groups clash

In a video circulating online, people could be seen scampering for safety as the confrontation disrupted activities at the festival venue

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

Babu Owino explains why he left Sifuna's Linda Mwananchi

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Issa Michuzi

KIBAHA KUONGEZA MAPATO KUPITIA MRADI WA MAEGESHO YA MALORI MISUGUSUGU

Na Victor Masangu, Kibaha HALMASHAURI ya Manispaa ya Kibaha inatarajia kuongeza vyanzo vya mapato ya ndani kupitia uboreshaji wa mradi wa maegesho ya malori katika eneo la Misugusugu, kwa kuweka huduma mbalimbali za kijamii zitakazowanufaisha watumiaji wa eneo hilo. Mradi huo unatarajiwa kuwa mkombozi katika kupunguza changamoto ya malori kuegeshwa kiholela pembezoni mwa barabara, hali inayoweza kusababisha usumbufu na kuhatarisha usalama wa watumiaji wengine wa barabara. Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha, Warda Maulid, wakati akijibu maswali ya madiwani katika kikao cha baraza la madiwani kilichojadili utekelezaji wa shughuli za robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2026/2027 (Julai–Septemba). Maulid amesema halmashauri imejipanga kuweka huduma mbalimbali za kijamii katika eneo hilo, hatua itakayosaidia kuboresha mazingira ya maegesho na kuongeza mapato ya ndani kupitia huduma zitakazotolewa. Amesema ameyapokea maoni na mapendekezo ya madiwani na kwamba halmashauri itaweka mipango ya muda mfupi na mrefu kuhakikisha mradi huo unakuwa na manufaa zaidi. Awali, Diwani wa Kata ya Misugusugu, Ally Simba, aliomba eneo hilo liboreshwe kwa kuweka huduma mbalimbali za kijamii pembezoni mwa maegesho ili kuongeza ufanisi wake. Kwa upande wake, Diwani wa Viti Maalumu, Sara Uledi, amesema kuna umuhimu wa kuhakikisha malori yanayoegeshwa kiholela barabarani yanaondolewa na kuelekezwa katika eneo maalumu lililotengwa kwa ajili hiyo. Naye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kibaha, Dkt. Nicas, amelipongeza baraza la madiwani kwa ushirikiano na kumkaribisha Mkurugenzi huyo mpya, akiahidi ushirikiano katika kutekeleza majukumu ya halmashauri. Wakati huo huo, Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Fadhili Emanuel Nkurlu, amewataka viongozi wa chama na Serikali kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria na kanuni zilizowekwa, bila kuingiliana katika maeneo ya kiutendaji. Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kibaha Mjini, Mwl. Mwajuma Amiri Nyamka, amesisitiza umuhimu wa uzalendo, ushirikiano na mshikamano miongoni mwa madiwani ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao.

Sat, 14 Nov 2026 09:50:54 +0000
Uncategorized · Kigali Today

Iyizire rata twitahire iwacu heza - abaganga bashubije imbogo mu rugo

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Issa Michuzi

SALIM ABRI ASAS ATIMIZA MIAKA 40 YA UANACHAMA CCM, AISHUKURU CHAMA KWA SAFARI YAKE YA UONGOZI

NA DENIS MLOWE, IRINGA MWANASIASA na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Salim Abri Asas, ameadhimisha miaka 40 tangu alipojiunga na chama hicho, akieleza kuwa safari yake ya uanachama imejengwa katika misingi ya uaminifu, utiifu na kujitolea katika kukitumikia chama. Asas ameadhimisha kumbukumbu hiyo Novemba 13, 2026, ikiwa ni miaka 40 tangu aanze safari yake ya kuwa mwanachama wa CCM, ambayo imeendelea kumfikisha katika ngazi mbalimbali za uongozi ndani ya chama hicho, ikiwemo nafasi ya Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa. Katika ujumbe wake alioandika katika mitandao yake ya kijamii ikiwemo Instagram jana wa kuadhimisha miaka hiyo, Asas amesema anajivunia kuwa mwanachama mwaminifu na mtiifu kwa CCM kwa kipindi chote cha miaka 40, akishukuru kwa nafasi na dhamana alizopata za kukitumikia chama chake. Amesema safari hiyo ya muda mrefu imekuwa sehemu muhimu ya maisha yake ya kisiasa, ikimpa fursa ya kushiriki katika shughuli za chama na hatimaye kufikia nafasi za juu za uongozi. Miaka 40 ya uanachama wa Asas inaweka alama ya safari ndefu ya kisiasa ndani ya CCM, chama ambacho amekuwa akikihusisha na maisha yake ya uongozi na utumishi. Kufikia nafasi ya Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ni hatua inayoonesha nafasi aliyoifikia ndani ya mfumo wa uongozi wa chama hicho, baada ya miongo minne ya kuwa mwanachama. Kwa Asas, maadhimisho hayo si kumbukumbu ya muda alioutumikia chama pekee, bali pia ni fursa ya kutafakari safari yake ya uanachama, uaminifu na dhamira ya kuendelea kuwa sehemu ya CCM.

Sat, 14 Nov 2026 09:46:14 +0000
Uncategorized · Watchdog Uganda

NAMAKAIRE SHADIA: Breaking the Silence and Building Resilience Among Young People

Behind the smile of a young person could be a…

Recently
Uncategorized · Watchdog Uganda

Naalya Book Club To Host Author Mohsin Hassan For Discussion on Uganda’s Political History

Naalya Book Club is set to host Ugandan author and entrepreneur Mohsin Hassan for a literary conversation exploring Uganda's turbulent post-independence history, including the events surrounding the assassination of form

Recently
Uncategorized · Watchdog Uganda

Afro-Arab Cooperation key to unlocking youth economic opportunities, says AAYC SG Dr. Agaba

By Fahim Muyingo The Secretary General of the Afro-Arab Youth Council (AAYC), Hon. Dr. Abbas Agaba, has called for stronger cooperation between Africa and the Arab World to expand opportunities…

Recently

Page 178 of 1137 · 22735 stories