Search the region
22831 stories
Tanzania’s food security needs more than chemical-based agricultural solutions
MBEYA: Farmers often associate good harvests with improved seeds and fertilisers. But what happens when traditional seeds disappear and the…
RecentlyKAMATI YA BUNGE YAIPONGEZA WAMI/RUVU KWA UHIFADHI WA MAZINGIRA NA UFUATILIAJI WA RASILIMALI ZA MAJI
Katika kuimarisha usimamizi na uhifadhi wa rasilimali za maji nchini, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira imeendelea na ziara ya kutembelea na kukagua vituo vya ufuatiliaji wa mwenendo wa maji katika mito vinavyosimamiwa na Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu. Katika ziara hiyo, wajumbe wa Kamati wametembelea kituo cha kupima hali ya wingi wa maji katika Mto Ruvu, kilichopo eneo la Ruvu Kibungo, Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, ambapo wamepata maelezo kuhusu namna kituo hicho kinavyofanya kazi katika kukusanya na kutoa takwimu za mwenendo wa maji mtoni. Vituo hivyo vina umuhimu mkubwa katika usimamizi wa rasilimali za maji kwani huwezesha Bodi kupata takwimu sahihi na za uhakika kuhusu kiasi cha maji kinachopita katika mito kwa nyakati tofauti. Taarifa hizo hutumika katika kupanga na kusimamia matumizi ya maji, kufanya maamuzi sahihi kuhusu ugawaji wa rasilimali hiyo, kutambua mabadiliko ya mwenendo wa maji pamoja na kutoa tahadhari mapema dhidi ya vihatarishi vinavyoweza kusababisha mafuriko au upungufu wa maji. Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Patrick Mwalunenge (Mb), ameipongeza Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu kwa juhudi zinazofanyika katika kusimamia na kuhifadhi mazingira, akieleza kuwa hatua hizo ni muhimu katika kulinda vyanzo vya maji na kuhakikisha upatikanaji endelevu wa rasilimali hiyo kwa matumizi ya sasa na vizazi vijavyo. Ziara hiyo ni sehemu ya mwendelezo wa Kamati hiyo kukagua utekelezaji wa miradi na shughuli mbalimbali za usimamizi, uhifadhi na ulinzi wa rasilimali za maji zinazotekelezwa na Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu.
Thu, 12 Nov 2026 12:47:05 +0000BUNIFU ZA KISAYANSI KULENGA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WANANCHI
Na Karama Kenyunko Michuzi Tv TAFITI na bunifu za kisayansi zinazolenga kutatua changamoto za wananchi zinatarajiwa kuwa sehemu muhimu ya maadhimisho ya miaka 40 ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), yatakayofikia kilele Novemba 18, 2026, jijini Dar es Salaam. Miongoni mwa bunifu zilizooneshwa ni mkanda maalumu wa kusaidia kudhibiti upotevu wa damu kwa mama baada ya kujifungua, chanjo ya samaki inayolenga kukabiliana na magonjwa yanayoathiri ufugaji wa samaki pamoja na teknolojia ya kuzalisha gesi kwa kutenganisha hidrojeni na oksijeni kutoka kwenye maji. Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho hayo, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, amesema bunifu hizo ni sehemu ya mchango wa sayansi, teknolojia na utafiti katika kutafuta suluhisho la changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi. mesema maonesho ya tafiti, teknolojia na bunifu yatafanyika Novemba 17 na 18 katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam, huku kilele cha maadhimisho hayo kikitarajiwa kufungwa na Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, Novemba 18. Kuhusu ubunifu wa kuzalisha gesi kwa kutenganisha hidrojeni na oksijeni kutoka kwenye maji, Prof. Mkenda amesema ameagiza wataalamu kuchunguza usalama wa teknolojia hiyo pamoja na uwezekano wa kuitumia kiuchumi na kibiashara. Katika eneo la afya, amesisitiza umuhimu wa vyuo vikuu na taasisi za utafiti kufanya uchunguzi wa kisayansi kuhusu mimea inayotumika kutibu magonjwa, ili kubaini ufanisi wake, kiwango sahihi cha matumizi na madhara yanayoweza kujitokeza. Amesema pia ni muhimu kuimarisha uwezo wa kufanya majaribio ya awali ya dawa nchini kabla ya kufikia hatua ya kuzijaribu kwa binadamu, hatua itakayoongeza nafasi ya watafiti wa Tanzania kushiriki katika maendeleo ya tiba. Prof. Mkenda ameeleza kuwa maadhimisho hayo pia ni fursa ya kutathmini mchango wa COSTECH katika maendeleo ya nchi na kuweka msukumo mpya wa matumizi ya sayansi, teknolojia na ubunifu katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050. Amebainisha kuwa matumizi ya teknolojia na tafiti yanapaswa kuimarishwa katika sekta za kilimo, ufugaji, uvuvi na uchimbaji wa madini ili kuongeza tija na kuwezesha rasilimali za nchi kutumika kwa manufaa ya wananchi. Amesema katika kilimo, tafiti zinapaswa kuelekezwa katika kuongeza uzalishaji katika eneo linalolimwa, kupunguza umaskini wa wakulima na kuchangia upatikanaji wa chakula kwa gharama nafuu. Aidha, amezitaja jitihada za ufadhili wa masomo kupitia Samia Scholarship, utoaji wa tuzo kwa watafiti na Mfuko wa Samia wa Ubunifu kuwa miongoni mwa hatua zinazolenga kuendeleza wataalamu na kuwawezesha wabunifu nchini. Ameeleza kuwa kabla ya kufikia kilele hicho, shughuli mbalimbali zimefanyika zikiwemo kliniki ya ubunifu wakati wa maonesho ya Nanenane, maonesho katika viunga vya Bunge na mikutano ya wadau wa sayansi na utafiti. Amewakaribisha wananchi, waandishi wa habari na wadau mbalimbali kutembelea maonesho hayo ili kujionea tafiti, teknolojia na bunifu zinazolenga kuchangia maendeleo ya Tanzania.
Thu, 12 Nov 2026 12:47:36 +0000Airtel Yafanya Ziara Maalum kwa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi
Dodoma, Novemba 10, 2026 KAMPUNI ya Airtel Tanzania imesema itaendelea kuimarisha mifumo ya ulinzi wa taarifa binafsi za wateja wake ili kuendelea kutoa huduma bora na kuhakikisha usalama wa huduma zake za kidijitali. Dhamira hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Charles Kamoto, wakati wa ziara ya heshima katika Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC), ambapo alikutana na Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo, Dkt. Emmanuel Lameck Mkilia, pamoja na viongozi wengine. Katika ziara hiyo, Kamoto aliishukuru Tume kwa mwongozo na ushirikiano iliowapatia katika kuendana na mfumo wa ulinzi wa taarifa binafsi, akieleza kuwa mafunzo na miongozo yaliyotolewa kwa wafanyakazi wa Airtel yamekuwa muhimu katika kuongeza uelewa wa namna sahihi ya kuchakata, kuhifadhi na kushughulikia taarifa za wateja. Alisema ulinzi wa taarifa binafsi haupaswi kuonekana kama suala la kutimiza matakwa ya kisheria pekee, bali ni sehemu muhimu ya uendeshaji wa biashara na kujenga uhusiano wa muda mrefu na wateja. “Kwa Airtel Tanzania, kulinda taarifa binafsi si wajibu wa kutimiza matakwa ya kisheria pekee, bali ni jukumu la msingi na sehemu muhimu ya namna tunavyoendesha biashara yetu. Kulinda taarifa za wateja ni muhimu katika kujenga na kudumisha imani pamoja na mahusiano ya muda mrefu,” alisema Kamoto. Aliongeza kuwa kampuni hiyo inaendelea kuwekeza katika mafunzo na programu za uhamasishaji kwa wafanyakazi, pamoja na kuweka sera na mifumo ya ndani inayolenga kuhakikisha kuwa ulinzi wa taarifa binafsi unazingatiwa katika shughuli zake za kila siku. Kamoto alisema hatua hizo ni muhimu zaidi wakati kampuni ikiendelea kupanua huduma zake za kidijitali na mipango ya ujumuishaji wa huduma za kifedha, hali inayoongeza umuhimu wa kutunza vyema taarifa za wateja ipasavyo. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC), Dkt. Emmanuel Lameck Mkilia, aliipongeza Airtel Tanzania kwa kutembelea ofisi za Tume na kutambua umuhimu wa ushirikiano kati ya Tume na sekta binafsi. Alisisitiza pia umuhimu wa makampuni mbalimbali kuelewa dhamira ya Tume, hususan katika kuhakikisha kuwa biashara zinaweka mifumo imara ya kulinda na kuhifadhi taarifa binafsi za wateja wao. “Naipongeza Airtel Tanzania kwa utayari wake wa kushirikiana na Tume katika kuunga mkono utekelezaji wa malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, hususan katika kuendeleza safari ya Tanzania kuelekea uchumi wa kidijitali na kuhakikisha Watanzania wengi zaidi wananufaika na fursa za kidijitali,” alisema Dkt. Mkilia. Airtel Tanzania inathamini ushirikiano wake na Tume na inaendelea kujizatiti kuimarisha uhusiano huo katika kukuza usimamizi na utunzaji sahihi wa taarifa binafsi kwa lengo la kukuza na kujenga mazingira salama ya kidijitali nchini.
Thu, 12 Nov 2026 12:50:28 +0000La commune Bukinanyana plaide pour l’accès à l’eau potable, au profit des zones Buganda et Ndava
Read the full report from the original source.
RecentlyMarché de Mukenke : des toilettes fermées, un risque sanitaire croissant
Read the full report from the original source.
RecentlyDore umuganga ushinjwa gutoranya abarwayi bagombaga kwicwa muri Jenoside
Read the full report from the original source.
RecentlyKenyan scholars, political leaders weigh lessons from China’s governance model
Read the full report from the original source.
RecentlyBishops to MPs: Don't tamper with laws ahead of 2027 polls
They want Parliament to reject divisive proposals and urge IEBC to strengthen election preparedness ahead of the 2027 General Election.
RecentlyTanzania awards EDTCO a tender to construct 92.3km, 33kv power project from Mtwara to Tandahimba
MTWARA: THE Tanzanian government has awarded a tender to Electrical Transmission and, Distribution Construction Maintenance Company (EDTCO), to build a…
RecentlyPM calls for increased investment in education to drive innovation
Read the full report from the original source.
RecentlyBuilding collapse kills several in Brooklyn, New York
Read the full report from the original source.
RecentlyWoman found dead in Murang'a hours after leaving newborn baby in hospital
Read the full report from the original source.
RecentlyCinquante-quatre jeunes primés pour leur créativité au service du tourisme burundais
Read the full report from the original source.
RecentlyDEMANDE DE CHANGEMENT DE NOMS
Thu, 12 Nov 2026 14:35:21 +0200Okot features as Australian basketball giants make history in local league
Latest · Basketball
RecentlyTanzania calls for stakeholders’ support in implementing its education reforms
Read the full report from the original source.
RecentlyDED KIMARA ATAKA SHAMBA LA KOROSHO UGEZI KUWA CHACHU YA UCHUMI KIBITI
Na Mwamvua Mwinyi, Kibiti Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti, Ramadhan Ali Kimara, ameitaka Halmashauri na wadau mbalimbali kutumia uwekezaji wa shamba la mikorosho lenye ukubwa wa ekari 400 katika Kitongoji cha Ugezi, Kata ya Mtawanya, kuwa chachu ya kukuza uchumi wa eneo hilo kupitia uzalishaji wa korosho na ajira kwa vijana. Alieleza ,uwekezaji huo una manufaa kwa Halmashauri na wananchi kutokana na fursa za ajira zinazopatikana katika shughuli za utunzaji wa shamba na uvunaji wa korosho, huku vijana wakipata nafasi ya kujifunza mbinu bora za kilimo cha kisasa. Kwa upande wake, msimamizi wa shamba hilo, Gilbert Masawe, alifafanua kuwa shamba hilo lina miaka mitatu tangu kuanzishwa na uzalishaji wake bado haujafikia kiwango cha juu katika eneo lote la ekari 400 kutokana na mikorosho kuendelea kukua. Alisema matarajio ni kuongeza uzalishaji kadri mikorosho inavyoendelea kukomaa, huku kukiwa na mpango wa kupanua matumizi ya zao hilo kwa kuanza uzalishaji wa mvinyo unaotokana na mabibo ya korosho. Alieleza kuwa kwa sasa mvinyo huo huzalishwa kwa kiwango kidogo kwa ajili ya matumizi ya wafanyakazi wa shamba hilo, lakini kuna mpango wa kupanua uzalishaji wake siku zijazo ili kuongeza thamani ya zao la korosho na kupanua wigo wa fursa za kiuchumi.
Thu, 12 Nov 2026 12:31:51 +0000U Rwanda rwesheje imihigo ku ngengo y'imari igenewe abana
Read the full report from the original source.
RecentlyProf Mbarawa orders speedy construction of Dar Port-Kurasini Park’s road link
DAR ES SALAAM: THE Minister for Transport Prof Makame Mbarawa has directed the Tanzania Ports Authority (TPA), Tanzania National Roads…
RecentlyPage 224 of 1142 · 22831 stories