Search the region
22842 stories
MAKAMU WA RAIS AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI WA BILIONI 38.4 NANYUMBU
Nanyumbu, Mtwara MAKAMU wa Rais ameweka jiwe la msingi la mradi wa maji wa Nanyumbu wenye thamani ya Shilingi bilioni 38.4, unaotarajiwa kunufaisha zaidi ya wananchi 81,000 na kupunguza adha ya kutafuta maji, ikiwemo hatari ya kushambuliwa na mamba katika Mto Ruvuma. Akizungumza katika hafla hiyo, akiwa katika Kijiji cha Masuguru Wilaya ya Nanyumbu wakati wa ziara yake mkoani Mtwara, Makamu wa Rais amesema mradi huo ni sehemu ya juhudi za Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuwafikishia wananchi maji safi na salama karibu na makazi yao. Amesema wananchi wa Masuguru na maeneo ya jirani wamekuwa wakitegemea maji ya mtoni, hali iliyosababisha baadhi yao kupoteza maisha kwa kushambuliwa na mamba, huku wanawake na wasichana wakikabiliwa na hatari ya ukatili wa kijinsia wakati wa kutafuta maji. Ameeleza kuwa Serikali ilichukua hatua baada ya Mwakilishi wa Jimbo hilo, , Yahya Mhata kuwasilisha changamoto hizo kwa Rais Samia. “Kazi ya Serikali ni kusikia kilio cha wananchi na kutafuta majawabu ambayo yanaleta mabadiliko katika maisha yao,” amesema. Makamu wa Rais amesema utekelezaji wa mradi huo unaonesha dhamira ya Serikali ya kufikisha uwekezaji mkubwa wa huduma za msingi vijijini. Amesema wananchi waliokuwa wakitarajia kuchimbiwa visima sasa wamepata miundombinu ya kuwafikishia maji karibu na makazi yao. “Leo hii mradi ule uko hapa kijijini kwenu, mnauona kwa macho, siyo kwa kuhadithiwa,” amesema na kuahidi kumfikishia Rais Samia taarifa ya mafanikio ya mradi huo pamoja na furaha ya wananchi wanaonufaika na huduma hiyo. Makamu wa Rais ameipongeza Wizara ya Maji kwa ufanisi na ubora katika utekelezaji wa mradi huo. Aidha, amewataka wananchi kuutunza mradi na kuhifadhi mazingira ya Mto Ruvuma, akisema umebuniwa kukidhi mahitaji ya maji kwa miaka 40 na uendelevu wake unategemea pia ulinzi wa chanzo hicho. Kwa upande wake, Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso amesema mradi huo ni kielelezo cha dhamira ya Serikali ya kuhakikisha huduma za msingi zinawafikia wananchi wote bila kujali maeneo wanayoishi. Amepongeza ushirikiano wa watendaji wa Wizara ya Maji, RUWASA, wataalamu, viongozi wa Serikali za mitaa na wananchi katika kufanikisha mradi huo. Pia amelishukuru Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kwa kuwezesha upatikanaji wa umeme wa kuendesha miundombinu ya mradi huo. Akiwasilisha taarifa ya mradi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri, amesema utekelezaji umefikia asilimia 98.45 na huduma imeanza kutolewa kupitia vioski na miunganisho ya majumbani. Amesema mradi huo ni sehemu ya mpango wa maji wa miji 28 nchini. Mkataba wake wa ujenzi ulisainiwa Juni 6, 2022, na utekelezaji kuanza Aprili 23, 2023. Mradi unahusisha uchukuaji wa maji kutoka Mto Ruvuma katika kijiji cha Masuguru, mtambo wa kutibu maji wenye uwezo wa lita milioni tano, matanki mawili yenye jumla ya ujazo wa lita milioni 1.1, bomba kuu la kilomita 65.3, mtandao wa usambazaji wa kilomita 35 na vituo 20 vya kuchotea maji. Mhandisi Mwajuma amesema mradi ulikabidhiwa kwa mwendeshaji Oktoba 23, 2026, na tayari unahudumia maeneo ya Masuguru, Nachura, Lidede, Mwambani, Sengenya, Mangaka, Kilimanihewa, Mkwajuni na Ngalinje, huku kazi za umaliziaji zikiendelea. Mradi huo unatekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na India.
Thu, 12 Nov 2026 10:37:10 +0000Carrick sacked as Man United coach amid relegation battle
Latest · Football
RecentlyLes quatre enquêtes que les démocrates pourraient ouvrir contre le gouvernement Trump
Les démocrates avaient promis une vague d'enquêtes contre l'administration Trump s'ils reprenaient le contrôle de la Chambre des représentants, ce qui s'est produit.
RecentlyUkraine: Ugutanga umuyagankuba birageramiwe, mu gihe ibitero vy'Uburusiya bituma haba umwijima n'imbeho
Ku bavyeyi bo mu mihingo imwe imwe ya Ukraine, kugerageza kubandanya ubuzima busanzwe bwo mu muryango, mu gihe umuyagankuba uboneka amasaha make gusa ku musi, biriko birabagora cane kandi birabavuna.
RecentlyFour Ugandan schoolgirls die after eating suspected poisoned oranges
Read the full report from the original source.
RecentlyEngland’s Blues brothers – how the Bellinghams helped save Birmingham
Latest · News
RecentlyRuto announces Sh4bn for teachers’ career progression
"I know that was the most important question you wanted to ask. But you also know that I am a good student, and I do my homework," he told the school heads
RecentlyWatumishi wa REA watakiwa kuimarisha nidhamu, uwajibikaji na utunzaji wa rasilimali
Read the full report from the original source.
RecentlyNBAA trains accountants how to administer funds for health sector
DODOMA: THE National Board of Accountants and Auditors (NBAA) has launched a two-day training programme aimed at strengthening public financial…
RecentlyQuickmart shares surge 33pc on NSE debut
Read the full report from the original source.
RecentlyENDP Karubanda school reduces dependence on markets through agriculture and livestock production
Read the full report from the original source.
RecentlyRuto announces Sh4bn for teachers’ career progression
"I know that was the most important question you wanted to ask. But you also know that I am a good student, and I do my homework," he told the school heads
RecentlyRDC : la loi référendaire divise les principales Églises congolaises
Read the full report from the original source.
RecentlyKagame arrives in Cambodia ahead of landmark Francophonie summit
Read the full report from the original source.
RecentlyPutin backs mineral processing in Africa to boost industrialisation
Russian President Vladimir Putin has called for increased investment in mineral extraction and processing in Africa to boost government revenues and help African countries gain greater control…
RecentlyHundreds turn up as Rotarians provide free healthcare in Kawangware
Latest · News
RecentlySERIKALI YAIMARISHA UMEME MTWARA, ETDCO KUTEKELEZA MRADI WA KM 92.3
Kampuni ya Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Usafirishaji na Usambazaji wa Umeme (ETDCO) imekabidhiwa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kilovoti 33 kutoka Mtwara mjini hadi Tandahimba, mkoani Mtwara, wenye urefu wa kilomita 92.3. Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Mtwara, Mhandisi Abdul Mihambo, amesema mradi huo unalenga kuimarisha upatikanaji wa huduma ya umeme katika Wilaya za Tandahimba na Nanyamba. Amesema utekelezaji wa mradi huo ni sehemu ya juhudi za Serikali za kuimarisha miundombinu ya umeme na kuboresha huduma kwa wananchi, huku TANESCO ikishirikiana na ETDCO kuhakikisha kazi inakamilika kwa wakati na kwa kuzingatia viwango vinavyotakiwa. Mihambo ameyasema hayo wakati wa ziara ya kuitambulisha ETDCO kwa viongozi wa Wilaya za Tandahimba na Nanyamba kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo. Kwa upande wake, Meneja Mkuu wa ETDCO, Mhandisi Richard Mwanja, amesema mradi huo unatarajiwa kukamilika ndani ya mwaka mmoja, huku kazi za awali zikianza kwa kusimika nguzo za umeme. Ameeleza kuwa kutokana na kasi ya utekelezaji, kampuni hiyo inalenga kukamilisha mradi kabla ya muda uliopangwa na kuomba ushirikiano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ili kufanikisha kazi hiyo. Naye Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba, Kanali Michael Mtinjele, ameishukuru Serikali kwa kuanza utekelezaji wa mradi huo, akisema utasaidia kuimarisha huduma ya umeme wilayani humo. Wabunge wa Majimbo ya Nanyamba, Abdallah Chikota, na Tandahimba wameahidi kushirikiana na ETDCO kuhakikisha changamoto zinazoweza kukwamisha utekelezaji wa mradi huo zinapatiwa ufumbuzi.
Thu, 12 Nov 2026 10:14:48 +0000Byamukama orders immediate sacking of Uganda Airlines finance officer Kyeyune
The minister of Works and Transport Fred Byamukama has ordered the immediate sacking of Uganda Airlines chief finance officer Allan Kyeyune over lack of requisite…
RecentlyCatholic bishops caution Parliament over divisive electoral bills ahead of 2027
Read the full report from the original source.
RecentlyWakiso: Man Arrested for Stabbing Former Girlfriend to Death
Read the full report from the original source.
RecentlyPage 228 of 1143 · 22842 stories