Unganishwa

Search the region

22487 stories

Uncategorized · UBC

Huang’s return fails to dispel doubts as Nvidia shares drop

Read the full report from the original source.

Recently
Health · Issa Michuzi

UKINARA WA SAMIA WAFUNGUA FURSA ZA AFYA KWA WATAALAMU NA VIJANA

Na Karama Kenyunko Michuzi Tv UKINARA wa Rais Samia Suluhu Hassan katika afya ya mama na mtoto barani Afrika umefungua fursa za mafunzo, kubadilishana utaalamu na ushirikiano kwa wataalamu wa afya, taasisi na vijana wa Kitanzania. Fursa hizo ni pamoja na nafasi 60 za awali za mafunzo ya kitiba kwa wataalamu wa afya kutoka nchi wanachama wa Afrika, ambazo zinatarajiwa kuongezeka katika miaka ijayo kulingana na ushirikiano wa wadau. Akizungumza na waandishi wa habari, Waziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa, amesema fursa hizo zimepatikana kufuatia kutambuliwa kwa Rais Samia na taasisi ya Gates Foundation kwa kutunukiwa tuzo ya Goalkeepers Award kutokana na mchango wake katika sekta ya afya, hususan afya ya mama na mtoto. Amesema Rais Samia alitambuliwa pia Februari 16, 2026, na Afrika kama kinara wa afya ya mama na mtoto, kabla ya kuzindua Mpango Elekezi wa Bara la Afrika wa Afya ya Uzazi, Mama, Watoto Wachanga, Watoto na Vijana Balehe wa mwaka 2026–2030, Novemba 23, 2026, jijini Addis Ababa, Ethiopia. Mchengerwa amesema mpango huo umejikita katika malengo matatu ya sifuri, ambayo ni sifuri ya kujifungulia nyumbani, sifuri ya vifo vinavyoweza kuzuilika vya akina mama na watoto wachanga na sifuri ya watoto wasiochanjwa. Amesema mpango huo unalenga kuimarisha uongozi wa kisiasa, ushirikiano na uwajibikaji, kuhamasisha na kuoanisha uwekezaji na mifumo ya utoaji huduma, pamoja na kuharakisha utekelezaji wa afua zenye ushahidi wa kuokoa maisha. Ameeleza kuwa hatua zinazofuata ni pamoja na kuendesha warsha za kikanda kuanzia Desemba mwaka huu na mwanzoni mwa mwaka 2027, zitakazoshirikisha wawakilishi wa nchi wanachama, wataalamu, taasisi za kikanda na washirika wa maendeleo. Amesema fursa 60 za awali za mafunzo zinalenga maeneo ya ukunga, magonjwa ya wanawake na uzazi, usingizi na ganzi pamoja na huduma za watoto wachanga. Mafunzo hayo yanatarajiwa kuongezeka katika miaka inayofuata kulingana na ushirikiano wa wadau. Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Bruno Sunguye, amesema ukinara huo unatoa fursa kwa taasisi za Serikali, vyuo vikuu, taasisi za mafunzo, vyama vya kitaaluma, asasi za kiraia, sekta binafsi na taasisi za utafiti kushirikiana na nchi nyingine za Afrika. Amesema taasisi za Serikali zitapata fursa ya kubadilishana uzoefu kuhusu sera, mipango na mifumo ya utoaji huduma, ikiwemo huduma za dharura za uzazi, watoto wachanga, chanjo, mifumo ya rufaa na huduma za afya ya msingi. Dkt. Sunguye amesema vyuo vikuu, hospitali na vituo vya mafunzo nchini vitapata nafasi ya kutoa mafunzo kwa wataalamu kutoka nchi nyingine za Afrika, huku wataalamu wa Kitanzania wakipata fursa ya kwenda kujifunza katika nchi hizo. Ameeleza kuwa vituo vya mafunzo nchini vilivyopata ithibati kupitia Jumuiya ya Afya ya Afrika Mashariki (ECSA Health Community) vitatumika kama vitovu vya mafunzo kwa wataalamu wa afya kutoka nchi mbalimbali za Afrika. Amesema pia vyama vya kitaaluma, ikiwemo AGOTA na TAMA, vitapata nafasi ya kushiriki katika mafunzo, kutoa ushauri elekezi, kuandaa miongozo ya kitaalamu na kubadilishana uzoefu. Kwa upande wa asasi za kiraia na mashirika yasiyo ya kiserikali, amesema ushirikiano huo utazipa nafasi ya kupanua wigo wa shughuli zake, kufanya tafiti na kutoa ushauri wa kitaalamu katika nchi nyingine za Afrika. Ameongeza kuwa sekta binafsi itapata nafasi za uwekezaji katika dawa, vifaa tiba, bidhaa za afya, teknolojia za kidijitali, mifumo ya usafirishaji wa wagonjwa na ubunifu, hatua ambayo inaweza kuongeza fursa za ajira kwa vijana. Dkt. Sunguye amesema taasisi za utafiti, zikiwemo vyuo vikuu, zitapata wigo mpana wa kufanya tafiti katika nchi wanachama wa Afrika na kubadilishana utaalamu na mawazo ili kuboresha huduma kwa wananchi. Amesisitiza kuwa fursa hizo hazimaanishi fedha, zabuni au nafasi za mafunzo ambazo tayari zimetengwa kwa wadau, bali ushiriki utategemea mahitaji ya nchi, uwezo wa taasisi, makubaliano na taratibu za uwekezaji. Amesema vijana wana nafasi muhimu katika mpango huo kupitia ushiriki katika uongozi, maamuzi na uwajibikaji, uhamasishaji wa afya, ubunifu, teknolojia na utafiti. Ameeleza kuwa vijana wanaweza kutumia teknolojia za kidijitali na ubunifu wa kijamii kuboresha upatikanaji wa taarifa za afya, kuongeza matumizi ya huduma na kusaidia mawasiliano kati ya jamii na vituo vya afya. Prof. Sunguye amesema mafanikio yaliyopatikana katika kupunguza vifo vya mama na mtoto nchini yanaweza pia kutumika katika kuboresha maeneo mengine ya sekta ya afya. Hata hivyo, amesema mradi huo bado unahitaji kukamilishiwa hatua za upembuzi yakinifu, usanifu wa kitaalamu na maandalizi ya kutafuta fedha, ambapo baada ya upembuzi yakinifu kukamilika itafahamika njia itakayopitiwa na reli hiyo kabla ya kuanza kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi.

Tue, 24 Nov 2026 19:33:48 +0000
Uncategorized · Radio Publique Africaine

Ruyaga : la faim guette des familles privées d’une alimentation équilibrée

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Issa Michuzi

TANGA KUWA KITOVU CHA NISHATI AFRIKA MASHARIKI

Na Karama Kenyunko, Michuzi TV TANZANIA imepanga kuharakisha utekelezaji wa mpango wa kuifanya Tanga kuwa kitovu cha nishati cha Afrika Mashariki, kupitia uendelezaji wa miundombinu ya kuhifadhi, kusafirisha na kusambaza mafuta pamoja na uwekezaji katika viwanda vinavyozalisha bidhaa zitokanazo na mafuta. Mpango huo ni miongoni mwa maeneo saba muhimu ya ushirikiano wa kiuchumi yaliyokubaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, na Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, wakati wa ziara ya kitaifa ya Rais Samia nchini Uganda iliyofanyika Novemba 18 na 19, 2026. Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya ziara hiyo, leo Novemba 24, 2026 Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, amesema mpango huo unalenga kuifanya Tanzania isiwe nchi ya kupitisha mafuta pekee, bali pia kuwa kitovu cha shughuli za kiuchumi zinazohusiana na nishati, viwanda na biashara. Amesema makubaliano hayo yanahusisha kuendeleza miundombinu ya kuhifadhi mafuta, kusafirisha mafuta, kusambaza bidhaa za mafuta na kuimarisha huduma za usafirishaji na ugavi, pamoja na kushirikiana katika uzalishaji wa mbolea, plastiki, kemikali za viwandani na bidhaa nyingine zinazotokana na mafuta. Amesema uwekezaji huo unatarajiwa kufungua fursa za ajira kwa vijana katika ujenzi, uhandisi, uendeshaji wa mitambo, huduma za usafirishaji, matengenezo ya vifaa na shughuli nyingine za viwandani, huku wajasiriamali wakipata nafasi za kutoa huduma na bidhaa zitakazohitajika wakati wa ujenzi na uendeshaji wa mitambo hiyo. Katika ziara hiyo, viongozi hao pia walipokea taarifa ya maendeleo ya utekelezaji wa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), ambao umefikia asilimia 93.9 ya utekelezaji, huku wakielekeza kazi zilizobaki kukamilishwa haraka ili kuruhusu kuanza kwa usafirishaji wa mafuta. Kwa mujibu wa Profesa Mbarawa, kukamilika kwa mradi huo kutafungua fursa za shughuli za uendeshaji, matengenezo, usalama, usafirishaji na huduma za ugavi, pamoja na kuchochea uwekezaji na shughuli nyingine za kiuchumi katika maeneo yanayopitiwa na bomba hilo. Ameeleza kuwa maeneo mengine yaliyokubaliwa katika ziara hiyo ni kuendeleza reli ya kisasa (SGR) katika njia ya Isaka, Lusahunga, Murongo, Kikagati hadi Mpondwe yenye urefu wa kilomita 620, kuimarisha usafiri wa majini katika Ziwa Victoria kupitia Bandari ya Port Bell nchini Uganda, kuondoa vikwazo vya biashara, kuchochea uwekezaji katika viwanda na kuimarisha ushirikiano wa nishati, ikiwemo kuunganisha mifumo ya umeme ya kilovolti 400 katika njia ya Umulenzi, Masaka, Ibadakuli hadi Shinyanga. Amesema utekelezaji wa makubaliano hayo utasaidia kupunguza gharama za usafirishaji na uzalishaji, kupanua masoko ya bidhaa za Tanzania nchini Uganda na kuongeza fursa za ajira na biashara, akisisitiza kuwa mafanikio ya ziara hiyo yatapimwa kwa namna makubaliano hayo yatakavyotekelezwa na kuleta manufaa kwa Watanzania.

Tue, 24 Nov 2026 19:28:40 +0000
Uncategorized · Issa Michuzi

TARURA YAANDAA MIRADI YA BARABARA KWA MFUMO WA PPP

Na Said Mwishehe,Michuzi TV WAKALA wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) umesema umeandaa miradi ya barabara itakayotekelezwa kwa ubia na sekta binafsi (PPP), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuongeza fedha za maendeleo ya miundombinu na kupunguza utegemezi wa bajeti ya serikali. Hayo yamesemwa leo Novemba 24,2026 jijini Dar es Salaam na Ofisa Mipango TARURA Ally Ismail alipokuwa akizungumza mbele ya Wahariri wa vyombo vya habari wakati wa kikao cha kutathimini mwitikio wa masoko ya miradi ya ubia kati ya Serikali na sekta binafsi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji wa Ubia (PPP). “Miradi hiyo italenga kuchochea shughuli za kiuchumi, kuunganisha jamii na kuboresha miundombinu iliyoharibiwa na athari za mabadiliko ya tabianchi.Pia mipango hiyo itazingatia maeneo matatu makuu, ambayo ni kukuza uchumi shindanishi kupitia sekta za kilimo na viwanda, kuimarisha maendeleo ya watu kwa kuunganisha vijiji na huduma za kijamii, pamoja na kukabiliana na changamoto za mazingira. Pia amesema mvua kubwa zilizonyesha katika kipindi cha miaka miwili hadi mitatu iliyopita zimesababisha uharibifu wa barabara na kukatika kwa madaraja katika maeneo mbalimbali, hali iliyosababisha TARURA kubainisha maeneo yanayohitaji kurekebishwa. Ismail amesema wakala huo unaandaa tafiti za uwezekano wa kutekeleza baadhi ya miradi hiyo kupitia mfumo wa PPP, ikiwemo ujenzi wa madaraja yaliyoharibiwa. “Mfumo wa PPP unaweza kutekelezwa kupitia utaratibu wa user-pay, ambapo watumiaji hulipia huduma wanazopata, au availability payment, ambapo serikali humlipa mwekezaji kwa awamu kulingana na makubaliano ya mkataba. “Mfumo wa availability payment unatarajiwa kutumika zaidi katika miradi ya TARURA kwa kuwa barabara nyingi zinazohudumiwa na wakala huo zina umuhimu wa kijamii na kiuchumi, lakini hazina idadi kubwa ya magari inayoweza kumwezesha mwekezaji kurejesha gharama zake kupitia ada za matumizi,”amesema Ismail. Akieleza zaidi amesema baadhi ya miradi katika maeneo yenye msongamano mkubwa wa magari inaweza kutekelezwa kwa mfumo wa user-pay, akitolea mfano pendekezo la daraja litakalounganisha eneo la Muhimbili na Annasif jijini Dar es Salaam. Katika kuongeza upatikanaji wa fedha, amesema TARURA inachunguza uwezekano wa kutumia dhamana za miundombinu (infrastructure bonds) kuvutia fedha kutoka kwa benki, mifuko ya hifadhi ya jamii na wawekezaji wengine. Kuhusu kupunguza msongamano wa magari, amesema TARURA imebainisha barabara zinazohitaji kuboreshwa katika majiji ya Dar es Salaam, Arusha, Mbeya, Dodoma na Mwanza ili kupunguza msongamano kwenye barabara kuu. “Utekelezaji wa miradi hiyo utahitaji mgawanyo wa wazi wa vihatarishi kati ya serikali na sekta binafsi. Wawekezaji wanaweza kuwajibika katika usanifu, ujenzi na matengenezo ya miundombinu, huku serikali ikishughulikia masuala ya ardhi, fidia na uhamishaji wa miundombinu iliyopo. “TARURA pia itafanya tathmini ya soko (market sounding) ili kubaini uwezo wa kifedha wa wawekezaji, ukubwa wa miradi wanayoweza kugharamia na mifumo ya malipo wanayopendelea,”amesema Ismail. Ameongeza kuwa mikataba ya PPP inaweza kuwa ya miaka 10 hadi 30, kutegemea aina na ukubwa wa mradi, ili kumpa mwekezaji muda wa kurejesha fedha alizowekeza bila kuongeza gharama kubwa kwa watumiaji. Pia amesema sekta binafsi inaweza pia kuibua miradi na kuwasilisha mapendekezo yake TARURA, ikiwemo kugharamia tafiti za awali za uwezekano wa utekelezaji wake.”Ushiriki huo utaongeza fursa za uwekezaji na kusaidia kuharakisha maendeleo ya miundombinu ya barabara nchini.”

Tue, 24 Nov 2026 19:22:42 +0000
Business · Issa Michuzi

TANZANIA YAPANUA USHAWISHI WAKE AFRIKA KUPITIA UONGOZI WA SAMIA

Na Karama Kenyunko, Michuzi TV TANZANIA imeendelea kupanua ushawishi wake katika masuala ya uchumi, biashara, uwekezaji na afya barani Afrika kupitia ziara za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, nchini Uganda na Ethiopia. Ziara hizo zilizofanyika Novemba 18 hadi 19, 2026, nchini Uganda na Novemba 22 hadi 23, 2026, nchini Ethiopia, zimeweka msukumo katika kuimarisha ushirikiano wa kikanda na kufungua fursa mbalimbali kwa Tanzania. Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu matokeo ya ziara hizo, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bakari Machumu, amesema ziara ya Uganda ilijikita katika kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi, biashara na uwekezaji, huku ile ya Ethiopia ikiimarisha nafasi ya Tanzania katika uongozi wa afya ya mama na mtoto barani Afrika. Amesema katika ziara ya Uganda, Rais Samia na mwenyeji wake, Rais Yoweri Kaguta Museveni, walikubaliana kuharakisha utatuzi wa vikwazo visivyo vya kikodi vinavyokwamisha biashara kati ya nchi hizo mbili ili kupanua masoko na kuimarisha biashara. Katika sekta ya nishati, viongozi hao walipokea taarifa kuwa utekelezaji wa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) umefikia asilimia 93.9, pamoja na taarifa ya kutiwa saini kwa mkataba wa mfumo wa ushirikiano kuhusu uendelezaji wa reli ya kisasa (SGR) katika njia ya Isaka, Rusahunga, Uromo, Kikagati hadi Mpondwe. Aidha, Rais Samia alishiriki uzinduzi wa kiwanda cha kuunganisha magari cha Double Q nchini Uganda, ambako alisisitiza umuhimu wa nchi za Afrika Mashariki kujenga viwanda vinavyosaidiana na kuunganisha mnyororo wa thamani. Kwa upande wa Ethiopia, Rais Samia alishiriki Mkutano wa Tano wa Kimataifa wa Afya ya Umma Barani Afrika (CPHIA 2026) na kuzindua Mpango Elekezi wa Kuboresha Afya ya Mama na Mtoto Barani Afrika wa mwaka 2026–2030, unaohusu nchi zote 55 za Umoja wa Afrika. Mpango huo umejikita katika malengo matatu ya sifuri, ambayo ni sifuri ya kujifungulia nyumbani, sifuri ya vifo vya uzazi na watoto wachanga vinavyoweza kuzuilika na sifuri ya watoto wasiochanjwa. Katika hatua nyingine, Rais Samia alitangaza ufadhili wa awali wa nafasi 60 za mafunzo ya ubobezi kwa wataalamu wa afya barani Afrika, katika fani za ukunga, ganzi, afya ya uzazi na huduma za watoto wachanga. Machumu amesema ziara hizo zinaonesha umuhimu wa ushirikiano wa kikanda katika kukuza uchumi na biashara, pamoja na kuimarisha huduma za afya kwa wananchi.

Tue, 24 Nov 2026 19:23:27 +0000
Business · Issa Michuzi

DUWASA YAFUNGUA MILANGO KWA WAWEKEZAJI,YATANGAZA FURSA

Na Said Mwishehe,Michuzi TV MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) imetangaza fursa mbili kubwa za uwekezaji kwa sekta binafsi, zikihusisha mradi wa kuhudumia eneo la viwanda la Nala na mradi wa kupunguza upotevu wa maji unaofikia asilimia 35.5. Akizungumza katika mkutano wa Wahariri wa vyombo vya habari uliokuwa umeandaliwa na Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi(PPPC)Mhandisi Yohana Msangula kutoka Kitengo cha Maendeleo ya Miundombinu DUWASA amesema lengo ni kuwafikia wananchi wengi zaidi wa Dodoma. Amesisitiza wawekezaji na wananchi wa kawaida wote wanapaswa kunufaika na uwekezaji huo huku akifafanua DUWASA inahudumia Dodoma mjini pamoja na miji ya pembezoni ya Kibaigwa, Bahi, Chamwino na Kongwa. “Mamlaka ilifanya utafiti wa kina kabla ya kuingia moja kwa moja kwenye utekelezaji wa miradi hiyo miwili,”amesema na kuongeza eneo la kwanza ni eneo la viwanda la Nala, lenye takriban viwanda 33 katika ekari 771. Pia amesema eneo hilo halina miundombinu ya kutosha ya maji, jambo linalokwamisha shughuli za wawekezaji waliopo. Amefafanua DUWASA imekuwa ikipokea maombi makubwa kutoka kwa wawekezaji, ambapo mmoja anaweza kuomba asilimia 10 hadi 20 ya maji yote yanayozalishwa na mamlaka hiyo.”Ombi la aina hii ni nje ya uwezo wa DUWASA, ndiyo maana sekta binafsi imeonekana kuwa suluhisho linalofaa. “Kwa makadirio ya sasa, mahitaji ni mita za ujazo 20,000, sawa na lita milioni 20 hadi 24 kwa siku, kutokana na wawekezaji waliopo pekee. Mradi huo una vipengele viwili vikuu, ambavyo ni usambazaji wa maji safi na uchakataji wa maji taka.” Kwa mujibu wa usanifu wa awali, mradi unahitaji uwekezaji wa takriban Shilingi Bilioni 14 bila VAT. Miundombinu itakayojengwa ni pamoja na visima 13, matanki mawili makubwa ya lita milioni 5 kila moja yatakayowekwa mlimani, na tangi la lita milioni 10 karibu na eneo la viwanda. Pia kutajengwa mtandao wa kukusanya maji taka na mtambo wa kuyachakata wenye uwezo wa mita za ujazo 20,000 kwa siku. Maji yatakayochakatwa yatatumika kwa kilimo na uhifadhi wa mazingira. Msangula ameongeza mwekezaji hahitaji kuweka Sh.bilioni 14 zote kwa mara moja, kwani uwekezaji unaweza kufanyika kwa awamu. Kwa sasa DUWASA inahudumia kiwanda kimoja kikubwa kwa kutumia visima viwili, hivyo upanuzi unaweza kwenda sambamba na mahitaji. Ametaja faida kuu tatu kwa wawekezaji ni wateja wa uhakika kwa kuwa viwanda vipo na Serikali inaendelea kuhamasisha uwekezaji Dodoma, mapato kutoka vyanzo viwili yaani mauzo ya maji safi na ada ya uchakataji wa maji taka, na gharama ndogo za uendeshaji kwa sababu mfumo umesanifiwa kutumia mteremko wa asili badala ya pampu nyingi. Amesema mradi wa pili ni wa kupunguza upotevu wa maji na kuongeza makusanyo. Kwa sasa DUWASA inapoteza asilimia 35.5 ya maji yake, na lengo ni kushusha hadi asilimia 20 ifikapo mwaka 2031. “Uchunguzi umebaini asilimia 75 ya upotevu huo ni wa kibiashara, yaani maji yanamfikia mteja lakini hayalipiwi kutokana na mita mbovu au wizi. Asilimia 25 pekee ni upotevu wa kimwili unaotokana na mabomba kupasuka. “Ili kuthibitisha uwezekano wa mradi, DUWASA na wadau waliwekeza Sh.milioni 29 kununua mita janja katika eneo dogo la majaribio (DMA). Matokeo yalikuwa makubwa, kwani sasa mamlaka inapata faida ya ziada ya Sh.milioni 44 kila mwezi kutokana na maji yaliyokuwa yanapotea. “Kutokana na mafanikio hayo, DUWASA imeanzisha Mfuko wa Mzunguko, ambapo faida ya milioni 44 huwekwa kwenye akaunti maalum na kutumika kununua mita nyingine kwa maeneo mengine. Mpango wa jumla ni kubadilisha mita 50,000 za wateja. Mhandisi Msangula amewaomba wawekezaji kuleta teknolojia nzuri ya mita za kisasa, akisema wateja na vyanzo vya maji vipo, na malipo yanahakikishwa kwa kuwa mteja hulipia kabla ya kutumia maji. Amesema hiyo ni biashara yenye uhakika, na akawakaribisha wadau wote wenye nia kufika ofisi za DUWASA kupata taarifa za kina za usanifu wa awali.

Tue, 24 Nov 2026 19:18:17 +0000
Uncategorized · The Star Kenya

ODM under siege as MDG and UDA raid power base

ODM is facing growing pressure ahead of the 2027 elections, with governors, MPs and MCAs exploring alternative parties amid fears of unfair nominations

Recently
Uncategorized · Radio Publique Africaine

Gihosha : trois semaines sans eau

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

52-member taskforce formed to probe 687 school unrest incidents

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

NPS announces police cadet recruitment, sets December 10 deadline

The service is seeking Kenyan citizens with undergraduate degrees and a minimum mean grade of C+ in KCSE, including at least C+ in English or Kiswahili

Recently
Sports · Chimpreports

CHIMP SPORT: Sand Cranes Name Final Squad for 2026 AFCON Beach Soccer

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · UBC

UEDCL appoints Joselynne Rwakakooko as managing director

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

Kenya Met forecasts rain in 23 counties

Residents are urged to remain alert to possible flooding and other weather-related risks as the October-December short-rains season continues.

Recently
Uncategorized · DW Afrique

Allemagne-Afrique : le commerce progresse mais reste modeste

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Business Daily

Vodafone reveals Sh430bn gain from Safaricom deal

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

Police lob teargas at Syokimau residents protesting poor roads

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Radio Publique Africaine

Sans eau, l’hôpital régional de Gitega devient une source d’inquiétude sanitaire

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Daily News

Tanzania develops Africa’s first national legislative drafting system

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · DW Afrique

RDC : la Cenco entre indignation et dialogue avec le pouvoir

Read the full report from the original source.

Recently

Page 24 of 1125 · 22487 stories