Search the region
22910 stories
Uganda Railways begins cement transportation for Hima Cement
Read the full report from the original source.
RecentlyMABADILIKO YA BOOST: Bil 604/- zajenga shule mpya 676 nchi nzima
Read the full report from the original source.
RecentlyAGITF YAWEKA WAZI FURSA ZA MIKOPO KWA WAKULIMA WA MATUNDA NA MBOGAMBOGA.
Mfuko wa Udhamini wa Pembejeo za Kilimo (AGITF) umewahimiza wakulima wa mazao ya matunda na mbogamboga, hususan vijana na wanawake, kutumia fursa za mikopo yenye riba nafuu inayotolewa na mfuko huo ili kuimarisha uzalishaji, kuongeza thamani ya mazao na kupanua masoko ya bidhaa za kilimo. Akizungumza Novemba 10, 2026, jijini Arusha katika Maonesho ya Kilimo cha Mbogamboga, Matunda na Maua (Hortilogistical Africa 2026), Kaimu Meneja Uendeshaji wa AGTIF, Jane Hebron, amesema mfuko huo unatoa mikopo ya moja kwa moja kwa wakulima binafsi, vikundi na vyama vya ushirika, pamoja na kuwawezesha kupata mikopo kupitia taasisi za fedha kwa utaratibu wa kuwapa hati ya dhamana ili waweze kukopesheka na kulindwa kama dhamana zao hazitoshelezi ili waweze kunufaika na kilimo. Amesema kupitia programu ya Jenga kesho Iliyobora (BBT), mfuko huo unatoa mikopo kwa vijana wa kiume wenye umri wa miaka 18 hadi 40 na wanawake wenye umri wa miaka 18 hadi 65 kwa riba ya asilimia 4.5 kwa mwaka, huku muda wa marejesho ukiwa kati ya mwaka mmoja hadi mitatu kulingana na aina ya mradi, mikopo hiyo inalenga kugharamia mahitaji mbalimbali ikiwemo uchimbaji wa visima, miundombinu ya umwagiliaji, greenhouses, vitalu nyumba, ununuzi wa mbegu na pembejeo pamoja na mitaji ya kuendesha shughuli za kilimo. Amesema pia mfuko huo unatoa mikopo kwa ajili ya ununuzi wa mashine za kuchakata mazao ili kuongeza thamani na kuwawezesha wakulima kuzalisha bidhaa zinazokidhi vigezo vya masoko ya ndani na nje ya nchi, ameeleza kuwa ushiriki wao katika maonesho hayo ni fursa ya kukutana na wakulima wa horticulture, kuwapatia elimu kuhusu huduma za kifedha na kuwaelekeza namna ya kupata mitaji ya kuendeleza shughuli zao. Ameongeza kuwa wakulima wanaweza kuomba mikopo hiyo kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya Taasis hiyo kwa kuchagua mfumo wa e-Kilimo na kufuata maelekezo ya maombi, amewahimiza wakulima na wadau wa kilimo kutembelea banda la AGITF katika maonesho hayo ili kupata elimu zaidi kuhusu mikopo na fursa za kukuza biashara zao za kilimo. Akizungumza Anjelina Silyvester Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Elite Brand kutoka Iringa amesema kupitia programu ya BBT wamefanikiwa kupata mkopo kutoka AGITF wenye riba nafuu uliowawezesha kuongeza mashine kiwandani, kupunguza muda wa uzalishaji na kuongeza uwezo wa kuingiza bidhaa zao sokoni, na kukuza biashara zao. Kwa upande wake, Kamal Haji Simba, mkulima kutoka Paje, Zanzibar, ambaye alitembelea banda la AGITF, amesema amejifunza kuhusu fursa za mikopo yenye riba nafuu inayotolewa na mfuko huo kwa vijana na wanawake, huku akiwashauri vijana kuchangamkia fursa hiyo ili kupata mitaji ya kuwekeza katika kilimo na kujikwamua kiuchumi.
Tue, 10 Nov 2026 20:16:34 +0000MAKAMU WA RAIS ATOA MAAGIZO UKAMILISHAJI WA BARABARA YA AMANI MAKORO – RUANDA
MBINGA, RUVUMA Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, ameonesha kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wa barabara ya Amani Makoro - Ruanda yenye urefu wa kilomita 35, wilayani Mbinga, mkoani Ruvuma, baada ya mradi huo wenye thamani ya shilingi bilioni 60.5 kuchelewa kwa miaka miwili na miezi 10. Akikagua maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo katika eneo la Amani Makoro, wilayani Mbinga, Makamu wa Rais amebaini kuwa ni kilomita 10.5 pekee zilizojengwa kati ya kilomita 35 zilizopangwa, licha ya mkataba wa awali wa ujenzi kuwa wa miezi 18. Kutokana na hali hiyo, Makamu wa Rais ameiagiza Wizara ya Ujenzi kuandaa mpango kazi na mkakati madhubuti wa kuhakikisha mradi huo unakamilika, huku akisisitiza umuhimu wa kubaini na kushughulikia sababu zinazokwamisha utekelezaji wake. Ameelekeza kuwa iwapo ucheleweshaji unasababishwa na mkandarasi, hatua stahiki zichukuliwe kwa kuzingatia sheria na taratibu za manunuzi ya umma. Aidha, iwapo changamoto inatokana na upatikanaji wa fedha, Serikali itafute ufumbuzi wa kuhakikisha fedha zinazohitajika zinapatikana ili kukamilisha mradi huo Akizungumza na wananchi wa Amani - Makoro, wakati wa ziara hiyo, Makamu wa Rais amesema Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, itaendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wa mradi huo ili kuhakikisha unakamilika na kuanza kutoa manufaa yaliyokusudiwa kwa wananchi. Amesema kukamilika kwa barabara hiyo kutakuwa kichocheo muhimu cha maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi wa Wilaya ya Mbinga na Mkoa wa Ruvuma kwa ujumla, hususan katika kurahisisha shughuli za uzalishaji, biashara na usafirishaji. Ameongeza kuwa barabara hiyo ina umuhimu wa kimkakati katika kuimarisha miundombinu inayohudumia shughuli za uwekezaji, ikiwemo miradi ya uchimbaji wa makaa ya mawe inayotekelezwa wilayani Mbinga. Katika hatua nyingine, Makamu wa Rais amesisitiza kuwa dhamira ya Serikali ni kutatua changamoto zinazowakabili wananchi kwa kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa ufanisi na fedha za umma zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa. Amesema Serikali itaendelea kuweka mbele maslahi ya wananchi, huku ikiimarisha usimamizi na uwajibikaji katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kuzuia upotevu wa fedha na kuhakikisha thamani ya fedha inaonekana katika miradi inayotekelezwa. Akizungumzia changamoto ya bei ya mahindi, Makamu wa Rais amewahakikishia wananchi kuwa Serikali inaendelea kushughulikia suala hilo ili kulinda maslahi ya wakulima na kuimarisha sekta ya kilimo. Amewataka wananchi kuendelea kujikita katika uzalishaji wa mazao, hususan mahindi, na kuongeza kiwango cha uzalishaji katika msimu ujao wa kilimo. Amesema Serikali inaendelea kufuatilia mwenendo wa bei ya mahindi na kuchukua hatua za kuhakikisha changamoto na makosa yaliyojitokeza katika upangaji wa bei hayajirudii. Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Mbinga Vijijini, Mhe. Judith Kapinga, ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa uwekezaji mkubwa katika miradi ya maendeleo mkoani Ruvuma, hususan katika Jimbo la Mbinga Vijijini. Amesema uwekezaji huo una mchango mkubwa katika kuboresha huduma za kijamii, kuimarisha miundombinu na kufungua fursa mpya za kiuchumi kwa wananchi. Hata hivyo, amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha miradi inayoendelea kutekelezwa inakamilika kwa wakati ili wananchi waanze kunufaika na uwekezaji huo. Aidha, ameiomba Serikali kuharakisha utekelezaji wa miradi mingine muhimu katika jimbo hilo, ikiwemo miradi ya maji, ili kuongeza upatikanaji wa huduma muhimu na kuboresha maisha ya wananchi. Kukamilika kwa barabara ya Amani Makoro - Ruanda kunatarajiwa kuimarisha shughuli za kiuchumi, kurahisisha usafirishaji wa watu na bidhaa pamoja na kuchochea uwekezaji katika Wilaya ya Mbinga na Mkoa wa Ruvuma kwa ujumla.
Tue, 10 Nov 2026 20:07:36 +0000MAJERUHI WA AJALI YA BASI LA MAOKOTO WANAENDELEA VIZURI, SERIKALI YATOA UHAKIKA WA MATIBABU
NA DENIS MLOWE, IRINGA MKUU wa Mkoa wa Iringa, Kheri James, amesema majeruhi wa ajali ya basi la Maokoto iliyotokea katika eneo la Masumbo, barabara kuu ya Iringa–Mbeya, wanaendelea vizuri na huduma za matibabu huku Serikali ikiahidi kuendelea kuhakikisha wanapata matibabu hadi watakapopona. Kheri ameyasema hayo baada ya kuwatembelea majeruhi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa, akiwa ameambatana na Kamati ya Usalama ya Mkoa, ambapo alipata nafasi ya kujionea hali zao na maendeleo ya matibabu wanayoendelea kupatiwa na kuwapatia fedha za matunda na kujikimu wakati wakiendelea na matibabu. Amesema mkoa umepata pigo kubwa kutokana na ajali hiyo iliyosababisha vifo vya watu na wengine kujeruhiwa, huku akieleza kuwa juhudi za kuokoa maisha ya majeruhi na kuhakikisha wanapata huduma stahiki zinaendelea. Amesema hali za majeruhi waliolazwa hospitalini hapo zinaendelea vizuri, jambo linaloonesha kuwa huduma zinazotolewa na wataalamu wa afya zinasaidia kurejesha afya zao ili waweze kurejea katika majukumu yao ya kila siku. “Serikali imedhamiria kuhakikisha wagonjwa wote ambao bado wanaendelea na matibabu wanapata huduma zinazostahili hadi watakapopona na kurejea katika shughuli zao za kawaida,” amesema Kheri. Aidha, amewapongeza madaktari, wauguzi, manesi na wasimamizi wa sekta ya afya mkoani humo kwa namna walivyojipanga kuwapokea na kuwahudumia majeruhi tangu walipopata taarifa za ajali hiyo. Amesema hakuna mgonjwa aliyepoteza maisha kutokana na uzembe wa wahudumu wa afya, akieleza kuwa majeruhi wote waliopokelewa wameendelea kupatiwa huduma kwa wakati na kwa kuzingatia mahitaji yao ya kiafya. Amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kufuatilia hali za majeruhi hadi watakapopata nafuu, huku wale watakaoruhusiwa kurejea nyumbani wakiendelea kufuatiliwa kuhakikisha wanaimarika kiafya. Pia amewataka madaktari na wahudumu wengine wa afya kuendelea kushirikiana na familia za majeruhi kwa kutoa taarifa za maendeleo ya matibabu katika kila hatua ili ndugu waweze kufahamu kinachoendelea katika vituo vya afya vinavyowahudumia wapendwa wao. Katika hatua nyingine, Kheri ametoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki waliopoteza wapendwa wao katika ajali hiyo, akieleza kuwa ni msiba mkubwa ambao utachukua muda kusahaulika. Amesema viongozi wa Serikali na wadau mbalimbali wataungana na familia zilizofikwa na msiba huo katika kipindi hiki cha maombolezo na shughuli za mazishi, huku akiwataka wananchi kuendelea kuonesha mshikamano na kuwafariji waliofiwa. Kwa upande wake, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake na Uzazi, Scholastica Malangalila, ambaye ni kaimu nafasi ya Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa, amesema hospitali hiyo ilipokea majeruhi watano wa ajali hiyo, wakiwemo mwanaume mmoja na wanawake wanne. Amesema tangu walipopokelewa, hospitali ilijipanga kutoa huduma kulingana na mahitaji ya kila mgonjwa na kwamba hadi wakati akizungumza, majeruhi wote watano walikuwa wakiendelea vizuri. Ameeleza kuwa kwa mujibu wa tathmini ya madaktari, wanatarajia majeruhi hao kurejea katika hali zao za kawaida baada ya siku tatu, iwapo maendeleo ya matibabu yataendelea kuwa mazuri. Kuhusu miili ya watu waliofariki katika ajali hiyo, Malangalila amesema hospitali imeendelea kutoa huduma kwa ndugu waliofika kuitambua na kuchukua miili ya wapendwa wao, huku akibainisha kuwa zoezi hilo lilikuwa likiendelea bila changamoto yoyote.
Tue, 10 Nov 2026 20:10:26 +0000US soldier arrested in UK on Russian espionage allegations
Read the full report from the original source.
RecentlySecurity Council LIVE: South Sudan’s first elections loom amid rising violence
Read the full report from the original source.
RecentlyTob Cohen amended will three times to exclude Sarah Wairimu, court told
Read the full report from the original source.
RecentlyUK court overturns Trinidad and Tobago law criminalizing gay sex
Read the full report from the original source.
RecentlyFIFA presidential hopeful Vega in it to win it
Read the full report from the original source.
RecentlyLawyers threaten nationwide strike until advocate Abshir Abdi is found
Read the full report from the original source.
RecentlyKenya to open missions in Azerbaijan and Congo, closes Bern Embassy
Read the full report from the original source.
RecentlyVodacom Yazindua M-Pesa MCHEZO, Kurahisisha Usimamizi wa Upatu Kidijitali
Kaimu Mkurugenzi wa M-Pesa Vodacom Tanzania Tulisindo Mlupilo (kushoto), Mkurugenzi wa Huduma za Kibenki kwa Wateja Binafsi wa ABSA Bank Ndabu Lilian Swere, (katikati) na Mkurugenzi wa Afropavo Limited Rwebu Mutahaba wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa MCHEZO, huduma mpya ya kidijitali inayowawezesha Watanzania kusimamia vikundi vya upatu kupitia M-Pesa. Huduma hiyo imezinduliwa kupitia ushirikiano wa Vodacom Tanzania, ABSA Bank na Afropavo Limited, kwa lengo la kuimarisha uwazi, kurahisisha usimamizi wa michango na kuhakikisha wanachama wanapata taarifa za miamala ya vikundi vyao. Kaimu Mkurugenzi wa M-Pesa wa Vodacom Tanzania, Tulisindo Mlupilo, akizungumza wakati wa uzinduzi wa M-PESA MCHEZO, huduma mpya ya kidijitali inayowawezesha Watanzania kusimamia vikundi vya upatu kupitia M-Pesa. Uzinduzi huo umefanyika leo Novemba 10, 2026, jijini Dar es Salaam, kwa ushirikiano wa Vodacom Tanzania, ABSA Bank na Afropavo Limited. Meneja wa Huduma Mpya za Kifedha wa M-Pesa, Brenda Msola akielezea namna huduma mpya ya kidijitali ya M-PESA MCHEZO, inayowawezesha Watanzania kuanzisha na kusimamia vikundi vya upatu kupitia M-Pesa, inavyofanya kazi. Wateja wanaweza kujiunga kwa kupiga *150*00#, kuchagua Huduma za Kifedha kisha M-PESA MCHEZO na kuanzisha au kujiunga na vikundi, kuchangia fedha na kufuatilia michango pamoja na taarifa za miamala. Kaimu Mkurugenzi wa M-Pesa wa Vodacom Tanzania, Tulisindo Mlupilo (wa nne kushoto), Mkurugenzi wa Huduma za Kibenki kwa Wateja Binafsi wa ABSA Bank, Ndabu Lilian Swere (wa tano kushoto) na Mkurugenzi wa Afropavo Limited, Rwebu Mutahaba (wa tano kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na wadau kutoka kampuni hizo wakati wa uzinduzi wa MCHEZO, huduma mpya ya kidijitali inayowawezesha Watanzania kusimamia vikundi vya upatu kupitia M-Pesa. Uzinduzi huo umefanyika leo Novemba 10, 2026, kupitia ushirikiano wa Vodacom Tanzania, ABSA Bank na Afropavo Limited. Baadhi ya Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania Plc pamoja na watengenezaji wa maudhui, wakiongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa M-Pesa, Tulisindo Mlupilo, wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa MCHEZO, huduma mpya ya kidijitali inayowawezesha Watanzania kuanzisha na kusimamia vikundi vya upatu kupitia M-Pesa. Huduma hiyo inawawezesha wanachama kuanzisha au kujiunga na vikundi, kuchangia fedha na kufuatilia michango pamoja na taarifa za miamala ya vikundi vyao.
Tue, 10 Nov 2026 19:07:25 +0000From Sakaja to Ochieng Ondugi Randa: Sakaja 'adopted' by Luo elders, endorsed for re-election
The elders bestowed upon him the cultural name Ochieng Odungi Randa, formally welcoming him into the community and urging Luo voters to support his re-election bid.
Tue, 10 Nov 2026 21:52:49 +0300The bar tab is due: Paying for Uganda’s oil before the first drop is pumped
For 20 years, the answer to every Uganda economic problem has been the same. Budget tight? Wait for the oil. Shilling falling? Wait for the…
RecentlyRironi-Mau Summit: Government announces plans to introduce cable cars at the Great Rift Valley Viewpoint
Read the full report from the original source.
RecentlyNews Brief: Why Ruto's Cabinet is under siege
Here are the stories making the headlines.
RecentlyNatembeya, security agencies clash over access to Masinde Muliro Market
Read the full report from the original source.
RecentlyUjenzi Viwango House Mwanza wafikia asilimia 95.2
Read the full report from the original source.
RecentlySERIKALI YATAKA HALMASHAURI KUIMARISHA USIMAMIZI WA TAKA ZA PLASTIKI
Serikali kupitia Ofisi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu -TAMISEMI imezitaka Wilaya ya Ilala, Temeke , Kinondoni pamoja na Mafia kuweke mifumo madhubuti wa uratibu uwajibikaji na ufuatiliaji wa mipango mkakati ya usimamizi wa taka za Plastiki jambo ambalo litaleta na tija kwa taifa katika kulinda mazingira na kuweka msingi wa mabadiliko ya kweli na kutengeneza fursa za kiuchumi. Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati akizindua mipango mkakati ya kuboresha Usimamizi WA Taka za Plastiki Wilaya ya Ilala, Temeke, Mafia na Kinondoni, Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI anayeshughulikia Miundombinu Mhandisi Rogatus Mativila, amesisitiza umuhimu wa vikao vya menejimenti na kamati za halmashauri kuhakikisha ufuatiliaji endelevu pamoja na kujadili utekelezaji wake. Mwenyekiti wa Bodi ya Mtandao wa Mashirika ya Kiraia yanayoshughulikia Mabadiliko ya Tabianchi Tanzania (FORUMCC - Forum CC) Yusta Kibona, meiomba serikali kutoa muongozo Kwa Halmashauri ili vipaombele vya mkakati hiyo viingizwe katika mipango ya maendeleo na bajeti kila mwaka. Mwakilishi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Elias Chundu, amesisitiza umuhimu wa wadau kushirikiana katika kulinda mazingira, kuwepo kwa sheria rafiki na kuimarisha utekelezaji wa mipango ya kupunguza uzalishaji wa taka ngumu. Kwa upande wao Wawakilishi wa halmashauri hizo wameahidi kutekeleza kwa vitendo mikakati iliyowekwa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuhakikisha malengo ya usimamizi bora wa taka za plastiki yanafikiwa. Katika hafla hiyo, wametoa Tuzo kwa masoko waliofanya vizuri katika usimamizi wa mazingira, ikiwa ni sehemu ya kuwahamasisha kuendeleza juhudi za kutunza mazingira.
Tue, 10 Nov 2026 18:53:25 +0000Page 269 of 1146 · 22910 stories