Unganishwa

Search the region

22924 stories

Science · Issa Michuzi

WANAFUNZI WA KIKE WAHAMASISHWA KUSOMA MASOMO YA SAYANSI ILI KUNUFAIKA NA SAMIA SCHOLARSHIP

Na Mwandishi Wetu, Korogwe WANAFUNZI wa Kike katika Shule za Sekondari nchini wametakiwa kusoma kwa bidii masomo ya sayansi ili kuwawezesha kupata ufadhili wa Samia Suluhu ambao utakuwa chachu kwao kuweza kufikia ndoto zao za kielimu. Hayo yalisemwa leo na Mkurugenzi Kampuni ya Shemnyama African Association Business Consultancy and Insurance Agency Rajab Shemnyama ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa maafali ya kidato cha nne katika shule ya Sekondari Old Korogwe, Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga. Ambapo alisema kwamba masomo ya sayansi yatawawezesha kukabiliana na ushindani wa soko la ajira kutokana na utandawazi uliopo Alisema wanafunzi wanapaswa kutumia fursa za elimu kwa kujituma katika masomo ili shule hiyo iweze kuzalisha wataalamu wengi katika fani mbalimbali. Pia, alisisitiza umuhimu wa matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii, akiwataka wanafunzi kuitumia kujifunza na kuongeza maarifa badala ya kujihusisha na mambo yanayoweza kuathiri maadili na maendeleo yao. Aliwaasa kujiepusha na vitendo vya ukatili wa kijinsia na tabia hatarishi zinazoweza kuhatarisha afya na mustakabali wao, huku akisisitiza umuhimu wa kujitambua na kulinda heshima zao. Aidha, alisema elimu inapaswa kwenda sambamba na ujuzi wa ziada utakaowawezesha vijana kujiajiri na kujipatia kipato, hasa kutokana na changamoto ya ajira inayoweza kuwakabili baada ya kuhitimu. Alisisitiza kuwa wanafunzi wanapaswa kushiriki katika matamasha na shughuli za ujasiriamali ili kujenga uwezo wa kujitegemea kiuchumi. Akizungumzia suala la chakula shuleni, Shemnyama aliwataka wazazi kushirikiana na walimu kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula cha mchana, akieleza kuwa njaa huathiri umakini na uwezo wa kufuatilia masomo darasani. Pia, aliomba uongozi wa shule kuimarisha miradi ya kilimo ili kuongeza uzalishaji wa chakula na kuwajengea wanafunzi ujuzi wa kilimo, akibainisha kuwa sekta hiyo inaweza kuwa chanzo cha fursa mbalimbali za kiuchumi kwa vijana. "Lakini pia kupitia Kampuni Yetu hii tutatoa madaftari kwa ajili ya watoto wasiokuwa na wazazi (Mayatima) kwa lengo la kuwapunguzia makali "Alisema Alisema amezipokea changamoto zilizowasilishwa na uongozi wa shule hiyo na kuahidi kushirikiana na wadau wengine kutafuta namna ya kuzitatua. Katika maafali hayo ameahidi kuchangia mifuko 20 ya saruji kwa ajili ya ukarabati wa maktaba ya Shule ya Sekondari Old Korogwe, Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia. Mchango huo umetangazwa na Rajabu Shemnyama, ambaye ni mhitimu wa shule hiyo, wakati wa mahafali ya Kidato cha Nne, akisema hatua hiyo inalenga kuunga mkono juhudi za shule kuinua kiwango cha ufaulu na kuondoa daraja sifuri katika matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne mwaka 2026 Shemnyama alisema ameamua kuchangia maendeleo ya shule hiyo kutokana na kutambua umuhimu wa elimu, akibainisha kuwa yeye ni zao la shule hiyo na anajivunia kuona mabadiliko yaliyofikiwa tangu alipokuwa mwanafunzi. Alisema maendeleo ya elimu yanahitaji ushirikiano wa wadau mbalimbali, hivyo kuwataka wahitimu na watu wengine waliowahi kusoma katika shule hiyo kujitokeza kuchangia kuboresha mazingira ya kujifunzia. Aliongeza kuwa kampuni yake itaendelea kushirikiana na shule hiyo katika shughuli za maendeleo, ikiwamo kuchangia madaftari kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu. Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Old Korogwe, Bilali Shemkai, alisema shule hiyo imeweka mikakati ya kuhakikisha hakuna mwanafunzi atakayepata daraja sifuri katika matokeo ya Kidato cha Nne mwaka 2026. Alisema juhudi hizo zimeanza kuonyesha matokeo kutokana na kupungua kwa idadi ya wanafunzi waliopata daraja hilo kutoka 38 mwaka 2023 hadi 20 mwaka 2024 na 10 mwaka 2025. Alisema mbali na kuondoa daraja sifuri, shule hiyo inalenga kuongeza idadi ya wanafunzi watakaopata madaraja ya kwanza, pili na tatu. Shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 2004 ina jumla ya wanafunzi 520, wakiwamo wasichana 284 na wavulana 236, pamoja na watumishi 32, wakiwamo walimu 31 na mtaalamu mmoja wa maabara. Ina vyumba 14 vya madarasa na maabara tatu, ambapo maabara za Kemia na Baiolojia zimekamilika, huku maabara ya Fizikia ikiwa bado haijakamilika. Pamoja na kuwa na huduma za maji, umeme na barabara, shule hiyo pia ina mradi wa kilimo unaohusisha uzalishaji wa mahindi na majaribio ya kilimo cha mpunga kwa lengo la kuongeza upatikanaji wa chakula. Hata hivyo, shule hiyo bado inakabiliwa na changamoto ya kuhakikisha wanafunzi wote wanapata chakula cha mchana, hali inayoufanya uongozi kuendelea kuwahamasisha wazazi kushiriki katika uchangiaji wa chakula. Kupitia utaratibu uliowekwa, kila mzazi anahamasishwa kuchangia kilo nane za mahindi, kilo mbili za maharage na Sh4,000 kwa kila muhula kwa ajili ya chakula cha wanafunzi. Hata hivyo, utekelezaji wake umekuwa na changamoto kutokana na mwitikio mdogo wa baadhi ya wazazi. Changamoto nyingine ni uchakavu wa baadhi ya vyumba vya madarasa na mazingira ya nje ya shule, ambayo wakati mwingine yanaweza kuathiri utulivu na maandalizi ya wanafunzi kitaaluma. Kutokana na hali hiyo, shule imekuwa ikishirikiana na viongozi wa serikali za mitaa na kata kukabiliana na changamoto zinazoweza kuathiri usalama na maendeleo ya wanafunzi. Uongozi wa shule hiyo unaamini kuwa ushirikiano kati ya wazazi, walimu, wanafunzi, wahitimu na wadau wengine wa elimu utasaidia kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia, pamoja na kufanikisha malengo ya kuinua ufaulu.

Tue, 10 Nov 2026 08:00:17 +0000
Business · Daily News

Barrick revenue hits $5.07bn as gold prices climb

TANZANIA: BARRICK Mining Corporation has recorded a 22 per cent increase in third-quarter this year revenue to 5.07 billion US…

Recently
Uncategorized · Issa Michuzi

KAMISHNA DKT.BADRU ATUA KAMBI YA TIMU YA NGORONGORO KAMA SELEMANI MWALIMU

Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro Dkt. Abdul-Razaq Badru jana usiku tarehe 9 Novemba. 2026 alitua kwenye kambi ya timu hiyo inayoshiriki mashindano ya SHIMMUTA mkoani Morogoro kukagua hali ya kambi hiyo na maendeleo ya wachezaji. Mara baada ya kukutana na wachezaji hao Dkt.Badru ametoa maelekezo ya wanamichezo wa Ngorongoro kutumia fursa hiyo Kama mojawapo ya kujifunza mambo mapya kutoka taasisi nyingine. “Tumieni michezo kuitangaza Ngorongoro, chezeni kwa nguvu zenu zote Ila mkumbuke michezo ni furaha na amani na muwe tayari kupokea aina yoyote ya matokeo,”alisema Dkt.Badru. Afisa Michezo wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Yotham Gitige alimshukuru kamishna kwa ziara hiyo na kusema kuwa imewatia moyo katika ushiriki wao kwenye michezo hiyo.

Tue, 10 Nov 2026 07:56:24 +0000
Uncategorized · The Star Kenya

Betty Maina bids political ‘goodbye’ to Murang’a voters

The Woman Representative says the July Ol Kalou by-election exposed the region’s political shift, prompting her to reconsider her political future.

Recently
Business · Daily News

Viwango SACCOS loan portfolio hits 11bn/-

DAR ES SALAAM: THE Tanzania Standards Bureau (TBS) Viwango SACCOS has recorded an 11bn/- loan portfolio, highlighting the growing role…

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

Honey Traps: sex, lies and a spy's oldest trick

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

China opens undergraduate to PhD scholarships for Kenyans

Thirty scholarships are up for grabs with applicants facing different application procedures and deadlines for the 2027 academic intake.

Recently
Uncategorized · Daily News

From village groups to rural agribusiness corporations

DAR ES SALAAM: FOR decades, Tanzanian agriculture has been organised around village groups. Farmers have come together in cooperatives, savings…

Recently
Uncategorized · Issa Michuzi

RAIS SAMIA AONDOKA NCHINI KUSHIRIKI MKUTANO WA COP31 NCHINI UTURUKI

Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiagana na viongozi mbalimbali katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere JNIA) Jijini Dar es Salaam, tarehe 10 Novemba, 2026 kabla ya kuondoka kuelekea Jijini Antalya, Uturuki, kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 31 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP31).

Tue, 10 Nov 2026 07:36:40 +0000
Technology · The Star Kenya

Huawei Kenya trains students, government officials on cybersecurity

The company said strengthening cybersecurity awareness would contribute to building a safer, more resilient and inclusive digital economy

Recently
Uncategorized · Daily News

Why Tanzania–Angola railway link could boost agricultural trade

TANZANIA: ON Thursday 30th October 2026, local and international media were awash with news of Tanzania and Angola’s agreement to…

Recently
Uncategorized · Daily News

Financial sector expands as investors turn selective

DAR ES SALAAM: FINANCIAL sector delivered a revealing contrast during the week of 2–8 November this year. Investors submitted almost…

Recently
Uncategorized · BBC Rwanda

Ukraine: Ibiganiro vy'amahoro vyasubiye gutangura, buri ruhande rushaka impinduka

Kyiv, Washington na Moscou bose barungitse intumwa muri Emirats Zunze Ubumwe z’Abarabu, mu biganiro vya mbere - kuva muri Ruhuhuma(2)- vy'impande zitatu.

Recently
Business · Daily News

Loan review: How banks make NPLs look healthy

TANZANIA: BANKS publish financial results to demonstrate their financial strength, but headline indicators do not always tell the whole story.…

Recently
Uncategorized · The Ankole Times

USE AND DUMP: Museveni’s Four-decade Political Game Of Exploiting Loyalists Before Throwing Them Under The Bus

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · KBC

Rationalisation: Kenya announces closure of Bern embassy

Foreign Affairs PS Korir Sing’oei says the move is part of ongoing rationalisation of Kenya’s diplomatic footprint globally, involving closing some Missions and opening new ones

Recently
Uncategorized · Daily News

103bn/- govt investment turns innovation into economic value

DAR ES SALAAM: FROM agricultural technologies to digital education and biological crop protection, four decades of government investment in research…

Recently
Uncategorized · Chimpreports

SUCCESSION: NRM CEC Meets Again Today as Muhoozi Eyes Vice Presidency

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Chimpreports

BLOG: What We Leave Woven Into Lives

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Daily News

TRA eyes longer validity for cooking oil import permits

UNGUJA: THE Tanzania Revenue Authority (TRA) is considering extending the validity period of cooking oil import permits to ensure uninterrupted…

Recently

Page 284 of 1147 · 22924 stories