Unganishwa

Search the region

22927 stories

Uncategorized · Chimpreports

Tubaale Safaris Proprietor Arrested Over Alleged $30,000 Tourist Fraud

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Chimpreports

From Nairobi to Kampala: How Ugandans Can Build Wealth Back Home While Doing Business Across Borders

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Rwanda News Agency

Handover ceremony of new Permanent Secretary of MINAFFET Juan Haguma

Read the full report from the original source.

Recently
Sports · Azam TV Videos

Kambi ya Yanga yazidi kunoga Zanzibar, Zimbwe atoa neno

KAMBI YA YANGA: “Ujio wa mwalimu umeongeza kitu kikubwa” Beki wa Yanga SC, Mohamed Hussein Zimbwe anasema kwa sasa wamempata mwalimu na kuelekea katika mechi za NBC Premier League na Ligi ya Mabingwa Afrika, watafanya vizuri. Zimbwe anasema kundi lao kwenye Ligi ya Mabingwa ni gumu na wao wamejipanga vema kuelekea mechi hizo. Kwa upande wake Meneja wa kikosi hicho Walter Harson anasema mapumziko hayo yanatoa fursa kwa benchi jipya la ufundi kuweza kupata muda vema na timu. Yanga kwa sasa ipo Zanzibar, kwa ajili ya maandalizi ya mechi zilizosalia za NBC Premier League pamoja na mashindano mengine. #YangaSC

2026-11-09T19:15:03+00:00
Uncategorized · BBC Afrique

Pourquoi les Sénégalais continuent-ils de prendre la mer malgré les dangers ?

Malgré les naufrages successifs, qui endeuillent des familles, et les nombreuses campagnes de sensibilisation et de dissuasion, les départs vers l’Europe par la mer se multiplient.

Recently
Uncategorized · KT Press

VIDEO – PHOTOS: Rwanda Receives Genocide Fugitive Jean Leonard Teganya From U.S.

Read the full report from the original source.

Recently
Sports · Azam TV Videos

Simba yarejea mazoezi9ni kujiandaa na mechi za NBC Premier League, Ligi ya Mabingwa

SIMBA YAREJEA MZIGONI KUJIFUA: “Wachezaji takribani 27 wote wamewasili hii leo” Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally anasema wachezaji watano ndio bado hawajaripoti kambini kutokana na kuwa na majukumu katika timu zao taifa. Ahmed amewataja wachezaji hao kuwa ni Nathaniel Chilambo, Anthony Mligo, Ino Loemba, Bakari Msimu na golikipa Mahamadou Tanja Kasali. #SimbaSC #KambiSimba

2026-11-09T18:57:12+00:00
Uncategorized · DW Afrique

En Allemagne, vers la dangereuse banalisation du passé nazi

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · KBC

President Ruto appoints five CEOs to state corporations, nominates Data Commissioner

President William Ruto has announced a series of appointments to key State Corporations, filling leadership positions in five institutions as part of efforts to strengthen their management and service delivery.…

Recently
Uncategorized · Issa Michuzi

WATAALAMU WA KUJITOLEA KUTOKA JAPAN WACHANGIA MAENDELEO YA TANZANIA

Na Peter Haule, WF, Dar es Salaam Tanzania imetambua na kuthamini mchango wa Serikali ya Japan kupitia Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) na mpango wa Japan Overseas Cooperation Volunteers (JOCV), katika kukuza maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini kwa kipindi cha miaka 60. Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, wakati akizungumza katika hafla ya kuadhimisha miaka 60 tangu kuanza kwa mpango wa kuleta wataalamu wa kujitolea kutoka Japan nchini Tanzania, iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Bw. Mwandumbya amesema maadhimisho hayo ni fursa muhimu ya kutambua urafiki, mshikamano na ushirikiano wa muda mrefu kati ya Tanzania na Japan, pamoja na kuthamini mchango wa wataalamu wa kujitolea kutoka Japan katika kusaidia juhudi za maendeleo ya Taifa, hususan katika ngazi za jamii. Amesema katika kipindi cha miaka 60, wataalamu kutoka Japan wamechangia maendeleo ya sekta mbalimbali zikiwemo elimu, afya, kilimo, mafunzo ya ufundi na maendeleo ya jamii kupitia uhamishaji wa maarifa, teknolojia na uzoefu, pamoja na kujenga uwezo wa taasisi na watumishi wa Kitanzania. “Mchango wa wataalamu kutoka Japan hauishii katika kutoa huduma za kitaalamu pekee, bali pia umeimarisha uhusiano kati ya wananchi wa Tanzania na Japan kupitia kubadilishana tamaduni, maarifa na uzoefu, hali iliyosaidia kujenga urafiki na mahusiano ya kudumu kati ya wananchi wa mataifa hayo mawili”, amesema Bw. Mwandumbya. Aidha, Bw. Mwandumbya amesema Serikali ya Tanzania inathamini pia mchango wa ushirikiano wa maendeleo unaotolewa na Serikali ya Japan kupitia JICA, ikiwemo mikopo yenye masharti nafuu, misaada na ushirikiano wa kiufundi. Amebainisha kuwa hadi sasa Tanzania imepokea mikopo yenye masharti nafuu kutoka Japan yenye thamani ya zaidi ya Yen bilioni 147.30 na misaada inayozidi Yen bilioni 176.76, huku Watanzania zaidi ya 22,000 wakinufaika na fursa za mafunzo ya kitaalamu nchini Tanzania na Japan. Amesema misaada na mikopo hiyo imechangia uwekezaji katika sekta za usafiri, nishati, maji, kilimo, afya, elimu na maendeleo ya rasilimali watu, hatua zilizosaidia kuboresha utoaji wa huduma za umma, kuongeza uwezo wa uzalishaji na kuweka mazingira wezeshi kwa ukuaji endelevu wa uchumi. Akizungumzia mwelekeo wa ushirikiano huo, Bw. Mwandumbya amesema Serikali itaendelea kushirikiana na Japan na JICA katika maeneo ya kipaumbele yakiwemo miundombinu ya usafiri, maendeleo ya rasilimali watu, uhamishaji wa teknolojia, ubunifu, maendeleo yanayozingatia mabadiliko ya tabianchi, viwanda na uimarishaji wa uwezo wa taasisi. Kwa upande wake, Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Yoichi Mikami, amesema wataalamu wa kujitolea kutoka Japan ni nguzo muhimu katika kuimarisha urafiki na mahusiano kati ya wananchi wa Tanzania na Japan. “Nanajivunia kuona wataalamu wakiendelea kuhudumu nchini Tanzania, kufanya kazi kwa karibu na wananchi, kujenga mahusiano ya kijamii na kukuza uelewa wa tamaduni za mataifa hayo mawili kupitia kubadilishana uzoefu”, amesema Mhe. Balozi Mikami. Naye Makamu wa Rais wa JICA, Bw. Hiroyuki Kobayashi, pamoja na Mwakilishi Mkuu wa JICA nchini Tanzania, Dkt. Katsuya Kuge, wamesema shirika hilo litaendelea kuimarisha ushirikiano na Tanzania katika maendeleo ya rasilimali watu kupitia programu mbalimbali, ikiwemo mpango wa wataalamu wa kujitolea. Wamesema JICA inaendelea kushirikiana na Tanzania katika sekta mbalimbali, ikiwemo usafiri na usafirishaji wa mizigo, pamoja na kutekeleza miradi inayochangia kufikia malengo ya Dira 2050, ambayo yanahitaji ushirikiano wa karibu kati ya wadau mbalimbali wa maendeleo. Akizungumza kwa niaba ya Makatibu Tawala wa Mikoa inayopokea manufaa ya miradi mbalimbali inayotekelezwa kwa ushirikiano na JICA, Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani, Bw. Richard Kayombo, amesema ushirikiano na Japan umekuwa na manufaa makubwa kwa jamii kutokana na wataalamu wa Japan kuishi pamoja na Watanzania, kufanya kazi kwa karibu na wananchi, kujifunza lugha ya Kiswahili na kuelewa tamaduni pamoja na mazingira ya maisha ya Watanzania. Ameeleza kuwa mwingiliano huo umewezesha kubadilishana maarifa, uzoefu na ujuzi, sambamba na kuimarisha uelewa na urafiki kati ya wananchi wa Tanzania na Japan. Ushirikiano kati ya pande hizo mbili ulianza rasmi mwaka 1966 baada ya kusainiwa kwa makubaliano ya mpango wa JOCV, huku kundi la kwanza la wataalamu wa kujitolea kutoka Japan likiwasili nchini mwaka 1967. Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, akieleza mchango wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) na Mpango wa Japan Overseas Cooperation Volunteers (JOCV) katika kukuza maendeleo ya kijamii na kiuchumi, wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwa Mpango wa JOCV, iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Yoichi Mikami, akieleza namna wataalamu wa kujitolea kutoka Japan walivyo nguzo muhimu katika kuimarisha urafiki na mahusiano kati ya Tanzania na Japan, wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwa Mpango wa Japan Overseas Cooperation Volunteers (JOCV), iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, akizungumza na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Yoichi Mikami, kabla ya kuanza kwa hafla ya kuadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwa Mpango wa Japan Overseas Cooperation Volunteers (JOCV), iliyofanyika jijini Dar es Salaam Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, akipata maelezo kuhusu historia ya Makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA), Bw. Hiroyuki Kobayashi, ambaye aliwahi kujitolea nchini Tanzania kama Mwalimu katika eneo la Ujiji, mkoani Kigoma, wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwa Mpango wa Japan Overseas Cooperation Volunteers (JOCV), iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, akizungumza na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Yoichi Mikami, pamoja na viongozi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA), kabla ya kuanza kwa hafla ya kuadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwa Mpango wa Japan Overseas Cooperation Volunteers (JOCV), iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Yoichi Mikami, na Makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA), Bw. Hiroyuki Kobayashi, wakiwa katika picha ya pamoja na wataalamu wa kujitolea kutoka Japan wanaohudumu katika sekta mbalimbali nchini Tanzania, wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwa Mpango wa Japan Overseas Cooperation Volunteers (JOCV), iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Mon, 09 Nov 2026 19:03:38 +0000
Uncategorized · The Star Kenya

News Brief: NHC delivers 50,000 homes

These are the stories making the headlines inyour Free Copy of the Tuesday Star

Recently
Uncategorized · Rwanda News Agency

Rwandan genocide fugitive Teganya Jean Léonard deported from US

Read the full report from the original source.

Recently
Sports · Azam TV Videos

Magwiji Yanga watoa neno kuhusu Kocha Fadlu Davids

MAGWIJI WA YANGA: “Fadlu ni mwalimu ambaye nimemuona wakati yupo Simba” Mchezaji wa zamani wa Yanga SC, Makumbi Juma anasema wakati Kocha Fadlu Davids anaifundisha Simba SC, kikosi hicho hakikuwa bora japo aliifikisha mbali. Makumbi anasema Kocha Fadlu akikutana na kikosi chenye wachezaji wazuri, atafanya vizuri. Kwa upande wake mchezaji wa zamani Bakari Malima, anasema Yanga ina wachezaji wazuri ambao Kocha Fadlu anaweza kuwafanya wawe imara ndani ya kipindi kifupi. #YangaSC #Mshikemshike

2026-11-09T18:39:34+00:00
National · Issa Michuzi

SERIKALI YAZITAKA TAASISI KUIMARISHA USHIRIKIANO KUFANIKISHA TATHMINI YA UTAKASISHAJI FEDHA HARAMU NA UFADHILI WA UGAIDI MWAKA 2028

Na. Josephine Majura, WF, Morogoro Serikali imezitaka taasisi zote zinazohusika na mapambano dhidi ya utakatishaji fedha haramu, ufadhili wa ugaidi na ufadhili wa silaha za maangamizi kuimarisha ushirikiano na uwajibikaji katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuiwezesha Tanzania kufanya vizuri zaidi katika Tathmini ya Tatu ya Mfumo wa Kupambana na Utakasishaji Fedha Haramu, Ufadhili wa Ugaidi na Ufadhili wa Silaha za Maangamizi (AML/CFT/CPF) inayotarajiwa kufanyika mwaka 2028. Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), wakati akifungua mafunzo ya maandalizi ya tathmini hiyo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Cate Hotel, Morogoro, chini ya Kundi la Afrika Mashariki na Kusini la Kupambana na Utakatishaji Fedha Haramu (ESAAMLG). Mhe. Munde amesema Serikali imejipanga kuhakikisha Tanzania inajiandaa kikamilifu kwa tathmini hiyo kwa kuimarisha mifumo ya kisheria, usimamizi, na utekelezaji wa majukumu ya taasisi zinazohusika. "Mapambano dhidi ya uhalifu huo hayawezi kufanikiwa kwa kutegemea Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) pekee, bali yanahitaji ushiriki wa pamoja wa taasisi zote zenye dhamana ya kupambana na uhalifu huo, zikiwemo Jeshi la Polisi, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na Idara ya Usalama wa Taifa (TISS), alisema Mhe. Mhandisi Munde. Ameeleza kuwa licha ya hatua zilizopigwa na Tanzania katika tathmini zilizopita, maandalizi ya tathmini ya mwaka 2028 yanahitaji kuimarisha zaidi utekelezaji wa viwango vya kimataifa na kuweka ushahidi wa matokeo halisi yanayopatikana kupitia shughuli za taasisi husika. Aidha amebainisha kuwa mafunzo hayo yanalenga kuongeza uelewa na uwezo wa watendaji kuhusu viwango vya kimataifa na wajibu wa kila taasisi, pamoja na kuimarisha uratibu na ubadilishanaji wa taarifa ili kuhakikisha maandalizi ya tathmini yanazingatia hali halisi ya utekelezaji. Mhe Mhandisi Munde, amesema mafunzo hayo yatatoa fursa kwa taasisi kubadilishana uzoefu, kujadili changamoto zinazokabili utekelezaji wa majukumu yao na kuweka mikakati ya pamoja ya kuzitatua. Amesisitiza kuwa udhaifu katika hatua yoyote ya mchakato wa haki jinai, kuanzia uchunguzi, uendeshaji wa mashauri hadi utoaji wa hukumu, unaweza kuathiri ufanisi wa mfumo mzima wa mapambano dhidi ya uhalifu huo. Amesisitiza kuwa maandalizi ya tathmini hiyo ni wajibu wa kitaifa unaohitaji ushirikiano endelevu na uwajibikaji wa kila taasisi ili kuimarisha mfumo wa fedha, kulinda rasilimali za umma na kuongeza imani ya washirika wa kimataifa katika uchumi wa Tanzania. Kwa upande wake, mwakilishi wa Katibu Mtendaji wa Kundi la Afrika Mashariki na Kusini la Kupambana na Utakasishaji Fedha Haramu (ESAAMLG) Bw. Joseph Jagada, ameipongeza Tanzania kwa kuonesha dhamira thabiti na utashi wa kisiasa katika kuimarisha mifumo ya kukabiliana na uhalifu wa kifedha, ikiwemo utakatishaji fedha na ufadhili wa ugaidi. Amesema ushiriki wa viongozi waandamizi wa Serikali katika shughuli hiyo unaonesha dhamira ya dhati ya Taifa katika kuhakikisha maandalizi ya tathmini yanafanyika kwa umakini na kupewa kipaumbele kinachostahili. Aidha, amesisitiza kuwa dhamira hiyo ya Serikali ya Tanzania ni mfano mzuri unaopaswa kuigwa na nchi nyingine wanachama wa ESAAMLG, huku akiwahimiza wataalamu na watendaji wa taasisi mbalimbali kutekeleza majukumu yao kwa weledi, uwajibikaji na ushirikiano ili kufanikisha maandalizi ya tathmini hiyo. Naye Kamishna wa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU), Wizara ya Fedha, Bw. Majaba Magana, ameeleza kuwa tathmini za kimataifa hufanyika ili kupima hatua zilizofikiwa na nchi katika kutekeleza viwango vya kimataifa vya kupambana na utakatishaji fedha haramu na ufadhili wa ugaidi, huku zikizingatia mabadiliko ya mbinu zinazotumiwa na wahalifu na umuhimu wa kuendelea kuboresha sheria, kanuni na mifumo ya udhibiti. Amefafanua kuwa tathmini hizo ni muhimu katika kubaini mafanikio na mapungufu yaliyopo, kuimarisha uwezo wa taasisi husika na kulinda mifumo ya fedha dhidi ya uhalifu. Mafunzo hayo yalihudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bw. Nsubili Joshua, Naibu Gavana wa Benki Kuu na Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Udhibiti Utakasishaji Fedha Haramu Bi. Sauda Msemo, Wasimamizi wa Taasisi za Fedha, Taasisi za Fedha zenyewe, Taasisi za Uchunguzi, Waendesha Mashtaka, Sekta Binafsi, Taasisi zisizo za kifedha za biashara na huduma kwa ujumla wao toka pande zote mbili za Muungano. Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Mhandisi  Mshamu Ali Munde akizungumza wakati  akifungua mafunzo ya Tathmini ya Tatu ya Mfumo wa Kupambana na Utakasishaji Fedha Haramu, Ufadhili wa Ugaidi na Ufadhili wa Silaha za Maangamizi (AML/CFT/CPF) inayotarajiwa mwaka 2028 yaliyofanyika katika Ukumbi wa Cate Hotel, Morogoro. Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde, akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bw. Nsubili Joshua, wakati mafunzo ya Tathmini ya Tatu ya Mfumo wa Kupambana na Utakasishaji Fedha Haramu, Ufadhili wa Ugaidi na Ufadhili wa Silaha za Maangamizi (AML/CFT/CPF) inayotarajiwa mwaka 2028 yaliyofanyika katika Ukumbi wa Cate Hotel, Morogoro. Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde, akiteta jambo na Naibu Gavana wa Benki Kuu na Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Udhibiti Utakasishaji Fedha Haramu Bi. Sauda Msemo, wakati mafunzo ya Tathmini ya Tatu ya Mfumo wa Kupambana na Utakasishaji Fedha Haramu, Ufadhili wa Ugaidi na Ufadhili wa Silaha za Maangamizi (AML/CFT/CPF) inayotarajiwa mwaka 2028 yaliyofanyika katika Ukumbi wa Cate Hotel, Morogoro. Baadhi ya washiriki wakifuatilia mawasilisho mbalimbali yaliyotolewa wakati wa mafunzo ya Tathmini ya Tatu ya Mfumo wa Kupambana na Utakasishaji Fedha Haramu, Ufadhili wa Ugaidi na Ufadhili wa Silaha za Maangamizi (AML/CFT/CPF) inayotarajiwa mwaka 2028 yaliyofanyika katika Ukumbi wa Cate Hotel, Morogoro.

Mon, 09 Nov 2026 18:45:14 +0000
Uncategorized · Business Daily

IMF wants Kenya to identify crypto traders in crime fight

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · DW Rwanda

Pope Leo draws 2.5 million to Argentina mass, warns against austerity

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

MCK's Bwire among 9 shortlisted for KNCHR CEO

The commission also invited members of the public to submit, in writing, any credible information concerning the shortlisted candidates

Recently
Uncategorized · KBC

Ruto announces five State Corporation CEO appointments

President William Ruto has announced a series of appointments to key State Corporations, filling leadership positions in five institutions as part of efforts to strengthen their management and service delivery.…

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

President Ruto nominates Lydia Chelagat as Kenya’s next Data Commissioner

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Business Daily

Retailers make billions as Naivas reports Sh3.3bn profit

Read the full report from the original source.

Recently

Page 291 of 1147 · 22927 stories