Search the region
22934 stories
SERIKALI YAZITAKA TAASISI KUIMARISHA USHIRIKIANO KUFANIKISHA TATHMINI YA UTAKASISHAJI FEDHA HARAMU NA UFADHILI WA UGAIDI MWAKA 2028
Na. Josephine Majura, WF, Morogoro Serikali imezitaka taasisi zote zinazohusika na mapambano dhidi ya utakatishaji fedha haramu, ufadhili wa ugaidi na ufadhili wa silaha za maangamizi kuimarisha ushirikiano na uwajibikaji katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuiwezesha Tanzania kufanya vizuri zaidi katika Tathmini ya Tatu ya Mfumo wa Kupambana na Utakasishaji Fedha Haramu, Ufadhili wa Ugaidi na Ufadhili wa Silaha za Maangamizi (AML/CFT/CPF) inayotarajiwa kufanyika mwaka 2028. Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), wakati akifungua mafunzo ya maandalizi ya tathmini hiyo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Cate Hotel, Morogoro, chini ya Kundi la Afrika Mashariki na Kusini la Kupambana na Utakatishaji Fedha Haramu (ESAAMLG). Mhe. Munde amesema Serikali imejipanga kuhakikisha Tanzania inajiandaa kikamilifu kwa tathmini hiyo kwa kuimarisha mifumo ya kisheria, usimamizi, na utekelezaji wa majukumu ya taasisi zinazohusika. "Mapambano dhidi ya uhalifu huo hayawezi kufanikiwa kwa kutegemea Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) pekee, bali yanahitaji ushiriki wa pamoja wa taasisi zote zenye dhamana ya kupambana na uhalifu huo, zikiwemo Jeshi la Polisi, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na Idara ya Usalama wa Taifa (TISS), alisema Mhe. Mhandisi Munde. Ameeleza kuwa licha ya hatua zilizopigwa na Tanzania katika tathmini zilizopita, maandalizi ya tathmini ya mwaka 2028 yanahitaji kuimarisha zaidi utekelezaji wa viwango vya kimataifa na kuweka ushahidi wa matokeo halisi yanayopatikana kupitia shughuli za taasisi husika. Aidha amebainisha kuwa mafunzo hayo yanalenga kuongeza uelewa na uwezo wa watendaji kuhusu viwango vya kimataifa na wajibu wa kila taasisi, pamoja na kuimarisha uratibu na ubadilishanaji wa taarifa ili kuhakikisha maandalizi ya tathmini yanazingatia hali halisi ya utekelezaji. Mhe Mhandisi Munde, amesema mafunzo hayo yatatoa fursa kwa taasisi kubadilishana uzoefu, kujadili changamoto zinazokabili utekelezaji wa majukumu yao na kuweka mikakati ya pamoja ya kuzitatua. Amesisitiza kuwa udhaifu katika hatua yoyote ya mchakato wa haki jinai, kuanzia uchunguzi, uendeshaji wa mashauri hadi utoaji wa hukumu, unaweza kuathiri ufanisi wa mfumo mzima wa mapambano dhidi ya uhalifu huo. Amesisitiza kuwa maandalizi ya tathmini hiyo ni wajibu wa kitaifa unaohitaji ushirikiano endelevu na uwajibikaji wa kila taasisi ili kuimarisha mfumo wa fedha, kulinda rasilimali za umma na kuongeza imani ya washirika wa kimataifa katika uchumi wa Tanzania. Kwa upande wake, mwakilishi wa Katibu Mtendaji wa Kundi la Afrika Mashariki na Kusini la Kupambana na Utakasishaji Fedha Haramu (ESAAMLG) Bw. Joseph Jagada, ameipongeza Tanzania kwa kuonesha dhamira thabiti na utashi wa kisiasa katika kuimarisha mifumo ya kukabiliana na uhalifu wa kifedha, ikiwemo utakatishaji fedha na ufadhili wa ugaidi. Amesema ushiriki wa viongozi waandamizi wa Serikali katika shughuli hiyo unaonesha dhamira ya dhati ya Taifa katika kuhakikisha maandalizi ya tathmini yanafanyika kwa umakini na kupewa kipaumbele kinachostahili. Aidha, amesisitiza kuwa dhamira hiyo ya Serikali ya Tanzania ni mfano mzuri unaopaswa kuigwa na nchi nyingine wanachama wa ESAAMLG, huku akiwahimiza wataalamu na watendaji wa taasisi mbalimbali kutekeleza majukumu yao kwa weledi, uwajibikaji na ushirikiano ili kufanikisha maandalizi ya tathmini hiyo. Naye Kamishna wa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU), Wizara ya Fedha, Bw. Majaba Magana, ameeleza kuwa tathmini za kimataifa hufanyika ili kupima hatua zilizofikiwa na nchi katika kutekeleza viwango vya kimataifa vya kupambana na utakatishaji fedha haramu na ufadhili wa ugaidi, huku zikizingatia mabadiliko ya mbinu zinazotumiwa na wahalifu na umuhimu wa kuendelea kuboresha sheria, kanuni na mifumo ya udhibiti. Amefafanua kuwa tathmini hizo ni muhimu katika kubaini mafanikio na mapungufu yaliyopo, kuimarisha uwezo wa taasisi husika na kulinda mifumo ya fedha dhidi ya uhalifu. Mafunzo hayo yalihudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bw. Nsubili Joshua, Naibu Gavana wa Benki Kuu na Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Udhibiti Utakasishaji Fedha Haramu Bi. Sauda Msemo, Wasimamizi wa Taasisi za Fedha, Taasisi za Fedha zenyewe, Taasisi za Uchunguzi, Waendesha Mashtaka, Sekta Binafsi, Taasisi zisizo za kifedha za biashara na huduma kwa ujumla wao toka pande zote mbili za Muungano. Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde akizungumza wakati akifungua mafunzo ya Tathmini ya Tatu ya Mfumo wa Kupambana na Utakasishaji Fedha Haramu, Ufadhili wa Ugaidi na Ufadhili wa Silaha za Maangamizi (AML/CFT/CPF) inayotarajiwa mwaka 2028 yaliyofanyika katika Ukumbi wa Cate Hotel, Morogoro. Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde, akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bw. Nsubili Joshua, wakati mafunzo ya Tathmini ya Tatu ya Mfumo wa Kupambana na Utakasishaji Fedha Haramu, Ufadhili wa Ugaidi na Ufadhili wa Silaha za Maangamizi (AML/CFT/CPF) inayotarajiwa mwaka 2028 yaliyofanyika katika Ukumbi wa Cate Hotel, Morogoro. Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde, akiteta jambo na Naibu Gavana wa Benki Kuu na Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Udhibiti Utakasishaji Fedha Haramu Bi. Sauda Msemo, wakati mafunzo ya Tathmini ya Tatu ya Mfumo wa Kupambana na Utakasishaji Fedha Haramu, Ufadhili wa Ugaidi na Ufadhili wa Silaha za Maangamizi (AML/CFT/CPF) inayotarajiwa mwaka 2028 yaliyofanyika katika Ukumbi wa Cate Hotel, Morogoro. Baadhi ya washiriki wakifuatilia mawasilisho mbalimbali yaliyotolewa wakati wa mafunzo ya Tathmini ya Tatu ya Mfumo wa Kupambana na Utakasishaji Fedha Haramu, Ufadhili wa Ugaidi na Ufadhili wa Silaha za Maangamizi (AML/CFT/CPF) inayotarajiwa mwaka 2028 yaliyofanyika katika Ukumbi wa Cate Hotel, Morogoro.
Mon, 09 Nov 2026 18:45:14 +0000IMF wants Kenya to identify crypto traders in crime fight
Read the full report from the original source.
RecentlyPope Leo draws 2.5 million to Argentina mass, warns against austerity
Read the full report from the original source.
RecentlyMCK's Bwire among 9 shortlisted for KNCHR CEO
The commission also invited members of the public to submit, in writing, any credible information concerning the shortlisted candidates
RecentlyRuto announces five State Corporation CEO appointments
President William Ruto has announced a series of appointments to key State Corporations, filling leadership positions in five institutions as part of efforts to strengthen their management and service delivery.…
RecentlyPresident Ruto nominates Lydia Chelagat as Kenya’s next Data Commissioner
Read the full report from the original source.
RecentlyRetailers make billions as Naivas reports Sh3.3bn profit
Read the full report from the original source.
RecentlyRC SENDIGA AZINDUA NAMBA MAALUMU YA SIMU KUPOKEA KERO ZA WANANCHI
Na Farida Mangube, Morogoro Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Queen Sendiga, amezindua namba maalumu ya simu itakayowawezesha wananchi kuwasilisha kero, changamoto na maoni yao ili zipatiwe ufumbuzi kwa haraka. Uzinduzi huo umefanyika Novemba 9, 2026, katika Ukumbi wa Mikutano wa Magadu, Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Sendiga amesema hatua hiyo ni sehemu ya jitihada za Serikali za kuhakikisha changamoto za wananchi zinashughulikiwa kwa wakati, akisisitiza umuhimu wa kuzitafutia ufumbuzi kwa haraka. Amesema wananchi watatumia namba 0800114045 kuwasilisha kero zao bila malipo, huku gharama za huduma hiyo zikigharamiwa na Serikali.
Mon, 09 Nov 2026 18:25:17 +0000Sellers drop shilling for dollar, euro land prices to woo buyers
Read the full report from the original source.
RecentlyLa malnutrition : manger à sa faim ne veut pas dire manger sainement
Read the full report from the original source.
RecentlyAmerika yoherereje u Rwanda Teganya Jean Léonard ukekwaho Jenoside
Ubushinjacyaha Bukuru bwatangaje ko bwakiriye Teganya Jean Léonard woherejwe mu Rwanda na Leta Zunze Ubumwe za Amerika, aho akurikiranyweho uruhare mu byaha bya Jenoside n’ibyaha byibasiye inyokomuntu byakozwe mu gihe cy
RecentlyState: Raila International Stadium 94% done
PS Kiptoo said the progress was confirmed during an inspection tour of the 60,000-seater facility led by Head of Public Service Felix Koskei.
RecentlyWAZIRI WA MAMBO YA NJE WA OMAN AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI
Waziri wa Mambo ya Nje wa Usultani wa Oman, Mhe. Sayyid Badr bin Hamad bin Hamood Albusaidi, Novemba 9, 2026 amewasili nchini Tanzania kwa ziara ya kikazi. Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Mhe. Albusaidi amepokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo. Katika ziara hiyo, Mhe. Albusaidi atashiriki kama Mgeni Maalumu katika Mkutano wa Tatu wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Oman (Joint Permanent Commission – JPC), unaofanyika kisiwani Zanzibar.
Mon, 09 Nov 2026 18:19:46 +0000Former Real Madrid star Raul to coach Oviedo
Read the full report from the original source.
RecentlyTob Cohen feared for his life before disappearance, murder trial hears
Read the full report from the original source.
RecentlyTrump questions midterm elections integrity
Trump has previously cast doubt on the integrity of US election results
RecentlyWANANCHI WATAKIWA KUWA NA IMANI NA TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA
NA MWANDISHI WETU Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Omar Ali Bhai, amewataka Watanzania kuwa na imani na Tume hiyo kwa kuwasilisha malalamiko na changamoto zao, akiahidi kuwa zitashughulikiwa kwa wakati. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam baada ya kikao cha Mwenyekiti wa Tume hiyo, Dunford George Mpelumbe, na wafanyakazi wa Tume, Bhai amesema Tume imejipanga kuimarisha huduma kwa wananchi, ikiwemo matumizi ya mifumo ya kidijitali katika kupokea na kushughulikia malalamiko. Amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, wakati wa kuwaapisha viongozi hao, alitoa maelekezo ya kuhakikisha Tume haitegemei malalamiko pekee bali pia inachukua hatua za kufuatilia changamoto za wananchi. Kwa upande wake, Ofisa Mtendaji wa THBUB Tawi la Dar es Salaam, Shoma Phili, amesema hadi Oktoba 2026, Tume ilikuwa na jumla ya malalamiko 262 yanayoendelea kushughulikiwa, yakiwemo 28 ya Haki za Binadamu, 104 ya Utawala Bora na 130 ya Haki Jinai. Ameeleza kuwa katika kipindi hicho, malalamiko mapya sita yalipokelewa, huku 11 ya awali yakifungwa au kuombewa vibali vya kufungwa. Awali, Katibu Mtendaji wa Tawi hilo, Patience Ntwina, amesema wamejipanga kuimarisha utendaji kazi na kuhakikisha changamoto mbalimbali zinazowasilishwa zinapatiwa ufumbuzi. Bhai amewahimiza pia wananchi kuendelea kushirikiana na Tume hiyo, huku akivitaka vyombo vya habari kushiriki katika kutoa elimu na taarifa zitakazosaidia kufanikisha majukumu yake.
Mon, 09 Nov 2026 18:12:23 +0000TISEZA YATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI KATIKA KILIMO CHA HORTICULTURE.
Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) imewahimiza wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuchangamkia fursa zilizopo katika sekta ya kilimo cha bustani (Horticulture), hususan uwekezaji katika uzalishaji, uhifadhi, usafirishaji na uongezaji thamani wa mazao. Meneja Uhamasishaji wa Uwekezaji wa nje kutoka TISEZA, Daudi Riganda, amesema sekta hiyo inayojumuisha maua, matunda, mbogamboga na viungo inaendelea kuwa na fursa za kiuchumi kupitia mauzo ya nje na kuvutia mitaji, huku akitaja uwekezaji katika umwagiliaji, maghala, vyumba vya ubaridi (Cold Rooms), vituo vya kuhifadhi mazao (Cold Stores) na viwanda vya kuongeza thamani. Akizungumza katika Maonesho ya Hortilogistical Africa 2026, Riganda amesema TISEZA imeshiriki kutoa elimu na kuhamasisha uwekezaji, huku ikitumia kituo cha huduma za pamoja (One Stop Center) kinachojumuisha taasisi takribani 15 za Serikali kuwezesha wawekezaji kupata huduma sehemu moja badala ya kufuata taasisi mbalimbali, amesema mwekezaji anayekidhi vigezo na kukamilisha nyaraka zinazohitajika anaweza kupata cheti cha uwekezaji ndani ya saa 24. Ameeleza kuwa kwa mujibu wa masharti aliyoyataja, Mtanzania anahitaji mtaji wa takribani Sh milioni 150, sawa na Dola za Marekani 50,000, huku mwekezaji wa kigeni au ubia akihitaji Dola za Marekani 500,000, akiwahimiza Watanzania kutumia fursa zilizopo katika sekta hiyo. Kwa upande wa Ofisi ya Mageuzi ya Kilimo, mwakilishi wake amesema moja ya malengo yanayohamasishwa kupitia maonesho hayo ni kupunguza upotevu wa mazao ya bustani baada ya mavuno kutoka asilimia 40 hadi asilimia 20, kupitia uwekezaji katika miundombinu ya uhifadhi na uongezaji thamani. Fursa hizo zinahusisha mazao ya kimkakati yakiwemo parachichi, ndizi, zabibu na viungo. Naye Nasrul Salum Nasrul kutoka Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), amesema ushiriki wao katika kituo hicho unalenga kuwaunganisha wazalishaji na masoko ya ndani, kikanda na kimataifa, pamoja na kukuza wajasiriamali wadogo ili waweze kupanua biashara zao na kufikia masoko makubwa. Kwa upande wake, Tulibako Minga kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA), amesema kituo hicho kinatoa huduma kwa wadau wa mnyororo wa thamani wa Horticulture, kuanzia uzalishaji, biashara ya ndani na nje ya nchi hadi usafirishaji wa mazao. Naye Mdili Katemani kutoka Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA), amesema mamlaka hiyo inasaidia kufungua masoko mapya ya kimataifa, kukagua mazao yanayosafirishwa nje ya nchi na kutoa cheti cha afya ya mimea huku ikiwawezesha wakulima kupata taarifa na kutimiza masharti ya masoko ya kimataifa.
Mon, 09 Nov 2026 18:15:54 +0000Homeowners ditch grills and padlocks for discreet, smarter security systems
Read the full report from the original source.
RecentlyPolice appeal for identification of decapitated woman linked to Masaka serial killer suspect
The police are asking the public to help identify a woman whose severed head and headless body were found at separate locations in Greater Masaka,…
RecentlyPage 292 of 1147 · 22934 stories