Unganishwa

Search the region

22943 stories

Uncategorized · The Standard

Lenku's FEDA party set to shake up Maa politics ahead of 2027 polls

The unveiling of Governor Ole Lenku's FEDA party could significantly alter the political arithmetic across the Maa community ahead of the 2027 General Election.

Sun, 08 Nov 2026 12:42:28 +0300
Uncategorized · The Star Kenya

Wamuchomba to Gachagua: I’m sorry, forgive me

Githunguri MP says she is willing to apologise to the former Deputy President, challenging him to unite Mt Kenya leaders instead of branding critics traitors.

Recently
Uncategorized · KBC

President Ruto begins four-day development tour in Gusii region

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

Nairobi residents face 24-hour water interruption

The water supply interruption will affect several residential estates, commercial areas and public institutions within Nairobi City County.

Recently
Uncategorized · BBC Afrique

Est-ce le début de l'indépendance économique de l'Afrique ?

De nombreux pays africains cherchent de plus en plus à valoriser leurs ressources en les transformant localement plutôt qu'en les vendant à l'état brut.

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

What we know so far after Krakow gun attack

The attack began shortly before 15:00 local time (14:00 GMT) in Krakow's Main Market Square, bustling central point of the city which is popular with tourists

Recently
Uncategorized · Mwananchi

TUONGEE KIUME: Kwa nini unawasahau wazazi kisa mke?

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Watchdog Uganda

One-on-One: Fred Ssenoga on building a complete economic ecosystem through Union Transport Alliance

The Union Transport Alliance chief executive discusses how digitalisation, access to finance, fuel, insurance, healthcare and online commerce could transform Uganda’s transport sector and the livelihoods of people who de

Recently
Uncategorized · Watchdog Uganda

LOCAL GOVERNMENT FOCUS: Kumumanya credits Museveni for decentralisation

In an interview with Brian Mugenyi, Ministry of Local Government Permanent Secretary Ben Kumumanya explains the philosophy behind Uganda's decentralisation policy, President Museveni's contribution, the responsibilities

Recently
Uncategorized · Issa Michuzi

POSTA TANZANIA YASHIRIKI MKUTANO WA MWAKA WA PMI, YATOA MAFUNZO YA USIMAMIZI WA MIRADI

Shirika la Posta Tanzania (TPC) limeendelea kuonesha mchango wake katika kuimarisha usimamizi na utekelezaji wa miradi kwa kutoa Mfunzo katika Mkutano wa Mwaka wa Taasisi ya Wataalamu wa Usimamizi wa Miradi Tanzania (PMI Tanzania Project Management Week & Annual Conference 2026), uliofanyika Novemba 5, 2026, katika ukumbi wa mikutano wa Cate Hotel, mkoani Morogoro. Mkutano huo ulilenga kuwakutanisha wataalamu wa usimamizi wa miradi, viongozi wa taasisi mbalimbali na wadau wengine kwa ajili ya kubadilishana maarifa, uzoefu, ubunifu na kujadili namna bora ya kuimarisha usimamizi na utekelezaji wa miradi nchini. Katika mkutano huo, Shirika la Posta Tanzania lilipata nafasi ya kushiriki katika mjadala wa jopo (Panel Discussion) uliokuwa na mada isemayo “Project Management Office in the Public Sector” (Ofisi ya Usimamizi wa Miradi katika Taasisi za Umma), ambapo Meneja wa Ofisi ya Miradi wa Shirika la Posta Tanzania, Bw. Seleman Daffy, alikuwa mzungumzaji (Speaker), huku Mjumbe wa Bodi na Makamu wa Rais wa Masuala ya Wanaojitolea wa Jumuiya ya Wataalamu wa Usimamizi wa Miradi Tanzania, Bi. Rahma Kova, akiwa msimamizi wa mjadala huo (Moderator). Akizungumza mara baada ya kushiriki mjadala huo, Bw. Daffy amesema, majadiliano hayo yalikuwa na manufaa makubwa, kwani yalitoa fursa ya kubadilishana uzoefu na kuonesha umuhimu wa taasisi za umma na binafsi kuwa na ofisi maalumu za usimamizi wa miradi. Amesema kupitia mjadala huo, imeonekana kuwa taasisi nyingine zinaweza kujifunza kutokana na uzoefu wa Shirika la Posta Tanzania katika kutekeleza mfumo huo wa usimamizi wa miradi. Kwa upande wake, Bi. Rahma Kova, amesema Posta ilipewa nafasi hiyo kutokana na kutambuliwa kwake kama miongoni mwa taasisi chache zenye ofisi maalumu ya usimamizi wa miradi, hivyo uzoefu wake ulikuwa muhimu kushirikishwa na wataalamu wengine waliohudhuria mkutano huo. Kupitia ushiriki huo, Shirika la Posta Tanzania limepata fursa ya kutangaza uzoefu wake katika usimamizi wa miradi na kushiriki katika mijadala ya kitaalamu inayolenga kuimarisha utendaji wa taasisi, matumizi bora ya rasilimali na utekelezaji wenye tija wa miradi kwa maendeleo ya Taifa.

Sun, 08 Nov 2026 09:12:29 +0000
Uncategorized · DW Rwanda

Germany news: Friedrich Merz set to confirm presidential nominee

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · KBC

Kenyan youth warned against fraudsters exploiting demand for overseas jobs

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

Recognising signs of a stroke

Sudden weakness or numbness in one arm is another warning sign, especially when the individual struggles to raise or keep the arm elevated.

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

Gachagua sets conditions for Mt Kenya support in 2027

The DCP leader says the region will no longer surrender its votes without negotiations, insisting that any opposition pact must address Mt Kenya's needs

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

Crew member missing as Indonesian water-bombing helicopter crashes

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

Kappa crowned Red Bull Wings Cup national champion

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

They are too much! Charlene unhappy with dad's security

In a moment that captured her displeasure, Charlene was seen signalling the security officers to allow her friends to accompany her, seemingly unhappy

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

They are too much! Charlene unhappy with dad's security

In a moment that captured her displeasure, Charlene was seen signalling the security officers to allow her friends to accompany her, seemingly unhappy

Recently
Uncategorized · Issa Michuzi

MULOKOZI ACHANGIA MILIONI 100 KANISA KATOLIKI MBULU

Na Mwandishi Wetu. MWENYEKITI wa Makampuni ya Mati Group of Companies Ltd, David Mulokozi, amechangia Sh milioni 100 kupitia kampuni ya Mati Super Brands Ltd pamoja na familia yake binafsi, kusaidia miradi ya maendeleo ya Jimbo Katoliki la Mbulu. Mchango huo umetolewa katika harambee iliyofanyika ndani ya Dekania ya Babati, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya maadhimisho ya Jubilei ya Almasi ya miaka 75 tangu kuanzishwa kwa Jimbo Katoliki la Mbulu, ambapo Mulokozi alikuwa mgeni rasmi. Akizungumza katika hafla hiyo, Mulokozi alisema mchango wake umetokana na imani yake kwa Mungu, akieleza kuwa kila alichonacho ni zawadi kutoka kwake na kwamba kuchangia maendeleo ya Kanisa na nyumba za ibada ni njia mojawapo ya kumshukuru Mungu. Alisema kusaidia shughuli za maendeleo ya Kanisa kwake ni sehemu ya imani na nadhiri yake mbele za Mungu, huku akihimiza jamii kuendeleza utamaduni wa kujitolea kwa kuchangia miradi ya maendeleo kulingana na uwezo wa kila mmoja. Aliongeza kuwa maendeleo ya taasisi za kidini yanahitaji ushirikiano wa waumini, wadau na watu wenye mapenzi mema, akisisitiza kuwa kila mchango unaotolewa kwa moyo wa kujitolea una nafasi muhimu katika kufanikisha malengo yaliyowekwa. Akisoma taarifa ya harambee hiyo, Dekano wa Dekania ya Babati, Reginald Kimati, alisema jumla ya fedha zilizopatikana pamoja na ahadi zilizotolewa zimevuka Sh milioni 200 zilizolengwa kukusanywa katika dekania hiyo. Alisema Jimbo Katoliki la Mbulu limeweka lengo la kukusanya Sh bilioni mbili kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwemo ujenzi wa hosteli za malazi, ukumbi, jukwaa la kudumu kwa ajili ya maadhimisho ya kijimbo pamoja na kuchangia ujenzi wa kituo cha kichungaji mjini Babati. Kimati alisema kukamilika kwa miradi hiyo kutasaidia kuboresha mazingira ya huduma za kichungaji na kuongeza uwezo wa Kanisa kuhudumia waumini pamoja na wadau mbalimbali watakaoshiriki shughuli za kijimbo. Kwa upande wake, Askofu wa Jimbo Katoliki la Mbulu, Mhashamu Anthony Lagwen, alimpongeza Mulokozi kwa mchango wake na moyo wa kujitolea, akisema hatua hiyo ni mfano mzuri wa ushirikiano katika kuendeleza miradi ya Kanisa. Alisisitiza kuwa fedha zitakazokusanywa zitatumika kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuhakikisha miradi iliyopangwa inatekelezwa na kuleta manufaa kwa Kanisa na waumini wake. Aidha, aliwahimiza waumini na wadau wengine kuendelea kushiriki katika kuchangia miradi hiyo ili kufanikisha lengo la Sh bilioni mbili na kuhakikisha maandalizi ya maadhimisho hayo yanakamilika kwa wakati. Maadhimisho ya Jubilei ya Almasi ya miaka 75 ya Jimbo Katoliki la Mbulu yanatarajiwa kufanyika Machi 2028, yakikumbuka historia ya kuanzishwa kwa jimbo hilo Machi 25, 1953. Fupisha habari kuwa ya gazetiBoresha kichwa kivutie zaidiAndika kwa mtindo wa habari fupi.

Sun, 08 Nov 2026 08:23:17 +0000
Health · Issa Michuzi

YAS KUUNGA MKONO KAMPENI YA AFYA BORA, MAISHA BORA KWA MIAKA 3 IJAYO

Kampuni ya mawasiliano ya Yas Tanzania imeahidi kuendelea kuunga mkono kampeni ya Afya Bora, Maisha Bora iliyo chini ya taaisisi ya Zanzibar Maisha Boara Foundation kwa miaka mitatu ijayo ili wananchi wengi zaidi Zanzibar waweze kunufaika na huduma za uchunguzi na matibabu bila malipo. Afisa Mtendaji Mkuu wa Yas Tanzania, Bw. Pierre Canton Bacara, ametangaza ahadi hiyo siku ya leo 07.11.2026, wakati wa kufunga kambi ya sita ya matibabu ya kampeni hiyo katika viwanja vya Kinduni Academy, Mkoa wa Kaskazini Unguja. Akifunga kambi hiyo, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, ambaye pia ni mlezi wa kampeni hiyo, alisema kwa siku tano wakazi wa eneo hilo wamepata fursa ya kuonana na madaktari, kufanyiwa uchunguzi na kupata matibabu bila malipo. Mhe. Abdulla alimpongeza Mwenyekiti wa ZMBF, Mama Mariam Mwinyi, kwa kufikisha huduma hizo katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar. Pia aliishukuru Yas kwa kudhamini kambi ya Kinduni na ahadi yao ya kuunga mkono kampeni hiyo kwa miaka mitatu ijayo. Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kushirikiana na kuziunga mkono taasisi ambazo zinazoleta huduma za kijamii karibu zaidi na wananchi. Kwa upande wake, Waziri wa Afya Zanzibar, Mhe. Nassor Ahmed Mazrui, alisema zaidi ya watu 4,200 walifika kambini katika siku nne za kwanza. Amewahimiza wale waliobainika kuwa na tatizo la kiafya wakati wa uchunguzi kufika mapema katika kituo cha afya au hospitali ili waendelee kupata huduma kabla hali zao hazijawa mbaya. Akiwasilisha taarifa ya kitaalamu ya kambi hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar, Dkt. Mngereza Mzee Miraji, alisema serikali inalenga kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2030, aina zote za huduma za uchunguzi wa magonjwa na matibabu ya kibingwa zinapatikana Zanzibar. Alisema hatua hiyo itapunguza gharama wanazobeba wagonjwa wanaolazimika kusafiri nje ya Zanzibar kufuata matibabu. Mapema mwezi Mei mwaka huu, Dkt. Miraji alitangaza kuwa serikali inapanga kutumia shilingi trilioni moja kwa ajili ya huduma za afya kuanzia mwaka 2026 hadi 2030. Sehemu ya fedha hizo itatumika kuboresha vituo vya kutolea huduma za afya na kuimarisha huduma za afya ya msingi Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa Yas Bw. Pierre Canton Bacara alimshukuru Mama Mariam Mwinyi kwa kuikaribisha Yas kuwa mshirika rasmi wa kambi hiyo na kuongeza kuwa “Kwa miaka mitatu ijayo, tutaendelea kushirikiana na Zanzibar Maisha Bora Foundation ili kambi hii ifanyike kila mwaka na kuwafikia Wazanzibari wengi zaidi,” alisema. Yas pia ilitoa kiti cha matibabu ya meno pamoja na vifaa vyake na vishikwambi (tablets) 30 kwa matumizi ya wahudumu wa afya baada ya kambi kumalizika. Bw. Bacara aliongeza kuwa kupitia kampeni ya Tumaini, wafanyakazi wa Yas wameweza kusaidia kuboresha huduma za afya ya uzazi katika hospitali ya Mwera Pongwe, Unguja, na Hospitali ya wilaya ya Kinyasini, Pemba. Alisema zaidi ya akina mama 3,000 wamenufaika na kampeni hiyo kwa Zanzibar pekee. Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa ZMBF, Bi. Rehema Tukai, alisema ushirikiano na Wizara ya Afya uliwawezesha wataalamu katika kambi ya Kinduni kutoa huduma za uchunguzi wa magonjwa ya moyo na saratani, kufanya upasuaji mdogo na kutoa huduma za afya ya uzazi, macho na ngozi. Alisema taasisi hiyo itaendelea kuandaa kambi katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar ili kuwafikia wananchi wengi zaidi. Hafla ya kufunga kambi hiyo pia iliambatana na uzinduzi wa Build Resilience, kampeni ya Umoja wa Wake wa Marais wa Afrika kwa Maendeleo (OAFLAD). Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na mlezi wa kampeni ya Afya Bora, Maisha Bora, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, akimkabidhi Afisa Mtendaji Mkuu wa Yas Tanzania, Bw. Pierre Canton Bacara, tuzo ya kutambua mchango wa Yas, wakati wa hafla ya kufunga kambi ya sita ya matibabu ya kampeni hiyo iliyofanyika Novemba 7 katika viwanja vya Kinduni Academy, Mkoa wa Kaskazini Unguja. Wanaoshuhudia ni Waziri wa Afya Zanzibar, Mhe. Nassor Ahmed Mazrui (wa pili kutoka kushoto), Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Dkt. Riziki Pembe Juma (kushoto), na Afisa Mtendaji Mkuu wa Zanzibar Maisha Bora Foundation, Bi. Rehema Tukai (kulia). Katika hafla hiyo iliyohitimisha kambi ya siku tano, Yas iliahidi kuendelea kuunga mkono kampeni hiyo kwa miaka mitatu ijayo.

Sun, 08 Nov 2026 08:26:25 +0000

Page 321 of 1148 · 22943 stories