Search the region
22945 stories
More than 40,000 gather as Pope Leo XIV celebrates Mass in Uruguay
Read the full report from the original source.
RecentlyMudavadi asks why Uhuru denied Sifuna Jubilee ticket if he backs his presidential ambitions
Read the full report from the original source.
RecentlyMudavadi urges Western Kenya to unite, says region cannot remain on sidelines
Prime Cabinet Secretary Musalia Mudavadi has urged Western Kenya to unite ahead of the 2027 General Election, saying the region must strengthen its political representation.
Sat, 07 Nov 2026 18:22:15 +0300Ousted FKF Executive Committee members dismiss process as "an illegal joke"
Read the full report from the original source.
RecentlyKWS seeks space as Ol Pejeta rhino sanctuary fills up
The conservancy is home to both black and white rhinos and has played a significant role in efforts to protect the endangered species.
RecentlyTANESCO yajenga njia mbadala ya umeme kupunguza changamoto ya umeme Mbagala, Mkuranga
Read the full report from the original source.
RecentlySababu noti za Sh1,000 na Sh2,000 kuchakaa mapema
Soma hapa...
RecentlyKamati ya Bunge yataka wanaopita daraja la Tanzanite kuanza kulipia
Read the full report from the original source.
RecentlyDes lions aux habitudes insolites dans la nature
Les spécialistes de la faune sauvage estiment que le fait de grimper aux arbres est l’une des méthodes qui aident ces lions à faire face à leur environnement.
RecentlyBREAKING: Afande Herbert Matanda Mabonga makes explosive allegations about the 2021 shooting of Gen. Katumba Wamala
Read the full report from the original source.
RecentlyPIC lauds TADB’s 8.4bn/- increase in dividends paid to the government
DAR ES SALAAM: THE Parliamentary Standing Committee on Public Investments (PIC) has commended the Tanzania Agricultural Development Bank (TADB) for…
RecentlySix Held as Police Probe Fatal Shooting of Deaf Link Uganda Director
Read the full report from the original source.
RecentlyTADB yaimarika, yadhamiria kuwafikia wakulima wadogo
Read the full report from the original source.
RecentlyPoland: At least 5 killed in shooting in Krakow, police say
Read the full report from the original source.
RecentlyNigeria's Aliko Dangote steps in to boost Cameroon's oil supply
Read the full report from the original source.
RecentlyPoland: At least 5 dead in shooting in Krakow
Read the full report from the original source.
RecentlyBALOZI OMAR ATAKA KASI ZAIDI UJENZI WA SGR KIPANDE CHA TATU
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), akizungumza jambo katika eneo la Tura, mkoani Tabora wakati wa ziara yake ya siku mbili ya kukagua Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), katika vipande vya Tatu, Nne na Tano, akiambatana na Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (hayupo pichani). Na. Joseph Mahumi na Asia Singano, WF, Tabora Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar, amewataka wakandarasi wanao jenga Reli ya Kisasa (SGR) kuongeza kasi ili kufidia muda uliopotea kutokana na changamoto mbalimbali zilizojitokeza, na kuzingatia ubora wa kazi na masuala ya mazingira na jamii. Akizungumza wakati wa ziara yake ya kukagua na kujionea maendeleo ya ujenzi wa Reli ya Kisasa(SGR), katika vipande vya tatu, nne na tano, Mhe. Balozi Omar alisema Serikali inataka kuona mradi huo unatekelezwa kwa kasi zaidi ili kufikia malengo yaliyokusudiwa ya kuunganisha maeneo mbalimbali ya nchi kwa njia ya reli ya kisasa. Alisema pamoja na changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa mradi huo na zilizoelezwa na mkandarasi, mshauri Melekezi pamoja na Shirika la Reli Tanzania (TRC), Serikali imeendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kutafuta suluhisho litakalowezesha kuharakisha maendeleo ya ujenzi. Mhe. Balozi Omar aliipongeza TRC, Wizara yake nawataalamu wengine walioshiriki kubuni utaratibu mbadala uliosaidia kuondoa baadhi ya vikwazo na kuimarisha kasi ya utekelezaji wa mradi huo. “Kwa mujibu wa taarifa, utekelezaji wa kipande hiki cha Tatu umefikia asilimia 16.1, na kipande cha Nne asilimia 10.08, ni maendeleo mazuri, ingawa juhudi zaidi zinahitajika ili kuongeza kasi na kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati” alisema Mhe. BaloziOmar Alibainisha kuwa ujenzi wa reli hiyo una umuhimu wa kimkakati katika kuunganisha maeneo ya mashariki na magharibi mwa Tanzania, kuanzia Dar es Salaam kupitia Dodoma hadi Mwanza na kuendelea kuelekea Kigoma. Aidha, Mhe. Balozi Omar alisema kukamilika kwa kipande cha kwanza cha Dar es Salaam hadi Dodoma na maendeleo ya ujenzi wa kipande cha tano kuelekea Mwanza ni hatua muhimu, lakini vipande vinavyounganisha maeneo hayo, ikiwemo kipande cha tatu, vina mchango mkubwa katika kuhakikisha mtandao wa reli hiyo unakamilika na kufikia malengo yaliyokusudiwa. “Tusipokamilisha vipande vinavyounganisha maeneo haya, hatutakuwa tumefikia kikamilifu malengo makubwa ya mradi huu ya kuiunganisha nchi kutoka mashariki hadi magharibi,” alisema Mhe. Balozi Omar. Aidha, aliwataka wakandarasi wote wanaotekeleza sehemu mbalimbali za mradi kuhakikisha wanakamilisha kazi walizokabidhiwa kwa wakati, akisisitiza kuwa mafanikio ya mradi hayatapimwa kwa upatikanaji wa fedha pekee, bali pia kwa kuzingatia muda wa utekelezaji na ubora wa kazi. Katika hatua nyingine, Mhe. Balozi Omar alisisitiza umuhimu wa kuzingatia masuala ya mazingira na kijamii katika utekelezaji wa mradi huo, akieleza kuwa ni miongoni mwa masharti muhimu yanayotiliwa mkazo na taasisi za kimataifa zinazofadhili miradi ya maendeleo kupitia mikopo. Alisema Serikali na washirika wake wa maendeleo wanapaswa kuhakikisha masuala hayo yanashughulikiwa mapema badala ya kusubiri hadi changamoto zijitokeze wakati wa utekelezaji au baada ya fedha za mradi kutolewa.Mhe. Balozi Omar alihimiza kuendelea kwa ushirikiano wa karibu kati ya Wizara ya Fedha, TRC, wakandarasi, washauri elekezi na wataalamu wengine ili kuhakikisha mradi wa SGR unakamilika kwa ufanisi na kutoa mchango uliokusudiwa katika kukuza uchumi, kurahisisha usafirishaji na kuimarisha maendeleo ya Taifa. Kwa upande wake Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Prof. Makame Mbarawa, amesema ziara ya pamoja na Waziri wa Fedha katika Mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) imelenga kuimarisha ushirikiano kati ya wizara hizo mbili katika kuhakikisha fedha zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo zinatumika ipasavyo. Alisema ni muhimu Wizara ya Fedha, ambayo inasimamia upatikanaji wa fedha, kujionea maendeleo ya miradi inayofadhiliwa, huku Wizara ya Uchukuzi ikiendelea kusimamia utekelezaji wake. Naye Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Mhandisi Machibya Shiwa, na Mhandisi Mshauri mradi, Bw. Salim Omary Salim, wameeleza hatua zinazochukuliwa na shirika hilo pamoja na wasimamizi wa mradi katika kuhakikisha changamoto zinazojitokeza zinapatiwa ufumbuzi, sambamba na kuhakikisha utekelezaji unaendeleakufanyika kwa kuzingatia masharti ya kimkataba, viwango vyaubora na matakwa ya kimazingira ili kuhakikisha ujenzi unakamilika kwa viwango vinavyotakiwa Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), (katikati), Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (wa pili kulia), wakikagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR, Kipande cha Nne – Tabora hadi Isaka (Km 165), ambacho hadi sasa kimefikia asilimia 10.08, wakati wa ziara yake ya siku mbili ya kukagua Mradi wa Ujenzi wa SGR, katika vipande vya Tatu, Nne na Tano, mkoani Tabora. Wengine katika picha ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya (kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Mhandisi Machibya Shiwa (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Miundimbinu Wizara ya Uchukuzi, Mhandisi. Shomari Omar Shomari Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), (wa kwanza kushoto), akisikiliza maelezo ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Mhandisi Machibya Shiwa, kuhusu maendeleo ya Mradi huo katika Kipande cha Tatu – Makutupora hadi Tabora (Km 368, wakati wa ziara yake ya siku mbili ya kukagua Mradi wa Ujenzi wa SGR, katika vipande vya Tatu, Nne na Tano, mkoani Tabora, akiambatana na Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Prof. Makame Mbarawa, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya na Viongozi na Maafisa waandamizi wa Wizara ya Fedha, Wizara ya Uchukuzi na Shirika la Reli Tanzania -TRC (hawapo pichani). Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), (wakwanza kushoto), akisikiliza maelezo ya Kiongozi wa Timu ya Ukandarasi wanaojenga Kipande cha Nne – Tabora hadi Isaka (Km 165), Bw. Sinan Doymus, kuhusu maendeleo ya Mradi huo ambao hadi sasa umefikia asilimia 10.08, wakati wa ziara yake ya siku mbili ya kukagua Mradi wa Ujenzi wa SGR, katika vipande vya Tatu, Nne na Tano, mkoani Tabora, akiambatana na Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Prof. Makame Mbarawa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya na Viongozi na Maafisa waandamizi wa Wizara ya Fedha, Wizara ya Uchukuzi na Shirika la Reli Tanzania -TRC (hawapo pichani). (Picha na Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini, WF -Tabora)
Sat, 07 Nov 2026 15:41:30 +0000No clear winner after tight New Zealand elections
Prime Minister Christopher Luxon's centre-right National Party won 42 seats but was 19 short of the simple majority.
RecentlyFrance braces for new round of Yellow Vest, student protests
Read the full report from the original source.
RecentlyWANUFAIKA 14 WA NGORONGORO SCHOLARSHIP KUTINGA VYUO VIKUU KIBABE
Waswahili husema Hayawi hayawi sasa yamekuwa na Mwanzo wa Ngoma ni Lele, na sasa Ngoma inachezwa kufuatia Ngorongoro Scholarship Fund iliyozinduliwa tarehe 4 Agosti, 2026 kuwezesha wanafunzi waishio hifadhi ya Ngorongoro kupata fursa ya elimu ambapo wanafunzi 14 wamepatikana na kuagwa leo Jijini Dar es Salaam kuelekea Vyuo vikuu mbalimbali. Kamishna wa Uhifadhi Ngorongoro Dkt. Abdul-Razaq Badru ameeleza kuwa kupitia Ngorongoro Scholarship Fund , NCAA kwa kushirikiana na Bodi ya Mikopo baada ya uchambuzi jumla ya wanafunzi 14 wamekidhi vigezo na kuchaguliwa kujiunga Vyuo vikuu ambavyo ni Chuo kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA), Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori-MWEKA, Chuo cha Uhasibu Arusha (AIA) na chuo Kikuu cha SAUT ambapo wamedahiliwa katika masomo ya u Uhifadhi wa Wanyamapori, misitu, Malikale na utalii. “ Kupitia Ngorongoro Scholarship Fund tumetenga Milioni 100 mwaka huu kufadhili wanafunzi, tunaamini wanafunzi hawa wakimaliza masomo yao itawawezesha kujiajiri ama kuajiriwa maeneo mbalimbali Serikalini na Sekta binafsi, Utekelezaji wa program hii ni utekelezaji wa majukumu matatu ya Ngorongoro katika uhifadhi, utalii na kuwaendeleza wakazi waishio ndani ya Hifadhi. Ufadhili huu unalenga kusaidia wenyeji wenye sifa za kupata elimu ya vyuo vikuu, mpango huu utatekelezwa kila mwaka kwa kushirikiana na Bodi ya Mikopo kwa kuzingatia muongozo wa utoaji wa mikopo” amesema Dkt. Badru. Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya juu Dkt. Bill Kiwia ameeleza kuwa kupitia Ngorongoro Scholarship Fund Bodi hiyo ilipokea maombi 26 na baada ya kuchakata jumla ya wanafunzi 14 walikidhi vigezo na kunufaika na ufadhili huo kwa kuzingatia misingi ya haki, usawa na uwazi kwa wote wanaostahili na kuongeza kuwa kwa wanafunzi 14 waliopatikana jumla ya shilingi Milioni 70.6 itatumika kufadhili gharama za masomo yao ili kutimiza ndoto zao za kupata ujuzi, fursa ya kusaidia taifa katika shughuli za uhifadhi, utalii, mazingira. Kwa upande wake Katibu wa Baraza la Wafugaji Ngorongoro Mhe. James Moringe ameipongeza Serikali kupitia Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro kwa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi 93 wa Sekondari, wanafunzi 33 wa kidato cha 5 na 6, wanafunzi 36 ngazi ya vyuo vya Kati na wanafunzi 14 waliopata ufadhili wa vyuo vikuu mwaka huu. Akitoa shukrani kwa niaba ya wanafunzi wenzake, Ndina Koyaki Mollel kutoka kata ya Alailelai ameishukuru Serikali kwa kuwawezesha kufikia ndoto ya kupata elimu iwe fursa kwao kujiajiri, kuajiriwa na kusaidia familia zao na kuiomba serikali kuongeza idadi ya wanafunzi wanaosajiliwa kwa miaka ijayo.
Sat, 07 Nov 2026 15:23:36 +0000Page 328 of 1148 · 22945 stories