Search the region
22966 stories
Guinée : pourquoi l’armée a fermé les mines d'or de Siguiri ?
Read the full report from the original source.
RecentlyGermany news: Trial of alleged 'Reichsbürger' group ringleaders begins
Read the full report from the original source.
RecentlyUlinzi Starlets target seventh straight win against Bungoma Queens
Read the full report from the original source.
RecentlyWATCH LIVE: LSK holds peaceful march over Abshir Ahmedsadak Abdi’s abduction and disappearance
Read the full report from the original source.
RecentlyTanzania invites Algerians to explore expanding oppo
DAR ES SALAAM: TANZANIA is seeking to translate its longstanding friendship with Algeria into stronger commercial partnerships, inviting Algerian companies…
RecentlyToddler dies during tonsil surgery in Bungoma
Leila Mutenyo died during an adenotonsillectomy, an operation to remove the tonsils and adenoids, at Bungoma Children's Hospital.
RecentlyBeyond Business as Usual: Zanzibar public firms seek Union growth
ZANZIBAR: A NEW drive to connect Zanzibar’s public institutions with mainland financial markets and investment opportunities is gaining momentum, as…
RecentlySPIKA WA BUNGE ZUNGU AWATUMA UJUMBEA KWA NCHI MAZIWA MAKUU
Na Said Mwishehe,Michuzi TV SPIKA wa Bunge, Mussa Azzan Zungu, ametuma ujumbe kwa nchi wanachama wa Mkutano wa Kimataifa wa Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR) akizitaka kutekeleza kwa vitendo makubaliano yaliyofikiwa katika mkutano wa Wabunge wanawake kuhusu amani, usalama na maendeleo. Akizungumza leo alipokuwa akifunga mkutano wa wanawake wabunge wa Jukwaa la Mabunge la ICGLR uliofanyika Dar es Salaam Spika Zungu amesema mafanikio ya mkutano huo yatapimwa kwa hatua zitakazochukuliwa na nchi wanachama kutekeleza maazimio yaliyopitishwa. “Tanzania inathamini ushiriki wa wajumbe wote na mchango wa wadau mbalimbali waliofanikisha mkutano huo, huku akimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa uongozi wake unaoendelea kuiweka Tanzania katika nafasi ya kuhimiza amani, mazungumzo, ushirikiano wa kikanda na maendeleo jumuishi.” Zungu pia amemshukuru Makamu wa Rais,Deogratius Ndejembi aliyemwakilisha Rais Samia katika ufunguzi wa mkutano huo, akisema Serikali imeonesha dhamira ya kuimarisha ushiriki wa wanawake katika michakato ya amani na usalama kupitia Mpango wa Kwanza wa Taifa wa Wanawake, Amani na Usalama wa mwaka 2025–2029. Kwa upande wake, Katibu mkuu(ICGLR) Balozi Dkt. Deo Mwapinga, amesema matokeo ya mkutano huo kufuatiwa na hatua za utekelezaji pamoja na kuanzishwa kwa mfumo wa uratibu na ufuatiliaji wa maendeleo ya maazimio yaliyokubaliwa. “Mfumo huo utasaidia kuimarisha ushirikiano kati ya nchi wanachama, kufuatilia utekelezaji na kuhakikisha Mpango wa Kikanda wa Wanawake, Amani na Usalama wa mwaka 2027–2031 unatekelezwa kwa ufanisi na uratibu unaofaa,” amesema Balozi Mwapinga Amesema mkutano huo umepitisha Azimio la Dar es Salaam linalozitaka nchi wanachama kuimarisha sheria na mifumo ya kitaasisi inayowezesha wanawake kupata uwakilishi sawa katika mabunge, serikali na nafasi za uongozi wa vyama vya siasa. Aidha, azimio hilo pia linahimiza kuongezwa kwa ushiriki wa wanawake katika majadiliano ya amani na timu za upatanishi, kuzuia ukatili dhidi ya wanawake katika siasa, pamoja na kuhakikisha wanaoshiriki katika michakato ya amani wanalindwa dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia. Mwapinga amesema wajumbe wamekubaliana pia kuimarisha usimamizi wa rasilimali za asili kwa kuzingatia usawa wa kijinsia, kupambana na unyonyaji haramu wa rasilimali unaochochea migogoro na kuhakikisha wanawake wanapata sehemu stahiki ya manufaa yatokanayo na rasilimali hizo. Aidha, alisema azimio hilo limeweka msisitizo katika kuwawezesha wanawake kiuchumi kupitia upatikanaji wa mikopo, ardhi, masoko, biashara za mipakani na elimu ya fedha na teknolojia, huku likitaka kulindwa kwa wanawake na wasichana wakimbizi na waliolazimika kuyahama makazi yao kutokana na migogoro na mabadiliko ya tabianchi. “Azimio hilo limeitaka Sekretarieti ya ICGLR kufuatilia utekelezaji wake na kuwasilisha taarifa katika kikao kijacho cha kawaida cha Bunge la Umoja huo, huku likihimiza viongozi wa kikanda kulifikisha kwa wakuu wa nchi na serikali, Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa,” alisema Wakati huo huo Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Saada Mkuya, alisema Serikali inaichukulia ajenda ya Wanawake, Amani na Usalama kuwa sehemu muhimu ya malengo mapana ya maendeleo ya Taifa, kwa kuwa uwezeshaji wa wanawake ni msingi wa kujenga familia imara na jamii zenye ustahimilivu. Dkt. Mkuya amesema dhamira hiyo inatekelezwa kupitia Mpango wa Kwanza wa Taifa wa Wanawake, Amani na Usalama wa mwaka 2025–2029 uliozinduliwa Agosti 2025, ambao unalenga kuunganisha taasisi za Serikali na wadau wengine katika kuhakikisha ajenda hiyo inatekelezwa katika ngazi zote. Amesema Tanzania itaendelea kushirikiana na nchi wanachama wa ICGLR kutekeleza Azimio la Dar es Salaam na Mpango wa Pili wa Kikanda wa Wanawake, Amani na Usalama wa mwaka 2026–2030, Aidha ametoa mwito kwa nchi hizo kudumisha mshikamano na kugeuza makubaliano yaliyofikiwa kuwa vitendo vitakavyoleta amani, usalama na maendeleo katika ukanda wa Maziwa Makuu. Pia amesema uwezeshaji wa wanawake na usawa wa kijinsia ni nguzo muhimu katika kujenga familia imara, jamii zenye ustahimilivu na taifa lenye ustawi. “Suala la usawa wa kijinsia halipaswi kuachiwa taasisi zinazoshughulikia masuala ya wanawake na jinsia pekee, bali linahitaji dhamira na ushiriki wa pamoja wa taasisi zote za serikali, jamii na wadau wa maendeleo. “Dhamira hiyo inaakisiwa katika Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 na ajenda ya kitaifa ya masuala ya jinsia, zinazolenga kuhakikisha wanawake, wanaume, wasichana na wavulana wanapata fursa sawa za kushiriki na kuchangia katika maendeleo ya taifa.” Alitaja Mpango wa Tatu wa Kitaifa wa Wanawake, Amani na Usalama wa mwaka 2025–2029, uliozinduliwa Agosti 2025, kuwa nyenzo muhimu ya kuratibu juhudi za taasisi na wadau mbalimbali katika kuendeleza ajenda hiyo, akisisitiza umuhimu wa kuhakikisha unatekelezwa kwa ufanisi katika ngazi zote. Akitoa salamu za shukrani katika mkutano huo Naibu Spika wa Bunge la Taifa la Zambia, Malungo Chisangano, amesema mkutano huo wa siku nne umewezesha wabunge, viongozi wa serikali, taasisi za kikanda, Umoja wa Mataifa, mashirika ya kiraia na vijana kujadili kwa pamoja nafasi ya wanawake katika kuimarisha amani na kuendeleza ustawi wa eneo la Maziwa Makuu. Ameongeza majadiliano yaliyofanyika yametoa fursa ya kuhamisha msisitizo kutoka kwenye ahadi za kisera na kuelekeza nguvu katika hatua za vitendo, ikiwemo utungaji wa sheria, utoaji wa fedha kupitia bajeti na usimamizi wa utekelezaji wa sera na mipango ya serikali. Chisangano amesema Azimio la Dar es Salaam na Mpango wa Kikanda wa Utekelezaji vinapaswa kutumika kama mwongozo kwa mabunge ya nchi wanachama katika kuhakikisha masuala ya Wanawake, Amani na Usalama yanaingizwa katika sheria, sera na mifumo ya usimamizi wa serikali. Amewataka maspika wa mabunge na wakuu wa ujumbe wa nchi wanachama kuhakikisha maazimio ya mkutano huo yanatekelezwa katika nchi zao, akisisitiza kuwa ushiriki wa wanawake katika ujenzi wa amani na maendeleo si jukumu la wanawake pekee, bali ni kipaumbele kinachopaswa kupewa uzito na mabunge pamoja na taasisi zote za kitaifa.
Fri, 06 Nov 2026 08:07:13 +0000Eastleigh tragedy: Rescue mission nears end
The Interior ministry said post-mortem examinations and formal identification of the recovered victims were ongoing at the Nairobi City Mortuary.
RecentlyUnlocking Vision 2050: Zanzibar’s private sector at the heart of delivery
ZANZIBAR: ALI Suleiman Amour advocates joint planning, stronger business links across the Union and a change in mindset to translate…
RecentlyWATCH LIVE: LSK Presser at Milimani Law Courts
Read the full report from the original source.
RecentlyTVS turns road signs into breast cancer awareness messages
Read the full report from the original source.
RecentlyDODOMA YAIPONGEZA TASAC KWA KUUNGANISHA WADAU KUPUNGUZA FOLENI ZA MAGARI YA MIZIGO
Na Mwandishi Wetu, Dodoma KAIMU Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Janeth Mayanja, ameipongeza Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) kwa juhudi za kuwaunganisha wadau wa sekta ya uchukuzi katika kutafuta suluhisho la changamoto ya foleni za magari ya mizigo, pamoja na kuimarisha ufanisi wa usafirishaji wa shehena nchini. Mayanja, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, ametoa pongezi hizo Novemba 5, 2026, alipokuwa akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma wakati wa kikao na Bodi ya Wakurugenzi ya TASAC iliyomtembelea ofisini kwake mkoani humo. Amesema Dodoma ina fursa kubwa ya kuwa kitovu muhimu cha shughuli za usafirishaji na biashara nchini, hususan kupitia uwekezaji katika miundombinu ya bandari kavu, hatua itakayosaidia kupunguza msongamano wa magari ya mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam na kurahisisha usafirishaji wa shehena kwenda maeneo mbalimbali nchini na nchi jirani. Amesema mkoa huo una maeneo yenye fursa nyingi za uwekezaji, hivyo amewahimiza wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuzitumia fursa hizo, akisisitiza kuwa Serikali ya Mkoa iko tayari kushirikiana nao kuwezesha uwekezaji wenye tija kwa maendeleo ya mkoa na taifa kwa ujumla. Aidha, ameiomba TASAC kuwa balozi wa Mkoa wa Dodoma kwa kutangaza fursa zilizopo na kuhamasisha wawekezaji kuelekeza mitaji yao katika sekta ya uchukuzi, hususan ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya bandari kavu. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TASAC, Nahodha Mussa Mandia, amesema ziara hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu ya bodi katika kufuatilia maendeleo ya miundombinu na shughuli za sekta ya uchukuzi, kutathmini hali halisi ya utoaji huduma na kuimarisha ushirikiano na Serikali za Mikoa pamoja na wadau mbalimbali. Amesema katika ziara hiyo, bodi imetembelea maeneo ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) yaliyopo Ihumwa na Bahi mkoani Dodoma, yanayohusika na kuhudumia na kusafirisha shehena za mizigo kutoka ndani na nje ya nchi. Ameeleza kuwa ziara hiyo inalenga kutathmini hali ya miundombinu na shughuli za usafirishaji katika maeneo hayo, kubaini fursa za uwekezaji na maeneo yanayohitaji maboresho, pamoja na kuimarisha ushirikiano wa kimkakati utakaosaidia kuongeza ufanisi wa huduma za usafirishaji na kupunguza changamoto zinazokwamisha mtiririko wa shehena nchini. Juhudi hizo ni sehemu ya mkakati wa kuimarisha mfumo wa usafirishaji wa mizigo nchini kwa kuunganisha wadau, kuboresha miundombinu na kutumia fursa za uwekezaji zilizopo katika maeneo mbalimbali.
Fri, 06 Nov 2026 07:50:42 +0000Exposed: Top Kampala Commander Lumumba Arrested For Defrauding Chinese investor Over USD1.25 Million In Tantalite Ore Deal
Read the full report from the original source.
RecentlyTayebwa Briefs Pacific Parliamentarians on OACPS Reforms
Read the full report from the original source.
RecentlyCharlene Ruto dazzles in grand bridal shower ahead of high-level wedding in Mwanza
Read the full report from the original source.
RecentlyKitisuru school issues statement after learner dies during Arusha trip
Read the full report from the original source.
RecentlyNTSA nets 24 drivers in Kakamega crackdown
"All PSV and commercial vehicle owners are required to ensure their speed limiters are functional at all times," the authority said.
RecentlyNCHI ZA EAC ZIJIFUNZE NA ATHARI ZA EL NIÑO YA 2023/2024
Na, Mwandishi Wetu – Nairobi, Kenya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zimetakiwa kuchukua tahadhari mapema ili kuepusha madhara yaliyotokea wakati wa mvua za El Niño za mwaka 2023/2024, zilizosababisha hasara iliyozidi dola za Marekani bilioni mbili na zaidi ya watu milioni 1.5 kuyahama makazi yao. Wito huo umetolewa wakati wa ufunguzi wa Mkutano Maalumu wa Kisekta wa Kikanda kuhusu Kujiandaa na Kukabiliana na Athari za Mvua za El Niño, uliofanyika jijini Nairobi, Kenya. Mkutano huo wa ngazi ya Makatibu Wakuu ulilenga kuweka mikakati ya pamoja ya kujiandaa na kukabiliana na athari za mvua hizo, kwa kuzingatia kuwa majanga ya aina hiyo hayaheshimu mipaka ya nchi na hivyo yanahitaji uratibu na ushirikiano wa kikanda. Tanzania iliwakilishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (EAC), Bw. Charles Kadonya. Katika kukabiliana na athari zinazotarajiwa, nchi wanachama zimetakiwa kulinda miundombinu muhimu ya usafirishaji na nishati inayounganisha nchi za ukanda huo, kuimarisha akiba ya chakula, kuwawezesha wakulima pamoja na kuwekeza katika miundombinu ya kuvuna na kuhifadhi maji. Vilevile, zimesisitizwa kuimarisha mifumo ya ufuatiliaji na udhibiti wa magonjwa ili kuzuia milipuko ya magonjwa yanayoweza kuongezeka kutokana na mafuriko, yakiwemo kipindupindu na malaria. Kwa upande wake, Tanzania iliwasilisha mpango kazi wake wa kukabiliana na athari za El Niño na kueleza utayari wa kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa mpango kazi wa kikanda ulioandaliwa kupitia mkutano huo. Mpango huo unalenga kuratibu hatua za dharura na kutambua maeneo ya kipaumbele ili kuhakikisha rasilimali zinazohitajika zinapatikana kwa wakati na kuwezesha nchi wanachama kulinda maisha na mali za wananchi.
Fri, 06 Nov 2026 07:37:24 +0000Court to sentence Paul Mackenzie, 28 others found guilty in Shakahola killings
The Mombasa High Court is set to deliver sentences against Pastor Paul Mackenzie, 28 co-accused persons in the case involving the deaths of 190 children and one adult in Shakahola.…
RecentlyPage 356 of 1149 · 22966 stories