Search the region
22984 stories
Suspect arrested after body of missing woman found dumped in River Nithi
Read the full report from the original source.
RecentlyWill US midterm election results spare Gulf states from further war?
Read the full report from the original source.
RecentlyIG Kanja leads security talks in Moyale after Kenyan killed in Ethiopia clashes
Read the full report from the original source.
RecentlyMPESA transfers push safaricom H1 profits to Sh58bn
Here are the stories making the headlines.
RecentlySan Siro Kuwaka Moto! Ac Milan Kukabiliana Na Ferencváros
MICHUANO ya UEFA Europa League inaendelea leo Alhamisi, Novemba 5, 2026, huku macho ya mashabiki wa soka yakielekezwa katika dimba la San Siro nchini Italia, ambako miamba ya soka AC Milan itakuwa mwenyeji wa Ferencváros ya Hungary katika mchezo wa nne wa hatua ya League Phase. Mchezo huo unaotarajiwa kuanza saa 20:45 usiku, unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa huku kila upande ukihitaji matokeo muhimu katika safari yake ya kusaka mafanikio ya Ulaya. AC Milan inaingia katika mchezo huo ikiwa na dhamira ya kutumia faida ya kucheza nyumbani kurejesha makali yake kwenye michuano hiyo. Baada ya kuanza kampeni kwa matokeo yasiyoridhisha dhidi ya Benfica na Bournemouth, kikosi hicho kilionyesha uwezo wake mkubwa kwa kuichapa Salzburg mabao 4-0. Hivyo, kurejea San Siro ni nafasi nyingine kwa Rossoneri kuonyesha kuwa bado ni moja ya timu zinazopaswa kuheshimiwa katika mashindano haya. Kwa upande wa Ferencváros, safari yao ya Europa League imekuwa na matokeo yanayotoa matumaini makubwa. Timu hiyo imeonyesha makali ya ushambuliaji kwa kupata ushindi dhidi ya Celtic, Viktoria Plzeň na Torreense katika michezo yake ya awali. Sasa wanakutana na mtihani mkubwa dhidi ya AC Milan, huku wakilenga kuendeleza kasi yao na kuthibitisha kuwa wana uwezo wa kushindana na vigogo wa soka la Ulaya. Kwa habari na taarifa mbalimbali za michezo usisite kutembelea meridianbet ili upate mambo yote yanayotokea na kuendelea kwenye ulimwengu wakimichezo, ikiwemo michuano mikubwa ya Africa, Ulaya na ile ya falme za kiaarabu zote zinapatikana hapa. Huu pia utakuwa mchezo wa kwanza kabisa wa kihistoria kukutanisha AC Milan na Ferencváros katika mashindano ya Ulaya. Hilo linaongeza mvuto wa pambano hilo, kwani hakuna historia ya matokeo ya ana kwa ana kati ya timu hizi mbili itakayoweza kumpa yeyote faida ya kisaikolojia. Kila upande utalazimika kutumia ubora wa wachezaji wake, nidhamu ya kiufundi na umakini katika kutumia nafasi zitakazojitokeza. Kwa AC Milan, kucheza mbele ya mashabiki wake katika uwanja wa San Siro ni nafasi ya kuonyesha ubora, kasi na uzoefu wake wa michuano mikubwa ya kimataifa. Hata hivyo, Ferencváros hawapaswi kudharauliwa kutokana na matokeo yao mazuri katika michezo iliyopita.
Thu, 05 Nov 2026 07:11:00 +0000Safari Ya Jewels Of Ra Kutafuta Hazina Za Misri Ya Kale Yawasili Meridianbet
KATIKA ulimwengu wa michezo ya kasino mtandaoni , safari ya kutafuta ushindi huwa na msisimko wake wa kipekee, hasa pale unapokutana na hazina zilizofichwa katika historia ya ustaarabu wa kale. Safari hiyo sasa inachukua sura mpya kupitia Jewels of Ra, mchezo mpya wa sloti kutoka Pragmatic Play unaopatikana Meridianbet. Mchezo huu unawapeleka wachezaji katika jangwa la Misri ya kale, ambako piramidi, mahekalu na vito vya thamani vinaweka mazingira ya safari yenye msisimko na matarajio makubwa. Kwa mashabiki wa michezo ya kasino wanaopenda changamoto na burudani yenye mabadiliko ya ghafla, Jewels of Ra una mengi ya kuvutia. Meridianbet inaendelea kupanua mkusanyiko wake wa michezo inayochota msukumo kutoka historia ya Misri ya kale. Jewels of Ra unaungana na michezo mingine maarufu yenye mandhari hiyo, ikiwemo Fury of Anubis na Throne of Ra. Hii inaonyesha namna Meridianbet inavyoendelea kuwapa wateja wake machaguo mbalimbali ya michezo yenye ubunifu na mazingira tofauti ya burudani. Katika mchezo huu mpya, kila mzunguko unaweza kuwa mwanzo wa safari nyingine ya kuvumbua vito na hazina zilizofichwa katikati ya jangwa. Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi. Kwa upande wa muonekano, Jewels of Ra umejengwa kwa michoro yenye ubora na rangi zinazovutia, huku gridi ya mchezo ikiwa na safu tano na mistari minne ya alama. Mchezo unachezwa katika mazingira ya kupatwa kwa jua, jambo linaloongeza upekee wa mandhari yake ya Misri ya kale. Ili kupata mchanganyiko wa ushindi, mchezaji anahitaji kupata alama tatu au zaidi zinazofanana kwenye reels zinazofuatana, kuanzia upande wa kushoto. Pia, kipengele cha Wild Multipliers kinaongeza msisimko katika mchezo wa kawaida kwa kuongeza uwezekano wa kupata malipo makubwa kulingana na matokeo ya mizunguko. Msisimko mwingine unapatikana kupitia Bonus Game, Total Multipliers na Jackpots zinazoongeza mvuto wa mchezo. Kwa wachezaji wanaotaka kubadilisha namna wanavyocheza, kuna vipengele vya Feature Buy na Special Bets vinavyoweza kuchaguliwa kwa gharama husika. Sasa hakuna haja ya kusubiri safari nyingine ya kuvumbua hazina za Misri ya kale, kwani Jewels of Ra inapatikana Meridianbet na unaweza kuufurahia kupitia simu yako, kompyuta au kifaa kingine cha kisasa. Meridianbet inaendelea kuwaletea mashabiki wa kasino michezo mipya yenye ubunifu, michoro ya kuvutia na vipengele vinavyoongeza burudani. Jisajili na Meridianbet, chunguza Jewels of Ra na ujionee mwenyewe safari hii ya kuvutia katika ulimwengu wa vito vya thamani.
Thu, 05 Nov 2026 07:13:00 +0000MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR AAHIDI KUSHIRIKIANA NA VIONGOZI WA CCM PWANI, ASEMA LENGO NI KUHUDUMIA WANANCHI
Na Victor Masangu, Pwani Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla, amesema lengo kuu la Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni kuwahudumia wananchi na kushirikiana na viongozi katika kuwaletea maendeleo. Amesema hayo wakati wa hafla ya kujitambulisha rasmi kwa viongozi wa CCM na Serikali mkoani Pwani, kufuatia kuteuliwa kwake kuwa mlezi mpya wa chama hicho mkoani humo. Amesema atashirikiana na viongozi na wanachama wa CCM katika Wilaya zote za Mkoa wa Pwani kuhakikisha chama kinaendelea kujengwa na kuimarishwa, huku akisisitiza kuwa hatowaangusha katika utekelezaji wa majukumu yake. Aidha, Hemed amewaahidi wanachama na wananchi kuwa ataendeleza mazuri yaliyofanywa na mlezi aliyemtangulia, akieleza kuwa dhamira yake ni kuona CCM inaendelea kukua na kuimarika mkoani humo. Ameeleza kuwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo kupitia Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2025–2030 umeendelea kujenga imani ya wananchi kwa chama hicho. Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Stanslaus Nyongo, ameahidi kumpa ushirikiano mlezi huyo katika kipindi chote atakachohudumu mkoani humo. Nyongo amesema mkoa huo unaendelea kupiga hatua za maendeleo na kuwataka wananchi kudumisha umoja na mshikamano, sambamba na kuunga mkono utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali. Naye Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha, Dkt. Nicas Mawazo, amempongeza Makamu huyo wa Pili wa Rais kwa uteuzi wake na kuahidi kumpa ushirikiano katika kusimamia utekelezaji wa Ilani ya CCM na kuwahudumia wananchi.
Thu, 05 Nov 2026 18:59:09 +0000Eastleigh tragedy: Six bodies recovered from rubble
Nairobi North County Commissioner Simon Asumba said the six bodies recovered on Thursday comprised four women and two men.
RecentlyMANISPAA KIBAHA WAIPA KONGOLE SAMIA LEGAL AID KUPUNGUZA GHARAMA ZA HUDUMA ZA KISHERIA
Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha WANANCHI Tangini, Mailmoja na Pangani, Manispaa ya Kibaha, Mkoa wa Pwani, wamesema Kampeni ya Samia Legal Aid imekuwa mkombozi kwao kwa kuwasogezea huduma za kisheria karibu na maeneo yao, ambazo awali walishindwa kuzimudu kutokana na gharama za usafiri na huduma hizo. Wakizungumza wakati wa kampeni hiyo inayofanyika katika kata hizo akiwemo Ally Mshamu, Fatuma Ismail, Mama Ikram na Seif Salim, walisema upatikanaji wa huduma za RITA, msaada wa mawakili na wanasheria umewapa nafasi ya kupata ushauri na kutafuta ufumbuzi wa changamoto zilizokuwa zikikwamisha maisha yao. Salim alifafanua kuwa wengi wao walikuwa wakikabiliwa na changamoto za kisheria lakini wakishindwa kufuata taratibu za kupata haki kutokana na gharama za kufika kwenye taasisi husika, hali iliyosababisha baadhi ya migogoro kuendelea kwa muda mrefu. Fatuma aliipongeza Serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuanzisha kampeni hiyo, akisema imewapa fursa ya kupata msaada wa kisheria bila kikwazo cha gharama, huku akiwahimiza wananchi wengine kujitokeza kutumia huduma hizo kabla wataalamu hawajarejea maofisini na kuwalazimu kuanza tena kuhangaika kutafuta nauli. Timu ya wataalamu kupitia Awamu ya Pili ya Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (Samia Legal Aid), Manispaa ya Kibaha, inayoongozwa na Wakili Revocatus Thadeo Mathew, inaendelea kutoa huduma hizo kwa wananchi kwa kutembelea kata mbalimbali. Revocatus alisema hadi Novemba 5, mwaka huu, kampeni hiyo ilikuwa imefikia siku ya nane kati ya 10, huku akishukuru wananchi kwa kujitokeza kupata huduma na ushauri, hususan kuhusu masuala ya ndoa, ardhi, mirathi na migogoro ya kifamilia. Alisema wataalamu wamekuwa wakiwapatia wananchi elimu na ushauri wa kisheria ili kuwasaidia kuelewa taratibu za kutafuta haki na kupata ufumbuzi wa migogoro yao kwa mujibu wa sheria. "Wananchi waendelee kujitokeza kutumia fursa hii kutoa taarifa za changamoto zinazowakabili na kufuata ushauri unaotolewa na wataalamu wa sheria ili kupata ufumbuzi wa migogoro yao kwa mujibu wa taratibu na sheria zilizopo," alisema. Mratibu wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (Samia Legal Aid), Wakili Innocent Magesa, alisema maelfu ya wananchi wamejitokeza katika kata, halmashauri na wilaya mbalimbali kutoa madukuduku yao na kupata msaada wa kisheria. Magesa alifafanua kuwa kampeni ya Samia Legal Aid awamu ya pili katika Mkoa wa Pwani inatekelezwa katika halmashauri tisa, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali za kuimarisha upatikanaji wa haki na kuhakikisha wananchi wenye uwezo mdogo wa kiuchumi wanapata huduma za kisheria. Alisema kampeni hiyo ilianza Oktoba 29, mwaka huu, na inatarajiwa kuhitimishwa Novemba 7, 2026, ikiwa na lengo la kuwafikia wananchi wengi zaidi na kuwapatia elimu, ushauri na msaada wa kisheria katika maeneo yao.
Thu, 05 Nov 2026 18:56:10 +0000High court dismisses Odonga-Otto’s election petition
The High court has dismissed a petition by former Aruu County MP Samuel Odonga-Otto challenging the election of Christopher Komakech. In a judgment delivered on…
RecentlyOpposition dismisses claims of 2027 election rigging plans, urges Kenyans to protect vote
Read the full report from the original source.
RecentlyKenya's junior Baseball5 and Judo teams jet back from Dakar Youth Olympics
Read the full report from the original source.
RecentlyParaguay President Santiago Peña resigns
His resignation comes after Paraguay's lower house of congress voted in favour of pursuing an impeachment trial.
RecentlyManispaa Kibaha waipa kongole Damia Legal Aid kupunguza gharama za huduma za kisheria
Read the full report from the original source.
RecentlyCourt freezes Embu MCA's land, six vehicles in Ksh.111.5M case
Read the full report from the original source.
RecentlyNchi za EAC zijifunze athari za El Nino ya 2023/2024
Read the full report from the original source.
RecentlyCheapest Bayern-Ajax tickets sell out in two hours
Tickets priced at Sh2,500, Sh3,500 and Sh5,000 were already marked as sold out by 9 pm.
RecentlyKindiki: Commonwealth must deliver jobs, trade and debt relief
Read the full report from the original source.
RecentlyLa circulation d'armes de guerre aggrave les conflits agropastoraux
Read the full report from the original source.
RecentlyWATU WATATU WAFARIKI, WAWILI AKIWEMO MTOTO WA MIAKA 6 HAWAJAPATIKANA KUFUATIA KUZAMA MTO RUFIJI
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani WATU watatu wamefariki dunia na wengine wawili hawajapatikana baada ya boti iliyokuwa imebeba watu 23 kuzama katika Mto Rufiji, mkoani Pwani, huku watu 18 wakiokolewa. Miongoni mwa waliofariki ni mwanamke mwenye umri wa miaka 60, mwanafunzi wa Kidato cha Pili katika Shule ya Sekondari Mwaseni na mtoto wa miaka saba. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Protas Mutayoba, amesema ajali hiyo ilitokea Novemba 4, 2026, saa 12 jioni katika eneo la Kijiji cha Mloka, Kata ya Mwaseni. Anasema boti hiyo mali ya Kijiji cha Mloka ilikuwa ikiendeshwa na Nassoro Abdallah Mkandu (32), mkazi wa Mloka, ikiwa na watu 23 waliokuwa wakitoka mashambani kuelekea kijijini kupitia Mto Rufiji. Mutayoba amewataja waliofariki kuwa ni Sikitiko Naimbu, Shushani Ibrahim Kitimai na Masha Ali Buriani, wote wakazi wa Mloka. Amesema kati ya watu 18 waliookolewa, watatu ni wanaume na 15 wanawake, ambao wanaendelea na matibabu katika Zahanati ya Mloka. Waliopotea ni Faimu Ibrahim Kitimai (6) na Nusra Makuka (28). Akieleza chanzo cha ajali hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Rufiji,Luteni Kanal Fredrick Komba, ameeleza boti hiyo iligonga gogo lililokuwa ndani ya maji na kusababisha kupinduka na kuzama. "Jeshi la Polisi Rufiji kwa kushirikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na wananchi linaendelea na juhudi za kuwatafuta watu wawili ambao hawajapatikana". Komba amesema miili ya waliofariki tayari imezikwa na kwamba taarifa zaidi kuhusu tukio hilo zitatolewa. Vyombo vya usafiri majini vimetakiwa kuzingatia kanuni za usalama, ikiwemo kutobeba abiria kupita uwezo wa chombo na kuhakikisha wanatumia vifaa vya kujiokolea, hususan maboya.
Thu, 05 Nov 2026 18:10:49 +0000Page 364 of 1150 · 22984 stories