Unganishwa

Search the region

23024 stories

Business · Issa Michuzi

WMA: VIPIMO SAHIHI NI MSINGI WA MAFANIKIO YA SERA ZA VIWANDA NA UJASIRIAMALI

Na. WMA - DODOMA, Wakala wa Vipimo (WMA) imesema matumizi ya vipimo sahihi ni msingi muhimu wa kuimarisha uzalishaji viwandani, kulinda haki za wafanyabiashara na walaji, na kuongeza ushindani wa bidhaa za Tanzania katika masoko ya ndani na nje. Kauli hiyo imetolewa wakati wa uzinduzi wa Sera ya Maendeleo Endelevu ya Viwanda ya Mwaka 2025 na Sera ya Maendeleo ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati ya Mwaka 2003 (Toleo la 2025), uliofanywa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete (JKCC), jijini Dodoma. Akizungumza katika tukio hilo, Afisa Mtendaji Mkuu wa WMA, Bw. Alban Kihulla, amesema vipimo sahihi vinajenga uaminifu katika biashara kwa kuhakikisha wanunuzi wanapata kiasi cha bidhaa kinacholingana na thamani ya fedha wanazolipa. Amesema WMA inatekeleza jukumu hilo kwa kukagua bidhaa zilizofungashwa zinazozalishwa nchini pamoja na zinazoagizwa kutoka nje ya nchi kupitia bandari na vituo vya mipakani, ili kuhakikisha kuwa uzito au ujazo ulioainishwa kwenye vifungashio unalingana na kiasi halisi cha bidhaa kilichomo. “Mnunuzi wa ndani au wa nje ya nchi anapochukua bidhaa yenye nembo ya Made in Tanzania, anatakiwa kupata kile hasa kilichoandikwa kwenye kifungashio. Hiyo ndiyo kazi yetu, na ndiyo sababu tunaziona sera hizi kama fursa ya kuimarisha imani kwa bidhaa za Kitanzania,” amesema Bw. Kihulla. Ameeleza kuwa WMA pia hushirikiana na taasisi na mashirika ya vipimo ya kikanda na kimataifa katika kuimarisha ulinganifu wa vipimo na kusaidia kupunguza vikwazo vya biashara vinavyohusiana na vipimo. Akizungumzia biashara ya mazao, amesema WMA inaendelea kuhakiki mizani inayotumika katika vituo vya ununuzi na viwanda vya usindikaji ili kuhakikisha wakulima wanapimiwa kwa usahihi na kulipwa kulingana na uzito halisi wa mazao yao. “Mkulima anapouza korosho, kahawa au pamba, mizani inayotumika lazima iwe sahihi ili alipwe kwa uzito halisi wa mazao yake. Tunaendelea kuhakiki mizani katika vituo vya ununuzi na viwanda vya usindikaji, na kupambana na ufungashaji wa lumbesa unaomnyima mkulima haki yake,” amesema. Kwa upande wa wajasiriamali wadogo na wa kati, amesema matumizi ya vipimo sahihi huwasaidia kufungasha bidhaa kwa kiasi kilichoainishwa, kudhibiti upotevu na kujenga uaminifu kwa wateja. Amesema WMA inaendelea kutoa elimu kupitia njia mbalimbali, zikiwemo redio na televisheni, ili kuwawezesha wajasiriamali na wafanyabiashara kuelewa na kuzingatia matakwa ya vipimo katika shughuli zao. Wakala pia hutumia klabu za vipimo mashuleni kujenga uelewa wa matumizi ya vipimo sahihi tangu umri mdogo. Aidha, amesema ukuaji wa viwanda na uwekezaji unaongeza mahitaji ya huduma za vipimo, ikiwemo uhakiki wa mizani, mita za umeme na mita za gesi asilia, pamoja na idhini za miundo ya vipimo vinavyokusudiwa kutumika katika shughuli zinazodhibitiwa kisheria. Ameongeza kuwa WMA inaendelea kuboresha mifumo ya kidijitali ili kurahisisha upatikanaji wa huduma, sambamba na kuimarisha ukaguzi wa bidhaa zinazozalishwa nchini na zinazoagizwa kutoka nje, pamoja na uhakiki wa vipimo vinavyotumika viwandani na katika biashara. “Tunawaomba wananchi wahakikishe mizani na vipimo wanavyotumia vina alama ya uhakiki ya WMA, na watoe taarifa pale wanapoona kipimo kisicho sahihi. Kipimo sahihi ni haki ya kila mwananchi,” amesisitiza. WMA ni miongoni mwa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara zilizoshiriki maonesho na kongamano lililoambatana na uzinduzi huo. Wananchi na wafanyabiashara waliotembelea banda la Wakala walipata elimu kuhusu matumizi ya vipimo sahihi na huduma zinazotolewa na WMA. Sera hizo zinalenga kuimarisha maendeleo ya viwanda na ujasiriamali kwa kuongeza uzalishaji, thamani ya malighafi za ndani, fursa za ajira na upatikanaji wa mitaji na masoko kwa wajasiriamali, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Thu, 05 Nov 2026 07:15:52 +0000
Uncategorized · Daily News

Who dares wins: LPG, the next frontier for Africa’s downstream

AT the IEA’s first Summit on Clean Cooking in Africa in Paris in May 2024, Akinwumi Adesina, then African Development…

Recently
Uncategorized · DW Rwanda

What the Democrats' midterms win means for the US economy and Trump

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · KBC

Vaginal tightening: Pharmacists warn against cetirizine misuse amid high demand

PSK also noted reports of increased demand, price rises and stock shortages in some outlets

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

Recruitment agency director charged with swindling Ksh.20M from UK job seekers

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

Antonelli back to work as Mercedes chase title double

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

Trans Nzoia county leads in TFGBV cases as most perpetrated on Facebook

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

Man arrested for impersonating cops on Jogoo Rd

When confronted, he introduced himself as a sergeant attached to the General Service Unit (GSU) Training School

Recently
Uncategorized · Rwanda News Agency

CHOGM 2026 opens with drive to unlock prosperity for Commonwealth’s 2.7 billion people

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

Types of press freedom violations recorded

The report, covering July to September 2026, lists 34 cases of assault, followed by five threats

Recently
National · Issa Michuzi

JESHI LA POLISI ULANGA LAENDELEA KUIMARISHA UHUSIANO, WANANCHI KITUTI WAITIKA KUPITIA KAMPENI YA 'ONGEA NA KAMANDA'

Jeshi la Polisi Wilaya ya Ulanga limeendelea kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati yake na wananchi kupitia programu ya “Ongea na Kamanda” iliyofanyika katika Kijiji cha Kituti, Kata ya Ruaha, wilayani Ulanga, Mkoa wa Morogoro kwa lengo la kujenga jamii yenye uelewa wa mambo ya amani na usalama pamoja na kuzuia vitendo vya uhalifu. Akitoa Elimu hiyo, Mkuu wa Polisi Wilaya ya Ulanga, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Deogratius Challe, alieleza maana na malengo ya kampeni hiyo, akisisitiza umuhimu wa wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kudumisha usalama na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu kwa wakati ili hatua sitahiki ziwezekuchukuliwa kwa wakati. Katika programu hiyo, wananchi walipatiwa elimu mbalimbali kuhusu utii wa sheria bila shuruti, usalama migodini, utunzaji wa fedha, ukatili wa kijinsia, utunzaji wa eneo la tukio la uhalifu, utoaji wa taarifa za uhalifu. Aidha Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Polisi Wilaya akatumia fursa hiyo kuwakumbusha wananchi wanaomiliki silaha kinyume na utaratibu kusalimisha silaha hizo katika vituo vya Polisi na ofisi za serikali za vijiji huku akiwakumbusha na tahadhari dhidi ya mvua za El Niño. Licha ya ananchi walilipongeza Jeshi la Polisi kwa juhudi zake za kuimarisha usalama na kudumisha amani katika jamii wananchi hao, wameliomba Jeshi hilo kuendelea kutoa elimu ili kuwajengea uelewa Juu ya mambo ya kiusalama. Kwa ujumla, programu ya “Ongea na Kamanda” imeendelea kuwa jukwaa muhimu la mawasiliano kati ya Jeshi la Polisi na wananchi, likichochea ushirikiano katika kuzuia uhalifu, kutatua changamoto za kiusalama na kujenga jamii yenye amani, utulivu na usalama.

Thu, 05 Nov 2026 07:00:49 +0000
Uncategorized · Daily News

Samia charts path towards peace, national unity

TANZANIA: AS Tanzania marks one year since President Dr Samia Suluhu Hassan was sworn in for her current term on…

Recently
Uncategorized · Issa Michuzi

TIRA YATAKA USHIRIKIANO WA TAASISI KUHARAKISHA ULIPAJI WA FIDIA ZA BIMA.

Pamela Mollel,Arusha Arusha .Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) imehimiza kuimarishwa kwa ushirikiano wa taasisi mbalimbali ili kuondoa vikwazo vinavyochelewesha ulipaji wa fidia za bima na kuhakikisha wananchi wanapata haki zao kwa wakati. Akizungumza wakati wa kikao kazi cha wadau wa sekta ya bima Kanda ya Kaskazini jijini Arusha, Meneja wa TIRA Kanda ya Kaskazini, Dkt. Emmanuel Lupilya, amesema ulipaji wa fidia ndiyo kipimo muhimu cha imani ya wananchi kwa sekta ya bima. Amesisitiza kuwa bima haipaswi kuishia katika kukusanya malipo ya awali, bali lazima itimize wajibu wake wa kumlinda mwananchi pale anapokumbwa na janga. Dkt. Lupilya amependekeza kuanzishwa kwa 'Mfumo wa Kitaifa wa Uratibu wa Madai ya Bima (National Insurance Claims Coordination Framework)' utakaounganisha kampuni za bima na taasisi muhimu, ikiwemo Jeshi la Polisi, hospitali, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na wadau wengine, ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa na kuharakisha maamuzi ya madai. Ameeleza kuwa mfumo huo utasaidia pia kuboresha takwimu za madai yaliyolipwa, yaliyocheleweshwa na yale yenye viashiria vya udanganyifu, huku akisisitiza umuhimu wa kila taasisi kutekeleza wajibu wake na kutoa taarifa kwa wakati. Dkt. Lupilya amesisitiza kuwa mafanikio ya sekta ya bima hayapimwi kwa idadi ya watu wanaokata bima pekee, bali pia kwa kasi, uwazi na haki katika kulipa fidia pale wanapohitaji huduma hiyo. Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa TIRA, Ponziano Rusiano Lukosi, amebainisha changamoto zinazochangia migogoro ya madai, zikiwemo magari kuwekewa bima bila ukaguzi wa kutosha, makadirio yasiyo halisi ya gharama za matengenezo na ucheleweshaji wa taarifa za uchunguzi wa ajali. Naye Mchunguzi Mwandamizi wa TAKUKURU Arusha, Julieth Mwambola, amewataka wananchi kuripoti vitendo vya rushwa vinavyohusiana na ufuatiliaji wa madai ya bima kupitia namba ya bure 113, huku akizihimiza kampuni za bima kutoa taarifa za viashiria vya udanganyifu. Kikao kazi hicho kimewakutanisha kampuni za bima, Jeshi la Polisi, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, LATRA, NHIF, wawakilishi wa gereji, mawakala wa bima na taasisi nyingine zinazoshiriki katika mnyororo wa kushughulikia madai ya fidia. Meneja wa TIRA Kanda ya Kaskazini, Dkt. Emmanuel Lupilya,akizungumza kwenye kikao kazi hicho kilichofanyika jijini Arusha.

Thu, 05 Nov 2026 06:54:04 +0000
Uncategorized · The Ankole Times

Kabaka Isn’t Ordered! Why Kabaka Missed Museveni’s Cultural Leaders Meeting

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

Kang’ata: Sifuna is Opposition's greatest engine

Kang’ata says Sifuna’s growing appeal could boost opposition numbers, backs Gachagua as key figure in uniting rival factions

Recently
Uncategorized · Daily News

Perfume oils bring touch of elegance

DAR ES SALAAM: PERFUME oils offer a beautiful way to enjoy fragrance without the strong burst of traditional spray perfumes.…

Recently
Uncategorized · DW Afrique

Les violences contre les migrants en Méditerranée explosent en 2026

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Isango Star

INGINGO Z'INGENZI Z'IMPAMVU YO GUSABA GUHINDUZA AMAZINA

Thu, 05 Nov 2026 08:43:59 +0200
Uncategorized · PML Daily

URSB takes business registration services to mobile phones with new app

KAMPALA — Entrepreneurs, company owners and other users of Uganda Registration Services Bureau (URSB) services will be able to access information and a range of registration services through their mobile phones...

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

Odera rallies Kenya Lionesses to give their all in quest for African 7s crown

Read the full report from the original source.

Recently

Page 384 of 1152 · 23024 stories