Unganishwa

Search the region

23065 stories

Sports · Capital FM

A new dawn? Kenya launch ambitious strategy to revolutionise women’s football

Latest · Sports

Recently
Uncategorized · Issa Michuzi

DKT. MWIGULU AKUTANA NA WAZIRI MKUU WA DRC

WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amekutana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemkorasi ya Kongo (DRC), Judith Suminwa Tuluka na wamejadiliana njia mbalimbali za kuimarisha uchumi baina ya nchi hizo mbili. Katika mazungumzo yao yaliyofanyika ofisini kwake Mlimwa, jijini Dodoma leo (Jumatano, Novemba 04, 2026), Dkt, Mwigulu amesema Tanzania na DRC zina fursa ya kukuza ushirikiano wa kiuchumi katika nyanja mbalimbali ikiwemo madini, usafirishaji na uchukuzi, chakula na utoaji wa huduma za afya. “Bado kuna fursa kubwa ya kukuza ushirikiano wa kiuchumi kati ya mataifa yetu mawili. Kama ujuavyo, Tanzania na DRC ni mataifa yaliyobarikiwa kuwa na utajiri mkubwa, ikiwemo madini, ardhi yenye rutuba, misitu, maziwa na mito.” Akielezea uwepo wa fursa za kibiashara, Waziri Mkuu Mwigulu amesema nchi hizo bado zinaweza kuongeza kiwango cha sasa  cha biashara ikiwa watahamasisha sekta binafsi kutumia fursa zinazotolewa na mifumo ya kikanda na ya bara. “Tanzania na DRC tuna nafasi chanya nyingi za kufanya biashara zaidi. Tutawatuma mawaziri wa sekta zinazohusika ili waendelee kukutana na kukamilisha hayo masuala,” amesema. Dkt. Mwigulu amesema DRC ni mtumiaji namba moja wa Bandari ya Dar es Salaam, ikiwa na mchango wa asilimia 48 ya shehena yote ya mizigo ya nchi zisizo na bandari na akatumia  fursa hiyo kumpongeza Waziri Mkuu wa DRC kwa kutenga muda na kutembelea bandari hiyo. “Nimefurahi kwenye ziara hii umepata fursa ya kutembelea Bandari ya Dar es Salaam na Bandari Kavu ya Kwala, ambako tumetoa eneo kubwa kwa DRC. Kipekee nitumie fursa hii kuipongeza Serikali ya DRC kwa uamuzi wake wa kujenga barabara kutoka Lubumbashi kuja Kalemie. Hatua hii itafungua fursa za kibiashara kwa upande wa Tanzania,” amesema. Kwa upande wake, Waziri Mkuu wa DRC, Judith Suminwa Tuluka aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa misaada yote iliyoipatia nchi hiyo ikiwemo ya kijeshi, kutunza wakimbizi na vyakula na vifaa tiba wakati nchi hiyo ilipopata maafa. “Tunaishukuru na Serikali ya Tanzania na hasa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye kupitia vikao mbalimbali vya kikanda na kimataifa alipambana na kuisaidia Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo iweze kubaki na amani,” alisema na kuongeza: “Hatuwezi kuisahau Tanzania kwa kuwapokea na kuwapa hifadhi wakimbizi zaidi ya 90,000 wakati nchi yetu ilipokuwa inapambana na Rwanda. Tunaishukuru sana Tanznaia kwa mshikamano huo.” Akielezea mafanikio ya nchi hiyo, alisema wamefanya mageuzi ya kiuchumi kupitia programu mbalimbali za ndani na nje. “Tumefanya mageuzi katika mfumo wetu wa kifedha na tukafanikiwa kujenga imani yetu kwenye medani za kimataifa. Faranga imepanda thamni ikilinganishwa na dola ya Marekani. Wakati naingia ofisini Juni 2024, dola moja ya Marekani ilikuwa sawa na Faranga 3,000 lakini hivi sasa dola moja ni sawa na Faranga 2,250.” Alisema kutokana na hali hiyo, nchi yao imefanikiwa mikopo ya Dola za Marekani milioni moja na imeanza kujiondoa kwenye orodha ya nchi zenye madeni chechefu. “DRC kwa sasa ina imani chanya katika ngazi ya kimataifa,” alisisitiza.

Wed, 04 Nov 2026 16:40:15 +0000
Uncategorized · Issa Michuzi

TAKUKURU YAOKOA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 106 KATIKA STESHENI YA SGR MOROGORO

NA FARIDA MANGUBE, MOROGORO Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Morogoro imefanikiwa kuokoa zaidi ya shilingi milioni 106.08 zilizokuwa zikitumika kwa ajili ya ununuzi na usafirishaji wa maji kwa magari maalumu (bowser) katika Stesheni ya Reli ya Kisasa ya Jakaya Kikwete kwa mwaka mmoja. Akizungumza na waandishi wa habari, Afisa Mwandamizi wa TAKUKURU Mkoa wa Morogoro Casius Kiaro, amesema hatua hiyo imefikiwa baada ya taasisi hiyo kubaini changamoto ya upatikanaji wa maji katika kituo hicho kupitia ufuatiliaji wa huduma za kijamii. Amesema ufuatiliaji huo ulihusisha Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA) pamoja na uongozi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), kwa lengo la kutafuta suluhisho la kudumu la changamoto hiyo. Ameeleza kuwa kabla ya hatua hiyo, Stesheni ya SGR ya Jakaya Kikwete haikuwa na huduma ya uhakika ya maji, hali iliyolazimu kituo hicho kununua na kusafirisha maji kwa kutumia magari maalumu kwa ajili ya matumizi ya kawaida pamoja na huduma za mabehewa ya treni. Kwa mujibu wa Kiaro, gharama za ununuzi na usafirishaji wa maji zilifikia zaidi ya shilingi milioni mbili kwa wiki, sawa na shilingi milioni 8.84 kwa mwezi na jumla ya shilingi milioni 106.08 kwa mwaka. “Kupitia ushirikiano huo, huduma ya maji safi na salama imeanza kupatikana kwa uhakika katika kituo hicho kuanzia mwezi Agosti 2026, hatua iliyopunguza utegemezi wa ununuzi wa maji kwa kutumia magari,” amesema Kiaro. Kwa upande wake, Kaimu Meneja wa Stesheni ya Jakaya Kikwete, Salvatory Kimaro, amekiri kuwa changamoto ya upatikanaji wa maji ilikuwa ya muda mrefu, lakini imekwisha baada ya TAKUKURU kufuatilia suala hilo na kuwakutanisha na MORUWASA ili kupata suluhisho. Kimaro amesema kwa sasa kituo hicho kinapata maji saa 24, ingawa bado kuna uhitaji wa kuboresha miundombinu ya kuhifadhi maji ili kuwa na akiba ya kutosha kwa matumizi ya kituo hicho. “Kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TRC, napenda kuishukuru sana TAKUKURU kwa hatua hii. Tulikuwa tunapata shida kubwa ya maji na kutumia gharama nyingi kununua na kusafirisha maji kwa ajili ya matumizi ya kituo,” amesema Kimaro. Naye Meneja wa Kanda Namba Moja wa MORUWASA, Mhandisi Gidion Chahe, amesema pamoja na kutatua changamoto hiyo, mamlaka hiyo inaendelea na mikakati ya kuboresha miundombinu ya maji ili kuhakikisha kituo hicho kinapata huduma ya uhakika kulingana na ongezeko la matumizi ya maji linalotokana na kuongezeka kwa idadi ya abiria. Amesema maboresho hayo ni muhimu ili kuhakikisha huduma ya maji inaendelea kupatikana kwa uhakika hata kadri shughuli za usafiri wa reli zinavyoendelea kukua. Hata hivyo, TAKUKURU imeeleza  itaendelea kufanya ufuatiliaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ili  kuhakikisha fedha zinazotolewa na Serikali pamoja na wadau wa maendeleo zinatumika ipasavyo na miradi inayotekelezwa inazingatia thamani halisi ya fedha.

Wed, 04 Nov 2026 16:35:07 +0000
Uncategorized · Agence Burundaise de Presse

Les enfants errants, une menace pour les commerçantes de Ndagala à Kabezi

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Capital FM

Kiambu officer found dead near duty station with two gunshot wounds

NATIONAL NEWS · 5 hours ago

Recently
Uncategorized · Capital FM

Over 200 Kilimani boda boda riders trained on road safety and emergency response

NATIONAL NEWS · 5 hours ago

Recently
Uncategorized · Capital FM

KMPDU issues 21-day strike ultimatum to 17 counties over doctors’ salaries

Latest · Capital Health

Recently
Uncategorized · CEO East Africa

Kyaggwe Clinches First Masaza Cup Crown as Centenary Bank Strengthens Sports Development Partnership

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · CEO East Africa

Why Gertrude Karugaba’s Private-Sector Experience Could Matter at Bank of Uganda

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Citizen

Tanzanian student develops water-powered cooking machine

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

President Ruto calls on Kenyans to prioritise local products over imports

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

Real Madrid set to appoint tennis great Nadal to board

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

‘I did not abandon Mosop’: Kirwa speaks amid court fight

A voter wants Mosop seat declared vacant, arguing that the MP's prolonged absence denied residents effective representation in parliament.

Recently
Uncategorized · Radio Publique Africaine

Muramvya : privés d’eau potable depuis cinq jours, les habitants redoutent une épidémie

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Capital FM

Junior Lionesses set for red carpet reception in Nairobi after making history at Dakar Olympics

Latest · Rugby

Recently
Uncategorized · Issa Michuzi

KIMARA ASISITIZA UPATIKANAJI WA CHAKULA KWA WANAFUNZI SHULEN

Na Mwamvua Mwinyi, Kibiti Novemba 4, 2026 MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti, Ramadhan Ali Kimara, amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha wanafunzi wote wanapata chakula wakiwa shuleni ili kuboresha lishe na kuongeza ufaulu. Kimara amewataka Wakuu wa Idara za Elimu ya Msingi na Sekondari kuhakikisha shule zinaimarisha uzalishaji wa chakula kupitia mashamba ya shule, hatua itakayosaidia kukidhi mahitaji ya wanafunzi na kuhakikisha hakuna anayekosa chakula. Akizungumza katika kikao cha robo ya kwanza cha Kamati ya Lishe ya Halmashauri kilichoshirikisha menejimenti, Oktoba 4, 2026, amesema upatikanaji wa chakula shuleni ni jambo muhimu katika kuboresha afya, lishe na uwezo wa wanafunzi kujifunza. "Tuhakikishe wanafunzi wetu wote wanapata chakula shuleni na si baadhi yao. " Tutumie vizuri mashamba yetu kwa kuwa yatasaidia kuongeza upatikanaji wa chakula na kuongeza ufaulu wa wanafunzi wetu," amesema Kimara. Vilevile amezitaka shule kuimarisha upandaji wa miti ya matunda, ikiwemo mipapai, ili kuongeza upatikanaji wa matunda na kuhakikisha wanafunzi wanapata mlo bora na wenye virutubisho vinavyohitajika kwa ukuaji na maendeleo yao. Amesisitiza kuwa ushirikiano kati ya shule, wazazi na wadau wengine ni muhimu katika kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula cha kutosha na chenye ubora wa lishe, hivyo kuchangia maendeleo ya elimu katika Halmashauri hiyo.

Wed, 04 Nov 2026 16:07:15 +0000
Uncategorized · Issa Michuzi

SAMIA LEGAL AID- WOSIA SI KUJICHULIA KIFO, NI KINGA YA MIGOGORO YA FAMILIA

Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha. WANANCHI wametakiwa kuandika wosia mapema wakielezwa kuwa kufanya hivyo si kujichulia kifo, bali ni hatua muhimu ya kuweka wazi matakwa ya mmiliki wa mali na kujikinga na migogoro ya kifamilia inayoweza kujitokeza baada ya kifo chake. Aidha, wananchi wameshauriwa kuhakikisha wosia una mashahidi wanaotakiwa kisheria na nyaraka hizo zinahifadhiwa mahali salama ili ziweze kupatikana na kutumika kwa wakati unaofaa, hatua itakayosaidia kupunguza chuki, migawanyiko na migogoro miongoni mwa warithi. Wito huo umetolewa Novemba 4, 2026 na wataalamu wa masuala ya kisheria wa Awamu ya Pili ya Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (Samia Legal Aid), Manispaa ya Kibaha, wakati wakitoa elimu ya masuala mbalimbali ya kisheria kwa wananchi wa Kata za Tumbi na Sofu. Timu hiyo inayoongozwa na Wakili Revocatus Thadeo Mathew, imetoa elimu kuhusu umuhimu wa kuandika wosia, taratibu za mirathi na namna ya kulinda haki za warithi, huku ikisisitiza kuwa wosia unapaswa kuandaliwa kwa kuzingatia matakwa ya mmiliki wa mali na taratibu za kisheria. Akizungumza na wakazi wa Kata ya Tumbi, Revocatus amesema kuandika wosia mapema kunasaidia kuondoa utata kuhusu mgawanyo wa mali na kupunguza migogoro inayoweza kujitokeza baina ya wanafamilia baada ya mmiliki wa mali kufariki. Katika kampeni hiyo, wananchi wa Kata za Tumbi na Sofu pia wamepatiwa elimu kuhusu masuala ya ardhi, ndoa na mirathi, huku wakipewa fursa ya kueleza changamoto zinazowakabili na kupata ufafanuzi pamoja na ushauri wa kisheria kutoka kwa wataalamu hao. Sambamba na hilo, elimu imetolewa kuhusu nafasi na majukumu ya Mabaraza ya Usuluhishi ya Kata katika kusaidia kutatua migogoro inayojitokeza katika jamii, kwa kusisitiza umuhimu wa kutumia njia sahihi za kisheria katika kutafuta ufumbuzi. Kadhalika, timu hiyo imetembelea shule za msingi na sekondari katika kata hizo na kutoa elimu kwa wanafunzi kuhusu ukatili wa kijinsia, namna ya kujitambua na kujilinda dhidi ya vitendo vya ukatili, pamoja na umuhimu wa kutoa taarifa wanapokumbana na vitendo hivyo. Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia inaendelea katika kata mbalimbali za Manispaa ya Kibaha ikiwa na lengo la kusogeza huduma za kisheria karibu na wananchi, kuongeza uelewa kuhusu haki na wajibu wao na kuwawezesha kupata ufumbuzi wa changamoto zinazowakabili kwa mujibu wa sheria.

Wed, 04 Nov 2026 16:05:12 +0000
Uncategorized · The Star Kenya

KMPDU issues 21-day strike notice to 17 counties

He warned that doctors in the affected counties would proceed with the strike if the salary adjustments were not implemented before November 25.

Recently
National · Issa Michuzi

WANANCHI MAKOLE MUHEZA WAMIMINIKA KUSHIRIKI UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI

Wananchi wa Makole Muheza wakiwa kwenye msururu kwa ajili ya kushiriki uchaguzi mdogo wa udiwani

Wed, 04 Nov 2026 15:58:18 +0000
Health · Issa Michuzi

WANANCHI ZAIDI YA 2,000 WAPATA HUDUMA ZA MACHO BURE KIGAMBONI

Na Mwandishi Wetu, Kigamboni ZAIDI ya wananchi 2,000 wenye matatizo mbalimbali ya macho wamepatiwa matibabu bure na kugawiwa miwani kupitia kambi maalumu ya matibabu iliyofanyika katika Kituo cha Afya Kigamboni, jijini Dar es Salaam. Akizungumza wakati wa kufunga kambi hiyo, Diwani wa Kata ya Kigamboni, Dotto Msawa, amesema huduma hizo zimekuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa kipato cha chini ambao wasingeweza kumudu gharama za matibabu ya macho, ambazo zinaweza kufikia kati ya Sh. 400,000 na 500,000 kwa mtu mmoja. Amesema huduma hizo zimepatikana kupitia msaada wa Serikali ya Kuwait kwa kushirikiana na taasisi ya Majay Foundation, kwa lengo la kuwasaidia wananchi wa Kigamboni na maeneo jirani kupata huduma za afya bila malipo. Dotto amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi za kuimarisha ushirikiano na mataifa mbalimbali, akisema hatua hiyo imechangia upatikanaji wa misaada inayowanufaisha wananchi wenye uhitaji. Amesema kambi hiyo haikuhudumia wakazi wa Kata ya Kigamboni pekee, bali pia wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo, yakiwemo Pembanazi, Kisarawetu na Vijibweni, baada ya taarifa za huduma hizo kusambazwa katika maeneo mbalimbali. Ameongeza kuwa juhudi hizo ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), pamoja na kuunga mkono shughuli za maendeleo zinazotekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na viongozi wa maeneo husika. Kwa upande wake, Daktari Mfawidhi wa Kituo cha Afya Kigamboni, Peter Nyang’anyi, amesema kambi hiyo imefanikiwa kuwafikia wananchi zaidi ya 2,000 waliopata huduma mbalimbali, zikiwemo vipimo vya macho, miwani, ushauri wa kitaalamu, matibabu na upasuaji kwa wagonjwa waliohitaji huduma hiyo. Amesema baadhi ya matatizo ya macho yanaweza kutokana na changamoto za kuzaliwa nazo, ambazo wakati mwingine huhusishwa na mambo mbalimbali yanayotokea wakati wa ujauzito. Aidha, amewataka wananchi kuzingatia elimu ya afya, kutumia lishe bora, kufanya uchunguzi wa afya mara kwa mara na kuwahi hospitalini wanapobaini changamoto za kuona. Naye Daktari wa Macho na Mratibu wa Huduma za Macho katika Manispaa ya Kigamboni, Josephine Ngonyani, amesema sekta ya huduma za macho inakabiliwa na changamoto mbalimbali, zikiwemo gharama kubwa za matibabu, wingi wa magonjwa ya macho na uelewa mdogo wa wananchi kuhusu matatizo hayo na maeneo sahihi ya kupata matibabu. Amesema kambi hiyo pia imetoa elimu kuhusu ugonjwa wa presha ya macho (Glaucoma), ambao umekuwa ukizungukwa na dhana potofu katika jamii, huku baadhi ya watu wakiuhusisha na imani za kishirikina badala ya kuutambua kama tatizo la kiafya linalohitaji uchunguzi na matibabu ya kitaalamu. Mmoja wa wananchi walionufaika na huduma hizo, Catherine Mwenda, amesema awali alikuwa akisumbuliwa na maumivu ya jicho la kushoto, lakini hali yake imeendelea kuimarika baada ya kupata matibabu kutoka kwa madaktari. "Nilipata taarifa kuwa kuna huduma za upimaji na matibabu ya macho bure hapa, nami nikafuatilia na hatimaye nikapata huduma nzuri sana. Kwanza wanatujali sisi wazee na tumekuwa tukihudumiwa vizuri," amesema Catherine.

Wed, 04 Nov 2026 16:00:59 +0000

Page 399 of 1154 · 23065 stories