Search the region
23186 stories
TAIFA GROUP YAGEUZA ZAWADI ZA MASHINDANO YA MBUZI KUWA FURSA YA ELIMU KWA WATOTO WENYE MAZINGIRA MAGUMU
KAMPUNI ya Taifa Group imekabidhi zawadi zote ilizoshinda katika Mashindano ya Mbuzi (Goat Races) yaliyofanyika Septemba 2026 kwa Klabu ya Rotary ya Dar es Salaam Oysterbay, kwa ajili ya kusaidia watoto na vijana wenye mazingira magumu nchini kupata fursa ya kuendelea na masomo ya elimu ya juu. Uamuzi huo unalenga kugeuza ushindi uliopatikana kupitia burudani kuwa fursa ya kujenga maisha ya baadaye kwa watoto na vijana wa Kitanzania. Hafla ya makabidhiano ya zawadi hizo imefanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa kila wiki wa Klabu hiyo uliofanyika katika Kahawa Café, Masaki. Zawadi hizo zilikabidhiwa na Deborah Kaluzi, Mtaalamu wa Masuala Endelevu kutoka Vodacom Tanzania, ambayo ilikuwa mdhamini mkuu wa Mashindano ya Mbuzi ya mwaka 2025. Kwa niaba ya Taifa Group, zawadi hizo zilipokelewa na Kemilembe Mugangala, Mkuu wa Chapa na Mawasiliano. Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi wa Klabu hiyo, akiwemo Paul Muhato, Rais wa Klabu ya Rotary ya Dar es Salaam Oysterbay; Benoit Ducarme, Makamu wa Rais; Rashida Nabulime, Rais Mteule; pamoja na Bhavesh Bhatt, mwanachama wa klabu hiyo. Akizungumza baada ya kupokea zawadi hizo, Mugangala aliishukuru Vodacom Tanzania pamoja na Klabu ya Rotary kwa kuandaa jukwaa linalounganisha jamii, burudani na dhamira ya kusaidia wengine. "Kwa niaba ya Taifa Group, tunajivunia sana kuwa sehemu ya jambo hili. Mashindano ya Mbuzi si utamaduni unaopendwa na wengi pekee, bali pia yanatukumbusha umuhimu na nguvu ya kurudisha kwa jamii," alisema. Alisema kwa kuzingatia kaulimbiu ya Rotary isemayo Huduma Kabla ya Maslahi Binafsi (Service Above Self), Taifa Group imeamua kurejesha zawadi zote kwa jamii, akisisitiza kuwa hakuna mtoto anayepaswa kunyimwa fursa ya kupata elimu ya juu kutokana na mazingira aliyozaliwa au hali ya familia yake. "Huko Taifa, hatufanyi biashara nchini Tanzania pekee, bali tunashiriki pia katika kujenga Tanzania. Ikiwa ushindi wetu unaweza kumsaidia mtoto mmoja kufikia ndoto yake ya kujiunga na chuo kikuu, basi huo ndio ushindi wa kweli," alisema. Aidha, aliishukuru Vodacom Tanzania kwa kuwezesha jambo hilo na Rotary Oysterbay kwa kazi wanayoendelea kuifanya kwa manufaa ya jamii. Kwa upande wake, Paul Muhato, Rais wa Rotary Oysterbay, aliipongeza Taifa Group kwa uamuzi huo wa kurejesha zawadi kwa jamii, akibainisha kuwa fedha zitakazopatikana zitaelekezwa moja kwa moja katika mpango wa klabu wa kusaidia elimu nchini. Mashindano ya kila mwaka ya Mbuzi, yanayodhaminiwa na Vodacom Tanzania, hukutanisha kampuni mbalimbali, familia na wadau wengine kwa lengo la kuchangisha fedha zitakazosaidia kufanikisha shughuli mbalimbali za kijamii na misaada ya kibinadamu katika maeneo tofauti nchini.
Tue, 03 Nov 2026 13:07:19 +0000Kenyan websites suffer blow as hackers exploit AI
Read the full report from the original source.
RecentlyAirtel Africa Half-Year Profit Rises 20.5% to $452m on Strong Data and Mobile Money Growth
KAMPALA – Airtel Africa has reported a 20.5% increase in profit after tax to US$452 million for the six months ended September 30, 2026, driven by strong growth in data…
RecentlyGachagua: I'm opposition's most committed leader
The Democracy for the Citizens (DCP) leader says his return from a two-month US tour has revived opposition politics and mobilisation.
RecentlyAfande Muhoozi, Help Us Resolve Gen Elwelu’s Issues to Enable PLU Members to Conduct Free Mobilisation in Teso
Read the full report from the original source.
RecentlyGachagua takes swipe at ‘lazy’ opposition leaders after bullying claims
Latest · News
RecentlyWapiga kura 213,024 watarajia kushiriki Uchaguzi Mdogo Chamwino na Kata 11
Read the full report from the original source.
RecentlyRICHARD TODWONG: One of The Most Consequential SGs NRM Has Had
Read the full report from the original source.
RecentlyGovernment targets 1,198 households in Sh93.99m electricity expansion
Read the full report from the original source.
RecentlyYoung women drive Uganda’s 34,400 new HIV infections as 2030 target faces test
KAMPALA - Uganda is at risk of missing its 2030 target of ending AIDS as a public health threat unless it urgently reverses the rising vulnerability of adolescent girls and young...
RecentlyHousehold electricity use rises 12 percentage points, KNBS survey shows
Business · 4 hours ago
RecentlyTanzania calls for effective use of financial literacy skills in improving the citizens, nation’s well-being
NJOMBE: THE Ministry of Finance has urged members of the public to make effective use of the financial literacy skills…
RecentlyPLU’s Mwesigye Frank Slams NUP Leaders Over Shs234,500 Kapere Fundraiser, Pledges Shs1 Million To Widow
Read the full report from the original source.
RecentlyRC MTANDA AKABIDHI CHETI TACOEJ, AAHIDI KUSHIRIKIANA KUINUA ZAO LA PAMBA SIMIYU
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Said Mtanda, amekabidhi rasmi Cheti cha Usajili kwa Chama cha Waandishi wa Habari za Pamba na Mazingira (TACOEJ), huku akiahidi kushirikiana na chama hicho kuhamasisha wakulima kuongeza uzalishaji wa pamba. Mtanda amekabidhi cheti hicho leo Novemba 3, 2026 ofisini kwake, mara baada ya kutembelewa na viongozi wa chama hicho. Akizungumza baada ya kukabidhi cheti hicho, Mtanda amesema pamba ni uti wa mgongo wa uchumi wa Mkoa wa Simiyu, na kwamba kama Mkuu wa Mkoa anapaswa kujifunza kwa haraka changamoto zinazolikabili zao hilo. "Pamba ni uti wa mgongo wa uchumi wa Mkoa wa Simiyu. Zao hili lina changamoto nyingi sana na mimi kama Mkuu wa Mkoa ninatakiwa kujifunza haraka ili nijue changamoto za zao la pamba," amesema Mtanda. Ameongeza kuwa Serikali imeagiza kufanyika kwa vikao vya wadau kabla ya msimu, na kwamba badala ya kongamano peke yake, ni vyema wadau wakashirikiana kuandaa kikao cha wadau wa pamba ili waandishi wawe sehemu ya wadau na kutumia kalamu zao kufikisha elimu kwa umma kuhusu maazimio yatakayofikiwa. Amesema lengo ni kuhamasisha wakulima kuongeza uzalishaji kutoka tani 133,000 hadi kufikia tani 200,000, kwa kushirikiana na waandishi wa habari za pamba na mazingira ili jamii ifahamu umuhimu wa pamba katika uchumi wa Simiyu. Pia amesema atahakikisha wanakutana mara kwa mara na wadau wengine wa sekta ndogo ya pamba na mazingira ili changamoto za zao hilo zipatiwe ufumbuzi kwa wakati. Awali, Katibu wa TACOEJ, Sitta Tumma, amesema chama hicho kitatumia taaluma yake ya uandishi wa habari kuhakikisha elimu sahihi ya kilimo cha pamba inawafikia wakulima ili waongeze tija katika uzalishaji.
Tue, 03 Nov 2026 12:42:06 +0000Government discharges five Ebola patients as 46 contacts exit quarantine
Five patients being treated for the Ebola Bundibugyo virus disease outbreak have been discharged, while 46 additional contacts have completed monitoring and been released from quarantine. In a statement, the…
RecentlyKenya moves to strengthen legal protection for older persons
PS Motari said the proposed Older Persons Bill had been completed and was currently at the Cabinet level, paving the way for its consideration
RecentlyDr Mollel hails Samia’s development drive in major strategic projects
DODOMA: SIHA MP (CCM) Dr Godwin Mollel, has commended President Samia Suluhu Hassan for her efforts to advance national development…
RecentlyUCSAF YAELEZEA JINSI INAVYOTOA HUDUMA ZA BURE ZA INTANET KATIKA MAENEO YA WAZI
-Pia yaweka mkakati kuimarisha mtandao wa simu katika SGR Dar -Dodoma Na Said Mwishehe,Michuzi TV SERIKKALI kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote(UCSAF) inatekeleza mradi wa kutoa huduma za bure za intaneti kwenye maeneo ya wazi ili wananchi kuweza kutumia huduma ya intaneti bure katika maeneo hayo muhimu ambayo yanawatumiaji wengi. Hayo yamesemwa leo Novemba 3,2026 jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi wa UCSAF Albart Richard alipokuwa akizungumza katika kikao kazi kilichohusisha Wahariri wa vyombo vya habari na waandishi chini ya uratibu wa ofisi yq Msajili wa Hazina. Amesema kupitia mradi huo, vituo vya Intaneti 17 vimeanzishwa katika Viwanja vya Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba, Dar es Salaam. Vilevile, vituo vya intaneti vimeanzishwa katika maeneo ya viwanja vya Nyerere Square (Dodoma), College of Informatics CIVE (Dodoma), Soko la Nyamagana (Mwanza), Kiembesamaki (Zanzibar), Soko la Tabora (Tabora), Lungemba Training college in Mafinga. “Huduma ya kutoa huduma bure za Intaneti bure katika maeneo ya wazi.Changamoto iliyopo tunapokamilisha mradi huo tunapowakabidhi wahusika wanashindwa kumudu zile gharama za kutoa huduma hiyo bure. “Tunapotekeleza mradi huwa kwa muda fulani kwa mfano mwaka mmoja au miaka miwili UCSAF huwa tunalipia gharama ,sasa tunapokabidhi kwa halmashauri husika wanashindwa kumudu gharama maana tunaposema tunatoa huduma za intanet bure maana yake mfuko wetu unalipia. “Hivyo tunafikiria njia nzuri itakayowezesha kutatua changamoto hiyo,kwa mfano Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM) wao wanayo huduma hiyo ingawa mtumiaji anapotumia huduma hiyo baada ya robo saa au nusu saa anatakiwa kulipia.” Wakati huo huo amesema UCSAF imepanga kutekeleza mradi wa kuimarisha mawasiliano ya simu katika maeneo ya kimkakati yakiwemo ya Reli ya Kisasa ya SGR kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma. “Katika Mradi wa Awamu ya 11 Serikall kupitia UCSAF, imepanga kutekeleza mradi wa kukamilisha mawasilano ya simu ketika maeneo ya kımkakali ya SGR,MGR, reli ya TAZARA,maeneo ya mipakani na Hifadhi za Taifa.” Akizungumzia miradi ya TEHAMA katika sekta ya elimu, amesema shule za umma 1,167 zimenufaika na mradi wa kupeleka vifaa vya TEHAMA na kujenga maabara, huku Serikali ikiwa imewekeza Sh17.7 bilioni hadi Oktoba 2026 katika utekelezaji wake. Ameongeza UCSAF imepeleka vifaa maalumu vya TEHAMA katika shule 22 zinazohudumia wanafunzi wenye mahitaji maalumu. Vifaa hivyo ni pamoja na mashine za nukta nundu,kompyuta maalumu, vifaa vya kurekodi sauti na vifaa vya kukuza maandishi, kwa lengo la kuwawezesha wanafunzi hao kupata elimu kwa usawa. Kuhusu kuwajengea uwezo watumiaji wa teknolojia, Mhandisi Richard amesema walimu 5,094 wa shule za msingi na sekondari za umma Tanzania Bara na Zanzibar wamenufaika na mafunzo ya TEHAMA tangu mwaka wa fedha 2016/2017.“Pia wanafunzi wa kike 1,581 wamejengewa uwezo kupitia maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wasichana katika TEHAMA.”
Tue, 03 Nov 2026 12:39:43 +0000IFC to borrow Sh13bn for new Kenya investments
Read the full report from the original source.
RecentlyTanzanian activist Mwaipaya not in police custody; IG Kanja tells court
Read the full report from the original source.
RecentlyPage 439 of 1160 · 23186 stories