Unganishwa

Search the region

23194 stories

National · Issa Michuzi

JAJI MKUU MASAJU AWAPA UJUMBE MZITO WAHITIMU WA KIDATO CHA NNE LAKE SEKONDARI

Awaasa kuwa Waadilifu, kuheshimu watu, kutumia teknolojia kwa busara... Awashauri kutokimbilia mafanikio ya haraka Afurahishwa na kupongeza maboresho ya miundombinu ya Shule hiyo kama mmoja wa Wanafunzi waliosoma hapo Na MARY GWERA, Mahakama-Mwanza Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju amewataka Wahitimu wa Kidato cha Nne wa Shule ya Sekondari Lake kutumia vema maarifa waliyopata kutoka katika shule hiyo kama mwanzo wa safari na si kikomo cha ndoto. Mhe. Masaju alieleza hayo tarehe 02 Novemba, 2026 jijini Mwanza alipokuwa akitoa hotuba yake akiwa Mgeni Rasmi katika Mahafali ya Kidato cha Nne ya Shule ya Sekondari Lake iliyopo jijini Mwanza shule ambayo naye alisoma katika safari yake ya kitaaluma. “Leo nimesimama kama mmoja wa watu ambao safari yao ilipita katika shule hii. Sitaki mnaponisikia mseme tu kwamba mwanafunzi wa zamani wa Lake amefika katika nafasi hii. Nataka mjifunze jambo pana zaidi: safari ya maisha hujengwa kwa hatua, kwa watu wanaotusaidia, kwa maamuzi tunayofanya na kwa juhudi tunazoweka kila siku. Msifikiri kwamba lazima muanze mkiwa na kila kitu. Anzeni kwa kutumia vizuri kile mlicho nacho, muda wenu, nafasi ya kujifunza, ushauri mnaopewa na vipaji mlivyonavyo,” alisema Jaji Mkuu. Mhe. Masaju amewataka Wahitimu hao kuendelea kujifunza, kuwa waadilifu, kutobadili misingi yao kwa faida ya muda mfupi, kuheshimu watu, kutumia teknolojia kwa busara, kuipenda Tanzania kwa vitendo kwa kufanya kazi kwa bidii, kuheshimu sheria, kulinda mali za umma na kutatua matatizo ya jamii. “Msisubiri mazingira yawe kamili ndipo mfanye bidii. Jengeni uwezo wenu katika mazingira mliyopo, huku mkiboresha mazingira hayo kwa manufaa ya wengine,” amesisitiza Jaji Mkuu na kusema kwamba, angependa siku zijazo, asikie simulizi za wahitimu wa leo: walioboresha huduma za afya, waliobuni teknolojia, walioanzisha biashara na ajira, waliotetea haki, waliofundisha vizazi vipya na walioleta mabadiliko chanya katika jamii zao. Hizo ndizo simulizi zinazojenga heshima ya taasisi. Ameongeza kuwa, Kidato cha Nne ni hatua muhimu, lakini si mwisho wa elimu wala mwisho wa kujijenga. Ni mlango unaofunguka kuelekea hatua nyingine. Amesema, “baadhi yenu mtaendelea na Kidato cha Tano na Sita; wengine mtachagua mafunzo ya ufundi na stadi; wengine mtajiandaa kwa njia nyingine za kujifunza na kujenga taaluma. Njia zinaweza kutofautiana, lakini wajibu ni mmoja: kuendelea kujifunza na kujitengeneza.” Aidha, amewakumbusha wahitimu hao kutokimbilia kutafuta mafanikio yanayoonekana kabla hawajajenga msingi wa mafanikio ya kweli kwakuwa Dunia ya sasa inaweza kumfanya kijana aamini kwamba mafanikio ni kuonekana, kuwa maarufu au kupata fedha haraka. Amesema, huo si msingi salama wa maisha kwani mafanikio ya kudumu yanahitaji maarifa, ujuzi, nidhamu, uvumilivu, uaminifu na uwezo wa kufanya maamuzi sahihi hata pale ambapo hakuna mtu anayewaangalia. Kadhalika, Jaji Mkuu amewaasa Wahitimu hao wa Kidato cha Nne kumcha Mungu na wawe na dhamira inayowaongoza kutenda yaliyo mema huku akinukuu Biblia Takatifu, katika Mithali 4:13, inayohimiza kuishika elimu na Qur’ani Tukufu, katika Suratul Al-Alaq (96:1–5), inatukumbusha umuhimu wa kusoma na kujifunza ambapo mafundisho hayo yanatuelekeza kuona elimu kama wajibu na neema inayopaswa kutumiwa kwa busara. Vilevile, amewataka kuwaheshimu wazazi, walezi na walimu wao na kusisitiza kuwa heshima si udhaifu; ni alama ya ukomavu. Katika hatua nyingine, Mhe. Masaju amewataka Wahitimu hao kutosubiri Taifa liwaite viongozi ndipo waanze kuonesha uongozi hivyo, amewasisitiza kuanza kuongoza maisha yao kwa nidhamu, kwa kuwa waaminifu, kwa kuwaheshimu wengine na kwa kutimiza wajibu wao kwakuwa Uongozi huanza kabla ya cheo. Akiizungumzia Shule ya Sekondari Lake, Jaji Mkuu amesema anaiheshimu na kusisitiza Lake isiwe shule inayojivunia tu watu waliopita hapo bale iwe shule inayowaandaa watu ambao Taifa litajivunia kesho. “Kila mhitimu anayekuwa muadilifu, kila mtaalamu anayefanya kazi kwa ubora, kila kiongozi anayewajibika na kila kijana anayebuni suluhisho jipya, anaongeza ukurasa katika historia ya Lake,” amesisitiza. Kadhalika, Mhe. Masaju amewakumbusha watu mbalimbali waliomaliza katika shule hiyo na katika shule nyingine nchini kuwa na utaratibu wa kuzitembelea shule walizosoma. Amesisitiza kwa kusema, “Tunaporejea mashuleni tulikosoma, tunapata fursa ya kutoa shukrani na kukutana na wale waliochangia kutujenga.” Jaji Mkuu amesema, amerudi shuleni hapo akiwa na dhamira ya kutoa shukrani, kutambua mchango wa shule hiyo na, muhimu zaidi, kuwaambia wanafunzi wa leo kwamba ndoto zao zinaweza kuwapeleka mbali zaidi ya mipaka wanayoiona sasa. Katika hatua nyingine, Jaji Mkuu ameushukuru Uongozi wa Shule hiyo kwa kumualika na kumpa nafasi ya kurejea katika Shule ya Sekondari Lake mahali pa kumbukumbu, malezi na sehemu ya safari ya maisha yake na wengine wengi waliopita katika shule hiyo. Ameomba shule hiyo iendelee kung’aa, si kwa historia yake tu, bali kwa ubora wa watu inaowaandaa kwa ajili ya Tanzania. “Nimepokea mwaliko huu kwa heshima kubwa. Lakini niseme wazi: kwangu mimi, leo si siku ya kutembelea shule nyingine tu; ni siku ya kurejea mahali ambapo sehemu ya safari yangu ya maisha ilianzia. Kabla ya vyeo vyetu, kabla ya ofisi zetu, kabla ya majukumu yetu kitaifa na kabla ya heshima tuliyokuwa nayo, tulikuwa wanafunzi. Nasi pamoja na Madaraka yetu tulikuwa vijana wenye safari mbele yetu, wenye mambo ya kujifunza, wenye ndoto na wenye wajibu wa kufanya bidii,” amesema Mhe. Masaju. “Ningependa niwaambie jambo moja mapema: msinitazame leo kwa kuona tu cheo nilichonacho. Nitajeni pia kama mmoja wa wanafunzi waliowahi kukaa madarasani hapa, kusoma, kufundishwa na kuandaliwa kwa maisha. Cheo ni dhamana ya leo; lakini historia ya mtu hujengwa hatua kwa hatua, na mara nyingi hatua hizo huanzia katika madarasa kama haya,” ameeleza. Kadhalika, Jaji Mkuu amekiri kupokea kwa furaha taarifa ya wazo la kuanzisha Chuo Kikuu cha Lake (Lake University) ambapo amewapongeza viongozi na wadau wa shule kwa kuwa na ndoto hiyo. Amesema, Taasisi inayothubutu kufikiria hatua inayofuata inaonesha kuwa haitaki kuishi kwa kutegemea historia pekee; inataka kushiriki katika kuandika historia mpya. “Nimeelezwa pia kuhusu changamoto ya eneo lililokuwa limetengwa kwa ajili ya mradi huo. Changamoto hiyo isitumike kuzima ndoto, bali iwe nafasi ya kutathmini upya mpango. Hata hivyo, ndoto ya chuo kikuu inahitaji maandalizi ya kitaalamu na ya muda mrefu: upembuzi yakinifu, mahitaji ya jamii na soko la ajira, maeneo ya kitaaluma yatakayopewa kipaumbele, uwezo wa kifedha, miundombinu, rasilimali watu, usimamizi na utii wa taratibu za mamlaka husika,” amesisitiza. Ameushari uongozi wa shule hiyo uandae mpango kabambe wa hatua kwa hatua, ukiangalia mahitaji ya sasa na ukuaji wa taasisi kwa miaka mingi ijayo. Eneo la chuo lisitazamwe kwa mahitaji ya leo pekee; litazamwe kwa uwezo wa kupanuka, usafiri, huduma, mazingira na mahitaji ya wanafunzi na wafanyakazi. Ndoto kubwa inahitaji maandalizi makubwa, lakini utekelezaji wake uanze kwa hatua zinazopimika. Kadhalika, ametoa wito kwa wadau wote kuendelea kuwekeza katika walimu, maabara, maktaba, teknolojia, michezo, ushauri nasaha na mazingira salama ya kujifunzia na si kuwekeza katika majengo pekee bali wawekeze pia kwa watu, mifumo na maadili yanayofanya majengo hayo yawe na maana. Awali akizungumza katika mahafali hayo, Mkuu wa Shule ya Sekondari Lake, Mwalimu Lucas Bunuma amesema jumla ya Wanafunzi 76 wamehitimu kidato cha nne, 30 Wanawake na 46 Wanaume. Mwalimu Bunuma amemshukuru Jaji Mkuu, Mhe. Masaju kwa heshima na fadhila kubwa ambayo amefanya kwa uongozi wa shule hiyo kwa kukubali kuwa mgeni rasmi wa siku hiyo muhimu. “Tunajua una majukumu mengi na katika shughuli zako ikiwa ni pamoja na familia, bado umetupa kipaumbele siku hii ya leo, na umetupa hadhi kubwa ya kitaifa, wewe ambaye ulikuwa mwanafunzi wa shule hii, ikiwa ni pamoja na wanafunzi wengine waliosoma hapa na wamehudhuria mahafali ya leo,” amesema Mkuu wa Shule huyo. Akizungumzia kuhusu maendeleo ya Taaluma, Mwalimu Bunuma ameishukuru Bodi ya Wamiliki ya Shule hiyo kwa kuboresha mazingira mazuri yanayohamasisha wanafunzi kujifunza na kufundisha. “Tumepata ushindi wa daraja la kwanza, la pili, la tatu pekee kwa mwaka 2025. Kidato cha nne na cha sita ufaulu wetu ni asilimia 100. Kwa mfano mwaka 2025, kidato cha nne daraja la kwanza tulikuwa na wanafunzi 44, daraja la pili wanafunzi 33, daraja la tatu wanafunzi 4. Kidato cha sita daraja la kwanza walikuwa ni wanafunzi 20, daraja la pili walikuwa ni wanafunzi 36, na daraja la tatu walikuwa ni wanafunzi 10,” amesema. Katika Mahafali hayo Kadhalika Jaji Mkuu alipata wasaa wa kutembezwa katika maeneo mbalimbali ya shule hiyo ikiwemo Maabara, Maktaba na sehemu nyingine kadhaa ambapo alijionea maboresho mbalimbali yaliyofanyika katika shule hiyo. Kadhalika, Mhe. Masaju amekutana na Mwalimu aliyemfundisha Somo la Kemia (Chemistry), Mwalimu Kiran Mody ambapo ameonesha furaha baada ya kukutana na Mwalimu huyo. Miongoni mwa Viongozi waliosoma katika shule hiyo ni pamoja na Rais wa Awamu ya Tano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, Mhe. Dkt. Stegomena Tax, aliyekuwa waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa, lakini pia alikuwa katibu mtendaji wa jumuiya ya maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika (SADC), Dkt. Angelina Mabula na wengine kadhaa. Mahafali hayo yalipambwa na burudani mbalimbali kutoka kwa Wahitimu, Wanafunzi na Kikundi cha Ngoma za Asili cha Bujora igizo la uendeshaji wa Mahakama ya Mazoezi (Moot Court). Matukio katika picha ya Mahafali ya Kidato cha Nne ya Shule ya Sekondari Lake ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju leo tarehe 02 Novemba, 2026 jijini Mwanza. Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju (aliyesimama katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wahitimu wa Kidato cha Nne wa Shule ya Sekondari Lake iliyopo jijini Mwanza. Mhe. Masaju alikuwa Mgeni Rasmi wa Mahafali hayo yaliyofan

Tue, 03 Nov 2026 11:48:03 +0000
Uncategorized · Daily News

Tanzania bolsters 220kv power transmission to connect Lindi, Mtwara with the national grid

DODOMA: THE Tanzanian government is continuing to implement 220-kilovolt (kV) power transmission projects aimed at connecting Lindi and Mtwara regions…

Recently
Uncategorized · DW Rwanda

Asian Cup postponed due to Middle East conflict

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

Kenya partners with China for off-grid electrification in remote areas

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Daily News

Tanzania advances 110tri/- LNG investment ambition

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · SoftPower News

Aponye Charts New Growth Strategy for Uganda’s Food Value Chain

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Daily News

Tanzania pledges to continue setting designated areas for women entrepreneurs

DODOMA: THE Tanzanian government will continue setting aside designated areas for women entrepreneurs to engage in production and business activities…

Recently
Uncategorized · DW Rwanda

Ukraine's Zelenskyy arrives in Berlin for talks with Merz

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

Gachagua puts opposition presidential hopefuls on notice over lack of grassroots effort

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

Gachagua invokes 2002 script, vows united opposition

“I want to assure the people of Kenya that we in the opposition have agreed we shall give the people of Kenya one presidential candidate."

Recently
Uncategorized · Capital FM

Two police officers injured as attackers steal loaded AK-47 rifles in Ruai

Latest · COUNTDOWN TO 2022

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

Early exposure biggest worry as KCSE enters day 2

KNEC has tightened controls on mobile phones, smartwatches and examination paper access amid concerns over early exposure and technology-enabled cheating.

Recently
Uncategorized · Capital FM

DPP Seeks Death Penalty for Pastor Mackenzie Over 191 Shakahola Deaths

Latest · NATIONAL NEWS

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

Gachagua taps Ngilu's coalition experience in latest opposition consultation ahead of 2027

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Issa Michuzi

TANZANIA DELEGATION HIGHLIGHTS THE OBSERVANCE OF HUMAN RIGHTS AND SUSTAINABLE DEVELOPMENT AHEAD OF TANZANIA'S FOURTH UPR REVIEW

Geneva, Switzerland | 3 November 2026 The Delegation of the United Republic of Tanzania to the UPR 53 has reaffirmed the relevance of Tanzania's legal framework in promoting human rights, inclusive development and international cooperation as Tanzania prepares for its Fourth Cycle of the Universal Periodic Review (UPR) under the United Nations Human Rights Council. The Delegation is making the preparation under the leadership of H.E. Ambassador Dr. Abdallah Possi at the Permanent Mission of the United Republic of Tanzania to the United Nations in Geneva, Switzerland. The engagement is part of Tanzania's preparations for the 53rd Session of the UPR Working Group, scheduled to take place from 2 to 13 November 2026 at the United Nations Office in Geneva. Tanzania's participation highlights the importance it accords to human rights and its contribution to national and international efforts to promote human dignity, equal opportunities, access to knowledge and inclusive societies. Through its areas of competence in Education, Natural Sciences, Social and Human Sciences, Culture, and Communication and Information, UNESCO supports initiatives that contribute to the advancement of human rights and sustainable development. The preparatory engagement provided an opportunity for members of the Tanzanian delegation to coordinate their preparations ahead of the national review. Tanzania's Fourth UPR Cycle offers an important platform to present progress made in fulfilling its human rights commitments, share national experiences and engage constructively with other Member States on recommendations arising from previous review cycles.

Tue, 03 Nov 2026 11:23:16 +0000
Uncategorized · BBC Rwanda

Uganda yataye muri yompi uwahoze ari icegera c'umukuru w'igisirikare, yari aherutse gukororwa amapete

Umuvugizi w'igisirikare yavuze ko inzego z'umutekano zafatiye muri imwe mu nzu za Elwelu inkoho 15, impuzu z'igisirikare hamwe n'imodoka zibiri zo mu bwoko bwa pick-up.

Recently
Uncategorized · KBC

Five arrested as police seize 1,300 litres of Kangara in Soweto, Nairobi

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

Ebola: All quarantined persons to be released by next week

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Jamhuri Media

NMB yatenga milioni 600/- kuwazawadia wateja wanaoweka akiba

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

Early exposure biggest worry as KCSE enters day 2

KNEC has tightened controls on mobile phones, smartwatches and examination paper access amid concerns over early exposure and technology-enabled cheating.

Recently

Page 442 of 1160 · 23194 stories