Search the region
23254 stories
DC KIBAHA AIFUNGIA KATOROSIA SEKONDARI KWA KUKIUKA MAAGIZO YA SERIKALI
Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha MWENYEKITI wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Kibaha, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Fadhil Emmanuel Nkurlu, ameifungia shule binafsi ya sekondari ya Katorosia, iliyopo Kata ya Pangani mkoani Pwani, kutokana na kukosa vigezo vinavyotakiwa pamoja na kukaidi maagizo ya serikali yaliyotolewa Julai 25, 2025. Shule hiyo ilielekezwa kufungwa kutokana na mazingira hatarishi na yasiyoridhisha kwa wanafunzi kuishi, ikiwemo hali mbaya ya mabweni, uchafu wa vyoo na maeneo ya kulala, vitanda vibovu pamoja na majengo chakavu. Aidha, shule hiyo iliyosajiliwa kutoa elimu ya kutwa, imebainika kuwa mmiliki alikuwa akilaza wanafunzi shuleni, huku wanafunzi wa kike na wa kiume wakilala katika mabweni yaliyotajwa kutokuwa na mazingira salama na yanayokidhi mahitaji ya wanafunzi. Nkurlu alifanya ziara ya kufunga shule hiyo November 2,2026 akiwa ameambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya pamoja na maofisa Idara ya Elimu Sekondari ya Manispaa ya Kibaha. Akizungumza wakati wa hatua hiyo, Nkurlu alisema shule hiyo imekiuka na kukaidi maagizo ya serikali pamoja na maelekezo ya Udhibiti Ubora wa Shule, licha ya kupewa muda wa kufanya marekebisho. Alisema maagizo hayo si mapya wala ya dharura, hivyo mmiliki alipaswa kuyatekeleza na kuhakikisha wanafunzi hawaendelei kuwepo shuleni. Aliongeza kuwa kufungwa kwa shule hiyo ni salamu kwa wamiliki wengine wa shule wanaokiuka taratibu, miongozo na maelekezo ya sekta ya elimu, akisisitiza kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi ya watakaobainika kufanya hivyo. Kwa upande wake, Ofisa Elimu Sekondari wa Manispaa ya Kibaha , Theresia Charles alisema shule hiyo ilisimamishwa usajili mwaka 2025 kutokana na kukosa sifa za kudahili wanafunzi. Alisema pia shule hiyo imekuwa na changamoto za utoaji wa elimu, ikiwemo walimu kutotoa majaribio ya mitihani na kutofundisha wanafunzi ipasavyo. Alieleza kuwa madai ya mmiliki kuwa shule imefungwa tangu Ijumaa iliyopita hayana msingi, kwa kuwa shule nyingine hazijafungwa na hakuna sababu ya shule hiyo kusitisha shughuli zake kabla ya muda. Naye Mtendaji wa Mtaa wa Mtakuja, Evena Michael, alisema mmiliki wa shule hiyo amekuwa mkaidi, akieleza kuwa licha ya viongozi kutoa maelekezo, alikuwa akiendelea na shughuli zake mara baada ya viongozi kuondoka. Alisema mazingira ya shule hiyo hayakuwa salama kwa wanafunzi kusomea na kuishi, hivyo hatua ya kuifunga ilikuwa muhimu kwa ajili ya kulinda usalama na afya za wanafunzi. Kwa upande wake, mmiliki wa shule hiyo, Emalieza Sekwao Chilemeji, alisema shule hiyo ilianza mwaka 2013 na kusajiliwa kama shule ya kutwa, huku akikiri kukiuka maagizo ya serikali kuhusu mazingira ya shule na afya za wanafunzi, pamoja na kuigeuza kuwa shule ya bweni. Chilemeji alisema amepokea maagizo yaliyotolewa na serikali na kuahidi kutoruhusu mwanafunzi yeyote kuendelea kuwepo shuleni kuanzia sasa.
Mon, 02 Nov 2026 13:35:25 +0000COMESA partners seek stronger geospatial planning to accelerate electricity access in Africa
Read the full report from the original source.
RecentlyWANANCHI WA MOROGORO KUSINI MASHARIKI KUNUFAIKA NA KAMBI YA MATIBABU YA BURE
Serikali kupitia Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), kwa kushirikiana na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, imeandaa kambi maalumu ya uchunguzi na matibabu ya kibingwa kwa wananchi wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki. Kambi hiyo itakayofanyika kuanzia Novemba 10 hadi 20, 2026, itatoa huduma hizo bila malipo kwa wananchi wenye uhitaji. Huduma hizo zitatolewa katika tarafa za Mikese, Ngerengere na Mkuyuni, kwa ufadhili wa Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki, Mheshimiwa Hamiss Taletale, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kusogeza huduma za afya karibu na wananchi. Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mussa Kilakala, amesema lengo la kambi hiyo ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma za uchunguzi na matibabu ya kibingwa kulingana na mahitaji yao. Aidha, amewahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kutumia fursa hiyo muhimu ya kupata huduma za afya bila gharama. Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Morogoro kusini Mashariki Hamisi Taletale, amesema ameamua kufadhili huduma hizo kutokana na changamoto zinazowakabili wananchi wa jimbo lake katika kupata matibabu ya kibingwa, ambayo kwa kiasi kikubwa hupatikana katika hospitali zilizo mbali na maeneo yao na kuhitaji gharama kubwa. Amesema hali hiyo imekuwa ikiwafanya baadhi ya wananchi kushindwa kupata matibabu kwa wakati kutokana na uwezo mdogo wa kiuchumi, jambo linaloweza kusababisha kuendelea kuugua au kupoteza maisha. “Jiografia ya Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki inaleta changamoto kubwa katika upatikanaji wa huduma za matibabu ya kibingwa. Hali hii imesababisha baadhi ya wananchi kushindwa kupata matibabu kwa wakati kutokana na uwezo wao mdogo wa kiuchumi. Ndiyo maana nimeona umuhimu wa kuwasogezea huduma hizi wananchi wangu,” amesema Taletale. Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Mussa Ali Mussa, amesema maandalizi ya kambi hiyo yamekamilika na kuwataka wananchi wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki pamoja na wakazi wengine wa mkoa huo kujitokeza kwa wingi kupata huduma zitakazotolewa. Ameongeza kuwa, pamoja na huduma za uchunguzi na matibabu, kutakuwa na fursa ya wananchi kupata huduma za Bima ya Afya kwa Wote, ambapo kila tarafa kati ya Mikese, Mkuyuni na Ngerengere itapatiwa jumla ya bima 50. Amesisitiza kuwa kambi hiyo ni fursa muhimu kwa wananchi kupata huduma za afya bila malipo, hivyo amewataka kuitumia ipasavyo kwa kujitokeza katika maeneo yatakayopangwa kutolea huduma hizo. Kambi hiyo inatarajiwa kuwa mkombozi kwa wananchi wengi ambao wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa huduma za matibabu ya kibingwa kutokana na umbali na gharama za matibabu.
Mon, 02 Nov 2026 13:27:11 +0000Devki tycoon Raval splashes over Sh200bn on cement, steel plants
Read the full report from the original source.
Recently‘The Unforgivable’ Screened in Kampala
Read the full report from the original source.
RecentlyGovernment Orders Public Servants to Repay Lost Funds or Property Within 30 Days
Read the full report from the original source.
RecentlyMTN Nigeria moves MoMo to new platform as fintech revenue falls 26%
Read the full report from the original source.
RecentlyTISEZA yasajili miradi 1,148 ya uwekezaji yenye thamani ya dola bilioni 15.32
Read the full report from the original source.
RecentlyBubanza : Des projets de développement malgré les défis
La commune Bubanza de la province Bujumbura s’active à exécuter des projets de développement mis en avant pour l’exercice budgétaire 2026-2027. Administration et élus affirment que ces programmes tiennent comptent des vœux de la population. Mais il est des fois où des fonds ne suivent pas.
Mon, 02 Nov 2026 13:25:23 +0000Stop political bullying and double-speak, Muturi tells Gachagua
Muturi said the current political trajectory being pursued by Gachagua raises serious questions about his commitment to the collective presidential ambition of the Wantam movement.
Mon, 02 Nov 2026 16:00:00 +0300NWSC to restore roads affected by Greater Kampala water project
KAMPALA - The National Water and Sewerage Corporation (NWSC) has assured residents affected by ongoing water pipeline installation works in the Greater Kampala Metropolitan Area (GKMA) that damaged roads, walkways and...
Recentlydfcu Bank Offers Up to 85% Property Financing in New 16.9% Home Loan Deal
Read the full report from the original source.
RecentlyINEC blames registration officers, but AI photos are the least of its worries
Read the full report from the original source.
RecentlyCourt: Cops liable for brutality even if victim can't identify shooter
Justice Joe Omido says victims of unlawful police shootings should not be denied justice because they cannot identify the shooter during chaotic operations
RecentlyMvua yatikisa Kigoma, nyumba 121 zaathirika
Read the full report from the original source.
RecentlyTISEZA creates million jobs from 3,538 projects worth 68.6bn US dollars in five years
DAR ES SALAAM: TANZANIA has registered 3,538 investment projects worth 68.6bn US dollars, equivalent to approximately 150tri/-, between 2021 and…
RecentlyDr Samia tasks CMA to adhere to labour laws in settling employer-employee disputes
DODOMA: PRESIDENT Samia Suluhu Hassan has urged the Commission for Mediation and Arbitration (CMA) to uphold the law and ensure…
RecentlyDIWANI SIMANJIRO AIOMBA SERIKALI KUDHIBITI TEMBO
Na Mwandishi Wetu, Simanjiro DIWANI wa Kata ya Naberera, Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara, Marco Munga, ameiomba Serikali kuchukua hatua za haraka kudhibiti tembo wanaovamia makazi ya wananchi na kusababisha vifo. Munga ametoa ombi hilo katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro kilichofanyika makao makuu ya wilaya hiyo, Orkesumet, akieleza kuwa matukio ya tembo kuvamia makazi yamesababisha hofu na taharuki miongoni mwa wananchi. Amesema wiki iliyopita, kijana mwenye umri wa miaka 16 aliuawa na tembo katika eneo hilo, hali inayohitaji hatua za haraka za kukabiliana na wanyama hao. “Wiki iliyopita kuna kijana mdogo wa miaka 16 ameuawa na tembo, jambo lililosababisha hofu kwa wakazi wa eneo hilo. Tunaomba hatua zichukuliwe ili kudhibiti tembo hao,” amesema Munga. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro, Kaleya Melita Mollel, ametoa pole kwa wananchi wa Naberera na maeneo mengine ya wilaya hiyo walioathiriwa na matukio ya tembo. Mollel amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri kushirikiana na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) kuandaa mpango mkakati wa kudhibiti wanyama hao. Aidha, amesisitiza umuhimu wa kufuatilia utaratibu wa kulipa fidia kwa wananchi walioathiriwa na matukio hayo ili kuhakikisha wanapata stahiki zao. Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Gracian Max Makota, amesema Halmashauri imeweka mikakati kwa kushirikiana na TAWA kukabiliana na changamoto hiyo. Amesema mikakati hiyo inahusisha kutoa elimu kwa jamii kupitia mikutano ya vitongoji, vijiji na nyumba za ibada, pamoja na kuwafundisha wananchi mbinu na kuwapatia zana za kujikinga na tembo. Makota ameongeza kuwa vituo vya kukabiliana na wanyama waharibifu vinaendelea kujengwa, ambapo kituo kimoja kinajengwa katika Kijiji cha Kandasikira na kingine kinatarajiwa kujengwa Naberera. Kwa upande wake, Afisa Wanyamapori wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro, Aloyce Olodonjilalo, amesema kikosi cha doria kinaendelea na msako wa tembo hao ili kudhibiti vitisho vinavyowakabili wananchi. Olodonjilalo amesema TAWA imepatia eneo hilo ndege mmoja aina ya ndege nyuki kwa ajili ya kusaidia kuwafukuza na kuwahamisha tembo. Ameongeza kuwa idadi ya askari imeongezwa baada ya kupatiwa mafunzo, huku baadhi yao wakipelekwa katika Chuo cha Wanyamapori cha Sekamaganga, Tabora, kwa ajili ya mafunzo zaidi.
Mon, 02 Nov 2026 13:20:55 +0000‘Can a School Operate on Shs7,000?’ Parent Challenges Government Over Education Funding
Read the full report from the original source.
RecentlyKenya eyes regional maritime security hub as Red Sea threats widen
Latest · Africa
RecentlyPage 468 of 1163 · 23254 stories