Search the region
22503 stories
Matiang’i disputes Ruto’s account of how Kenya printed its 2026 exams
Read the full report from the original source.
RecentlyNvidia reinstates Jensen Huang as CEO in major U-turn
The board voted unanimously to reinstate Jensen Huang, a statement released on Nvidia's website says.
RecentlyNHIF YATOA FURSA KWA WANAFUNZI IFM KUPATA UZOEFU
Na Mwandishi Wetu MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Dkt. Irene Isaka, ameitaka Taasisi ya Usimamizi wa Fedha (IFM) kuendelea kuzalisha wataalamu wenye ubunifu, uadilifu na uwezo wa kutatua changamoto zinazolikabili Taifa kupitia teknolojia na mifumo mbalimbali. Dkt. Isaka amesema wataalamu wanaozalishwa na vyuo wanapaswa kuwa sehemu ya kutafuta suluhisho la changamoto za jamii kwa kutumia maarifa waliyonayo, ikiwemo kubuni mifumo inayorahisisha shughuli za kiuchumi na kijamii. Amesema hayo wakati wa Kongamano la Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) lililofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Utalii jijini Dar es Salaam, ambapo amesisitiza umuhimu wa wataalamu kuzingatia uadilifu katika utekelezaji wa majukumu yao. Amesema pamoja na kuwa na ufaulu mzuri kitaaluma, mtaalamu anapaswa kuwa na maadili na kujitambua ili aweze kutumia ujuzi wake katika kutatua changamoto za wananchi na kuchangia maendeleo ya Taifa. “Jamii ina changamoto nyingi ambazo wataalamu wetu wanapaswa kuzitumia kama fursa za kuzitatua kwa kubuni teknolojia na mifumo mbalimbali itakayorahisisha maisha ya watu,” amesema. Aidha, amesema mabadiliko ya teknolojia na utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050 yanatoa fursa kwa IFM kuboresha mitaala yake ili kuzalisha vijana wenye uwezo wa ubunifu, uzalishaji na kuchangia maendeleo ya Taifa. Amesema NHIF itatoa fursa kwa wanafunzi 10 bora wa mwaka wa tatu wa IFM kufanya mafunzo ya vitendo katika taasisi hiyo ili kuwajengea uzoefu wa kazi na kuwaandaa kwa fursa za ajira na kujiajiri. Kwa upande wake, Mkuu wa IFM, Profesa Henry Chalu, amesema chuo hicho kitaendelea kuimarisha mifumo ya elimu inayozalisha wataalamu wanaokidhi mahitaji ya soko la ajira na kuchangia maendeleo ya nchi. Amesema kongamano hilo ni sehemu ya mkakati wa chuo kuhamasisha tafiti na ubunifu unaolenga kutatua changamoto katika sekta mbalimbali, huku wanafunzi wakipata fursa ya kuwasilisha mawazo na mifumo waliyoibuni. Profesa Chalu amesema chuo kinaendelea kusimamia misingi ya elimu inayowawezesha wanafunzi kutumia maarifa yao katika mazingira halisi ya kazi na kujibu mahitaji ya jamii. Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Kongamano hilo, Dkt. Shaban Ngole, amesema kongamano hilo limekuwa na mawasilisho mbalimbali yanayolenga kuonesha ubunifu wa wanafunzi na fursa zinazoweza kuwasaidia katika maisha yao ya kitaaluma na kiuchumi. Amesema wanafunzi 10 wamepata nafasi ya kufanya mafunzo ya vitendo NHIF, hatua itakayowasaidia kuongeza ujuzi na uzoefu katika mazingira ya kazi. Mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa IFM, Adrian Kachocho, amesema amebuni mfumo unaowasaidia wafanyabiashara kufuatilia mapato na matumizi ya biashara zao, hatua inayoweza kuwasaidia kufanya maamuzi sahihi na kuboresha usimamizi wa biashara.
Mon, 23 Nov 2026 15:12:41 +0000TUMIENI MEWAKA KATIKA KUFUNDISHANA MBINU ZA JOLLY PHONICS - DKT. KOMBA
MKURUGENZI Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania Dkt. Aneth Komba ametoa wito kwa walimu wanao shiriki mafunzo ya mbinu za ufundishaji wa somo la Kiingereza (Jolly Phonics) kutumia MEWAKA zao ili kuwafundisha walimu ambao hawajapata fursa ya kushiriki mafunzo hayo. Ametoa wito huo kwa njia ya darasa janja (smart class) leo Novemba 23, 2026 wakati akifungua mafunzo hayo yanayotarajia kufanyika katikati mikoa ya Dar es Salaam, Mbeya, Ruvuma na Lindi ili kukuza stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK) kwa lugha ya kiingereza. Dkt. Komba amesema, mafunzo hayo yatasaidia kuboresha ufundishaji na ujifunzaji wa somo la Kiingereza huku, akiwahimiza walimu kufuatilia mafunzo kwa makini na kuomba ufafanuzi wa ziada pindi itapohitajika. “Naomba sana mfuatilie kwa makini mafunzo haya ili muweze kupata ujuzi utakaowasaidia kuwafundisha wanafunzi katika madarasa yenu. Hakikisheni mnajifunza vizuri ili msaidie wanafunzi wenu kuelewa zaidi,” amesema Dkt. Komba. Poa, Dkt. Komba amewashukuru Jolly Futures kwa kushirikiana na TET katika kutoa mafunzo hayo, yanayoendeshwa kwa mfumo wa darasa janja, huku wakufunzi wa TET na Jolly Futures wakiwasaidia walimu ana kwa ana. Kwa upande wake mkufunzi wa mafunzo hayo Bi. Sheba Moyo amesema kuwa, mafunzo hayo ni muhimu kwa walimu ambapo itasaidia wanafunzi shuleni kuelewa zaidi somo la kiingereza na kuwataka walimu hao waendelee kujifunza zaidi kupitia jumuiya zao za ujifunzaji kama vile MEWAKA. Mafunzo yameanza katika Mkoa wa Dar es Salaam na yataendelea katika mikoa ya Lindi, Ruvuma na Mbeya.
Mon, 23 Nov 2026 15:18:52 +0000Call for African nations to enhance trade ties by adding value to domestic products
ADDIS ABABA: ETHIOPIA’S Deputy Prime Minister, Temesgen Tiruneh, has urged African countries to strengthen trade cooperation by adding value to…
RecentlyCall for Tanzanians to uphold moral values, ethical Tanzania
DAR ES SALAAM: THE Minister for Finance, Ambassador Khamis Mussa Omar, has called on Tanzanians to work together to restore…
RecentlyNAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA CHINA AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Miao Deyu, amewasili nchini Novemba 23, 2026, kwa ziara ya kikazi inayolenga kuimarisha ushirikiano wa kihistoria kati ya Tanzania na China, kupitia majadiliano kuhusu masuala mbalimbali yenye maslahi ya pamoja kwa nchi hizi mbili. Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Mhe. Miao alipokelewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Ngwaru Maghembe akiwa ameambatana na Viongozi wengine kutoka Tanzania na China, akiwemo Balozi wa Tanzania nchini China, Mhe. Dkt. Suleiman Haji Suleiman na Balozi wa China nchini, Mhe. Chen Mingjian. Wakati wa ziara hiyo, masuala yatakayojadiliwa ni pamoja na utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa wakati wa ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Mhe. Wang Yi, iliyofanyika mwezi Januari, 2026, maendeleo ya mradi wa ukarabati na uboreshaji wa Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA), pamoja na maeneo mengine ya ushirikiano wa kiuchumi na kidiplomasia. Aidha, ziara hiyo itahusisha mkutano wa utatu kati ya Tanzania, China na Zambia, utakaotoa fursa kwa nchi hizo kujadili masuala mbalimbali yanayohusu mradi wa TAZARA, ikiwemo utekelezaji wake na nafasi yake katika kukuza biashara, usafirishaji na maendeleo ya uchumi wa kikanda. Katika kuenzi urafiki na mshikamano wa muda mrefu kati ya Tanzania na China, Mhe. Miao pia atatembelea makaburi ya wataalam wa China yaliyopo Gongo la Mboto, jijini Dar es Salaam, kwa heshima ya raia wa China waliopoteza maisha wakati wa kushiriki ujenzi wa Reli ya TAZARA. Vilevile, atashiriki warsha maalumu kuhusu TAZARA itakayofanyika katika Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere kilichopo Wilayani Kibaha, mkoani Pwani. Ziara hiyo inatarajiwa kutoa fursa ya kuendeleza majadiliano kuhusu masuala ya kipaumbele kwa mataifa hayo mawili, kuimarisha ushirikiano uliopo na kuweka msingi wa utekelezaji wa mipango ya pamoja yenye manufaa kwa wananchi wa Tanzania, China na Zambia.
Mon, 23 Nov 2026 15:12:56 +0000U Rwanda rugiye gufatanya na Korea guteza imbere AI mu burezi
Read the full report from the original source.
RecentlyOmukama Nyabongo Appoints Benard Tungwako as New Prime Minister of Tooro Kingdom
Read the full report from the original source.
RecentlyCHIMP SPORT: Nam Blazers Overcome Dolphins in Elite 16 Opener
Read the full report from the original source.
RecentlyTotally Headless Ii Yaleta Msisimko Ndani ya Meridianbet!
BURUDANI ya kasino inazidi kupamba moto ndani ya Meridianbet kupitia mchezo mpya wa Totally Headless II kutoka kwa kampuni maarufu ya utengenezaji wa michezo ya kasino, Games Global. Mchezo huu umewasili kwa namna ya kipekee, ukiwaletea wapenzi wa kasino fursa ya kuingia katika ulimwengu wa maajabu, burudani na msisimko unaovutia. Bila kusahau kujisajili ili ufurahie msisismko huu leo ndani ya meridianbet. Kupitia Totally Headless II, wachezaji wanakaribishwa kufurahia mazingira ya kipekee yaliyojaa matukio ya kusisimua, huku kila mzunguko ukiendelea kuongeza ladha ya burudani. Ni mchezo unaokualika kuchunguza ulimwengu wake wa kuvutia na kufurahia kila hatua ya safari yako ya kasino . Kinachoufanya mchezo huu kuwa sehemu ya burudani inayostahili kuifahamu ni mchanganyiko wa ubunifu wa Games Global na msisimko unaotokana na kucheza. Kila unapozungusha, unapata nafasi ya kufurahia uzoefu tofauti huku ukiwa na matarajio ya matokeo yatakayokuletea furaha. Sasa unaweza kuufurahia mchezo huu kupitia jukwaa la Meridianbet, ambalo linaendelea kukuletea michezo mbalimbali ya kasino kutoka kwa watengenezaji wanaotambulika. Totally Headless II ni fursa nyingine ya kuongeza ladha ya burudani yako kwa kuingia katika ulimwengu wake wa kipekee. Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi. Usibaki nyuma wakati burudani hii mpya imewasili! Tembelea Meridianbet, fungua mchezo wa Totally Headless II na ugundue msisimko unaokusubiri. Totally Headless II Zungusha, furahia msisimko na uwe sehemu ya burudani mpya ndani ya Meridianbet!
Mon, 23 Nov 2026 10:30:00 +0000UTEKELEZAJI WA PURA WAIBUA MATARAJIO YA UCHIMBAJI MAFUTA TANGA MWAKA 2027
Na Karama Kenyunko, Michuzi TV MAMLAKA ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) imeeleza kuwa maandalizi ya kuchimba kisima cha utafutaji wa mafuta katika Kitalu cha Tanga yanaendelea, huku uchimbaji huo ukitarajiwa kufanyika mwaka 2027 baada ya kubainika kwa maeneo matatu yenye viashiria vya uwepo wa mafuta. Maeneo hayo yaliyotambuliwa kama Prospect 1, Prospect 3 na Prospect 5 yamebainika kupitia tafsiri mpya ya takwimu za mitetemo za pande tatu (3D seismic data) zilizokusanywa katika Kitalu cha Tanga. Akizungumza jana wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu na mafanikio ya PURA kwa mwaka wa fedha 2025/26 katika kikao na wahariri na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mkuu wa PURA, Charles Sangweni, alisema maandalizi ya uchimbaji wa kisima cha utafutaji yanaendelea. Katika utekelezaji wa shughuli za utafiti, PURA pia iliendelea kusimamia tafiti za awali za mafuta na gesi asilia katika maeneo ya Eyasi-Wembere na Lindi-Mtwara. Katika eneo la Eyasi-Wembere, ukusanyaji wa takwimu za mitetemo za pande mbili (2D seismic data) ulikuwa umefikia kilomita 772 kati ya kilomita 779 zilizopangwa hadi Juni 30, 2026, sawa na asilimia 99. Kwa upande wa Lindi-Mtwara, ukusanyaji wa takwimu za mitetemo za pande tatu ulikuwa umefikia kilomita za mraba 257.96 kati ya kilomita za mraba 736.3, sawa na asilimia 35. Aidha, katika Kitalu cha Ruvuma, PURA iliendelea kusimamia shughuli za uendelezaji wa gesi asilia, zikiwemo maandalizi ya uchimbaji wa kisima cha Chikumbi-1 (CH-1), ukarabati wa kisima cha Ntorya-1 (NT-1) na majaribio ya uzalishaji wa kisima cha Ntorya-2 (NT-2). Katika Kitalu cha Mnazi Bay, PURA ilisimamia uchimbaji wa visima vitatu vya gesi asilia katika mwaka wa fedha 2025/26, ambapo viwili vilikamilika na kuanza uzalishaji. Visima hivyo ni Mnazi Bay Five (MB-5) chenye uwezo wa kuzalisha wastani wa futi za ujazo milioni 40 za gesi kwa siku na Msimbati Two (MS-2) chenye uwezo wa kuzalisha wastani wa futi za ujazo milioni 50 kwa siku. Kisima cha tatu, Kasa-1X, kilikuwa cha utafutaji wa gesi asilia, ambapo kupitia uchimbaji wake kiasi cha futi za ujazo bilioni 223 za gesi asilia kiligundulika. Katika kuimarisha usimamizi wa mapato ya Serikali, PURA kupitia ukaguzi wa gharama na mapato katika mikataba ya Uzalishaji na Ugawanaji Mapato (PSA) iliwezesha kuokolewa na kurejeshwa kwa Dola za Marekani 3,306,678, sawa na Sh8,861,897,040, katika fungu la ugawanaji wa mapato kutoka kwa waendeshaji wa vitalu husika. Ukaguzi huo ulihusisha Kitalu cha Songo Songo kwa miaka ya 2023 na 2024, Vitalu Na. 1 na 4 kwa miaka ya 2023 na 2024 pamoja na Kitalu cha Ruvuma kwa mwaka 2024. Aidha, ukaguzi ulianza katika Kitalu cha Songo Songo kwa mwaka 2025 na Kitalu Na. 2 kwa mwaka 2023. Katika hatua nyingine, PURA imekamilisha uandaaji wa mfumo wa kuhifadhi kumbukumbu za hesabu za gharama na mapato ya utafutaji na uzalishaji wa mafuta na gesi asilia nchini, unaojulikana kama PURA Cost Recovery Management System (CRMS), ambao umerahisisha uwasilishaji na uhifadhi wa taarifa za mapato na gharama kutoka kwa kampuni zinazojihusisha na shughuli za mkondo wa juu wa petroli nchini. Katika kuongeza ushiriki wa Watanzania katika shughuli za mkondo wa juu wa petroli, thamani ya bidhaa na huduma zilizotolewa na kampuni za ndani ilikuwa zaidi ya Dola za Marekani milioni 30 mwaka 2026, ikilinganishwa na Dola milioni 14 mwaka 2025. PURA imesema itaendelea kuimarisha utendaji na usimamizi wa shughuli za mkondo wa juu wa petroli ili kuhakikisha sekta ya nishati inaendelea kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi, huku ikiimarisha ushirikiano na wadau mbalimbali, ikiwemo sekta binafsi, kwa ajili ya kuboresha upatikanaji wa gesi asilia kwa shughuli za kiuchumi na kijamii.
Mon, 23 Nov 2026 15:10:29 +0000Kiungani: Syokimau neighbourhood where staying exclusive pays
Read the full report from the original source.
RecentlyJumatatu ya Burudani Imefika
WIKENDI hii usikubali ikupite hivi hivi bila kufurahia burudani kwenye mechi za leo. Msako wa pointi 3 kama kawadia unaendelea huku baadhi ya wachezaji wakiendelea kupambania kupachika mabao. Ligi kuu ya Uingereza EPL itapigwa mechi moja kali kati ya Brentford dhidi ya Everton, ukitarajiw akuwa mchezo wa kukata na shoka kutokana na aina ya uchezaji ambao hutumia timu zote mbili. Mechi itapigwa pale Gtech Community kila timu ikitaka ushindi siku ya leo. Brentford wametoka kupoteza mechi yao liyopita, hivyo hii ni mechi ambayo wanaitazama kwa jicho lingine, wakati The Toffees wao wametoka kushinda mechi yao iliyopita kwa kishindo huku tofauti ya pointi kati yao ni 2 pekee. Je nani kushinda leo? Kivumbi kingine kitakuwa kule LALIGA ambapo Elche atakuwa ugenini kupepetana dhidi ya Levante ambao mpaka sasa wapo nafasi ya 18 huku wenyeji wao wakiwa nafasi ya 17, na tofauti yao ikiwa ni pointi 1 pekee hadi sasa. Yaani zinakutana timu mbili ambazo pointi 3 ni muhimu sana kwa kila mtu kutokana na nafasi walizpo kwenye msimamo wa ligi. Levante wanaingia kwenye mchezo huu wakitoka kupata sare tasa ya 0-0 dhidi ya Celta Vigo. Matokeo hayo yanaonyesha kuwa wanaweza kucheza kwa nidhamu katika safu ya ulinzi, lakini wanahitaji kuongeza makali kwenye eneo la ushambuliaji ili kutumia vizuri nafasi wanazopata. Elche wanakwenda kwenye mchezo huu wakitafuta kurejea kwenye ushindi baada ya kupoteza mabao 2-0 dhidi ya Real Betis. Wanahitaji kuboresha uimara wa safu yao ya ulinzi na kutumia vizuri nafasi za kushambulia. Takwimu zinaonesha kuwa msimu uliopita kwenye mechi mbili walizokutana kwenye ligi, kila mtu alishinda nyumbani kwake. Je historia inaweza ikajirudia?. Bila kusahau kuwa mechi hii unazipata kule Meridianbet ambapo pia unaweza ukapata taarifa za wachezaji ambao wanaweza kucheza na ambao ni majeruhi. SERIE A kule Italia kuendelea pia ambapo AC Monza atamenyana dhidi ya Fiorentina ambapo mchezo huu unatarajiw akuwa na ushindani mkubwa sana kutokana na hali za timu zote mbili, yaani wote wapo chini kwenye msimamo wa ligi. Wenyeji wanaingia kwenye mchezo huu nia yao ikiwa ni ushindi kwani mpaka sasa kwenye mechi 5 za mwisho wamepoteza 4 huku shida ikiwa ni safu yao ya ulinzi wakishinda kutumia nafasi pia. Wageni wao Fiorentina wao hawana ule mwendelezo mzuri wa matokeo chanya kwani wanawez akushinda, kutoa sare na kufungwa lakini baadhi ya mechi wamefanya vyema kutokana na kuwa na wachezaji wenye uwezo mkubwa akiwemo Mastantuono, Pellegrino na wengine wengi. Je nani kushinda leo?
Mon, 23 Nov 2026 10:00:00 +0000Maumivu bei mpya ya gesi
Soma hapa..
RecentlyPURA YAREJESHA SH8.86 BILIONI KUPITIA UKAGUZI WA GHARAMA ZA MAFUTA NA GESI
Na Karama Kenyunko, Michuzi TV MAMLAKA ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) imewezesha kuokolewa na kurejeshwa kwa Dola za Marekani milioni 3.3, sawa na Sh bilioni 8.86, katika fungu la ugawanaji wa mapato kupitia ukaguzi wa gharama na mapato ya kampuni zinazojihusisha na shughuli za utafutaji na uzalishaji wa mafuta na gesi asilia nchini. Akizungumza jana wakati akiwasilisha taarifa ya tathmini ya utekelezaji wa majukumu na mafanikio ya PURA kwa mwaka wa fedha 2025/26, katika kikao na wahariri na waandishi wa habari kilichoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina, Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, Charles Sangweni, alisema jumla ya Dola za Marekani 3,306,678, sawa na Sh8,861,897,040, ziliokolewa kupitia ukaguzi huo. Alisema PURA ilikamilisha ukaguzi wa gharama na mapato katika Kitalu cha Songo Songo kwa miaka ya 2023 na 2024, Vitalu Na. 1 na 4 kwa miaka ya 2023 na 2024, pamoja na Kitalu cha Ruvuma kwa mwaka 2024. Aidha, alisema mamlaka hiyo ilianza ukaguzi katika Kitalu cha Songo Songo kwa mwaka 2025 na Kitalu Na. 2 kwa mwaka 2023. Katika kuimarisha usimamizi wa taarifa za kifedha, Sangweni alisema PURA imekamilisha uandaaji wa mfumo wa kuhifadhi kumbukumbu za hesabu za gharama na mapato ya utafutaji na uzalishaji wa mafuta na gesi asilia nchini, unaojulikana kama PURA Cost Recovery Management System (CRMS). Alisema mfumo huo umerahisisha uwasilishaji na uhifadhi wa taarifa za mapato na gharama kutoka kwa kampuni zinazojihusisha na shughuli za mkondo wa juu wa petroli nchini. Katika hatua nyingine, alisema thamani ya bidhaa na huduma zilizotolewa na kampuni za ndani katika miradi ya mkondo wa juu wa petroli mwaka 2026 ilikuwa zaidi ya Dola za Marekani milioni 30, ikilinganishwa na Dola milioni 14 mwaka 2025. Aidha, PURA iliendelea kusimamia na kuhakikisha kampuni zinazofanya shughuli za utafutaji, uendelezaji na uzalishaji wa mafuta na gesi asilia nchini zinatekeleza programu na miradi ya Uwajibikaji wa Kampuni kwa Jamii (CSR), ikiwemo ujenzi wa Shule ya Msingi Likong’o katika Halmashauri ya Manispaa ya Lindi, ujenzi wa majiko ya kisasa ya kupikia kwa kutumia nishati ya LPG katika shule nne zilizopo Kata ya Msimbati, Mtwara, na ufadhili wa vijana kusoma masuala ya ufundi katika Chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) mkoani Lindi.
Mon, 23 Nov 2026 14:56:28 +0000Rosatom eyes Africa after synchronising nuclear project with Bangladesh’s national power grid
DHAKA, BANGLADESH: Unit 1 of Rooppur Nuclear Power Plant (NPP), a project executed by the Rosatom, has been successfully synchronised…
RecentlyTwo Health Centres Receive Ambulances as Lango MPs Call for Unity Beyond Party Politics
Read the full report from the original source.
RecentlyU Rwanda rushobora kubyaza imyanda ingufu rugendeye ku bunararibonye bwa Danemark
Read the full report from the original source.
RecentlyNBAA KUWAKUTANISHA WAHASIBU
Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) inatarajia kuwakutanisha Wahasibu, Wakaguzi na wadau mbalimbali wa Taaluma ya Uhasibu katika Mkutano Mkuu wa 39 wa Wahasibu 2026 utakaofanyika Novemba 24 hadi 27, 2026, jijini Dar es Salaam, kujadili mchango wa Taaluma ya Uhasibu katika kufanikisha Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050. Akizungumza na waandishi wa Habari, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) CPA Prof. Sylvia Temu amesema mkutano huo utajumuisha shughuli za kijamii na kitaaluma, ambapo Novemba 24, Bodi hiyo itakabidhi vifaa tiba kwa Hospitali ya Mwananyamala na Hospitali ya Taifa ya Rufaa ya Watoto ya CCBRT jijini Dar es Salaam. Amesema vifaa hivyo vimenunuliwa kupitia michango ya wahasibu mbalimbali waliojitokeza kuunga mkono juhudi za kuboresha huduma za afya nchini, akieleza kuwa hatua hiyo ni sehemu ya mchango wa wataalamu hao katika kusaidia jamii. Amesema mkutano rasmi utaanza Novemba 25 na kufunguliwa na Waziri wa Fedha, Balozi Hamisi Mussa Omar, huku mada kuu ikijikita katika mchango wa Wahasibu na Wakaguzi wa hesabu katika kufanikisha Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050. Ameeleza kuwa dira hiyo inalenga kuifanya Tanzania kuwa na uchumi wenye thamani ya dola trilioni moja za Marekani ifikapo mwaka 2050, huku pato la mtu mmoja mmoja likitarajiwa kufikia angalau dola 7,000. Pia inalenga kuimarisha elimu na uelewa wa matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) ili kuongeza uwezo wa wananchi kutumia na kuendeleza teknolojia katika shughuli za maendeleo. Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo, siku ya pili ya mkutano, Novemba 26, itajadili masuala mbalimbali ya kitaaluma pamoja na afya ya mwili na akili, uwiano kati ya kazi na maisha binafsi na umuhimu wa wataalamu kutenga muda kwa ajili ya familia zao. Washiriki pia watapata fursa ya kushiriki michezo mbalimbali na kupata elimu ya afya kutoka kwa wataalamu. Pia jioni ya tarehe 26 Novemba kutakuwa na hafla ya utoaji Tuzo kwa Taasisi za Umma, kampuni binafsi na Taasisi zisizo za kiserikali zilizofanya vizuri katika kuandaa taarifa bora za hesabu. Hafla hiyo itafanyika katika ukumbi wa mkutano wa APC Bunju jijini Dar es Salaam. Amesema mchakato wa kupata washindi wa Tuzo hizo una ushindani mkubwa na unazingatia usiri, huku tathmini ikifanywa na wataalamu huru wenye ujuzi na uzoefu katika Taaluma ya Uhasibu na uandaaji wa taarifa za hesabu. Ameongeza kuwa majina ya washindi yataendelea kuwa siri hadi wakati wa kutangazwa, akizihimiza Taasisi zote zilizoshiriki kuhudhuria hafla hiyo ili kushuhudia kutangazwa kwa washindi. Mkutano huo unatarajiwa kuwa jukwaa la kujadili mustakabali wa Taaluma ya Uhasibu nchini, kubadilishana uzoefu na kuimarisha mchango wa Wahasibu na Wakaguzi wa hesabu katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya taifa. Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NBAA CPA Prof. Sylvia Temu akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkutano mkuu wa 39 wa mwaka wa Wahasibu 2026 utakaofanyika katika ukumbi wa mkutano wa APC Bunju jijini Dar es Salaam.
Mon, 23 Nov 2026 14:53:02 +0000Page 50 of 1126 · 22503 stories