Unganishwa

Search the region

23365 stories

Uncategorized · TechCabal East Africa

Nigeria’s AI ambitions depend on building for local realities

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

Bayern-Ajax clash in Nairobi presents AFCON readiness test

Read the full report from the original source.

Recently
Business · Issa Michuzi

DED KIBAHA AAHIDI KUWAWEZESHA KIUCHUMI WANAWAKE WA UWT KUPITIA MIKOPO YA ASILIMIA 10

Na Victor Masangu, Kibaha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha, Walda Maulid, ameahidi kushirikiana na Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), Wilaya ya Kibaha Mjini, katika kuwawezesha kiuchumi kupitia fursa mbalimbali, ikiwemo mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri. Walda ameyasema hayo alipokuwa mgeni rasmi katika Baraza la Dharura la UWT Wilaya ya Kibaha Mjini, lililoandaliwa kujadili masuala mbalimbali ya jumuiya hiyo, pamoja na kumkaribisha rasmi mkurugenzi huyo mpya. Amesema mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri ni fursa muhimu kwa wanawake kujikwamua kiuchumi kwa kuanzisha na kuendeleza shughuli mbalimbali za ujasiriamali. “Nimefarijika sana kualikwa katika kikao hiki cha Baraza la UWT Wilaya ya Kibaha Mjini. Nitakuwa pamoja nanyi kuhakikisha mikopo inayotolewa inawafikia walengwa ili waweze kuanzisha biashara mbalimbali na kujikwamua kiuchumi,” amesema Walda. Aidha, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kumteua kushika nafasi hiyo, akiahidi kutekeleza majukumu yake kwa uadilifu na kuendelea kuwatumikia wananchi. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Kibaha Mjini, Elina Mgonja, amemshukuru mkurugenzi huyo kwa kuahidi kushirikiana na wanawake katika juhudi za kuwawezesha kiuchumi kupitia fursa za mikopo inayotolewa na halmashauri. Naye Katibu wa UWT Mkoa wa Pwani, Aziza Omary, amewahimiza wanawake kuachana na migogoro na mifarakano, badala yake washikamane na kuimarisha umoja wao kwa ajili ya maendeleo ya chama na jumuiya zake. Awali, Katibu wa UWT Wilaya ya Kibaha Mjini, Cesilia Ndalu, amesema amefurahishwa na utayari wa mkurugenzi huyo wa kushirikiana na wanawake katika kuleta maendeleo. Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Picha ya Ndege, Grace Jungulu, ameahidi kuendelea kushirikiana na mkurugenzi huyo mpya katika kuharakisha maendeleo ya wananchi wa maeneo mbalimbali ya manispaa hiyo. Baraza hilo la dharura limeenda sambamba na hafla fupi ya kumkaribisha rasmi Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha.

Sat, 31 Oct 2026 15:19:56 +0000
Uncategorized · Issa Michuzi

MDIME: SIMBA INAHITAJI VIONGOZI WENYE MAONO

Na Mwandishi Wetu, TANGA Wakati saa ya uchaguzi wa viongozi wa Klabu ya Simba ikianza kusogea, viongozi wa matawi ya klabu hiyo Mkoa wa Tanga wamefunguka na kutoa wito kwa wanachama kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali zilizotangazwa, wakisisitiza umuhimu wa kupata viongozi watakaosimamia maendeleo ya klabu hiyo kwa miaka minne ijayo. Mwenyekiti wa Matawi ya Simba Mkoa wa Tanga, Edgar Mdime, amesema wanachama wenye sifa na vigezo wanapaswa kutumia fursa hiyo kuchukua fomu, kuzijaza na kuzirejesha kwa wakati ili waweze kushiriki katika kinyang'anyiro cha kuwania nafasi za uongozi. Mdime amesema uongozi wa matawi mkoani humo umepokea taarifa rasmi iliyotolewa na Bodi ya Wakurugenzi ya Simba Sports Club kuhusu kuitishwa kwa Mkutano Mkuu wa klabu hiyo unaotarajiwa kufanyika Januari 3, 2027. Amesema Mkutano Mkuu huo ambao hufanyika mara moja kila baada ya miaka minne, ni sehemu muhimu ya mchakato wa kuamua mustakabali wa uongozi wa klabu, hivyo wanachama wanapaswa kuonyesha mwitikio kwa kujitokeza kushiriki katika mchakato huo. Akisisitiza msimamo wa uongozi wa matawi mkoani Tanga, Mdime amesema wanahitaji kuona wanachama wengi wenye nia njema na Simba wakijitokeza kuwania nafasi hizo ili klabu ipate viongozi watakaoshirikiana katika kuleta maboresho na kuendeleza mafanikio yake. Ameongeza kuwa uchaguzi huo ni fursa inayopatikana baada ya kipindi cha miaka minne, hivyo wanachama hawapaswi kuipuuza bali kuitumia kuchangia mustakabali wa klabu yao. AIGUSA TFF, BMT NA SERIKALI Katika hatua nyingine, Mdime amevitaka vyombo vinavyosimamia masuala ya michezo nchini, ikiwemo Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Baraza la Michezo la Taifa (BMT) pamoja na Serikali, kuhakikisha Mkutano Mkuu wa Simba unafanyika kwa kuzingatia sheria, kanuni na Katiba ya klabu hiyo. Amesema ni muhimu taratibu zote zinazohusu mkutano huo kufuatwa ili kuhakikisha mchakato mzima unakwenda kwa mujibu wa misingi inayotambuliwa na Katiba ya Simba. BAVUMA AUNGANA NA MDIME Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Matawi ya Simba Mkoa wa Tanga, Bavuma Jr, ameunga mkono wito huo kwa kuwataka wanachama wenye sifa kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali zilizotangazwa na klabu hiyo. Bavuma amesema Simba inahitaji viongozi watakaokuwa tayari kubeba majukumu ya kuiongoza klabu na kusukuma mbele gurudumu la maendeleo katika kipindi chote cha uongozi wao. Amesema kwa upande wao kama viongozi wa matawi, wataendelea kutekeleza wajibu wao kwa kushirikiana na makao makuu ili kuhakikisha klabu inapata mafanikio na kusonga mbele. Ameeleza kuwa ushirikiano kati ya viongozi wa matawi na uongozi wa makao makuu ni jambo muhimu katika kuimarisha klabu na kufanikisha malengo yake. Kwa ujumla, viongozi hao wa matawi ya Simba Mkoa wa Tanga wameeleza kuwa wanatarajia kuona wanachama wakitumia fursa ya uchaguzi huo kushiriki katika kuunda uongozi wa klabu kwa kipindi kingine cha miaka minne.

Sat, 31 Oct 2026 15:15:23 +0000
Uncategorized · PML Daily

Corporate firms urged to support Kampala cleaning drive

KAMPALA - Corporate companies have been urged to provide cleaning equipment and mobilise their employees to support the national cleaning day initiative, with officials warning that limited resources and public participa

Recently
Uncategorized · KBC

Morocco welcomes historic turning point for Moroccan Sahara

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Issa Michuzi

NGORONGORO KUTUMIA VYOMBO VYA HABARI KUTANGAZA UTALII KIMATAIFA

Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imesema itaendelea kushirikiana na vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo katika hifadhi hiyo ili kuvutia watalii wengi zaidi kutoka maeneo mbalimbali duniani. Akizungumza katika mkutano wa Waandishi wa Habari Vijijini, Afisa Uhifadhi Mkuu anayeshughulikia Uhusiano kwa Umma wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Kassim Nyaki, amesema vyombo vya habari vina mchango mkubwa katika kufikisha taarifa kwa watu wengi kwa wakati mmoja. Amesema mamlaka hiyo itaendelea kutumia fursa ya vyombo vya habari kuhakikisha wananchi wanapata taarifa kuhusu vivutio vya utalii vilivyopo Ngorongoro, sambamba na kuvitangaza katika masoko ya utalii ya kimataifa. Kwa upande wake, Afisa Utalii wa Ngorongoro, CO II Hillary Kimaro, amesema Ngorongoro ni kitovu cha maajabu mengi (Destination of Many Wonders), kutokana na kuwa na vivutio mbalimbali vinavyojumuisha wanyamapori, malikale na urithi wa utamaduni. Ameeleza kuwa eneo hilo la Urithi wa Dunia linatoa fursa ya kipekee kwa watalii kujionea maajabu ya asili, ikiwemo kuzaliwa kwa ndama na uhamaji wa nyumbu katika eneo la Ndutu. Naye Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Vijijini (RUJAT), Neville Meena, amelipongeza Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa kutambua na kuthamini mchango wa waandishi wa habari katika kutangaza vivutio vya utalii nchini. Amesema ushirikiano kati ya mamlaka hiyo na vyombo vya habari ni muhimu katika kuongeza uelewa kuhusu utalii wa Tanzania na kuvutia maelfu ya watalii kutoka sehemu mbalimbali za dunia.

Sat, 31 Oct 2026 15:10:59 +0000
Uncategorized · Rwanda News Agency

Rwanda to collaborate with Russia’s Rosatom in developing nuclear infrastructure

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Rwanda News Agency

EU Special Representative to the Great Lakes Region visited Rwanda

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Rwanda News Agency

EASF Logistics MAP Exercise concludes

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

Kenya fires back at Saudi Arabia over Ebola travel ban

Kenya has asked Riyadh to lift the restrictions, arguing that the outbreak is contained and there is no evidence of community transmission.

Recently
Uncategorized · Rwanda News Agency

MPs call for stronger measures to improve tontine management

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Ankole Times

MUSEVENI GIFTS COWS WORTH SHS10M TO NEWLYWEDS! President Praises Don Bwana’s Loyalty and Service to NRM

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Rwanda News Agency

President Kagame in Dakar for the Opening Ceremony of the 2026 Youth Olympic Games

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

Verstappen slams Red Bull stable-mate after clash

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

‘I’m soon going to be out’: Oburu gives health update

Oburu expressed gratitude to Kenyans who sent messages of sympathy and wished him a quick recovery during his illness.

Recently
Uncategorized · KBC

Duale faults Saudi Arabia’s Ebola travel ban, says Kenya needs support, not isolation

Health CS Aden Duale has described the move as excessive and unsupported by the current epidemiological situation in the country.

Recently
Uncategorized · Capital FM

Murkomen condemns heckling of Kalonzo at Sifuna’s party launch, invites him to join government

News · 5 hours ago

Recently
Business · Daily News

Can Tanzania’s youth turn Vision 2050 into jobs, businesses and a trillion-dollar economy by 2050?

RUVUMA: Tanzania’s ambition to build a US$1 trillion economy by 2050 will depend not only on government policies and investment…

Recently
Uncategorized · Daily News

Tanzania must protect girls online as firmly as it protects them in schools and communities

DAR ES SALAAM: Digital technology is opening new paths for girls and young women to learn, communicate, create businesses and…

Recently

Page 509 of 1169 · 23365 stories