Search the region
23371 stories
Benki ya Exim Tanzania Yaunga Mkono Uhifadhi wa Mazingira na Maendeleo ya Jamii Kilolo
Benki ya Exim Tanzania imeendelea kudhihirisha dhamira yake ya kushirikiana na jamii katika kuchochea maendeleo endelevu kupitia udhamini wake Mkuu wa Kitonga Marathon 2026, mbio zilizolenga kuhamasisha uhifadhi wa mazingira na kutangaza fursa mbalimbali za kiuchumi zilizopo katika Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa. Mbio hizo zilizofanyika chini ya kaulimbiu “Tunza Mazingira, Wekeza Kilolo” ziliwakutanisha washiriki na wadau mbalimbali kwa lengo la kuhamasisha utunzaji wa mazingira, ushiriki wa jamii na kuangazia fursa za maendeleo zilizopo wilayani humo, ikiwemo katika sekta za kilimo, utalii na biashara za wenyeji. Kama Mdhamini Mkuu, Benki ya Exim iliunga mkono mbio hizo kama sehemu ya dhamira yake pana ya kushirikiana na jamii na wadau katika masuala yanayochangia maendeleo endelevu. Akizungumzia udhamini huo, Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Exim Tanzania, Stanley Kafu, alisema udhamini huo unaakisi imani ya Benki kwamba jukumu lake haliishii katika kutoa huduma za kifedha pekee, bali linajumuisha pia kuunga mkono mipango inayowaunganisha wadau katika kutekeleza vipaumbele vya pamoja vya maendeleo. “Mbio za Kitonga zinatoa fursa ya kuitangaza zaidi Kilolo na uwezo wake wa kiuchumi, huku zikihamasisha uwajibikaji wa pamoja katika uhifadhi wa mazingira. Sisi Exim Bank tunaamini kuwa maendeleo endelevu yanahitaji ushirikiano kati ya jamii, wafanyabiashara na wadau wengine. Udhamini wetu wa mbio hizi unaakisi dhamira yetu ya kushirikiana na jamii tunazozihudumia na kuchangia juhudi zinazolenga kuleta maendeleo katika maeneo yao,” alisema Kafu. Udhamini huo ni sehemu ya jitihada za Benki ya Exim Tanzania za kuchangia maendeleo ya jamii kupitia mpango wake wa uwajibikaji kwa jamii, Exim Cares. Kupitia mpango huo, Benki inaunga mkono shughuli mbalimbali zinazolenga kuboresha maisha ya jamii katika sekta za afya, elimu, uhifadhi wa mazingira, ubunifu na elimu ya masuala ya fedha. Mwaka 2026, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 29 tangu kuanzishwa kwake, Benki ya Exim ilifanya shughuli za usafi katika jamii zinazozunguka matawi yake nchini. Mkoani Iringa, timu ya tawi la Benki hiyo ilikabidhi vifaa vya usafi katika Hospitali ya Wilaya ya FLERIMO ili kusaidia kuboresha usafi katika hospitali hiyo. Benki ya Exim Tanzania ilifungua tawi lake mkoani Iringa mwaka 2009. Tawi hilo hutoa huduma za kifedha kwa watu binafsi, wafanyabiashara, kampuni na taasisi, kulingana na mahitaji yao. Ushiriki wa tawi hilo katika Mbio za Kitonga unaonyesha namna Benki inavyoendelea kushirikiana na jamii inayohudumia pamoja na wadau wengine katika kuunga mkono mipango inayochangia maendeleo ya mkoa huo. Kupitia Tawi lake la Iringa, Benki ya Exim Tanzania inaendelea kuwahudumia watu binafsi, wafanyabiashara na kampuni kwa kuwapatia huduma mbalimbali za kifedha. Wakazi na wamiliki wa biashara mkoani humo wanaweza kutembelea tawi hilo kupata maelezo kuhusu bidhaa na huduma za Benki, pamoja na ushauri kuhusu huduma zinazoweza kukidhi mahitaji yao ya kifedha.
Sat, 31 Oct 2026 08:00:00 +0000DKT. MWIGULU AREJEA NCHINI AKITOKEA URUSI
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amerejea nchini leo, Oktoba 31, 2026, akitokea Moscow, Urusi, ambako alimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Mkutano wa Tatu wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Afrika na Urusi, uliofanyika Oktoba 28–29, 2026. Mkutano huo ulilenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia, ushirikiano wa kiuchumi na biashara, pamoja na kupanua fursa za ushirikiano katika sekta mbalimbali kati ya Urusi na nchi za Afrika.
Sat, 31 Oct 2026 12:21:07 +0000MPs DECLARE WAR ON BALAAM! Alebtong Legislators Threaten Impeachment Over Arrests and Interdictions Ahead of November Visit
Read the full report from the original source.
RecentlyJaji Mwambegele Awasisitiza Makarani Uchaguzi Nonde Kuzingatia Sheria
Read the full report from the original source.
RecentlyNew Peasants Party Secretary General Sets Release of Political Prisoners as Condition for Government Talks
Read the full report from the original source.
RecentlyArsenal boss Arteta fires 'Disneyland' warning at Dowman after Fleetwood red card
Read the full report from the original source.
RecentlyMurkomen to Kalonzo after heckling: You are welcome in government
Murkomen said the Wiper leader deserved respect and invited him to work with the broad-based government.
RecentlyMvua ya mawe yabomoa nyumba zaidi ya 70 Kigoma, wananchi wakosa makazi
Zaidi ya nyumba 70 za makazi pamoja na makanisa mawili zimeezuliwa na kubomolewa na mvua ya mawe iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Kigoma Ujiji, na...
RecentlyQue font les forces militaires dans les écoles iraniennes ?
Les autorités iraniennes expliquent que ces programmes s'inscrivent dans le cadre de l'éducation patriotique, de la défense nationale et de la formation d'une génération conforme aux principes de la révolution du pays.
RecentlyKenya, Russia wakubaliana kusitisha uandikishaji Wakenya jeshini
Rais wa Russia, Vladimir Putin, amekubaliana na Rais wa Kenya, William Ruto, kusitisha uandikishaji wa raia wa Kenya katika jeshi la Russia, huku serikali ya Nairobi ikianza kufuatilia fidia kwa...
RecentlyJournalists Trained on Responsible Election Reporting Ahead of 2027 Polls
Latest · 2027 KENYA ELECTIONS
RecentlyWhy North Korea's 'elite' hackers are suspect in major Binance hack
If the accusations are true, the record-making heist shows how powerful suspected North Korean hackers have become.
RecentlyUganda’s Agricultural Credit Facility Hits UGX1.52 Trillion, but Who Gets the Money?
Read the full report from the original source.
RecentlyDriver escapes as police intercept vehicle ferrying 282kg of suspected bhang in Kisumu
Latest · County News
RecentlyRed Bull Wings Cup taps into Kenya’s growing E-sports scene
Read the full report from the original source.
RecentlyRD Congo: Abarenga 5000 bamaze kwicwa na Ebola ya kabiri yishe abantu benshi ku isi
Nubwo ibikorwa byo kurwanya Ebola bikomeje, umutekano mucye mu bice byo mu burasirazuba bw'igihugu byibasiwe n'iki cyorezo watumye akazi k'abakozi bo mu rwego rw'ubuzima kagorana.
Recently12 drivers arrested as NTSA intensifies road safety checks
8 of the 12 drivers were driving under the influence of alcohol.
RecentlyHow to clear an earwax blockage
If directed by healthcare guidelines, warm water can be used to gently soften any loosened wax.
RecentlyGermany news: Merkel calls for first female president
Read the full report from the original source.
RecentlyCinema, cocktails and conversation as Kwiso Movie Nights returns
Cinema lovers had another reason to step away from their usual Friday routines on October 30, as Kwiso Movie Nights returned with an evening that brought together film, cocktails and conversation...
RecentlyPage 512 of 1169 · 23371 stories