Search the region
23445 stories
MAKAMU WA RAIS AMFARIJI IGP WAMBURA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius John Ndejembi, amemtembelea na kumfariji Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Camillus Wambura, kufuatia kifo cha baba yake mzazi, marehemu Deusdedit Mwita Wambura. Mzee Deusdedit Wambura alifariki dunia Oktoba 24, 2026, jijini Dar es Salaam. Makamu wa Rais ametoa salamu za pole kwa familia hiyo alipoitembelea katika makazi ya IGP Camillus Wambura, yaliyopo Masaki, jijini Dar es Salaam.
Wed, 28 Oct 2026 07:40:44 +0000CRDB nine-month profit up 29pc
CRDB Bank Group’s profit after tax rose 29.1 per cent to 672.07bn/- in the nine months to September, driven by…
RecentlyThrough strengthening screening services, early cancer detection can save lives
ZANZIBAR: THE fear of discovering cancer can be enough to keep many people away from a health facility. Others may…
RecentlyUkerewe expands loans to empowerment groups
MWANZA: UKEREWE District Council has disbursed 351m/- in loans to 35 groups of women, youth and persons with disabilities, strengthening…
RecentlyUgandan, Sudanese photographers among FOTEA 2026 award winners
KAMPALA, Uganda — A project following Sudanese refugees in Uganda and a series on evictions in Kampala are among the winning entries in this year's awards by the Foundation for East...
RecentlyIs Uganda ready for the Gen Z labour force?
Imagine a young employee completing a report electronically, only to be told to print it, sign it, scan it and email it back. Somewhere between…
RecentlyStudents acquire practical skills under youth empowerment programme
ARUSHA: SIXTY-SIX students from Mswakini Secondary School in Monduli District, Arusha Region, have completed a youth empowerment programme designed to…
RecentlyRock City Mall pays shareholders 1.19bn/- dividend
DODOMA: MWANZA Rock City Company Limited (MRC), owner of Rock City Mall, has paid dividends totalling 1.189bn/- to its three…
RecentlyKilimanjaro RC urges residents to secure health cover
KILIMANJARO: THE Kilimanjaro Regional Commissioner (RC), Nurdin Babu has urged residents to enrol in the Universal Health Coverage (UHC) scheme,…
RecentlyPPRA: Framework deals open for e-journal purchases
DODOMA: LIBRARIES and other public institutions can buy online journals and other electronic learning resources through framework agreements of one…
RecentlyWAHITIMU WA MZUMBE MBEYA KUWA CHACHU YA MABADILIKO KATIKA JAMII
Wahitimu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Ndaki ya Mbeya, wametakiwa kutumia elimu na ujuzi walioupata chuoni kuleta mabadiliko chanya katika jamii kwa kuzingatia utu, uadilifu na maadili ya Kitanzania, huku wakitumia ubunifu na uthubutu kutafuta suluhisho la changamoto zinazowazunguka. Mwito huo umetolewa na Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais Mstaafu wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mstaafu na Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, wakati wa Mahafali ya 25 ya chuo hicho yaliyofanyika katika Ndaki ya Mbeya, mkoani Mbeya. Dkt. Shein amewasisitiza wahitimu hao kutumia maarifa na ujuzi walioupata kwa manufaa ya jamii, akieleza umuhimu wa kujitofautisha kupitia matendo yanayoonesha utu, uadilifu, kuheshimu wengine na kuzingatia maadili ya Kitanzania. Amesisitiza kuwa elimu inapaswa kuwa nyenzo ya kuboresha maisha ya watu na kuchangia maendeleo ya Taifa. Kwa upande wake, Mlau wa Mahafali, Prof. Elizabeth Lulu Genda, amewataka wahitimu kukabiliana na changamoto za maisha kwa uvumilivu, ubunifu na uthubutu badala ya kulaumu Serikali, mifumo au jamii wanapokutana na vikwazo. Prof. Genda amesema ukosefu wa ajira, mitaji, urasimu na uhaba wa fursa ni miongoni mwa changamoto ambazo wahitimu wanaweza kukutana nazo wanaporejea katika jamii, hivyo wanapaswa kutafuta mbinu sahihi za kuzivuka badala ya kukata tamaa. “Msipoteze muda na rasilimali zenu kugombana na mambo yatakayowakinga katika safari ya maisha. Chunguzeni kwa makini na kutafuta namna ya kuvuka vikwazo hivyo,” alisisitiza Prof. Genda. Naye Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha, amewataka wahitimu kutumia elimu yao kwa uadilifu, ubunifu na bidii ili kuanzisha shughuli za uzalishaji mali, kutengeneza fursa na kuchangia maendeleo ya Taifa. Prof. Mwegoha pia amewahimiza wahitimu kudumisha uhusiano na chuo chao kwa kushirikiana, kushauriana na kusaidia wanafunzi kupata fursa za ajira na ujasiriamali, akisisitiza kuwa mtandao wa wahitimu unaweza kuunganisha maarifa, uzoefu na fursa kwa manufaa ya wahitimu wenyewe, chuo na jamii kwa ujumla. Katika mahafali hayo, jumla ya wahitimu 1,212, wakiwemo wanaume 587 na wanawake 625, wametunukiwa tuzo za kitaaluma katika ngazi za Shahada ya Umahiri, Shahada ya Awali, Stashahada na Astashahada. Naye, mhitimu bora wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Mbeya, Ndg. Lugano Mwapongo amewataka wahitimu kutumia maarifa waliopata chuoni hapo kuleta maendeleo katika jamii. Aidha, ameeleza kuwa ni mwiko kukata tamaa hivyo wahitimu na wanafunzi waendelee kuweka juhudi zenye kuleta mafanikio. Mahafali hayo yanaweka bayana kuwa thamani ya elimu haipo katika vyeti pekee, bali pia katika uwezo wa wahitimu kutumia maarifa yao kutatua changamoto, kufungua fursa na kuboresha maisha ya watu. Kwa wahitimu hao, hatua inayofuata ni kuyageuza maarifa waliyoyapata chuoni kuwa matokeo yanayoonekana katika jamii na maendeleo ya Taifa.
Wed, 28 Oct 2026 07:17:17 +0000KITWIMA YOUTH GROUP, SHAMBA DARASA KWA VIJANA KUCHANGAMKIA FURSA ZA UCHUMI
NA: DK. REUBENI LUMBAGALA Serikali ina vipaumbele vingi vya maendeleo kwa ajili ya watu wake. Miongoni mwao ni uwezeshaji wananchi kiuchumi. Hapa serikali huweka mazingira rafiki na wezeshi kwa ajili ya kuhakikisha wananchi wanatumia fursa mbalimbali za kiuchumi zilizopo ili kujiongezea kipato na kuchangia maendeleo ya nchi. Katika juhudi za maendeleo, kundi la vijana ni muhimu kuwezeshwa ili nao washiriki kikamilifu katika maendeleo. Vijana wana nguvu na maarifa ya kuweza kuzalisha na hatimaye kubadili hali zao za maisha kutoka hali duni na kuwa nzuri zaidi. Ni kundi ambalo likiwezeshwa, maendeleo yatasonga mbele kwa haraka zaidi. Kutokana na umuhimu wa kundi la vijana katika maendeleo, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ameanzisha wizara maalum ya kushughulikia masuala ya vijana - Ofisi ya Rais - Maendeleo ya Vijana chini ya uongozi wa Waziri wake, Joel Nanauka. Wizara hii hajachanganywa na sekta nyingine yeyote, imebaki kushughulikia masuala ya maendeleo ya vijana. Basi. Huu ni upekee wa aina yake kutokana na dhamira ya serikali ya kuhakikisha kundi la vijana linakamata fursa muhimu za uchumi kwa maendeleo. Katika kuhakikisha uwezeshaji vijana kiuchumi haubaki kuwa mpango wa kwenye makaratasi tu, serikali ikaweka katika vitendo kwa kutoa shilingi bilioni 200 ili zikopeshwe kwa vijana bila riba. Fedha hizi zikawekewa utaratibu kwa vijana katika vikundi waungane na watume maombi na kwa wale watakaokidhi vigezo watakopeshwa. Kikundi cha vijana cha Kitwima yaani Kitwima Youth Group (KYG) ni miongoni mwa wanufaika wa mkopo wa shilingi bilioni 200 zilizokopeshwa na vijana nchi nzima. Kikundi hiki ni cha vijana wasomi ambapo wamejikita katika ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba, katika Ziwa Viktoria, mkoani Mwanza. Ni kwamba, kikundi hiki kilipata mkopo wa shilingi milioni 106.9, mwezi Machi, 2026. Baada ya kupokea fedha hizo, walinunua vifaranga vya samaki 60,000 kwa shilingi milioni tisa, wakaongezwa vifaranga 6,000 na kufanya vifaranga vya samaki kufika 66,000. Vilevile, walitengeneza keji kwa shilingi milioni 35, wakanunua mtumbwi, chakula cha samaki na majaketi ya kuwasaidia katika shughuli zao za uvuvi (life jackets). Ndani ya miezi saba ya shughuli hiyo (Machi - Oktoba, 2026) wameweza kuzalisha samaki tani 15 aina ya Sato ambao mauzo yake yana thamani ya shilingi milioni 127.5. Kimsingi, kikundi hiki kimeonyesha uthubutu mkubwa na kimetoa darasa kwa vijana wenzao katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu, kuchangamkia fursa za uchumi zinazoratibiwa na serikali. Kupitia mradi huu, vijana hao wamejihakikishia kipato kupitia mauzo ya samaki pindi wanapowavuna. Pengine sana, kupitia mafanikio ya kikundi cha Kitwima, vijana waongeze ari ya kufuatilia mikopo inayotokewa na Wizara ya Vijana na Wizara nyingine ili vijana waweze kubadili maisha yao kwa kujiajiri wenyewe. Aidha, waliopewa dhamana ya kushughulikia mikopo ya vijana watende haki, waondoe urasimu ili vijana wanufaike na fursa hizo muhimu kwa maendeleo endelevu. Maoni : 0620 800 462.
Wed, 28 Oct 2026 07:19:30 +0000AAYC, NIMD Explore Strategic Partnership to Advance Youth Leadership, Democracy and Peacebuilding
The Afro-Arab Youth Council (AAYC) and the Netherlands Institute for Multiparty Democracy (NIMD) are exploring opportunities for strategic collaboration to strengthen youth leadership, democratic participation, peacebuil
RecentlyTBS warns traders ahead of new energyefficiency rules
DAR ES SALAAM: THE Tanzania Bureau of Standards (TBS) will begin enforcing mandatory energy-efficiency standards for electrical appliances in November…
RecentlyCashew sales generate over 300bn/- in two weeks
MTWARA: MORE than 100,000 tonnes of raw cashew nuts have been sold in the country so far during the 2026/2027…
RecentlyMuseveni Proposes Muhoozi as Successor at NRM CEC Meeting
Read the full report from the original source.
RecentlyFreedom of worship shouldn’t turn into freedom of exploitation
I wanted to avoid the ongoing debacle on pastors and fake miracles until I read about Kenyan pastor Paul Mackenzie, who was convicted for starving…
RecentlyHow Mackenzie sustained doomsday teachings behind bars
Prison searches uncovered mobile phones, SIM cards and a notebook containing telephone numbers, exposing the alleged network of unauthorised communication.
RecentlyBusia family seeks justice after man suffers multiple fractures during therapy
Read the full report from the original source.
RecentlyFormer Machakos County official among 11 suspects in Ksh.283M cemetery land scandal
Read the full report from the original source.
RecentlyPage 592 of 1173 · 23445 stories