Search the region
23416 stories
TPDC : Tunapima mafanikio ya miradi ya mafuta na gesi kwa manufaa kwa wananchi
Read the full report from the original source.
RecentlyAI company Anthropic files its IPO in hopes of raising $100 billion
Read the full report from the original source.
RecentlyUganda pitches ‘Beach to Bush’ tourism link with Kenyan coast
KAMPALA - Uganda is promoting a joint "Beach to Bush, Bush to Beach" tourism circuit with Kenya's coast. The plan would let visitors combine Indian Ocean holidays with Uganda's wildlife and...
RecentlyMAONO YA RAIS DKT.SAMIA YA KUONGEZA VIWANDA VIPYA KUINUA UCHUMI YATIMIA,WAZIRI KAPINGA AZINDUA KIWANDA KIPYA.
📌 Ni kiwanda cha vinywaji baridi cha Simba beverages Limited kilichopo Kibaha mkoa wa Pwani; 📌 Asifu uwekezaji mkubwa bilioni 28 wa kiwanda hicho sambamba na asilimia 90 ya ajira za wazawa; 📌 Serikali yasisitiza uzalishaji wa bidhaa bora na salama, matumizi ya malighafi za ndani, uhamishaji wa teknolojia na uongezaji wa ajira kwa Watanzania. KIBAHA, PWANI Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga (Mb), ameipongeza kampuni ya Simba Beverages Limited kwa uwekezaji wa takribani Shilingi bilioni 28 katika sekta ya viwanda nchini, akieleza kuwa uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za kuimarisha uchumi kupitia uzalishaji wa bidhaa nchini, kuongeza ajira na kupanua wigo wa mapato ya Serikali. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kiwanda hicho kilichopo katika eneo la viwanda la Zegereni, Kibaha, mkoani Pwani, Waziri Kapinga amesema,Serikali inaendelea kutekeleza maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan ya kufungua viwanda vipya nchini na kuvutia uwekezaji wa viwanda vipya ili kuchochea ukuaji wa uchumi na kuongeza fursa za ajira kwa Watanzania. Amesema sekta ya vinywaji baridi ni miongoni mwa sekta muhimu katika kukuza uchumi wa viwanda kutokana na mchango wake katika uzalishaji, ajira na uwekezaji, pamoja na kuunganisha shughuli nyingine za kiuchumi zikiwemo kilimo, usindikaji na usambazaji wa bidhaa. Amesisitiza kuwa maendeleo ya sekta hiyo yanapaswa kwenda sambamba na matumizi ya malighafi zinazopatikana nchini ili kuongeza thamani ya rasilimali za ndani na kunufaisha wazalishaji wa Kitanzania. Waziri Kapinga ameeleza kuwa Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji, huku akiwataka wawekezaji kuhakikisha bidhaa zinazozalishwa nchini zinazingatia sheria, kanuni na viwango vya ubora na usalama. Amesisitiza pia umuhimu wa kulinda wafanyakazi na kuboresha mazingira ya kazi ili kuimarisha ushindani wa bidhaa za Tanzania katika masoko ya ndani na nje ya nchi. Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Mhe. Fadhili Nkurlu, amesema idadi ya viwanda katika Mkoa wa Pwani imeongezeka kutoka viwanda 387 katika kipindi cha mwaka 2021/2022 hadi kufikia viwanda 768 kufikia Septemba 2026. Alieleza kuwa viwanda hivyo vinajumuisha viwanda vikubwa 33, vya kati 33, vidogo 248 na vidogo zaidi 454. Ameongeza kuwa viwanda vikubwa na vya kati 38 vilikuwa katika hatua za ujenzi ila sasa vimekamilika, vikiwemo viwanda vikubwa 27 na vya kati 11, huku viwanda vingine 99 vikiwa katika hatua mbalimbali za ujenzi na maandalizi. Aidha, alisema viwanda 35 vilivyopo katika maeneo ya uwekezaji mkoani humo vimechangia kuzalisha ajira za moja kwa moja 2,357 na ajira nyingine zisizo rasmi 6,062 zinazotokana na shughuli za kiuchumi zinazohusiana na viwanda hivyo. Mhe. Nkurlu amesema Mkoa wa Pwani unaendelea kuweka kipaumbele katika kuvutia uwekezaji wa viwanda vipya, kuongeza ajira kwa vijana, kuhamasisha matumizi ya malighafi zinazopatikana nchini na kusimamia ubora na usalama wa bidhaa zinazozalishwa. Ameeleza kuwa uwekezaji wa Simba Beverages Limited ni sehemu ya juhudi za kujenga uchumi imara na wenye ushindani kupitia sekta ya viwanda. Kwa upande wake, Afisa mkuu wa fedha Surya Murthy, Afisa Mkuu wa Fedha (CFO) wa Simba Beverages Limited, ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na viongozi wa Mkoa wa Pwani na Wilaya ya Kibaha kwa ushirikiano wao katika kuwezesha uwekezaji huo. Ameeleza kuwa uzinduzi wa kiwanda hicho ni hatua muhimu katika kuendeleza shughuli za uzalishaji nchini, kuongeza thamani ya bidhaa na kuimarisha minyororo ya ugavi, huku kampuni ikiendelea kutekeleza dhamira yake kupitia kaulimbiu ya “Imezaliwa Tanzania, Inatumikia Afrika.” Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa katika hafla hiyo, Simba Beverages Limited imewekeza katika uzalishaji wa vinywaji baridi vyenye gesi pamoja na vifungashio vya plastiki. Mitambo ya kiwanda hicho ina uwezo wa kuzalisha chupa 12,000 za vinywaji baridi kwa saa, huku kampuni ikitarajia kuzalisha ajira za moja kwa moja 100 na ajira nyingine 200 zisizo za moja kwa moja kadri shughuli zake zitakavyopanuka. Aidha, kampuni hiyo imeeleza kuwa inatumia zaidi ya asilimia 90 ya malighafi zinazopatikana nchini, hatua inayochangia kuimarisha mnyororo wa thamani wa uzalishaji wa ndani. Kampuni pia inalenga kuongeza mauzo yake hadi Sh bilioni 15.4 ifikapo mwaka 2027 na Sh bilioni 33 ifikapo mwaka 2030, kwa mujibu wa taarifa zilizowasilishwa katika uzinduzi huo. Uwekezaji wa Simba Beverages Limited unaonesha nafasi ya sekta binafsi katika kuendeleza viwanda nchini, kuongeza ajira na kuimarisha uchumi unaotegemea uzalishaji wa bidhaa na matumizi ya rasilimali zinazopatikana ndani ya nchi. Serikali inaendelea kuhimiza wawekezaji kutumia malighafi za ndani, kuongeza thamani ya bidhaa, kuhamisha teknolojia na kuhakikisha Watanzania wananufaika na fursa zinazotokana na maendeleo ya sekta ya viwanda.
Mon, 26 Oct 2026 14:30:00 +0000Israeli President Herzog receives credentials from Rwanda’s New Ambassador
Read the full report from the original source.
RecentlyCrime thriller Hit Point premieres on M-Net
DStv is bringing a new British crime thriller, Hit Point, to South African audiences, with the six-part series premiering on M-Net (DStv Channel 102) today,…
RecentlyFarmers ditch family loans for banks, sacco borrowing
Read the full report from the original source.
RecentlyWAZIRI KAPINGA AZINDUA KIWANDA KIPYA CHA SIMBA BEVERAGES LIMITED
*Ni kiwanda cha vinywaji baridi kilichopo Kibaha mkoa wa Pwani; *Asifu uwekezaji mkubwa bilioni 28 wa kiwanda hicho, ajira kwa wazawa asilimia 90 Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Pwani WAZIRI wa Viwanda na Biashara Judith Kapinga ameipongeza kampuni ya Simba Beverages Limited kwa uwekezaji wa takribani Sh.bilioni 28 katika sekta ya viwanda na uwekezajo huo ni sehemu ya juhudi za kuimarisha uchumi kupitia uzalishaji wa bidhaa nchini. Ametoa pongezi hizo alipokuwa akizindua kiwanda hicho kilichopo katika eneo la viwanda la Zegereni wilayani Kibaha mkoani Pwani ambapo ameeleza pia Serikali inaendelea kutekeleza maelekezo ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ya kufungua viwanda vipya nchini na kuvutia uwekezaji wa viwanda vipya ili kuchochea ukuaji wa uchumi na kuongeza fursa za ajira kwa Watanzania. “Sekta ya vinywaji baridi ni miongoni mwa sekta muhimu katika kukuza uchumi wa viwanda kutokana na mchango wake katika uzalishaji, ajira na uwekezaji, pamoja na kuunganisha shughuli nyingine za kiuchumi zikiwemo kilimo, usindikaji na usambazaji wa bidhaa.” Waziri Kapinga amesema maendeleo ya sekta hiyo yanapaswa kwenda sambamba na matumizi ya malighafi zinazopatikana nchini ili kuongeza thamani ya rasilimali za ndani na kunufaisha wazalishaji wa Kitanzania. Pia amesema Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji, huku akiwataka wawekezaji kuhakikisha bidhaa zinazozalishwa nchini zinazingatia sheria, kanuni na viwango vya ubora na usalama. Awali Ofisa Mkuu wa Fedha Surya Murthy, Afisa Mkuu wa Fedha (CFO) wa Simba Beverages Limited, ametoa Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na viongozi wa Mkoa wa Pwani kwa ushirikiano wao katika kuwezesha uwekezaji huo. “Uzinduzi wa kiwanda hiki ni hatua muhimu katika kuendeleza shughuli za uzalishaji nchini, kuongeza thamani ya bidhaa na kuimarisha minyororo ya ugavi, huku kampuni ikiendelea kutekeleza dhamira yake kupitia kaulimbiu ya “Imezaliwa Tanzania, Inatumikia Afrika.” Amefafanua pia Simba Beverages Limited imewekeza katika uzalishaji wa vinywaji baridi vyenye gesi pamoja na vifungashio vya plastiki. Mitambo ya kiwanda hicho ina uwezo wa kuzalisha chupa 12,000 za vinywaji baridi kwa saa.Kampuni inatarajia kuzalisha ajira za moja kwa moja 100 na ajira nyingine 200 zisizo za moja kwa moja kadri shughuli zake zitakavyopanuka. Aidha zaidi ya asilimia 90 ya malighafi zinazotumika katika kutengeneza bidhaa katika kampuni hiyo zinazopatikana nchini hatua inayochangia kuimarisha mnyororo wa thamani wa uzalishaji wa ndani. “Kampuni pia inalenga kuongeza mauzo yake hadi Sh bilioni 15.4 ifikapo mwaka 2027 na Sh bilioni 33 ifikapo mwaka 2030, kwa mujibu wa taarifa zilizowasilishwa katika uzinduzi huo.” Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Fadhili Nkurlu, amesema idadi ya viwanda katika Mkoa wa Pwani imeongezeka kutoka viwanda 387 katika kipindi cha mwaka 2021/2022 hadi kufikia viwanda 768 kufikia Septemba 2026. Alieleza kuwa viwanda hivyo vinajumuisha viwanda vikubwa 33, vya kati 33, vidogo 248 na vidogo zaidi 454. Ameongeza viwanda vikubwa na vya kati 38 vilikuwa katika hatua za ujenzi ila sasa vimekamilika, vikiwemo viwanda vikubwa 27 na vya kati 11, huku viwanda vingine 99 vikiwa katika hatua mbalimbali za ujenzi na maandalizi. Pia amesema viwanda 35 vilivyopo katika maeneo ya uwekezaji mkoani humo vimechangia kuzalisha ajira za moja kwa moja 2,357 na ajira nyingine zisizo rasmi 6,062 zinazotokana na shughuli za kiuchumi zinazohusiana na viwanda hivyo. “Mkoa wa Pwani unaendelea kuweka kipaumbele katika kuvutia uwekezaji wa viwanda vipya, kuongeza ajira kwa vijana, kuhamasisha matumizi ya malighafi zinazopatikana nchini na kusimamia ubora na usalama wa bidhaa zinazozalishwa.” Pia amesema kwa mujibu wa takwimu ya mwaka 2021 hadi 2022 viwanda 1387 vimejengwa na kufikia Septemba 2026 vimejengwa viwanda 1768.Viwanda 99 vingine vinajengwa na kwamba Mkoa wa Pwani lenye ukubwa wa Hekta 148000 likiwa na kongani 35. Wakati huo huo Mkurugenzi wa TanTrade, Ephraim Mafuru amesema uwekezaji uliofanywa na Simba Beverages ni mchango mkubwa wa Pato la Taifa huku akitoa mwito kwa wawekezaji ili waweze kutambulika watumie nembo ya uzalishaji ya Tanzania. Kwa upande wake Mkurugenzi wa Sera, Utafiti na utetezi wa TPSF Mwanahamis Hussein alipongeza hatua hiyo ya uwekezaji kwa sababu imeongeza soko la ajira na kuleta ushindani wa kiuchumi.Pia ameupongeza Mkoa wa Pwani kwa kutenga maeneo kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda.
Mon, 26 Oct 2026 18:15:45 +0000Focus RDC : la RDC et l'Allemagne misent sur la diplomatie
Read the full report from the original source.
RecentlyContre la Russie à tout prix : l‘Ukraine et les Touaregs du Mali
Read the full report from the original source.
RecentlyMAKUTUPORA YAZALISHA ZAIDI YA LITA MILIONI 61 ZA MAJI KWA SIKU DODOMA
Na Janeth Raphael - MichuziTv Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) imesema chanzo cha maji cha Makutupora kina mchango mkubwa katika upatikanaji wa huduma ya maji jijini Dodoma, kikizalisha zaidi ya nusu ya maji yote yanayozalishwa na mamlaka hiyo kwa siku. Akizungumza na waandishi wa habari Oktoba 26, 2026, jijini Dodoma, Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA, Mhandisi Aron Joseph, amesema chanzo hicho ni nguzo muhimu katika kukidhi mahitaji ya maji kwa wakazi wa jiji hilo, kutokana na uwezo wake mkubwa wa uzalishaji ikilinganishwa na vyanzo vingine vinavyotumiwa na mamlaka hiyo. Amesema kwa sasa mahitaji ya maji jijini Dodoma yanafikia lita milioni 159.9 kwa siku, huku DUWASA ikiwa na uwezo wa kuzalisha lita milioni 91 pekee kwa siku, hali inayoonesha kuwepo kwa pengo kubwa kati ya mahitaji ya wananchi na maji yanayopatikana. Mhandisi Joseph amesema chanzo cha Makutupora huzalisha lita milioni 61.5 kwa siku, huku kiasi kingine cha maji kikitokana na vyanzo mbalimbali vidogo vilivyosambaa katika maeneo tofauti ya jiji, ikiwemo Nzuguni, Iyumbu, Nala, Ihumwa, Nkuhungu, Miganga, Mkonze na Makulu. Ameeleza kuwa licha ya mchango wa vyanzo hivyo, upatikanaji wa maji bado unaathiriwa na uhaba wa vyanzo vya uzalishaji. Kwa sasa, DUWASA ina visima 72 vinavyofanya kazi katika maeneo mbalimbali, vikiwemo visima 17 vilivyopo Makutupora ambavyo vinachangia kwa kiasi kikubwa uzalishaji wa maji jijini humo. Katika kukabiliana na hali hiyo, Mhandisi Joseph amesema mamlaka hiyo imeweka mpango wa miaka mitano unaolenga kuongeza uwezo wa uzalishaji wa maji kutoka lita milioni 91 hadi lita milioni 121 kwa siku, hatua inayotarajiwa kupunguza pengo kati ya maji yanayozalishwa na mahitaji ya wananchi. Amesisitiza kuwa utekelezaji wa mpango huo ni sehemu ya juhudi za kuboresha upatikanaji wa maji safi na salama kwa wakazi wa Dodoma, sambamba na kukabiliana na ongezeko la mahitaji linalotokana na kukua kwa jiji na kuongezeka kwa idadi ya watumiaji wa huduma hiyo.
Mon, 26 Oct 2026 18:08:03 +0000MADIWANI SIMANJIRO WALALAMIKIA MIGODI KUTOTEKELEZA CSR
Na Mwandishi Wetu, Mirerani MADIWANI wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro, mkoani Manyara, wameilalamikia Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kuhusu migodi mingi ya madini ya Tanzanite kutotekeleza ipasavyo miradi ya Uwajibikaji kwa Kampuni kwa Jamii (CSR) na kulipa tozo za huduma kwa jamii (Service Levy). Wametoa malalamiko hayo mbele ya kamati hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti wake, Subira Mgalu, ilipotembelea machimbo ya madini ya Tanzanite katika mji mdogo wa Mirerani. Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Kaleiya Melita Mollel, amesema wamiliki wengi wa migodi ya Tanzanite hawachangii ipasavyo maendeleo ya jamii kupitia CSR na tozo za huduma, licha ya wajibu huo kuwepo kisheria. Amesema ni kampuni chache tu zinazoshiriki katika shughuli hizo, akizitaja Franone, Chusa Mining, God Charity na kampuni zinazohusishwa na bilionea Laizer kuwa miongoni mwa zinazochangia maendeleo ya jamii. “Ni kampuni chache zinazotekeleza CSR au kulipa Service Levy, jambo ambalo lipo kisheria, lakini kampuni nyingi zimekuwa zikisuasua,” amesema Mollel. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya na Maji ya Halmashauri hiyo, Albert Msole, amesema kampuni nyingi za uchimbaji hazina mwitikio wa kutosha katika kuchangia maendeleo ya halmashauri, licha ya suala hilo kuwa na msingi wa kisheria. Amesema halmashauri imekuwa ikibeba mzigo wa kulea na kusomesha baadhi ya watoto yatima ambao wazazi wao walifariki dunia baada ya kuugua magonjwa ya kifua yaliyohusishwa na mazingira ya kazi migodini. “Suala la kampuni za uchimbaji kuchangia CSR limekuwa likichukuliwa kama hisani, japokuwa lipo kisheria. Ni kampuni chache tu zilizotajwa na mwenyekiti ndizo zinazochangia,” amesema Msole. Akizungumzia suala hilo, Naibu Waziri wa Madini, Steven Lemomo Kiruswa, amesema kampuni za uchimbaji zinapaswa kuzingatia wajibu wa kuchangia miradi ya CSR kwa mujibu wa sheria. Amesema hata katika Mkoa wa Geita, ambako utekelezaji wa CSR unaonekana kufanya vizuri, bado wabunge wamekuwa wakilalamikia kiwango cha fedha zinazotolewa, wakitaka kiongezwe. “Hata kule Geita, ambako CSR inafanya vizuri, bado wabunge wanalalamikia kiwango kinachotolewa kuwa ni kidogo, hivyo kinapaswa kuongezwa,” amesema Kiruswa. Naye Kamishna wa Madini, Dkt. Abdurahman Mwanga, amesema utekelezaji wa CSR ni wajibu wa kisheria kwa kampuni za uchimbaji, akibainisha kuwa suala hilo limeainishwa katika Kifungu cha 105 cha sheria husika. Amesema halmashauri zinapaswa kuweka mwongozo utakaosaidia kusimamia utekelezaji wa wajibu huo na kuhakikisha jamii zinazozunguka migodi zinanufaika na shughuli za uchimbaji. Kuhusu tozo ya huduma kwa jamii (Service Levy), Dkt. Mwanga amesema kampuni zinapaswa kulipa kwa mujibu wa masharti ya sheria, akitaja kiwango cha asilimia 0.3 ya mauzo ghafi kwa mwaka kwa kampuni zinazohusika katika eneo la Simanjiro.
Mon, 26 Oct 2026 18:10:07 +0000Bishops apologise for 'exploited' Trump meet
Two Catholic bishops in the US have said they regret meeting President Donald Trump at the White House, after images of them praying with him
Recently50 Years of Impact: Top PR Agencies and Communicators Crowned at 10th PRAU Excellence Awards
Read the full report from the original source.
RecentlyMultiChoice cuts DStv prices in bid to win back subscribers
Read the full report from the original source.
RecentlyUganda Urges Predictable Funding for African Peace Operations
Read the full report from the original source.
RecentlyOpen letter to President Museveni: PDM funds used to pay medical bills in Ankole
Your Excellency, Research from the Greater Ankole subregion shows a clear and troubling pattern; many beneficiaries of the Parish Development Model (PDM) are using the…
RecentlyDay 4 of rescue operations at Eastleigh building
The multi-storey building, which was under construction, collapsed along 9th Street on Friday, October 23, prompting a search-and-rescue operation
RecentlyVidéo — Thérèse Kayikwamba Wagner : "Je vois une RDC jeune et ambitieuse"
Read the full report from the original source.
RecentlyPearl Bank Wins Inaugural PR Crown Jewel Accolade at 10th PRAU Excellence Awards
Read the full report from the original source.
RecentlyPage 621 of 1171 · 23416 stories