Unganishwa

Search the region

23409 stories

Uncategorized · The Star Kenya

Chris Brown avoids prison time for nightclub attack

The United States R&B star was given an eight-month prison sentence, suspended for 12 months, over the attack in on February 19, 2023.

Recently
Uncategorized · Issa Michuzi

Vodacom Tanzania yaendelea kukuza Golf nchini, Paul Chidale aibuka kinara Vodacom Tanzania Open 2026

Mkurugenzi wa Vodacom Business, Nguvu Kamando (kulia) akimkabidhi mshindi kutoka Malawi Paul Chidale, tuzo baada ya kutwaa ubingwa wa Vodacom Tanzania Open 2026 jijini Arusha, Chidale alimaliza mashindano hayo kwa mikwaju 289 na kujinyakulia Sh9.35 milioni, akifuatiwa na Mtanzania Nuru Mollel aliyeshika nafasi ya pili kwa mikwaju 293 na Robinson Owiti kutoka Kenya aliyemaliza wa tatu kwa mikwaju 294. Rais wa chama cha Golf nchini (Tanzania Golf Union - TGU) Gilman Kasiga, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mchango wa Vodacom Tanzania Open katika kukuza ushindani na kuendeleza mchezo wa golf nchini, wakati wa mashindano hayo yaliyofanyika Kili Golf Course jijini Arusha, Oktoba 22 hadi 25, 2026. Mashindano hayo yaliwakutanisha wachezaji kutoka Tanzania na nchi mbalimbali wakishindania zawadi za jumla ya Sh40 milioni. Mkuu wa Idara ya Masoko na Uwezeshaji wa Vodacom Tanzania Plc, Joseph Sayi, akishiriki mchezo wa gofu wakati wa mashindano ya Vodacom Tanzania Open 2026 yaliyofanyika jijini Arusha. Katika mashindano hayo, mchezaji kutoka Malawi, Paul Chidale, aliibuka mshindi na kujinyakulia Sh9.35 milioni baada ya kumaliza kwa mikwaju 289, akiwashinda Nuru Mollel wa Tanzania na Robinson Owiti wa Kenya. Mkurugenzi wa Vodacom Business, Nguvu Kamando (kulia) akimkabidhi mchezaji golf kutoka Malawi, Paul Chidale, mfano wa hundi ya Sh9.35 milioni baada ya kutwaa ubingwa wa Vodacom Tanzania Open 2026 jijini Arusha. Chidale alimaliza mashindano hayo ya siku nne kwa jumla ya mikwaju 289, akimzidi Mtanzania Nuru Mollel aliyeshika nafasi ya pili kwa mikwaju 293 na Robinson Owiti kutoka Kenya aliyemaliza nafasi ya tatu kwa mikwaju 294. Baadhi ya washiriki na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania Plc wakiwa kwenye mazoezi wakati wa mashindano ya Vodacom Tanzania Open 2026 yaliyofanyika jijini Arusha katika viwanja vya Kili Golf Club jijini Arusha. Mashindano hayo ya siku nne yaliwakutanisha wachezaji kutoka Tanzania na nchi nyingine mbalimbali, wakishindania zawadi za jumla ya Sh40 milioni. Mkurugenzi wa Vodacom Business, Nguvu Kamando, akishiriki mchezo wa gofu wakati wa mashindano ya Vodacom Tanzania Open 2026 yaliyofanyika katika viwanja vya Kili Golf Club jijini Arusha, Oktoba 22–25, 2026. Mashindano hayo yaliofanyika kwa siku nne yaliwakutanisha wachezaji wa gofu kutoka Tanzania na nchi nyingine, huku jumla ya zawadi za Sh40 milioni zikitolewa kwa washindi. Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania PLC na wadau mbalimbali, wakiongozwa na Mkurugenzi wa Vodacom Business, Nguvu Kamando (wa nne kulia), wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa kilele cha mashindano ya Vodacom Tanzania Open 2026 yaliyofanyika jijini Arusha. Mashindano hayo yaliwashirikisha wachezaji kutoka Tanzania na nchi nyingine, yakiwa sehemu ya mchango wa Vodacom katika kukuza mchezo wa gofu, kuendeleza vipaji na kuimarisha ushindani wa mchezo wa gofu nchini.

Mon, 26 Oct 2026 05:30:00 +0000
Uncategorized · Burundi Forum

Burundi – Histoire : 13 commissaires de la CVR prêtent serment pour quatre ans, sur fond de mémoire coloniale

13 membres de la Commission vérité et réconciliation (CVR) ont prêté serment, lundi 26 octobre 2026, devant  S.E. le Président Ndayishimiye Evariste et le Parlement burundais réuni en Congrès. Leur nouveau mandat de quatre ans s’inscrit dans la recherche de la vérité...

Mon, 26 Oct 2026 13:20:58 +0000
National · Issa Michuzi

MBUNGE MNZAVA ATATUA KERO YA MAJI,WANANCHI WAMSHANGILIA DKT.SAMIA

Na Mwandishi Wetu, Korogwe WANANCHI wa Kijiji cha Vuje, kilichopo Kata ya Bungu Korogwe Vijijini, wameingia kwenye furaha kubwa baada ya kushuhudia mkandarasi akabidhiwa rasmi mradi wa maji wa shilingi milioni 107.65 utakaokomesha adha ya ukosefu wa huduma hiyo iliyodumu kwa zaidi ya miongo mitano tangu kuanzishwa kwake mnamo mwaka 1972. Akizungumza kwa niaba ya wananchi katika hafla hiyo ya kihistoria iliyovuta hisia za wengi, Mwenyekiti wa Kijiji cha Vuje, Muhammad Dhahabu, alieleza namna jamii ilivyoteseka kwa muda mrefu kusaka maji na kupoteza imani kutokana na ahadi za mara kwa mara zilizokosa utekelezaji, akimshukuru Mbunge wa Jimbo, Timotheo Mnzava, kwa kuwatendea haki. Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Bungu, Stephen Mdoe, licha ya kuishukuru serikali kwa uamuzi huo wa kishujaa, aliwasilisha kilio cha wananchi kuhusiana na uhaba wa maeneo ya kilimo kufuatia mashamba ya chai yaliyozunguka kijiji hicho kutelekezwa na wakulima kupigwa marufuku kuyatumia kwa mazao ya muda mfupi kama mahindi na magimbi. Akiweka wazi takwimu za mradi huo, Meneja wa RUWASA Wilaya ya Korogwe, Muharami K. Mohamedi, alieleza kuwa mradi huo unatekelezwa na kampuni ya kizalendo ya Amani Civil and Water Works, ukilenga kuwanufaisha wakazi 1,297 kupitia ukarabati wa banio huko Sakale, matanki ya maji, na ulazaji wa mabomba yenye urefu wa kilomita 4.5 kwa kipindi cha miezi mitatu. Akihutubia kwa niaba ya Mbunge Mnzava, mwakilishi wake Shebila Idd — ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira — alimpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha zilizowawezesha wakazi wa Vuje kulala kwa amani, huku wananchi wakicheza na kuimba nyimbo za kumsifu kiongozi huyo mkuu wa nchi. "Rais Samia amedhihirisha kuwa yeye ni daktari wa kutatua na kutibu changamoto mbalimbali zinazotukabili sisi wananchi, hakika ni mama msikivu sana," alisema Shebila. Shebila aliwataka wananchi wa Korogwe kuendelea kumlinda na kumuunga mkono Mbunge Mnzava, akisisitiza kuwa amefanya makubwa yaliyowashinda watangulizi wake katika sekta za maji, umeme, barabara, afya na elimu, jambo linalofanya jimbo hilo kupiga hatua kubwa za maendeleo. "Mheshimiwa Mnzava ni mbunge tunatakiwa tumlinde, asituponyoke, tumuunge mkono, kazi zetu tunazomtuma anazifanya, waliomtangulia hawakuwa na Kasi kama yake," alisema Shebila. Akizungumza kwa njia ya simu na wananchi hao, Mbunge Timotheo Mnzava alisisitiza kuwa utekelezaji wa mradi huo ni uthibitisho tosha wa namna Serikali ya Awamu ya Sita inavyotatua kero za wananchi kwa vitendo. "Leo (Oktoba 25, 2026), tumefanya jambo kubwa na la kipekee kukabidhi mradi huu wa maji, tumshukuru sana mhe Rais kwa anajali matatizo ya wananchi wake," alisema. Mnzava alisema alipofika katika Kijiji hicho alipopewa kero ya maji hakuwa akipata usingizi na anamshukuru Rais kumpatia fedha ambazo zimeweza kutimiza ahadi yake. Mnzava alisema kuwa utekelezaji wa mradi huo ni wa pamoja na diwani na Mwenyekiti wa Kijiji hicho ambaye alikuwa akifuatilia kuona fedha zinapatikana ili wananchi waondokane na kero hiyo. Mbunge huyo aliwataka wakazi wa Vuje kushirikiana kwa karibu na mkandarasi ili kazi ikamilike kwa ubora uliokusudiwa.

Mon, 26 Oct 2026 13:17:18 +0000
Uncategorized · Issa Michuzi

MITA ZA MAJI ZAIDI YA 100 ZAIBIWA DODOMA NDANI YA MIEZI MITATU

Na Janeth Raphael - MichuziTv Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), Mhandisi Aron Joseph, amesema wizi wa mita za maji ni miongoni mwa changamoto kubwa zinazoikabili mamlaka hiyo, baada ya zaidi ya mita 100 kuibwa ndani ya kipindi cha miezi mitatu. Amesema takwimu za DUWASA zinaonesha kuwa vitendo hivyo vinaendelea kuwa changamoto katika usimamizi wa huduma za maji, huku baadhi ya vifaa vinavyoibwa vikidaiwa kutumika kwa shughuli nyingine zisizohusiana na matumizi yake ya awali. Mhandisi Joseph, ameyazungumza hayo leo jijini Dodoma katika Mkutano na waandishi wa habari ambapo amesema ufuatiliaji uliofanywa umebaini kuwa baadhi ya mita hizo hutumika kutengeneza bangili, huku nyingine zikiishia kuuzwa kama vyuma chakavu. Hali hiyo inaibua wasiwasi kuhusu uharibifu wa vifaa vinavyotumika katika utoaji wa huduma muhimu kwa wananchi. Katika kukabiliana na changamoto hiyo, DUWASA imekubaliana na baadhi ya wateja kufunga mita za maji ndani ya nyumba au katika maeneo yenye ulinzi, ikiwa ni hatua ya kupunguza uwezekano wa vifaa hivyo kuibwa. Hatua hiyo inalenga kuhakikisha mita zinakuwa salama huku mamlaka ikiendelea kutoa huduma kwa wateja wake. Hata hivyo, Mhandisi Joseph amesema utaratibu wa kufunga mita ndani ya nyumba nao una changamoto zake, hasa pale watumishi wa DUWASA wanapohitaji kuingia katika maeneo ya wateja kwa ajili ya kufanya usomaji wa mita. Amesema baadhi ya wananchi hawatoi ushirikiano unaohitajika, hali inayowapa watumishi hao wakati mgumu katika kutekeleza majukumu yao. Ameeleza kuwa katika baadhi ya matukio, watumishi wanaofika kufanya usomaji wa mita hukumbana na mazingira yasiyo rafiki, ikiwemo kufunguliwa mbwa, jambo linaloweza kuwazuia kutekeleza majukumu yao kwa urahisi. Kutokana na hali hiyo, ushirikiano wa wananchi unahitajika katika kulinda mita za maji, kurahisisha usomaji wake na kuimarisha utoaji wa huduma. DUWASA inaendelea kukabiliwa na jukumu la kuhakikisha vifaa hivyo vinalindwa dhidi ya wizi huku wananchi wakitakiwa kutoa ushirikiano kwa watumishi wake.

Mon, 26 Oct 2026 13:20:46 +0000
Sports · Mwanaspoti

Mwagala ageuka jinamizi kwa Yanga

Soma zaidi hapa

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

17Th Oct 2026 Part 3

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

Episode 11 (22Nd Oct 2026)

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

Disconnect Reconnect

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

An Encounter With Messiah

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

Gũthathaũra Matirũka Ma 2024 Mwĩhoko Wa 2025 Na Rigathi Gachagua

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

President Moi 'The Professor Of Politics'

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

Raila: Home and Away

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

Man arrested after confessing to killing wife and employer in Siaya

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Mwanaspoti

Aucho alivyogoma kurudi nyumbani, gari lake halirudi nyuma

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Capital FM

High Court fast-tracks petition challenging SRC pay regulations

Latest · Business

Recently
Uncategorized · Daily News

66 students benefit from multi-sectoral YEM training

MONDULI: A new Youth Empowerment Program is rolling out in Monduli District, Arusha Region, where students are being practically trained…

Recently
Uncategorized · Business Daily

Kenya flags ‘exploitative’ carbon-trade schemes

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · PML Daily

brainchild Burson’s Lynn Nasirumbi wins PRAU Rising Star award

KAMPALA — Lynn Nasirumbi, a Senior PR Executive at brainchild Burson, has won the PR Rising Star award at the 10th Public Relations Association of Uganda (PRAU) Excellence Awards, years after...

Recently
Uncategorized · Watchdog Uganda

‘Practice what you preach,’ Bishop Egesa urges MPs

The Bishop of Bukedi Diocese, Rt. Rev. George Egesa has urged Members of Parliament to lead with integrity, promote justice and serve vulnerable Ugandans. Delivering a sermon during the 12th…

Recently

Page 626 of 1171 · 23409 stories