Search the region
23362 stories
Tororo Leaders Raise Concern Over Delayed Release of Government Funds
Read the full report from the original source.
RecentlyTumwebaze Calls for More Research to Increase Coffee and Cocoa Production
Read the full report from the original source.
RecentlyWaziri wa Nishati akabidhi magari ya Zimamoto na TANESCO Namtumbo
Read the full report from the original source.
RecentlyMSHIKEMSHIKE 22/10/2026 - AZAM TV
Tazama kipindi cha Mshikemshike kikiwa na habari kemkem za michezo ikiwemo maandalizi ya Simba, Yanga, Azam FC kuelekea mechi zao zinazofuata.
2026-10-23T07:26:53+00:00Kocha Yanga aichambua TRA United kuelekea mchezo wao NBC Premier League
TRA UNITED vs YANGA: “Ni lazima nikiri kwamba tunacheza na timu nzuri sana” Kocha wa Yanga SC, Manqoba Mngqithi amesema Kocha Hemed Suleima Ali ‘Morocco’ wa TRA United, amefanya kazi nzuri ya kuitengeneza timu yake na inavutia. Manqoba ameendelea na utaratibu wake wa kuwachambua wapinzani kwa kutaja majina ya wachezaji na hata namba za jezi zao. Kocha huyo amesema wamejeruhiwa na mashabiki wanapaswa kwenda uwanjani kwa kiwango kikubwa ili kuhakikisha timu inakaa katika nafasi nzuri. Manqoba anasema hawakuwa na mchezo mzuri dhidi ya Simba SC na hilo hawezi kudanganya na kwamba waliadhibiwa kutokana na makosa yao. Kwa upande wake golikipa Hussein Masalanga anasema wao kwa sasa hawaangalii yaliyopita kwasababu wakiwekeza huko, watatoka kwenye malengo yao. Ni mechi ya NBC Premier League na itapigwa saa 10:00 jioni LIVE #AzamSports1HD #TRAUnitedVsYanga
2026-10-23T12:38:58+00:00Waziri Mkuu Dkt. Nchemba alipia tiketi zote kuiona Singida BS dhidi ya Tusker FC
SINGIDA BS vs TUSKER FC: “Mechi hii haitokuwa na kiingilio kwa mashabiki wote” Ofisa Habari na Mawasiliano wa Singida BS, Hussein Massanza anasema mlezi wa timu hiyo Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba amelipia tiketi zote ili Watanzania wakaitazame mechi ya mkondo wa pili ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Tusker ya Kenya. Massanza anasema wazo hilo lilianzia kwake Waziri Mkuu kwa kuishauri klabu na katika kutia nguvu wazo lake, akaamua kununua tiketi zote. Mechi hiyo itapigwa Jumapili Oktoba 25, 2026 katika dimba la Azam Complex, Chamazi, saa 1:00 usiku na itakuwa LIVE #AzamSports1HD #CAFCC #KombeLaShirikishoAfrika
2026-10-23T12:43:12+00:00TRA United yajipanga kukabiliana na Yanga iliyojeruhiwa
TRA UNITED vs YANGA: “Yanga wamepoteza mechi yao ya mwisho waliyocheza” Kocha wa TRA United, Hemed Suleiman ‘Morocco’ amesema wapinzani wao Yanga SC, watahitaji kujiweka katika mazingira mazuri baada ya kupoteza mechi ya #KariakooDerby iliyopigwa Oktoba 10, 2026. Morocco anasema wanajua kwamba hawapo katika nafasi nzuri msimu huu na ndio maana wanajipanga kuhakikisha wanapata matokeo kesho Oktoba 24, 2026. Ni mechi ya NBC Premier League na itapigwa saa 10:00 jioni LIVE #AzamSports1HD #TRAUnitedVsYanga
2026-10-23T12:48:08+00:00Polisi Tanzania 1-1 Pamba Jiji | Magoli I NBC Premier League - 23/10/2026
#NBCPL: Tazama namna FVS ilivyofanya kazi na kuzipatia magoli timu zote mbili kwa njia ya penati. Goli la Pamba Jiji limefungwa na Nathanael Ndwangou huku goli la Polisi Tanzania likifungwa na Anuari Jabir. FT: Polisi Tanzania 1-1 Pamba Jiji #NBCPremierLeague #LigiKuuYaNBC #NBCPL #NBCPLUpdates #ImenogaZaidi #PolisiTanzaniaVsPambaJiji #PolisiTanzania #PambaJiji #PLSPMB
2026-10-23T15:51:06+00:00Kocha JKT Tanzania asifu uwezo wa Kocha Cedric Kaze
JKT TANZANIA vs KAGERA SUGAR: Kocha wa JKT Tanzania, Ahmad Ally amesifu uwezo wa Kocha Cedric Kaze wa Kagera Sugar na kuongeza kuwa kwa sasa vijana hao kutoka mkoani Kagera, wameimarika kwa kiwango kikubwa. Kocha huyo anasema wanapaswa kuwa bora ili mechi hiyo waweze kuiweka katika himaya yao. Kwa upande wake mchezaji Ally Msengi anasema mabadiliko ya benchi la ufundi kwa wapinzani wao Kagera Sugar, yameifanya ibadilike kwenye mtindo wa uchezaji wao. Mechi hiyo ni ya NBC Premier League na itapigwa kesho Oktoba 24, 2026 saa 12:00 usiku. #NBCPremierLeague #LigiKuuYaNBC #NBCPL #NBCPLUpdates #ImenogaZaidi
2026-10-23T16:42:55+00:00Kocha Cedric Kaze asema kikosi chake kinaimarika siku hadi siku
JKT TANZANIA vs KAGERA SUGAR: “Tumekuwa na kiwango kizuri katika mechi mbili zilizopita” Kocha wa Kagera Sugar, Cedric Kaze anasema nafasi waliyopo sasa kwenye msimamo wa NBC Premier League ni swala la muda tu na watafanya jitihada ili kujiimarisha. Kwa upande wake mchezaji Erick Emmanuel anaamini kwamba kesho watakuwa na mchezo mzuri dhidi ya mpinzani wao JKT Tanzania. Mechi hiyo ni ya NBC Premier League na itapigwa kesho Oktoba 24, 2026 saa 12:00 usiku. #NBCPremierLeague #LigiKuuYaNBC #NBCPL #NBCPLUpdates #ImenogaZaidi
2026-10-23T17:05:42+00:00Polisi Tanzania 1-1 Pamba Jiji | Neno kutoka kwa makocha baada ya mechi
#NBCPL: “Tulistahili kushinda” Kocha wa Polisi Tanzania, Mbwana Makata anasema changamoto waliyonayo ni kuzifanyia kazi nafasi wanazozitengeneza. Kwa upande wake Kocha Fransic Baraza wa Pamba Jiji amewapongeza wachezaji wake kwa namna walivyojituma na kuzuia vema lango lao kiasi ambacho wamefanikiwa kuondoka na alama moja, japo walikuwa pungufu kutokana na kadi nyekundu. FT: Polisi Tanzania 1-1 Pamba Jiji #NBCPremierLeague #LigiKuuYaNBC #NBCPL #NBCPLUpdates #ImenogaZaidi #PolisiTanzaniaVsPambaJiji #PolisiTanzania #PambaJiji #PLSPMB
2026-10-23T17:44:31+00:00Mashabiki Yanga wasema wanachukuliwa poa baada ya kufungwa na Simba
MASHABIKI YANGA: “Watoto wanaleta dharau” Mmoja wa mashabiki wa Yanga SC, Amir Dazi anasema baada ya kupoteza kwenye mchezo wa #KariakooDerby dhidi ya mtani wao Simba SC, kumekuwa na dharau kwa baadhi ya watu na kesho Oktoba 24, 2026 watashinda zaidi ya magoli matatu dhidi ya TRA United. Yanga kesho itakuwa ugenini dhidi ya TRA United kwenye mchezo wa NBC Premier League saa 10:00 jioni LIVE #AzamSports1HD #YangaSC
2026-10-23T18:49:42+00:00Mashabiki Simba sasahivi ni full kujiamini mtaani
MASHABIKI SIMBA: “Doumbia mpira anajua” Mmoja wa mashabiki wa Simba SC, Munoi Imunu anasema maneno ya watu ndio yanafanya nyota wao Ibrahim Doumbia aonekane hajui mpira. Mashabiki hao wanaamini Jumapili ya Oktoba 25, 2026 lazima wapate magoli 10 kwenye mchezo wa mkondo wa pili wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya 15 de Agosto. #SimbaSC
2026-10-23T18:57:55+00:00MSHIKEMSHIKE 23/10/2026 - AZAMTV
Tazama kipindi cha Mshikemshike kikiwa na habari kemkem za michezo ikiwemo maneno ya makocha TRA United dhidi ya Yanga SC.
2026-10-24T04:18:02+00:00KURASA ZA MWISHO | Wikiendi ya Moto inaanza leo, Yanga, Azam kibaruani...
Wachambuzi wa shusha nondo, Jabir Juma, Charles Abel, Philip Nkini, Khatimu Naheka kuelekea michezo ya Ligi Kuu ya NBC ambapo leo Yanga SC itakuwa ugenini dhidi ya TRA United. Mchezo mwingine ni Azam FC vs ZED FC Kombe la Shirikisho Afrika.
2026-10-24T06:45:14+00:00WEDNESDAY NIGHT LIVE | Nahodha wa Dar City, Amini Mkosa aja na ndoo, baada ya ubingwa
Mahojiano maalum na Mchezaji bora wa mpira wa kikapu nchini, Amini Mkosa. Mwenyeji wake ni mtangazaji Patrick Nyembera.
2026-10-24T09:25:01+00:00NYAVUNI | 22/10/2026 | Magoli 10 bora na 'saves' kali Ligi Kuu ya NBC 2026/2027.
Magoli ya Libase Gueye, Khleffin Hamdoun na Gradi Kiala ndiyo yamechukua nafasi tatu za juu. Goli nambari moja linatoka kwa Libase Gueye akiiongoza Simba SC ikiichapa Mashujaa Magoli 6 -1. Upande wa saves kali, kinara ni ya golikipa wa Mashujaa FC, Mussa Malika katika mchezo dhidi ya Simba SC. Mkali wetu wa wiki ni Khleffin Hamdoun wa Dodoma Jiji. Usikose #Nyavuni kila Alhamisi saa 4:00 usiku #AzamSports1HD
2026-10-24T09:58:23+00:00CAFCC | Nani kuondoka na alama tatu Azam Complex? Ni Azam FC au ZED FC?
CAFCC | ''Ni burudani nyingine kutoka Azam Complex'', @van_msumi ameanza namna hii kwenye uchambuzi kuelekea mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika unaowakutanisha wenyeji Azam FC wakiwaalika ZED FC ya Misri. Wachambuzi wake ni @abissay_stephen na @jabir_aziz Mechi ni saa 10:00 jioni na itakuwa LIVE #AzamSports2HD ✍ @rajjmsangi #CAFCC #KombeLaShirikishoAfrika #CAFConfederationCup #AzamFC #ZEDFC
2026-10-24T12:22:11+00:00Audio — Journal 17 h TU (23.10.2026)
To play this audio please enable JavaScript, and consider upgrading to a web browser that supports HTML5 video
RecentlyAprès un premier cas d'Ebola au Nigeria, les pays voisins en alerte
Read the full report from the original source.
RecentlyPage 662 of 1169 · 23362 stories