Search the region
23329 stories
TASAF ILIVYOWEZESHA UFUGAJI SAMAKI WA VIZIMBA KWA KAYA MASKINI KATIKA MANISPAA YA ILEMELA
-Wanufaika wamshukuru Rais Dk.Samia kwa kuwajengea uwezo kiuchumi Na Mwandishi Wetu, Ilemela MRADI wa ufugaji samaki kwa njia ya vizimba katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, mkoani Mwanza, umeendelea kufungua fursa za kiuchumi kwa kaya zenye kipato duni, kuwaongezea kipato walengwa na kuwasaidia kujikwamua dhidi ya umaskini. Mradi huo unaotekelezwa na wanachama wa vikundi vya Maligana Kasafu na Temeke, vilivyopo Mtaa wa Kae Ndogo, Kata ya Kigongo, unawawezesha walengwa kutumia fursa ya uwepo wa Ziwa Victoria kuendesha shughuli za uzalishaji mali na kuboresha maisha yao. Akizungumza kuhusu mradi huo, Mratibu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii(TASAF) katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela David Macha amesema vikundi hivyo vilibuni wazo la kufuga samaki kwa njia ya vizimba baada ya kutambua kuwa mazingira yao ya kuishi karibu na ziwa ni fursa muhimu inayoweza kutumika kuongeza kipato. Amesema awamu ya kwanza, vikundi hivyo vilipatiwa Sh milioni 34 kupitia TASAF, fedha zilizotumika kutengeneza vizimba viwili, kununua vifaranga vya samaki na chakula kwa ajili ya kuendesha shughuli za ufugaji. Amefafanua baada ya kuanza ufugaji, vikundi hivyo vilifanikiwa kuvuna samaki na kupata mapato ya takribani Sh milioni 27, mafanikio yaliyowapa motisha ya kuendelea na mradi huo ili kuongeza kipato na kuimarisha shughuli zao za kiuchumi. “Baada ya mavuno, wanachama waliamua kuendeleza uwekezaji katika ufugaji wa samaki kwa kutumia sehemu ya fedha zilizopatikana, huku kiasi kingine kikitumika kusaidia shughuli nyingine za wanachama, ikiwemo kukopeshana kwa ajili ya mahitaji na shughuli za kujipatia kipato.” Pia amesema ufugaji samaki kwa njia ya vizimba ni fursa inayoweza kusaidia kuongeza upatikanaji wa samaki katika mazingira ambayo yamekuwa yakikabiliwa na changamoto ya upungufu wa samaki, huku ukiwawezesha walengwa kujenga msingi wa kujitegemea kiuchumi. Amefafanua TASAF imekuwa ikisaidia kaya zenye hali duni kupitia shughuli mbalimbali za uzalishaji mali, zikiwemo ufugaji na kilimo cha bustani, kwa lengo la kuongeza kipato cha kaya na kuboresha ustawi wa jamii. Amebainisha kabla ya kuanza kunufaika na miradi hiyo, baadhi ya walengwa walikuwa wakikabiliwa na changamoto ya kukosa uhakika wa chakula cha kutosha kwa siku, lakini kwa sasa shughuli za kiuchumi wanazofanya zimewasaidia kuboresha upatikanaji wa mahitaji yao ya msingi. “Wanufaika wa Mradi huu kwa sasa wamepunguza utegemezi, kuimarisha uwezo wa kuhudumia familia zao na kuhakikisha watoto wanapata fursa ya kuendelea na masomo, ikiwemo elimu ya juu.Jumla ya walengwa 30 wanahusishwa na shughuli hizo ambazo zimechangia kubadilisha maisha yao.” Macha amesema baadhi ya walengwa ambao awali walikabiliwa na changamoto za kiuchumi na kutengwa katika jamii sasa wameendelea kujenga uwezo wa kujitegemea kupitia shughuli za uzalishaji mali, hali inayoongeza nafasi yao ya kushiriki kikamilifu katika maendeleo. “Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela itaendelea kusimamia miradi inayotekelezwa katika eneo hilo ili kuhakikisha inakuwa endelevu na kuleta matokeo yaliyokusudiwa, sambamba na juhudi za Serikali katika kuboresha maisha ya wananchi.” Kwa upande wake mnufaika wa TASAF, Modesta Makonya amesema mradi wa ufugaji samaki kwa njia ya vizimba umemsaidia kuboresha maisha yake na familia yake, ikiwemo kupata kipato na kujenga nyumba kupitia shughuli za uzalishaji mali. Amesema walianza kufikiria shughuli mbadala za kiuchumi baada ya kuelekezwa kuwa mpango wa kunusuru kaya maskini katika awamu waliyokuwa wananufaika nayo ungefikia mwisho. Amefafanua walikaa pamoja na kuanzisha kikundi cha wanawake, ambacho baadaye kilipata msaada wa Serikali kupitia TASAF, chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kupatiwa fedha Sh milioni 34 zilizowawezesha kuanzisha mradi wa ufugaji samaki kwa njia ya vizimba. “Baada ya kupata fedha hizo, tuliweka vizimba viwili, kila kimoja kikiwa na samaki 650. Tulifanya shughuli za ufugaji na tulipofikia wakati wa kuvuna, tulifanikiwa kupata mapato ya takribani Sh milioni 29, jambo lililotupa moyo wa kuendelea na mradi huo,” amesema Makonya. Ameongeza mafanikio ya mavuno ya kwanza yaliwafanya kuendelea na awamu ya pili ya ufugaji, ambapo walitumia Sh milioni 22.4 kwa mahitaji mbalimbali ya mradi, huku wakiendelea na maandalizi ya kuongeza uzalishaji ili kupata mapato makubwa zaidi katika mavuno yajayo. Amesema pia manufaa ya TASAF yameonekana pia kwa walengwa wengine ambao wameanzisha shughuli mbalimbali, zikiwemo ufugaji wa mbuzi, bata na kuku, kilimo cha mboga za majani na biashara ya dagaa, hatua zinazowasaidia kuongeza kipato na kuimarisha maisha ya familia zao.
Fri, 23 Oct 2026 14:13:14 +0000CHATANDA: CCM NI CHAMA IMARA KISICHOYUMBA
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa, Mary Pius Chatanda (MCC), amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaendelea kuwa imara na kusimamia utekelezaji wa Ilani yake kwa lengo la kushughulikia changamoto za wananchi na kuimarisha maendeleo. Chatanda ameyasema hayo leo, Oktoba 23, 2026, wakati akiendelea na mikutano ya ndani katika Kata ya Ikowa, Kijiji cha Makoja, Jimbo la Chamwino mkoani Dodoma, ikiwa ni sehemu ya kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge katika jimbo hilo. Amesema wananchi hawapaswi kuyumbishwa na kauli mbalimbali, bali wanapaswa kuzingatia mipango ya maendeleo inayotekelezwa kwa mujibu wa sera na Ilani ya CCM. Ameeleza kuwa mgombea wa ubunge kupitia CCM, Dkt. Netho Ndilito, endapo atapata ridhaa ya wananchi, atakuwa na jukumu la kusimamia utekelezaji wa Ilani ya chama hicho na kuwasilisha mahitaji ya wananchi wa Chamwino katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aidha, Chatanda amesema mbunge ana jukumu la kuwa kiunganishi kati ya wananchi na Serikali, hususan katika kufuatilia utekelezaji wa mipango na miradi ya maendeleo inayolenga kuboresha maisha ya wananchi.
Fri, 23 Oct 2026 14:18:15 +0000NYONGO ASISITIZA WENYE BIMA YA AFYA KUPATIWA HUDUMA BILA VIKWAZO
Mwamvua Mwinyi, Pwani MKUU wa Mkoa wa Pwani, Stanslaus Nyongo, amesisitiza kuwa wananchi wenye bima ya afya wanapaswa kupata huduma bila vikwazo visivyo halali, huku akielekeza vituo vya kutolea huduma za afya kuhakikisha upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na huduma muhimu kwa wagonjwa. Nyongo ametoa maelekezo hayo wakati wa uzinduzi wa Awamu ya Pili ya Utekelezaji wa Mpango wa Bima ya Afya kwa Wote uliofanyika Maili Moja, Kibaha, mkoani Pwani, akiwataka wakuu wa wilaya na watendaji wao kuimarisha uhamasishaji ili wananchi waelewe umuhimu wa bima hiyo, faida zake na utaratibu wa kujiunga. Amesisitiza kuwa usajili unapaswa kuratibiwa katika vijiji, mitaa na kata zote, huku Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ukitakiwa kuweka mawakala katika maeneo husika ili kurahisisha wananchi kujiunga na mpango huo. Aidha, ameelekeza kufanyika kwa tathmini ya usajili baada ya siku 10 ili kubaini hatua iliyofikiwa na changamoto zinazohitaji kutatuliwa. Ameagiza taarifa za utekelezaji kuwasilishwa kwa Katibu Tawala wa Mkoa, huku wakuu wa wilaya wakitakiwa kusimamia zoezi hilo kwa karibu. Nyongo pia amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kusimamia utekelezaji wa mpango huo unaolenga kupanua upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi. Kwa upande wake, Meneja wa NHIF Mkoa wa Pwani, Tully Mwakyusa, amesema katika awamu ya kwanza, kaya 4,463 kati ya 6,212 zilizolengwa zimesajiliwa, sawa na asilimia 72 ya lengo lililowekwa. Amesema awamu ya pili inalenga kusajili kaya 12,872 zenye jumla ya wanufaika 23,304, ikihusisha wananchi wasio na uwezo wa kifedha pamoja na wale wenye uwezo wa kuchangia gharama za bima. Mwakyusa amesema kaya yenye watu wasiozidi sita itachangia Shilingi 150,000 kujiunga na mpango huo, huku Serikali ikianza tangu Februari 2026 kugharamia bima kwa makundi maalumu yenye uhitaji, yakiwemo wazee, watoto, wajawazito na watu wenye ulemavu.
Fri, 23 Oct 2026 14:22:08 +0000SAMIA LEGAL AID AWAMU YA PILI KUZINDULIWA KIBAHA, LENGO KUFIKIA ASILIMIA 50 YA WANANCHI
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani MKOA wa Pwani unalenga kuongeza wigo wa upatikanaji wa huduma za msaada wa kisheria kwa wananchi hadi kufikia asilimia 50 kupitia kampeni ya Samia Legal Aid Awamu ya Pili, itakayotekelezwa kwa siku 10 katika halmashauri tisa za mkoa huo. Ufunguzi rasmi wa kampeni hiyo unatarajiwa kufanyika Oktoba 28, 2026, katika uwanja wa stendi ya zamani, Maili Moja, mjini Kibaha, huku utoaji wa huduma ukianza Oktoba 29 hadi Novemba 7, mwaka huu. Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Stanslaus Nyongo, amesema kampeni hiyo itatoa fursa kwa wananchi kupata ushauri na huduma za msaada wa kisheria, kuwasilisha changamoto zao na kupata elimu kuhusu masuala mbalimbali ya kisheria, yakiwemo ndoa na talaka, mirathi na wosia, ardhi pamoja na utatuzi wa migogoro kwa njia mbadala. Amesema wananchi wenye mashauri mahakamani au katika vyombo vingine vya utoaji haki pia watanufaika na huduma za uwakili zitakazotolewa bure na mawakili wa kujitegemea pamoja na mawakili wa serikali walioidhinishwa kutoa huduma hizo. Ameongeza kuwa kampeni hiyo itahusisha pia huduma za usajili wa matukio muhimu ya kibinadamu kupitia Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), ikiwemo usajili wa vyeti vya kuzaliwa na vifo. Kwa mujibu wa Nyongo, kampeni hiyo ni sehemu ya juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita kuimarisha upatikanaji wa haki, hususan kwa makundi yenye uhitaji zaidi, yakiwemo wanawake, watoto, wazee, watu wenye ulemavu na vijana. Akizungumza kuhusu utekelezaji wa kampeni hiyo, Mkurugenzi Msaidizi wa Ufuatiliaji wa Huduma za Msaada wa Kisheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Osborn Paisi, amesema awamu ya kwanza iliwafikia wananchi 200,000, sawa na asilimia 9 na kutoa huduma katika kata 10 na vijiji vitatu kila wilaya, huku awamu ya pili ikilenga kufikia kata 136 za Mkoa huo.
Fri, 23 Oct 2026 14:23:55 +0000TANZANIA NA ANGOLA KUFUNGUA FURSA MPYA ZA USHIRIKIANO WA KIDIPLOMASIA
Tanzania na Angola zimeazimia kuimarisha uhusiano wa kihistoria na kidiplomasia kwa kuimarisha ushirikiano wa kimkakati na kubaini fursa mpya za maendeleo kwa manufaa ya wananchi wa nchi hizo mbili. Dhamira hiyo imejidhihirisha katika mazungumzo kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo (Mb), na Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola, Mhe. Téte António. Katika mazungumzo hayo, viongozi hao wamejadili namna ya kuimarisha ushirikiano wa nchi hizo mbili, pamoja na kubaini fursa mpya katika sekta mbalimbali zenye manufaa kwa pande zote. Mazungumzo hayo yanaonesha dhamira ya Tanzania na Angola ya kuendeleza uhusiano wa kirafiki na kuimarisha ushirikiano wa kimkakati, hatua inayolenga kufungua fursa zaidi za maendeleo na kuleta manufaa kwa wananchi wa mataifa hayo mawili.
Fri, 23 Oct 2026 15:33:58 +0000SERIKALI KUENDELEA KUIBORESHA LST
Na Mwandishi Wetu KATIBU Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Seif Shekalaghe ameahidi kuwa Serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya utoaji mafunzo katika Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (LST) ili taasisi hiyo iendelee kuzalisha wahitimu bora zaidi watakaosaidia taifa kwenye masuala mbalimbali ya kisheria. Dkt. Shekalaghe ameyasema hayo wakati akizungumza na menejimenti ya LST katika ziara yake ya kikazi alipotembelea taasisi hiyo leo tarehe 23 Oktoba, 2026 jijini Dar es Salaam. "Nawapongeza kwa kutekeleza kwa ufanisi jukumu lenu la kuwanoa wanafunzi wetu wa sheria ambao wakihitimu mafunzo haya ya uanasheria kwa vitendo wanaenda kulisaidia taifa kwenye mambo mbalimbali hivyo nawaahidi Serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria itaendelea kushirikiana nanyi katika kuboresha miundombinu ya kufundishia na kujifunzia", alisema Dkt. Shekalaghe. Aidha, katika ziara hiyo Dkt. Shekalaghe alipata fursa ya kutembelea miundombinu ya LST ikiwemo jengo la mahakama ya kufundishia pamoja na kuwasalimia wanafunzi ambao aliwahimiza kusoma kwa bidii na kuzingatia maadili. Kwa upande wake Mkuu wa Taasisi ya LST, Prof. Sist Mramba alieleza kuwa Taasisi yake inajivunia mafanikio yaliyopatikana tangu kuanzishwa kwake na kubainisha mikakati ya muda mfupi na mrefu iliyowekwa na Taasisi katika kuendelea kuboresha utoaji mafunzo ya uanasheria kwa vitendo. "Kwa kuwa Watanzania wanaohitaji huduma za kisheria na wanaotumia mawakili ni watu wanaoweka dhamana ya mali zao na maisha yao, imebidi taasisi yetu tuhakikishe tunazingatia ubora na vigezo ili wanaohitimu na kupewa leseni za uwakili au kufanya kazi za uhakimu waweze kutoa huduma bora kwa umahiri na weledi", alibainisha Prof. Mramba. Dkt. Shekalaghe ametembelea LST ikiwa ni muendelezo wa ziara zake za kikazi katika taasisi zote zinazosimamiwa na Wizara ya Katiba na Sheria.
Fri, 23 Oct 2026 16:02:07 +0000NGORONGORO YAWATAKA WATUMISHI KUTUMIA MAFUNZO KUONGEZA UFANISI
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imewataka watumishi wake kuyafanyia kazi mafunzo ya kiutumishi waliyopata ili kuongeza ufanisi, uwajibikaji na ubora wa huduma katika maeneo yao ya kazi. Wito huo umetolewa na Naibu Kamishna wa Mamlaka hiyo anayeshughulikia Huduma za Shirika, Aidan Makalla, wakati wa kufunga mafunzo ya siku tano yaliyofanyika jijini Dodoma, yaliyolenga kuwajengea watumishi uelewa kuhusu utawala bora, usimamizi wa rasilimali watu, matumizi ya teknolojia ya kisasa katika uhifadhi, huduma kwa wateja na nidhamu mahali pa kazi. Makalla amesema Mamlaka imewekeza kwa watumishi hao kwa kuwapatia mafunzo yanayohusu utumishi, maadili, uwekezaji, afya ya akili na itifaki, kwa kuamini kuwa elimu ni nyenzo muhimu katika kuimarisha uwajibikaji na utendaji wenye tija. “Sisi viongozi wa Mamlaka ni kama wazazi, tuna wajibu wa kuwapa mafunzo ili msiharibikiwe na baadaye Mamlaka ikaja kulaumiwa. Yatumieni mafunzo haya kujijenga katika kazi zenu,” alisema Makalla. Mafunzo hayo ni awamu ya pili kwa mwaka huu wa fedha, ambapo Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro inaendelea kuwekeza katika kuwajengea uwezo watumishi wake, kwa kuzingatia msemo wa Kiswahili unaosema, “Asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu.”
Fri, 23 Oct 2026 16:02:55 +0000JESHI LA MAGEREZA TANZANIA, USHELISHELI ZASAINI HATI YA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO
Ssgt Mawazo Mtondo na Wdrs Irine Nkana – DODOMA. Mkuu wa Jeshi la Magereza, CGP Jeremiah Yoram Katungu, leo Oktoba 23, 2026, amepokea ujumbe wa Maafisa wa Magereza kutoka nchini Ushelisheli, ukiongozwa na Kamishna wa Magereza wa nchi hiyo, CP Antoine Denousse, katika Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Msalato jijini Dodoma. Akizungumza mara baada ya kupokea ujumbe huo, CGP Katungu amepongeza ushirikiano wa kindugu na wa muda mrefu uliopo kati ya Jeshi la Magereza Tanzania na Idara ya Magereza ya Ushelisheli, akieleza kuwa ushirikiano huo umekuwa na mchango katika kubadilishana uzoefu na kuimarisha utendaji wa taasisi hizo. Amebainisha kuwa ushirikiano huo umetoa fursa kwa Maafisa wa Magereza kutoka Tanzania kufanya kazi katika Magereza ya Ushelisheli, hatua inayochangia kubadilishana ujuzi na kuboresha mfumo wa uendeshaji wa magereza nchini humo. Kwa upande wake, Kamishna wa Magereza wa Ushelisheli, CP Antoine Denousse, amesema ziara hiyo inalenga kuendeleza na kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili, hususan katika kubadilishana uzoefu na mbinu bora za kiutendaji ili kuongeza ufanisi katika usimamizi wa magereza. Aidha, ziara hiyo imeambatana na utiaji saini wa Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano inayohusu uwezekano wa Maafisa wa Magereza wa Tanzania kufanya kazi katika Magereza ya Ushelisheli. Makubaliano hayo yanalenga kuendeleza ushirikiano na kuwezesha pande hizo mbili kubadilishana uzoefu katika masuala ya usimamizi na uendeshaji wa magereza. Maafisa wengine walioambatana na Mkuu wa Msafara huo ni Chief Inspector Gerry Uranie, Inspector George Santache na Bi. Diana Asba Marie, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu. Aidha, ujumbe huo uliambatana na maafisa kutoka upande wa Tanzania ambao ni Alex Rusegawa Makabe, Wakili wa Serikali kutoka Wizara ya Mambo ya Nje; Sandra Peter Panyika na Mariam Hamoud Jumaa, Maafisa Sheria kutoka Wizara ya Mambo ya Nje; pamoja na Godfrida Damas Kayumba, Afisa Sheria kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani.
Fri, 23 Oct 2026 16:12:54 +0000TMA YAONYA MAFURIKO, MAGONJWA YA MLIPUKO KUFUATIA MVUA ZA MSIMU
Na Karama Kenyunko Michuzi Tv MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetabiri mvua za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo mbalimbali nchini kuanzia Novemba mwaka huu hadi Aprili 2027, huku ikitoa tahadhari ya mafuriko, milipuko ya magonjwa na uharibifu wa miundombinu unaoweza kusababishwa na mvua hizo. Akitangaza utabiri huo, leo Oktoba 23, 2026 Mkurugenzi wa TMA, Dkt. Ladislaus Chang’a, amesema mvua nyingi zaidi zinatarajiwa katika kipindi cha Novemba 2026 hadi Januari 2027, huku kiwango cha mvua kikitarajiwa kupungua katika miezi ya Februari hadi Aprili mwakani. "Hali hiyo inatarajiwa kuchangiwa kwa kiasi kikubwa na El Niño yenye nguvu kubwa, inayohusishwa na ongezeko la joto la maji katika eneo la tropiki ya kati ya Bahari ya Pasifiki. Hata hivyo Dkt. Chang'a amewataka wananchi na wadau wa sekta mbalimbali kuendelea kufuatilia utabiri wa hali ya hewa wa kila siku, siku 10 na kila mwezi ili kupanga shughuli zao kwa kuzingatia mabadiliko ya hali ya hewa katika maeneo yao. Kwa mujibu wa TMA, mikoa ya Kigoma, Tabora, Katavi, Singida, Dodoma, Njombe, Iringa, Mbeya, Songwe na Rukwa, pamoja na maeneo ya kusini mwa Morogoro, inatarajiwa kupata mvua za juu ya wastani hadi wastani. Mikoa ya Ruvuma, Mtwara na Lindi inatarajiwa kupata mvua za wastani hadi juu ya wastani. Mamlaka hiyo imeeleza kuwa mvua za msimu zitaanza kuenea katika maeneo mengi nchini mwezi Novemba. Hata hivyo, baadhi ya maeneo ya Tabora, Katavi, Kigoma, Lindi na Mtwara yanatarajiwa kuanza kupata mvua hizo kuanzia wiki ya nne ya Oktoba hadi wiki ya kwanza ya Novemba. Mvua hizo zinatarajiwa kukoma katika maeneo mengi kati ya wiki ya tatu na ya nne ya Aprili 2027, huku maeneo ya magharibi na nyanda za juu kusini magharibi yakitarajiwa kuendelea kupata mvua hadi wiki ya kwanza ya Mei. Katika Kanda ya Kati, inayojumuisha Dodoma na Singida, mvua zinatarajiwa kuanza katika wiki ya pili na ya tatu ya Novemba na kuisha mwishoni mwa Aprili. Kwa upande wa Ruvuma, mvua zinatarajiwa kuanza baadaye, kati ya wiki ya kwanza na ya pili ya Desemba, na kukoma mwishoni mwa Aprili. Akizungumzia sababu nyingine zinazoweza kuimarisha mvua hizo, Dkt. Chang’a amesema mifumo ya bahari na upepo inatarajiwa kuchangia ongezeko la mvua, ikiwemo upepo wenye unyevunyevu kutoka misitu ya Kongo kuelekea maeneo ya magharibi na Kanda ya Kati. Ameongeza kuwa joto la maji katika eneo la magharibi mwa Bahari ya Hindi linatarajiwa kuwa juu ya wastani ikilinganishwa na eneo la mashariki, hasa katika nusu ya kwanza ya msimu, hali inayoweza kuimarisha mifumo ya mvua nchini. Kuhusu maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka, yakiwemo maeneo ya Ziwa Victoria, kaskazini mwa nchi na ukanda wa pwani, amesema mvua za Vuli zimeanza kunyesha katika baadhi ya maeneo kama ilivyotabiriwa. Ongezeko la mvua hizo linatarajiwa Novemba na Desemba 2026, huku mvua za nje ya msimu zikitarajiwa kuendelea Januari 2027. Wakulima na wafugaji kupewa tahadhari Katika sekta ya kilimo, TMA imeonya kuwa mvua nyingi zinaweza kusababisha maji kutuama mashambani, mafuriko na ongezeko la unyevunyevu kwenye udongo, hali inayoweza kudhoofisha ukuaji wa mazao na kuharibu miundombinu ya kilimo. Kwa mujibu wa mamlaka hiyo, mazingira hayo yanaweza kuongeza magonjwa ya mazao yanayosababishwa na fangasi, bakteria na virusi, na kuathiri uzalishaji wa viazi mviringo, alizeti, maharage, ufuta, matunda na mbogamboga. Aidha, mvua za muda mrefu zinaweza kuvuruga shughuli za uvunaji, ukaushaji, usafirishaji na uhifadhi wa mazao, na hivyo kuongeza upotevu wa chakula baada ya kuvuna. Ili kupunguza athari hizo, wakulima wameshauriwa kuandaa mashamba mapema, kupanda kwa wakati, kutumia mbegu zinazofaa kwa mazingira yao na kuzingatia ushauri wa maafisa ugani. Pia wametakiwa kuweka mifereji ya maji, kutumia matuta na mbinu za kilimo cha kontua ili kupunguza kutuama kwa maji, mmomonyoko wa udongo na upotevu wa rutuba. Kwa wafugaji, TMA imesema mvua hizo zinatarajiwa kuongeza upatikanaji wa malisho na maji kwa mifugo. Hata hivyo, imeonya kuwa unyevunyevu mwingi unaweza kuongeza hatari ya magonjwa, yakiwemo homa ya bonde la ufa na kuoza kwa kwato. Miundombinu na afya kuwa hatarini Dkt. Chang’a amesema mvua nyingi zinaweza kuongeza kina cha maji katika mito na mabwawa, huku uchafuzi wa vyanzo vya maji ukiongeza uwezekano wa kutokea kwa magonjwa ya mlipuko. Katika sekta ya usafiri, athari zinazoweza kujitokeza ni pamoja na uharibifu wa barabara, kuporomoka kwa kingo, kuharibika kwa madaraja na njia za reli, pamoja na kuchelewa kwa huduma za usafiri wa anga na majini. Amesema mvua kubwa zinazoambatana na radi na upepo mkali zinaweza kupunguza uono kwa marubani na kuathiri ratiba za safari za ndege. Katika sekta ya ujenzi, mvua zinaweza kuchelewesha utekelezaji wa miradi, kuongeza gharama, kuharibu vifaa na kuhatarisha usalama wa wafanyakazi pamoja na watumiaji wa miundombinu. TMA imewashauri wakandarasi kuzingatia utabiri wa hali ya hewa wanapopanga shughuli zao, kuhamisha mitambo kutoka maeneo ya mabonde na chemchemi, na kuhifadhi vifaa vinavyoweza kuharibika vikilowa, ikiwemo saruji, katika sehemu salama. Vilevile, mamlaka hiyo imetoa tahadhari kwa shughuli za uchimbaji madini, hasa katika migodi midogo, ikieleza kuwa mvua nyingi zinaweza kuongeza hatari ya maporomoko ya ardhi na kuporomoka kwa mashimo yasiyo imara. Serikali na wananchi watakiwa kuchukua tahadhari Kutokana na utabiri huo, TMA imezitaka mamlaka za serikali za mitaa kuimarisha mifumo ya mifereji ya maji, kutoa elimu kwa wananchi na kuimarisha kamati za maafa katika ngazi za mikoa, wilaya, kata, vijiji na mitaa. Katika sekta ya afya, imeshauri kuimarishwa kwa udhibiti wa mazalia ya mbu, upatikanaji wa dawa na vifaa tiba, pamoja na kuandaliwa kwa mipango mbadala ya kuendelea kutoa huduma za afya endapo miundombinu ya usafiri itaharibika. TMA pia imeeleza kuwa mvua zinaweza kuathiri wanyamapori na shughuli za utalii, huku baadhi ya wanyama wakihamia katika makazi ya watu na kuongeza uwezekano wa migogoro kati ya binadamu na wanyamapori. Mamlaka hiyo imehitimisha kwa kuwataka wananchi na wadau wa sekta mbalimbali kutumia taarifa rasmi za hali ya hewa katika kupanga shughuli zao na kufuatilia tahadhari zinazotolewa ili kupunguza athari zinazoweza kujitokeza wakati wa msimu huo wa mvua.
Fri, 23 Oct 2026 16:19:04 +0000MOROGORO YAZINDUA AWAMU YA PILI YA BIMA YA AFYA KWA WOTE
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Queen Sendiga, amesema Serikali mkoani humo imejipanga kuboresha miundombinu ya afya, upatikanaji wa dawa na vifaa tiba ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na za uhakika. Sendiga ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa awamu ya pili ya usajili wa Bima ya Afya kwa Wote mkoani Morogoro, akiwahimiza wananchi kujiunga na mpango huo ili kujihakikishia upatikanaji wa huduma za matibabu wanapozihitaji. Aidha, amewaagiza wakuu wa wilaya kuhakikisha Bima ya Afya kwa Wote inakuwa ajenda ya kudumu katika vikao vyao hadi wananchi wote waweze kusajiliwa katika maeneo yao. “Bima ya Afya kwa Wote tunayozungumzia hapa iwe ajenda maalumu katika vikao vya ICC na RCC. Ni lazima suala hili lipewe kipaumbele,” amesema Sendiga. Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Best Magoma, amesema utoaji wa huduma za afya kupitia mfumo wa bima ni endelevu, huku Serikali ikiendelea kuimarisha huduma katika ngazi mbalimbali na kukabiliana na changamoto zinazojitokeza. Naye Meneja wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Karunje Mbura, amesema mafanikio ya Bima ya Afya kwa Wote yatategemea ongezeko la wananchi wanaojiunga na mpango huo pamoja na upatikanaji wa huduma wanazohitaji. Mbura amesisitiza kuwa wananchi wenye bima ya afya wanapaswa kuhudumiwa kwa heshima, kupewa maelekezo sahihi na kutendewa haki. Amewahimiza wananchi wa Morogoro kuwasilisha TIRA malalamiko kuhusu changamoto wanazokutana nazo, ikiwemo kunyimwa huduma wanazostahili kupata kupitia bima zao.
Fri, 23 Oct 2026 17:03:15 +0000NAIBU WAZIRI LONDO AAHIDI KUFUATILIA CHANGAMOTO ZA VIWANDA KUKUZA UZALISHAJI WA NDANI
📌 Asisitiza umuhimu wa kuboresha miundombinu na kuhakikisha leseni za viwanda zinaendana na shughuli halisi za uzalishaji; 📌 Serikali kuendelea kuhamasisha ujenzi wa viwanda vipya na kutatua changamoto za viwanda vilivyopo; 📌 Atembelea viwanda vya Insignia limited coral paints na Mara Nile Group Limited vilivyoko mkoa wa Pwani; 📌 Viwanda vya ethanol kuongeza mahitaji ya mahindi na kuchochea uzalishaji wa zao hilo kwa matumizi ya viwandani. Kibaha, Pwani. Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Mhe. Dennis Londo (Mb), amefanya ziara katika viwanda vya Insignia limited Coral Paint na Kiwanda cha kuzalisha Ethanol cha Mara Nile vilivyoko Kibaha mkoa wa Pwani, kwa lengo la kujionea shughuli za uzalishaji kwenye Kongani zilizopo mkoa wa Pwani na kusikiliza changamoto na namna ya kuzitatua. Akiwa kwenye kiwanda cha Insignia sambamba na Mkuu wa wilaya ya Kibaha aliyeambatana nae, Bwana Fadhili Nkurlu pamoja na wadau mbalimbali Mhe. Londo amesema, Serikali inaendelea kuhamasisha ujenzi wa viwanda vipya pamoja na kutembelea viwanda vilivyopo ili kubaini changamoto zinazokwamisha uzalishaji na kuzitafutia ufumbuzi. Amesema Mkoa wa Pwani una nafasi muhimu katika kukuza sekta ya viwanda kutokana na fursa zake za uwekezaji na umuhimu wake katika shughuli za kiuchumi na kumpongeza mwekezaji wa kiwanda hicho kupitia Mkurugenzi wake Bwana Isack Kiwango kwa kupanua uwekezaji kwenye uzalishaji wa rangi pamoja na bidhaa za vifungashio. Kiwanda cha Insignia, ambacho kilianza shughuli zake Temeke kabla ya kuhamia Kibaha, kinajishughulisha na uzalishaji wa rangi pamoja na bidhaa za vifungashio vya plastiki na chuma. Kwa upande wake, mkurugenzi wa kiwanda hicho, Bwana Isack, amesema kiwanda kina matarajio ya kupanua shughuli zake na kutoa ajira zisizopungua 1,000, huku akiomba Serikali kusaidia kutatua changamoto za miundombinu, hususan barabara zinazohudumia maeneo ya viwanda. Akiwa katika kiwanda cha kutengeneza Ethanol cha Mara Nile, Mhe. Londo amesema kiwanda hicho kinatatarajia kuleta mapinduzi kwenye kilimo kupitia Teknolojia ya kuzalisha ethanol kwa kutumia mahindi na hivyo kuongeza matumizi ya mahindi katika shughuli za viwandani, ikiwemo uzalishaji wa ethanol. Akitoa majumuisho ya ziara hiyo Mhe Londo amesema pia mahitaji ya mahindi yataongezeka kwasababu ya matumizi ya viwanda na hivyo zao hilo kuongezeka thamani na kusisitiza umuhimu wa kutafuta matumizi na masoko mbalimbali ya mahindi ili kuongeza thamani ya zao hilo na kupanua fursa za kibiashara kwa wakulima. Akizungumza katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Mhe. Londo amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha leseni zinazotolewa kwa viwanda zinaendana na shughuli halisi zinazofanyika. Amesema ni muhimu kufuatilia viwanda vinavyopewa leseni za uzalishaji kamili lakini katika utekelezaji wake vinafanya shughuli za kuunganisha bidhaa pekee, ili kuhakikisha shughuli za viwanda zinaendana na madhumuni ya leseni zao. Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Fadhili Nkurlu, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Serikali na wadau wa sekta binafsi katika kuboresha mazingira ya uwekezaji na kutatua changamoto zinazokabili wafanyabiashara na wawekezaji. Ziara hiyo ni sehemu ya maandalizi ya uzinduzi wa Sera ya Maendeleo Endelevu ya Viwanda ya mwaka 2025 na Sera ya Maendeleo ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati, Toleo la 2025, unaotarajiwa kufanyika Novemba 4, 2026. Sera hizo zinalenga kutoa mwelekeo wa maendeleo ya viwanda na kukuza shughuli za wajasiriamali nchini.
Fri, 23 Oct 2026 17:07:09 +0000MABALOZI WASTAAFU WARIDHISHWA NA UWEKEZAJI WA SERIKALI NIT
Umoja wa Mabalozi Wastaafu Tanzania umeridhishwa na uwekezaji wa Serikali katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), ikiwemo vifaa vya kisasa vya kufundishia na miundombinu bora, inayochangia kuzalisha wataalamu mahiri wa kuhudumia miradi mikubwa ya kimkakati katika sekta ya usafirishaji nchini. Akizungumza wakati wa ziara ya umoja wa mabalozi hao wastaafu Chuoni hapo iliyofanyika tarehe 23 Oktoba 2026, Katibu wa umoja huo Balozi Irene Kasyanju ameushukuru Uongozi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji kwa mapokezi mazuri wakati wa ziara hiyo ambapo wamepata fursa ya kutembelea Chuo na kupata fursa ya kujifunza na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na NIT, ikiwemo mafunzo yanayohusu usafiri wa anga,mabomba,reli na majini. Amesema uwekezaji huo ni hatua muhimu katika kujenga uwezo wa Tanzania kuandaa wataalamu wake wenyewe, badala ya kutegemea wataalamu kutoka nje ya nchi, huku akibainisha kuwa NIT ina nafasi kubwa katika kutoa ujuzi unaohitajika kuendesha na kuendeleza miradi ya kimkakati inayotekelezwa katika sekta ya usafirishaji nchini ikiwemo ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR,ujenzi wa meli na uimarishwaji wa shirika la ndege la Tanzania (ATCL). Aidha,Balozi Kasyanje ametoa wito kwa mabalozi wa Tanzania ambao bado wanahudumu nje ya nchi kutembelea NIT ili kujionea uwekezaji na maendeleo yaliyofikiwa Chuoni hapo, akisema hatua hiyo itawasaidia kufahamu uwezo wa Tanzania katika kuzalisha wataalamu mahiri wazawa kwaajili ya kusimamia miradi ya kimkakati ya sekta ya usafirishaji Aidha Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Dkt. Prosper Mgaya, amesema Chuo kitafanyia kazi mapendekeza yote yaliyowasilishwa na mabalozi hao wastaafu ikiwemo kuimarisha ushirikiano na wadau mbalimbali wa kisekta katika masuala ya usalama barabarani wakati wa hatua za ujenzi wa barabara kwa kuzingatia usalama wake kuanzia hatua ya usanifu, ujenzi hadi ukarabati wake ili kupunguza ajali. Ziara imehusisha mabalozi wa Tanzania waliohudumu katika nchi mbalimbali duniani ikiwemo Malawi,Cuba, Uholanzi,Uswisi,Marekani,Misri,Afrika ya Kusini,Ufaransa na Uturuki.
Fri, 23 Oct 2026 20:00:45 +0000SportPesa brings Kariakoo Derby to Segerea as Simba stage historic 2-1 comeback
SportPesa brings Kariakoo Derby to Segerea as Simba stage historic 2-1 comeback A SportPesa screening truck set up in Segerea gave supporters across the Dar es Salaam neighbourhood a shared view of Simba’s 2-1 comeback against Young Africans in the Kariakoo Derby. Yanga scored early at Uhuru stadium, then Simba hit back twice after the break. Simba’s win reshuffled the order at the top of the league table. The SportPesa march coverage linked a local football gathering to a match that shaped the early league standings. Alongside the community screening, SportPesa Tanzania provides live football markets through its digital platform, where eligible adults can view available in-play betting options. Yanga held their one-goal lead through half-time, then Simba used the second half to take the match back with two strikes. Yanga struck first, but Simba turned the match around Peter Shalulile put Yanga ahead in the fifth minute after an attacking move involving Maxi Nzengeli, with more than 80 minutes still to play. Simba found no way back before the interval, so Yanga went in at half-time with a 1-0 lead. That left Simba the whole second half to recover. Neo Maema equalised for Simba in the second half, and Elie Mpanzu then put them ahead with the winner. Both goals turned a one-goal deficit into a 2-1 victory. SportPesa’s match report on Simba’s comeback records the full sequence and a result that meant more for the title race. “Football in Tanzania is about more than what happens inside the stadium. The Kariakoo Derby brings supporters together across communities, and our screening experience in Segerea was about bringing that shared passion closer to fans. Moments like Simba’s comeback show why local football continues to create such strong connections among supporters” said SportPesa Tanzania Head of Marketing Tracy Humplick. The truck took the action to Segerea’s doorstep The Segerea screening offered the match a viewing point other than Uhuru Stadium. The truck delivered the broadcast to the neighborhood so supporters could watch the same match together. The screen brought the action from the pitch to a local gathering while the outcome was still hanging in the balance. Shared viewing changes the context in which people follow football. Everyone is watching the same game at the same time, so every goal and missed opportunity becomes something for the whole crowd to talk about as it happens. In Segerea, supporters came together for a domestic fixture that mattered to fans of both clubs. Live bets moves with a changing match SportPesa’s Live bets covers betting on a changing match once play starts, as the score and the clock keep moving. It differs from betting before the teams take the field. The encounter showed how the picture can shift. Yanga led at the interval, yet Simba ended the night with all three points. Live football markets track a match that is still unfolding, rather than a final score. Segerea’s screening and SportPesa live betting covered two different sides of the same matchday. The truck showed supporters the game live, while Live bets handled the real time in-play betting. Three clear points for Simba after the victory Simba had not won a league meeting against Yanga since April 2023. Mpanzu’s winner ended a wait of three and a half years. Supporters in Segerea watched that wait end on a truck screen rather than from the stands. The win lifted Simba to 21 points in the Tanzania Premier League, three clear of Yanga. A gap that size is small this early in the season, and one result can erase it. Yanga has plenty of matches left to do exactly that. Conclusion Simba’s 2-1 comeback against Yanga will be remembered for more than its impact on the NBC Premier League table. The result ended a league victory drought stretching back to April 2023. The SportPesa screening in Segerea gave local supporters a chance to experience the rivalry together, away from the stands at Uhuru Stadium. For SportPesa Tanzania, the screening reflects the role football can play in connecting the brand with communities through shared sporting experiences. From Yanga’s early lead to Simba’s dramatic second-half turnaround, the Kariakoo Derby showed how one match can bring a neighbourhood together. It created memories that last beyond the final whistle.
Sat, 24 Oct 2026 03:00:00 +0000SERIKALI YAOMBWA KUTOA KIPAUMBELE BIMA YA AFYA KWA WATOTO WENYE ULEMAVU
NA DENIS MLOWE, IRINGA SERIKALI imeombwa kuhakikisha watoto wenye ulemavu na yatima wanaotoka katika familia zenye hali duni ya kiuchumi wanapewa kipaumbele katika upatikanaji wa bima ya afya, ili kuwawezesha kupata matibabu kwa wakati bila kuathiri hali ya kiuchumi ya familia zao. Ombi hilo limetolewa na Mkurugenzi wa Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Lebao’s Kids Foundation (BKF), Theophil Muyinga, wakati wa zoezi la kugawa bima za afya kwa watoto wenye ulemavu wanaohudumiwa na taasisi hiyo pamoja na watoto yatima kutoka kituo cha kulelea watoto yatima kilichopo Migoli, mkoani Iringa. Zoezi hilo limeandaliwa na BKF kwa kushirikiana na Mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii (CHF), ikiwa ni sehemu ya juhudi za kusaidia watoto wenye uhitaji kupata huduma za afya na kupunguza changamoto zinazowakabili wanapohitaji matibabu. Muyinga amesema familia nyingi za watoto hao zinakabiliwa na hali ngumu ya kiuchumi, jambo linalozifanya kushindwa kumudu gharama za matibabu, hivyo umuhimu wa Serikali kuweka utaratibu utakaohakikisha watoto hao wanapata bima ya afya kwa kuzingatia mahitaji yao maalumu. Amesema upatikanaji wa bima ya afya kwa watoto wenye ulemavu na yatima ni hatua muhimu katika kulinda afya zao na kuhakikisha changamoto za kifedha hazigeuki kuwa kikwazo cha kupata huduma za matibabu wanapougua. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mwenza wa BKF, Catherine Moreno, amesisitiza umuhimu wa kuendeleza juhudi za kusaidia watoto wenye uhitaji, akieleza kuwa upatikanaji wa huduma za afya ni miongoni mwa mahitaji muhimu yanayopaswa kuzingatiwa katika ustawi wa watoto hao. Akijibu ombi hilo, Afisa Uandikishaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) katika Manispaa ya Iringa, Kokwiliza Katemana, amesema Serikali ina jukumu la kulinda afya za wananchi wake, huku watoto wakiwa miongoni mwa makundi yanayohitaji kupewa kipaumbele katika upatikanaji wa huduma za afya. Katemana amesema katika awamu hii, Serikali imeweka mkazo katika kuwafikia watu wa makundi maalumu pamoja na kaya zisizo na uwezo wa kiuchumi, ili kuhakikisha nao wanapata fursa ya kunufaika na huduma za bima ya afya. Amesema juhudi hizo zinalenga kupanua wigo wa wananchi wanaofikiwa na huduma za bima ya afya, hususan wale ambao hali zao za kiuchumi zinawafanya washindwe kugharamia matibabu wanapougua. Utoaji wa bima hizo unatarajiwa kupunguza mzigo wa gharama za matibabu kwa watoto hao na familia zao, huku ukiwapa nafasi ya kupata huduma za afya kwa urahisi zaidi wanapokabiliwa na changamoto za kiafya. Hatua hiyo inaendana na juhudi za Serikali za kutekeleza awamu ya pili ya mpango wa Bima ya Afya kwa Wote, unaolenga kupanua upatikanaji wa huduma za afya na kupunguza gharama za matibabu zinazobebwa na wananchi. Kwa watoto wenye ulemavu na yatima kutoka familia zenye kipato cha chini, upatikanaji wa bima ya afya ni sehemu muhimu ya kuhakikisha wanapata huduma za matibabu bila kubaguliwa kutokana na hali zao za kiuchumi.
Sat, 24 Oct 2026 07:21:11 +0000MAHAFALI YA 15 YA PSPTB YAFANA JIJINI DAR
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Deogratius Luswetula (Mb) (kushoto) akikabidhiwa tuzo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Jacob Kibona (kulia) kwa kutambua mchango wa Wizara ya Fedha wakati wa Mahafali ya 15 ya Wahitimu wa Mitihani ya Kitaaluma ya PSPTB yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Deogratius Luswetula (Mb) akizungumza wakati wa Mahafali ya 15 ya Wahitimu wa Mitihani ya Kitaaluma ya PSPTB yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Jacob Kibona akizungumza katika Mahafali ya 15 ya Wahitimu wa Mitihani ya Kitaaluma ya PSPTB yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) Godfred Mbanyi akizungumza wakati wa Mahafali ya 15 ya Wahitimu wa Mitihani ya Kitaaluma ya PSPTB ambapo amewaasa wahitimu kufanya kazi kwa kufata maadili ya kitaaluma wakati wa mahafali hayo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam. Mshehereshaji ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma ( PSPTB), Shamim Mdee akizungumza jambo wakati wa Mahafali ya 15 ya Wahitimu wa Mitihani ya Kitaaluma ya PSPTB. Baadhi ya Wageni waalikwa pamoja na wafanyakazi wa PSPTB wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Deogratius Luswetula (Mb) wakati wa Mahafali ya 15 ya Wahitimu wa Mitihani ya Kitaaluma ya PSPTB. Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Deogratius Luswetula (Mb) akitoa zawadi kwa baadhi ya wanafunzi waliofanya vizuri kwenye mitihani ya Bodi wakati wa mahafali ya 15 ya Bodi ya wataalumu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa huduma za Uanachama na Ushauri wa Kitaalamu, Amani Ngonyani akizungumza wakati wa mahafali ya 15 ya Bodi ya wataalumu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Deogratius Luswetula (Mb) akiwatunuku wahitimu wa walioudhuria Mahafali ya 15 ya Wahitimu wa Mitihani ya Kitaaluma ya PSPTB yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam. Wahitimu wa mahafali ya 15 ya Bodi ya wataalumu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) wakila kiapo cha utii na uaminifu Picha mbalimbali za pamoja katika mahafali ya 15 ya wahitimu wa mitihani ya kitaaluma ya PSPTB
Sat, 24 Oct 2026 07:24:38 +0000MAPENDEKEZO YA VIJANA YATAPOKELEWA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA, KUKABILIANA NA MIMBA ZA UTOTONI - PROF. SHEMDOE
Na: OWM–TAMISEMI, Arusha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM–TAMISEMI), Mhe. Prof. Riziki Shemdoe, amesema Serikali itapokea na kufanyia kazi mapendekezo ya vijana yanayolenga kuboresha huduma za afya ya msingi katika zahanati, vituo vya afya na hospitali za wilaya, kupitia mfumo wa Serikali wa kupanga mipango kwa kushirikisha wananchi wa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O&OD). Prof. Shemdoe amesisitiza umuhimu wa kusikiliza maoni ya vijana akieleza kuwa asilimia 90 ya vijana hupata huduma za afya katika vituo vya afya ya msingi. Hata hivyo, vijana wenye umri wa miaka 10–24, ambao ni asilimia 31 ya Watanzania milioni 61, bado wanakabiliwa na changamoto za huduma za afya zisizo rafiki kwao, ikiwemo mimba na ndoa za utotoni. Prof. Shemdoe amesema hayo Oktoba 23, 2026, jijini Arusha, wakati akifungua mjadala unaoongozwa na vijana wa Tanzania kuhusu afya ya uzazi na afya ya akili, ulioandaliwa na Jumuiya ya Afya ya Afrika Mashariki, Kati na Kusini (ECSA). “Niwatake vijana kutumia siku hizi mbili vizuri na kuja na mapendekezo yanayotekelezeka, yenye muda maalumu wa utekelezaji, ili yapimwe na, pale inapowezekana, yaandaliwe mipango na bajeti kwa ajili ya utekelezaji,” ameeleza Prof. Shemdoe. Aidha, Prof. Shemdoe amesema Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amewekeza fedha nyingi katika ujenzi wa miundombinu ya afya ya msingi, hivyo amewataka vijana kuilinda ili iendelee kuhudumia wananchi na vizazi vijavyo. Pia, amewahimiza kupata elimu ya afya ya mama na mtoto ili kumuunga mkono Rais kwa vitendo, akimtaja kuwa kinara wa afya ya mama na mtoto barani Afrika. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa ECSA, Dkt. Ntuli Kapologwe, amesema vijana wenye umri chini ya miaka 24 katika nchi wanachama wa jumuiya hiyo ni asilimia 65. Ameeleza kuwa kuwawezesha kupata elimu ya afya ya akili na afya ya uzazi kutasaidia kupunguza vifo vya kina mama na watoto, pamoja na kuhamasisha wanawake kujifungulia katika vituo vya kutolea huduma za afya. Naye, Mwakilishi wa Vijana wa Mtandao wa ECSA, Dkt. Kuduishe Kisowile, amesema sehemu kubwa ya vifo vya kina mama inahusishwa na mimba za utotoni na za vijana ambao hawajafikia umri unaofaa. Ameeleza kuwa vijana watashiriki kujadili namna ya kuzuia vifo hivyo na kuimarisha ushirikiano kati ya wizara mbalimbali katika kutokomeza mimba za utotoni. Mkutano huo umewakutanisha vijana takribani 200 kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani kwa lengo la kujadili afya ya uzazi kwa vijana, afya ya akili na utekelezaji wa afua mbalimbali zinazosimamiwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, zikiwemo kuhakikisha hakuna mama anayejifungua nyumbani, kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi na kuhakikisha kila mtoto au mtu mzima anayehitaji chanjo anaipata.
Sat, 24 Oct 2026 07:36:32 +0000Interview avec Léonce Ngendakumana : « Le pouvoir actuel est une dictature voilée »
Le parti Sahwanya-Frodebu a décidé de ne pas présenter un candidat à la présidentielle de 2027. Pour Léonce Ngendakumana, membre de ce parti et ancien président de l’Assemblée nationale, cette décision s’explique par les conditions dans lesquelles le scrutin est organisé. Il dénonce la manipulation du processus électoral et l’impossibilité du pays d’organiser des élections libres et démocratiques. Il revient également sur l’héritage du président Melchior Ndadaye, les divisions au sein du Frodebu et les difficultés économiques du pays.
Tue, 20 Oct 2026 05:13:09 +0000Le soir où le Parc devint opéra : Paris terrasse Barcelone (4-2)
Il y a des soirs où le football cesse d'être un sport. Il devient drame, il devient lyre, il devient serment. Ce mardi 20 octobre, sous les cieux allumés du Parc des Princes, le Paris Saint-Germain a offert au FC Barcelone sa première désillusion de la saison, au terme d'une symphonie en quatre actes : 4-2. Une victoire d'une beauté cruelle, tant elle fut conquise dans la douleur.
Thu, 22 Oct 2026 06:12:18 +0000Saido Berahino : La révérence d’un enfant de Bujumbura
Il y a des lettres qui ne se lisent pas. Elles se ressentent. Celle que Saido Berahino a déposée ce mardi 20 septembre 2026 sur Instagram appartient à cette race rare. L'enfant prodige de Bujumbura, devenu flamme des Hawthorns, vient de raccrocher les crampons. Non pas dans le fracas, mais dans une pudeur immense, une gratitude presque sacrée.
Thu, 22 Oct 2026 06:16:09 +0000L’Europe s’embrase : Quand les princes chancellent et que les gueux deviennent rois
La Ligue des Champions a rendu son verdict pour sa troisième levée, et quelle levée ! Deux soirs. Dix-huit théâtres. Le football dans ce qu'il a de plus cruel et de plus sublime.
Thu, 22 Oct 2026 16:20:20 +0000Page 675 of 1167 · 23329 stories