Search the region
23288 stories
Magoli na kadi nyekundu | Simba SC 6-1 Mashujaa FC | NBC Premier League 13/10/2026
Simba SC imeibonda Mashujaa FC kipigo cha mabao 6-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa kwenye Dimba la Uhuru Dar es Salaam. Wa kwanza kufunga ni Libasse Gueye, akafuata Elie Mpanzu aliyefunga mawili.. huku wengine wakiwa ni Anicet Oura, Morice Abraham na Ismael Olivier Toure... Goli la kufutia machozi ni la maajabu kutoka kwa Selemani Bwenzi... Tazama magoli yote saba, na kadi nyekundu waliyopata Mashujaa FC kupitia kwa straika wake Hassan Kabunda.
2026-10-13T18:21:01+00:00En RDC, Joseph Kabila lance le FRN, 30 ans après l’AFDL
Read the full report from the original source.
RecentlyOrengo calls for peace at Raila’s anniversary in Siaya
Orengo says the October 15 commemoration will bring together local and international guests
RecentlyPour les Etats de l’AES veulent décoloniser les savoirs
Read the full report from the original source.
RecentlyWizara, PURA kuimarisha utoaji habari miradi ya mafuta, gesi
Read the full report from the original source.
RecentlyPSSSF YATUMIA MAONESHO YA WIKI YA VIJANA KITAIFA KUTOA ELIMU YA HIFADHI YA JAMII
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) Bw. Paul Kijazi, (katikati), akimuhudumia Mwanachama wa Mfuko kwenye banda la PSSSF katika Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Vijana kitaifa kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Ndua Manispaa ya Mji wa Sumbawanga Mkoani Rukwa Oktoba 13,2026. Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) Bw. Paul Kijazi (kushoto), akiangalia jinsi vijana wanavyoshona katika banda la Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kitaifa Viwanja vya Shule ya Msingi Ndua Manispaa ya Mji wa Sumbawanga Mkoani Rukwa Oktoba 13,2026. Mkuu Wa Mkoa Kusini Unguja, Zanzibar, Mhe. Hamida M. Khamis (kushoto), akipatiwa mkoba wenye machapisho na taarifa mbalimbali zinazohusu huduma zitolewazo na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), kutoka Afisa Uhusiano wa Mfuko wa PSSSF, Bi. Zaituni Hemed, alipotembelea banda la Mfuko huo katika Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Vijana kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Ndua, Mainispaa ya Mji wa Sumbawanga Mkoani Rukwa Oktoba 12, 2026. Wafanyakazi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), wakiwa kwenye banda la Mfuko huo kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kitaifa kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Ndua, Manispaa ya Mji wa Sumbawanga mkoani Rukwa, Oktoba 11, 2026. Mwanachama wa PSSSF, akieekezwa namna ya kujiunga na psssf portal, kwenye banda la PSSSF katika Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kitaifa 2026 yanayofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Ndua, Manispaa ya Sumbawanga, mkoani Rukwa, Oktoba 10, 202 Mwanachama wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Ally Mussa Haraka (Aliyeketi) akihudumiwa na Afisa Uhusiano Mkuu wa PSSSF, Bw. Abdul Njaidi kwenye Banda la Mfuko huo katika Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Vijana kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Ndua, Mainispaa ya Mji wa Sumbawanga Mkoani Rukwa Oktoba 12, 2026. Na Mwandishi Wetu, Sumbawanga Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) unashiriki katika Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kitaifa 2026 yanayofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Ndua, Manispaa ya Sumbawanga, mkoani Rukwa, kwa lengo la kutoa elimu kuhusu huduma za hifadhi ya jamii na matumizi ya mifumo ya kidijitali inayorahisisha upatikanaji wa huduma za Mfuko. Akizungumza katika maonesho hayo, Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu na Utawala wa Mfuko wa PSSSF, Bw. Paul Kijazi, amesema maonesho hayo ni fursa muhimu kwa Mfuko kuwafikia wanachama na wananchi kwa ujumla, kuwapatia elimu ya hifadhi ya jamii na kuwaelimisha kuhusu umuhimu wa kujiandaa mapema kwa maisha baada ya kustaafu. Amesema PSSSF inaendelea kutumia majukwaa mbalimbali, ikiwemo maonesho, kuimarisha uelewa wa wananchi kuhusu huduma za Mfuko na maboresho mbalimbali yaliyofanywa ya mifumo na mafao. Aidha, amesema katika maonesho hayo, PSSSF inatoa huduma na elimu kwa wanachama na wastaafu kuhusu matumizi ya mfumo wa mtandao wa PSSSF Portal unaowawezesha mwanachama na mstaafu kupata huduma mbalimbali za Mfuko kwa njia ya kidijitali. Kupitia mfumo huo, wanachama wanaweza kupata taarifa zinazohusu michango yao, taarifa za mafao na huduma nyingine zinazopatikana mtandaoni, hatua inayosaidia kurahisisha upatikanaji wa huduma na kupunguza ulazima wa kufika ofisini kwa baadhi ya mahitaji. Maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kitaifa hufanyika kila mwaka kwa lengo la kuhamasisha vijana kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo ya Taifa, pamoja na kuwajengea uelewa kuhusu fursa zinazoweza kuwawezesha kujikwamua kiuchumi na kijamii. Maadhimisho ya mwaka 2026 yanaongozwa na kauli mbiu isemayo: “Mazingira Tofauti, Fursa Sawa kwa Vijana.”
Tue, 13 Oct 2026 18:11:02 +0000MISA TAN YATUMIA MIRADI YA KIMKAKATI MWANZA KUCHOCHEA UANDISHI WA MAENDELEO
Jitihada za kutumia uandishi wa habari kuchochea ukuaji wa uchumi na kuunga mkono maendeleo nchini zimepewa kipaumbele katika kongamano la wadau wa habari lililoandaliwa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA Tanzania) jijini Mwanza. Kongamano hilo lililofanyika Oktoba 12, 2026, chini ya kaulimbiu "Uhuru wa Vyombo vya Habari Kiuchumi", liliwashirikisha wanachama 60 wa MISA kutoka Kanda ya Ziwa, Magharibi na Kati, pamoja na wadau kutoka taasisi za umma na sekta binafsi. Kama muendelezo wa kongamano hilo, wanachama hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa MISA Tanzania, Edwin Soko, wamefanya ziara ya kutembelea miradi ya kimkakati Oktoba 13, 2026, ikiwemo Daraja la John Pombe Magufuli (Kigongo-Busisi) na mradi wa ujenzi wa meli ya kisasa ya MV New Mwanza katika Bandari ya Mwanza. Akizungumza wakati wa ziara, Afisa Uhusiano Mwandamizi wa TASHICO, Abdulrahman Ally, amesema MV New Mwanza ni kichocheo muhimu cha uchumi kwani itaboresha usafiri wa abiria na mizigo na kuchochea biashara katika Ukanda wa Ziwa na nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Naye Mwenyekiti wa MISA Tanzania, Edwin Soko, amesema ziara hiyo inalenga kuwawezesha waandishi kujionea uwekezaji wa Serikali ili waweze kuhabarisha umma kwa taarifa sahihi. Amesema waandishi wana wajibu wa kuwa mabalozi wa maendeleo kwa kuelimisha wananchi kuhusu mchango wa miradi hiyo katika kuboresha maisha na kukuza uchumi wa Taifa.
Tue, 13 Oct 2026 18:08:47 +0000Audio — Journal 17h TU (13.10)
To play this audio please enable JavaScript, and consider upgrading to a web browser that supports HTML5 video
RecentlyGor launch FKF PL title defence with win over Murang’a
Latest · football
RecentlyWASHIRIKI KONGAMANO LA VYAMA VYA USHIRIKA AFRIKA WAFURAHIA KUJENGEWA UWEZO
Na Said Mwishehe,Michuzi TV WASHIRIKI wa Kongamano la kimataifa la Vyama vya Ushirika vya Akiba na Mikopo Barani Afrika(SACCA) wamesema kongamano hilo limekufa fursa muhimu ya kuwaongezea maarifa viongozi wa vyama hivyo. Wakizungumza leo Oktoba 13,2026 wakati wa kongamano hilo linaloendelea katika Ukumbi wa mikitano wa Kimatata Julius Nyerere jijini Dar es Salaam washiriki hao wamesema kupitia kongamano kuna mada mbalimbali znazotolewa ambazo kwa sehemu kubwa zinawajengea uelewa na maarifa kuhusu usimamizi bora wa vyama vya ushirika. Akizungumza kuhusu kongamano hilo ambalo limeshirikisha washriki zaidi ya 600 , Mwenyekiti wa Chama cha Akiba na Mikopo (SACCOS) cha Kinole kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, Hasira Zahoro ambaye ni miongoni mwa washiriki amesema limekuwa fursa katika kuwaongezea viongozi wa vyama hivyo maarifa ya uongozi na usimamizi bora. “Katika kongamano hili kumekuwa na mijadala mbalimbali inayotolewa na wawezeshaji waliobobea katika vyama vya ushirika na hivyo imetusaidia viongozi kubaini mapungufu yaliyopo na namna ya kuyatatua ili kufikia malengo yaliyowekwa hasa kwenye kuboresha mifumo ya uongozi na usimamizi wa watendaji. Ameongeza kupitia mafunzo yanayohusu uongozi na kuimarisha mifumo ya uongozi, amepata maarifa mapya kuhusu umuhimu wa kufanya tathmini kabla ya kuchukua hatua, kutambua mahitaji ya taasisi na kuweka mikakati inayolenga kutatua changamoto zilizopo. Pia amesema mijadala hiyo imewajengea uwezo wa kutathmini utendaji wa wafanyakazi, kuendesha mchakato wa ajira, kubaini changamoto za kiutendaji na kutafuta suluhisho, pamoja na kuweka mazingira yatakayowafanya watendaji kuwa na imani na taasisi wanazozifanyia kazi. Zahoro amesema SACCOS ya Kinole ina wanachama wengi ambao ni wakulima na wajasiriamali wakiwemo vijana, hivyo kuboresha uongozi na usimamizi wa chama hicho kutasaidia kuimarisha utoaji wa huduma na kuchochea maendeleo ya wanachama. Ametumia hiyo kutoa shukrani kwa taasisi za SCALT, TCDC pamoja na Serikali kwa kuwezesha kufanyika kwa kongamano hilo huku akisisitiza kila chama kitakachoshiriki kongamano hilo kupitia mwakilishi wake kitapata maarifa yatakayosaidia kuboresha shughuli za vyama vya ushirika.
Tue, 13 Oct 2026 18:02:20 +0000Argentina lodges legal claim against UK's Falklands oil exploration
The action filed with an international maritime tribunal is the latest development
RecentlyS.4 student dies after ambulance overturns in Agago
A senior four student of Patongo Seed School has died after an ambulance transporting her to a referral hospital overturned in Agago district, raising concerns…
RecentlyIda: Raila’s legacy belongs to all Kenyans
Ida urges Kenyans to set aside political differences ahead of Raila’s memorial in Bondo
RecentlyMinistry, PURA to strengthen public information on oil gas projects
Read the full report from the original source.
RecentlySifuna meets Mt Kenya leaders Njeri Maina, Senator Murango as opposition unity calls intensify
Read the full report from the original source.
RecentlyKenyan rally star Karan hails Rwanda’s historic Formula 1 deal
featured · 3 hours ago
RecentlyNairobi water supply to be disrupted for 24 hours in parts of city
Latest · News
RecentlyCMA seeks risk ratings of 320 money market funds
Read the full report from the original source.
RecentlyCashAfrica brings mobile tap-to-pay to Chicken Republic outlets
Read the full report from the original source.
RecentlyFAO KUMUENZI MWANAMKE MKULIMA, KUTOA TUZO, ZAWADI KWA VINARA TANGA.
Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) nchini Tanzania limesema maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani mwaka huu yataweka mkazo katika kutambua na kuenzi mchango wa mwanamke mkulima katika uzalishaji wa chakula, biashara ya kilimo na kuboresha lishe katika kaya. Akizungumza na Waandishi wa habari Oktoba 13, 2026, Jijini Tanga, Jane Mstagati, Mtaalamu wa Masuala ya Jinsia kutoka FAO Tanzania, mara baada ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Prof. Peter Msofe, kutembelea Banda la Umoja wa Taifa, amesema mwanamke ana nafasi kubwa katika kuhakikisha chakula kinapatikana na kuandaliwa nyumbani, huku akishiriki kwa kiwango kikubwa katika shughuli za uzalishaji mashambani. Amesema maadhimisho hayo yanalenga kutambua wanawake wanaofanya vizuri katika kilimo, kwa kuzingatia mchango wao katika kuzalisha chakula cha kutosha kwa familia na jamii, kushiriki katika biashara ya kilimo pamoja na ufugaji wa mifugo inayozalisha maziwa na mayai. Mstagati amesema FAO kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo na Mkoa wa Tanga, ilitumia vigezo mbalimbali kuwapata wanawake vinara wa kilimo, ikiwemo uzalishaji wa mboga mboga za aina mbalimbali na matumizi ya mbolea za asili zinazolenga kupunguza madhara yanayoweza kusababishwa na matumizi ya kemikali. Amesema kabla ya kilele cha maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani, Oktoba 16, 2026, kutakuwa na hafla ya kuwatambua na kuwapongeza wanawake vinara wa kilimo Oktoba 15, mwaka huu, jijini Tanga, ambapo tuzo zitatolewa kwa wanawake waliofanya vizuri katika sekta hiyo. Wanawake hao wanajumuisha wanaojihusisha na kilimo cha mboga mboga, ufugaji wa ng’ombe, kuku na mbuzi, pamoja na shughuli nyingine katika mnyororo wa thamani wa kilimo. Ameeleza kuwa mmoja wa wanawake watakaotambuliwa atashiriki katika mdahalo utakaolenga kujadili changamoto na fursa zilizopo katika kilimo, mchango wa ubunifu katika kuboresha upatikanaji wa chakula na lishe, pamoja na namna wanaume na Serikali wanavyoweza kumuunga mkono mwanamke mkulima. Amesisitiza kuwa upatikanaji wa chakula cha kutosha pekee hautoshi kuhakikisha lishe bora, kwani maandalizi ya chakula, mgawanyo wa rasilimali na maamuzi ndani ya kaya pia vina mchango mkubwa katika hali ya lishe ya familia.
Tue, 13 Oct 2026 17:34:56 +0000Page 690 of 1165 · 23288 stories