Unganishwa

Search the region

23275 stories

Uncategorized · Business Daily

Kibra set for one of Nairobi’s tallest residential buildings

Read the full report from the original source.

Recently
National · Jamhuri Media

Serikali kuendelea kuwekeza katika shughuli za uzalishaji za vijana- Dk Mwigulu

Read the full report from the original source.

Recently
Business · Issa Michuzi

MAENEO YANAYOWEZA KUIMARISHA SEKTA VYAMA VYA USHIRIKA BARANI AFRIKA YATAJWA

Na Said Mwishehe,Michuzi TV MATUMIZI ya teknolojia, utoaji wa mikopo kwa ufanisi na usimamizi bora ni miongoni mwa maeneo muhimu katika kuimarisha sekta ya ushirika wa fedha na kuongeza manufaa kwa wanachama barani Afrika. Hayo yameelezwa leo Oktoba 13,2026 jijini Dar es Salaam na Naibu Mrajisi wa Vyama vya Ushirika -Tume ya Maendeleo ya Vyama vya Ushirika iliyo chini ya Wizara ya Kilimo,  Udhibiti Collins Nyakunga, alipokuwa akizungumzq na waandishi wa habari katika Kongamano la vyama vya ushirika wa akiba na mikopo barani Afrika linaloendelea nchini Tanzania. Ambapo amesema pia kongamano hilo linatoa  fursa kwa washiriki kujadili mbinu bora za kuimarisha SACCOS na kuboresha huduma zinazotolewa kwa wanachama huku akisisitiza matumizi ya teknolojia, utoaji wa mikopo kwa ufanisi na usimamizi bora ni miongoni mwa maeneo muhimu kuimarisha sekta ya ushirika wa fedha na kuongeza manufaa kwa wanachama. Pia amesema vyama vya akiba na mikopo vinatakiwa  kuboresha huduma zake na kutumia teknolojia kuvutia vijana kujiunga navyo ili kuwawezesha kupata huduma za kifedha, kuanzisha biashara na kushiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji Kuhusu Tanzania kuwa mwenyeji wa kongamano hilo amesema imetokana na mafanikio yaliyopatikana katika usimamizi na uendelezaji wa sekta ya vyama vya ushirika wa akiba na mikopo nchini.Kongamano hilo linaonesha umuhimu wa kubadilishana uzoefu miongoni mwa nchi za Afrika katika kuboresha mifumo ya uendeshaji wa vyama hivyo na kuimarisha mchango wake katika maendeleo ya kiuchumi. Kwa mujibu wa Nyakunga, matumizi ya teknolojia ni miongoni mwa masuala yanayojadiliwa, yakilenga kuboresha utoaji wa mikopo, kuongeza ufanisi wa marejesho na kurahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha. “Huduma zinazozingatia mahitaji ya vijana zinaweza kuwa muhimu katika kuwahamasisha kujiunga na SACCOS, hasa wale wanaotaka kuanzisha biashara ndogo, kupanua shughuli za ujasiriamali au kuwekeza katika shughuli nyingine za kiuchumi.” Aidha, mikopo inayotolewa inapaswa kutumika kwa shughuli za uzalishaji na uwekezaji ili kuwasaidia wanachama kuongeza kipato, kuboresha maisha yao na kuimarisha uwezo wao wa kurejesha mikopo kwa wakati. Nyakunga amesema masuala mengine yanayojadiliwa katika kongamano hilo ni utawala bora, uwajibikaji na usimamizi wa rasilimali, ambayo ni muhimu katika kuhakikisha SACCOS zinaendeshwa kwa ufanisi na kulinda maslahi ya wanachama. Amesema kuimarisha mifumo ya usimamizi kutasaidia vyama hivyo kuboresha huduma zake, kuongeza imani ya wanachama na kuendeleza uhusiano mzuri kati ya taasisi hizo na watu wanaotafuta huduma za kifedha. Kongamano hilo, linaloratibiwa na Chama cha Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo Afrika (ACOSCA), linafanyika Tanzania kuanzia Oktoba 11 hadi 16, 2026, likitarajiwa kuwashirikisha wajumbe zaidi ya 600 kutoka Tanzania na nchi nyingine za Afrika. Ufunguzi rasmi umepangwa kufanyika Oktoba 15, ukitarajiwa kuongozwa na Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba. Kongamano hilo linatarajiwa kutoa nafasi ya kujifunza mbinu mpya za kuimarisha huduma za kifedha, kuongeza ufanisi wa SACCOS na kupanua fursa za wananchi kushiriki katika maendeleo ya kiuchumi.

Tue, 13 Oct 2026 14:42:43 +0000
Uncategorized · Daily News

Stakeholders push for stronger SACCOS across Africa

DAR ES SALAAM: SAVINGS and Credit Cooperative Societies (SACCOS) have been urged to strengthen financial services to meet members’ needs…

Recently
National · Issa Michuzi

SERIKALI KUENDELEA KUWEKEZA KATIKA SHUGHULI ZA UZALISHAJI ZA VIJANA: DKT MWIGULU

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema Serikali chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea kuweka mkazo katika kuwawezesha vijana na kuzipa kipaumbele shughuli zao za uzalishaji ili kuongeza mchango wao katika ukuaji wa uchumi wa Taifa. Dkt. Mwigulu ameyasema hayo wakati alipotembelea mabanda ya maonesho katika Maadhimisho ya Wiki ya Vijana 2026, yanayofanyika katika Viwanja vya Ndua, Manispaa ya Sumbawanga, mkoani Rukwa na kuona bunifu mbalimbali za vijana. Amesema dhamira ya Serikali ya kuwawezesha vijana inaonekana kupitia hatua mbalimbali zinazochukuliwa, ikiwemo kutenga Shilingi bilioni 200 kwa ajili ya kuwawezesha vijana kiuchumi. “Mara tu baada ya kumalizika kwa uchaguzi, Rais Dkt. Samia alitenga Shilingi bilioni 200 kwa ajili ya kuwezesha shughuli za vijana, na tunaona matunda yake,” amesema Dkt. Mwigulu. Ameeleza kuwa Serikali inafurahishwa na mwitikio wa vijana katika kujikita kwenye shughuli za uzalishaji, hali inayoonesha kuongezeka kwa matumizi ya fursa zinazopatikana kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi. Aidha, amesema Serikali itaendelea kuongeza bajeti kwa ajili ya shughuli za uzalishaji za vijana ili kupanua wigo wa wanufaika na kuwawezesha vijana wengi zaidi kushiriki katika shughuli za kiuchumi. “Vijana endeleeni kukua zaidi kimtaji ili uchumi wa Tanzania uweze kushikwa na Watanzania. Hongereni sana,” amesisitiza. Kadhalika, Dkt. Mwigulu amempongeza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Joel Nanauka, kwa kutekeleza kwa vitendo maono ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuifanya Wizara ya Vijana kuwa Wizara ya uzalishaji

Tue, 13 Oct 2026 14:35:40 +0000
Business · Jamhuri Media

Kongamano la 11 la Kitaifa la Kilimo Misitu kufanyika wiki ijayo Musoma

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Jamhuri Media

Leseni 74 za dhahabu zatolewa Nkasi, maombi 366 yachakatwa

Read the full report from the original source.

Recently
Health · The Standard

Oburu Oginga to leave hospital soon - ODM

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · DW Rwanda

Video — What happened to Germany's Transrapid?

To view this video please enable JavaScript, and consider upgrading to a web browser that supports HTML5 video

Recently
Uncategorized · DW Rwanda

Why Germany is backing tougher EU trade defenses against China

Read the full report from the original source.

Recently
Sports · Azam TV Videos

Simba SC 2-1 Yanga SC | Utamu wa Kariakoo Derby kwa dakika 4 | NBC PL 10/10/2026 (Montage)

KARIAKOO DERBY | Pata uhondo wa mechi ya Simba vs Yanga (2-1), iliyopigwa Oktoba 10/10/2026 kwenye Dimba la Uhuru, Dar es Salaam. Hii ni Ligi Kuu ya NBC...

2026-10-13T14:21:18+00:00
Uncategorized · Kigali Today

Nyuma y'u Rwanda, Komisiyo y'abahuza ya Afurika Yunze ubumwe igiye gukomereza Kinshasa

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · DW Rwanda

White House asks Ambassador to Greece Kimberly Guilfoyle to step down

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

Maraga vows to jail the corrupt if elected President

Maraga said his government would uphold the Constitution, respect the courts

Recently
Uncategorized · Mwanaspoti

Chuchu Hans; Miaka 10 na Ray bila ndoa, siri ni hii

Soma zaidi hapa

Recently
National · Issa Michuzi

WANAFUNZI LOIBORSIRET WAASWA KUJIPANGA NA MITIHANI YA KIDATO CHA NNE

Na Mwandishi Wetu, Simanjiro Wahitimu wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari Loiborsiret, wilayani Simanjiro, mkoani Manyara, wameaswa kutumia muda uliobaki kujisomea kwa bidii na kujiandaa kikamilifu kwa mitihani yao ya mwisho ili waweze kufanya vizuri na kufikia malengo yao ya kielimu. Wito huo umetolewa na Afisa Mtendaji wa Kata ya Loiborsiret, Charles Msangya, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 13 ya kidato cha nne ya shule hiyo. Msangya amewataka wahitimu 56 wa mwaka 2026 kutumia siku zilizobaki kabla ya kuanza kwa mitihani kujikumbusha masomo waliyofundishwa na kuimarisha maandalizi yao ili kupata matokeo mazuri. “Hatua mliyofikia kielimu hampaswi kuridhika nayo, safari bado ni ndefu. Nawaasa msisikilize maneno ya mitaani kwamba watu wasiosoma wana fedha. Hiyo ni mipango ya Mungu, lakini mtu mwenye elimu huwezi kumfananisha na ambaye hajasoma,” amesema Msangya. Aidha, amelizipongeza shirika lisilo la kiserikali la Namayana Foundation kwa kuahidi kununua mashine ya fotokopi kwa ajili ya shule hiyo, akieleza kuwa msaada huo utasaidia kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji. Kwa upande wake, Mkuu wa Shule ya Sekondari Loiborsiret, Mwalimu Fabian Amsi Doriye, amesema shule hiyo imeendelea kufanya vizuri katika mitihani ya kitaifa, ambapo kwa miaka miwili mfululizo wanafunzi wa kidato cha pili na cha nne wamepata ufaulu wa asilimia 100. Amesema wanafunzi 56 wanaotarajia kufanya mtihani wa kuhitimu kidato cha nne mwaka huu wameandaliwa ipasavyo, huku matarajio ya shule yakiwa ni kupata ufaulu wa madaraja ya kwanza na ya pili. Doriye, ambaye amekuwa mkuu wa shule hiyo tangu mwaka 2024, amesema mafanikio hayo yametokana na ushirikiano kati ya walimu, wanafunzi, wazazi na walezi katika kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora. Amesema shule hiyo imeendelea kuimarika pia kupitia miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali, ikiwemo ujenzi wa majengo mawili ya maabara yenye thamani ya shilingi milioni 30 kupitia fedha za mpango wa EP4R, pamoja na upatikanaji wa madarasa na nyumba za walimu. Ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwekeza katika miradi ya elimu inayolenga kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia. Naye mmoja wa wahitimu hao, Lena Nebuti, amesema ndoto yake ni kuwa mwanasheria, akieleza kuwa ana matumaini ya kufaulu mtihani wa kidato cha nne ili kuendelea na masomo na kutimiza azma hiyo.

Tue, 13 Oct 2026 14:15:31 +0000
Uncategorized · HabariLeo

Naibu Mwanasheria Mkuu akutana na Askofu Malasusa

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Issa Michuzi

ASA YATAMBULISHA MBEGU ZINAZOSTAHIMILI UKAME NA MVUA NYINGI

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Profesa Peter Msofe, amepongeza Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) kwa kuzalisha mbegu bora zenye uwezo wa kustahimili ukame na mvua nyingi, akisema zinaweza kusaidia wakulima kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa na kuimarisha usalama wa chakula nchini. Profesa Msofe ameyasema hayo Oktoba 13, 2026, alipotembelea banda la ASA katika maadhimisho ya kitaifa kuelekea Siku ya Chakula Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara, jijini Tanga. Akiwa katika banda hilo, alipata maelezo kuhusu mbegu ya mahindi aina ya T105, inayotajwa kuwa na uwezo wa kustahimili vipindi vya ukame na mvua nyingi, huku ikitarajiwa kutoa mavuno ya magunia 18 hadi 22, kutegemea ukubwa wa eneo na masharti ya uzalishaji. Afisa Masoko wa ASA, Suzan Ludovick, amesema mbegu hiyo ya uchavushaji huria ina uwezo wa kutoa hadi gunzi mawili kwa kila mmea, hivyo kuwapa wakulima fursa ya kuongeza uzalishaji wanapozingatia kanuni bora za kilimo. Amesema mbegu hiyo inapatikana kwa wakulima katika maonesho hayo, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuhamasisha matumizi ya mbegu bora zinazoweza kukabiliana na changamoto za hali ya hewa, zikiwemo ukame na mvua nyingi zinazoweza kuathiri uzalishaji wa mazao. Katika hatua nyingine, Profesa Msofe alipata maelezo kuhusu mbegu ya mpunga aina ya SARO 5, inayoweza kutoa mavuno ya magunia 30 hadi 40 kwa ekari, kutegemea mazingira ya kilimo na usimamizi wa shamba. Suzan amesema SARO 5 inafaa kwa kilimo cha mpunga katika maeneo ya mabondeni na inakubalika katika soko la mchele kutokana na harufu yake nzuri, sifa inayoweza kuongeza mvuto wa zao hilo kwa walaji. Ameeleza kuwa matumizi ya mbegu bora zinazolingana na mazingira ya wakulima, yakichanganywa na uzingatiaji wa kanuni bora za kilimo, ni muhimu katika kuongeza tija, kuimarisha uzalishaji wa chakula na kuboresha kipato cha wakulima. Juhudi za ASA za kuhamasisha matumizi ya mbegu bora zinatarajiwa kuchangia kuongeza uzalishaji wa mazao, kupunguza athari za mabadiliko ya hali ya hewa na kuimarisha upatikanaji wa chakula nchini.

Tue, 13 Oct 2026 13:25:42 +0000
Uncategorized · Citizen Digital

Nairobi Water announces 24-hour supply disruption across city estates

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Capital FM

Ichung’wah calls Gachagua a ‘fool’ over Gikomba claims

Latest · News

Recently

Page 694 of 1164 · 23275 stories