Search the region
23252 stories
EACC arrests teacher over 300K recruitment bribe
EACC said the suspect allegedly demanded Sh100,000 from each of the three jobseekers
RecentlyTARURA Rukwa yawezesha vikundi 21 vya vijana kupitia mpango wa CBRM
Read the full report from the original source.
RecentlySomalia CDF Hails Uganda’s Mentorship Role, Seeks More Training Partnership
The Chief of Defence Forces of the Somali National Army, Brig Gen Ibrahim Mohamed Mohamud, has praised Uganda’s training and mentorship support to his forces and appealed for further training…
RecentlyDr. Ayub Mukisa: Karamoja: Why Development Interventions Must Start by Listening to the People
As the Department for Critical Thinking and Alternative Analysis at the Karamoja Anti-Corruption Coalition (KACC), we are back with our Karamoja articles. This time, we analyse why development projects should…
RecentlyWoman killed, another critically injured in Kajiado stabbing incident
Read the full report from the original source.
RecentlyNTSA gives motorists two months to collect physical logbooks
Read the full report from the original source.
RecentlyRemembering RJ Mitte, The Trailblazer Who Redefined Disability In Hollywood
Entertainment · 5 hours ago
RecentlyKalonzo to outline opposition’s policy agenda at Chatham House
Latest · NATIONAL NEWS
RecentlyReasons for withdrawing retirement money: What Kenyans said
Capital needs for commercial ventures remain the primary motivation.
RecentlyTAASISI REVIVAL EDUCATION TRUST KUSAIDIA WANAFUNZI 100 KUREJEA SHULE
Na Mwandishi wetu SHIRIKA la Revival Education Trust limepanga kuwasaidia wanafunzi 100 kutoka familia zenye changamoto za kiuchumi kurejea shuleni mwaka ujao, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuwapa nafasi ya kuendelea na masomo na kutimiza ndoto zao. Akizungumza katika mahafali ya 20 ya Shule ya Sekondari Huria ya Ukonga Skillful, Muasisi wa shule hiyo ambayo ndio inalisimamia shirika hilo, Diodorus Tabaro amesema mpango huo unalenga wanafunzi waliolazimika kuacha shule kutokana na changamoto za kifedha, licha ya kuwa na uwezo na vipawa vya kufanikiwa kielimu. Amesema kati ya wanafunzi 100 watakaonufaika na mpango huo, 50 watapata nafasi za bweni, huku wengine 50 wakisoma bila kulala shuleni, ili kuwawezesha kuendelea na masomo kulingana na mazingira yao. Tabaro ameeleza kuwa mpango huo ni sehemu ya dhamira ya shirika hilo ya kufungua milango ya elimu kwa watoto wanaotoka katika familia zenye uhitaji, akisisitiza kuwa changamoto za kiuchumi hazipaswi kuwa kikwazo cha kutotimiza ndoto za watoto. Aidha, amesema kwa kutambua umuhimu wa kusaidia watoto wenye uhitaji, yeye binafsi ana mpango wa kugharamia masomo ya watoto saba katika mwaka wa masomo alioutaja awali, huku akiwahimiza watu wengine wenye uwezo kujitokeza kusaidia wanafunzi wanaokabiliwa na changamoto hizo. Ameongeza kuwa ushirikiano wa wadau mbalimbali ni muhimu katika kuhakikisha watoto wanaotoka katika familia zenye hali ngumu wanapata fursa ya elimu na kujenga maisha bora ya baadaye. Awali mgeni rasmi katika mahafali hayo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Can Tanzania, Sixbert Mwanga ameahidi kuchangia jumla ya Sh milioni 10 kwa kipindi cha miaka mitano mfululizo kupitia Taasisi ya Revival Education Trust iliyochini ya Shule ya Sekondari Huria ya Ukonga Skillful, kwa lengo la kusaidia wanafunzi wanaotoka katika familia zenye changamoto za kiuchumi kupata fursa ya elimu. Mwanga amesema katika safari yake ya elimu, alikumbana na changamoto ambazo zilimfanya atambue umuhimu wa kupata msaada, akibainisha kuwa baadhi ya wanafunzi hukosa fursa ya kuendelea na masomo kutokana na hali ngumu za kifamilia, hata pale wanapokuwa na uwezo wa kufanya vizuri kitaaluma. Amesema wapo wanafunzi ambao hushindwa kuendelea na masomo baada ya kutofaulu mitihani au kukosa uwezo wa kugharamia elimu, huku wengine wakipata nafasi ya kuendelea kutokana na msaada wa wazazi, ndugu au watu wengine wenye uwezo wa kifedha. Nao baadhi ya wanafunzi wamesema kuwa jambo la kusaidia baadhi ya wenzao wasiojiweza ni nzuri na wanaliunga mkono kwani lina lengo la kwenda kuwainua wale waliokata tamaa ya kuendelea na masomo kutokana na changamoto ya kifedha. Wamesema wanamtakia kila la kheri aliyebuni na kuja taasisi hiyo ya kuwasaidia wanafunzi wenzao wenye changamoto hiyo ya kifedha katika familia zao.
Tue, 13 Oct 2026 08:03:00 +0000Transport, mining sectors spur credit growth
DAR ES SALAAM: BANK lending to key economic activities accelerated in the period ending August this year, with mining and…
RecentlyWAZIRI SANGU AZINDUA MSIMU WA SEMINA ZA WASTAAFU WATARAJIWA WA PSSSF
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu, akizungumza kwenye Semina ya Maandalizi ya Kustaafu alipofanya ufunguzi wa Semina hiyo katika ukumbi Ukumbi wa Jjegoen Park Sumbawanga Mkoani Rukwa, Leo tarehe 12 Octoba 2026 Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu na Utawala, Bw. Paul Kijazi akizungumza wakati wa ufunguzi Semina ya Maandalizi ya Kustaafu katika ukumbi wa Jjaggoen Park Sumbawanga Mkoani Rukwa, Leo tarehe 12 Octoba 2026. Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko, Bw Hajji Khamis na Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu na Utawala, Bw. Paul Kijazi wakiendelea na utambulisho na utambuzi katika Semina ya Maandalizi ya Kustaafu katika ukumbi wa Jjaggoen Park Sumbawanga Mkoani Rukwa, Leo tarehe 12 Octoba 2026. Meneja wa Pensheni wa Mfuko Bw. Victor Kikoti akitoa mada wakati wa Semina ya Maandalizi ya Kustaafu iliyofanyika katika ukumbi wa Jjaggoen Park Sumbawanga Mkoani Rukwa, Leo tarehe 12 Octoba 2026. Afisa Matekelezo wa Mfuko wa PSSSF Bw. Frank Fute wakitoa mada wakati wa Semina ya Maandalizi ya Kustaafu iliyofanyika katika ukumbi wa Jjaggoen Park Sumbawanga Mkoani Rukwa, Leo tarehe 12 Octoba 2026. Afisa uwekezaji wa Mfuko, Bw. Filbert Francis Bagenda akitoa Mada wakati wa Semina ya Maandalizi ya Kustaafu iliyofanyika katika ukumbi wa Jjaggoen Park Sumbawanga Mkoani Rukwa, Leo tarehe 12 Octoba 2026. Mstaafu mtarajiwa Bw. Mohamed Suleiman Lugoya akiuliza swali wakati wa Semina ya Maandalizi ya Kustaafu iliyofanyika katika Ukumbi wa Jjegoen Park Sumbawanga Mkoani Rukwa, Leo tarehe 12 Octoba 2026 Mstaafu mtarajiwa Bi. Anthonia Amando Ndasi akiuliza swali na kuchangia Mada wakati wa Semina ya Maandalizi ya Kustaafu iliyofanyika katika Ukumbi wa Jjegoen Park Sumbawanga Mkoani Rukwa, Leo tarehe 12 Octoba 2026. Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mhe. Makongoro Nyerere kwenye picha ya pamoja na Viongozi wa Mfuko wa PSSSF walipotembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Na Mwandishi Wetu, Sumbawanga Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu, ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuimarisha mifuko ya hifadhi ya jamii na kuboresha utoaji wa huduma kwa wanachama na wastaafu, hususan katika ulipaji wa mafao kwa wakati. Mhe. Sangu ameyasema hayo Oktoba 12, 2026, mjini Sumbawanga, mkoani Rukwa, wakati akizindua msimu wa semina za kuwaandaa wastaafu watarajiwa wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kwa kipindi cha mwaka 2026/2028. Akizungumza katika uzinduzi huo, Waziri Sangu amesema mafanikio yaliyopatikana katika kuimarisha mifuko ya hifadhi ya jamii ni pamoja na ulipaji wa mafao kwa wakati, kuendelea kulipa madeni ya mifuko hiyo nao kuboresha kiwango cha chini cha pensheni kwa wastaafu. “Kwa kweli tuna kila sababu ya kumpongeza Rais wetu kwa kuhakikisha mifuko ya hifadhi ya jamii ikiwemo PSSSF inaimarika. Hivi sasa mafao yanalipwa kwa wakati, Serikali inaendelea kulipa madeni yake kwa mifuko ya hifadhi ya jamii, pensheni za kila mwezi zinalipwa kwa wakati, na kiwango cha chini cha pensheni kimeboreshwa. Hakika, hayo ni mafanikio makubwa ya Serikali ya Awamu ya Sita,” amesema Mhe. Sangu. Ameongeza kuwa, kiwango cha chini cha pensheni kwa wastaafu kimefikia Shilingi 250,000 kwa mwezi, akieleza kuwa hatua hiyo ni miongoni mwa maboresho yaliyofanywa na Serikali kwa lengo la kuimarisha ustawi wa wastaafu. Akizungumzia umuhimu wa semina hizo, ambazo zitafanyika katika mikoa ya Mwanza, Arusha, Dar es Salaam na Dodoma pamoja na Unguja kwa upande wa Zanzibar, Mhe. Sangu ameipongeza PSSSF kwa kuandaa mafunzo yanayolenga kuwaandaa watumishi wanaokaribia kustaafu kukabiliana na maisha baada ya kumaliza utumishi wa umma. “Ninawapongeza PSSSF kwa kuandaa semina hizi ambazo zinazinduliwa leo. Hakika, haya ni mafunzo muhimu yanayowaandaa wastaafu watarajiwa kuishi maisha bora baada ya kustaafu. Hongereni sana PSSSF, na ninawasihi semina hizi ziwe endelevu,” amesema. Akizungumzia kaulimbiu ya PSSSF ya ‘Tunalipa Jana’, Waziri Sangu amesema kaulimbiu hiyo inaakisi utekelezaji wa huduma za Mfuko katika kulipa mafao kwa wakati, akiwahimiza wastaafu watarajiwa kuwa na imani na Mfuko huo. “Kulipa Jana si nadharia, ni ukweli mtupu, na wengi wameshathibitisha hilo. Shukrani za pekee ziende kwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuiwezesha PSSSF kulipa jana. Hivyo, kuweni na amani kwani PSSSF ipo tayari kuwalipa,” amesema. Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mhe. Makongoro Nyerere, akitoa salamu za mkoa, ameitaka PSSSF kuendelea kuwa karibu na wastaafu na kuhakikisha wanapata mafao yao kwa usahihi na kwa wakati, akisisitiza kuwa Mfuko huo unapaswa kuwa chanzo cha faraja na uhakika kwa wanachama wake wanapomaliza utumishi. Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw. Paul Kijazi, amesema kuwa hadi Juni 30, 2026, Mfuko ulikuwa umelipa jumla ya wanachama 390,761 mafao yenye thamani ya Shilingi trilioni 12.94. Amesema PSSSF inaendelea kuimarisha mifumo yake ya utoaji huduma ili kuhakikisha wanachama wanaostahili wanapata mafao yao kwa wakati, akibainisha kuwa kaulimbiu ya ‘Tunalipa Jana’ inaendelea kuwa sehemu muhimu ya juhudi za Mfuko katika kuboresha huduma kwa wanachama na wastaafu. Akifafanua kuhusu maudhui ya semina hizo, Bw. Kijazi amesema washiriki watapatiwa elimu kuhusu usimamizi wa fedha na fursa mbalimbali za uwekezaji, ikiwemo uwekezaji katika viwanda vidogo na vya kati kulingana na uwezo wao, masoko ya fedha, kilimo-biashara na ujasiriamali. Amesema mafunzo hayo yanalenga kuwasaidia wastaafu watarajiwa kufanya maamuzi sahihi kuhusu matumizi na uwekezaji wa mafao yao, ili yaweze kuwapatia manufaa ya muda mrefu na kuwawezesha kukabiliana na mahitaji ya maisha baada ya kustaafu. Semina hizo zinawezeshwa na wadau mbalimbali, wakiwemo Azania Bank, NMB Bank, CRDB Bank, Amana Bank, Orbit Security, UTT, Watumishi Housing investment,, Absa Bank na NBC Bank, ambao wanatoa elimu na mwongozo kuhusu huduma za kifedha na fursa za uwekezaji kwa wastaafu watarajiwa wa PSSSF.
Tue, 13 Oct 2026 07:58:13 +0000India detains top ‘cockroach’ leaders after flash protest
Read the full report from the original source.
RecentlyWataalam kuamua Papa Leo XIV kufanyiwa upasuaji kuondoa uvimbe kwenye mapafu
Read the full report from the original source.
RecentlyDED KIBITI ASISITIZA UKAMILISHAJI WA MIRADI KWA WAKATI KIBITI
Mwamvua Mwinyi, Kibiti MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti, mkoani Pwani, Ramadhan Kimara, amewataka mafundi na wasimamizi wa miradi ya maendeleo kuhakikisha kazi zinakamilika kwa wakati, kwa kuzingatia mikataba na matumizi sahihi ya vifaa vya ujenzi. Kimara ametoa maelekezo hayo Oktoba 12, 2026, wakati akikagua ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Mkupuka yenye thamani ya Sh milioni 528, iliyopo katika Kijiji cha Mkupuka wilayani Kibiti. Akiwa katika eneo la mradi huo, Kimara amezungumza na fundi pamoja na msimamizi wa ghala la vifaa vya ujenzi, akiwataka kuhakikisha vifaa vinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na kazi inakamilika ndani ya muda uliowekwa kwenye mkataba. Aidha, amemtaka Mhandisi wa mradi kutembelea eneo la ujenzi mara kwa mara ili kufuatilia maendeleo ya kazi na kushughulikia changamoto zinazoweza kujitokeza wakati wa utekelezaji. “Mjulisheni Mhandisi wa mradi ahakikishe muda wote anafika katika eneo la ujenzi ili kusiwe na changamoto zozote katika ujenzi huu,” amesisitiza Kimara. Katika ziara hiyo, Kimara pia ametembelea Kijiji cha Nyamisati, Kata ya Salale, ambako amekagua Kiwanda cha Samaki kwa lengo la kujionea hali ya miundombinu iliyopo na kubaini changamoto zinazokikabili. Ukaguzi wa kiwanda hicho ulilenga kutathmini hali yake na kubaini maeneo yanayohitaji kufanyiwa kazi ili kuwezesha shughuli za uzalishaji kuanza au kuimarishwa. Hatua hiyo inalenga kuongeza mapato ya Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti, kukuza uwekezaji na kuchochea shughuli za kiuchumi zitakazochangia maendeleo ya wilaya hiyo.
Tue, 13 Oct 2026 07:52:43 +0000Is Tanzania getting maximum economic value from its gold?
DAR ES SALAAM: THE head of the Bank of Tanzania’s (BoT) gold purchasing section announced a significant milestone: gold acquisitions…
RecentlyTechnical University of Kenya advertises 25 jobs
TUK is hiring a senior lecturer, 21 lecturers, two nurses and a chief internal auditor.
RecentlyChina yawawekea vikwazo mawaziri wa Paraguay na Belize
Read the full report from the original source.
RecentlySILINDE APONGEZA TEKNOLOJIA ZA KILIMO BANDA NAESA, ATOA MAAGIZO
Naibu Waziri wa Kilimo, David Silinde (Mb) ameipongeza Wakala wa Taifa ya Huduma za Ugani (NAESA) kwa kazi zinazofanywa kusaidia Wizara ya Kilimo kutekeleza majukumu yake, huku akifurahishwa na teknolojia ya uchakataji wa mpunga kwa kutumia mvuke inayosaidia kupata mchele wenye ubora na kupunguza kuvunjika kwa punje wakati wa kusaga. Silinde ametoa pongezi hizo Oktoba 12, 2026, alipotembelea banda la NAESA katika maadhimisho ya kitaifa ya kuelekea Siku ya Chakula Duniani, yaliyofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara, jijini Tanga, ambapo alijionea teknolojia mbalimbali zinazolenga kuongeza thamani ya mazao na kuboresha uzalishaji wa chakula. Amesema kuanzishwa kwa NAESA kuna umuhimu mkubwa katika kusaidia utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Kilimo, hususan kuratibu na kusimamia huduma za ugani nchini na kuhakikisha wakulima wanapata elimu, teknolojia na ushauri wa kitaalamu unaoweza kuongeza tija katika uzalishaji. Akizungumzia teknolojia ya uchakataji wa mpunga kwa kutumia mvuke (parboiling), Silinde amefurahishwa na namna mfumo huo unavyosaidia kuimarisha punje za mchele na kupunguza kuvunjika kwake wakati wa kusaga, hatua inayoweza kumwezesha mkulima kuongeza thamani ya mazao yake na kupata manufaa zaidi kiuchumi. Katika hatua nyingine, ameitaka NAESA kuimarisha usimamizi wa huduma za ugani nchini na kuwasilisha taarifa kwa Wizara ya Kilimo kila wiki kuhusu mwenendo wa shughuli za kilimo katika maeneo mbalimbali, ili kubaini changamoto zinazowakabili wakulima na kuwezesha hatua za haraka kulingana na mahitaji halisi ya maeneo husika. Kwa upande wake, Kaimu Meneja wa Sehemu ya Masoko na Uongezaji Thamani ya Mazao wa NAESA, Bi. Esther Mwaisango, amesema taasisi hiyo imeanzishwa kwa mujibu wa sheria na wamejipanga kuhakikisha wanaongeza tija kwenye uzalishaji ili upatikanaji wa chakula uwe mzuri. Aidha Mwaisango amesema NAESA imeshiriki maadhimisho hayo kuonyesha teknolojia mbalimbali za usindikaji wa mazao na kuwafahamisha wananchi namna zinavyoweza kutumika kuongeza thamani ya mazao ya kilimo. Aidha Bi. Mwaisango amesema NAESA inaendelea kuandaa mafunzo kwa maafisa ugani katika halmashauri mbalimbali kuhusu tafsiri ya taarifa za mvua na namna ya kuzitumia kutoa ushauri sahihi kwa wakulima. Akielezea teknolojia ya uchakataji wa mpunga kwa kutumia mvuke, Mkufunzi kutoka Chuo cha Uhaulishaji Teknolojia za Kilimo (MATI Ilonga), Kilosa mkoani Morogoro, Bw. Hamis Abdalah Ramadhani, amesema mfumo huo unahusisha kuloweka mpunga kabla ya kuupitisha kwenye mchakato wa mvuke, unaosaidia kuimarisha punje na kupunguza kuvunjika wakati wa kusaga.
Tue, 13 Oct 2026 07:47:55 +0000Matiang’i: Forming Opposition coalition won’t be easy
Opposition still negotiating power-sharing terms ahead of the 2027 polls
RecentlyPage 704 of 1163 · 23252 stories