Unganishwa

Search the region

23203 stories

Uncategorized · Daily News

Who Defines Africa’s Problems?

AFRICA: International partnerships can provide laboratories, technology, expertise, training and access to global scientific networks that many African institutions would…

Recently
Uncategorized · Daily News

Could Tanzania miss the manufacturing opportunity?

DAR ES SALAAM: Africa is becoming increasingly important to the global transition towards cleaner energy, with countries across the continent…

Recently
National · Issa Michuzi

Serikali, Vodacom Tanzania Foundation Waongeza Upatikanaji wa Mafunzo ya Kidijitali kwa Walimu Nchini

-Ni kituo cha kwanza kati ya 50 vinavyotarajiwa kujengwa katika maeneo mbalimbali hapa nchini -Kupitia ushirikiano wa TIE na Vodacom Tanzania Foundation, maelfu ya Walimu watanufaika na mafunzo ya kidijitali yatakayoboresha uwezo wa ufundishaji na matumizi ya TEHAMA Arusha, Tanzania – 9 Oktoba 2026; Maelfu ya walimu nchini sasa watanufaika na upatikanaji wa mafunzo ya maendeleo ya kitaaluma kupitia matumizi ya teknolojia, hatua inayolenga kuongeza umahiri wa ufundishaji, kuongeza ufaulu wa wanafunzi na kuchochea maendeleo ya taifa kupitia elimu. Mafanikio hayo yanatokana na ushirikiano kati ya Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE) na Vodacom Tanzania Foundation katika utekelezaji wa Programu ya Mafunzo Endelevu ya Walimu Kazini (TCPD/MEWAKA), ambayo imeimarisha matumizi ya Mfumo wa Usimamizi wa Kujifunza (LMS) pamoja na Vituo vya Rasilimali za Walimu (TRC) nchini. Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi na kuzindua kituo cha Rasilimali za Walimu kilichojengwa shule ya Msingi Naurei, wilayani Arusha, kikiwa ni cha kwanza kati ya 50 vinavyotarajiwa kujengwa hapa nchini, Mkuu wa wilaya ya Arumeru Neema Lugangira alisema uwekezaji kwa walimu ni uwekezaji wa moja kwa moja katika kuongeza uwezo wa kufundisha kwa kutumia TEHAMA, na kwa ujumla mustakabali wa elimu nchini. “Leo nimekuja kuzindua kituo hiki, hili sio jambo dogo maana kituo hiki kitaongeza ubora wa elimu hapa nchini, na pia ni uthibitisho kwamba serikali na sekta binafsi zikishirikiana kuimarisha miundombinu, teknolojia na mifumo inayomwezesha mwalimu kujifunza na kujiendeleza wakati wote matokeo yake ni kuboresha elimu kwa ujumla wake. Mwalimu anayepata maarifa mapya, anayeongeza kiwango cha elimu alichonacho na kutumia teknolojia kwa ufanisi, huongeza nafasi ya wanafunzi kufaulu na kufikia ndoto zao,” alisema Mh Lugangira. Alisema tathmini ya mahitaji ya TCPD/MEWAKA iliyohusisha Vituo vya Rasilimali za Walimu 178, walimu 350 na wadau mbalimbali imebaini kuwa walimu wengi wana hamasa ya kujifunza na kutumia teknolojia, huku asilimia 99 wakifahamu LMS na asilimia 71 wakiwa na uelewa wa msingi wa TEHAMA. Hata hivyo, tathmini hiyo imeonesha kuwa changamoto za upatikanaji wa vifaa vya TEHAMA, kompyuta, intaneti na usaidizi wa kiufundi bado zinaendelea kuathiri matumizi kamili ya mfumo huo, hasa katika maeneo ya vijijini. “Mafanikio ya TCPD/MEWAKA hayategemei motisha ya mwalimu pekee. Yanahitaji uwekezaji katika vifaa, uwepo wa intaneti, mafunzo ya vitendo na mifumo imara. Ndio maana ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi una umuhimu mkubwa katika kuhakikisha walimu wanapata mazingira bora ya kujifunza,” alisisitiza. Mkuu wa Wilaya pia aliipongeza Vodacom Tanzania Foundation kwa mchango wake katika kuendeleza elimu nchini na kuzihamasisha taasisi nyingine za sekta binafsi kuunga mkono juhudi hizo. Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Foundation, Zuweina Farah alisema uwekezaji katika walimu ni moja ya njia zinazoleta matokeo makubwa katika kuboresha mfumo wa elimu na kukuza uchumi wa kidijitali wa taifa. “Tunafahamu kuwa walimu ndiyo nguzo ya maendeleo ya elimu. Wanapopewa fursa za kujifunza na kutumia teknolojia kwa ufanisi, matokeo chanya huonekana moja kwa moja kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla. Hii ndiyo sababu Vodacom Tanzania Foundation imeamua kuwekeza katika mifumo na miundombinu inayowezesha maendeleo ya walimu kwa njia endelevu,” alisema Farah. Aliongeza kuwa kupitia ushirikiano na TIE, matumizi ya LMS yameondolewa gharama za data kwa watumiaji wa mtandao wa Vodacom, hatua iliyolenga kupunguza vikwazo vya upatikanaji wa maudhui ya maendeleo ya kitaaluma kwa walimu. “Kupitia ushirikiano wetu na TIE, walimu wanaotumia mtandao wa Vodacom wanaweza kuifikia LMS bila gharama yeyote. Tunaamini teknolojia ina uwezo mkubwa wa kuondoa vikwazo vya upatikanaji wa elimu na kuhakikisha walimu wengi zaidi wanapata fursa ya kuendeleza taaluma zao bila kujali mahali walipo,” alisema. Farah aliongeza kuwa sekta binafsi inaweza kuharakisha utekelezaji wa mipango ya elimu kwa kuwekeza katika teknolojia, muunganisho wa intaneti, vifaa vya TEHAMA, ubunifu na utaalamu wa kidijitali unaohitajika ili kujenga mfumo wa elimu unaoendana na mahitaji ya karne ya 21. Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Neema Lugangira (katikati) na Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Foundation, Zuweina Farah (wa pili kutoka kulia) wakikata utepe wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kituo cha kwanza kati ya 50, vinavyojengwa kwa ajili ya Rasilimali za Walimu katika Shule ya Msingi Naurei, wilayani Arusha, wakiwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya, Selemani Msumi (wa kwanza kushoto), Mkuu wa Shule, Getrude Tarimo (wa tatu kutoka kushoto) na wanafunzi tukio hilo limefanyika mwishoni mwa wiki jijini Arusha. Kituo hicho kimejengwa kupitia ushirikiano wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE) na Vodacom Tanzania Foundation kwa lengo la kuimarisha mafunzo ya kidijitali kwa walimu na kuboresha ubora wa elimu nchini. Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Neema Lugangira (wa tatu kutoka kulia) na Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Foundation, Zuweina Farah (wa tatu kutoka kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine wa Serikali na uongozi wa Shule ya Msingi Naurei katika Kituo cha Rasilimali za Walimu kilichozinduliwa rasmi shuleni hapo, Kituo hicho kimeanzishwa kupitia ushirikiano wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE) na Vodacom Tanzania Foundation kwa lengo la kuimarisha mafunzo ya kidijitali kwa walimu na kuboresha ubora wa elimu nchini. Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Foundation, Zuweina Farah, akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Rasilimali za Walimu katika Shule ya Msingi Naurei, wilayani Arusha. Kituo hicho kimeanzishwa kupitia ushirikiano wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE) na Vodacom Tanzania Foundation kwa lengo la kuwekeza katika maendeleo ya walimu kwa kutumia teknolojia na miundombinu ya kidijitali, ili kuwawezesha waalimu walio kazini kujiendeleza kitaaluma, kuboresha mbinu za ufundishaji na hatimaye kuongeza ubora wa elimu kwa wanafunzi nchini. Baadhi ya vifaa vya TEHAMA vilivyowekwa katika Kituo cha Rasilimali za Walimu katika Shule ya Msingi Naurei, wilayani Arusha, kituo hiki kimejengwa kupitia ushirikiano wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE) na Vodacom Tanzania Foundation kwa lengo la kuwawezesha walimu walio kazini kupata mafunzo ya kidijitali na kuimarisha uwezo wao wa kutumia teknolojia katika ufundishaji. Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Neema Lugangira, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa Kituo cha Rasilimali za Walimu katika Shule ya Msingi Naurei, wilayani Arusha. Alisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi katika kuimarisha miundombinu na matumizi ya teknolojia ili kuwawezesha walimu kujiendeleza kitaaluma, kuboresha mbinu za ufundishaji na kuongeza ubora wa elimu nchini. Muonekano wa jengo la Kituo cha Rasilimali za Walimu (TRC) katika Shule ya Msingi Naurei, wilayani Arusha. Kituo hicho ni cha kwanza kati ya vituo 50 vinavyotarajiwa kujengwa nchini kupitia ushirikiano wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE) na Vodacom Tanzania Foundation, kwa lengo la kuongeza upatikanaji wa mafunzo ya kidijitali na TEHAMA kwa walimu, kuimarisha mbinu za ufundishaji na kuboresha ubora wa elimu nchini.

Mon, 12 Oct 2026 04:30:00 +0000
Uncategorized · Mwananchi

Rekodi za Dabi ya Kariakoo 2026

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Daily News

Tanzania must learn from Africa’s costly mining deals

DAR ES SALAAM: As competition for Africa’s minerals intensifies, Tanzania faces another major challenge: how to negotiate mining agreements that…

Recently
Business · Issa Michuzi

BANGU: KIWANGO STAHIKI CHA UNYEVU KWENYE KOROSHO KIZINGATIWE

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB), Bw. Asangye Bangu, amewataka wakulima na waendesha ghala kuhakikisha korosho zinakidhi kiwango stahiki cha unyevu ili kulinda ubora na thamani ya zao hilo katika msimu wa mauzo wa 2026/27. Akizungumza Oktoba 11, 2026 katika ghala la BUCO lililopo Masasi mkoani Mtwara, linaloendeshwa na Kampuni ya Pugna, Bw. Bangu amesema hayo wakati akihitimisha ziara maalum ya ukaguzi wa maghala katika mikoa ya Lindi na Mtwara, iliyolenga kujiridhisha na utayari wa ghala kupokea na kuhifadhi korosho pamoja na kuchukua tahadhari dhidi ya athari zinazoweza kusababishwa na mvua nyingi. Amesema ukaguzi huo umehusisha tathmini ya uimara wa paa, hali ya sakafu, mifumo ya kuondoa maji, mazingira ya uhifadhi, taratibu za upokeaji wa korosho pamoja na uhakiki wa ubora na kiwango stahiki cha unyevu ili kuhakikisha mazao ya wakulima yanahifadhiwa katika mazingira salama. Aidha, Bw. Bangu amewasisitiza wakulima kuhakikisha wanakausha korosho vizuri kabla ya kuziwasilisha kwenye ghala, huku akiwataka waendesha maghala kuzingatia viwango vya ubora wakati wa upokeaji na uhifadhi ili kuepusha uharibifu unaoweza kusababisha kushuka kwa thamani ya zao hilo. Mkurugenzi Bangu pia amezielekeza AMCOS kutopokea korosho ambazo hazijakauka vizuri na kuhimiza ziendelee kutoa elimu kwa wa wakulima namna ya kukausha korosho. "Niwatake waendesha ghala kufanya ukaguzi wa mara kwa mara na kurekebisha mapungufu yanayoweza kuhatarisha usalama wa korosho, hususan kipindi cha mvua nyingi. Sisi WRRB tutaendelea kuimarisha ukaguzi na kushirikiana na wadau wote kuhakikisha mazao ya wakulima yanalindwa na Mfumo wa Stakabadhi za Ghala unaendelea kuaminika," amesema Bw. Bangu.

Mon, 12 Oct 2026 08:10:58 +0000
Uncategorized · Daily News

Kigamboni VETA college to open some programmes next month

KIGAMBONI: THE construction of Kigamboni Vocational Education and Training Authority (VETA) College has reached 85 per cent, with some training…

Recently
Uncategorized · PML Daily

NWSC shifts focus from numbers served to lives changed, MD Dr. Silver Mugisha tells IWA podcast

GLASGOW, Scotland — National Water and Sewerage Corporation (NWSC) Managing Director Dr Eng Silver Mugisha says the corporation is shifting its focus from how many Ugandans it serves to the impact...

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

Raila's long-serving aide Maurice Ogeta recounts his final moments in India

Read the full report from the original source.

Recently
National · Issa Michuzi

WABUNGE WA EALA WAPONGEZA SERIKALI YA SAMIA UJENZI WA UWANJA WA AFCON ARUSHA

NA DENIS MLOWE, ARUSHA WABUNGE wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) wameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji katika ujenzi wa uwanja wa kisasa mkoani Arusha, unaotarajiwa kutumika katika maandalizi ya mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027. Wabunge hao walitoa pongezi hizo wakati walipotembelea eneo la ujenzi wa uwanja huo jijini Arusha, ambapo walipata fursa ya kujionea mradi huo na kujadili umuhimu wake katika kukuza michezo, utalii na uchumi wa Tanzania pamoja na ukanda wa Afrika Mashariki. Akizungumza kwa niaba ya wabunge wenzake, Mbunge wa EALA, Cosato Chumi, alisema ujenzi wa uwanja huo ni hatua kubwa inayodhihirisha uwezo wa Tanzania kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati pale dhamira na rasilimali zinapowekwa katika kufikia malengo ya taifa. “Kwa kweli ni jambo kubwa, si jambo dogo. Huu ni uthibitisho kwamba Watanzania tukiamua tunaweza,” alisema Chumi. Alisema maandalizi ya AFCON yanatoa fursa muhimu kwa Tanzania kuimarisha miundombinu ya michezo na kuweka mazingira yatakayoiwezesha nchi kuendelea kuwa mwenyeji wa mashindano makubwa hata baada ya michuano hiyo kumalizika. Chumi alisisitiza kuwa uwanja huo haupaswi kutumika kwa kipindi cha AFCON pekee, bali unapaswa kuwa kituo cha kudumu cha kuandaa mechi za kimataifa, mashindano ya klabu na matukio mengine makubwa ya michezo yatakayovutia timu na mashabiki kutoka mataifa mbalimbali. Alisema ni muhimu kwa wadau wa michezo kuanza kupanga mapema namna ya kutumia miundombinu hiyo, ikiwemo kuandaa mashindano ya klabu kutoka Afrika Mashariki na Kati na kualika timu kubwa za bara la Afrika. Alitaja uwezekano wa kuzialika klabu zenye majina makubwa kama Gor Mahia na AFC Leopards za Kenya, Mamelodi Sundowns na Kaizer Chiefs za Afrika Kusini, pamoja na Vipers na URA za Uganda, ili kushiriki mechi za kirafiki na mashindano yatakayoongeza ushindani wa soka katika ukanda huo. Alisema hatua hiyo itazipa klabu za Tanzania fursa ya kupima uwezo wao dhidi ya timu zenye uzoefu wa mashindano ya kimataifa, huku ikisaidia kuboresha viwango vya wachezaji na kuinua ubora wa soka la ndani. Aidha, alieleza kuwa uwanja huo unaweza kuwa chachu ya kukuza utalii wa michezo mkoani Arusha, kutokana na uwezo wa kuvutia wageni, mashabiki na wadau wa soka ambao watatumia huduma mbalimbali za kitalii na kibiashara wakati wa mashindano. Alisema kuongezeka kwa wageni kutafungua fursa za kiuchumi kwa wafanyabiashara, watoa huduma za malazi, usafiri, migahawa na biashara ndogondogo, huku vijana wakipata nafasi za ajira katika sekta zinazohusiana na michezo. Chumi alitoa wito kwa Serikali, wabunge, vyama vya michezo na sekta binafsi kushirikiana kuandaa mikakati ya kuhakikisha uwanja huo unatumika kwa tija na kuendelea kuingiza manufaa kwa taifa kwa miaka mingi. Alisema ni wajibu wa wadau kuanza kufikiria namna ya kuandaa mashindano ya kimataifa mara baada ya AFCON, badala ya kusubiri hadi michuano hiyo imalizike ndipo waanze kutafuta matumizi mengine ya uwanja huo. Chumi alisema uwekezaji unaofanyika katika miundombinu ya michezo ni fursa ya kuendeleza vipaji vya vijana na kuiweka Tanzania katika nafasi nzuri ya kushiriki na kuandaa mashindano makubwa ya kimataifa. Ujenzi wa uwanja huo ni sehemu ya maandalizi ya Tanzania kuwa mwenyeji mwenza wa AFCON 2027 pamoja na Kenya na Uganda. Mashindano hayo yanatarajiwa kutoa fursa ya kuimarisha ushirikiano wa kikanda na kuongeza mwonekano wa Afrika Mashariki katika ramani ya soka la Afrika. Wadau wa michezo wanatarajiwa kunufaika na miundombinu hiyo kupitia maandalizi ya mashindano, mafunzo na shughuli nyingine zinazohusiana na michezo, huku matumizi endelevu ya uwanja yakitarajiwa kuwa muhimu katika kuhakikisha uwekezaji huo unaendelea kuleta matokeo chanya hata baada ya AFCON. Ziara ya wabunge wa EALA inaonesha umuhimu wa ushirikiano wa kikanda katika kukuza michezo na kutambua fursa zinazoweza kupatikana kupitia uwekezaji wa miundombinu, hususan katika kuimarisha soka, utalii na shughuli za kiuchumi katika nchi za Afrika Mashariki.

Mon, 12 Oct 2026 08:09:23 +0000
Uncategorized · The Citizen

Dual citizenship: Is diaspora’s political involvement helpful?

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Isango Star

Ibicuruzwa bifite agaciro ka miliyari 30 Frw nibyo byahiriye mu nkongi yafashe isoko rya GOICO

Ibicuruzwa bifite agaciro k’ibanze ka miliyari 30 Frw ni byo byahiriye mu nkongi y’umuriro yafashe isoko rya GOICO mu Karere ka Musanze ku wa Gatandatu, ku wa 10 Ukwakira (10) 2026, nk’uko byatangajwe n’ubuyobozi bw’Intara y’Amajyaruguru. Ni mu gihe abantu 17 bajyanywe kwa muganga nyuma y’iyo nkongi, barimo babiri bakomerekejwe n’umuriro,15 bamaze gusezererwa.

Mon, 12 Oct 2026 09:42:02 +0200
Uncategorized · The Ankole Times

Uganda Independence at 64: Four Decades Later, Family Seeks Recognition for Teso NRA Mobiliser Capt. Ongodia

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · PML Daily

NWSC MD Dr. Silver Mugisha asks Danish pump maker Grundfos to make pumps, spare parts in Uganda

GLASGOW, Scotland — National Water and Sewerage Corporation (NWSC) Managing Director Dr Eng Silver Mugisha has asked Danish pump maker Grundfos to partner with National Enterprise Corporation (NEC) to manufacture pumps..

Recently
Uncategorized · Watchdog Uganda

Dr. Ayub Mukisa: When the Abnormal Becomes Normal: Morality and Vulgarity in Uganda — A Rejoinder

On 5 October 2026, Watchdog News published an article by Dr. Nestor Basemera titled “Bye-Bye Morals, Welcome Vulgarity: Uganda’s New Normal.” In a similar vein, the Department for Critical Thinking…

Recently
Uncategorized · Watchdog Uganda

Kadaga Leads EALA Oversight Mission as Arusha Stadium Edges Toward AFCON 2027 Handover

Rt. Hon. Rebecca Alitwala Kadaga, Uganda’s First Deputy Prime Minister, Minister for East African Community Affairs, and Chairperson of the EAC Council of Ministers, has led an East African Legislative…

Recently
Uncategorized · KBC

Dozens of gold prospectors killed in strikes on Egypt-Sudan border, rights group says

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Capital FM

1 in 4 Kenyans lives in multidimensional poverty: UNDP

Latest · Africa

Recently
Business · Jamhuri Media

Bangu: Kiwango stahiki cha unyevu kwenye korosho kizingatiwe

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Daily News

Rosemary’s National Costume triumph at Miss Global 2026

DAR ES SALAAM: TANZANIA may not have secured a place in the final five at Miss Global 2026, but Rosemary…

Recently

Page 727 of 1161 · 23203 stories