Search the region
22509 stories
Pickleball ni mchezo gani? Kocha afunguka
Athuman Hamisi, kocha wa mchezo wa Pickeball kupitia kipindi cha #SportsAM kinachoongozwa na @hassanahmedy_ anatupatia darasa maalumu kuhusu mchezo huo, akieleza namna unavyochezwa, kanuni zake na mambo muhimu ambayo wadau wanapaswa kuyafahamu. Kwa upande mwingine Mratibu wa Mashindano ya Pickeball , Dkt. Sajad Habib Rai amefunguka tarehe ya kuanza kwa msimu wa tatu wa mashindano hayo.
2026-11-22T09:51:34+00:00Ruto moves to balance US, China interests in scramble for Kenya's strategic minerals
President William Ruto has previously ruled out choosing between Washington and Beijing, saying Kenya would pursue multiple partnerships based on its interests
RecentlyNGORONGORO YAWATEKA WAHARIRI, YAJIPANGA KUPOKEA WAGENI AFCON 2027
Wahariri wa vyombo vya habari nchini kupitia Jukwaa la Wahariri wamevutiwa na maajabu ya Hifadhi ya Ngorongoro baada ya kutembelea hifadhi hiyo na kujionea vivutio mbalimbali vya utalii pamoja na urithi wake wa kihistoria na kiutamaduni. Wakiongozwa na Mwenyekiti wa Jukwaa hilo, Deodatus Balile, wahariri hao walipata maelezo kuhusu ushahidi wa kisayansi unaothibitisha uwepo wa binadamu wa kale katika Bonde la Olduvai, pamoja na simulizi ya mchanga unaohama maarufu kama mchanga wa mahaba. Akizungumza na wahariri hao, Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Dkt. Abdul-Razaq Badru, amesema hifadhi hiyo ina mvuto wa kipekee kutokana na utajiri wa vivutio vya utalii na urithi wa utamaduni. Amesema kuelekea Mashindano ya AFCON 2027, Ngorongoro imejipanga kupokea wageni kwa kuboresha miundombinu na huduma za utalii, ikiwemo mifumo ya malipo na ujenzi wa barabara yenye tabaka gumu kutoka Lango la Loduare hadi Seneto yenye urefu wa kilomita 29.5. Aidha, amesema maboresho yanafanyika katika kivutio cha Maporomoko ya Maji ya Endoro, yakihusisha ujenzi wa ofisi za kisasa za kutolea huduma na njia za watembea kwa miguu. Kwa upande wake, Balile amesema Ngorongoro ni mdau muhimu katika kuchangia pato la taifa na kuboresha huduma kwa wananchi kupitia mapato ya utalii, akiahidi kuwa Jukwaa la Wahariri litaendelea kutoa ushauri na kushirikiana kwa karibu na mamlaka hiyo katika kuendeleza hifadhi.
Sun, 22 Nov 2026 10:08:40 +0000Biioni 4.2/- zasogeza huduma za mahakama karibu na wananchi Lushoto – Prof. Shemdoe
Read the full report from the original source.
RecentlyDKT. MWIGULU ASEMA MIGOGORO YA ARDHI ISICHOCHEE VISASI
▪️ Aonya dhidi ya kujichukulia sheria mikononi na kuuza ardhi kinyemela ▪️ Serikali yakamilisha usanifu wa barabara ya njia sita kutoka Picha ya Ndege hadi Chalinze WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, amekemea tabia ya watu kujichukulia sheria mkononi na kuonya kuwa Serikali haiungi mkono uvunjaji wa sheria wa makusudi. “Tusiruhusu uvunjifu wa sheria wa makusudi kwa sababu utaua udugu wetu uliokuwepo kwa miaka mingi. Lazima tuzingatie utawala wa sheria, tuache utaratibu wa uvunjifu wa sheria na kujichukulia sheria mkononi,” amesisitiza. Akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Viwanja vya Polisi, wilayani Chalinze, mkoani Pwani, jana jioni (Jumamosi, Novemba 21, 2026), Waziri Mkuu alisema mmomonyoko wa utawala wa sheria unaalika visasi na makovu yasiyopona. “Tusibaguane au kuchukiana kwa sababu ya ardhi kwani yenyewe haiongezeki lakini mahitaji ya ardhi yanaongezeka. Tunatakiwa tuweke nguvu kubwa katika kupanga matumizi bora ya ardhi na tuheshimu sheria,” alisisitiza. Dkt. Mwigulu alisema Serikali haitavumilia vitendo vinavyofanywa na baadhi ya watu vya kulisha mifugo kwenye mashamba ya watu wengine kwa makusudi, kujeruhi mifugo au kushambulia watu kwa kulipiza kisasi. “Kama mifugo yako inapenda kula mazao ya mashambani, basi lima mashamba yako kisha uingize mifugo yako shambani mwako. Mambo ya kuchukua chukua sheria mkononi yanaalika visasi. Na damu ikimwagika katika ardhi inaleta laana,” alisema. Aliwaagiza viongozi wa wilaya na vijiji washughulikie migogoro hiyo kwa mujibu wa sheria, huku akikemea uuzaji wa ardhi kinyemela na kusisitiza kuwa kosa la mtu mmoja halipaswi kugeuzwa kuwa kosa la jamii nzima. Kwa upande wake, Mbunge wa Chalinze ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete, alisema uchunguzi wa mgogoro wa mipaka kati ya vijiji vya Pingo na Chamakweza umekamilika na taarifa yake iko tayari kwa hatua zinazofuata. Alitumia fursa hiyo kuishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kupeleka miradi mingi kwenye Halmashauri ya Wilaya hiyo, ikiwemo ya maji, elimu, afya na barabara. “Wakati naanza ubunge, hatukuwa na Hospitali ya Wilaya lakini hivi sasa tumekamilisha ujenzi wake na tumepata shilingi bilioni tatu za ujenzi wa ICU,” alisema. Alisema zamani, pakitokea ajali yoyote kati ya Kabuku (Tanga) na Chalinze (Pwani), walikuwa wakikimbilia Hospitali ya Tumbi ili kupeleka majeruhi huko, lakini kwa sasa hawatalazimika kuitegemea tena hospitali hiyo kwani wamepata kitengo cha wagonjwa wa dharura (EMD) cha kisasa kabisa. Naye, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Kaspar Mmuya, alisema vijiji hivyo ni miongoni mwa vijiji 16 vilivyopangwa kuandaliwa mipango bora ya matumizi ya ardhi mwaka huu ili kusaidia kutatua migogoro iliyodumu kwenye maeneo hayo. Katika hatua nyingine, Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, alisema Serikali imekamilisha usanifu wa barabara ya njia sita yenye urefu wa kilometa 74, kutoka Picha ya Ndege hadi Chalinze, inayotarajiwa kutekelezwa kupitia ubia kati ya Serikali na sekta binafsi (PPP). Alisema uthamini wa maeneo yanayohitajika kwa ajili ya mradi huo unaendelea, huku Serikali pia ikipanga kuboresha barabara iliyopo ya Dar es Salaam–Kibaha–Mlandizi–Chalinze ili kupunguza msongamano wa magari.
Sat, 21 Nov 2026 14:38:53 +0000NRM Treasurer Nekesa Urges Namayingo Crowds to Embrace Four-Acre Model, PDM as MP Mukisa Introduces Husband to Parents
NAMAYINGO — In a powerful blend of family celebration and political mobilisation, Ambassador Hon. Nekesa Barbara Oundo, widely regarded as an NRM National Treasure, yesterday challenged a massive gathering of…
RecentlyOP-ED: Minister Jonard Asiimwe Akiiki: A New Voice in the Fight Against Corruption and Embezzlement, and a Leadership Agenda That Must Deliver in Uganda!
By Kagisha Emmanuel [email protected] When leadership speaks boldly against corruption and embezzlement, the real test is whether words translate into institutional action, justice, recovery of stolen public resources an
RecentlyBenki ya Exim Tanzania Yalinda Hustle za Madereva Kupitia Twende BBM Festival 2026
-Yawasogezea madereva wa bodaboda, bajaji na magari huduma za malipo ya kidijitali, bima na huduma za kibenki zinazolenga kulinda vyanzo vyao vya kipato. Dar es Salaam, 14 Novemba 2026: Benki ya Exim Tanzania imetumia tamasha la Twende BBM Festival 2026 kuwasogezea madereva wa bodaboda, bajaji na magari huduma za kifedha zinazolenga kurahisisha shughuli zao za kila siku na kulinda vyanzo vyao vya kipato, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha uhusiano na wadau wa sekta ya usafiri nchini. Ikiwa mdhamini wa tamasha hilo, Exim Bank ilitumia fursa hiyo kuwafikia madereva wanaohusishwa na jukwaa la Twende. Jukwaa la Twende linahusisha madereva takribani 12,000 na jumuiya pana ya zaidi ya watumiaji 46,000 wa huduma zake. Kupitia tamasha hilo, Benki ya Exim ilipata fursa ya kukutana na kuwafahamisha madereva kuhusu huduma za kifedha zinazoweza kuwasaidia katika shughuli zao za kila siku. Katika tamasha hilo, Benki ya Exim iliendeleza ujumbe wa kampeni “Exim Inalinda Hustle Yako” kwa kutambulisha huduma nne zinazolenga mahitaji ya madereva katika shughuli zao za kila siku. Huduma hizo ni Exim Lipa ChapChap, Tumaini Health Insurance, Motor Insurance na Exim Quick Account. Kwa pamoja, huduma hizi zinalenga kurahisisha upatikanaji wa malipo, kuwawezesha madereva kupata ulinzi wa afya na kulinda vyombo vya usafiri wanavyotegemea kujipatia kipato. Akizungumza wakati wa tamasha hilo, Andrew Lyimo, Mkuu wa Kitengo cha Wateje Binafsi na Wakati wa Benki ya Exim Tanzania alisema benki inatambua mchango wa madereva katika kurahisisha usafiri na shughuli za kiuchumi, hivyo inaendelea kuwasogezea huduma zinazowasaidia kusimamia shughuli zao na kulinda vipato vyao. “Kwa madereva wengi, bodaboda, bajaji na magari si vyombo vya usafiri pekee, bali ni nyenzo muhimu za kujipatia kipato na kutunza familia zao. Tunatambua changamoto na mahitaji yanayoambatana na kazi zao za kila siku. Ndiyo maana kupitia huduma zetu, tunalenga kurahisisha upatikanaji wa malipo, kuwapatia fursa ya kupata ulinzi wa afya na vyombo vyao vya usafiri, pamoja na huduma za kibenki zinazowawezesha kusimamia fedha zao kwa urahisi zaidi. Hii ndiyo maana halisi ya ujumbe wetu, Exim Inalinda Hustle Yako,” alisema Lyimo. Kupitia Exim Lipa ChapChap, madereva wanaweza kurahisisha upokeaji na ufanyaji wa malipo. Tumaini Health Insurance inawawezesha kupata ulinzi wa bima ya afya, huku Motor Insurance ikitoa ulinzi wa bima kwa vyombo vya usafiri wanavyotumia katika shughuli zao za kila siku. Kw aupande wa Exim Quick Account, inawapa fursa ya kufungua akaunti na kutumia huduma za kibenki za Exim. Xxxxxxx Mmoja wa madereva walioshiriki tamasha hilo, alisema ushiriki wa Exim Bank umewapa madereva fursa ya kufahamu huduma za kifedha zinazoweza kuwasaidia katika kusimamia na kulinda shughuli zao za kila siku. “Ni jambo zuri kuona taasisi za kifedha zikija karibu nasi na kutuletea huduma zinazozingatia mahitaji yetu. Kazi yetu ya kila siku inategemea vyombo vyetu vya usafiri na uwezo wetu wa kuendelea kufanya kazi ili kupata kipato. Kwa hiyo, kufahamu huduma za malipo na bima zinazoweza kutusaidia kulinda kazi zetu ni jambo lenye umuhimu mkubwa kwetu,” alisema. Kupitia ushiriki wake katika Twende BBM Festival 2026, Exim Bank imelenga kuongeza idadi ya watumiaji wa Exim Lipa ChapChap, kuwafikia wateja wapya wa Tumaini Health Insurance na Motor Insurance, pamoja na kuongeza idadi ya akaunti za Exim Quick Account zinazofunguliwa. Benki pia inalenga kujenga mahusiano ya muda mrefu na madereva, vikundi vyao na wadau wengine wa sekta ya usafiri kwa ajili ya fursa za ushirikiano wa baadaye. Benki ya Exim inawaalika madereva, abiria na wadau wengine wa sekta ya usafiri kutembelea matawi yake nchini kote ili kupata maelezo zaidi kuhusu huduma hizo, kujisajili na kufungua akaunti. Kupitia huduma hizo, benki inalenga kuwasaidia wateja kurahisisha miamala yao, kupata ulinzi wa bima ya afya na vyombo vya usafiri, pamoja na kusimamia fedha zao kwa urahisi.
Sun, 22 Nov 2026 09:54:57 +0000Ruku: Why I'm vying for Nairobi governorship
The Public Service CS says his experience, years of living in Nairobi and record in government make him suitable to lead the capital in 2027.
RecentlyBia zavuruga kambi ya Pirates kuelekea mechi na Simba
Soma zaidi hapa
RecentlyUne "autoroute minière" soutenue par les États-Unis peut-elle apporter la paix et la prospérité en RDC ?
Le corridor de Lobito est au cœur d'un effort soutenu par les États-Unis pour garantir l'accès aux minéraux critiques de l'Afrique.
Recentlydfcu Bank Champions Strategic Financing Partnerships to Unlock Uganda’s Industrial Potential
Read the full report from the original source.
RecentlyBetibu Casino Test: Übersicht und Optionen 2024
Read the full report from the original source.
RecentlyBetmode Casino App – Konto‑Verifizierung Schritt für Schritt für deutsche Spieler
Read the full report from the original source.
RecentlyBetmode Bonusbedingungen: Übersicht und Optionen
Read the full report from the original source.
Recentlydfcu’s Annet Kiconco Urges Early Banking Engagement to Unlock Growth
Read the full report from the original source.
RecentlyDefence Ministry Seeks Shs1.9 Tn to Double UPDF Salaries
Read the full report from the original source.
RecentlyArusha businesses urged to go digital to tap into AFCON 2027 opportunities as Tanzania steps up preparations
Read the full report from the original source.
RecentlyMiley Cyrus marries Maxx Morando in California ceremony
Photos of the wedding on Saturday show the ceremony took place by a swimming pool with the pair standing under an arch covered in white flowers.
RecentlyTanzania yasistiza matumizi ya gesi asilia na makaa ya mawe katika COP 31
Read the full report from the original source.
RecentlyPage 73 of 1126 · 22509 stories