Search the region
23162 stories
Kaka alivyokodi wauaji wa mdogo wake kwa Sh3 milioni, kisa kauli ya baba
Read the full report from the original source.
RecentlySimba 2-1 Yanga | Ahmed Ally afunguka siri ya ushindi na mipango kuelekea mechi zijazo
#KariakooDerby Baada ya kuichapa Yanga mabao 2-1, Simba SC kupitia kwa msemaji wake Ahmed Ally imeeleza siri ya ushindi huo, kubwa ikiwa ni maandalizi, lakini pia imeweka hadharani ratiba yake kuelekea mechi zijazo za Ligi Kuu ya NBC na Ligi ya Mabingwa Afrika. Huyu hapa Ahmed Ally akizungumza LIVE kupitia kipindi cha #SportsAM cha leo Oktoba 11, 2026
2026-10-11T10:09:59+00:00Ruto: ‘I came to Likuyani for a wife’
"Yesterday I was thinking and said it had been a long time since I visited my in-laws,” Ruto said.
RecentlyEWURA yasimamia bei za mafuta kwa kuzingatia gharama halisi za soko
Read the full report from the original source.
RecentlyNSSF YAPAA THAMANI YA MFUKO YAFIKIA SH.TRILIONI 11.42
Thamani ya mfuko wa NSSF imeongezeka kwa asilimia 16 ndani ya mwaka mmoja, huku Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Dk Batilda Burian, akiwataka waajiri kulipa michango ya wafanyakazi kwa wakati na kutumia fursa ya msamaha wa tozo. Na Oscar Assenga, Tanga THAMANI ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) imefikia Sh trilioni 11.42 hadi Juni mwaka huu, kutoka Sh trilioni 9.84 zilizorekodiwa Juni 2025, ikiwa ni ongezeko la asilimia 16. Kutokana na ukuaji huo, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Dk Batilda Burian, ameitaka menejimenti ya mfuko huo kuendelea kuboresha huduma kwa wanachama na kuhakikisha zinawafikia wananchi katika maeneo yao. Alisema hayo wakati wa kilele cha Wiki ya Huduma kwa Wateja ya NSSF mkoani Tanga, akisisitiza kuwa huduma bora zinapaswa kuonekana kwa vitendo kwa wanachama wa sekta rasmi na isiyo rasmi. Dk Burian alisema matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) pamoja na kuongeza mawakala vijijini ni hatua zinazoweza kurahisisha upatikanaji wa huduma za hifadhi ya jamii kwa wananchi wengi zaidi. Alisema wanachama wanapaswa kutambuliwa kulingana na mahitaji yao, wakiwamo wakulima, wafanyabiashara wadogo, wajasiriamali na wafanyakazi wa viwandani, badala ya kuchukuliwa kama namba katika mifumo ya huduma. Katika hatua nyingine, aliielekeza menejimenti ya NSSF mkoani Tanga kuendelea kuwafuatilia waajiri wanaoshindwa kuwasilisha michango ya wafanyakazi wao kwa wakati. Alisema zoezi la kuwafuatilia waajiri lililofanyika mwaka juzi liliwezesha kukusanywa kwa Sh milioni 633, hivyo akaitaka timu ya mkoa kuendelea na kazi hiyo ili kuhakikisha michango inawasilishwa kwa mujibu wa taratibu. Dk Burian pia aliwataka waajiri wenye malimbikizo ya michango kutumia fursa ya msamaha wa tozo iliyotolewa na NSSF kabla ya Desemba 31, 2026, ili kurekebisha madeni yao na kulinda haki za wafanyakazi. Aidha, aliipongeza NSSF kwa kuboresha mifumo ya ulipaji mafao, akisema kupungua kwa muda wa kushughulikia malipo kutoka siku 60 hadi 19 ni hatua inayopunguza usumbufu kwa wanachama. Alisema huduma za kidijitali zinapaswa kuendelea kuimarishwa ili wanachama waweze kufuatilia michango na kuwasilisha madai ya mafao bila kulazimika kufika katika ofisi za mfuko huo. Dk Burian pia aliitaja NSSF kuwa miongoni mwa taasisi zilizochangia kuendeleza shughuli za kiwanda cha mkonge cha Sisalana, akisema hatua hiyo imesaidia kulinda ajira za wafanyakazi zaidi ya 1,000. Awali, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba, alisema mfuko huo utaendelea kushirikiana na uongozi wa mkoa kuwafikia watu waliojiajiri na walio katika sekta isiyo rasmi ili waweze kunufaika na huduma za hifadhi ya jamii. Mshomba alisema matumizi ya TEHAMA yamechangia kuboresha utendaji wa mfuko huo, akieleza kuwa muda wa wastani wa kulipa mafao kwa wastaafu umepungua kutoka siku 63 mwaka wa fedha 2020/21 hadi siku 19 kwa sasa. Alisema NSSF itaendelea kuimarisha huduma kwa wateja na kuwataka watumishi kuongeza juhudi ili kuhakikisha wanachama wanapata huduma kwa wakati. Aliongeza kuwa thamani ya mfuko ilipofikia Sh trilioni 4.8 Machi 2021, ilikuwa chini kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na Sh trilioni 11.42 zilizofikiwa Juni mwaka huu, jambo linaloonyesha ukuaji wa thamani ya mfuko katika kipindi hicho.
Sun, 11 Oct 2026 10:10:00 +0000Tom Cruise is Digger
Digger is a dark comedy featuring Tom Cruise as Digger Rockwell, a powerful oil tycoon who wants to save the world from the disaster he…
RecentlyTTCL YAKABIDHI VIFAA VYA KUFANYIA USAFI JIJINI DAR
Na Said Mwishehe,Michuzi TV SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania(TTCL)limekabidhi vifaa vya kufanyia usafi kwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kuhamisisha usafi. Vifaa hivyo vilivyotolewa na TTCL vimekabidhiwa leo Oktoba 10,2026 kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo aliyekuwq ameambatana na Mkurugenzi wa Halmshauri ya Jiji la Dar es salaam Elihuruma Mabelya bada ya kufanyika kwa shughuli ya kufanya usafi katika maeneo ya Posta ambapo pia watumishi wa TTCL wameshiriki kufanya usafi huo. Akizungumza baada ya kupokea vifaa hivyo Mkuu wa Wilaya Edward Mpogolo ametoa Shukrani kwa Bodi ya Wakurugenzi ya TTCL sambamba na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania CPA. Moremi Marwa kwa dhamira yao ya kuunga mkono jitihada za Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ya kufanya usafi katika Jiji hilo. “Kwa niaba ya Serikali nitoe shukrani kwa Bodi ya Wakurugenzi ya TTCL na wafanyakazi wote kwa kuona umuhimu wa kushiriki katika kutekeleza maelekezo ya Rais wetu npendwa Dk.Samia Suluhu Hassan aliyeelekeza tufanye usafi katika Jiji letu la Dar es Salaam. “Tunawashukuru TTCL kwa kazi kubwa ambayo mmeendelea kuifanya nchini Tanzania lakini kwa kazi kubwa ambayo mmeendelea kuifanya kwa Jiji letu la Dar es Salaam .Leo hii TTCL mnatamba kila mahala.Leo hii mmeamua kuwika na kutamba katika eneo la usafi,tunawashukuru na tunawapongeza.” Amesisitiza suala la usafi ni muhimu katika eneo na Taifa lolote kwani ni kichocheo kikubwa cha maendeleo na TTCL wameona kuna kila sababu ya kushirikiana na Jiji la Dar es Salaam kwa vitendo . “Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa na kwa niaba ya Serikali tunawashukuru TTCL kwa vifaa mlivyotoa kwa ajili ya kurahisisha shughuli za usafi katika Jiji la Dar es Salaam, mmetupa vifaa vingi ikiwemo mabuti ,vifaa vya kuhifafhi taka ,fagia.Thamani ambayo sisi tunaiona sio fedha iliyopitishwa kununua vifaa hivi bali ni dhamira ya TTCL kuona Jiji la Dar es Salaam linakuwa safi. “Umuhimu wa usafi katika maendeleo ya Taifa lolote ninyi TTCL tunawaona katika thamani hiyo ,vifaa hivi ambavyo mmetukabidhi maana yake kuna watu mmewakinga kupata magonjwa ya kipindi hiki ambacho tunakwenda kwenye matur iko kwa kuhakikisha tunaondoa uchafu katika mitaro.” Ametumia nafasi hiyo kutoa shukrani kwa taasisi zote zinazounga mkono jitihada za Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kuitaka Tanzania kuwa safi na salama kwani dhamira ya Rais Samia ya kutaka Jiji la Dar es es Salaam kuwa safi na salama. “Tuwaombe wale ambao bado wanachechemea njooni tushirikiane mkongo wa Taifa wa TTC umeshika hatamu. rai kwa mashirika na taasisi nyingine kushiriki kikamilifu katika kufanya usafi wa mazingira kwani haipendezi kuona mbele ya taasisi au Shirika la umma mazingira ni mchafu lakini walioko wala hawachukui hatua kusafisha maeneo yao. Wakati huo huo Mpogolo ametoa shukrani kwa niaba ya Serikali kwa wote walioshiriki kufanya usafi wakiongozwa na wenyeviti wa Serikali za mitaa ,madiwani na maofisa afya kwa kushiriki kufanya usafi katika mitaa yote 159. Awali Wakati akikabidhi vifaa vya usafi kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TTCL ,Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirika hilo Mhandisi Cecil Francis amesema wanampomgeza jitihada za kuunga mkono maelekezo kutoka kwa Rais na viongozi wote ambao katika kipindi hiki wanahimiza usafi kama utamaduni lakini kama kinga dhidi ya janga ambalo linaweza kutokea kama mvua kubwa itanyesha. “Mungu ametupa maarifa kwamba kuna hatari inakuja hivyo kama tusipofanya usafi kwa ajili ya kuzibua mitaro maji yapite vizuri tunaweza kutengeza janga jingine. Hivyo tunawapongeza Jiji la Dar es Salaam kwa kuchukua jitihada hizo na katika kuunga mkono TTCL tumeshiriki kufanya usafi na tutaendelea na kubwa zaidi tumeamua kuchangia vifaa na kusisitiza Shirika letu litaendelea kutoa huduma bora za mawasiliano.”
Sun, 11 Oct 2026 10:02:32 +0000EWURA YASIMAMIA BEI ZA MAFUTA KWA KUZINGATIA GHARAMA HALISI ZA SOKO
KATIKA mazingira ya sasa, ambapo bei za bidhaa za mafuta katika soko la dunia zinabadilika kutokana na migogoro ya kimataifa, gharama za usafirishaji na mabadiliko ya viwango vya ubadilishaji fedha, usimamizi wa bei una umuhimu mkubwa katika kulinda maslahi ya wananchi na uchumi wa taifa. Nchini Tanzania, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) ina jukumu la kusimamia bei katika sekta inazozidhibiti kwa mujibu wa sheria. Katika sekta ndogo ya mafuta, EWURA hutangaza bei kikomo za petroli, dizeli na mafuta ya taa ili kuhakikisha kuwa bei zinazotozwa zinazingatia gharama halisi na utaratibu wa udhibiti uliowekwa. Kwa nini EWURA inatangaza bei? Lengo la EWURA si kufanya mafuta yawe na bei ya juu, bali kuhakikisha kuwa bei zinazotozwa ni za haki, zinazingatia mwenendo wa soko na kulinda maslahi ya watumiaji pamoja na watoa huduma. Katika kupanga bei kikomo za mafuta, EWURA huzingatia gharama mbalimbali, zikiwemo bei za ununuzi katika soko la dunia, usafirishaji, bima, viwango vya ubadilishaji fedha, kodi, tozo na gharama nyingine zinazotambuliwa katika mfumo wa ukokotoaji wa bei. Mwananchi anafaidikaje? Kwanza, bei kikomo humlinda mwananchi dhidi ya kutozwa bei zinazozidi kiwango kilichoidhinishwa. Hii husaidia kuzuia baadhi ya wafanyabiashara kutumia mabadiliko ya soko kuongeza bei kiholela. Pili, utangazaji wa bei huongeza uwazi. Mwananchi anaweza kujua bei inayopaswa kutozwa katika eneo lake na hivyo kuwa na msingi wa kudai haki yake anaponunua mafuta. Tatu, usimamizi wa bei husaidia kuweka uwiano kati ya maslahi ya watumiaji na wafanyabiashara, ili wananchi wapate bidhaa kwa bei zinazozingatia gharama huku biashara zikiendelea kuwa endelevu. Uchumi wa taifa unanufaikaje? Mafuta ni bidhaa muhimu katika shughuli za uchumi. Hutumika katika usafirishaji wa abiria na mizigo, kilimo, viwanda na utoaji wa huduma mbalimbali. Kwa hiyo, usimamizi wa bei unaozingatia gharama na uwazi husaidia biashara kupanga matumizi, kupunguza uwezekano wa utozaji wa bei holela na kuongeza utabirika wa gharama katika shughuli za kiuchumi. Aidha, mfumo wa bei unaotabirika na unaozingatia gharama unaweza kusaidia kudumisha ushindani wa haki, kulinda uwekezaji na kuwezesha upatikanaji endelevu wa bidhaa za mafuta nchini. Nini kinaweza kutokea EWURA isipotangaza bei kikomo? Katika mazingira ya sasa ya mabadiliko ya bei za mafuta duniani, kutokuwepo kwa bei kikomo na mfumo madhubuti wa usimamizi kunaweza kuongeza hatari ya baadhi ya wafanyabiashara kutoza bei kubwa zisizoendana na gharama halisi. Hali hiyo inaweza kuongeza gharama za usafirishaji, uzalishaji na maisha ya wananchi. Pia, inaweza kupunguza uwazi wa bei na kufanya iwe vigumu kwa watumiaji kutambua iwapo wanatozwa bei inayostahili.
Sun, 11 Oct 2026 10:03:42 +0000"Tumetangaza ubingwa leo" - Mashabiki wa Simba watamba baada uifunga Yanga 2-1 NBC PL 10/10/2026
#KariakooDerby “…tumefuta uteja.... tumetangaza ubingwa leo…. Simba ni bingwa” Furaha ya mashabiki wa Simba baada ya kumfunga mtani wao Yanga kwa mara ya kwanza kwenye ligi kuu baada ya miaka mitatu… Yupo K-Mziwanda, yupo, Dkt. Mayala, yupo Dkt. Mohamed ambaye anasema “….ukimfunga Yanga maana yake wewe ni bingwa” Hapa ni Uhuru Stadium baada ya mechi, Simba ikiibuka na ushindi wa mabao 2-1. #NBCPL #NBCPremierLeague #SimbaYanga #AhmedAlly #SportsAM
2026-10-11T09:44:33+00:00India: 'Cockroach' leaders vow new protests after release
Read the full report from the original source.
RecentlySimba yafafanua kuhusu ukubwa wa 'bonasi' baada ya kuifunga Yanga 2-1 kwenye NBC PL 10/10/2026
AHMED ALLY: “Hiyo bilioni moja, hata mimi natoa”. Kuhusu bonasi….. Je, waliahidiwa shilingi bilioni moja? Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally anafafanua akisema shilingi bilioni moja ni ‘level’ yake yeye, akimaanisha kuwa bonasi itakayotolewa kwa kuifunga Yanga ni zaidi ya shilingi bilioni moja… Kuhusu program ya timu….. Ahmed Ally ameeleza kuhusu ratiba akisema baada ya ushindi wa jana, hakuna kupumzika, “ni kazi na dawa”, na leo kikosi kinaendelea na tizi kuelekea mchezo ujao.. Kuhusu goli la Mpanzu, Ahmed anasema “..siwezi kulizungumza kwa dakika moja”. Huyu hapa kupitia kipindi cha Sports AM asubuhi ya leo (11/10/2026) akianza kwa kutoa ufafanuzi kuhusu utaratibu na muundo wa bonasi zao ambapo amesema zinatolewa endapo timu imeshinda tu…. Lakini utaratibu huo uko tofauti kidogo upande wa mechi za kimataifa… #NBCPL #NBCPremierLeague #SimbaYanga #AhmedAlly #SportsAM
2026-10-11T09:36:59+00:00Ruto attends church service in Likuyani, Kakamega
He was accompanied by Likuyani MP Innocent Mugabe and Navakholo MP Emmanuel Wangwe.
RecentlyMagogo yafungua fursa soko la miti
Read the full report from the original source.
RecentlyOptics tell it all: Why William Ruto looks tell of a desperate politician
President William Ruto has taken on a worrying look of late – sweating profusely, eyes wild and blazing, teeth bared in a rictus smile, absolutely furious, panicking and shouting.
Sun, 11 Oct 2026 12:30:00 +0300Des camps infestés de rats et des blessures qui ne guérissent pas : un été à Gaza
Des Palestiniens racontent à la BBC les difficultés auxquelles ils sont confrontés à Gaza suite à la destruction quasi totale des infrastructures dont ils dépendent.
RecentlyYemen's Houthis warn passengers not to use Saudi airports
Read the full report from the original source.
RecentlyPakistan: Khan stronghold province put under emergency rule
Read the full report from the original source.
RecentlyFSCs zageuka daraja la wakulima
Read the full report from the original source.
RecentlySimba SC 2-1 Yanga SC | Ahmed Ally aomba radhi kwa "ushindi kiduchu"
#KariakooDerby Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally baada ya ushindi, anawaomba radhi mashabiki “kwa ushindi kiduchu”, lakini anasema malengo yao ni ubingwa, hivyo hawabweteki na ushindi huu kwakuwa bado wana mechi 23. Huyu hapa akiwa bado wa motrooooooo!!!! #NBCPL #NBCPremierLeague #SimbaYanga #AhmedAlly #SportsAM
2026-10-11T09:26:46+00:00MoH Urges Kenyans to Use Protective Gear When Handling Suspected Ebola Cases
NATIONAL NEWS · Quick read
RecentlyPage 742 of 1159 · 23162 stories