Search the region
22893 stories
Prof Kabudi asisitiza majadilino kumaliza changamoto
Read the full report from the original source.
RecentlyWIZARA YA AFYA YAIMARISHA USHIRIKI WA JAMII KUKABILIANA NA VVU
Na Mwandishi Wetu. Wizara ya Afya kupitia Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi, Magonjwa ya Ngono na Homa ya Ini (NASHCoP), imeendelea kuimarisha ushiriki wa jamii katika kukabiliana na changamoto za VVU na UKIMWI kupitia mafunzo yanayolenga kuwajengea uwezo viongozi na wadau wa afya katika kutambua changamoto na kutafuta suluhisho zinazozingatia mazingira halisi ya jamii. Mafunzo hayo yamefanyika Mkoani Morogoro na ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa miaka miwili unaofadhiliwa na Global Fund katika mikoa ya Tanga, Morogoro, Geita, Dodoma na Singida. Kupitia mafunzo hayo ya Adaptive Leadership, washiriki wamejengewa uwezo wa kuchambua changamoto za afya kulingana na mazingira ya jamii, kushirikisha wadau mbalimbali na kuandaa suluhisho endelevu, hususan katika kukabiliana na VVU na magonjwa ya ngono. Mwanaharuna Ramadhani Saidi, muelimishaji rika kutoka Taasisi ya TAYOA mkoani Morogoro, amesema mafunzo hayo yamemsaidia kuelewa kwa kina mazingira yanayoweza kuchangia maambukizi ya VVU miongoni mwa vijana, ikiwemo maeneo ya starehe, matumizi ya dawa za kulevya na maeneo ya uchimbaji wa madini. Amesema changamoto ya maambukizi ya VVU haiwezi kuhusishwa na wingi wa watu pekee katika eneo fulani, bali inapaswa kuangaliwa kwa kuzingatia sababu mbalimbali za kijamii na kitabia zinazowazunguka vijana. Kwa upande wake, Hezron Yuda, Mratibu wa Huduma za Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto Wilaya ya Chato mkoani Geita, amesema mafunzo hayo yamempa uelewa zaidi kuhusu umuhimu wa kuishirikisha jamii katika kutambua changamoto za afya na kushiriki katika kutafuta suluhisho. Amesema wataalamu wanapaswa kutambua kuwa jamii yenyewe ina maarifa muhimu kuhusu changamoto zinazowakabili, hivyo ushirikishwaji wake unaweza kusaidia kupata suluhisho linaloendana na mazingira na mahitaji halisi ya wananchi. Naye Ayubu Bwanamadi, Kiongozi wa Dini ya Kiislamu na Katibu wa Jumuiya ya Vijana wa Kiislamu mkoani Geita, amesema mafunzo hayo yamemsaidia kuelewa kuwa uongozi si suala la kuwa na nafasi au mamlaka pekee, bali ni wajibu wa kutumia nafasi hiyo kuleta mabadiliko chanya katika jamii. Amesema viongozi wa dini wana nafasi kubwa katika kuwafikia vijana, kuwaelimisha kuhusu afya, maadili na namna ya kujikinga dhidi ya VVU na magonjwa ya ngono. Washiriki wa mafunzo hayo yaliyofanyika Dodoma wameitaka Serikali na wadau wa afya kuendelea kuwekeza katika elimu kwa vijana, kuimarisha ushiriki wa jamii na kuhakikisha afua za kukabiliana na VVU zinazingatia mazingira halisi ya wananchi. Wamesema ushiriki wa jamii na uongozi unaozingatia changamoto zilizopo katika mazingira husika ni muhimu katika kuhakikisha jitihada za kuzuia maambukizi ya VVU na magonjwa ya ngono zinakuwa na matokeo endelevu.
Wed, 07 Oct 2026 14:12:17 +0000Burundi : le Conseil des droits de l’homme renouvelle le mandat du rapporteur spécial
Read the full report from the original source.
RecentlyRwanda records 6.8% growth in industrial output in August
Read the full report from the original source.
RecentlyDukore iki ko imvura ikomeje kugwa nabi?
Read the full report from the original source.
RecentlyProf Kabudi tasks the Council of Political Parties to embrace the 4Rs philosophy
Read the full report from the original source.
RecentlyTAMTHILIA YA REHANI KUJA KUBADILI TASWIRA YA SANAA YA BONGO
Tamthilia mpya ya Rehani, inayowakutanisha wasanii Aunt Ezekiel na Kobisi, inatarajiwa kuanza kurushwa Oktoba 19, 2026, kupitia St Swahili, huku ikiahidi kuleta uhalisia wa maisha ya Kitanzania. Mtayarishaji wa tamthilia zilizopata umaarufu nchini za Komborela, Saluni ya Mama Kimbo na Zahanati ya Kijiji, Abdul Juma, amesema tamthilia mpya ya Rehani ni mwanzo wa safari mpya katika tasnia ya filamu na tamthilia nchini, akiahidi kuwasilisha kazi yenye ubora, uhalisia na maudhui yanayogusa maisha ya Watanzania. Tamthilia hiyo inayozalishwa kwa ushirikiano na Kampuni ya StarTimes Limited kupitia chapa yake ya St Swahili, itaanza kurushwa Oktoba 19, 2026, kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa, ikiwa na maudhui mbalimbali yanayolenga kuburudisha, kuelimisha na kufundisha jamii. Juma amesema Rehani imewashirikisha wasanii mbalimbali wenye uwezo mkubwa wa kuigiza, wakiwemo Aunt Ezekiel, anayeigiza mhusika wa Mwajabu, pamoja na Kobisi, ambao kwa pamoja wanatarajiwa kuipa tamthilia hiyo mvuto wa kipekee. Amesema mafanikio ya utayarishaji wa tamthilia hiyo yametokana kwa kiasi kikubwa na ushirikiano alioupata kutoka kwa Aunt Ezekiel, ambaye amekuwa mstari wa mbele kumtia moyo na kumsaidia kuhakikisha mradi huo unakamilika. "Kipekee nitoe pongezi kwa dada yangu Aunt Ezekiel. Amekuwa mtu wa kwanza kunishika mkono na kunipa moyo kuhakikisha Rehani inafanyika, hadi kufikia hatua ya kutoa fedha zake mwenyewe kwa ajili ya kutengeneza kipande kifupi cha video (Demo)," amesema Juma. Ameongeza kuwa kazi zake za awali zimekuwa na mafanikio makubwa, ikiwemo kutwaa tuzo mbalimbali, hivyo ana matumaini kuwa Rehani itaendeleza mafanikio hayo kutokana na ubora wa utayarishaji wake, maudhui ya Kitanzania na kuzingatia uhalisia wa maisha ya kila siku. Kwa upande wake, Meneja Masoko wa StarTimes, David Malisa, amewahakikishia watazamaji wa St Swahili kuwa tamthilia hiyo itapatikana kupitia vifurushi vyote, kuanzia kifurushi cha chini kabisa, ili kuwapa nafasi watazamaji wengi zaidi kufurahia burudani hiyo. Malisa amewataka wateja wa StarTimes kulipia vifurushi vyao mapema ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza katika huduma za malipo na mitandao, na hivyo kuhakikisha hawakosi vipindi vya tamthilia hiyo mpya.
Wed, 07 Oct 2026 14:04:37 +0000SILAHA AINA YA GOBORE 68 ZASALIMISHWA TANGA KATIKA KIPINDI CHA MSAMAHA
Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga limepokea silaha aina ya gobore 68 kutoka kwa wananchi walioitikia wito wa kusalimisha silaha hizo katika kipindi cha msamaha kinachoendelea hadi Oktoba 31, 2026. Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Almachius Mchunguzi, amesema mwitikio wa wananchi umekuwa mkubwa kutokana na elimu inayotolewa na Jeshi hilo kuhusu umuhimu wa kusalimisha silaha hizo. Amesema baadhi ya wananchi wamekuwa wakizifikisha wenyewe katika vituo vya Polisi kwa ajili ya kuzisalimisha, hatua inayowapa fursa ya kutekeleza wito huo ndani ya kipindi cha msamaha na kuepuka kuchukuliwa hatua za kisheria baada ya muda huo kumalizika. Aidha, Kamanda Mchunguzi amewataka wananchi wa Mkoa wa Tanga kuacha kujihusisha na utengenezaji wa silaha aina ya gobore, akisisitiza kuwa utengenezaji na umiliki wa silaha hizo ni kinyume cha sheria. Amewataka pia wananchi wenye taarifa kuhusu watu wanaojihusisha na utengenezaji wa silaha hizo kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi ili hatua stahiki za kisheria ziweze kuchukuliwa.
Wed, 07 Oct 2026 14:07:04 +0000Tanzania woos Dutch investors for mining, agriculture, logistics
Read the full report from the original source.
RecentlyLa France suspend l'utilisation de grenades assourdissantes après qu'un garçon a eu la main arrachée lors de manifestations étudiantes
Cette mesure fait suite aux plaintes de plusieurs groupes dénonçant l'usage disproportionné de la force par la police envers les adolescents.
RecentlyNduhungirehe, Kenyatta discuss security in eastern DRC
Read the full report from the original source.
RecentlyWHO chief urges parliamentarians to cut aid dependency, strengthen pandemic preparedness
Latest · Africa
RecentlyMIJADALA YA CATA KUWA CHACHU YA KUBORESHA ZAIDI HUDUMA ZA KODI TANZANIA – CG MWENDA
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Yusuph Juma Mwenda, amesema mijadala ya Mkutano wa 46 wa CATA itakuwa chachu ya kuboresha zaidi huduma za kodi nchini. Ameyasema hayo akiongoza ujumbe wa CATA ulipotembelea Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) jijini Arusha, ikiwa ni sehemu ya programu ya mkutano huo ulioanza tarehe 5–9 Oktoba 2026. Bw. Mwenda amesema ziara hiyo imewapa Makamishna fursa ya kujifunza uzoefu wa EAC katika matumizi ya teknolojia, ubadilishanaji wa taarifa na uboreshaji wa mifumo ya Forodha, maeneo yanayochangia kuongeza ufanisi wa ukusanyaji wa mapato na kurahisisha biashara katika ukanda wa Afrika Mashariki. Amesema TRA itaendelea kutumia maarifa na uzoefu unaopatikana kupitia mijadala ya CATA katika kuboresha huduma kwa walipakodi, kurahisisha ulipaji wa kodi na kuimarisha ufanisi wa ukusanyaji wa mapato kwa maendeleo ya Taifa.
Wed, 07 Oct 2026 13:56:43 +0000DP Kindiki: Bold and radical reforms have made agriculture more beneficial to farmers over the last four years
Read the full report from the original source.
RecentlyKenya tightens JKIA Ebola controls, sets dedicated gate for travellers from 10 African countries
Latest · Africa
RecentlyAbanyeshuri, abakozi ba Cornell University bigaragambije kubera imikirize y'urubanza rw'ihohoterwa rishingiye ku gitsina
Read the full report from the original source.
RecentlyUasin Gishu Youth embrace affordable housing to secure future assets
Read the full report from the original source.
RecentlyAbanyeshuri n'abakozi ba Kaminuza ya Cornell bigaragambije kubera imikirize y'urubanza rw'ihohoterwa rishingiye ku gitsina
Read the full report from the original source.
RecentlyWataalamu waonya madhara ya kisukari cha mimba
Read the full report from the original source.
RecentlyYas deepens support for Zanzibar’s digital economy
ZANZIBAR: Yas Tanzania has strengthened its support for Zanzibar’s digital transformation after receiving recognition for its contribution to the island’s…
RecentlyPage 814 of 1145 · 22893 stories