Unganishwa

Search the region

22858 stories

Uncategorized · The Star Kenya

WHO praises Kenya’s response after Ebola case

WHO says the case was imported and no ongoing local transmission has been detected in Kenya

Recently
Health · The Star Kenya

Ebola alert: Nairobi Hospital steps up staff monitoring

Staff who had relevant contact with the patient will be individually contacted

Recently
Uncategorized · Watchdog Uganda

Police Arrest Prime Suspect in Online Fraud Targeting Foreign Tourists

Police have arrested a man suspected of running an online fraud scheme targeting foreign tourists through a purported car-hire and tour company, FK Car Rental. The suspect, identified as Faisal…

Recently
Uncategorized · Watchdog Uganda

Lost Receipts, Big Win: Kira Bettor Rides Away with 4th KBET & VROOOM Motorcycle

Ninsiima Rominate, an SGA receptionist and avid USSD bettor from Kira, Wakiso, has won the fourth motorcycle in the KBET & VROOOM giveaway from Kagwirawo. Rominate’s win came with an…

Recently
Uncategorized · KBC

Mazingira week puts the power to protect nature in every Kenyan’s hands

Read the full report from the original source.

Recently
Health · The Star Kenya

Ebola alert: Nairobi Hospital steps up tracing, staff monitoring

Staff who had relevant contact with the patient will be individually contacted, risk-stratified and followed up according to Ministry of Health protocols.

Recently
Business · Issa Michuzi

Benki ya Exim Yaadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja 2026

Benki ya Exim Tanzania imeadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja 2026 kwa kusisitiza dhamira yake ya kuendelea kutoa huduma bora, zenye mwitikio na zinazomweka mteja mbele, kupitia kaulimbiu ya mwaka huu, “The Extra Mile.” Ikiwa ni sehemu ya maadhimisho hayo, wafanyakazi wa Benki ya Exim walishiriki katika matembezi ya huduma kwa wateja jijini Dar es Salaam, yakiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu, Jaffari Matundu, ikiwa ni ishara ya wazi ya dhamira ya Benki ya kumweka mteja katika kiini cha kila jambo linalofanywa. Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo, Matundu alisema kwenda “The Extra Mile” kunamaanisha kumweka mteja kwanza na kuhakikisha kuwa kila mwingiliano na mteja unaongeza thamani kwake. Alisisitiza kuwa huduma bora kwa wateja ni jukumu la pamoja ndani ya Benki, ambapo kila mfanyakazi ana nafasi ya kuhakikisha huduma za kibenki zinakuwa rahisi, zenye urahisi zaidi na zenye mwitikio kwa mahitaji ya wateja. Wafanyakazi wa Exim Bank Tanzania wakiongozwa na Afisa Mtendaji wa Benki hiyo, Jaffari Matundu, wakishiriki matembezi ya huduma kwa wateja 2026 jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki hiyo yenye kaulimbiu “The Extra Mile” na kuonesha dhamira ya Benki ya kuwaweka wateja mbele. Wafanyakazi wa Exim Bank Tanzania wakishiriki matembezi ya huduma kwa wateja 2026 jijini Dar es Salaam, yenye kaulimbiu “The Extra Mile”. Afisa Mtendaji wa Exim Bank Tanzania, Jaffari Matundu, akizungumza na wafanyakazi wa Benki hiyo wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja 2026. Alisisitiza umuhimu wa kwenda hatua ya ziada katika kuwahudumia wateja na kuhakikisha kila mwingiliano unaleta thamani kwao. Afisa Mtendaji wa Exim Bank Tanzania, Jaffari Matundu, akikata keki pamoja na baadhi ya wafanyakazi wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja 2026. Wiki hiyo yenye kaulimbiu “The Extra Mile” inalenga kuimarisha dhamira ya Benki ya kutoa huduma bora, rahisi na zinazozingatia mahitaji ya wateja. Wafanyakazi wa Exim Bank Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kushiriki matembezi ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja 2026 jijini Dar es Salaam, yenye kaulimbiu “The Extra Mile”, wakionesha mshikamano na dhamira ya pamoja ya kutoa huduma bora, yenye ufanisi na inayoweka wateja mbele.

Tue, 06 Oct 2026 12:00:00 +0000
Uncategorized · Citizen Digital

Kariobangi Sharks vs Mombasa United playoff abandoned following pitch invasion

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

Ruto presides over signing of Ksh.389 billion electric vehicle investment deal

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Business Daily Africa

To rent or to buy? The costs Kenyans foot to live abroad

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Issa Michuzi

WAZIRI HOMERA AZINDUA MKATABA WA HUDUMA KWA WATEJA ULIOHUISHWA NA HUDUMA NYINGINE KWA WATEJA WA TANESCO

*Asisitiza mifumo iliyozinduliwa ifanye kazi kwa ufanisi na kuendana na mahitaji ya wateja *Aipongeza TANESCO kwa ubunifu na kuimarisha huduma kwa wateja wakubwa Na Mwandishi Wetu Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Juma Zuberi Homera, leo Oktoba 6, 2026 amezindua Mkataba wa Huduma kwa Wateja uliohuishwa pamoja na huduma mbalimbali za TANESCO zinazolenga kuboresha zaidi namna ya utoaji wa huduma kwa wateja kwa ufanisi na kwa wakati, uzinduzi uliofanyika katika Ukumbi wa Super Dome, jijini Dar es Salaam. Mhe. Homera amesema matumizi ya mifumo ya teknolojia za kisasa katika utoaji wa huduma kwa wateja yanazidi kuiwezesha TANESCO kupiga hatua kubwa katika kuboresha huduma zake kwa kuzingatia uwajibikaji, uwazi na weledi unaolenga kuleta matokeo chanya kiutendaji. Ametoa rai kuhakikisha changamoto zinazowakabili wananchi katika matumizi ya umeme zinashughulikiwa kwa haraka kwa kuwa changamoto katika huduma ya umeme zinaweza kuathiri moja kwa moja uzalishaji na shughuli za kiuchumi. “Mwelekeo wa Serikali ni kujenga sekta ya nishati inayoweza kuunga mkono kasi ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania. Tunataka kuona shughuli za uzalishaji zinaendelea bila vikwazo visivyo vya lazima na tunataka wananchi wapate huduma kwa urahisi zaidi,” ameeleza Waziri Homera. Amesema Tanzania hivi sasa ina umeme wa kutosha, ambapo uwezo wa uzalishaji umefikia jumla ya Megawati 4,606 dhidi ya mahitaji ya juu ya Megawati 2,316, hatua inayotoa fursa zaidi za kukuza shughuli za kiuchumi kupitia uwekezaji katika viwanda, biashara na shughuli za kijamii. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Mhe. Subira Mgalu, ameipongeza Wizara ya Nishati kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa kuendelea kuja na ubunifu unaolenga kutatua changamoto zinazowakabili wananchi katika nyanja mbalimbali. Naye Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TANESCO, Mhe. Balozi Zuhura Bundala, amesema Bodi itaendelea kuisimamia TANESCO katika kuhakikisha utoaji wa huduma unaenda sambamba na matumizi ya teknolojia za kisasa, ili huduma zimfikie mteja moja kwa moja bila vikwazo. “Bodi itaendelea kuishauri TANESCO katika utoaji wa huduma kwa ufanisi. Kwetu sisi, mteja ni mfalme, na huduma inayotolewa na Shirika inamgusa mwananchi moja kwa moja. Tumejipanga kuhakikisha jitihada hizi zinaendelea kupiga hatua,” amesisitiza Balozi Bundala Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Bw. Lazaro Twange, ametoa ufafanuzi kuhusu uzinduzi wa Twiga Assistant, mfumo unaolenga kuachana na utoaji wa huduma kwa njia za makaratasi na kuingia katika matumizi ya mifumo ya kielektroniki inayompunguzia mteja kutumia muda mrefu kusubiri huduma anayohitaji. “TANESCO inafanya kazi kubwa kuhakikisha nishati ya umeme inawafikia wananchi baada ya kukamilika kwa miradi mingi ya kimkakati, ukiwemo Mradi wa Chalinze–Dodoma. Hatua hii inatupa nguvu ya kuja na ubunifu wa kuona namna ya kumfikia mteja kwa haraka. Ndiyo maana TANESCO imeamua kushuka chini na kusogeza huduma zake karibu na wananchi,” amefafanua Bw. Twange. Hafla hiyo iliyobeba kaulimbiu ya “EXTRA MILE” imeenda sambamba na uzinduzi wa namba mpya ya 185 kwa ajili ya wateja wakubwa, Twiga AI Chatbot, mfumo saidizi wa kidijitali unaolenga kujibu maswali ya wateja, Kitengo cha watwja wakubwa kilichoboreshwa, pamoja na Premium Customer Portal, mfumo maalumu kwa ajili ya wateja wakubwa, ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wao katika shughuli za Shirika. Uzinduzi huo umefanyika katika kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja, ikiwa ni sehemu ya jitihada za TANESCO kuendelea kuboresha huduma kwa kutumia teknolojia za kisasa na kuhakikisha mteja anapata huduma kwa urahisi, haraka na kwa ufanisi.

Tue, 06 Oct 2026 15:36:36 +0000
Uncategorized · Issa Michuzi

TANESCO LINDI YAUNGANA NA WANANCHI KUKABILIANA NA EL-NINO

Shirika la Umeme Tanzania TANESCO Mkoa wa Lindi, kwa kushirikiana na wananchi wa Kata ya Mwenge, Manispaa ya Lindi, limefanya zoezi la kusafisha mitaro ya maji katika maeneo mbalimbali ya kata hiyo, ikiwa ni hatua ya kujiandaa na kukabiliana na mvua za El-Nino. Meneja wa TANESCO Mkoa wa Lindi, Theodory Hall, amesema zoezi hilo limefanyika ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja, huku shirika hilo likikabidhi mashine mbili aina ya Moha kwa ajili ya kusaidia shughuli za usafi katika kata hiyo. Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi, Juma, amewashukuru TANESCO kwa kushirikiana na Halmashauri katika kuimarisha usafi na maandalizi ya kukabiliana na mvua za El-Nino, akisema Halmashauri imefikia utayari wa asilimia 95. Baadhi ya wananchi wakiongozwa na Diwani wa Kata ya Mwenge, Ali Kanjoro, wamesema usafishaji wa mitaro hiyo utasaidia kupunguza athari za mafuriko pamoja na magonjwa ya mlipuko wakati wa msimu wa mvua.

Tue, 06 Oct 2026 15:41:55 +0000
Uncategorized · Issa Michuzi

Taka Za Plastiki zatishia Afya Ya Bahari

Na Karama Kenyunko Michuzi tv KATIBU Mtendaji Msaidizi wa Umoja wa Mataifa na Katibu Msaidizi wa Umoja wa Mataifa wa Mazingira (UNEP), Elizabeth Mrema, amesema taka za plastiki ni miongoni mwa changamoto kubwa zinazoathiri afya ya bahari, akisisitiza umuhimu wa elimu kwa wananchi kuhusu madhara ya kutupa taka hizo baharini. Mrema amesema hayo leo Oktoba 6, 2026 wakati wa Mkutano wa Waratibu wa Kitaifa na Washirika wa COP12, uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam. Mrema amesema bahari ni muhimu kwa maisha ya binadamu kwa kuwa hutoa chakula na rasilimali nyingine muhimu, hivyo uchafu wa plastiki unapojazana baharini husababisha madhara kwa samaki na mimea ya baharini. “Samaki wanameza, na ndio wanakufa,” amesema Mrema, akisisitiza umuhimu wa kuongeza elimu kwa wananchi kuhusu madhara ya kutupa chupa na taka nyingine za plastiki katika mazingira. Amesema suala la usafi wa bahari si jukumu la Serikali pekee, bali ni wajibu wa kila mwananchi. “Wananchi wanapaswa kuelewa kuwa matendo yao ya leo yanaweza kuathiri maisha yao, watoto wao na vizazi vijavyo,” amesema. Mrema pia amesema elimu hiyo inapaswa kutolewa kwa lugha rahisi inayoweza kueleweka na makundi yote, wakiwemo wavuvi na watu wanaoishi katika maeneo ya mwambao, ili waweze kushiriki kikamilifu katika kulinda mazingira ya bahari. Kwa upande mwingine, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Hamza Hassan Juma, amezitaka nchi wanachama wa Mkataba wa Nairobi kuimarisha ushirikiano na kuchukua hatua za vitendo kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, uchafuzi wa bahari, upotevu wa bioanuwai na matumizi yasiyo endelevu ya rasilimali za baharini. Juma amesema mwaka huu unaadhimisha miaka 40 ya Mkataba wa Nairobi, ikiwa ni miaka 40 ya ushirikiano, kujifunza na kufanya kazi pamoja kwa ajili ya kuwa na Bahari ya Magharibi mwa Bahari ya Hindi yenye afya na tija. Amesema Tanzania inajivunia urithi wake wa maeneo ya pwani na visiwa, ikiwamo mwambao wa Dar es Salaam na visiwa vya kihistoria vya Zanzibar, ambavyo vina historia ya utunzaji wa bahari, biashara ya majini, utamaduni wa Kiswahili na uhusiano wa karibu kati ya watu na bahari. “Urithi huu unatukumbusha kuwa bahari si rasilimali ya mazingira pekee, bali pia ni chanzo cha maisha, utamaduni, utambulisho na fursa za kiuchumi kwa watu wetu,” amesema. Juma amesema pamoja na kusherehekea mafanikio yaliyopatikana katika miaka 40, nchi wanachama zinatambua changamoto zinazoukabili bahari, zikiwemo mabadiliko ya tabianchi, uchafuzi wa bahari, upotevu wa bioanuwai na matumizi yasiyo endelevu ya rasilimali za baharini. Amesema miaka 40 ijayo inapaswa kuwa ya kuimarisha ushirikiano, kuchukua hatua za vitendo na kupata matokeo yatakayogusa maisha ya watu na kuonekana katika bahari. Mkataba wa Nairobi ulipitishwa Juni 21, 1985 na kuanza kutumika Mei 30, 1996. Tanzania iliuridhia Machi 1, 1996 na baadaye kuridhia Mkataba uliorekebishwa Septemba 4, 2017. Tanzania ni miongoni mwa nchi 10 wanachama wa Mkataba huo, pamoja na Comoro, Ufaransa, Kenya, Madagascar, Mauritius, Msumbiji, Shelisheli, Somalia na Afrika Kusini. Katika kipindi cha miaka 40, Mkataba huo umewezesha ushirikiano katika maeneo mbalimbali ya uhifadhi wa bahari, ikiwamo maeneo ya bahari yaliyohifadhiwa, mipango ya kikanda ya kukabiliana na uchafuzi, ulinzi wa bioanuwai na kuimarisha uwezo wa kisayansi. Tanzania imekuwa sehemu ya safari hiyo kupitia Kitengo cha Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu, kilichoanzishwa mwaka 1996, ambacho kilisimamia kutangazwa kwa Hifadhi ya Bahari ya Mnazi Bay–Ruvuma Estuary mwaka 2000 na Hifadhi ya Bahari ya Tanga Coelacanth mwaka 2009. Juma pia amewakaribisha wajumbe wa COP12 kutembelea Zanzibar, akisema kutoka Dar es Salaam hadi Zanzibar ni dakika 20 kwa ndege au dakika 90 kwa kivuko cha mwendokasi. Amesema ziara hiyo itawapa fursa ya kufurahia utamaduni na vivutio vya utalii vya Zanzibar wakati watakapokuwa nchini.

Tue, 06 Oct 2026 15:35:10 +0000
National · Issa Michuzi

DAS SAME ASISITIZA ELIMU YA TAHADHARI KWA WANANCHI

Na Mwandishi Wetu- Same Katibu Tawala Wilaya ya Same Bi. Mamndolwa Gembe amewataka Kamati ya Usimamizi wa Maafa Wilaya ya Same kuendelea kutoa elimu ya tahadhari kwa wananchi wa maeneo yote ya wilaya hiyo hususani wakulima na wafugaji. Bi. Gembe amesisitiza hayo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo, leo Octoba 06, 2026, wakati akifungua kikao kazi cha Kamati za usimamizi wa maafa za wilaya na timu ya wataalamu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na Shirika la Chakula Duniani (WFP) sambamba na kuimarisha utoaji wa matumizi ya taarifa za tahadhari za awali katika kujiandaa na kukabiliana na madhara ya El nino. “Wilaya ya Same ni miongoni mwa maeneo yanayokabiliwa na mabadiliko makubwa ya tabianchi, kijiografia wilaya yetu ina maeneo ya milima na tambarare, hivyo inatufanya tuwe katika hatari ya kukabiliwa na changamoto za pande mbili, kutokana na hilo mipango na mapendekezo yatakayotolewa katika kikao kazi hiki yasibaki kwenye nyaraka tu, bali yakatimizwe na kuingizwa kwenye mipango kazi ya halmashauri, mamlaka za kata na vijiji” amesisitiza Bi. Gembe. Aidha, Bi. Gembe ameishukuru Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na Shirika la Chakula Duniani (WFP) kwa ushirikiano lakini pia amesema kuwa Serikali ya Wilaya ya Same ipo tayari kufanya kazi bega kwa bega ili kuhakikisha malengo ya programu hiyo yanatimia. “Tunawashukuru sana kwa kuchagua Wilaya ya Same kuwa sehemu yay a ziara na kikao kazi hiki cha kimkakati, ujio wenu ni Ushahidi tosh awa dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita katika kulinda Maisha na mali za wananchi dhidi ya athari za majanga Ameongeza Katibu Tawala huyo. Nae, Mwakilishi kutoka Shirika la Chakula Duniani (WFP) Bi. Sandra Hakim amebainisha kuwa, lengo la programu hiyo ni kuifanya taarifa ya Mamlaka ya Hali ya Hewa inashuka chini ili jamii ikiwemo wazee, wamama, walemavu na watoto waweze kupata taarifa kwa wakati kwani upatikanaji wa taarifa za hali ya hewa mapema zitakuwa na thamani pale utakapochukua hatua kabla ya majanga kutokea. Katika kikao hicho mada mbalimbali kuhusu Utabiri wa Msimu, El nino na madhara tarajiwa, Dhana ya Maafa ikiwemo mzingo wa maafa, Mpango wa Dharurawa Kukabiliana na Maafa na majukumu ya kamati na utekelezaji wa mpango pamoja na Usambazaji wa Huduma za Hali ya Hewa ziliwasilishwa kwa Kamati ya Usimamizi wa Maafa.

Tue, 06 Oct 2026 15:37:53 +0000
Uncategorized · DW Rwanda

UK: Seventh arrest made after air base plot

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

Inflation trends in Kenya

September 2025 - September 2026.

Recently
National · PML Daily

Parliament checks EACOP readiness as Uganda targets first oil in December

DAR ES SALAAM – Parliament’s Committee on Environment and Natural Resources has raised fresh scrutiny over the readiness of the East African Crude Oil Pipeline (EACOP) as Uganda moves closer to...

Recently
Health · The Star Kenya

Ebola alert: Nairobi Hospital steps up tracing, staff monitoring

Staff who had relevant contact with the patient will be individually contacted, risk-stratified and followed up according to Ministry of Health protocols.

Recently
Uncategorized · Capital FM

Chaos force Sharks, Mombasa United second leg playoff abandoned

Latest · football

Recently
Uncategorized · TechCabal East Africa

Nigeria’s global hiring push must create jobs, not just train workers

Read the full report from the original source.

Recently

Page 837 of 1143 · 22858 stories